Nenda kwa yaliyomo

Sahifa Sajjadiyya

Kutoka wikishia
Kitabu cha Sahifa Sajjadiyya

Sahifa Sajjadiyya (Kiarabu: الصحيفة السجادية) ni kitabu kinachojumuisha dua zilizonukuliwa kutoka kwa Imamu Sajjad (a.s). Kitabu hichi ni urithi muhimu wa maandishi kwa wafuasi wa madhehebu ya Shia, nacho ni kitabu chenye hadhi kubwa baada ya Qur'ani na Nahjul Balagha, nacho kinajulikana kwa majina tofauti kama vile «Dada wa Qur'ani» na «Injili ya Ahlul Bayt».

Imamu Zainul al-Abidina (a.s) aliwasilisha idadi ya dua 75 kwa Imamu Baqir (a.s) na Zaid bin Ali, ambaye ni mwana wa Imamu Zainul al-Abidina (a.s). Imamu Sadiq (a.s) pia alimnukulia dua hizo bwana Mutawakkil bin Harun Balkhi, ila baada ya muda fulani baadhi yake zilipotea na hatimae zikabai dua 45 tu kati yake.

Sahifa Sajjadiyya ya Imamu Sajjad (a.s) pia imekuwa ni kitabu maarufu mbele wanazuoni wa madhehebu ya Ahlu Sunna, ambapo baadhi ya wanazuoni wa madhehebu hayo wameonekana kunukuu baadhi ya dua zake. Baadhi ya watafiti wanaojishughulisha na utafiti wa mambo ulimwengu wa Mashariki wanaamini kwamba; Sahifa Sajjadiya ya Imamu Sajjad (a.s) inaweza kuonyesha sura mpya ya Uislamu mbele ya walimwengu. Katika Sahifa, Imamu Sajjad (a.s) amejitahidi kuelezea kanuni za kimaadili na njia bora za maisha ya kijamii na kisiasa kupitia dua na maombi yake hayo. Kulingana na maoni ya watafiti, kwa kuwa Imamu Sajjad (a.s) aliishi katika kipindi cha taqiyyah katika maisha yake, aliamua kutoa mafunzo elimu hizi kwa njia ya dua.

Suala la Uimamu ni mojawapo ya mada muhimu za kisiasa na kidini zilizojadiliwa katika Sahifa hii ya Imamu Sajjad. Kitabu hichi kimefafanua mada kadhaa muhimu, ambazo zihitajika kujulikana na walimwengu. Miongoni mwa mada zilizo anikwa kitabuni humo ni; Ufichuaji na uwekaji hadharani wa ukweli dhidi ya wavamizi wa ukhalifa, kueneza ni halisi na dhamira ya utawala wa Maimamu, kusisitiza suala la kulinda mipaka na sharia za dini pamoja na suala la kutetea wanyonge na kupambana na madhalimu.

Kitabu hichi ni maarufu na kinachokubalika kwa kiasi kikubwa mbele ya wanazuoni wa madhehebu ya Shia, hata hivyo baadhi ya wanazuoni wa fani ya Hadithi wamezihisabu nukuu zake, kuwa ni nukuu zenye daraja ya mutawatir. Kwa upande mwengine, baadhi ya wanazuoni wa fani ya fiqhi (mafaqihi), hawaoni kuwa ni jambo lililo sawa, kunasibisha kila kipengele cha dua hizo kwa Imamu Sajjad (a.s). Hii ni kwa sababu ya shaka juu ya uaminifu wa Mutawakkil bin Harun, ambapo hapana ushahidi tosha juu ya uwaminifu wake.

Kitabu cha Sahifa Sajjadiya kimefasiriwa katika lugha mbalimbali kama vile; Kifaransa, Kiingereza, Kihispania, Kituruki, Kiarabu, Kiurdu, Kibosnia, Kialbania, na Kitamil. Kitabu hichi kimefasiriwa na watu tofauti, ambapo tafsiri maarufu zaidi ni Riyadhus al-Salikin ilioandikwa na Sayyid Ali Khan Kabir. Pia kuna baadhi ya watafiti walio kusanya dua nyingine za Imam Sajjad ambazo zimepatikana katika vyanzo vingine na kuziweka ndani ya vitabu vyao.

Nafsi ya Sahifa Sajjadiyya Ndani ya Tamaduni za Mashia

Sahifa Sajjadiyya ni moja wapo ya vitabu muhimu baada ya kitabu Nahju al-Balagha mbele ya Mashia. [1] Kitabu hichi kimekusanya ndani yake dua zilizo nukuliwa kutoka kwa Imamu Sajjad (a.s). [1] Kulingana na maelezo ya Ibnu Shari Ashub (aliye fariki mwaka 588) ni kwamba; Sahifa Sajjadiyya ni miongoni mwa vitabu vya mwazo kuandikwa katika ulimwengu wa Uislamu. [3] Mtafiti wa Kiislamu aitwaye Murtadha Mutahhari, amekizingatia kitabu hichi kuwa ndiyo kitabu cha kale zaidi katika ulimwengu wa Kiislamu baada ya Qur’ani. Pia Mutahhari anaamini ya kwamba; Sahifa Sajjadiyya ni kitabu chenye umadhubuti katika pande zote mbili, katika nukuu zake na pia katika madhumuni yaliomo ndani yake. [4] Yeye amekiarifisha kitabu hichi kwa kusema kuwa; kitabu hichi ndio kitabu pekee kilicho andikwa kwa mfumo wa katibu mwishoni mwa karne ya kwanza na mwanzoni mwa karne ya pili Hijiria. [5]

Agha Bozorge Tehrani mtafiti wa nyaraka za wa Kishia ameandika kwa kusema; Sahifa Sajjadiyya ni ‘dada wa Qur’ani’, ni Injili ya Ahlulbait, Zaburi Aalu Muhammad na ni Sahifa Kamilifu. [6] Kwa maelezo ya ‘Izzu al-Ddin Jazaairi ni kwamba; kitabu hichi kilikuwa kikitumika katika kusomeshea wanufunzi wa vyuo vya kidini vilivyopo nchini India. [7]

Jina Jengine la Sahifa Sajjadiyya

Kwa maoni ya Sayyid Ali Khan Kabir, ambaye ni miongoni mwa wafafanuzi na wafasiri wa Sahifa Sajjadiyya, ni kwamba; kitabu hiki kimepewa jina la Sahifa Kamilifu kwa sababu ya kule dua zake kutosheleza mahitaji yote mawili ya mwanadamu, nayo ni mahitaji ya kidunia na Kiakhera. [8] Pia, inawezekana kwamba jina hili lilikuwa na nia ya kutofautisha nakala ya Sahifa Sajjadiyya ilioko kwa Mashia Ithna'asharia na nakala iliopo kwenye madhehebu ya Zaidiyya. Hii ni kwa sababu Mashia Zaidiyya pia nao wana nakala ya Sahifa Sajjadiyya ambayo ni karibu ya nusu ya nakala iliopo mikononi mwa Mashia Ithna'asharia. [9]

Idadi ya Dua Katika Sahifa Sajjadiyya

Awali, Sahifa Sajjadiyya ilikuwa na mkusanyiko wa dua 75 ambazo Imamu Sajjad (a.s) alizo ziwasilisha kwa watoto wake, yaani Imam Baqir (a.s) na Zaid bin Ali. Kwa hivyo toleo la kwanza likawa na nakala mbili zilizo milikiwa na watoto wake hao wawili. [10] Yahya bin Zaid (mwana wa Zaid bin Ali), akatoa ile nakala iliyo andikwa na baba yake na kumkabidhi Mutawakkil bin Harun al-Balkhi (mpokezi wa kwanza aliye anza kunukuu Sahifa Sajjadiyya). [11] Naye Mutawakkil bin Harun al-Balkhi alimpelekea nakala hiyo Imamu Swadiq (a.s) na kuiweka sambamba na nakala iliyobaki kutoka kwa Imamu Baqir (a.s), ambapo naka hizi zilionekana kufanana bila ya kupatikana tofauti kati ya nakala mbili hizo. [12] Imamu Sadiq (a.s) alimsomea kitabu hicho Mutawakkil bin Harun al-Balkhi na Mutawakkil akakiandika; lakini hatimae aliipoteza dua 11, kwa hivyo zilibaki dua 64. [13] Ila baadhi ya dua hizo 64 hazikurithiwa na kizazi kinachofuata. Hiyo ndio sababu ya nakala za Sahifa Sajjadiyya kuwa na dua 54 tu. [14]

Mwana wa Mutawakkil bin Harun (Umair bin Mutawakkil) ndiye mtu pekee aliye ipokea na kuinukuu Sahifa Sajjadiyya kutoka kwa babake, na baada yake wakafuata waandishi wengine. Watu maarufu zaidi walio inukuu Sahifa Sajjadiyya ni; Ahmad bin Muslim Muttahari, Ali bin Nu’umaan A’alam, Muhammad bin Saleh, Hussein bin Ashkiib al-Marwazi, Ubaidullah bin Fadhl Nabhani, na Ali bin Hammad bin ‘Alaa. [15] Sahifa Sajjadiya ina hadithi mbalimbali za riwaya, na Riwaya Bahaa al-Sharaf ni maarufu zaidi. [16]

Pia Sahifa Sajjadiyya inapatikana kwa hati za Kaf-ami ambayo ni miongoni mwa matoleo ya mwanzo ya Sahifa Sajjadiyya ambalo ukiachana na dua 45 zilizomo kitabuni humo, pia ndani yake kuna dua tano za ziada katika toleo hili la Kaf-ami.[17]

Kushamiri kwa Umaarufu wa Sahifa Sajjadiyya

Kwa mujibu wa maoni ya wanazuoni wa Hadithi, kitabu cha Sahiha Sajjadiyya kilijulikana na kushamiri umaarufu wake katika kipindi cha Majlisi wa kwanza, yaani Muhammad Taqi Majlisi. [18] Yeye alipata nakala ya kitabu hichi kwa njia ya ndoto au kwa kukutana na Imamu wa Zama (Imamu Mahdi), na akajitahidi sana kukisambaza, kiasi ya kwamba katika nyumba kukawa na Sahifa Sajjadiyya sambaba na Qur'ani. [19] Kwa mujibu wa maelezo ya Muhammad Taqi Majlisi, nusu ya watu wa Isfahan, waliweza kufikia daraja ya kujibiwa dua zao kwa baraka za kitabu hichi. [20]

Mtazamo wa Wanazuoni wa Kisunni na Watafiti Uuu ya Uislamu

Muhammad Zaki Mubarak (aliye zaliwa mwaka 1310 na kufariki 1371 Hijiria), ambaye ni mwandishi na mtafiti Kimisri, akielezea wasifu wa Sahifa Sajjadiyya katika kitabu chake «Tasawwufu al-Islami wa Aadabu al-Akhlaq», alikifananisha kitabu cha Sahifa Sajjadiya na Injili iliyoteremshwa kwa nabi Isa (a.s) ambayo ni Injili asili na ile inayotumiwa na Wakristo wa hivi sasa. na akasema kwamba Sahifa hiyo ni neema kutoka kwa Mungu iliyotamkwa kupitia ulimi wa Imamu Zainul Abidin. [21] Ibn Jawzi (alifariki mwaka 654 Hijiria), ambaye mwandishi wa kitabu Tadhkiratu al-Khawas, anaamini kwamba; Imamu Sajjad ana haki maalumu mbele ya umma wa Kiislamu, kutokana na kufundisha Waislamu jinsi ya kuzungumza na kumwomba msaada Mwenyezi Mungu. Yeye aliwafundisha watu jinsi ya kuzungumza na Mungu wao wakati wa kuomba toba, jinsi ya kuomba mvua ya rehema kutoka kwa Mwenyezi Mungu na jinsi ya kumwomba Mungu kinga dhidi ya maadui wakati wa hofu. [22]

Sulaiman bin Ibrahim Ganduzi (alifariki mwaka 1294 Hijiria), mmoja wa wanazuoni wa Kisunni, katika kitabu chake Yanabi’u al-Mawadda, ameitaja Sahifa na kunukuu sehemu za dua zake, kitabuni mwakw humo. [23] Tantawi Jawhari, ambaye ni mwandishi wa kitabu “al-Jawahiri fi Tafsiri al-Quran al-Karim”, baada ya kupokea nakala ya Sahifa Sajjadiya kutoka kwa Mar’ashi Najafi mnamo mwaka 1358 Hijiria, alikisifu kitabu hicho kwa kusema «Haya ni maneno yalioko juu ya maneno ya viumbe na chini ya maneno ya Muumbaji». [24]

Kulingana na maelezo ya William Clark Chittick, mtafiti wa masuala ya Kiislamu wa Marekani ni kwamba; wengi wa watu Magharibi wanaufahamu Uislamu kuwa ni dini isiyo endana na mantiki, inayo amini mambo Dhahiri tu bila utafiti na inayoshika na sharia kibubusa; ila Sahifa Sajjadiya inaweza kutoa mandhari mpya kabisa kwa wasomaji, na kuangaza mwelekeo na ufahamu sahihi wa kibinadamu ambao ni sharti la kupatikana na kukamilika malengo ya Kiislamu. [25]

Hadhi ya Sahifa Sajjadiyya

Kwa mujibu wa wataalamu na watafiti wa Hadithi, Sahifa Sajjadiya daima imekuwa ni maarufu na inayo kubalika miongoni mbele ya wanazuoni. Wanazuoni kama vile; Sheikh Tusi, Qutubuddin Rawandi, Shahid Awwal na Kaf-‘ami wamezinukuu dua zake katika vitabu vyao. [26] Muhammad Baqir Majlisi, mwandishi wa kitabu cha Bihar al-Anwar, [27] na Agha Bozorge Tehrani pia wanaamini kuwa Sahifa Sajjadiya ni kulingana na nukuu zake, ni kitabu sahihi chenye ushahidi mutawatir (kulicho nukuliwa kupitia njia tofauti), kwani wapokezi wake wa kila tabaka, walipata idhini kamili ya kunukuu dua za kitabu hichi (yaani wamepata ijaza). [28] Muhammad Taqi Majlisi ameandika akisema; Sahifa Sajjadiya ina zaidi ya nyaraka milioni moja kama vielelezo na ithibati za kitabu hichi. [29]

Muhammad Baqir Majlisi pia anaamini kuwa kitabu hichi pia ni mutawatiri mbele wafuasi wa madhehebu ya Zaidiyya. [30] Kwa maoni yake, kutokana na umahiri wa maneno ya Sahifa Sajjadiya na ukweli wa kwamba kitabu kimekusanya ndani yake elimu ya utambuzi wa kumtambaua Mungu, basi hakuna shaka kuwa maneno yaliomo ndani yake ni maneno yatokayo kwa Imamu Sajjad (a.s). [31] Baadhi ya wanazuoni wakiegemea kwenye maoni ya Allama Majlisi, wanaamini kuwa; Sahifa Sajjadiya ni mustafidhu (yenye nukuu nyingi mno) mutawatiru (iliyo pokewa kupitia nukuu za watu walioishi katika matabaka na zama tofauti). [32] Walakini, baadhi ya watafiti wanahisi kuwa madai ya nukuu zake kuwa ni mutawatiri si madai sahihi, hii ni kwa sababu ya mpokezi wake asili kuwa ni mtu mmoja tu. [33]

Abu al-Qasim al-Khui pia ameona kuwa; kukihisabu kitabu hichi kuwa ni mtawatir ni jambo lenye mashaka ndani yake kwa sababu mpokeze na msimulizi wake halisi ni mtu asiye julikana. [34][35] Kwa maoni ya Imam Khomeini, ingawa inajulikana kuwa Sahifa Sajjadiya ina ubora mkubwa na maana nzito, ila haiwezekani kumhusisha Imam Sajjad (a.s) na maneno yote ya kitabu hicho na kuyachukulia kama ni hoja za kisheria katika kutoa fatwa. [36] Mafaqihi na wafasiri kadhaa wamezinukuu sehemu za Sahifa Sajjadiya katika vitabu vyao na katika kusimamisha hoja zao mbali mbali. [37] Abu al-Ma’ali al-Kalbasi (aliye fariki mwaka 1315 Hijiria) alitunga risala makhususi katika kutafiti ushahidi wa Sahifa Sajjadiyya. [38] Risala hii imechapishwa katika kitabu cha Al-Rasa’il al-Rijaliyah. [39]

Chapa na Matoleo Mbali Mbali

Ukurasa wa kwanza wa nakala kongwe zaidi ya Sahifa Sajjadiyyah

Safina ya Sajjadiyya ni mojawapo ya vitabu ambavyo vina nakala nyingi za kimaandishi. [40] Nchi Iran pekee, kuna zaidi ya nakala elfu tatu za kimaandishi zilizosajiliwa kuhusiana na kitabu hiki. [41] Moja ya nakala za zamani zaidi za Sahisa Sajjadiyya, ni nakala ya uandishi ya tarehe: 695 Hijiria, ambayo imehifadhiwa katika Maktaba ya Ayatollah Marashi Najafi. [42] Katika ukarabati wa Haramu ya Imam Ridha mnamo uliofanyika mnamo mwaka 1348 Hijiria, pia ilipatikana nakala ya zamani ya Sahifa Sajjadiyya, ambayo tarehe ya uandishi wake ni mwaka 416 Hijiria, [43] na wapokezi wake wote ni wa Kisunni. [44] Kitengo cha huduma cha Qudsi Radhawi kilichapisha nakala hii ambayo ina tofauti na nakala maarufu na ni pungufu zaidi kulinganisha na nakala nyeka nyengine mbali mbali. [45]

Imepokewa kutoka kwa Sayyid Murtadha Nujumi kwamba; mmoja wa jamaa zake aliiona nakala asilia ya Sahifa Sajjadiyya iliyoandikwa na Zaid bin Ali katika Maktaba ya Vatican. [46] Inawezekana kwamba nakala asilia nyingine ya Sahifa Sajjadiyya iliyoandikwa na Imamu Baqir (a.s) ni mojawapo ya amana za Imamu na ilioko mikononi mwa Imamu wa Zama (Imamu Mahdi) (a.s). [47]

Sahifa Sajjadiyya kwa mara ya kwanza kabisa ilichapishwa mnamo mwaka 1248 Hijiria katika mji wa Kolkata nchini India. [48] Katika miongo iliyofuata, tafsiri ya kitabu hichi kwa lugha tofauti pia ufafanuzi wa vitabu vyenye ufafanuzi wa kitabu hichi vilichapishwa katika jiji hilo hilo nchini India. [49] Pia Iran mnamo mwaka 1262 Hijiria, Misri mnamo mwaka 1322 Hijiria, Damascus mnamo mwaka 1330 Hijiria, na Iraq mnamo mwaka 1352 Hijiria kitabu hichi kilichapisha kwa mara ya kwanza kabisa ndani ya zama hizo. [50]

Maudhui Yake

Kwa mujibu wa maoni ya baadhi ya watafiti, maudhui kuu za dua za Sahifa za Sajjadiyya zinahusiana zaidi na mada ya tauhidi (upwekeshaji wa Mungu), na dhana kuu ya dua zake, ni kujinyenyekeza mbele ya Mwenye Ezi Mungu. [51] Imamu Sajjad (a.s) katika Sahifa yake, ameeleza misingi ya maadili na njia ya maisha ya kijamii na kisiasa katika mfumo wa dua na maombi [52] kwa njia ambayo, watu wangeweza kuufahamu mwelekeo wa kisiasa wa Imamu kwa kupitia dua hizi. [53] Inaaminika kuwa; sababu kuu ya Imamu Sajjad (a.s) kueleza na kufikisha ujumbe wa elimu hii kupitia mfumo wa dua, ni hali maalum ya kisiasa iliyo tanda katika kipindi cha maisha yake (hasa wakati wa utawala wa Abdulmalik bin Marwan, [54]) ambapo yeye aliishi kwa njia ya taqiyyah. [55] Katika Sahifa hii kuna dua chache ambazo ndani yake hamna sala za kumsalia Mtume (s.a.w.w). [56] Kulingana na Rasul Ja'fariyan, kumsalia Mtume (s.a.w.w) na kulinda fungamano la uhusiano kati ya Mtume (s.a.w.w.) na Ahlul Bayt wake, ni jambo lenye umuhimu mkubwa katika imani ya Kishia. [57]

Mada ya Uimamu ni mojawapo ya mada muhimu za kisiasa na kidini zinazojadiliwa katika Sahifa Sajjadiyya, [58] ambapo Imamu Sajjad (a.s) pamoja na kuthibitisha uhalali wa Maimamu wa Kishia katika kushika nafsi ya Ukhalifa, pia anazungumzia ndani ya dua za ujuzi elimu za Maimamu ziendazo sawa na elemu za manabii na utakatifu wao wa kuto tenda dhambi (umaasumu wao). [59] Uwanikaji wa ukweli dhidi ya wasaliti wa Ukhalifa, kueneza malengo halisi ya dhana ya utawala wa Imamu, masisitizo juu ya kulinda mipaka ya dini na kupambana na uovu, kuunga mkono na kutetea wanyonge na kupambana na madhalimu, ni masuala mengine ya kisiasa yaliyojadiliwa katika Sahifa Sajjadiyya. [60] Ja'far Subhani ameandika akisema ya kwamba; katika Sahifa Sajjadiyya kuna baadhi ya miujiza ya kisayansi iliomo ndani yake, ambayo haikujulikana katika siku hizo, [61] nayo ni kama vile kuenea kwa maradhi ya kolera kwa njia ya maji, jambo ambalo limeashiriwa katika dua isemayo:

«اللَّهُمَّ وَ امْزُجْ مِیاهَهُمْ بِالْوَبَاءِ»
Ewe Mola, maji ya maadui yachanganye na virusi vya kolera. [62]

Baadhi ya dua katika Sahifa Sajjadiyya ni dua ziombwazo katika siku maalum; kama vile dua ya Arafa, dua ya kuaga Ramadhani na dua ya kuona mwezi mpevu. Na kwa upande wa pili pia, kuna baadhi ya dua ambazo hazina masharti ya kusomwa katika siku maalum. [62]

Orodha ya Dua Za Sahifa ya Sajjadiyya

Sahifa ya Sajjadiyya ina dua 54, orodha ya majina ya dua hizo ni kama ifuatavyo:

Tarjama za Sahifa Sajjadiyya

Makala Asili: Orodha ya Tarjama za Sahifa Sajjadiyya

Sahihi ya Sajjadiyyah imetarjumiwa na kuchapishwa katika lugha tofauti, kama vile; Kifaransa, Kiingereza, Kiindonesia, Kituruki, Kiurdu, Kihispania, Kikroeshia, Kialbania, na Kitamil. [63] Baadhi ya tarjama hizi ni kama ifuatavyo:

Maelezo Uchambuzi na Hitimisho

Agha Bozorge Tehrani katika kitabu chake al-Dharī’ah ametaja karibu ya tafsiri chambuzi 70 za Sahifa Sajjadiyya. [72] Tafsiri chambuzi maarufu zaidi ya Sahifa Sajjadiyya ni Riyādhu al-Sālikin iliyoandikwa na Said Alikhān Kabīr. Inasemekana kwamba; tafsiri chambuzi ya zamani zaidi inayo patikana hadi sasa, ni Al-Fawā'id al-Sharīfah fī Sharhi al-Sahīfa iliyo andikwa na Kafʿamī. [73]

Miongoni mwa tafsiri fafanuzi nyengine ni yafuatayo:

Jumla ya dua zilizopokewa kutoka kwa Imamu Sajjad (a.s) ni zaidi ya dua zilizopo katika Sahifa ya Sajjadiyya. [79] Baadhi ya wanazuoni wamejaribu kukusanya dua nyingine za Imamu kutoka katika vyanzo vingine na kuzichapisha katika kitabu makhususi. [80] Vitabu hivi vinajulikana kwa majina yafuatayo:

  • الصَّحیفةُ السَّجادیةُ الثَّانیه (kilicho andikwa na Sheikh Hurru al-ʿAmilī).
  • الصَّحیفةُ السَّجادیةُ الثّالثة (kilicho andikwa na Abdallāhi bin ʿIsā Afandi).
  • الصَّحیفةُ السَّجادیةُ الرَّابعة (kilicho andikwa na Muḥaddith Nūrī).
  • الصَّحیفةُ السَّجادیة الخامسه (kilicho andikwa na Sayyid Muhsin ʿAmīn).
  • الصَّحیفةُ السَّجادیةُ السّادسه (kilicho andikwa na Muḥammad Sāleh Hāʾirī Māzandarāni). [81] Sayyid Muḥammad-Bāqir Muwahhiid Abtahī katika kitabu chake kilichoitwa Sahīfatu al-Sājidiyyatu al-Kāmila amekusanya ndani yake dua zipatazo 272 kutoka kwa Imamu Sajjad. [82] Muḥammad Bāqir Majlisi aliongeza dua nyengine kutoka kwa Imamu Sajjad (a.s) na kuziweka mwishoni mwa Sahifa Sajjadiyya, ambazo zinajulikana kama Mulaḥaqatu Sahīfa. [83] Katika nakala nyingi za Sahifa Sajjadiyya, nyonge za dua zimeengenzwa ndani yake. [84]

Tafiti na Athari za Kimaandishi Kuhusiana na Sahifa Sajjadiyya

Kuna vitabu kadhaa vilivyo andikwa kuhusu bibliografia ya Sahifah Sajjadiyah, ambapo kwa haraka tunaweza kuashiria jarida la utafiti juu ya Sahifah Sajjadiyah liloandikwa na Majid Ghulami Jaliseh pia bibliografia ya Imam Sajjad, Sahifah Sajjadiyah na risalatu al-Huquuq viliyoandikwa na waandishi wawili, ambao ni Salman Habibi na Mukhtar Shamsaldini. [85] Pia kuna vitabu kadhaa vilivyo fanya kazi kusajili na kurikodi mada na maudhui za Sahifa Sajjadiyya ndani yake, miongoni mwavyo ni:

  • Al-Dalilu ilaa Maudhuu’ati Sahifah al-Sajadiyya cha Muhammad Hossein Modhaffar. Katika kazi hii, mada zote kuu zilizotajwa katika Sahifa al-Sajjadiyya zimejadiliwa ndani yake katika sura kumi na tisa, ambapo pia mada ndogo ndogo zinazohusiana na mada kuu hizo zimejadiliwa ndani yake. [86] Kitabu hichi kilichapishwa na Qom Islamic Publishing House mwaka wa 1403 Hijiria. [87]
  • Kamusi ya mada ya Sahifah Sajjadiyya, iliyoandikwa na Sayyid Ahmed Sajjadiy na washirika wake wengine: kitabu hichi, ambacho mada zake zimepangwa kwa mpangilio wa alfabeti, kilichapishwa na Taasisi ya Mafunzo ya Kitamaduni ya Al-Zahra ya Qom mwaka 2005 katika juzuu tatu. [88]
  • Fahirisi ya mada ya Sahifah Sajjadiyya (Namaayenaame Mauzuui Sahife Sajjadiyye) cha Mustafa Draiti na washirika wake. Kitabu hiki kilichapishwa mwaka wa 1377 Shamsia, kwa juhudi za Kituo cha Habari za Kisayansi na Hati za Kielemu    nchini Iran huko Tehran kikiwa katika juzuu mbili. [89]
  • Riwaya za Ucamungu (Hadithi Bandgi), cha Sayyid Kadhim Arfa’a: Katika kazi hii, mwandishi anaeleza mada zilizoko katika Sajjadiyya kwa mpangilio wa alfabeti. [90] Kazi hii ilichapishwa na Faidhu Kashani Publishing House huko Tehran mwaka 2008 Miladia. [91]
  • Al-Mu’ujam al-Mufahras li Alfadhi al-Sahifati al-Kamila, cha Sayyid Ali Akbar Qurashi. Uchapishaji wa kitabu hichi ulifanywa na Daru Tabligh Islamic Publishing House of Qom mwaka 1343 Shamsia. [92]
  • Al-Mu’ujam al-Mufahras li Alfadhi al-Sahifati al-Sajadiyyah cha Fatima Ahmadi. Kitabu hichi kilichapishwa na Uswa Publications mwaka 1394 Shamsia. [93]

Vyanzo

  • Al-Ṣaḥīfa al-Sajjādīyya. Translated to Farsi by Mubashshirī. Beirut: Dār al-Taʿāruf li-l-Maṭbūʿāt, 1402 AH.
  • Āqā Buzurg Tihrānī, Muḥammad Muḥsin. Al-Dharīʿa ilā taṣānīf al-Shīʿa. Beirut: Dār al-Aḍwāʾ, 1403 AH.
  • Balādhurī, Aḥmad b. Yaḥyā al-. Ansāb al-ashrāf. Edited by Suhayl Zakkār & Riyāḍ al-Ziriklī. Beirut: Dār al-Fikr, 1417 AH.
  • Ḥabībī, Salmān and Shams al-Dīnī, Mukhtār. Kitābshināsi-yi Imām Sajjād (a), Ṣaḥīfa-yi Sajjādīyya wa Risāla-yi Ḥuqūq. Qom: Majmaʿ Jahānī Ahl al-Bayt (a), 1394 Sh.
  • Ibn Abī l-ḥadīd. Sharḥ nahj al-balāgha. Beirut: Muʾssisat al-Aʿlamī, 1415 AH.
  • Irbilī, ʿAlī b. ʿIsā al-. Kashf al-ghumma fī maʿrifat al-aʾimma. Beirut: Dār al-Aḍwāʾ, 1405 AH.
  • Imām Khomeinī, Sayyid Rūḥ Allāh. Ṣaḥīfa-yi Imām. Tehran: Markaz-i Nashr-i Āthār-i Imām, 1389 Sh.
  • Jazāʾirī, ʿIzz al-Dīn. Sharḥ al-Ṣaḥīfa al-Sajjādīyya. Beirut: Dār al-Tʿāruf li-l-Maṭbūʿāt, 1402 AH.
  • Majlisī, Muḥammad Taqī. Rawḍat al-muttaqīn. Qom: Muʾssisat Farhangī Islāmī Kūshānpūr, 1406 AH.
  • Qundūzī, Sulaymān b. Ibrāhīm al-. Yanābīʿ al-mawadda. Edited by ʿAlī Jamāl al-Ashraf. Tehran: Nashr-i Uswa, 1416 AH.
  • Sahmī, Ḥamza b. Yusuf. Tārīkh-i Jurjān. Ālam al-Kutub. Beirut: [n.p], [n.p].