Ufufuo

Kutoka wikishia

Ma’ad au ufufuo (Kiarabu: المَعَاد) Kwa mujibu wa imani ya dini ya Kiislamu pamoja na dini nyengine za mbinguni, na kwa mujibu wa maana zilizotolewa na wanatheolojia, neno Ma’ad ambalo ni la lugha ya Kiarabu; lina maana ya kurudi kwa roho mara nyengine kwenye mwili wa mwanadamu baada ya kifo chake, kisha mwanadamu huyo kuanza maisha mengine mapya kabisa katika siku ya Kiyama. Kulingana na msingi huu wa imani, binadamu wote watafufuliwa tena siku ya Kiyama, kisha matendo yao yatahukumiwa (yatahisabiwa) na Mola wao, na hatimae ima wataishia kwenye adhabu au watafaulu, na hilo ni kulingana na matendo yao mema au maovu walio yatenda humu duniani.

Ma’ad katika dini ya Kiislamu ni msingi mkuu wa imani baada ya msingi wa Tawhidi, kuamini kwa msingi huu kunahisabiwa kuwa ndio moja ya misingi na masharti muhimu ya mtu kukubalika ndani ya Uislamu. Kuna kiasi cha Aya 1400 hadi 2000 katika Qur’ani kuhusiana na Ma’ad (ufufuo) na maisha ya Akhera. Imani katika Ma’ad imeorodheshwa kama ndio sababu ya kutekelezwa kwa haki, kupatikana usalama wa jamii, kutokata tamaa kutokana mawimbi ya matatizo na shida za maisha, kuheshimu haki za wengine na kadhalika.

Waislamu hawana khitilafu yoyote ile katika kukubali imani ya uwepo wa tukio la Kiyama (siku ya kufufuliwa); ila khitilafu zao zinahusiana na kina cha suala hilo lilivyo. Kiujumla kuna mitazamo mitatu ilio wasilishwa kuhusiana na suala hili: Wanazuoni wengi wa Kiislamu, wakiwemo wanafalsafa, wanaamini juu imani ya kuwepo kwa ufufuo wa kimwili na kiroho. Wataalamu wengi wa fani ya kitheolojia wanaamini kuwa ufufuo huo ni ufufuo wa kimwili tu, huku wanafalsafa wa falsafa ya Kimashsha'i (wanafalsafa wa Aristotelian), wakiamini juu ya ufufuo wa kiroho peke yake. Hata hivyo, Ibn Sina, mwanafalsafa mkuu wa Kimashsha'i, alikua akikubaliana na imani ya ufufuo wa kimwili kupitia sheria za kidini.

Wafuasi wa mtazamo wa ufufuo wa kimwili na kiroho wametoa maelezo na uchambuzi tofauti kuhusu mwili wa Kiakhera, miongoni mwa nadharia zao kuhusiana na suala hili ni; kurejea kwa roho kwenye mwili wa kidunia, kurejea kwa roho kwenye mwili wa Kibarzakh, na kurejea kwa roho kwenye mwili wa Kiakhera.

Wanafalsafa wa Kiislamu wamejaribu kuthibitisha umoja wa mwanadamu duniani na Akhera kwa kutegemea suala la nafsi na hali halisi yake ya kimaumbile ya kutokuwa na maumbile ya kiwiliwili cha mada yenye kuhisiwa kupitia hisia tano mashuhuri (hisia za: ngozi, macho, masikio, pua, na ulimi). Wao wanaihisabu nafsi kuwa ndio chombo unganishi kinacho muunganisha mwanadamu na kumpa utambulisho mmoja katika maisha yake ya kiduniani na Kiakhera.

Ili kuthibitisha hisia za kiakili katika kuamini juu ya uwezekano tokeo la Ma’ad (Kiyama) sambamba na ulazima wa kutokea kwake, wanazuoni na watafiti mbali mbali wamewajibika kuingia uwanjani na kutoa hoja mbalimbali. Uwezekano wa kuwepo kwa Kiyama umethibitishwa kupitia Aya za Qur'an kama zile Aya zinazorejelea suala la ufufuo wa ardhi na mifano ya ufufuo wa wanadamu wa zama zilizopita, kama vile As-habul Kahf na Uzair. Ili kuthibitisha ulazima au wajibu wa kutokea kwa Kiyama, wanazuoni wamejaribu kutoa hoja tofauti kama vile: ukweli wa Mwenye Ezi Mungu katika kuliarifisha tokeo la kutokea kwa Kiyama, uwepo wa hamu ya maisha ya milele ndani ya asili ya maumbile ya mwanadamu, pamoja uwepo wa sifa za uadilifu na hekima za Mwenye Ezi Mungu.

Pamoja na hoja nyingi zilzizopo katika kuthibitisha kuwepo kwa uwezekano wa kutokea kwa Kiama, pamoja na ulazima wa kutokea kwa Kiyama hicho, ila bado kuna baadhi ya watu walio kataa au wanao kataa Kiyama. Ujinga, kupuuza uwepo wa nguvu za Mungu, tamaa ya uhuru usio na mipaka na kutokuwajibika, ni miongoni mwa sababu za kukataa Kiyama. Shaka mbalimbali zimeibuka kuhusiana na suala la ufufuo (Ma’ad au Kiama), miongoni mwazo ni kama vile; kikwazo cha Mla na Kiliwacho, kiwazo cha Kurudishwa Kile Ambacho Tayari Kimesha Potea na kikwazo juu ya Elimu na Uwezo wa Mwenye Ezi Mungu Katika Kutokea kwa Kiyama. Hivi ndio vikwazo na shaka mashuhuri zaidi zilizoibuka miongoni mwa wakataao Kiyama, na wanazuoni wa Kiislamu nao wakajaribu kujibu hoja za vikwazo hivyo kwa njia mbalimbali.

Ufufuo, Imani ya Msingi ya Dini za Mbinguni

Imani ya ufufuo na kufufuka kwa mwanadamu kwenye ulimwengu wa Akhera,[1] inatambuliwa kuwa ni mojawapo ya imani msingi na ni moja wapo ya imani kuu ndani ya dini zote za mbinguni.[2] Katika kitabu Adyane zinde Jihan: Dini Hai za Ulimwengu, maisha baada ya kifo yamehesabiwa kuwa ni miongoni mwa imani na mafundisho ya dini zote, zikiwemo dini za zinazohusishwa na Mungu Mmoja, Uhindu, Ubuda, Taoism na Shinto.[3]

Kwa mujibu wa wanazuoni wa Kishia, ufufuo ni imani muhimu zaidi baada ya imani ya tawhidi (upweke wa Mungu), na ndio msingi ulionadiwa na manabii wote ambao ulitakiwa watu kuuamini.[4]Imani ya ufufuo na kuwepo kwa maisha ya Akhera ni sharti msingi ya Uislamu, na anayekataa hilo, huhisabiwa kuwa ametoka nje ya kundi la Waislamu.[5]

Kwa mujibu wa maelezo ya Muhammad-Taqi Misbah Yazdi, ni kwamba; imani ya ufufuo katika Qur'ani, inalinganishwa sambamba na imani ya Mungu, na kuna zaidi ya Aya ishirini zenye maneno ya «Allah» yalio fungamanishwa na ibara ya «Siku ya Mwisho».[6] Pia kuna idadi ya Aya kumi na mbili, ambazo ndani yake ibara ya Siku ya Mwisho imefuata baada ya juu imani ya kuamnini Mungu.[7] Misbah Yazdi anaamini kuwa; Uchambuzi wa kina wa Aya za Qur'an, unaonesha kuwa, sehemu kubwa ya mazungumzo ya manabii na mijadala yao na watu wa jamii zao ilikuwa ni kuhusiana na ufufuo, kiasi ya kwamba yaweza kusemwa kuwa; manabii walijitahidi zaidi kuthibitisha ufufuo kuliko kuthibitisha umoja (upweke) wa Mwenye Ezi Mungu, hii ni kwa sababu ya kwamba, watu walikuwa na ukaidi mkubwa zaidi katika kukubali ufufuo kutokana na kukanusha mambo ya ghaibu na tamaa ya uhuru usio na mipaka na hamu ya kutokuwajibika au kuto jali majukumu yao.[8]

Imeezwa kuwa neno Ma’ad lenye maana ya ufufuo, limetumika mara moja tu katika Aya za Qur'an[9] likimaanisha maana yake halisi ya kilugha (kwa maana ya marejeo).[10] Lakini kuna Aya zaidi ya 1400[11] au elfu mbili za Qur'an (ambayo ni karibu ya theluthi moja ya Aya za Qur'an),[12] zinazozungumzia suala hili la Ma’ad (ufufuo) pamoja na masuala yanayo husiana na maisha ya Akhera. Aya zinazohusiana na Ma’ad zimegawanywa katika makundi kadhaa yafuatayo:

  • Aya zinazohusu wajibu wa imani juu ya siku Kiama (Akhera).[13]
  • Aya zinazozungumzia natija na matokeo ya kukanusha ufufuo.[14]
  • Aya zinazohusiana na neema za milele za Peponi.[15]
  • Aya zinazozungumzia adhabu za milele za motoni.[16]
  • Aya zinazorejelea uhusiano wa matendo mema na mabaya na matokeo yake katika Siku ya Kiyama.
  • Aya zinazohusiana na uwezekano na umuhimu wa ufufuo ambazo zinajibu maswali na shaka za wakanushaji.[17]

Wakristo pia wanaamini katika ufufuo kupitia kisa cha ufufuko wa Yesu (Nabii Issa (a.s) na mifano ya kihistoria ya watu waliofufuka baada ya vifo vyao.[18][19] Kwa mujibu wa Agano la Kale[20] na Jipya,[21] watu wote baada ya kifo huenda katika ulimwengu wa wafu, ambao una sehemu mbili: sehemu moja kwa watu waovu ambayo ni mahali pa mateso, na sehemu nyingine kwa watu wema ambayo inaitwa Paradiso (Peponi).[22] Kwa upande wa Wakristo imani ya ufufuo na maisha ya Akhera imetajwa katika kanuni ya Imani Mitume na kanuni ya Imani ya Nikea, ambazo ni kanuni za imani za ulimwengu mzima zinazokubaliwa na Wakristo wote. [23]

Yasemekana kwamba; Imani ya ufufuo, haikutajwa katika Agano la Kale (Tanakh), ambacho ni kitabu kitakatifu cha Wayahudi, ila suala hili la ufufuo limetajwa mara kadhaa katika kitabu cha Talmud, ambacho ni kitabu kinacho jumuisha hadithi na sheria za Kiyahudi.[24] Inawezekana maandishi yanayo husiana na ufufuo yaliondolewa kupitia uharibifu uliofanywa ndani ya Agano la Kale.[25] Hata hivyo, katika sehemu moja ya Agano la Kale imeandikwa: Yehova huua na kuhuisha, huwatia watu makaburini na huwafufua tena.[26]

Kwa mujibu wa dini ya Zoroastrian (Wamajusi), roho baada ya kifo hutenganishwa kutokana na mwili, na hubaki katika hali hiyo hadi siku ya ufufuo kwa ajili ya hesabu na hukumiwa.[27] Yasemekana kuwa wasifu wa Pepo ya Wazoroastrian ni sawa na wasifu wa Pepo ya Uislamu; lakini jehanamu katika dini ya Zoroastrian, siyo yenye moto wa kuunguza, bali ni mahali penye baridi kali na giza la kutisha.[28] Wao pia wanaamini juu ya kuwepo kwa Daraja la Chinwat ambalo ni Daraja la Sirat la Kiyama.[29]

Athari za Imani ya Ufufuo (Ma’ad) katika Maisha ya Kidunia

Tukizingatia suala la imani ya ufufuo, hasa katika uchambuzi wake wa kina, tutaona kuwa kuna athari kubwa za kisaikolojia na kimaadili zziimarishazo roho pamoja na nafsi ya mwanadamu na katika maisha yake yote ulimwenguni humu.[30] Kulingana na mtazamo wa Misbah Yazdi, mtu anayemwamini juu ya ufufuo, ambaye hakihisabu kifo kuwa ndio mwisho wa maisha ya mwanadamu, kikawaida mtu kama hunapanga na kutekeleza maisha yake kwa njia yenye manufaa kwa ajili ya maisha ya milele (ya Akhera). Aidha mtu kama huyu, hafadhaishwi na ugumu wa maisha ya duniani, na wala matatizo ya maisha hayo huwa hayamkatishi tamaa na kumvunja moyo katika juhudi zake za kupata furaha ya mafanikio na ukamilifu wa milele (Akhera). Kwa mtazamo wake, athari ya imani juu ya ufufuo, haiishii tu katika maisha ya mtu binafsi; bali pia ina nafasi muhimu katika maisha ya kijamii kama vile; kuheshimu haki za wengine pamoja na kujali na kuwapa msaada wanyoge. Katika jamii inayo amini kuwepo kwa ufufuo, huwa kuna haja ndogo tu ya kutumia nguvu na shinikizo kwa ajili ya kutekeleza sheria na kanuni za haki na kuzuia dhuluma na ukiukaji wa sharia dhidi ya wengine.[31] Ayatullah Jawadi Amuli, ambaye ni mfasiri na mwanafalsafa wa Kishia, anaeleza akisema kuwa; miongoni mwa athari kuu ya kukumbuka imani ya ufufuo, ni kupatikana kwa utekelezaji wa haki za watu na kusimamia usawa wa watu binafsi pamoja na usawa wa kijamii, na athari kuu ya kusahau ufufuo ni ufisadi na dhuluma kwa watu binafsi pamoja na jamii kwa jumla.[32]

Mtu anaye amini imani ya ufufuo, huiangalia dunia kama  ni shamba na uwanja wa kupanda mbegu kwa ajili ya Akhera na matendo yake ni kama mbegu ambazo matunda yake yatavunwa ndani ya maisha ya Akhera. Kwa hiyo, mtu kama huyu huishi maisha ya duniani kwa njia iliyopangwa kwa mipango madhubuti na hafanyi uzembe katika kutii amri za Mwenye Ezi Mungu wala katika kutekeleza majukumu yake.[33] Aidha, imani katika ufufuo, hubadilisha mtazamo wa mtu juu ya kifo na kukifanya kionekane kama ni daraja na njia ya kuelekea ulimwengu mwengine ambao ni mzuri na bora zaidi.[34] Madunda mengine ya kuamini imani ya kuwepo kwa ulimwengu wa Akhera (Ma’ad), ni kuondokana na fikra za finyu za kudhania kuwa maisha ya mwanadamu yamo ndani ya mabano mawili ya maisha ya kidunia tu, na kwamba lengo la kuumbwa kwake hukamilika kupitia masha ya starehe na anasa za kidunia.[35]

Yasemekana kwamba; imani katika ufufuo inaweza kuwa na athari katika maisha ya duniani ikiwa kuna uhusiano wa kiusababishi (causality) baina ya dunia na Akhera. Yaani kuwepo sifa za kuathiriana kati ya maisha ya duniani na ya akhera, ndiko kunakoweza kuleta baraka za ima mtu kupata adhabu za au thawabu huko Akhera na kulipwa malipo ya matendo mazuri na mabaya aliyo yatenda katika dunia hii.[36]

Kwa mtazamo wa wengine, imani katika ufufuo ni sababu ya kupatikana usalama na amani ya jamii, kupatikana kwa haki za kisheria na kijamii, na ni sababu ya kupatikana suluhu na mahusiano mema kati ya watu.[37]

Maana ya Ufufuo

Katika istilahi za wanatheolojia, neno (Ma’ad) lina maana ya kurudi kwa roho kwenye mwilini katika Siku ya Kiyama na kufufuliwa tena, ili matendo yake yahesabiwe na walio wema wapate Pepo na neema za milele na waovu wapate adhabu na mateso wanayostahiki nayo.[38] Abdullah Jawadi Amuli ameeleza maana ya Ma’ad (ufufuo) kama ni; kurudi kwa mwanadamu mbele ya Mola wake.[39] Sa’aduddin Taftazani, ambaye ni miongoi mwa wanazuoni wa kutoka upande wa Ahlu-Sunna wa karne ya nane, ametaja maana nne tofauti za ufufuo, ambazo ni: Kurudi kwa uwepo (wujuud) baada ya kutoweka (adamu wujuud), kukusanyika tena kwa sehemu za mwili baada ya kutawanyika, kurudi kwa uhai baada ya kifo, na kurudi kwa roho kwenye mwili baada ya kutengana.[40] Wengine wameufasiri ufufuo (Ma’ad) kwa maana ya mfululizo wa safari na maisha ya mwanadamu katika ulimwengu mwingine baada ya kifo chake.[41] Kwa mujibu wa maelezo ya Allama Majlisi, ni kwamba; ufufuo katika lugha ni kitenzi kinacho ashiria jina la wakati au mahali. Kwa msingi huu, neno Ma’ad litakuwa na maana tatu, nazo ni: Kurudi kwa kitu mahali kilipo kuwepo hapo awali au kurudi kwa kitu kwenye hali yake ya mwanzo, wakati wa kurudi, na mahali pa kurudi.[42]

Dhana Zinazohusiana na Ufufuo (Ma’ad)

Kwa mujibu wa maoni ya Nasir Makarim Shirazi, ambaye ni mfasiri na faqihi, ni kwamba; Kuna tafsiri mbalimbali za ufufuo katika Qur’ani, ambapo Kiyama ndio tafsiri maarufu zaidi ya neno ufufuo, na Mwenye Ezi Mungu amelizungumzia suala la Ma’ad kwa kutumia neno Kiyama mara sabini ndani ya Quran.[43] Kwa maoni ya Naser Makarim Shirazi, kila moja ya majina na sifa hizi, inalenga moja ya vipengele vya sifa za ufufuo na siku ya Kiyama.[44] Kwa mtazamo wa Jafar Subhani, mfasiri na mwanatheolojia, ni kwamba; Majina na sifa mbalimbali za ufufuo katika Qur’ani, zinaonyesha mtazamo wa Qur’ani juu umuhimu wa ufufuo. Yeye akitoa ufafanuzi juu ya msingi huu, ameeleza kuwa; Kiyama ni mojawapo ya majina ya ufufuo katika Qur’ani.[45]

Baadhi ya majina na sifa mbalimbali za Ma’ad (ufufuo) katika Quran ni:

  1. Siku ya Akhera (یوم الآخِر)
  2. Siku ya Kukusanyika (یوم الجَمْع)
  3. Siku ya Ufufuo (یوم القِیامَة)
  4. Siku ya Malipo (یوم الدّین)
  5. Siku ya Kufufuliwa (یوم البَعْث)
  6. Siku ya Majuto (یوم الحَسْره)
  7. Siku ya Kutenganishwa (یوم الفَصْل)
  8. Siku ya Umilele (یوم الخُلود)
  9. Siku ya Kutoka Kaburini (یوم الخُروج)
  10. Siku ya Hesabu (یوم الحِسَاب)
  11. Siku ambayo watu watakusanywa (یَومً مَجْموعً له النّاس)
  12. Siku Inayozunguka Kila Kitu (یوم مُحیط)
  13. Siku Kubwa (یوم عَظیم)
  14. Siku ambayo itawafanya watoto kuwa wazee (یَومً یَجْعَلُ الوِلْدانَ شِیْباً)
  15. Siku Iliyowahidiwa (الیَوْمُ المَوْعُودُ)
  16. Siku ya Maumivu (یَوْمٌ أَلِيمٌ )
  17. Siku ya Kufichuka kwa Hasara (یوْمُ التَّغَابُنِ)
  18. Siku ya Kukutana (یوْمَ التَّلَاق)
  19. Siku ambayo hakuna nafsi itakayobeba adhabu ya nafsi nyingine (یَوْمَ لاتَجْزى‌ نَفْسٌ عَنْ نَفْسٍ شَیْئاً)
  20. Siku ambayo siri zitafichuka (یَوْمَ تُبْلَى السَّرَائِرُ)[46]

Uhalisia wa ufufuo (Ma’ad): Kiroho au Kijisimu (kiwiliwili)

Makala Asili: ufufuo wa Kijisimu

Kulingana na Fayyadh Lahiji ni kwamba; Hakuna khitilafu miongoni mwa Waislamu juu ya kukubalika kwa dhana na imani ya asilia uwepo wa maad;[47] hata hivyo, kuna tofauti juu ya kina cha uchambuzi wa Ma’ad, na jinsi ya utokeaji wake, na kwamba je, Ma’ad au ufufuo ni wa kijisimu, wa kiroho, au ni mchanganyiko wa kijisimu pamoja na kiroho.[48] Tofauti hizi za maoni zimetokana na tofauti katika ukweli na uhakika maumbile ya mwanadamu kiuhalisia yalivyo.[49] Mitazamo ya wanazuoni wa Kiislamu kuhusiana na jinsi ya ufufuo utakavyo tokea ni kama ifuatavyo:

  1. Ufufuo wa Kijisimu na Kiroho: Wanazuoni wengi wa Kiislamu wanaamini kuwa ufufuo ni ya kijisimu na kiroho.[50] Mtazamo huu umenukuliwa kutoka kwa wanafalsafa wote wa Kiislamu na hata tunaweza kusema ni kutoka kwa wanafalsafa wote wa kidini.[51] Hata Allama Majlisi pia naye ameeleza kuwa huu ndio mtazamo wa wanateolojia wengi.[52] Kulingana na maandishi ya Nassir Makarim Shirazi, ambaye ni mfasiri wa Quran, ni kwamba; Katika Quran kuna maelezo yanayo husiana na aina moja tu ya ufufuo, nao ni ufufuo (Ma’ad) wa Kijisimu na Kiroho peke yake. Ikimaanisha kwamba; wakati wa ufufuo, miili na roho zote zitarejea Akhera.[53] Yeyote yule anayeelewa na kuamini kuwa, uhakika wa maumbile halisi ya mwanadamu ni mchanganyiko wa nafsi isiyoonekana na mwili huu unaohisika, atakuwa ni mwenye kukubaliana na ufufuo wa Kijisimu na Kiroho.[54]
  1. Ufufuo wa Kijisimu pekee: Kulingana na Fakhruddin Razi na Fayyadh Lahiji, ni kwamba; wanateolojia wengi [55] na baadhi ya wanazuoni wa fiqh na waandishi wa Hadithi,[56] wanaamini tu juu ya uwepo wa Ma’ad ya Kijisimi, na wanakanusha uwezekano wa kuwepo kwa Ma’ad ya Kiroho. Sababu ya imani yao hii ni kwamba; kundi hili linaamini kuwa uhakika na uhalisia wa maumbile ya mwanadamu ni mwili huu wa kidunia tu.[57] Kwa maoni yao, roho ni kitu cha kimwili kinachotiririka mwilini kama moto kwenye makaa au maji kwenye majani ya maua, na hivyo, mwili unapokufa, roho nayo pia hufa na kuangamia.[58] Katika msingi wa imani hii juu ya ufufuo, mwili ulioharibika utajengwa upya na kurejeshwa kupitia elimu ya Mwenye Ezi Mungu isiyo na mipaka pamoja na uwezo wake.[59]
  2. Ufufuo wa Kiroho pekee: Kulingana na maelezo ya Ja’afar Subhani, ambaye ni mwanatheolojia wa Kimashsha'i ni kwamba; Wanafalsafa wengi wenye mwelekeo wa Kimashsha'i (wanafalsafa wa Aristotelian), wanakubali tu uwepo wa ufufuo (Ma’ad) wa Kiroho na wa Kiakili, na wanakanusha kuwepo kwa ufufuo (Ma’ad) wa Kijisimu. Kwa maoni yao; mwili huangamia baada ya matokeo ya kifo na hakuna kitu kinachobaki ili kirejeshwe tena Siku ya Kiama; ila nafsi, kwa kuwa haina umbo na kiwiliwili, hubaki hai bila ya kuangamia na baada ya kutenganishwa na mwili huu wa kidunia,[60] hujiunga na ulimwengu wa roho.[61] Ibn Sina, mwanafalsafa mkubwa wa falsafa ya Kimashsha'i (wanafalsafa wa Aristotelian), anaamini kuwa; ufufuo wa Kijisimu na kurejea kwa mwili kwenye ulimwengu wa Ma’ad, kunathibitishwa na kukubaliwa kupitia sheria na Hadithi za Mtume Muhammad (s.a.w.w) peke yake.[62] Allamah Majlisi amelihisabu suala la kukana na kukataa ufufuo wa Kijisimu kwa njia ya wazi kabisa, kuwa na ukafiri na ni sawa na kuikana Qur’ani, kumkana Mtume na Maimamu (a.s). [63] Yeye amewajumuisha wanafalsafa kuwa ni miongoni mwa wale wanaokanusha ufufuo wa Kijisimu, hii ni kwa kuwa wao wanaamini kuwa; urejeshwaji wa kitu kilichotoweka ni jambo la muhali na lisilowezekana.[64] Kwa maoni ya Fayyadh Lahiji, wale wanaoamini kuwa uhakika wa mwanadamu ni nafsi isiyoonekana na kwamba mwili ni chombo tu kinachotumiwa na nafsi, wao wanakubali tu uwepo wa ufufuo wa Kiroho peke yake.[65]

Nadharia Kuhusu Jinsi ya Ma’ad ya Kijisimu na Kiroho

Wale wanaoamini katika Ma’ad ya kiroho na kijisimu wameelezea maoni yao kwa namna tofauti kama ifuatavyo:

  1. Kurejea kwa Roho kwenye Mwili Hisiwa wa Kidunia: Kwa mujibu wa nadharia hii ambayo inachukuliwa kuwa ndio nadharia maarufu zaidi, nayo ni nadharia inayo husishwa na wanateolojia wa Kiislamu,[66] ambayo kwa mujbu wake; Mwenye Ezi Mungu katika Siku ya Kiama atakusanya sehemu zilizotawanyika za miili na kuumba miili inayofanana na ile miili wa mwanzo ya kidunia, kisha atazirejesha roho ndani ya miili hiyo.[67] Baadhi ya wanateolojia wanaamini kuwa sehemu kuu za mwili wa kila mtu ambazo hazibadiliki, ndizo zitakazo fufuliwa na kurudishwa katika uwanja wa Ma’ad. Kwa maoni yao sehemu hizo hutenganishwa na mwili wakati wa kifo cha mwanadamu, na hubaki kama zilivyo bila ya kubadilika, kisha Siku ya Kiama hukusanywa na kurejeshwa tena.[68]
  2. Kurejea kwa Roho kwenye Mwili wa Barzakh (Mwili wa Mbinguni): Kwa mujibu wa nadharia hii, roho zitarejea kwenye miili ya Kibarzakh ndani ya siku ya ufufuo (Ma’ad).[69] Ayatullah Subhani ameihusisha nadharia hii na wanahikima (wanafalsafa) wa Kiishraqi na kwa Mulla Sadra, akieleza tofauti zilizopo baina yao amese; Wanahikima (wanafalsafa) wa Kiishraqi hawakuweza kuthibitisha uhalisia wa fungamano la umoja lililopo kati mwili wa Kibarzakh (Mwili wa Mbinguni) wa Akhera na mwili huu wa kidunia, lakini Mulla Sadra alithibitisha uhusiano na umoja wa miili miwili hiyo. Kisha Mulla Sadra akazirudisha tofauti zilizopo baina ya miili miwili hiyo kwenye uhakika wa mfumo mapungufu wa ukamilifu, ambapo mwili wa kidunia hupevuka na kuachana na mapungufu yake hadi kufia hadhi ya kupaa na kuwa ni mwili wa mbinguni.[70]
  3. Kurudishwa kwa Roho Ndani ya Mwili wa Kifalaki, Ambao ni Mwili Ulio na Mfumo wa Moshi au Hewa: Kwa mujibu wa nadharia hii ambayo inahusishwa na Farabi na Ibn Sina, roho za wale ambao hawajakamilika na hawajakaitisha tamaa miili yao na matamanio ya dunia, miili yao itarudishwa kwenye roho za angani za kifalaki au miili ulio na umbile la moshi na hewa; lakini wale ambao wamekamilika roho zao zitaendelea kuishi bila mwili.[71]  

Nadharia nyingine ni pamoja na: Nadharia kurejea kwa 'mwili hisiwa (wa kimaada) kwenye roho isiyo na mwili hisiwa (nadharia ya Aqa Ali Mudarrisi), kurejea kwa roho kwenye mwili hisiwa (wa kimaada) uliokamilika (mtazamo wa Sayyid Abu al-Hasan Rafiei Qazwini), na kurejea kwa roho kwenye mwili wa Hurqaliaii ambao ni mwili wa Kibarzakh (Mwili wa Mbinguni), (nadharia ya Sheikh Ahmad Ahsa'i).[72]

Fungamano la Ma’ad na Suala la Nafsi

Imedaiwa kwamba; Kuthibitisha uwepo Ma’ad na kurejea kwa roho na nafsi kwenye miili, kunategemea uwepo wa nafsi isiyokuwa na maumbile hisiwa ya kiwiliwili na kudumu kwake.[73] Muhammad-Taqi Mesbah Yazdi anaamini kwamba; Maisha baada ya kifo yanaweza kufikirika na kueleweka kwa usahihi iwapo nafsi itachukuliwa kuwa ni kitu kisichoweza kugusika wala kuhisika ambacho kinatofauti na mwili pamoja na sifa zake.[74][75] Kwa msingi huu, dhana sahihi na ya busara ya maad inategemea kukubaliana na mambo yafuatayo: Uwepo wa roho (nafsi), roho kuwa ni kiini asili (jauhar), huru mpambanuko wa roho kutokana na mwili na kudumu kwake baada ya kifo cha mwili, na kukubali kwamba, roho ndiyo sehemu kuu na uhalisia wa mwanadamu, na uwepo wake, ndio unao dhamini uwepo wa ubinadamu wa mwanadamu.[76]

Wakristo pia wanakubali kwa kiasi kikubwa maisha baada ya kifo kwa; kuamini kwamba nafsi ni kiumbe kisicho hisika wala kugusika na ni kiumbe huru kipambanukacho na mwili, hadi kufikia hatua ya kusemekana kwamba; wasomi wote muhimu katika historia ya Ukristo walikuwa wakikubaliana na mtazamo huu.[77]

Suala la Utambulisho Sawa wa Mwanadamu wa Maisha ya Kidunia na wa Akhera

Imani ya ufufuo (Ma’ad) inategemea ukweli kwamba mtu anayefufuliwa Akhera ni yule yule aliyekuwa akiishi duniani humu. Hili kwa lugha ya Kiarabu linajulikana kama dhana ya "hauhawiyyah" yenye mana ya utambulisho ule ule (wa mwanzo).[78] Kusudi la dhana ya utambulisho huu wa mtu uitwao "hauhayyah", katika mjadala wa ufufuo ni kujenga swali ya kwamba, je, mtu anayebaki baada ya kifo chake ni yule yule mmoja kwa upande wa idadi?  Na siyo upande wa kihali na sifa.[79]

[Maelezo 1]

Wanafalsafa wengi wa Kiislamu [Chanzo kinahitajika] na wa Kikristo[80] wanakubali umoja wa utambulisho wa mwanadamu wa idadi (yaani yeye ndiye yule yule mmoja duniani na Akhera). Imeelezwa kuwa hata Biblia ya Wakristo pia inafundisha mtazamo huu.[81]

Kuhusiana na swali la kwamba ni kipengele gani kinacholeta umoja wa utambulisho wa mtu wa kidunia (kabla ya kifo) na mtu wa Akhera (baada ya kifo)? Wanafalsafa wa Kiislamu wanasema kwamba; nafsi ndio kigezo na kipengele unganishi cha umoja wa mtu wa kidunia na wa Akhera. Kwa mtazamo wao, mwili hauwezi kuwa kipengele unganishi cha kuleta umoja wa utambulisho, hii ni kwa sababu ya mabadiliko na uharibikaji wake.[82] Kwa mujibu wa maoni ya Mulla Sadra; Kigezo cha kudumu umoja wa utambulisho wa mtu, ni kule kudumu kwa nafsi yake. Kwa mtazamo wake, madhali nafsi ya mtu ipo, naye pia yupo, hata kama sehemu za mwili wake zitakuwa zimebadilika. Kwa mfano tukiulizia habari za utotoni za mtu fulani aitwaye “Zaidi”, na ujana kwake hadi uzee kwake, kwa mtazamo wa Mulla Sadra, sisi tutakuwa tunaulizia habari “Zaidi” mmoja tu, na ni yule yule “Zaidi” wa mwanzo, hii ni kwa sababu ya kwamba nafsi yake inabakia kuwa ni nafsi ile ile ya awali. Hivyo basi hata Akhera bado “Zaid” atabakia kuwa ni yule yule “Zaid” wa duniani, kwa sababu ya kudumu kwa nafsi yake.[83]

Muhammad-Taqi Misbah Yazdi naye kwa kutokana na kukubaliana na kigezo cha nafsi; na anaamini kuwa bila kukubali uwepo wa nafsi huru isiyogusika wala kuhisika ambayo inapambanuka na mwili, katu dhana ya maisha ya pili ya mtu aliyeishi kabla ya kifo haiwezi kueleweka.[84] Kwa mtazamo wake, kwa kuwa nafsi ni kitu kisichokuwa umbile la kimaada na wala haibadiliki si kabla wala si baada ya kifo, na kwamba inaweza kudumu hata baada ya kifo cha mwili na inaungana tena na mwili, bila shaka nafsi hii ndiyo inayo hifadhi umoja na utambulisho wa mwanadamu. Ila ikiwa mtu ataamini kuwa uhakika wa mwanadamu ni mwili wake huu wa kidunia peke yake unaohisika kwa hisia tano, basi kuharibika kwa mwili wake, kutakuwa ndio kumalizika na kuhitimika kwa uwepo wake. Kwa hiyo, mwenye imani kama hii katu haotoweza kutoa mtazamo sahihi unao ingia akilini juu ya dhana ya ufufuo.[85]

Aya ya 11 ya Surat al-Sajda inachukuliwa kuwa ni ushahidi wa mtazamo huu, ikionyesha kuwa utambulisho halisi wa mwanadamu na utu wake ndiyo kitu kitiwacho mkononi na Malaika wa Mauti, sio mwili wake unaoangamia na kuoza.[86]

Kigezo chengine ni kigezo cha mwili au ubongo (kuwa na mwili au ubongo mmoja kwa muda wote), pia kigezo cha kumbukumbu (kuendelea kwa kumbukumbu na kukumbuka matukio kwa muda wote) ni miongoni mwa vigezo na nadharia nyingine zilizopendekezwa na wale wanaokataa uwepo wa nafsi katika suala la utambulisho mmoja endelevu wa mwanadamu.[87]

Uwezekano wa Tukio la Ufufuo

Ili kuthibitisha uwezekano wa ufufuo na kutouona kama ni jambo lisilowezekana, wametegemea makundi matatu,[88] matano[89] au sita ya[90] Aya za Qur'ani. Ayatullah Jawadi Amuli ameeleza Aya hizo katika makundi matano tofauti yafuatayo:

  1. Aya zinazohusiana na uumbaji wa awali wa binadamu: Aya ya 79 ya Surat Yasin, Aya ya 27 ya Surat Rum, na Aya ya 19 ya Surat Ankabut. Aya ya 27 ya Surat Rum inasema kwamba; Mwenye Ezi Mungu huanzisha uumbaji na kisha huurudisha tena, na kurejesha uumbaji ni jambo rahisi zaidi kwake.
  2. Aya zinazozungumzia uumbaji wa ulimwengu, hasa mbingu: Aya ya 99 ya Surat Isra, Aya ya 57 ya Surat Ghafir, na Aya ya 33 ya Surat Ahqaf. Aya ya 81 ya Surat Yasin inasema; Je, yule aliyeziumba mbingu na ardhi hana uwezo wa kuwafufua binadamu siku ya Kiyama?
  3. Aya zinazozungumzia uhai wa ardhi kama mfano wa uwezekano wa ufufuo wa wafu: Aya ya 19 na 50 ya Surat Rum, Aya ya 9 ya Surat Fatir, na Aya ya 57 ya Surat A'raf.
  4. Aya zinazozungumzia mwanzo wa uumbaji wa binadamu na hatua za maendeleo ya kijusi hadi kuwa binadamu kama mfano wa uwezekano wa ufufuo: Aya ya 5 na 6 ya Suratu Hajj, Aya ya 12 hadi 16 ya Suratu Muminun, na Aya ya 37 hadi 40 ya Suratu Qiyama. Aya ya 37-40 za Suratu Qiyama, zinasema kwamba; Je Mungu aliyemuumba binadamu kutoka kwa tone la manii na damu iliyoganda, hawezi kuwafufua (kuwarudisha) wafu?
  5. Aya ambazo zinazotoa baadhi ya mifano hai na ya wazi ya wafu waliofufuliwa baada ya kufa kwao.[91]

Baadhi ya mifano hai ya kufufuliwa kwa kwa wafu waliotajwa ndani ya Qur'ani kama ifuatavyo:

Hoja za Uhitaji na Uthibitisho wa Ufufuo

Kuna hoja na sababu nyingi zilizo tolewa ili kuthibitisha uhitaji na ukweli juu ya ufufuo. Kwa mfano, Abdullah Javadi Amuli, mwanafalsafa na mfasiri wa Qur'ani, ametaja hoja tisa,[93] Ja’afar Subhani ametaja hoja sita,[94] na Nassir Makarim Shirazi ametaja hoja saba.[95] Hoja za Ayatullah Jawadi Amuli ni kama zifuatazo: Hoja ya Tawhidi, Hoja ya Ukweli, Hoja ya Asili ya Kimaumbile, Hoja ya Safari katika Nyenendo Tofauti na  uwepo wa Malengo, Hoja ya Hekima, Hoja ya Rehema, Hoja ya Hakika Asilia, na Hoja ya Uadilifu na Roho Kuishi Bila Mwili.[96]

Hoja ya (Ta’abbudi) au Hoja ya Kuamini Ukweli wa Maneno ya Mungu

Mojawapo ya sababu za ulazima wa kuwepo kwa ufufuo ni hoja ya kuanimi maneno ya Mungu. Tunapojua na kukubali kuwa Qur'ani ni maneno ya Mwenye Ezi Mungu, na mara nyingi Mwenyezi katika Qur'ani Mungu amesema kwamba; baada ya maisha haya ya kidunia, kuna maisha mengine ya baadae yatakayo jiri baada ya kufufuliwa kwa wanadamu, basi bila shaka jambo hilo halitakwenda kinyume.[97] Kulingana na uchambuzi wa Muhammad Taqi al-Misbah al-Yazdi, ni kwamba; kuna karibu ya Aya elfu mbili za Qur'ani zinaashiria moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja kuhusiana na ufufuo.[98] Kwa mujibu wa maelezo ya Javadi Amuli; Kwa kuwa Mwenye Ezi Mungu, ambaye ni mkweli kabisa, ametamka wazi kuhusiana na utekelezaji wa maisha ya baadae, basi bila shaka maisha hayo ya baadae yatatimia tu bila ya kuwepo pingamizi yoyote.[99]

Imeelezwa ya kwamba wafuasi wa Ash'ari wanathibitisha uwepo wa Maisha ya baadae (ufufuo) kupitia Qur'ani na Sunna, na si kwa hoja za akili wala za kimantiki.[100]

Hoja ya Maumbile Asilia (Hoja ya Kifitra)

Fitra kwa maana ya uumbaji, tabia na asili ambayo kila kiumbe anayo mwanzoni mwa uumbaji wake.[101] Misingi kuhusiana na hoja hii imeelezewa kwa mfumo ufuatao:

  • Katika maumbile asilia ya binadamu, kuna hamu ya kupenda dunia na maisha ya milele, na kuto penda au kuto ridhika na suala la kutokuwepo na kuangamia.
  • Kila kitu kilichowekwa ndani ya maumbile asilia ya binadamu ni kweli na sahihi, na siyo bure.
  • Hamu na upendo wa binadamu kuwa na maisha ya kudumu na kuendelea kuwepo, ni ushahidi wa kuwepo kwa dunia ya milele na iliyo hifadhiwa kutokana na kuangamia.
  • Dunia hii ya asili haina ustahili wala uwezo wa kudumu na kubaki milele.
  • Kwa hivyo, kama hakuna dunia nyingine yenye uwezo wa kudumu, tamaa ya binadamu ya kudumu na kuendelea kuwepo, iliowekwa (ilioko) katika maumbile yake itakuwa batili isio na faida wala malengo.
  • Katika dunia ya hii hisiwa na ya kimaada, hakuna kitu batili; kwa sababu imeumbwa na Mungu mwenye hekima. Kwa hivyo natija misingi sita ya mwanzo ni kwamba, kuna dunia na maisha ya milele.[102]

Hoja ya Hekima

  • Hoja hii ina tafsiri tofauti.[103] Moja ya tafsiri na uwasilishaji wake hoja unategemea (umeegemea kwenye) nguzo ya lengo la uumbwaji wa mwanadamu na ulimwengu kwa jumla. Kulingana na tafsiri hii:
  • Maisha ya Akhera ndio lengo na madhumuni hasa ya kuumbwa kwa mwanadamu na ulimwengu.
  • Ikiwa ulimwengu wa Akhera hauta kuwepo! Basi maisha ya mwanadamu na ulimwengu mzima yatamazilizia ndani ya ulimwengu huu tu wa kimaada, na uumbwaji wa mwanadamu utakuwa ni bure na batili na usio na thamani thaminika; hii ni kwa sababu ulimwengu huu wa kimaada pamoja na yaliomo ndani yake, yote kwa jumla ni mambo ya mpito tu.
  • Mwenyezi Mungu ni mwenye hekima na yumbali mno na wala haiyumkiniki kufanya kitu cha bure kisicho na maana wala thamani yenye kuthaminika kimantiki.
  • Kwa hivyo, natija ya misingi hii ni kwamba; Ni lazima kuwe na ulimwengu mwingine baada ya ulimwengu huu hisika wa kimwili (kimaada), ili ikubalike kimantiki kwamba; kuumba kwa mwanadamu kuna malengo yathaminikayo kiakili.[104]

Pia Aya ya 115 ya Surat Muminun, Aya ya 27 ya Surat Sa’ad na Aya ya 38 na 39 ya Surat Dukhan zinachukuliwa kama ni dalili zinazorejelea hoja hii.[105]

Hoja ya Haki au Uadilifu

Hoja hii inayotegemea uadilifu wa Mungu, imethibitisha kama ifuatavyo:

  • Moja ya sifa za Mwenye Ezi Mungu ni uadilifu, na ulimwengu huu umesimama juu ya msingi wa uadilifu.
  • Mwanadamu katika dunia ana huru wa ima kufanya matendo mema au mabaya.
  • Kwa sababu ya uhuru huo, baadhi ya watu hutumia uwezo waliokuwa nao kwa ajili ya Mungu na kutenda wema, na wengine hutumia huutumia uwezo wao wote waliokuwa nao kwa ajili ya kuridhisha tamaa zao na kufanya dhambi.
  • Dunia hii haina uwezo wa kumfanya mmoja aone kikamilifu natija na matokeo ya matendo yake; yaani si thawabu, wala adhabu zinaweza kulipwa kwa viwango vyake kamili.

Natija ya misingi hii ni kwamba; Dhana ya uadilu wa Mwenye Ezi Mungu inatoa msukumo wa ulazima wa kuwepo kwa ulimwengu mwingine wa haki baada ya ulimwengu huu wa kimwili, ili haki itendeke na kila mmoja apate hesabu yake kikamilifu na kwa hadhi na thamani ya juu kabisa anayostahiki kupata.[106]

Aya Isemayo: (أَمْ نَجْعَلُ الَّذِینَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ كَالْمُفْسِدِینَ فِی الأَرْضِ أَمْ نَجْعَلُ الْمُتَّقِینَ كَالْفُجَّارِ ; Je, (yayumkinika kwamba) tuwafanye wale waliomuamini Mwenye Ezi Mungu na kufanya matendo mema kuwa sawa na wafanyao ufisadi duniani, au (yayumkinika kwamba) tunawafanya wale wenye kumcha Mungu kuwa sawa na mafisadi?)[107] Pamopa na Aya ya 21 - 22 za Surat al-Jathiya, Aya ya 58 ya Surat al-Muumin, Aya ya 35 na 36 ya Surat al-Qalam, zinahisabiwa kama Aya zinazorejelea hoja hii.[108]

Kukanusha Ufufuo

Kwa mujibu wa maoni ya Ayatollah Jawadi Amoli, ni kwamba; Mara nyingi suala la kukataa na kukanusha mambo ya kiitikadi na imani, ikiwemo imani ya ufufuo (Ma’ad), hutokana na kutokukua na elimu juu ya masuala hayo. Wale wanaokataa ma’ad hawakuwa na uelewa sahihi na wa kina juu ya maana ya ufufuo, na hoja yao katika ukanushaji wao, ilikuwa ni kuona kwamba suala la ufufuo ni jambo lisilowezekana. Kamwe hawakutoa hata sababu moja iliopelekea kukataa na kukanusha Ma’ad.[109]

Sababu za kukataa Ma’ad zimehusishwa na mambo kadhaa ikiwemo: ujinga, kupuuza uwezo wa Mwenye Ezi Mungu,[110] tamaa ya kuwa na huru bila mipaka, kutojali wajibu unaomkabili mwanadamu[111] na tamaa ya uongozi na nguvu za kiutawala.[112] Katika Aya ya 24 ya Surat al-Jathiya, ujinga umetajwa kuwa ndio sababu ya kukataa Ma’ad,[113] na katika Aya ya 3-5 ya Surat al-Qiyama, tamaa ya uhuru usio na mipaka na kutokuwa na wajibu ndio sababu za jambo hilo,[114] ila katika Aya ya 33-38 za Surat Muminun, kutafuta nguvu na kutawala ndiko kunakompa mtu kukataa Ma’ad.[115]

Wanafalsafa wanao shikamana na nadharia ya kukataa uwepo wa nafsi isiyo hisiwa (Naturalistic philosophers) wamekuwa wakikanusha msingi wa imani ya ufufuo.[116] Kwa mtazamo wa Wanafalsafa hawa, uhakika wa mwanadamu ni kiwiwili hisiwa tu ambacho kwa sababu ya tukio la kifo huharibika na kutoweka kabisa kabisa. Kwa upande mwingine, kurejesha kitu kilichopotea ni jambo muhali na lisilowezekana. Kwa hivyo, kurejeshwa kwa mwanadamu baada ya kifo ni jambo lisilowezekana.[117] Imesemekana kuwa baadhi kama vile Galen na wafuasi wake walikuwa na shaka juu ya asili ya ufufuo (Ma’ad),[118] hii ni kwa sababu wao walikuwa na shaka kama je, nafsi ya mwanadamu ni mchanganyiko wa kimwili ambao hupotea kupitia tukio la kifo au ni dutu (substance) yenye uwezo wa kubaki baada ya kifo.[119]

Vikwazo Juu ya Ufufuo

Kuna vikwazo vingi kuhusiana na uwezekano na uhakika wa ufufuo (Ma’ad) ambavyo vimetajwa na wale wanaokataa kuwepo kwa jambo hilo. Baadhi ya vikwazo hivyo ni kama ifuatavyo:

Kikwazo cha Mla na Mliwa

Kwa mujibu wa kikwazo hichi; kama mwanadamu mmoja ataliwa na mwanadamu mwingine, je, katika ulimwengu wa Ma’ad (ufufuo), sehemu za mwili wa yule aliyeliwa zitarejeshwa katika mwili wa yule mlaji, au zitarejeshwa kwenye mwili wa yule aliyeliwa? Ikiwa sehemu hizo zitarejeshwa kwa yeyote yule kati yao, basi mwili wa mmoja wao hautakuwa ni mwili kamili katika siku hiyo ya Ufufuo.[120] Kikwazo hichi pia kimeelekezwa kwa namna nyengine isemayo kwamba; kama kafiri ataula mwili wa muumini, basi siku ya Kiama muumini ataingia matesoni na kafiri ataneemeka kwa kiwango fulani, hili ndio tatizo la kukubaliana na dhana ya ufufuo wa miili ya kidunia siku ya Kiama.[121]

Majibu ya Kikwazo

Kuna majibu mbalimbali yaliyotolewa katika kujibu hoja za kikwazo hichi. Baadhi ya wanatheolojia kama vile Allamah Hilli wanasema kwamba; Hoja za kiwazo hichi zinaweza kujibiwa njia ya kutofautisha kati ya sehemu kuu au asilia na zile zisizo asilia za mwili ya kilimwengu, sehemu kuu za mwili wa kila mtu zinabaki kama zilivyo tokea mwanzo hadi mwisho wa maisha na hazigeuki kuwa ni sehemu kuu za mwili wa mtu mwingine. Kwa hiyo sehemu kuu hizo ndizo zitakazorejeshwa siku hiyo ya ufufuo.[122] Mulla Sadra anaamini kwamba; Utambulisho halisi na ukweli wa mwanadamu ni nafsi yake, na siyo mwili wake. Kwa hivyo, hakuna haja Akhera kufufuliwa mwili uleule wa kidunia ulioliwa na mwanadamu au mnyama mwingine; badala yake, mwili wowote ule ambao nafsi itahusishwa nao, kwa maana halisia mwili huo utakuwa ni mwili wa mtu huyo bila ya kutokea matatizo yoyote yale. Kwa mujibu wa maoni yake, ni kwamba; kinachohitajika katika ufufuo wa miili ni kule kila mmoja atakaye muona mtu huyo aliyefufuliwa aweze kusema kwamba; huyu ndiye mtu yule yule wa kidunia, na mwili wake ni mwili uleule wa kidunia.[123]

Pia kiwazo hichi kimejadiliwa katika Ukristo kama ni kikwazo cha ulaji wa nyama za watu.[124]

Kikwazo Juu ya umuhali Kurudishwa Kile Kilichopotea na Kuangamia

Makala Asili: Kurudishwa Kile Kilichopotea na Kuangamia

Kutowezekana na umuhali wa kurudisha kilichopotea na kuangamia; Ni moja ya hoja na vikwazo vinavyowekwa na wale wanaokanusha uwepo wa ufufuo.[125] Kwa mujibu wa kikwazo hichi; wanaokanusha ufufuo walidhani kwamba uhalisia na uhakika kamili wa mwanadamu ni huu mwili wa hisiwa (wa kimaada) tu, na pale mtu anapokufa anapotea na kutokomea kabisa kabisa. Hivyo basi iwapo mtu huyo atakuja kufufuliwa tena, basi yeye atakuwa ni mtu mwingine kinyume na yule wa awali; hii kwa kuwa ni muhali kukirudisha tena kitu ambacho tayari kimesha angamia na potea.[126]

Katika kujibu hoja za kikwazo hicho, imeelezwa ya kwamba; Kwa kuzingatia Aya ya 10 na 11 za Surat Sajda, ni kwamba, utambulisho halisi na uhakika wa mwanadamu unategemea roho yake, na siyo mwili na viungo vya kiwiliwili hisiwa. Kwa hiyo, ufufuo hauna maana ya kurudisha kile kilichopotea; bali ni kurudishwa kwa roho asilia.[127] Katika kujibu kikwazo hichi, baadhi ya wanatheolojia wamedai kwamba; Hakuna umuhali wowote ule katika suala la kurudishwa kitu kilichopotea. Kwa maoni yao ni kwamba; Ikiwa tutakubaliana juu ya umuhali wa kurudisha kile kilichopotea, basi ufufuo utakuwa na maana ya ni kurudisha sehemu za miili kama vile ilivoumbwa mwanzo kabla ya tukio la kifo.[128]

Kikwazo Kuhusiana na Elimu na Uweza wa Mungu

Moja ya vikwazo kuhusiana na ufufuo ni kwamba; Kufufulia kwa wafu kunategemea elimu na ufahamu wa sehemu zote zilizotawanyika za miili ya wafu hao, ili sehemu za kila mtu zirudi kwenye mwili wa mhusika asilia wa mwili huo, hali ya kwamba ni muhali uwezekano wa kuwepo kwa elimu na ufahamu kama huo. Inawezekanaje kuitambua miili iliyokuwa tayari imeshakuwa udongo, na chembechembe zake zimechanganyika?[129] Baadhi ya waliojibu hoja za kikwazo hichi, wamerejea Aya ya 3 ya surat Saba inasemayo: «عَالِمِ الْغَيْبِ لَا يَعْزُبُ عَنْهُ مِثْقَالُ ذَرَّةٍ فِي السَّمَاوَاتِ وَلَا فِي الْأَرْضِ وَلَا أَصْغَرُ مِنْ ذَلِكَ وَلَا أَكْبَرُ إِلَّا فِي كِتَابٍ مُبِينٍ ; (Mwenye Ezi Mungu ni) Mwenye kujua siri, (Naye Ndiye Yule) ambaye hakuna hata chembe ndogo ya vumbi mbinguni wala ardhini inayofichika Naye, wala ndogo kuliko hiyo, wala kubwa zaidi kuliko hiyo, isipokuwa ipo katika kitabu kilichowazi».[130] Kikwazo hichi kimetolewa na wale waisotambua uwezo wa elimu ya Mwezye Ezi Mungu isiyo na mipaka, ambao wanailinganisha ya Mungu na elimu zao finyu; lakini elimu ya Mungu haina mipaka, na Mwezye Ezi Mungu ni mweye ulimu juu ya wa kila kitu.[131]

Kikwazo chengine kuhusiana na ufufuo ni kwamba; Inawezekanaje kuthibitisha kwa Mwezye Ezi Mungu ana uwezo wa kufufua wafu? Katika kujibu shaka hii, imesemwa kuwa; Uwezo wa Mwezye Ezi Mungu hauna mipaka na unahusiana na kila kitu kinachoyumkinika kiakili kutokea; kama ilivyo katika Qur’ani: «وَ اللَّهُ‏ عَلى‏ كُلِ‏ شَيْ‏ءٍ قَدِير ; Na Mwenyezi Mungu ni Mueza juu ya kila kitu».[132] Zaidi ya hayo, kuumba tena kama haitakuwa ni si rahisi zaidi kuliko ugumu wa kuanzisha umbile kwa mara ya kwanza, bila shaka hakutakuwa ni kazi ngumu zaidi.[133] Pia Aya za Qur’ani zimetaja wazi kwamba; Mungu atakurudisheni tena baada ya kifo chenu, Ndiye Mungu Yule Yule aliye kuumbeni mara ya kwanza.[134]

Biliografia (Vitabu Kuhusu Masuala ya Ufufuo)

Kitabu Manhaj al-Rashad fi Ma'arifat al-Ma'ad kilichoandikwa na Muhammad Na’īm Taliqani.

Masuala ya ufufuo kwa kawaida huchukua muhimu sehemu katika vitabu vya kitheolojia[135] na tafsiri za Qur'an,[136] lakini zaidi ya hayo, kuna vitabu kadhaa vilivyoandikwa ambavyo ni maalum kuhusiana mada hii. Katika kitabu cha cha rikodi kuhusiana na mada hii Manba’a Shenasi Ma’ad, kumerikodiwa vitabu 1098, tasnifu 240, na makala 512 zinazozungumzia masuala ya ufufuo.[137] Baadhi ya vitabu hivi ni kama ifuatavyo:

  • Sabīl al-Rashād fī Ithbāt al-Ma'ād: Kilichoandikwa na Aqā Ali Mudrris Tihrānī (aliyeidhi mnamo mwaka 1234 hadi 1307 Hijiria); Mwandishi katika kazi hii anaeleza maoni yake binafsi dhidi ya nadharia ya Mullā Ṣadrā kuhusiana na mada ya ufufuo wa kimwili.
  • Manhaju al-Rashādi fī Ma'rifati al-Ma'ād kilichoandikwa na Muhammad Na’īm Tāliqānī, ambaye ni mmoja wa wanazuoni wa Shia wa karne ya 12 Hijiria.
  • Ma'ādshenāsī: kilichoandikwa na Sayyid Muhammad Hussein Husseinī Tehrānī: Kitabu hichi chenye tafiti kumi ndani yake, ni mfululizo wa mihadhara ya Allamah Tehrānī juu ya ufufuo na masuala yanayohusiana nayo. Tafiti zake zinajumuisha Aya za Qur'an, Hadithi, na tafiti za kifalsafa na kiifrani kuhusu ufufuo.[138]
  • Ma'ād dar Qur'an: (Juzuu ya Nne na ya Tano ya kitabu “Tafsiri Maudhui Qur'an”) kilichoandikwa na Abdullah Jawādī Āmulī: Kitabu hichi ni mkusanyiko wa maelezo ya Ayatullah Jawādī Āmulī katika vikao vya “Tafsiri Maudhui Qur'ani”, tafiti za mada ya ufufuo zimewasilishwa katika juzuu mbili za kitabu hichi, amabazo ni juzuu ya nne na ya tano.
  • Ma'ād Insani wa Jahān: kilichoandikwa na Jafa’ar Subhānī: Kitabu hichi chennye jina hili, ni juzuu ya sita ya mkusanyiko wa kitabu chenye juzuu sita kuhusiana na imani za Kiislamu, kilichochapishwa kwa mara ya kwanza kabisa mnamo mwaka 1358 Shamsia na Taasisi ya Uchapishaji ya Sadr.[139] Kitabu cha «Ma'ādshenāsī» pia kinatokana na tafiti za Ayatullah Subhānī juu ya masuala ya ufufuo ziliopo katika kitabu chake kiitwacho Ilāhiyyāti 'alā Hudā al-Kitābi wa al-Sunnati wa al-'Aqli, ambacho kilikuja kufasiriwa na Ali Shirwani na kuchapishwa kama ni kitabu huru.

Vitabu vingine kuhusu na masuala ya ufufuo ni:

Vitabu hivi vinatoa mitazamo na tafiti za kina kuhusiana na imani ya Kiislamu juu ya ufufuo, pamoja na marejeo kutoka kwenye Qur'ani, hadithi, falsafa, na tafsiri mbalimbali.  

Maudhui Zinazo Husiana

  • Tajarud al-Nafsi (Nafsi katika umbile lake lisilo la kimaada (kiwiliwili hisika)).
  • Tanasukh (Marudio ya Nafsi mara mara kwenye ulimwengu huu wa Maada (kiwiliwili hisika)).

Maelezo

  1. Ubakiaji wa utambulisho wa mwanadamu kwa upande wa kiidadi, unamaanisha kuwa; mtu aliyekuwepo kabla ya kifo na mtu aliyefufuliwa baada ya kifo hicho ni yule yule. Hii ni tofauti na ubakiaji wa utambulisho wa mtu kihali ambapo watu wawili (wa kidunia na Kiakhera) huwa ni wamoja kimfanano tu kutokana na kuwa na sifa zifananazo. (Tazama: Maslin, Daraamad Bar Falsafeye Zihni, 1391 Shamsia, uk. 361.)

Rejea

  1. Ashtiani, Sayyid Jalaluddin, Sharh Bar Zad al-Musafir, Qom, Bustan Kitab, Toleo la kwanza, 1381 S.
  2. Ashtiani, Mirza Ahmad, Lawamiu al-Haqaiq Fi Usul al-Aqaid, Tahqiq Mohsen Ashtiani, Qom, Congress Allamah Ashtiani , 1390 S.
  3. Ibrahimzadeh, Abdullah na Ali-Ridha Ali-Nuri, Adiyan Ilahi wa Firaq Islamami, Qom, Intisharat Tahsin, Toleo la pili, 1383 S.
  4. Ibn Sina, Hussein bin Ali, Al-Shafa (Al-Ilahiyyat), Qom, Maktaba Ayatullah Mar-ashi, 1404 AH.
  5. Ikhwan Muqadam, Zahra na Wenzake, Man'bai-Sheneasi Ma'ad, Tehran, Daneshyaran Iran, Toleo la kwanza, 1395 S.
  6. Misbah Yazdi, Amuzish Aqaid, 1384 S, uk. 363.
  7. Mutahari, Majmue Athar, 1390 S, juz. 2, uk. 507.
  8. Misbah Yazdi, Amuzish Aqaid, 1384 S, uk. 341-342.
  9. Surat al-Qasas, Aya ya 82.
  10. Subhani, Ma'adshenasi, 1387 S, uk. 15.
  11. Subhani, Ilahiyat, 1413 AH, juz. 4, uk. 164.
  12. Misbah Yazdi, Amuzish Aqaid, 1384 S, uk. 341-363.
  13. Tazama: Surat al-Baqarah, Aya ya 4; Surat Naml, Aya ya 3.
  14. Tazama: Surat al-Israa, Aya ya 10; Surat al-Furqan, Aya ya 11; Surat Sabaa, Aya ya 8; Surat al-Muuminun, Aya ya 74.
  15. Tazama: Surat ar-Rahman, Aya ya 46 hadi mwisho; Surat al-Waqia, Aya ya 15-38; Surat ad-Dahr, Aya ya
  16. Tazama: Surat al-Haqah, Aya ya 20-27; Surat: al-Mulku, Aya ya 5-11; Surat al-Waqia, Aya ya 42 na 56.
  17. Misbah Yazdi, Amuzish Aqaid, 1384 S, uk. 341.
  18. Tazama: Injili ya Yohana, sura ya 5, Mstari wa 28 na 29; Injili ya Luka, Sura ya 20, Aya ya 34-38; Injili ya Mathayo, sura ya 22, mstari wa 23-33.
  19. Mary na Ray, Dar-omadi Be Falsafe Dini, 1398 S, uk. 399 na 400.
  20. Tazama: Ayubu, sura ya 24, Kifungu cha 19; Zaburi, sura ya 9, Kifungu cha 17 na sura ya 49 Kifungu cha 14 na 15.
  21. Tazama: Ufunuo, sura ya 9, Kifungu nambari 1 na 2 na sura ya 20, Kifungu nambari 1-3.
  22. Tisin, Ilahiyat Masihi, Intisharat Hayat Abadii, uk. 362 na 363.
  23. McGrath, Darsname Ilahiyat Masihi, 1384 S, juz. 1, uk. 55-57; Patterson na Wenzake, Aqlu wa Itiqad Dini, 1376 S, uk. 319.
  24. Tawfiqi, Ashnai Ba Adiyan Buzurge, 1386 S, uk. 110.
  25. Subhani, Ilahiyat, 1413 AH, juz. 4, uk. 160.
  26. Mwanzo Samuel, sura ya 2, Kifungu cha 6.
  27. Ibrahim-zadeh na Ali-Nuri, Adiyan Ilahi wa Firaq Islami, 1383 S, uk. 119; Tawfiqi, Ashnai Ba Adiyan Buzurge, 1386 S, uk. 62.
  28. Ibrahim-zadeh na Ali-Nuri, Adiyan Ilahi wa Firaq Islami, 1383 S, uk. 119 na 120; Tawfiqi, Ashnai Ba Adiyan Buzurge, 1386 S, uk. 62.
  29. Ibrahim-zadeh na Ali-Nuri, Adiyan Ilahi wa Firaq Islami, 1383 S, uk. 119 na 120.
  30. Makarim Shirazi, Payam Qur'an, 1386 S, juz. 5, uk. 17.
  31. Misbah Yazdi, Amuzish Aqaid, 1384 S, uk. 339 na 340.
  32. Jawadi Amuli, Ma'ad Dar Qur'an (1), 1395 S, uk. 22
  33. Subhani na Baranjkar, Ma'arif wa Aqaid 1 na 2, 1397 S, uk. 358.
  34. Subhani na Baranjkar, Ma'arif wa Aqaid 1 na 2, 1397 S, uk. 358.
  35. Subhani na Baranjkar, Ma'arif wa Aqaid 1 na 2, 1397 S, uk. 358.
  36. Misbah Yazdi, Amuzish Aqaid, 1384 S, uk. 340 na 341; Misbah Yazdi, Insan-Shenasi Dar Qur'an, 1401 S, uk. 173.
  37. Namazi, Ma'ad Az Didegi Ayat wa Riwayat, 1385 S, uk. 12-15.
  38. Tazama: Fayadh Lahiji, Gohar Murad, 1383 S, uk. 596; Majlisi, Haqu al-Yaqin, Intisharat Islami, juz. 2, uk. 369; Khatami, Farhang Ilmu Kalam, 1370 S, juz. 1, uk. 204.
  39. Tazama: Jawadi Amuli, Ma'ad Dar Qur'an (1), 1395 S, uk. 21 na 137.
  40. Taftazani, Sharh al-Maqasid, 1409 AH, juz. 5, uk. 82.
  41. Namazi, Ma'ad Az Didegi Ayat wa Riwayat, 1385 S, uk. 15.
  42. Majlisi, Haqu al-Yaqin, Intisharat Islami, uk. 369.
  43. Makarim Shirazi, Payam Qur'an, 1386 S, juz. 5, uk. 29 na 31.
  44. Makarim Shirazi, Payam Qur'an, 1386 S, juz. 5, uk. 44.
  45. Subhani, Ilahiyat, 1413 AH, juz. 4, uk. 166.
  46. Tazama: Subhani, Al-Ilahiyat, 1413 AH, juz. 4, uk. 166; Makarim Shirazi, Payam Qur'an, 1386 S, juz. 5, uk. 45-102.
  47. Fayadh Lahiji, Gohar Murad, 1383 S, uk. 621.
  48. Tazama: Fakhr Razi, Al-Arbain Fi Usul al-Din, 1986, juz. 2, uk. 55; Fayadh Lahiji, Gohar Murad, 1383 S, uk. 621; Subhani, Manshur Javid, 1383 S, juz. 5, uk. 153.
  49. Fayadh Lahiji, Gohar Murad, 1383 S, uk. 621.
  50. Fayadh Lahiji, Gohar Murad, 1383 S, uk. 621; Subhani, Manshur Javid, 1383 S, juz. 5, uk. 153.
  51. Fayadh Lahiji, Gohar Murad, 1383 S, uk. 622.
  52. Majlisi, Haqu al-Yaqin, 1386 S, juz. 2, uk. 370.
  53. Makarim Shirazi, Tafsir Nemune, 1371 S, juz. 2, uk. 307.
  54. Fayadh Lahiji, Gohar Murad, 1383 S, uk. 621.
  55. Fakhr Razi, Al-Arbain Fi Usul al-Din, 1986, uk. 55; Fayadh Lahiji, Gohar Murad, 1383 S, uk. 621.
  56. Subhani, Manshur Jawid, 154, juz. 5, uk. 154.
  57. Fayadh Lahiji, Gohar Murad, 1383 S, uk. 621; Subhani, Manshur Jawid, 1383 S, juz. 5, uk. 156.
  58. Subhani, Manshur Jawid, 154, juz. 5, uk. 154.
  59. Rejea: Khosh Sohbat, «Ma'ad Jisman Az Mandhur Allamah Tabatabai Ba Taakid Bar Tafsiri al-Mizan», uk. 38.
  60. Subhani, Manshur Jawid, 154, juz. 5, uk. 154.
  61. Allamah Hilli, Babu Hadi Ashara, 1370 S, uk. 206.
  62. Ibn Sina, Al-Shifa (Ilahiyat), 1404 AH, uk. 423.
  63. Majlisi, Haqu al-Yaqin, Intisharat Islami, juz. 2, uk. 369 na 370.
  64. Majlisi, Haqu al-Yaqin, Intisharat Islami, juz. 2, uk. 369.
  65. Fayadh Lahiji, Gohar Murad, 1383 S, uk. 621.
  66. Subhani, Manshur Jawid, 1383 S, juz. 5, uk. 199.
  67. Subhani, Manshur Jawid, 1383 S, juz. 5, uk. 199.
  68. Bahrani, Qawaid al-Maram, 1406 AH, uk. 144; Allamah Hilli, Kashf al-Murad, 1413 AH, 406.
  69. Subhani, Manshur Jawid, 1383 S, juz. 5, uk. 188 na 199.
  70. Subhani, Manshur Jawid, 1383 S, juz. 5, uk. 188-199.
  71. Tazama: Mulla Sadra, Al-Hikmah al-Mu'taaliyyah, 1981, juz. 9, uk. 148-151; Subhani, Manshur Jawid, 1383 S, juz. 5, uk. 179-187.
  72. Tazama: Fayadh na Shukri, [http://kalami.nashriyat.ir/node/665 «Ma'ad Jismu Unsuri (Dalail Naqli wa Naqdi Didegihaye Raqib)».
  73. Ashtiani, Al-Haqaiq Fi Usul al-Aqaid, 1390 S, uk. 440.
  74. Misbah Yazdi, Amuzish Aqaid, 1384 S, uk. 349.
  75. Misbah Yazdi, Amuzish Aqaid, 1384 S, uk. 355.
  76. Misbah Yazdi, Amuzish Aqaid, 1384 S, uk. 349-350.
  77. Baker, «Material Persons and the Doctrine of resurrection», uk. 151-152.
  78. Misbah Yazdi, Insan-Shenasi Dar Qur'an, 1401 S, uk. 174.
  79. Muslin, Dar-Omadi Bar Falsafe Dhihni, 1391 S, uk. 361.
  80. Merricks, «The Resurrection of the Body and the Life Everlasting», uk. 268.
  81. Merricks, «The Resurrection of the Body and the Life Everlasting», uk. 268.
  82. Tazama: Mulla Sadra, Al-Hikma Al-Mu'taaliyyah, 1981, juz. 9, uk. 190; Ashtiani, Sharh Bar Zad al-Musafir, 1381 S, uk. 19 na 224; Misbah Yazdi, Amuzish Aqaid, 1384, uk. 348, 349 na 355.
  83. Ashtiani, Sharh Bar Zad al-Musafir, 1381 S, uk. 19 na 224
  84. Misbah Yazdi, Amuzish Aqaid, 1384, uk. 348 na 355.
  85. Misbah Yazdi, Amuzish Aqaid, 1384, uk. 349.
  86. Misbah Yazdi, Amuzish Aqaid, 1384, uk. 349.
  87. Tazama: Husseini Shahroudi na Fakharnughani, «In-hamani Shakhsi», uk. 28-32.
  88. Misbah Yazdi, Amuzish Aqaid, 1384 S, uk. 371.
  89. Jawadi Amuli, Ma'ad Dar Qur'an (1), 1395 S, uk. 109-126.
  90. Makarim Shirazi, Tafsir Nemune, 1371 S, juz. 18, uk. 485-487.
  91. Jawadi Amuli, Ma'ad Dar Qur'an (1), 1395 S, uk. 109-126.
  92. Tazama: Jawadi Amuli, Ma'ad Dar Qur'an (1), 1395 S, uk. 120-126; Misbah Yazdi, Amuzish Aqaid, 1384 S, uk. 373-375.
  93. Jawadi Amuli, Ma'ad Dar Qur'an (1), 1395 S, uk. 139-177.
  94. Subhani, Ilahiyat, 1413 AH, juz. 4, uk. 167.
  95. Makarim Shirazi, Payam Qur'an, 11386 S, juz. 5, uk. 182.
  96. Jawadi Amuli, Ma'ad Dar Qur'an (1), 1395 S, uk. 139-177.
  97. Misbah Yazdi, Insan-Shenasi Dar Qur'an, 1401 S, uk. 213
  98. Misbah Yazdi, Insan-Shenasi Dar Qur'an, 1401 S, uk. 213.
  99. Jawadi Amuli, Ma'ad Dar Qur'an (1), 1395 S, uk. 141-142.
  100. Fayadh Lahiji, Gohar Murad, 1383 S, uk. 620 na 621.
  101. Jawadi Amuli, Ma'ad Dar Qur'an (1), 1395 S, uk. 143-144.
  102. Tazama: Mulla Sadra, Al-Hikma Al-Mutaaliyyah, 1981, juz. 9, uk. 241; Jawadi Amuli, Ma'ad Dar Qur'an (1), 1395 S, uk. 143.
  103. Misbah Yazdi, Insan-Shenas Dar Qur'an, 1401 S, uk. 223.
  104. Tazama: Subhani, Al-Ilahiyat, 1413 AH, juz. 4, uk. 168; Makarim Shirazi, Payam Dar Qur'an, 1386 S, juz. 5, uk. 192; Misbah Yazdi, Insan-Shenas Dar Qur'an, 1401, uk. 223.
  105. Jawadi Amuli, Ma'ad Dar Qur'an (1), 1395 S, uk. 158-155; Subhani, Al-Ilahiyat, 1413 AH, juz. 4, uk. 168; Misbah Yazdi, Insan-Shenas Dar Qur'an, 1401 S, uk. 220-223.
  106. Jawadi Amuli, Ma'ad Dar Qur'an (1), 1395 S, uk. 165 na 166; Misbah Yazdi, Insan-Shenasi, 1401, uk. 227.
  107. Surat Sa'ad, Aya ya 28.
  108. Tazama: Jawadi Amuli, Ma'ad Dar Qur'an (1), 1395 S, uk. 167; Misbah Yazdi, Insan-Shenasi, 1401, uk. 225-226.
  109. Jawadi Amuli, Ma'ad Dar Qur'an (1), 1395 S, uk. 95.
  110. Subhani na Baranjakar, Ma'arif wa Aqaid 1 na 2, 1397 S, uk. 364 na 365.
  111. Misbah Yazdi, Amuzish wa Aqaid, 1384 S, uk. 342; Subhani, Manshur Jawid, 1383 S, juz. 5, uk. 73 na 74.
  112. Subhani, Manshur Jawid, 1383 S, juz. 5, uk. 74.
  113. Subhani na Baranjakar, Ma'arif wa Aqaid 1 na 2, 1397 S, uk. 364 na 365.
  114. Misbah Yazdi, Amuzush Aqaid, 1384 S, uk. 342; Subhani, Manshur Jawid, 1383 S, juz. 5, uk. 73 na 74.
  115. Subhani, Manshur Jawid, 1383 S, juz. 5, uk. 75.
  116. Fakhr Razi, Al-Arbain Fi Usul al-Din, 1986, juz. 2, uk. 55; Fayadh Lahiji, Gohar Murad, 1383 S, uk. 621; Subhani, Manshur Jawid, 1383 S, juz. 5, uk. 153.
  117. Subhani, Manshur Jawid, 1383 S, juz. 5, uk. 153-154.
  118. Fakhr Razi, Al-Arbain Fi Usul al-Din, 1986, juz. 2, uk. 55; Fayadh Lahiji, Gohar Murad, 1383 S, uk. 621; Subhani, Manshur Jawid, 1383 S, juz. 5, uk. 154.
  119. Fakhr Razi, Al-Arbain Fi Usul al-Din, 1986, juz. 2, uk. 55; Subhani, Manshur Jawid, 1383 S, juz. 5, uk. 154.
  120. Allamah Hilli, Kashf al-Murad, 1413 AH, uk. 406; Mulla Sadra, Al-Hikmah al-Mu'ta'aliyyah, 1981, uk. 199-200; Subhan, Ilahiyat, 1413 AH, juz. 4, uk. 396.
  121. Mulla Sadra, Al-Hikma Al-Mu'taaliyyah, 1981, juz. 9, uk. 200; Subhani, Ilahiyat, 1413 AH, juz. 4, uk. 396.
  122. Tazama: Allamah Hilli, Kashf al-Murad, 1413 AH, 406 na 407; Taftazani, Sharh al-Maqasid, 1409 AH, juz. 5, uk. 95.
  123. Mulla Sadra, Al-Hikma Al-Mu'taaliyyah, 1981, juz. 9, uk. 200
  124. Tazama: Baker, «Death and the Afterlife», uk. 377.
  125. Mulla Sadra, Al-Hikmah al-Mut'aliyyah, 1981, juz. 9, uk. 167; Taftazani, Sharh al-Maqasid, 1409 AH, juz. 5, uk. 93 na 94.
  126. Misbah Yazdi, Amuzish Aqaid, 1384 S, uk. 379.
  127. Misbah Yazdi, Amuzish Aqaid, 1384 S, uk. 379.
  128. Taftazani, Sharh al-Maqasid, 1409 AH, juz. 5, uk. 94 na 95.
  129. Subhani, Al-Ilahiyat, 1413 AH, juz. 4, uk. 186; Misbah Yazdi, Amuzish Aqaid, 1384 S, uk. 381.
  130. Subhani, Al-Ilahiyat, 1413 AH, juz. 4, uk. 186.
  131. Misbah Yazdi, Amuzish Aqaid, 1384 S, uk. 381.
  132. Tazama: Surat al-Baqarah: Aya ya 284; Surat al-Ahqaf: Aya ya 33.
  133. Misbah Yazdi, Amuzish Aqaid, 1384 S, uk. 380-381.
  134. Tazama: Surat al-Israa: Aya ya 51; Surat Ruum: Aya ya 27.
  135. Tazama: Tusi, Tajrid al-I'tiqaad, 1407 AH, Sura ya 6, uk. 297-310; Allamah Hilli, Kashf al-Murad, 1413 AH, Sura ya 6, uk. 399-427;
  136. Tazama: Subhani, Manshru Jawid, juz. 5; Makarim Shirazi, Payam Qur'an, 1386 S, juz. 5.
  137. Ikhwan Muqadam na Wenzake, Man-bashenasi Ma'ad, 1395 S, uk. 8.
  138. Husseini Tehrani, Ma'ādshenāsī, 1427 AH, juz. 1, uk. 8 na 9.
  139. Subhani, Ma'ad Insan na Jahan, 1373 S, uk. 10-7.
  140. Mutahari, Ma'ad, Intisharat Sadra, uk. 9.

Vyanzo

  • Khatami, Ahmad, Farhang 'ilm kalam, Tehran: Nashr Saba, 1370.
  • Misbah Yazdi, Muhammad Taqi, Amuzish 'aqaid, Tehran: Chap wa Nashr Bayn al-Milal, 1377.
  • Razi, Fakhr al-Din al-, Al-Arba'in fi usul al-din, Cairo: Maktaba al-Kulliyat al-Azhariyya, 1986.
  • Ibn Sina, al-Hussein bin 'Ali, Al-Shifa, Qom: Maktaba Ayatullah Mar'ashi, 1404.
  • Khush Suhbat, Murtada, Ma'ad-i jismani az manzar 'Allama Tabataba'i ba ta'kid bar tafsir-i al-mizan, Ma'rifat-i Kalami mag. N.12 uk.35-56 1393.
  • Hilli, al-Hassan bin Yusuf al-, Al-Bab al-hadi 'ashr ma'a sharhayh al-nafi' yam al-hashr wa miftah al-bab. Tehran: Mu'assisa Mutali'at Islami, 1365.
  • Mulla Sadra, Sadr al-Din Muhammad, Al-Hikma al-muta'aliyya fi al-asfar al-arba'at al-'aqliyya, Beirut: Dar Ihya' al-Turath, 1981.
  • Kadiwar, Muhsin, Majmu'i Musannafat Hakim Mu'assis Aqa 'Ali Mudarris Tehrani, Tehran: Mu'assisa Ittila'at, 1378.
  • Fayd Kashani, Musin, 'Ilm al-yaqin fi usul al-din, Qom: Bidar, 1418.
  • Khomeini, Ruh Allah, Sharh-i chihil hadith, Mu'assisa Tanzim wa Nashr Athar Imam Khomeini, 1378.
  • Sa'idi Mihr, Muhammad, Amuzish kalam Islami, Kitab Taha, 1385.
  • Rabbani Gulpayigani, 'Ali, 'Aqayid-i istidlali, Nasayih, 1380.