Ubahai (Kiarabu: البهائية) ni dhehebu la kidini ambalo lilijitenga na dini ya Baabi (babism), ambayo ilianzishwa katika karne ya 13 Hijria na Mirza Hussein Ali Noori anayejulikana kama Baha'u'llah. Mirza Hussein Ali alikuwa mmoja wa wafuasi wa Sayyid Ali Muhammad Bab ambaye alianzisha madhehebu ya Baha'i baada ya kifo cha Bab. Baada ya Baha'u'llah, mwanawe Abbas Effendi, anayejulikana kama Abdu'l-Bahá, na kisha Shoghi Effendi, mjukuu wa Abdu'l-Bahá, alichukua uongozi wa Wabaha'í. Baada ya Shoghi, kuliibuka tofauti kuhusiana na mrithi wake na Wabaha'i wakagawanyika katika makundi tofauti kama vile Wabahai wa Bait al-Adli na Wabaha'i wa Kiorthodox. Leo, uongozi wa Wabaha'i uko mikononi mwa Bayt al-Adli A'dham.

Wabaha'i wanamchukulia Baha'u'llah kuwa ni Mtume na kwamba, Ubahai ni dini mpya ambayo ilikuja na kuufuta Uislamu. Baha'u'llah anaamini kwamba, Kiyama cha Uislamu kitatokea baada ya ujio wa Bab na kitamalizika kwa kifo chake. Kadhalika Kiyama cha Wababia kitatokea baada ya kutokea Bahá'u'llah na kumalizika kwa kifo chake. Wabahá'í hutekeleza ibada kama vile Sala, Saumu, Hija na Hudud (adhabu za kisheria zisizo za kimali) kwa namna ambayo ni tofauti na Waislamu.

Bayt al-Adl ni kituo muhimu zaidi cha Mabahai na marejeo ya mambo yao yote. Kituo hiki kiko katika Mlima Carmel huko Haifa na wajumbe wake huchaguliwa na duru za kitaifa ambapo kiunganishi cha jamii ya Bahai katika kila nchi ni Bayt al-Adl. Nyumba ya Ali Muhammad Báb huko Shiraz, nyumba ya Baha'u'llah huko Baghdad, Bustani ya Rezvan (mahali atakapodhihiri wa Baha'u'llah kama inavyodaiwa na Mabahai), Maqam A'la (kaburi la Bab juu ya Mlima Carmel) na Rawdha Mubarak (kaburi la Hussein Ali Nouri huko Acre) ni miongoni mwa maeneo yanayohesabiwa na Wabaha'í kuwa ni matakatifu. Kadhalika sikukuu ya Nairuzi na kumbukizi ya kuaga dunia na kuzaliwa Bab na Bahaullah ni miongoni mwa sikukuu za Mabahai.

Athari za Mabahai ni kama vitabu vya Aqdas, Iqan, Kalimat Maknunah na Alwah, athari za Abdul Baha na Shoghi Effendi na vitabu vya al-Faraid na Ganjineh Hudud va Ahkam ni mionmgoni mwa vitabu vikatifu vya Mabahai.

Waislamu wanaamini kuwa, Ubahai ni kundi potovu na lililo nje ya Uislamu. Marajii Taqlidi wa Kishia wanachukulia kuamini Ubahai kuwa ni kukufuru na Bahai ni najisi na kafiri Muharib (anayepigana vita na Mwenyezi Mungu na Mtume wake). Zaidi ya vitabu 400 na makala zimeandikwa kwa ajili ya kuukosoa Ubahai. Baadhi ya vitabu hivi viliandikwa na Mabahai waliotoka kwenye imani ya Kibahai na kurejea katika imani sahihi ya Uislamu, kama vile Abdul Hussein Ayati Bafqi Yazdi.

Kudai Uungu, Utume na Baha'u'llah muahidiwa (atakayekuja) ni imani zinazopingana na itikadi za Kiislamu na inachukuliwa kuwa ni aina ya ibada ya masanamu na kujiabudu. Mgongano wa imani za Kibaha'i, tofauti nyingi kati yao, na kukufurishana shakhsia wakubwa wa kundi hili, ni miongoni mwa ukosoaji wa Ubaha'i. Kwa mtazamo wa wakosoaji, Ubahai ni chama na kundi la kisiasa linaloungwa mkono na serikali za Urusi, Uingereza, Israel na Marekani.

Historia fupi

Ubahai ni kundi la kidini linalotokana na Baab (babism)[1], kundi ambalo lilianzishwa katika karne ya 13 Hijria (19 Miladia) na Mirza Hussein Ali Noori anayejulikana kama Baha'u'llah.[2] Imekuja katika kitabu kilichoandikwa kwa mnasaba wa kumbukumbu ya mwaka wa 100 tangu kuaga dunia na ambacho kilisambazwa kwa maagizo ya Beit al-Ad kwamba: Risala na ujumbe wa Bahaullah ulianza Agosti 1852 akiwa gerezani.[3]

Imeelezwa kuwa, neno «Bahai» lilitumika baina ya miaka ya 1282-1284 Hijria kuhusiana na Ubahai.[4] Pamoja na hayo, Mabahai wanafadhilisha majina ya «mafundisho ya Ubahai», «Dini ya Kibahai» na «Amri ya Ubahai» ( The Bahai Faith).[5]

Mazingira ya Kuibuka Ubahai

Baada ya kifo cha Sayyid Ali Muhammad Bab, mwanzilishi wa kundi la Babia mwaka wa 1266 Hijria[6], Wababi walihamishwa hadi Iraq. Huko, Mirza Yahya Nouri, aliyejulikana kama Sobh-e-Azal, alichukua jukumu la uongozi wao; lakini alikuwa akiishi kwa siri, na kaka yake Mirza Hussein Ali Noori ndiye aliyekuwa akishikilia hatamu za uongozi.[7] Mwaka 1280 Wababi kutokana na kuwa na tabia mbaya na zisizo za maadili mema, walibaidishwa na kupelekwa uhamishoni huko Istanbul Uturuki na ni katika zama hizi ambapo Mirza Hussein Ali alidai kudhihiri hatua ambayo iliibua hitilafu baina ya Wababi. Siku hizi 12 Wabahai wameziita kuwa Sikukuu ya Ridhwan na kubaathiwa Bahaullah.[8] Baada ya hapo, Mirza Hussein Ali akadai kuwa Ubabi ni itikadi ya kale na ambayo imepitwa na wakati hivyo akatangaza rasmi madhehebu ya Ubahai.[9] Baada ya kushadidi hitilafu baina ya makundi hayo mawili, serikali ya utawala wa Othmania (Ottoman Empire) mwaka 1385 Hijria, ulimpeleka Mirza Hussein Ali huko Acre (Akka) moja ya miji ya Palestina na Mirza Yahya akapelekwa katika nchi ya Cyprus.[10] Wababi ambao waliendelea kutambua urithi na uongozi wa Sobh Azali na kukataa madai ya Hussein Ali waliitwa na wafuasi wa Mirza Hussein Ali «Bahai» kwa jina la Azalia.[11]

Takwimu na Hali ya Sasa

Leo, Ubahai unachukuliwa kuwa kundi la kimataifa lenye makao yake makuu huko Israel na lina matawi katika nchi zote za ulimwengu, hasa katika nchi za Asia na Afrika.[12] Kulingana na ripoti ya Dairat al-Maarif Jahan Novin Islam" Bahai ina mabaraza ya kiroho ya kitaifa 165 na mabaraza ya kiroho 20,000 ya kieneo ulimwenguni. Athati za fasihi za Kibahai zimetarjumiwa kwa lugha mbalimbali. Kadhalika kuna Mashriq al-Adhkar (Maabadi ya Wabahai) saba duniani.[13]

Wabahai wanaona Baha'í kuwa dini ya pili katika suala la mgawanyo wa idadi ya watu baada ya Ukristo; hata hivyo, ikilinganishwa na wafuasi wa dini nyingine, hawana idadi kubwa ya watu.[14] Inasemekana kwamba ingawa jumuiya inayoongoza Baha'i linafahamu idadi ya wafuasi wake, bado halijatoa takwimu rasmi za Idadi ya Wabaha'i.[15]

Takwimu zisizo rasmi zimetangaza idadi ya wafuasi wa Baha'i kuwa ni watu milioni tano hadi saba.[16] Kulingana na baadhi ya ripoti, jumuiya ya kimataifa ya Wabaha'i imeripoti idadi ya Wabaha'i kuwa zaidi ya milioni tano mwaka wa 2010.[17] Hata hivyo, takwimu hizi zimezingatiwa kuwa zimetiwa chumvi; kwa sababu, kwa mfano, idadi ya Wabaha'i nchini India imeelezwa kuwa ni zaidi ya milioni 2 na Iran ni 300,000, jambo ambalo haliendani na takwimu rasmi za nchi hizi mbili.[18] Kulingana na takwimu rasmi za serikali ya India, idadi ya Wabaha'i nchini India ni 110,000, [19] na idadi ya Wabaha'i nchini Iran inakadiriwa kuwa 100,000. [20]

Leo, wengi wa Wabaha'i wanaishi nchini Marekani. [21] Idadi kubwa ya Wabaha'i nchini Iran inahusiana na mji wa Tehran, hasa jiji la Fardis Karaj, Isfahan (Shahinshahr na Najafabad), Shiraz, Hamadan na Tabriz. [22]

Katika itikadi ya Kibahai, watu hawachukuliwi kuwa ni Wabaha'i mara tu wanapokubali imani za Kibaha'í; badala yake, wanatambuliwa kama Wabaha'i baada ya kufikia umri wa ukomavu na kujiandikisha katika Jumuiya ya Kibaha'i, kupokea namba ya uanachama na kutii jumuiya ya usimamizi wa bahai.[23]

Itikadi

Bahaullah alifuta dini ya Uislamu na kuja na dini mpya.[24] Wabaha'i wanasisitiza juu ya kuwa mapya mafundisho ya Baha'u'llah na wanamtambulisha kuwa ni Nabii kwa ujumbe mpya na ambao haujawahi kutokea kutoka kwa Mungu. Kulingana na madai yao, mwanadamu alifikia kiwango cha ukomavu wakati wa Baha'u'llah na kwamba anaweza kupokea mafundisho mapya kutoka kwa Mungu. Kwa hiyo, Mungu alimpa msukumo Hussein Ali Bahai kuleta mafundisho mapya kwa wanadamu.[25] Kwa mujibu wa Wabaha'i, Mwenyezi Mungu ametuma mfululizo wa walimu na wajumbe wa kiungu kwa wanadamu katika historia yote, ambapo wa hivi karibuni zaidi ni Baha'ullah.[26] Baadhi ya mafundisho na imani za Wabaha'i ni:

Tawhidi

Wabahai wanadai kwamba, Bahaullah sio Mungu bali ni mja ambaye amefikia daraja na dhihirisho la Mungu kwa hivyo ni dhihirisho la Mungu katika ardhi;[27] hata hivyo wahakiki na wakosoaji wa Ubahai wanaamini kwamba, Wabahai wakitumia na kutegemea maneno ya Bahaullah wanamini kuwa, Wabahai wanamtambua yeye kuwa Mungu wa walimwengui.[28] Miongoni mwa ibara za maneno na ibara za Bahaullah ambazo zinathibitisha madai yake ya uungu [29] ni:

Hapana Mola isipokuwa mimi mfungwa pekee (لا اله اِلّا اَنا المَسجونُ الفَرید) Yule aliyeiumba dunia kwa ajili yake ametiwa jela katika sehemu mbaya zaidi kwa mikono ya madhalimu. "Ndivyo alivyoamrisha Mola wako Mlezi alipo fungwa katika miji mibaya."[30] Hapana Mola isipokuwa mimi niliyebakia, mpweke na mkongwe (انَّهُ لا الهَ اِلّا اَنا الباقی الفردُ القدیم), Hapana Mola isipokuwa mimi nilebakia mwenye kusamehe, mkarimu (لا الهَ اِلّا اَنا الباقی الغفورُ الکریم) [31] Mirza Hussein Ali Nuri anaandika kuhusiana na usiku wa kuzaliwa kwake: Alizaliwa asubuhi hii, hakuzaa wala hakuzaliwa (وَ فیهِ وُلِدَ مَنْ لَمْ یَلِدْ وَ لَمْ یُولَدْ). [32] Dakta J.E. Esslemont, mhubiri wa Kimarekani wa kundi la Bahai anasema katika kitabu cha “Baha'u'llah and the New Era” (Bahaullah na Zama Mpya): Kuna wakati Bahaullah anazungumzia upande wa kibinadamu na daraja yake ya uja na kuabudu na kuna wakati anazungumzia daraja ya uola na Uungu na katika ibara zake hakuonekani athari za shakhsia yake kama mwanadamu. Kulingana naye, katika nafasi ya uungu, Mungu huzungumza na viumbe Wake kupitia Baha'u'llah, huonyesha upendo Wake na kutangaza sheria na amri Zake. [33] Itikadi ya Uungu ya Bahaullah inaonekana katika athari za Abdul-Bahai na wahubiri wa Ubahai.[34]

Katika maandishi ya Kibahai, tafsiri ya maneno na misemo imepigwa marufuku na inaamriwa kushikamana na maana zake kidhahiri na kilunga.[35]

Utume

Mirza Hussein Ali Nouri alidai Utume katika vitabu vyake na akajiita Mtume wa Mwenyezi Mungu.[36] Abbas Effendi, mwanawe na kiongozi wa pili wa Wabaha'i, pia alimjumuisha Ali Muhammad Bab katika safu za Mitume kama vile Ibrahim (as), Mussa (a.s.), Issa (a.s.) na Muhammad (saww) na anamchukulia Bab kuwa mtoa bishara ya kutokea na kudhihiri kwa Bahá'u'lláh. Kwa maoni yake, Baha'u'llah ni miongoni mwa Manabii hao na hata bora kuliko wao.[37]

Dakta J.E. Esslemont amesema: Wabaha'i, wanawaheshimu Manabii wote na wanaamini kwamba, Baha'u'llah ndiye mleta ujumbe wa Mungu kwa zama hizi. Yeye ndiye mkufunzi na mwalimu mkuu zaidi ulimwenguni aliyekuja kukamilisha juhudi za Mitume waliotangulia.[38] Hata hivyo, Mirza Hussein Ali alikubali katika baadhi ya kazi na athari zake kwamba, Mtume (s.a.w.w) hitimisho la Mitume.[39]

Kulingana na Alireza Rozbahani, mtafiti wa zama hizi wa Ubaha'i ni kwamba, haijabainika vyema na kwa umakini kama Baha'u'llah ni Mungu au Nabii au si Mungu wala si Mtume; kwa sababu katika baadhi ya vifungu, wakimfuata Abdu'l-Bahá, wanamuona kuwa ni Mtume, na katika sehemu nyingine, kwa kuzingatia kuwa Muhammad ni Mtume wa mwisho, wanamuona Baha'u'llah kama mtu muahidiwa na dhihirisho la Mwenyezi Mungu na mbora kuliko Mitume.[40]

Ufufuo

Kwa mujibu wa Rozbahani, katika madhehebu ya Baha'i, ufufuo unasemwa bila kueleweka, kiasi kwamba, inaweza kufahamika tu kwamba kuna ulimwengu baada ya kifo.[41] Wabahai wanakifasiri kile kilichokuja katika Qur'ani kuhusiana na Siku ya Kiyama na sifa zake maalumu kuwa ni harakati na mapinduzi ya Bab na Baha.[42] Báb alisema katika kitabu "Bayan" kwamba kwa kuja kwangu, Kiyama cha Waislamu kitatokea, na maadamu niko hai, Kiyama chao kitabakia, na siku nikifa ndipo Kiyama chao kitafikia tamati.[43] Kwa maoni ya Hussein Ali Baha ni kuwa, Kiyama cha Wababiya (Babiyan) kitatokea kwa kudhihiri yeye na kitaisha na kufikia tamati kwa kifo chake.[44]

Dakta J.E. Esslemont amenukuu kwamba: Bahaullah na Abdul-Baha wanakihesabu kile kilichokuja katika vitabu vitakatifu kuhusiana na pepo na jahanamu kwamba, ni alama ya siri na hawaitambui maana yake ya kidhahiri kwamba, ni sahihi. Kwa mtazamo wao ni kuwa, hali ya ukamilifu na jahanamu ni ulimwengu wa mapungufu. Pepo ni kupata radhi za Mwenyezi Mungu na kuanisika na wote na katika jahanamu ni kuweko hali hii. Furaha na nishati ya pepo ni furaha na buraha ya roho na maumivu na masaibu ya jahanamu ni kunyimwa kwa furaha na buraha hii.[45]

Mafundisho Kumi na Mbili

Abbas Effandi, kiongozi nambari mbili wa Wabahai alifanya safari Ulaya na Marekani na kushiriki katika makongamano, na makanisa kueneza fikra na athari za Bahaullah na hivyo akatambulisha misingi 12 iliyofahamika kama mafundisho ya Kibahai ambayo yameondokea kuwa mashuhuri kwa jina la Mafundisho na Misingi 12 ya Ubahai.[46] Misingi na mafundisho hayo ni:

  1. Kutafuta ukweli.
  2. Umoja wa ulimwengu wa kibinadamu.
  3. Dini inapaswa kuwa sababu ya huba na mapenzi.
  4. Dini inapaswa kuendana na elimu na akili.
  5. Kuacha taasubi (chuki) za kijinsia, kidini, kimadhehebu, kinchi na kisiasa ambazo kwa hakika zinaangamiza misingi ya mwanadamu.
  6. Kuboresha maisha ya watu.
  7. Umoja wa dini.
  8. Ulazima wa kutoa mafunzo na malezi kwa umma.
  9. Umoja wa lugha na hati (kuanzisha lugha ya pili kwa ajili ya walimwengu).
  10. Umoja wa wanawake na wanaume na haki sawa kwao.
  11. Kuleta amani kwa wote na kuanzisha Mahakama ya Kimataifa.
  12. Ulimwengu wote unahitajia upuliziaji wa Roho Takatifu (yaani ulimwengu wa utu na ubinadamu haukwei kwa nguvu ya kiakili na kimaada; bali ili kupatikane mafanikio ya kimaanawi na saada ya kiutu kuna haja ya kuweko ilhamu na msaada na upuliziaji wa roho takatifu.[47]

Mabahai wanadai kwamba mafundisho haya ni mapya na kabla ya hapo hakuna mtu ambaye aliwaletea wanadamu mafundisho kama haya;[48] lakini watafiti wa Ubahai wanaamini kuwa, mafundisho haya yamechukuliwa kutoka katika dini mbalimbali hususan Uislamu, na baadhi wanasema yamechukuliwa kutoka katika anga ya kifikra na kiutamaduni ya ulimwengu wa Magharibi.[49]

Hukumu

 
Kaburi la Baha'u'llah katika mji wa Acre (Kibla cha Wabahai).

Kwa mujibu wa watafiti, hukumu na sheria za Ubahai ndio zilezile zilizobainishwa na Ali Muhammad Bab katika kitabu; hata hivyo kuna tofauti kadhaa.[50] Baadhi ya hukumu za Ubahai ni:

  • Sala: Kwa mujibu wa Bahaullah katika kitab-i-Aqdas, Sala ni wajibu mwanzoni mwa baleghe.[51] Katika Ubahai kuna Sala tatu: Sala ya Sughra (ndogo), Wustaa (ya kati) na Kabir (kubwa).[52] Sala ya Kabir (kubwa) inatosha kusali mara moja[53], na mtu ambaye ataswali Sala hii anasamehewa Sala zingine mbili zilizobakia yaani Sughra na Wustaa.[54] Wakati wa Sala ya Wustaa ni asubuhi, adhuhuri na usiku na wakati wa Sala Saghir ni wakati wa adhuhuri (zawali/kupinduka jua)[55].

Kwa mujibu wa maandiko ya Ubahai, Bahaullah alishusha pia Sala moja yenye rakaa tisa[56] na namna ya kuisali Sala hiyo imeandikwa katika karatasi nyingine; hata hivyo kwa mujibu wa Abdul-Baha karatasi hiyo imeibiwa.[57] Vipi Sala hii mpaka leo haijafahamika.[58] Kwa mujibu wa Kitab al-Aqdas, ni marufuku kusali Sala ya Jamaa isiokuwa Sala ya maiti.[59]

Kibla cha wahabai kama alivyosema Bahaullah katika zama za uhai wake ni mahali anapoishi Bahaullah na baada ya kifo chake Rawdha yake takatifu yaani kaburi lake.[60]

  • Saumu: Saumu ni wajibu kwa Wabahai kuanzia siku ya kwanza ya kubaleghe.[61] Siku za Saumu za Wabahai huanza katika mwezi wa Ala (Loftiness) moja ya miezi ya kalenda ya Mabahai na kumazikia katika sikukuu ya Nairuzi.[62] Sikukuu ya Nairuzi, ni Sikukuu ya Saumu (Eidul-Fitr) ya Mabahai.[63] Watu kama wasafiri, wagonjwa, wanawake wajawazito, wanawake walioko katika ada (siku) zao za mwezi, wanaofanya kazi ngumu na watu ambao umri wao ni zaidi ya miaka 70 wamesamehewa kufungwa.[64]
  • Hija: Kwa mujibu wa mafundisho ya Ubahai, Hija ni wajibu kwa wanaume tu.[65] Hija ya Mabahai ni kuzuru nyumba ya Muhammad Ali Bab katika mji wea Shiraz, Iran au nyumba ya Bahaullah mjini Baghdad, Iraq.[66]
  • Adhabu zisizo za kimali: Kwa mujibu wa Kitab-i-Aqdas, kuua, kuzini, kusengenya na uzushi ni haramu.[67] Endapo mtu atamuua mwingine kwa makusudi, anapaswa kuuawa. Kama mtu atachoma kwa makusudi nyumba ya mwingine adhabu ya mtu huyo ni kuchomwa moto.[68] Kwa mujibu wa Kitab-i-Aqdas, adhabu ya zinaa ni kutoa dia (fidia) ambayo kiwango chake ni dhahabu yenye uzito wa shekel (mithqal) tisa ambayo inapaswa kupatiwa Baytul-Maal (hazina ya dola).[69] Endapo mhusika atakariri kosa, basi fidia hiyo itakuwa mara mbili.[70]

Katika Ubahai kila kitu ni tohara na kisafi na hakuna najisi.[71] Kwa mujibu wa kauli ya Bahaullah, ni wajibu kwa Mabahai kama mali yao imefikia dhahabu yenye uzito wa shekel (mithqal) mia moja, basi mhusika anapaswa kutoa shekeli 19 kwa anuani ya haki ya Mwenyezi Mungu.[72] Hukumu hii imetambuliwa kuwa ni kwa ajili ya kudhamini mahitaji ya kifedha ya Ubahai na hili limeigwa na kufanywa kuwa kigezo kutoka katika Uislamu.[73] katika mafundisho ya Mabahi inajuzu kuoana na maharimu isipokuwa mke wa baba.[74]

Viongozi

Viongozi wa Ubahia ni:

Bahaullah

Makala kuu: Mirza Hussein-Ali Noori
 
Mirza Hussein Ali Noori anayejulikana kama Baha'u'llah, mwanzilishi wa imani ya Kibaha'i.

Mirza Hussein Ali Noori (aliyezaliwa 1233 Hijria), anayejulikana kama Bahaullah, ndiye mwanzilishi wa Ubaha'i, na jina la imani na itikadi ya Kibaha'i limechukuliwa kutoka katika lakabu hii.[75] Alijifunza kusoma na kuandika kwa baba yake, Mirza Abbas Noori.[76] Baada ya Ali Mohammad Shirazi kudai Ubabiya (babiyan) alijiunga na Ubabiya na kuanza kueneza itikadi zake.[77] Mirza Hussein-Ali mwaka 1863 yaani takribani miaka 13 baada ya kuaga dunia Muhammad Ali Bab, alidai kwamba, yeye ndiye mtu aliyeahidiwa na akadai daraja la mtu ambaye Mwenyezi Mungu atamdhihirisha na akaondokea kuwa mashuhuri kwa jina la Bahai.[78]

Mwaka 1868 Mirza Hussein Ali Bahá, akiwa pamoja na wafuasi wake, alibaidishiwa katika mji wa Acre, moja ya miji ya Palestina.[79] Mwaka 1892 mwafaka na 1309 Hijria aliaga dunia huko akiwa na umri wa miaka 75, [80] na kuzikwa katika nyumba yake aliokuwa akiishi katika bustani ya Bahji.[81]

Abdul- Baha

 
Abdu'l-Baha, mtoto mkubwa wa Baha'u'llah na mrithi wake.

Mirza Abbas Nouri, mashuhuri kwa jina la Abbas Effendi na Abdul- Baha (1260-1340 Hijria), alikuwa mtoto mkubwa wa Mirza Hussein Ali Baha na ambaye alichukua uongozi wa Ubahai baada yake. Bahaullah alimtaja yeye kama mrithi wake katika «Kitab Ahdi» (Wasia wa Baha) na kumuita kwa jina la «Ghasn A’dham».[82] Mabahai wanamuita kwa jina la «Markaz Mithaq»; lakini yeye mwenyewe anajiita Abdul- Baha.[83]

Kwa mwaliko wa Wabahai wa Ulaya na Marekani, Mwaka 1328 Hijria, Abdu'l-Baha alitoka Palestina na kwenda hadi Misri na kutoka huko hadi Ulaya na Marekani. Wakati wa safari hii, iliyodumu kwa miaka mitatu, Abdu'l-Baha aliwasilisha mafundisho ambayo yanajulikana leo kama «Mafundisho Kumi na Mbili».[84] Kutokana na Abdu'l-Baha kudhamini chakula kwa ajili Waingereza katika Vita vya Kwanza vya Dunia[85], Aprili 1920 alipatuniwa na serikali ya Uingereza nishani ya Knighthood na kupewa lakabu ya Sir. [86] Aliaga dunia 1920. Kaburi lake liko jirani na kaburi la Bab katika Mlima Carmel Palestina.[87]

Shoghi Effendi

 
Shoghi Effendi, mrithi wa Abdu'l-Baha na kiongozi wa tatu wa Wabaha'í.

Huyu ni mjukuu wa binti ya Abbas Effendi ambaye alikuwa kiongozi wa Wabahai baada yake. Yeye ni mtoto wa Mirza Hadi Afnan na Dhiaiyyah binti ya Abdu'l-Baha ambaye alizaliwa 11 Esfand 1276 Hijria Shamsia huko Acre na alibakia huko mpaka alipofikisha umri wa miaka 11.[88] Mwaka 1908 Shoghi akiwa pamoja na familia yake alifanya safari huko Haifa na kusoma katika Chuo Kikuu cha Beirut Lebanon na kisha baadaye alisoma katika Chuo Kikuu cha Oxford Uingereza.[89] Kutekeleza mpango wa kuhajiri Wabahai na kwenda katika maeneo mbalimbali ya dunia, kupanua wigo wa muundo wa kiidara na wa kitaasisi wa kidini wa Ubahai[90] na kuasisi Kamati ya Kimataifa ya Kibahai au «Bayt al-Adl» Nyumba ya Uadilifu[91] ni miongoni mwa hatua zake alizochukua. Katika kipindi cha uongozi wake Abdul-Hussein Tafti (Ayti) na Mirza Saleh Iqtisad Maragheh miongoni mwa waliokuwa mubalighina na wahubiri wa Ubahai walirejea katika Uislamu.[92]

Aliaga dunia 1957 London Uingereza na kuzikwa huko.[93]

Uongozi wa Ubahai Baada ya Shoghi Effendi

Baada ya Shoghi Effendi, kuliibuka hitilafu baina ya Mabahi kuhusiana na mrithi wake katika uongozi na hilo likapelekea kumeguka na kugawanyika Mabahai. Mary Maxwell, (Rúhíyyih Khánum) mke wa Shoghi Effendi na baadhi ya kundi teule la Shoghi waliokuwa na lakabu ya «Ayadiyan Amrullah» walifanikiwa kuwavuta upande wao akthari ya Wabahai na kuasisi «Bayt Al-Adl Al-A’dham» na kuchukua uongozi wa Ubahai. Kundi hili liliondokea kuwa mashuhuri kwa jina la “Mabahai wa Baytul-Adl” na kuweka kando milele cheo la Walii Amr.[94]

Mkabala wao kulikuweko na Charles Mason Remey ambaye alidai kuwa ni mrithi wa uongozi wa Shoghi na Walii Amr na akaanzisha kundi lililojulikana kwa jina la Mabahai wa Othodoksi au Wa- Remey.[95] Wafuasi wa Remey wanaamini kwamba, kila kundi iwe ni Ayadiyan Amrullah au Taasisi ya Baytul-Adl linapaswa kuwa chini ya usimamizi wa Wilayat Amr (uongozi ) wa Mabahai na kinyume na hivyo tasisi husika haitakuwa na uhalali. Kwa muktadha huo, wanawatambua Ayadiyan Amrullah na Baytul Adl kuwa ni taasisi haramu ambazo hazina uhalali wa kisheria kwa mujibu wa mtazamo wa Mabahai.[96] Mason Remey aliamchagua Joel Bray Marangella kuwa Walii Amr wa tatu wa Mabahai na mrithi wake na Marangella naye mwaka 2006 alimteua Nasrullah Bahramand kuwa Walii Amr wa Nne wa Wabahai.[97]

Mgawanyiko

Baada ya kifo cha Bahaullah, kuliibuka mgawanyiko katika Ubahai na katika zama za Shoghi Effendi, mgawanyiko huo ulishadidi zaidi.[98] Baadhi ya migawanyiko na mitengano ya kundi hili ni kama ifuatavyo:

  1. Bahai Muwahid: Ni Mabahai wanaoamini kwamba, baada ya Bahaullah, mrithi wake wa kweli ni mwanawe Mirza Muhammad Ali.
  2. Mabahai Huru: Hawa ni wafuasi wa Zimer Herman ambao wanaamini kwamba, kwa kufa Bahaullah, zama za nguvu za uhai zimefikia tamati na hivyo kuna haja ya kusubiri kudhihiri Baha muahidiwa kwa muda wa miaka 1000.
  3. Mabahai Wapigania Mageuzi: Ni Mabahai walioathirika na fikra na mitazamo ya Ruth White na Mirza Ahmad Sohrab ambapo Mabahai ambao ni wafuasi wa Baytul-Adl wanawatambua hawa kama watu waliopotea. Kiongozi wa sasa wa kundi hili ni Frederick Glischer.
  4. Mabahai walio chini ya uongozi wa Mithaq: Hawa ni Mabahai ambao wanamtambua Shoghi Effendi kuwa ni walii wa Afnan na Mason Remey kuwa ni Walii Amr wa Aghsan. Joseph Pih, ni Walii Amr wa Pili wa Aghsan na Neil Chase Walii Amri wa Tatu kutoka Aghsan na kiongozi wa sasa wa kundi hili.
  5. Mabahai wa Kiothodoksi: Kundi hili linaona kuwa, kuweko Walii Amr (kiongozi) hai katika kila zama ni jambo la dharura. Shoghi, Remey, Marangella ni Mawalii Amr (viongozi) wa namna hii.
  6. Wafuasi wa Baytul-Adl (Mabahai wa Haifa): Kundi hili ambalo linaunda sehemu kubwa ya Mabahai, linaamini kwamba, baada ya Shoghi hakuna udharura wa kuweko Walii Amr na marejeo ya masuala ya kiidara, maamuzi na utoaji hukumu ni Bayt A’dham huko Haifa.[99]

Baadhi ya Makundi Mengine Yaliyogawanyika katika Ubahai ni:

  • Jumuiya ya Malezi ya Ubahai (Mabahai ambao wamemkubali Remey kama Naibu na wanaamini kwamba, katika mustakabali atakuja Walii Amr kutoka katika kizazi cha Bahaullah.
  • Jumuiya ya Historia Mpya: (wafuasi wa Mirza Ahmad Sohrab, mmoja wa wanaharakati wa Ubahai nchini Marekani na katibu na mtarjumi wa ʻAbdu'l-Bahá).
  • Dehesh’ha (Wadeheshi: (wafuasi wa Daktari Dehesh Salim Mussa al-Awshi). [100]

Taasisi

Jumuiya au taasisi ya Ubahai ambayo imetokana na matawi mawili ya uchaguzi na uteuzi inaendeshwa na Bayt al-Adl al-A’dham.[101]

 
Kituo cha Kimataifa cha Ubahai (Beit al-Adl na majengo yake yanayozunguka) katika Mlima Carmel, Haifa.
  • Bayt al-Adl A’dham: Bahaullla ndiye aliyetoa amri ya kuundwa Bayt al-Adl A’dham;[102] hata hivyo eneo hili liliasisiwa 1963[103] na uchaguzi wake wa kwanza ukafanyika.[104] Kituo hiki kinaundwa na watu 9 na wote wanapaswa kuwa wanaume[105] na huchaguliwa kila baada ya miaka mitano.[106] Kituo hiki kiko katika Mlima Carmel katika mji wa Haifa.[107]

Bayt al-Adl A’dham ni marejeo ya mambo yote ya Mabahai.[108] Kituo hiki kina majukumu ambapo muhimu zaidi ni kufasiri maandiko na athari za viongozi wa Ubahai, kuweka sheria ambazo zinanasibiana na hali na mazingira ya zama,[109] kusimamia mambo ya jumuiya ya Mabahai katika maeneo mbalimbali duniani, kuanzisha taasisi na vituo vya mahubiri ya Ubahai na kutatua hitilafu zinazojitokeza katika jamii ya Mabahai.[110]

Kwa mujibu wa Abdul-Hamid Eshraq Khavari, mtafiti na mwandishi wa Kibaha'i, kinachoidhinishwa katika Bayt al-Adl ni haki na matakwa ya Mwenyezi Mungu, na kupinga sheria za chombo hicho ni dhihirisho la unafiki na kujitenga na Mwenyezi Mungu.[111] Kwa kuzingatia maandishi ya Kibahai, Jumuiya ya Kibaha'í imesimama juu ya misingi miwili ya Walii Amrullah na Bayt al-Adl. Walii Amr Mungu ndiye kiongozi wa kudumu wa Bayt al-Adl na kwa mujibu wa kauli ya Abdu'l-Baha, Bayt al-Adl haina uhalali bila ya Walii Amr. Ni kutokana na sababu hii ndio maana, wengine wanasema kwamba kutokana na ugumba wa Shoghi Effendi, mlolongo wa Wilayat al-Amr ulifikia tamati kwa kifo chake. Kwa hiyo, Bayt al-Adl haina uhalali, na hii pia imesababisha migawanyiko mingi katika Ubaha'i.[112]

  • Mahafali za Kitaifa na Kieneo: Katika kila mji au kijiji ambacho idadi ya Mabahai inafikia 9, wana jukumu la kufanya mahahali ya kiroho. Mahafali za kieneo ziko chini ya mahafali za kitaifa na wawakilishi wake wanachaguliwa na mahafali ya kitaifa.[113] Wajumbe wa Bayt al-Adl pia wanachaguliwa na mahafali ya kitaifa.[114] Wajumbe wa asasi hizo huchauliwa kila baada ya miaka miwili.[115]

Kila mwezi wa Kibahai (kila baada ya siku 19 mara moja) hufanyika kikao ambacho kinafahamika kwa jina la «Mwaliko wa Siku Kumi na Tisa».[116]

Mabahai wana asasi ambayo wajumbe wake huteuliwa na miongoni mwao ni kamati za ushauri wa kimabara ambao huteuliwa na Bayt al-Adl.[117]

Maeneo Matakatifu

 

Katika Ubahai kuna maeneo matakatifu na yanayoheshimiwa ambapo baadhi yao ni:

  • Nyumba ya Ali Muhammad Bab katika mji wa Shiraz Iran.
  • Nyumba ya Bahaullah, Baghdad.
  • Kaburi la Bab katika Mlima Carmel, Haifa.
  • Kaburi la Mirza Hussein Ali Noori katika mji wa Acre (Akka).
  • Kaburi la Abdul-Baha, kando ya kaburi la Bab.
  • Kaburi la Shoghi Effendi, mjini London Uingereza.
  • Makaburi ya Mabahai yanayojulikana kama Golestan Javid.[118]

Kalenda ya Mabahai

Kwa mujibu wa kalenda mwaka wa Kibahai unafahamika kwa jina la Badi [123] au Mzunguko wa Kibahai, [124] ambapo kila mwaka mmoja wa Kibahai una miezi 19 na kila mwezi una siku 19. [125] Kalenda ya Kibahai inaanzia 1844 ambapo kwa mujibu wao ndio mwaka wa kudhihiri Bab [126] na mwezi wa kwanza wa mwaka unafahamika kwa jina la Shahrul-Baha ambapo kawaida huanza 21 Machi. [127] Mwezi wa mwisho wa mwaka wa Badi (kalenda ya Bahai) ni Shahrul-Ala ambao huanza 2 Machi.[128]

Sikukuu za Mabahai

Sikukuu za Mabahai ambazo zinahesabiwa kuwa siku za likizo na mapumziko na ni haramu kufanya kazi yoyote au biashara katika siku hizi[129] ni:

  1. Sikukuu wa Nairuz (mwanzo mwa mwaka mpya) (Machi 21).
  2. Siku ya kwanza ya Sikukuu ya Ridhwan (kuangazwa daawa na wito wa Bahaullah) (Aprili 21).
  3. Siku ya Tisa ya Sikukuu ya Ridhwan (Aprili 30).
  4. Siku ya 12 ya Sikukuu ya Ridhwan. (2 Mei).
  5. Tangazo la mwito wa Bab (23 Mei).
  6. Kuaga dunia Bahaullah (29 Mei).
  7. Kuaga dunia Bab (Julai 9).
  8. Kuzaliwa Bab (12 Novemba).[130]

Siku ya Agano (Novemba 26) na kifo cha Abdu'l-Baha (Novemba 28) pia zimeitwa kwa jina la «Matukio ya Emiriyah» [131] lakini katika vyanzo vingine, siku hizi mbili badala ya tarehe 9 na 12 za Sikukuu ya Ridhwan zimehesabiwa kuwa miongoni mwa sikukuu za Ubahai. [132]

Kulingana na Esslemont, Sikukuu ya Nowruz, Sikukuu ya Ridhwan, siku ya kuzaliwa kwa Báb na Baha'u'llah na tangazo la wito wa Báb (ambalo linaendana na kuzaliwa kwa Abdu'l-Bahá) zinachukuliwa kuwa sikukuu kubwa zaidi na siku za furaha kwa Mabaha'i.[133]

Vitabu vya Mabahai

Maandishi ya viongozi wa Mabaha'i, hasa Mirza Hossein Ali na mwanawe Abbas Effendi, ni matakatifu kwa Mabaha'i na yanasomwa katika mikusanyiko yao.[134] Baadhi ya kazi na maandiko matakatifu ya Baha'i ni kama ifuatavyo.

  • Athari za Bahaullah: Kitab Aqdas, Kitab Iqan, Hafte Vadi, Kalimat Maknunah Mubin, Ishraqat, Iqtidarat, Badi’, na Alwah Salatin zinahesabiwa kuwa miongoni mwa athari za Mirza Hussein Ali Noori.[135] Kwa mujibu wa Abdul-Baha Kitab Aqdas, kimehifadhi vitabu na suhuf zote, kimefuta vitabu vyote na ni marejeo ya hukumu na maarisho na makatazo.[136]

Kwa mtazamo wa Shoghi Effendi ni kuwa, hiyo ni athari muhimu zaidi ya Bahaullah na Ummul-Kitab ya Ubahai.[137] Kitabu hiki kina sheria na mafundisho ya Ubaha'i na kiliandikwa huko Acre (Akka).[138] Mabahai wanakitambua Kitab Bayan kwamba, kimefuta Qur'ani na Kitab Aqdas kimefuta Kitab Bayan.[139] Mkusanyiko wa athari na kazi Babaullah zimmechapishwa katika mkusanyiko unaoitwa "”Athari za Kalamu ya Ala” katika juzuu sita.[140]

  • Athari za Abdul-Baha: Miongoni mwa kazi za Abdu'l-Bahá ni makala binafsi ya kitalii, Risalah Madaniya, Kitab Siyasah, Kitabu Mufawidhaat, Kitabu Makatib, Tadhkirat Al-Wafa, Khitabata Mubarakah na wasia.[141]
  • Athari za Shoghi Effendi: baadhi ya athari na maandiko ya Shoghi Effendi ni: Tandhim Badi, Nazm Idarai Diyanat Bahai (ni mjumuiko wa kanuni za kuanzishwa Ubahai), Dhuhur Adl Ilahi, Laweh Qur’an, Nidhamat Bahai na Mataliu al-Anwar. Baadhi ya vitabu vyake vimeandikwa kwa lugha ya kifarsi na vingine kwa Kiingereza.[142]

Kitabu «Al-Faraid» cha Mirza Abul-Fadhl Golpayegani, mmoja wa wahubiri na waandishi mashuhuri wa Kibaha'i, «Ganjineh Hudud va Ahkam» cha Abdul Hamid Ishraq Khavari, mmoja wa walimu, wahubiri na waandishi mashuhuri wa Baha'i, na «Kawakib al-Dur'riyya fi Ma'athar al-Baha'iyya» na Abdul Hussein Aiti, mmoja wa wahubiri wa zamani wa Baha'i ambaye alikuja kuwa Mwislamu, ni miongoni mwa zinazohesabiwa kuwa athari na vitabu vingine vitakatifu vya Baha'i. [143] Al-Faraid kimetambuliwa kuwa kitabu cha ujengeaji hoja zaidi cha Mabahai.[144] Gonjineh Hudud va Ahkam, ni mjumuiko wa sheria na hukumu za Ubahai ambapo sehemu kubwa ya sheria na hukumu za Mabahai imekuja katika kitabu hiki.[145]

Kuna vitabu vingine kama Kashf al-Ghitaa, Durar al-Bahiyyah, Hujaj al-Bahiyya na Burhan Lami’ vilivyoandikwa na Abul-Fadhl Golpeygani.[146]

Mitazamo ya Maraji’i wa Kishia

 
Fat’wa ya Imamu Khomeini kuhusu Ubaha'i.

Marajii Taqlidi wa Shia wanaichukulia imani ya Ubaha'i kuwa ni ukafiri[147] na Wabaha'i ni najisi[148] na huonya dhidi ya kushirikiana nao kwa namna yoyote ile.[149] Kwa mtazamo wao ni kuwa, Mabahai ni maadui wa dini na imani[150] na ni katika makafiri muharib (wanaopigana vita na Mwenyezi Mungu na Mtume wake),[151] na ni haramu na batili kuoana nao, [152] sio haramu kutumia mali zao[153] na haifai kufanya kitendo na jambo lolote lile ambalo linazingatiwa kuwa kuimarisha na kukuza na kueneza kundi hili.[154].

Ayatullah Buroujerdi (1292-1380 Hijria), mmoja wa Marajii Taqlidi wa Kishia alikuwa akiwatambua Mabahai kuwa watu waliokuwa dhidi ya Shia na mamlaka ya kujitawala nchi ya Iran.[155] Alikuwa akiwatambua Mabahai kuwa ni hatari kubwa na inaelezwa kuwa, mapambano dhidi ya Ubahai yalianzishwa na yeye. Akiwa na nia ya kufikia lengo hilo, alikuwa akiwatuma katika miji mingine Maulamaa kama Ayatullah Muntazeri, Ibrahim Amini na Ahmad Shahroudi.[156] Hatua zilizochukuliwa na Sayyid Hussein Buroujerdi zilipelekea kufungwa jengo la makao makuu ya ofisi za Mabahai katika mji Tehran, Iran. Hatua hiyo ilichukuliwa kwa amri ya Shah mwaka 1334 Hijria Shamsia.[157]

Imamu Khomeini alikuwa akiwatambua Mabahi kuwa ni vibaraka wa Israel[158] na majasusi wa Israel na Marekani.[159] Kwa mtazamo wa Imamu Khomeini ni kuwa, Ubahai umekuja kutoa pigo kwa madhehebu ya Shia.[160] Aidha kwa mtazamo wa Imamu Khomeini ni kuwa, Wazayuni wamedhihiri nchini Iran kwa sura ya chama cha Kibahai na wanafanya njama za kudhibiti mamlaka ya kujitawala na uchumi wa Iran.[161]

Mnamo mwaka wa 2003, Baraza la Utafiti wa Kiislamu katika Chuo Kikuu cha Al-Azhar nchini Misri lilifikia natija hii kwamba, Ubaha'i ni bidaa na uzushi na likatangaza kwamba madhehebu hii haina uhusiano wowote na dini za mbinguni. Muhammad Sayyid Tantawi, Sheikh Mkuu wa Al-Azhar pia aliuona Ubaha'i kuwa unapingana kabisa na Uislamu, na aliamini kwamba haupaswi kutambuliwa kama dini inayojitegemea. Kwa maoni yake, Baha'i ni dini ya iliyobuniwa ambayo iliundwa mwishoni mwa karne ya 19 na wakoloni wa Uingereza kuhoji Uislamu na kuwagawanya Waislamu.[162]

Ukosoaji

Imesemekana kuwa ingawa viongozi wa Bahai hapo awali walikuwa ni Mashia na harakati zao za mwanzo ziliegemezwa kwenye mafundisho ya Kishia, lakini kwa madai ya dini mpya na Sharia mpya, ambayo ndani yake inalazimu kukanusha hitimisho la Utume yaani Muhammad ndiye Mtume wa mwisho, madhehebu hii haiwezi kuchukuliwa kuwa aina mpya ya Shia. Ni kwa muktadha huo, ndio maana wanazuoni wa Kishia na Kiislamu wanauchukulia Ubaha'i kuwa uko nje ya dini ya Kiislamu.[163] Aidha itikadi ya Kibahai baina ya Waislamu, inatambulika kuwa potofu na Ubahai ni kundi lilipotea.[164] Pamoja na hayo, B. Todd Lawson mwandishi wa makala ya «Ubahai» katika «Dairat al-Maarif Jehan Novin» anasema kuwa, Ubahai ni aina mpya ya Tawhidi ya Uislamu na Ushia.[165]

Hassan Mustafawi, mfasiri na fakihi wa Kishia wa karne ya 15 Hijria anataja kanuni kumi za jumla na za kimsingi za Uislamu katika kitabu «Mohakemeh va baresi dar aqaid va ahkam bva adab wa tarikh bab va bahai» na anasema kwamba kila moja ya kanuni hizi inatosha kubatilisha na kuonyesha kwamba, Ubahai hauna msingi na ni bandia.[166] Baadhi ya kanuni hizi kumi ni: Hitimisho la Mitume, kubakia kwa dini ya Kiislamu hadi Siku ya Kiyama; Uimamu wa Imam Mahdi (a.t.f.s), Imam wa kumi na mbili; Utume na Tawhidi.[167] Kwa mujibu wa Alllama Mustafawi ni kuwa, kama dini ya Uislamu, Qur'ani, Hukumu na Adabu za Kiislamu vitalinganishwa na kitabu kilichojaa makosa ya kilafudhi, kifasihi na kimaanawi cha Bayan na Aqdas na kisha kukafanyika ulinganishaji wa yaliyomo ndani yake itafahamika na kueleweka wazi juu ya kubakia na kuwa thabiti dini ya Uislamu.[168]

Ufafanuzi wa Baadhi ya Ukosoaji dhidi ya Ubahai:

  • Madai ya Uungu: Kwa mujibu wa Abdul-Baha katika kitabu cha Makatiib, Bahaullah amedai Uungu na Uola mara chungu nzima.[169] Mirza Hussein Ali Noori naye amedai mara nyingi Uungu.[170] Madai ya Uungu ni kinyume na mafundisho ya Uislamu na kwa namna fulani kumetambuliwa kuwa ni kulingania kuabudu masanamu, hurafa na upotofu, ujinga na ujahilia.[171] Kadhalika katika Ubahai, kinyume na mafundisho sahihi na ya wazi ya Uislamu, Mirza Hussein Ali ametajwa kuwa ni muabudiwa na kumuabudu yeye kumetambuliwa kuwa miongoni mwa wadhifa na majukumu ya Mabahai.[172]
  • Madai ya Utume: Kwa kuzingatia kwamba, kuainisha cheo cha Utume na kusadikisha madai ya Utume ni jambo gumu, Mitume wakiwa na lengo la kuthibitisha Utume wao wanapaswa kufanya muujiza.[173] Mirza Hussein Ali Noori licha ya kuwa alidai Utume, lakini alidai kwamba, Utume unahitaji kushusha Aya tu. Kwa msingi huo, alidai kuwa, mambo yaliyoko katika kitab-i-Aqdas na ubao zingine ambayo yana muundo maalumu wa maneno na sentensi zikiwa zinaiga muundo wa Qur’ani, lakini zikiwa na makosa mengi ya kilafudhi, kimaanawi na kifasihi ni Aya kutoka mbinguni na akayaita maneno hayo kuwa ni muujiza.[174] Hata hivyo maneno yaliyomo ndani ya vitabu hivyo yamekosolewa kwani kwa msingi huo kila ambaye atazungumzia Kiarabu kwa ufasaha anaweza kudai Utume.[175]
  • Khatamiyah: Miongoni mwa mambo ambayo Mabahai wanakosolewa nayo ni suala la Khatamiya (hitimisho la Utume). Kwa mujibu wa imani ya Waislamu, kila dai ambalo haliendani na itikadi hii batili na si la kukubalika na kila kundi ambalo halitakubali asili hii (hakuna Mtume baada ya Muhammad), litakuwa liko nje ya Uislamu.[176] Mirza Hussein Ali alijiita kuwa ni: «Atakayedhihirishwa na Mwenyezi Mungu» na akadai kuwa na sheria za kujitegemea.[177]
  • Madai ya Mtu aliyeahidiwa: Licha ya kuwa, Mirza Hussein Ali alidai kuwa ni Mtume lakini alikuwa akiijita kuwa ni Muntadhar «mtu anayesubiriwa» na wakati huo huo alikuwa akizitambulisha hadithi zinazozungumzia ghaiba, kudhihiri na Imamu Muntadhar (Imamu Mahdi) kuwa ni dhaifu. Hii ni katika hali ambayo, kama hadithi hizi ni dhaifu hakubakii nafasi yoyote ya Muahidiwa au msubiriwa. Kwa maana kwamba, hata madai yake yatabatilika.[178] Mbali na hayo, kwa kuzingatia hadithi na matamshi ya Maulamaa na wataalamu na wasomi wa elimu ya hadithi ni kwamba, Mirza Hussein Ali hakuwa na jina, sifa maalumu, nasaba wala alama maalumu inayomshabihisha na Muahidiwa wa kweli.[179] Aidha Man Yudhhiruh Allah (Atakayemdhuhirisha Mwenyezi Mungu) na Bab Muahidiwa naye sifa zake haziendani na Hussein Ali; kwa sababu kwa mujibu wa matamshi ya Bab katika Kitab Bayan, jina lake ni Muhammad, lakabu yake ni Qaim na mahala pa kudhihiri kwake ni Masjid al-Haram (Msikiti wa Makka) na hakuna hata sharti moja kati ya hayo ambalo linaoana na Bahaullah.[180] Kadhalika kwa mujibu wa matamshi ya Ali Muhammad Bab, kudhihiri kwa Man Yudhihiruh Allah kutatokea miaka 1511 au 2001 baada ya kudhihiri Bab.[181]
  • Migongano: Katika dini na kitabu cha mbinguni haipasi kuweko migongano na mikinzano;[182] lakini kwa mujibu wa Sayyid Muhammad Baqir Najafi, mwandishi wa kitabu cha Bahaiyan, kuna migongano katika athari za Mabahai kuhusiana na masuala muhimu ya kiitikadi na ni lazima kukubali baadhi ya itikadi kwa kukataa zingine na haiwezekani kuzikubali zote.[183] Pia Hassan Mustafavi amesema, maandiko na matamshi ya Mirza Hussein Ali yamejaa migongano na kisha anabainisha baadhi ya migongano hiyo.[184] Kwa mfano kwa mujibu wa vyanzo muhimu vya Mabahai, Qur’ani haijapotioshwa, lakini wakati huo huo wanaamini kwamba, Qur’ani imefutwa na Kitab Bayan kutokana na kupotoshwa.[185]
  • Hitilafu na Mizozo ya Ubahai: Kwa mtazamo wa Hassan Mustafavi ni kwamba, hadi sasa hakuna dini au madhehebu ambayo yamekuwa na hitilafu, utakfiri na mizozo kama ilivyo kwa Mabahai.[186] Baada ya kuaga dunia Bab, Mirza Baha alingia katika mzozo na hitilafu na kaka yake Sobh Azal na kila mmoja akaandika kitabu kumkashifu mwenzake. Baada ya kufariki duniani Baha kukaibuka hitilafu kubwa baina ya Abdul Baha na Muhammad Ali.[187] Abdul- Baha akamtaja na kumtambua Mirza Muhammad Ali kama mtu mkiukaji mkubwa na Muhammad Ali naye aliwatambua wafuasi wa Abbas na Shoghi kuwa ni Washirikina.[188] Baada ya kuaga dunia Shoghi Effendi pia hitilafu zilishadidi mno na kupelekea kugawanyika kundi hilo katika makundi kadhaa.[189]
  • Ubahai, Chama cha Siasa: Wakosoaji wa Ubahai wanalitambua kundi hili kuwa ni chama na kundi la kisiasa[190 na linadhibiti wafuasi wake kama asasi za kisiasa na linanufaika nao[191] na linaungwa mkono na Russia,[192] Uingereza, Israel na Marekani.[193] Inaelezwa kuwa, himaya na uungaji mkono wa madola haya kwa Ubahai unatokana na kuwa, kuenezwa kwa itikadi za Ubahai ni moja ya njia za kukabiliana na harakati za Kiislamu hususan katika eneo la Mashariki ya Kati.[194] Kwa mtazamo wa Ali Ridha Roozbahani, mtafiti wa Ubahai ni kwamba, mahusiano ya karibu baina ya Ubahai na madola ya kikoloni yako wazi kiasi kwamba, waandishi wa historia wa zama hizi wa Iran wanautambua Ubahai kuwa umezaliwa na kuundwa na siasa za kikoloni za Magharibi kwa ajili ya kubadilisha misingi ya kifikra na kijamii ya jamii za Kiislamu.[195] Hii leo Ubahai ni jumuiya ya kimataifa na makao yake makuu yako Israel na akthari ya wafuasi wake wanaishi Marekani.[196]

Sayyid Saeed Zahidzahdani, mwanasosholojia na mtunzi wa kitabu cha “Ubaha'i nchini Iran”, ameichukulia Baha'i kuwa chombo cha madola ya kikoloni cha kuvunja mamlaka ya kidini nchini Iran; kwa sababu popote pale ambapo kuna suala la kupambana na kukabiliana na dini na kuiondoa katika taasisi ya siasa au basi Wabaha'i wana nafasi na mchango mkubwa katika hili. Wakati wa mapinduzi ya kikatiba nchini Iran na wakati wa Pahlavi, ushirikiano wa wageni na Wabaha'i kwa ajili ya kukabiliana na dini na viongozi wa dini ulionekana wazi. Vuguvugu hili, hata sasa ni mojawapo ya zana za kitamaduni katika Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, zinazoweza kutumiwa na mataifa makubwa ya ulimwengu kukabiliana na harakati za Kiislamu.[197] Roozbahani anasema hakuna utawala wowote ule wa Kiislamu ambao unautambua rasmi Ubahai.[198]

Bibliografia

Makala kuu: Faharasa ya Vitabu vya Kuukosoa Ubahai
 
Picha ya kitabu cha Kashf Al Hail

Kumeandikwa vitabu na makala mbalimbali kuhusiana na Ubahai na ukosoaji dhidi yake. Katika programu ya Compyuta inayojulika kwa jina la «Be Suye Haghighat: Radd Fergheh Zaalaeh Bahaiyat» (Kuelekea Ukweli: Jibu Dhibi ya Kundi Potovu la Ubahai) iliyozalishwa na Hawza Elmiya (Chuo Kikuu cha Kidini) na Asasi ya Masuala ya Waqfu ya Isafahan kuna vitabu na makala 313 ambazo zimekusanywa humo na katika Programu ya Compyuta ya : «Baha Bi Baha» iliyotolewa na Taasisi ya Ahrar Andisheh kumekusanywa humo vitabu na makala 416.[199]

Hapa tunaashiria baadhi tu ya vitabu vilivyoandikwa na wahubiri wa Kibahai wakikosoa Ubahai baada ya kuachana na Ubahai na kurejea katika Uislamu:

  • Kashf al-Hil, Abdul Hussein Aiti.
  • Falsafe Niku, Mirza Hassan Niku.
  • Iqaz ya Bidar dar kashf Khiyanat dini va vatani bahai, Salih Iqtisad Maraghei.
  • Rahe Rast; Chera az Bahayiyat Bargashtam (Njia ya Kweli; Kwa nini nimetoka katika Ubahai): Mwandishi, Masihullah Rahmani (alikuwa mnmoja wa viongozi wa Mabahai).
  • Name Az San Palo, mwandishi Amanullah Shafa.[200]

Vitabu vingine vilivyoandikwa kukosoa Ubahai:

  • "Mohakemeh va baresi dar aqaid va ahkam va adab va tarikh bab va Bahai” (Juzuu Tatu), Hassan Mustafavi.
  • Bahaiyan, mwandishi Sayyid Muhammad Baqir Najafi.
  • Tarikh Jami’ Bahaiyat, mwandishi Bahram Afrasiyabi.
  • Majaraye Bab va Baha’, mwandishi Mustafa Husseini tabatabai.[201]

Makala Zinazo Husiana

Rejea

Vyanzo