Liwati

Kutoka wikishia

Liwati au Amali ya Ubaradhuli (Kiarabu: اللِّواط), ni kitendo cha kujamiana kati ya wanaume wawili. Sheria za Kiislamu zimekiorodhesha kitendo hichi miongoni dhambi kubwa katika zinazoweza kutokea katika jamii mbli mbali. Pia Hadithi mbali mbali zimelihisabu tendo hili kuwa ni tendo hatari kupindukia amali nyengine za uzinzi. Mafaqihi wa Kiislamu wamekihukumu kitendo hichi kuwa ni kitendo haramu, hukumu mbayoa imesimama juu ya msingi wa Aya za Qur'an pamoja na Hadithi mbali mbali. Kwa mujibu wa fatwa (hukumu) za wanazuoni; Ikiwa mwanamme fulani atamwingilia mwenzake katika kitendo hicho, basi hukumu yao itakuwa ni kifo. Hukumu hii hufanyika bila kujali hali ya ndoa ya mhalifu aliyetenda tendo hilo. Adhabu hii ya kifo inaweza kutekelezwa kwa njia mbalimbali kulingana na hukumu ya kadhi (hakimu wa Kiislamu). Kwa upande mwingine, ikiwa tendo hilo litafanyika bila kuingiliana, basi adhabu ya tendo hilo itakuwa ni mapigo ya bakora mia moja. Hii ni sawa na adhabu inayotolewa kwa mtu aliyefanya uzinzi huku akiwa bado hajaoa au kuolewa.

Kwa mujibu wa maelezo kutoka katika Hadithi mbali mbali ni kwamba; sababu ya kuharamishwa kwa liwati, ni kule tendo hili kuweza kuzuia kukatisha kizazi na kuleta madhara makubwa ndani ya jamii na kuvuruga mpangilio na mfumo wa maisha ya ulimwengu. Katika dini nyingine za Ibrahimu, kama vile Uyahudi na Ukristo, pamoja na madhehebu mbalimbali ya Kiislamu, liwati pia limekataliwa na kuzuiliwa kama kitendo haramu na kisichokubalika. Kitendo cha liwati hakikatazwa tu na dini ya Kiislamu, bali hata dini nyengine pia zimeharamisha amali hii potofu.

Liwati; Dhambi Kubwa Kuliko Zinaa

Kulingana na sheria za Uislamu, amali ya Liwaat inatambuliwa kuwa; ni moja ya dhambi kubwa mno, ikielezwa kuwa na uzito mkubwa kuliko dhambi ya zinaa. [1] Hii ni kama ilivyoelezwa katika Hadithi kutoka kwa Imamu Swadiq (a.s). [2] Kwa mujibu wa Riwaya za Mtume Muhammad (s.a.w.w), mtu anayefanya kitendo hichi hughidhibiwa na kupata laana ya Mwenye Ezi Mungu. [3]

Tendo la liwati Katika Qur'ani, limeelezwa kupitia maneno tofauti, kama vile «munkar» (kitendo kibaya kisichokubalika) na «fahisha» (dhambi ya wazi). [4] Mara nyingi kaumu ya Nabii Lut hutajwa na kulaaniwa kwa kuhusika kwake na kitendo hichi kichafu, [5] huku ikitangazwa kuwa mustakbali wa amali yao hii, ilikuwa ni adhabu ya maangamizi. [6]

Fasili ya Dhana ya Liwati

Pia angalia: Ubaradhuli

Kwa mujibu wa istilahi za kifiqhi Liwati; ni tendo la mwanamme mmoja kuingiza kiungo chake cha uzazi katika sehemu ya nyuma (sehemu ya haja kubwa) ya mwanamme mwingine. [7] Kulingana na maelezo ya Ali Meshkini, mwanazuoni mashuhuri wa Kishia, ni kwamba; baadhi ya mafaqihi wamefafanua wakieleza kwamba; hata kama kuingo cha mwanamme atendaye tendo hilo kitakuwa hakikuzama hadi hakufiki kwenye sehemu ya tohara (kwenye msirimbo wa alama ya mkato wa govi), bado kitendo hicho kitachukuliwa kuwa ni tendo la liwaat. [8] Aidha, wanazuoni wengine wamefafanua wakisema kwamba; liwati inahusisha aina yoyote ile ya mahusiano ya kimwili kati ya wanaume wawili, hata bila kuingiza kiungo cha uzazi kwenye eneo la haja kubwa la mtendewa tendo hilo. [9]

Kwa mujibu wa moja ya Hadithi iliyosimuliwa kutoka kwa Imamu Ridhaa (a.s), ni kwamba; jina la dhambi hii kubwa linahusishwa moja kwa moja na kaumu ya Nabii Lut, ambao walikuwa ndiwo wa kwanza kujihusisha na kitendo hichi. Na hiyo ndiyo sababu ya dhambi kubwa hii kupewa jina liwati kutokana na uhusiano wake na watendaji hawa wa mwanzo wa dhambi hii. [10]

Hukumu ya Kisheria ya Liwati

Katika sheria za Uislamu kitendo cha Liwati moja kwa moja kinachukuliwa kuwa ni miongoni mwa matendo ya haramu, na ni miongoni mwa dhambi kubwa mno. [11] Kwa mujibu wa sheria za Kiislamu, liwaat inakabiliwa na adhabu kali (hudud), pamoja na nyengi adhabu nyengine ambazo huanishwa na faqihi wa Kiislamu kulingana tokeo hilo lilivyo. Miongoni mwa adhabu za kisheria za kosa la liwaat, ni vikwazo maalumu katika ndoa. [12]

Vikwazo katika Ndoa kwa Mwenye Kufanya Liwati

Miongoni mwa taathira za dhambi ya liwaat katika sheria za Kiislamu, ni kusababisha vikwazo na mipaka maalum katika ndoa kwa yule anayefanya kitendo hicho. Kwa mujibu wa fatwa za wanazuoni wa Kishia, ni kwamba; ni haramu kwa mwanaume aliyefanya liwati na mtu fulani, kuoa mama, binti, au dada wa yule aliyefanya naye kitendo hicho, na haramu hii ni ya kudumu na ya milele, kwa hiyo katu yeye hataweza kuoana watu hao. [13] [14] Hukumu hii pia imewekwa kwenye kifungu cha 1056 cha Sheria ya Kiraia ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ambacho kimekuja kuthibitisha uharamu wa ndoa kati ya aliyejihusisha na liwaat na jamaa wa karibu wa mwenzake aliyefanya naye kitendo hicho. [15] Hata hivyo, baadhi ya wanazuoni wanaeleza kuwa hukumu hii ya uharamu wa milele inahusiana na pale ambapo mtendaji wa liwati atakapokuwa ni mtu mzima (baleghe). [16] Aidha, kama kitendo cha liwaat kitatokea baada ya kufungwa kwa ndoa kati ya mwanamke (mama, dada, au binti wa aliyeathirika) na mwanaume huyo, basi ndoa hiyo haitabatilishwa na wala wahusika wake hawatahukumiwa kuwa wanaishi kwenye ndoa ya haramu, bali ndoa yao itaendelea kuwa ni ndoa halali. [17]

Adhabu ya Liwati

Kulingana na fat’wa za mafaqihi, adhabu ya liwaat kifo ndiyo adhabu ya pande zote mbili zinazohusika na tendo hilo, hii ni wale waliotenda tendo hilo hali wakiwa tayari wamefikia baleghe (umri wa kuwajibika kisheria). [18] Hata hivyo, ikiwa mmoja wao au wote hawajafikia umri wa baleghe, basi hukumu yao itakuwa ni kuadhibiwa kwa njia nyepesi inayojulikana kama ni ta’adiib (kuadabishwa). [19] Ta’adiib ni itolewayo na kiongozi wa Kiisalmuni dhidi ya mtenda kosa aliyekuwa bado hajafikia umri wa kubaleghe, adhabu adabu ambayo ni ndogo kuliko ile ya kisheria itambulikayo kwa jina la hudud (itokayo kwa Mungu mwenyewe). [20]

Hata hivyo baadhi ya mafaqihi kama vile Ayatullahi Abu al-Qasim al-Khui wamekuwa na mitazamo maalum, ambao ni kinyume na maoni ya wanazuoni mashuhuri kuhusiana na adhabu hii. Kwa mujibu wa maoni yake, adhabu ya kifo hutolewa kwa yule tu anayefanya kitendo hicho huku akiwa yeye ni muhsana (yaani, ana mke na ana uwezo wa kufanya ngono halali). Na iwapo mtu huyo atakuwa hana mke, basi adhabu yake itakuwa ni viboko mia moja. [21]

Aidha, kama tendo la liwati litakuwa limetimia bila ya kuhusisha uingizaji wa uume ndani ya tupu ya mtendewa tendo hilo, basi adhabu kwa wahusika wa tendo hilo, itakuwa ni viboko mia moja kila mmoja wao. [22] Vilevile, mafaqihi wengi wanakubaliana kuwa, ikiwa mhalifu atatubu kabla ya kitendo cha liwati kuthibitishwa kisheria, basi mtu huyo hatopaswa kuhukumiwa wala kuadhibiwa. [23]

Njia za Kutekeleza Adhabu ya Kifo kwa Mwenye Kufanya Liwati

Kuna njia kadhaa zilizotajwa katika Riwaya [24] na ndani ya vyanzo vya fiqhi mbali mbali, [25] kwa ajili ya kutekeleza adhabu ya kifo kwa mhalifu wa tendo la liwati. Njia hizi ni pamoja na: kukatwa kichwa, kuchomwa moto, kutupwa kutoka kwenye mlima, kupigwa mawe hadi kufa, au kuporomoshewa ukuta juu yake. Kiongozi wa Kiislamu huamua kutumia mojawapo ya njia hizi kulingana na maslahi ya jamii ya Kiislamu yalivyo. [26] Hata hivyo, ikiwa utekelezaji wa baadhi ya adhabu hizi utapelekea kudhalilisha au kudhoofisha misingi ya dini, basi kiongozi wa Kiislamu anaweza kuakhirisha adhabu hiyo kwa muda fulani, [27] au kuagiza matumizi ya njia nyingine, kama vile kunyongwa au kupigwa risasi, ili kuhifadhi maslahi makubwa zaidi ya Uislamu. [28]

Falsafa ya Uharamu wa Liwati

Kuhusiana na hekima ya kuharamishwa kwa tendo la liwati, moja ya Hadithi kutoka kwa Imamu Ridha (a.s), inasema kwamba; Mwenye Ezi Mungu aliwaumba wanawake kwa ajili ya kukukidhi mahitaji ya maumbile ya wanaume kulingana na hali za kimaumbile wa wawili hao. Ila kitendo cha liwati kinapelekea kuhatarisha mwendelezo wa uzazi, na ni sababu za kukatika kwa kizazi, na hatimae kuleta machafuko katika utaratibu wa maisha duniani. [29]

Allama Tabatabai, katika tafsiri yake ya Qur'an iitwayo Al-Mizan, anabainisha akisema kwamba; Qur'an imelitaja tendo la liwati kwa ibara isemayo: «تَقْطَعُونَ السَّبِيلَ» (mnakata njia “ya mwendelezo wa kizazi”), [30] [31] ikionesha kwamba kitendo hichi kinakata njia ya mwendelezo wa uzazi, na kuleta madhara makubwa ulimwenguni. Ama pale Mwenye Ezi Mungu alipozungumzia tendo la zinaa, ametumia ibara isemayo: «سَاءَ سَبِيلًا» (ni njia mbaya), [32] ikionesha kuwa; madhara ya liwati ni makubwa na hatari zaidi kuliko yale ya zinaa. Hii inadhihirisha kwamba liwaat sio tu linakandamiza uwezo wa kuzaa, bali pia linaweza kuharibu kabisa uwezo wa kuendeleza kizazi, hivyo kuathiri mfumo wa kijamii na familia kwa ujumla. [33]

Msimamo wa Dini na Madhehebu Mengine Kuhusiana na Liwati

Kwa upande wa madhehebu ya Ahlu Al-sunna; tendo la liwati linachukuliwa kama tendo haramu, na kumewekwa adhabu maalum kwa mwenye kutenda tendo hilo. [34] Hata hivyo, fatwa ya Abu Hanifah inasema kwamba; mtu anayefanya kitendo cha liwati anapaswa kupewa adhabu ya ta'dhiir (kukomeshwa kwa adhabu ya kawaida iainishwayo na kadhi), badala ya adhabu ya kisheria ambayo ni haddu (ya Mungu). [35]

Pia tendo la liwati katika dini nyingine (zinazo aminiwa kuwa niza mbinguni) linachukuliwa kuwa ni tendo baya na la haramu. Kwa mfano katika dini ya Zoroastrianism (dini ya kimajusi), tendo la liwati linachukuliwa kuwa ni amali mbaya zaidi, na mtu anayefanya hivyo anastahili adhabu ya kifo. [36] Katika Torati, tendo la liwati limetajwa kwa jila la «فُجور» (ufisadi). [37] Aidha, katika Agano Jipya (Biblia ya Wakristo), watekelezaji wa amali ya liwati wamewekwa sambamba na wapotovu, wanyang'anyi, na wanaoabudu masanamu. Pia, katika kitabu hicho inasisitizwa kwamba, watu hawa hawataweza kurithi Ufalme wa Mungu. [38]

Kwa ujumla, msimamo wa dini mbalimbali ni kwamba; tendo la liwati sio tu linachukuliwa kuwa na madhara makubwa kwa mtu binafsi, bali pia linaathiri jamii kwa ujumla na hivyo linatakiwa kukatazwa na kukomeshwa kadri iwezekanavyo.

Rejea

Vyanzo