Manabii na mitume

Kutoka wikishia

Manabii na Mitume (Kiarabu: الأنبياء و المرسلون) ni watu ambao Mwenye Ezi Mungu huwatumi katika kuwaongoza wanadamu kwenye njia yake ya haki. Mwenye Ezi Mungu huwasiliana na Manabii wake kupitia ufunuo (wahyi).

Isma (kuto tenda dhambi), ujuzi wa mambo ya ghaibu, miujiza, na kupokea ufunuo, iwe ni ufunuo wa kisheria au ufunuo fafanuzi, ni miongoni mwa sifa za Manabii. Ufunuo wa kisheria ni ule ufunuo asili, na ufunuo fafanuzi ni tafsiri ya ufunuo asili. Qur'ani inataja baadhi ya miujiza ya Manabii, kama vile kupoza moto kwa Ibrahimu, fimbo ya Mussa kugeuka na kuwa nyoka, kufufuka kwa wafu kupitia mkono wa Nabii Issa, na kumeguka kwa mwezi kulikotokea katika zama za Nabii Muhammad (s.a.w.w).

Qur'ani inasisitiza juu ya kuwepo kwa ubora wa baadhi ya Manabii kuliko wengine. Baadhi ya Manabii, mbali na Unabii wao, pia walikuwa na hadhi ya Mitume, na wengine walikuwa na hadhi ya Uimamu. Kulingana na Hadithi ni kwamba; Manabii walio na sifa ya Ulul Azmi - Nuhu, Ibrahimu, Mussa, Issa, na Muhammad (s.a.w.w) - ni wabora zaidi kuliko manabii wengine, na Mtume Muhammad (s.a.w.w) ni mbora zaidi kuliko Mitume na Manabii wote. Aidha, kati ya Manabii wa Mwenye Ezi Mungu; Shithi, Idrisi, Mussa, Daudi, Isau, na Mtume Muhammad Muhammad (s.a.w.w), wanachukuliwa kuwa Mitume walio pewa vitabu vya mbinguni, na Manabii "Ulul Azmi" wote wanachukuliwa kuwa ni Manabii waliokuja na sheria za Kiungu, yaani nao pia walikuwa na vitabu vyao.

Ni vyema kueleweka ya kwamba; yawezekana Mtume akawa na kitabu bila kuwa na sharia mpya, yaani akaja na kitabu cha kudumisha yale yalioletwa na Mtume aliyepita kabla yake. Kulingana na imani maarufu, idadi ya manabii ni 124,000, ambapo 26 kati yao wametajwa katika Qur'ani. Nabii wa kwanza kabisa ni Adamu, na Nabii wa mwisho ni kabisa ni Muhammad (s.a.w.w).

Wanazuoni wa upande wa madhehebu ya Shia wamechunguza historia ya manabii katika kazi zao tofauti, na wameandika vitabu maalumu na makhususi juu ya mada hii. Baadhi ya kazi zao hizo ni pamoja na; An-Nur Al-Mubinu fi Qasas Al-Anbiya' wa Al-Mursalina kilicho andikwa na Sayyid Neematullah al-Jazayiri, Qasas al-Anbiyaa cha Rawandi, Tanzihu al-Anbiyaa cha Sayyid Murtadha, cha Hayatu al-Qulubi cha Allama Majlisi.

Mjumbe (Mtume)

Makala Asili: Unabii

Mjumbe ni mtu anaye pokea ujumbe moja kwa moja kutoka kwa Mungu na kuufikisha kwa binadamu bila kuwepo kwa mtu mwengine kati kati. [1] Mtume ni kiungo kati i ya Mwenye Ezi Mungu na waja vyake, na kazi ya Mtume ni kuwaongoza watu kwenye njia ya Mwenye Ezi Mungu [2].

Kupokea ufunuo, maarifa ya elimu ya ghaibu [3], kuto tenda makosa [4], na kujibiwa maombi yao ni miongoni mwa sifa za manabii. Wanatheolojia wengi wa Kiislamu wanaamini kuwa manabii hawatendi dhambi wala hawakosei katika kipengele chochote kila maishani mwao. [6] Kwa hivyo, matukio kama vile kuomba msamaha na ibara ziashiriazo kusamehewa kwao na Mwenye Ezi Mungu zilizotajwa katika Qur'an [7], kama vile tukio la nabii Mussa kumuua Mmisri, [8], Nabii Yunus kuacha jukumu lake na kukimbia [9], na kisa cha Nabii Adam kula tunda alilokatazwa [10], yote yamefasiriwa kwa maana ya wao kuacha kutenda lililo bara zaidi, na badala yake wakatenda lenye ubora wa daraja ya chini. Upande wa pili pia kuna baadhi ya wanatheolojia wanao chukulia suala la kutokuwa na makosa kwa manabii kuwa linahusiana na masuala yanayohusiana na nyanja za kufikisha ujumbe, kwa hiyo wanajuzisha Mitume kufanya makosa katika mambo yanayo husiana na maisha yao ya kila siku [11].

Idadi ya Manabii

Kuna Hadithi tofauti kuhusu na idadi ya wajumbe wa Mwenye Ezi Mungu. Allama Tabatabai, kulingana na Hadithi maarufu, ametaja idadi ya wajumbe hao kuwa ni wajumbe 124,000. [12] Kulingana na Hadithi hii, 313 kati yao ni mitume, watu 600 ni manabii kutoka katika wa Bani Israili, na wane ambao ni Huud, Saleh, Shu'ayb, na Muhammad (s.a.w.w) ni Waarabu. [13] Katika Hadithi nyingine, idadi ya manabii ni imetajwa kwa idadi tofauti, wakati mwengine wametajwa kwa idadi ya 8,000, [14] au 320,000, [15] au 144,000. [16] Allama Majlisi anadhani kwamba yawezekna idadi ya 8,000 inarejelea manabii wakubwa. [17] Mtume wa kwanza kabisa alikuwa ni nabii Adamu na wa mwisho alikuwa ni Mtume Muhammad (s.a.w.w). [18] [19]

Qur'an inataja majina ya baadhi tu ya manabii. [20] Adamu (a.s), Nuh (a.s), Idris (a.s), Hud (a.s), Saleh (a.s), Ibrahim (a.s), Lut (a.s), Ismail (a.s), Elisha (Al-Yasa’a) (a.s), Zulkifli (a.s), Ilyas (a.s), Yunus (a.s), Ishaq (a.s), Ya'aqub (a.s), Yusuf (a.s), Shu'aib (a.s), Mussa (a.s), Harun (a.s), Daudi (a.s), Suleiman (a.s), Ayubu (a.s), Zakaria (a.s), Yahya (a.s), Issa (a.s), na Muhammad (s.a.w.w) ni manabii ambao majina yao yamekuja katika Qur'an. [21] Baadhi ya wafasiri wanaamini kwamba; jina la Ismail bin Ezekiel pia limetajwa katika Qur'an. [22] [Maelezo 1]

Wengine wanaamini kwamba Qur'an imetaja sifa za baadhi ya manabii, kama vile Yeremia na Samweli, lakini haikutaja majina yao. [23] Ndani ya Qur'an, kuna Sura maalumu inayoitwa "Anbiya" pia ndani yake mna Sura nyengine kadhaa zenye majina ya Mitume kama vile; Yunus, Hud, Yusuf, Ibrahim, Muhammad (s.a.w.w), na Nuh.

Katika vyanzo vya Hadithi pia kumetajwa mitume ndani yake, ambao ni; [24] Ezekiel, [25] Habakuk, [26] Daniel, [27] George, [28] Ezra (Uzair), [29] Handhala, [30] na Yeremia. [31] Kiuhalisia kuna utata kuhusiana utume wa baadhi watu kama vile; Khidhr, [32] Khalid bin Sinan, [33] na Dhul-Qarnayn. [34] Kulingana na maoni ya Allama Tabatabai, ni kwamba; hata Ezra (Uzair) pia naye ni miongoni mwa wale ambao utume wao hauko wazi. [35] Kulingana na Aya za Qur'an, baadhi ya manabii waliishi katika zama mmoja; kwa mfano, nabii Mussa na Harun katika zama moja, [36] Ibrahim na Lut pia nao waliishi katika zama moja [37]. Pia, kutoka katika vyanzo vya baadhi ya Hadithi, ianafahamika wazi ya kwamba; baadhi ya manabii walikuwa wakiishi katika zama moja. Kwa mfano, Sayyid bin Tawus katika kitabu chake Luhuuf amenukuu Hadithi kutoka kwa Imamu Hussein (a.s) akisema kwamba; wakati alipokuwa akijiandaa kuondoka Makka kuelekea mji wa Kufa, alimwambia Abdullah bin Omar: Je, unajuwa ni kiasi gani Bani Israili ulifikia uasi wao! ilifikia hali ya kwamba; baina ya kuchomoza kwa alfajiri hadi kuchomoza kwa jua waliuua manabii sabini wa Mwenye Ezi Mungu, kisha wakaendelea na biashara zao za kuuza na kununua bila kuhisi ubaya na janga la mauaji haya ya kutisha, kana kwamba hakuna janga lililotokea? [38] Katika Hadithi nyingine ilioko katika kitabu Majmaul Bayan imenukuliwa kutoka kwa bwana Mtume (s.a.w.w) akimwambia Abu Ubaida al-Jarrah akisema: Ewe Abu Ubaida! Bani Israili waliua manabii 43 kwa wakati mmoja katika nyakati za asubuhi na mapema, baada ya hapo wakasimama watu 112 wa Bani Israili mbele ya wauaji wa manabii hao, kwa nia ya kuamrisha mema na kuzuia maovu, nao pia wakauawa mwishoni mwa siku hiyo hiyo. [39]

Viwango na daraja za Mitume

Kulingana na Aya isemayo: (وَلَقَدْ فَضَّلْنَا بَعْضَ النَّبِيِّينَ عَلَىٰ بَعْضٍ ; Na kwa hakika tumewapandisha viwango baadhi ya manabii na tukawapa daraja kubwa kuliko wengine). [81] Kiuhalisia hadhi na nafasi za manabii haziko sawa, bali baadhi yao wana daraja kubwa zaidi kuliko wengine. Katika Hadithi ni kwamba; hadhi ya bwana Mtume Muhammad (s.a.w.w), ni bora ya juu zaidi kuliko manabii wengine. [82] [Maelezo 2]Kulingana na mtazamo wa Wayahudi, manabii watokao ukoo wa Wana wa Israeli, ni bora zaidi kuliko manabii wengine, ambao kati yao, Nabii Mussa (a.s), kwa mtazamo wao Nabii Musa (a.s) ni bora kuliko manabii wengine. [83]

Ulu al-Azmi

Makala Asili: Ulu al-Azmi

Kulingana na maoni ya Ayatullahi Tabatabai ni kwamba, maana ya "al-Azm" katika Aya ya 35 ya Surat al-Ahqaf ni sheria na maana ya Ulu al-Azm ni Mitume wenye sharia au walikuja na sheria. Kwa mtazamo wake, Mitume watano (Nuhu, Ibrahim, Mussa, Issa, na Muhammad (s.a.w.w)) ndio wenye sheria amabo wnajulikana kwa jina la Ulu al-Azm. [84] Baadhi ya wanazuoni wengine wanaamini kuwa "Ulu al-Azm" siyo jina linalohusiana na Mitume wenye sheria tu. [85] Kulingana na maelezo ya moja ya Riwaya za bwana Mtume (s.a.w.w), ni kwamba; Ulu al-Azm ni bora kuliko Mitume wengine. [86]

Mamlaka na cheo cha Utume (Urasuli)

Kulingana na kauli maarufu, dhana ya Unabii ni pana zaidi kuliko dhana ya Utume (Urasuli). Kilingana na kauli hii ni kwamba; kila Mtume ni Nabii, lakini siyo kila Nabii ni Mtume (Rasuli). [87] Kwa mujibu wa moja ya Hadithi, ni kwamba wajumbe wote wa Mwenye Ezi Mungu, 313 kati yao walikuwa ni Mitume (Marasuli). [88] Baadhi ya tofauti zilizopo kati ya Nabii na Mtume (Rasuli) ni kama ifuatavyo:

  • Mtume (Rasuli) hupokea ufunuo kutoka kwa Malaika Jibrail (Gabriel) katika hali akiwa macho na hata ndotoni, lakini Nabii hupokea ufunuo hali akiwa ndotoni tu. [89]
  • Ufunuo kwa Mtume (Rasuli) hushushwa kupitia Malaika aitwae Jibrail (Gabriel), lakini ufunuo kwa Nabii unaweza kushushwa na malaika wengine au kupitia ilhamu ishushwayo moyoni, au kupitia ndoto. [90]
  • Mtume, mbali na kuwa na cheo cha unabii, pia ana jukumu la kutimizi huja (kufikisha ujume) kwa wengine. [91]
  • Mtume ni mjumbe aliyekuja na sharia na huanzisha sharia ndani ya jamii, ila Nabii ni mlinzi wa sheria iliyopo au iliopita kabla yake. Tabrisi amenasibisha kauli hii na mwanazuoni aitwaye Jahidh. Hata hivyo, baadhi ya wafasiri kama vile Tabari, wanachukulia Nabii na Mtume kama ni maneno yanayoweza kutumika kwa kunaibiana, kwa mtazamo huu, yote mawili yatakuwa na maana moja. [93]

Wajumbe Waanzilishi wa Sharia na Wajumbe Wasambazaji wa Sharia

Kulingana na mgawanyiko wa wajumbe na mitume katika makundi mawili; wajumbe waanzilishi sharia na wahubiri au wasambazaji wa sharia, wajumbe wasambazaji sharia wanajukumu la kukuza, kutangaza, kutekeleza, na kufasiri sheria ambazo zilikuwepo wakati wa ujumbe wao. Kinyume na mitume au wajumbe ambao ni waanzilishi wa sharia, ambao ni kama vile; Nuhu, Ibrahimu, Musa, na Isa [95], ambao wao wenyewe walikuwa ni waanzilishi wa sharia. [96] Kiuhalisia idadi ya wajumbe waliokuja na sharia mpya, ni ndogo mno. [97]

Nafasi na Cheo cha Uimamu

Kulingana na Aya ya kutahiniwa kwa nabii Ibrahimu, yaonekana kwamba; baadhi ya Mitume walikuwa na cheo cha Uimamu. [98] Katika baadhi ya Riwaya kunai bara zioneshazo kwamba; cheo cha Uimamu ni kikubwa zaidi kuliko cheo cha Utume na Unabii, dhana hii inaeleweka kupitia maelezo ya Aya hiyo ya kutahiniwa kwa nabii Ibrahim (a.s), kwani yeye alipata cheo hicho mnamo mwishoni mwa umri wake, ambapo hapo mwanzo alikuwa ni nabii au mtume ila haukuwa ni Imamu. [99] [Maelezo 3] Katika Surat al-Anbiyaa, kuna mitume kadhaa waliotambuliwa kuwa ni Maimamu, nao ni; Ibrahimu, Is'haq, Yaaqub na Lut (a.s). [100] Katika moja ya Hadirhi ilionukuliwa kutoka kwa Imamu Swadiq (a.s) ni kwamba; Mitume wa Ulu al-Azmi ni wenye cheo cha Uimamu. [101]

Kuwakiuka Malaika kwa Utukufu

Kulingana na kauli ya Sheikh Mufidu ni kwamba; Mashia na Ahlul-Hadith wa upande wa Masunni, wanawatambua Mitume kuwa ni wenye cheo kukubwa zaidi kuliko Malaika, ila Mu’utazila wao wanaamini ya kwamba; Mailka ni wenye cheo kikubwa kuwazidi Mitume (a.s). [102] Katika baadhi ya Hadithi yaonesha kwamba; cheo na Nabii Muhammad (s.a.w.w) pamoja na Maimamu 12 (a.s), kikubwa zaidi kuwazidi Malaika. [103]

Manabii Waliopewa Vitabu

Baadhi ya manabii wamekuwa na vitabu vya mbinguni; kwa mujibu wa Aya za Qur'an, Zabur ni kitabu cha Nabii Daud (a.s) [104], Taurati ni kitabu cha Nabii Mussa (a.s), Injil ni kitabu cha Nabii Issa (a.s) [105], na Qur'an ni kitabu cha Mtume Muhammad (s.a.w.w) [106]. [Maelezo 4] Quran haitaji kitabu makhususi kwa ajili ya Nabii Ibrahim (a.s) na badala yake imetumia neno Suhuf kuhusiana na kitabu chake. [107] Zaidi ya hayo, kwa kuzingatia maelezo ya baadhi ya Hadithi, Mwenyezi Mungu alituma Suhuf 50 kwa Nabii Sheith (a.s), Suhuf 30 kwa Nabii Idris (a.s), na Suhuf 20 kwa Nabii Ibrahim (a.s) [108].

Wafasiri wameamini kuwa Nabii Nuhu (a.s), Ibrahim (a.s), Mussa (a.s), Issa (a.s), na Muhammad (s.a.w.w) walikuja na sheria mpya kutoka mbinguni, imani hii inatokana na ufahamu wao kulingana na Aya isemayo: (شَرَعَ لَكُمْ مِنَ الدِّينِ مَا وَصَّىٰ بِهِ نُوحًا وَالَّذِي أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ وَمَا وَصَّيْنَا بِهِ إِبْرَاهِيمَ وَمُوسَىٰ وَعِيسَىٰ ; Tumekupangieni sheria kutokana na dini sawa yale tuliyomuamrisha Nuhu, sharia ambazo tumekuusia wewe (tumekufunulia wewe), na ambazo tuliyowausia Ibrahim, Mussa na Issa)) [109] [110]. Katika baadhi ya Riwaya, emeelezwa kwamba; sababu ya Manabii hawa kuitwa Ulu al-Azimi inatokana na Manabii hawa kuwa sheria zao mpya katika jamii zao. [111]

Alama Tabatabai amesema kuwa kila Mtume wa Ulu al-Azmi alikuja na kitabu na sheria yake maalumu [112], na suala la kuwepo kwa vitabu vya Manabii ambao sio Ulu al-Azmi kama Daud (a.s) [113], Shiith (a.s) na Idris (a.s) [114], halikinzani na kauli inayo dai kwamba; Manabii wa Ulu al-Azmi ndio walikuja na sharia mpya kutoka kwa Mola wao; kwa sababu kwa vitabu vya Manabii ambao sio Ulu al-Azmi havijumuishi ndani yake amri na sheria [115].

Miujiza

Miujiza ni njia moja wapo za kutofautisha kati ya manabii na wadanganyifu wa unabii. Muujiza ni kitendo cha ajabu kinachotekelezwa na Mungu kupitia mtume, ambacho huambatana na madai ya unabii wake na kutoa changamoto kwa wapinzani wake. [116] Qur'an imetaja baadhi ya miujiza ya baadhi ya manabii, miongoni mwayo ni; Ngamia wa nabii Saleh [117], kupoza kwa moto alio tupwa ndani yake nabii Ibrahim [118], Kufufuka kwa ndege wanne kwa mkono wa nabii Ibrahim. [119] Pia Qur’ani imetaja baadhi ya miujiza tisa ya nabii Mussa, kama vile; fimbo kugeuka nyoka [120], kutiririka kwa chemchem ishirini na mbili za maji kwa makabila ya Waisraeli [121], kupasuka kwa bahari na kupata njia ya wokovu kwa Waisraeli [122], kung’ana na kuwa mweupe mkono wa nabii Mussa.[123] Miujiza mingine ilioashiriwa ndani ya Qur’ani, ni miujiza ya nabii Issa, ambayo ni; kuponya wagonjwa, kuwafufua wafu, na kugeuza udongo kuwa ndege. [124] Muujiza muhimu uliotajwa ndani ya Qur’ani kuhusiana na Mtume Muhammad (s.a.w.w), ni; Qur'an Tukufu [125] na kugawanyika kwa mwezi. [126] Tulio iashiria hapa ndio miujiza mashuhuri ya manabii iliyotajwa katika Qur'an tukufu. Ibn Jawzi naye akinukuu kutoka katioka vyanzo mbali mbali, ametaja zaidi ya miujiza 1000 iliyo nukuliwa kuhusiana na Mtume Muhammad (s.a.w.w) [127].

Watambuzi wanaamini kwamba; tofauti katika miujiza inatokana na tofauti katika maarifa, mawazo na mahitaji ya watu yalivyo katika nyakati tofauti. Hekima ya Mungu imepelekea muujiza wa kila nabii kuwa na uhusiano na mahitaji ya hadhira yake. Kwa mfano, wakati wa Nabii Mussa, uchawi na kiinimacho vilikuwa vimeenea kila pembe, hivyo basi Mwenye Ezi Mungu alimpa Mussa muujiza wa fimbo iliyo waajizi wachawi na kuwafanya washindwa kuiga na kutengeneza mfano wake, na ikawa ni hoja dhidi yao.[128]

Viashio (Irhaasaat)

Makala Asili: Irhaas (Viashiria)

Matukio yaliyotokea kabla ya utume wa manabii na kwa lengo la kuwaandaa watu kwa ajili ya kukubali dai lao la baadaye (la utume), [129] katika istilahi za wanatheolojia hujulikana kwa jila la Irhaasaat ارهاصات (vithibitisho na viashirio). Kuokolewa kwa Nabii Mussa (a.s) kutoka kwenye Mto Nile, kuzungumza kwa Nabii Isa (a.s) hali akiwa ni mtoto mchanga, kukauka kwa Ziwa la Sawe, kutetemeka kwa kasri la utawala wa Kisra, kuzimika kwa moto wa Faris (Iran) na matukio mengine ambayo yalitokea wakati wa kuzaliwa kwa bwana Mtume (s.a.w.w) yalikuwa ni miongoni mwa ishara za unabii. [131]

Bibliografia (seti ya orodha ya vitabu)

Wanahadithi, wafasiri, na wanatheolojia wa Kiislamu wamehusiha sehemu maalumu ya kazi zao za uandishi kuhusiana na manabii. Alama Majlisi ametnga juzu za kitabu chake Bihar al-Anwar kwa ajli ya Riwaya zinazohusiana na manabii [132], na juzu tisa kwa ajili ya historia ya bwana Mtume Muhammad (s.a.w.w). [133] Pia kuna vitabu kadhaa vilivyoandikwa makhususis kuhusisna na manabii tu, ambavyo vingi miongoni mwavyo vimechapishwa kwa jina la "Qasasu al-Anbiyaa" (Hadithi za Manabii). Kwa kiasi kikubwa Katika kazi hizi, zimejikita katika kuelezea maisha ya manabii, na wakati mwengine vinahusiana na uchambuzi wa mada za imani zinazohusiana nao. Baadhi ya kazi hizi ni pamoja na:

Pia, kuna vitabu kadhaa vilivyo andikwa na wanazuoni wa Kisunni kuhusiana na visa vya Manabii ambavyo baadhi yake ni; Arā'isu al-Majālisi kilichoandikwa na Ahmad bin Muhammad Tha'alabi, "Qasas al-Anbiya" kilichoandikwa na Ibnu Kathir, na "Qasas al-Anbiya" kilichoandikwa na Abu Ishaq al-Nisaburi.

Maelezo

  1. Isma'il bin Hizqiil (Ezekiel) ni miongoni mwa manabii wa Waisraeli. Allama Tabatabai anaamini kwaba; Isma'il aliye tajwa na Qur'an katika Suratu Mariam, ni nabii Hizqiil (Ezekiel), ambapoMwenye Ezi Mungu katika Aya hiyo alisema: (واذكُر فِى الكِتبِ اِسمعيلَ اِنَّهُ كانَ صادِقَ الوَعدِ و كانَ رَسولاً نَبيـّا ; Na mtaje katika kitabu Isma'il. Hakika yeye alikuwa mwaminifu wa ahadi, na alikuwa Mtume na Nabii) (Surat Maryam, aya 54), (Tabatabai, Al-Mizan, Chapa ya Mwaka 1417 Hijiria, Juzuu ya 14, Ukurasa 63).
  2. قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (ص‌) مَا خَلَقَ اللَّهُ خَلْقاً أَفْضَلَ مِنِّي وَ لَا أَكْرَمَ عَلَيْهِ مِنِّي قَالَ عَلِيٌّ (ع) فَقُلْتُ يَا رَسُولَ اللَّهِ فَأَنْتَ أَفْضَلُ أَمْ جَبْرَئِيلُ؟ فَقَالَ (ص) يَا عَلِيُّ! إِنَّ اللَّهَ تَبَارَكَ وَ تَعَالَى فَضَّلَ أَنْبِيَاءَهُ الْمُرْسَلِينَ عَلَى مَلَائِكَتِهِ الْمُقَرَّبِينَ وَ فَضَّلَنِي عَلَى جَمِيعِ النَّبِيِّينَ وَ الْمُرْسَلِينَ ; Mjumbe wa Allah (s.a.w.w) alisema, "Allah hajamuumba kiumbe bora zaidi kuliko mimi, wala hajamtukuza yeyote zaidi yangu." Ali (a.s) anasema, nilimuuli nikasema: "Ewe mjumbe wa Allah, je, wewe ni bora zaidi au Jibril?" Bwana Mtume (s.a.w.w) akasema, "Ewe Ali, hakika Allah, Mtukufu Alie wa juu kabisa, amewapandisha na kuwatafautisha mitume wake kidaraja kuliko hata Malaika wake wa karibu, na akanikweza mimi kuwa ni mbora kuliko manabii na mitume wote. (Saduq, Kamal al-Din, 1395 A.H., Juz. 1, uk. 254)
  3. Kwenye Hadithi maarufu kutoka kwa Imamu Sadiq (a.s), hatua za Ibrahimu (a.s) kabla ya kuwa Imam zimeorodheshwa kama ifuatavyo: 1- Uchamungu 1- Unabii 2- Utume 3- Ukhalifa (Khalilu Llahi) na 4- Uimamu. Hadithi imekuja kama ifuatavyo: (إنّ اللّه َ تباركَ و تعالى اتَّخَذَ إبراهيمَ عَبدا قَبلَ أن يَتَّخِذَهُ نَبيّا ، و إنّ اللّه َ اتَّخَذَهُ نَبيّا قَبلَ أن يَتَّخِذَهُ رَسولاً ، و إنّ اللّه َ اتَّخَذَهُ رَسولا ً قَبلَ أن يَتَّخِذَهُ خَليلاً ، و إنّ اللّه َ اتَّخَذَهُ خَليلاً قَبلَ أنْ يَجعَلَهُ إماما ، فلَمّا جَمَعَ لَهُ الأشياءَ قالَ : «إنّي جاعِلُكَ لِلنّاسِ إماماً... ; Hakika Mwenyezi Mungu amemfanya Ibrahimu kuwa mtumwa (mchamungu) kabla ya kumfanya kuwa nabii, na hakika Mwenyezi Mungu amemfanya kuwa nabii kabla ya kumfanya kuwa mtume, na hakika Mwenyezi Mungu amemfanya kuwa mtume kabla ya kumfanya kuwa Khalifa, na hakika Mwenyezi Mungu amemfanya kuwa Khalifa kabla ya kumfanya kuwa Imamu, na alipokamilishia vyeo vyote hivyo, alisema: "Hakika mimi nimekufanya wewe kuwa ni Imamu wa watu...) Al-Kulayni, Al-Kafi, Chapa ya mwaka 1407 Hijiria, Juzuu ya 1, Ukurasa 175.
  4. Qur'an haitoi tamko la moja kwa moja kuhusiana na suala la kuteremshiwa nabii Musa Taurati; lakini inakiri kuteremshwa kwa Taurati kutoka kwa Mwenye Ezi Mungu. Jambo ambalo limethibitishwa kwenye (Surat al-Ma'ida, Aya 44) na pia inathibitisha kuteremshwa kwa Al-waahu kwa ajili ya nabii Musa, jambo ambalo linapatikana kwenye (Surat al-A'araf, Aya 154). Baadhi ya wafasiri wamesema kuwa; Al-waahu ni Taurati (Tabatabai, Al-Mizan, Chapa ya 1417 Hijiria, Juzuu ya 8, Ukurasa 250).

Rejea

Vyanzo