Nabii Is’haka

Kutoka wikishia

Is’haka (Kiarabu: النبي إسحاق (ع)) alikuwa ni mmoja wa manabii wa Mwenye Ezi Mungu, mwana wa Ibrahimu na ndugu wa Ismaili. Yeye ni babu wa Waisraeli, na pia ni babu wa baadhi ya manabii, ambao ni pamoja na; Nabii Yakobo, Daudi, Sulemani, Yusufu, na Mussa, wote wanatokana na kizazi chake. Isaka pamoja masuala yanayo husiana na unabii wake, miongoni mwa mada zilizojadiliwa ndani Qur'an tukufu. Taurati pamoja na baadhi ya vyanzo vingine kutoka madhehebu ya Sunni vimemuhisabu Is’haka kuwa ndiye Dhabihu-llah. lakini kulingana na imani ya madhehebu ya Shia; Ismail -mwana mwingine wa Ibrahimu- ndiye Dabihu-llah.

Is’haka alizaliwa huku baba yake akiwa na umri wa miaka 100 huku mama yake (Sarah) akiwa na miaka 90. Bishara za Mwenye Ezi Mungu juu ya kuzaliwa kwake, ni miongoni mwa yaliyo tajwa ndani ya qur'an Tukufu. Is’haka alifikia cheo cha unabii, baada ya kifo cha ndugu yake (Ismaili) (a.s).

Utafiti juu ya wasifu na utambulisho wake

Is’haka ni mmoja wa manabii wa mungu na mwana wa Ibrahimu na Sarah. [1] ambaye alizaliwa na kuishi huko Palestina. [2] Is’haka ni neno la Kiibrania linalomaanisha mwenye tabasamu. [3] Baadhi pia wameamini kuwa; jina hili limetokana na lugha ya Kiarabu. [4] Inaaminika kuwa; Is’haka alizaliwa miaka mitano au kumi na tatu baada ya Ismaili. [5] Wakati wa kuzaliwa kwa Isaka, baba yake alikuwa na zaidi ya miaka 100, na mama yake alikuwa na miaka 90. [6] Isaka alioa mwanamke aliye julikana kwa jina la Rafaqa akiwa na umri wa miaka 40 na akapata watoto wawili walioitwa ‘Aisu na Yaakubu.

Yeye ni babu wa wana wa Israeli na kama ilivyotabiriwa na Malaika Gabriel, manabii kama Yakobo, Yusufu, Daudi, Suleimani, Ayubu, Mussa, Haruni na manabii wengine wa wana wa Israeli walizaliwa kutoka kizazi chake. [8] Kulingana na ripoti za kihistoria, Ibrahimu alikuwa ni ami wa nabii Luti, na nabi Isaka alikuwa ni binamu yake. [9]

Tukio la kuchinjwa kwa Ismaili, katika Biblia ya Kiyahudi, linasibishwa kwa Is’haka na siyo Ismaili, Wayahudi pia huona kuwa; tukio la kuchinjwa kwa kwa Is’haka, moja ya sababu za ubora wake juu ya Ishmaeli. [10] Baadhi ya wanazuoni wa madhehebu ya Sunni, pia nao wanashikamana na imani hii. [11] Walakini, Washia wamekataa nadharia ya kuchinja kwa Isaka kwa kurejelea aya ya 112 ya Surat As-Saffat, [12] na aya ya 71 ya Surat Hud, [13] wamekanusha tukio la kuchinjwa kwa Is’haka. [14]

Kabla ya kifo chake, kulingana na amri ya Mwenye Ezi Mungu, unabii wa Is’haka ulirithiwa na mwanawe (Yakubu). [15] Kwa mujibu wa maandiko ya Taurati, Is’haka alitaka utume wake urithiwe na mwanawe mwingine ajulikanaye kwa jina la ‘Ais au ‘Isu, lakini Yakubu na mama yake walimhadaa, na hatimae unabii huo ukahamia kwa Yakubu. [16] Muhammad Hadi Marifati, ambaye ni mtafsiri na mtafiti wa Qur’ani, ameichukulia Imani hiyo ilioko kwenye Taurati, kuwa ni mfano hai katika masuala ya kuwavunjia heshima mitume. Ameendelea kuleze ya kwamba; usemi huu unamaanisha kwamba, familia ya nabii Yakubu ilikuwa ni familia danganyifu, ambayo kuto kuona kwa nabii Is’haka, ilikuwa ni kama nafasi nyeti waliotumia kwa ajili ya kufikia malengo yao. [17] Pia yeye amaihisabu dhana hii ilioko kwenye Taurati, kuwa ni dhana ya jeuri dhidi ya manabii watukufu wa Mwenye Ezi Mungu. [18]

Is’haka alifariki dunia karibu na Baitu al-Muqaddas (ilioko nchini Palestina), akiwa katika umri wa miaka 180, na akazikwa katika mji wa al-Khalili ulioko huko huko Palestina. (19)

Bishara ya kuzaliwa kwake

Kwa mujibu wa Aya za Qur'an, kabla ya kuzaliwa kwa Is’haka, Mungu aliwajulisha wazazi wake juu ya tukio hili na kuwapa habari njema juu ya kuzaliwa kwa mtoto huyo. [20] Bishara njema hii imetajwa katika Aya ya 71 ya Surat Huud. Kisa cha kuzaliwa kwa Is’haka, bila kutaja jina lake, pia imetajwa katika Aya ya 53 ya Surat Hijri na Aya ya 29 ya Surat Dhariyat. Jina Isaka limetajwa mara 17 katika Sura 12 za Qur'an Tukufu. [21]

Utume wake

Ramani ya mahali alipokuwa akiishi Nabii Is'haka

Baada ya kifo cha kaka yake (Ismail), Is’haka alirithi nafasi yake ya utume, [22] na baada yake manabii wote walitoka katika kizazi cha Is’haka; Isipokuwa Mtume Muhammad (s.a.w.w), ambaye alitokana na kizazi cha Ismail. [23] Nasabu ya bwana Mtume (s.a.w.w), kupitia mababu 21 inamfikia Adnan ambaye ni miongoni watu wa kizazi cha Ismail. Ila hautambulikani ni idadi gani ya mababu kutoka kwa Adnan hadi kumfikia Ismail. [24]

Katika Qur’ani Kuna Aya 8 kadhaa, ambazo ima zanashiria utume wa nabi Is’haka kwa njia ya wazi au kwa njia isiyo. Miongoni mwazo, ni Aya makhususi inayo zungumzia utume wa nabi Isaka, [25] Aya inayo zungumzia kuteremshiwa watoto wake kitabu kitakatifu, [26] Aya inayo zungumzia sharia alizoshushiwa nabi Is’haka, [27] Aya ianayo zungumzia kuteremshiwa kwake wahyi, [28] Aya zinazotoa amri ya kumfuata Is’haka, [29] na Aya inayo zungumzia Uimamu wa nabi Isaka. [30] Katika Aya hizi, dini ya Isaka na Sheria zake, zilikuwa ni sawa na dini ya baba yake (Ibrahimu), yaani, dini ya Hanif (isiyo ya kishirikina), ambayo msingi wake ni tawhidi (kumpwekesha Mwenye Ezi Mungu. [31]

Maudhui yanayo fungamana

Vyanzo

  • The Holy Qurʾān.
  • Bible, tarjuma barāy-i aṣr-i jadīd. Anjumanhā-yi Muttaḥid-i Kitāb-i Muqaddas. 2007.
  • Ibn Kathīr, Ismāiʿl b. ʿUmar. Al-Bidāya wa al-nahāya. Edited by Khalīl Shaḥāda. Beirut: Dār al-Fikr. [n.d].
  • Markaz-i Farhang wa Maʿārif-i Qurʾān. Dāʾirat al-maʿārif Qurʾān karīm. Qom: Muʾassisa Būstān-i Kitāb, 1382 Sh.
  • Masʿūdī, ʿAlī b. al-Ḥusayn al-. Ithbāt al-waṣīyya li-l Imām ʿAlī b. Abī Tālib. Qom: Muʾassisat Anṣārīyān, 1384 Sh.
  • Muṣṭafawī, Ḥasan. Al-Tahqīq fī kalimāt al-Qur'ān al-karīm. Tehran: Bungāh tarjuma wa nashr-i kitāb, 1360 SH.
  • Makārim Shīrāzī, Nāṣir. Tafsīr-i nimūnah. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmiyya, 1374 Sh.
  • Qurashī Bunābī, ʿAlī Akbar. Qāmūs-i Qurān. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmiyya, 1412 AH.
  • Qurtubī, Muḥammad b. Aḥmad al-. Al-Jāmiʿ li-aḥkām al-Qurʾān. Tehran: Intishārāt-i Nāṣir Khusraw, 1364 Sh.
  • Qazwīnī, Sayyid Mahdī. Al-Mazār: Madkhal li taʿyīn qubūr al-ʾanbīyā wa al-shuhadāʾ wa awlād al-aʾimma wa al-ʿulamāʾ. Edited by Jawdat al-Qazwīnī. Beirut: Dār al-Rafdayn, 1426 AH.
  • Shuqī, Abū Khalīl. Aṭlas-i Qurān. Translated to Farsi by Kirmanī. Mashhad: Āstān-i Quds-i Raḍawī, 1389 Sh.
  • Ṭabarānī, Sulaymān b. Aḥmad. Tafsīr al-kabīr: tafsīr al-Qurʾān al-ʿazīm. Edited by Hishām ʿAbd al-Karīm al-Badrānī al-Mouselī. Jordan: Dār al-Kitāb Thiqāfī, 2008.
  • Ṭabarī, Muḥammad b. Jarīr al-. Tārīkh al-Ṭabarī. Edited by Muḥammad Abu l-faḍl Ibrāhīm. Beirut: Dar al-Turāth, 1387 AH.
  • Ṭabāṭabāyī, Mūhammad Ḥusayn. Al-Mīzān fī tafsīr al-Qurʾān. Fifth edition. Qom: Maktabat al-Nashr al-Islāmī, 1417 AH.