Nenda kwa yaliyomo

Suhuf

Kutoka wikishia

Suhuf (Kiarabu: الصُحُف) ni kila ambacho kimeandikwa ndani yake maarifa, hukumu na Aya za Mwenyezi Mungu. Katika Qur’ani na hadithi neno Suhuf kwa sura ya jumla limetajwa kuwa ni vitabu vya Mitume na baadhi ya vitabu maalumu kama vile Qur’an na kitabu cha Ibrahim. Suhuf imetumika pia kwa maana ya kitabu au daftari la amali na matendo ya mtu.

Maana

Hussein Mustafavi, mfasiri na mwandishi kamusi (1426-1334 Hijiria) ameandika katika kitabu cha utafiti, Suhuf katika istilahi ina maana ya kitu ambacho ndani yake kumeandikwa mafundisho ya Kimungu, hukumu na Aya zilizoshushwa kwa Mitume. Aina ya Suhuf hizi zilikuwa tofauti kulingana na zama: Wakati mwingine zilitengenezwa kwa mbao, baadhi ya wakati zilikuwa za ngozi na wakati mwingine zilitengenezwa kutokana na karatasi, nk. [1]

Suhuf ni wingi wa neno Sahifah [2] na maana yake halisi ni kitu chochote kipana [3] au kitu kinachoandikwa juu yake. [4]

Vitabu vya mbinguni

Katika Aya ya 133 ya Surat Taha, Mwenyezi Mungu amevitaja vitabu walivyoshushiwa Mitume kwa jina la Suhuf. [5]

Kadhalika katika Aya ya 52 ya Surat Muddathir Allah anasema: ((بَلْ يُرِيدُ كُلُّ امْرِئٍ مِّنْهُمْ أَن يُؤْتَى صُحُفًا مُّنَشَّرَةً ; Bali kila mmoja katika wao anataka apewe nyaraka zilizofunuliwa)).Wafasiri wa Qur’ani wanasema kuwa, makusudio ya Suhuf katika Aya hii ni kitabu cha mbinguni. [6]

Katika Qur’ani vitabu vya Nabii Ibrahim (a.s) na Mussa (a.s) vimetajwa pia kwa jina la Suhuf. ((صُحُفِ إِبْراهیمَ وَ مُوسى‏ ; Kitabu cha Ibrahim na Mussa)). [7] Wafasiri wanasema kuwa, makusudio ya Suhuf Mussa ni Torati na wanaitakidi kwamba, makusudio ya Suhuf Ibrahim ni kitabu cha Ibrahim alichoshushiwa. [8] Aidha katika hadithi vitabu vya Nabii Adam, [9], Shith, [10] na Idrissa [11] vimetajwa kwa jina la Suhuf.

Wafasiri wanaamini kwamba, katika Aya ya 13 ya Surat Abasa na Aya ya 2 ya Surat al-Bayyinah, makusudio ya Suhuf ni Qur’ani. [12]

Daftari la amali

Wafasiri wanasema, katika Aya ya: ((وَ إِذَا الصُّحُفُ نُشِرَتْ ; Na madaftari yatakapo enezwa)), [13] daftari la amali na matendo ya mtu limetajwa kwa jina la Suhuf: [114] Imamu Ridha (a.s) pia amenukuliwa katika hadithi moja akitaja daftari na kitabu cha amali kwa jina la Suhuf. [15]