Nenda kwa yaliyomo

Miujiza

Kutoka wikishia

Muujiza ni istilahi maalumu inayotumika katika fani na taaluma ya itikadi (ilmu al-Kalamu). Neno hili kiistilahi, humaanisha kupatikana au kutendeka kwa tendo fulani la ajabu lisichokuwa la kawaida, na linachoambatana na madai ya unabii, lenye nia ya kutoa changamoto kwa wengine, ambao hawawezi kutekeleza tendo kama hilo. Katika Qur'ani, kuna simulizi nyingi kuhusiana na miujiza ya Manabii mbalimbali, ambazo kwa mujibu wa wanazuoni Waislamu, kila muujiza uliendana na zama za na hali maalimu za kijamii walizokuwa wakiishi Manabii hao ndani yake. Baadhi ya miujiza maarufu iliyojiri ndani ya zama mbali mbali, ni pamoja na: kufufua wafu kulikofanywa na Nabii Isa (a.s), kubadilika kwa fimbo ya Nabii Musa (a.s) na kuwa joka mwenye uhai kamili, mkono wake (Nabii Musa) kuwa mweupe (Yadu Baidhaa), na kule Nabii Ibrahim (a.s) kunusurika katika moto aliotumbukizwa ndani yake. Wanazuoni wa Kiislamu wanaamini kwamba; Qur'ani Tukufu ni muujiza wa kudumu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w). Pia, katika baadhi ya vyanzo vya Hadithi vya Kishia, kuna miujiza kadhaa iliyonukuliwa kutoka kwa Maimamu wa Kishia (a.s), miojiza amabyo ilijiri kwa ajli ya kuthibitisha uongozi wao kwa amri ya Mungu. Wanatheolojia wa Kishia wanaamini kuwa; katu miujiza haipingani na kanuni ya kimaumbile isemayo kwamba; kila jambo kupatikana kupia sababu maalumu, na kwamba kila zasabu huwa na athari yake maalumu. Hivyo miujiza yote ni yenye kufuata msingi huu, isipokuwa matukio ya kimiujiza hutokea katika isiyo ya kawaida au isiyozoweleka, ambapo huvunja ile fikra ya wanadamu walioizoea katika utokeaji wa mambo hayo. Jambo halimaanishi kwamba mambo hayo yanatokea bila sababu maalumu. Badala yake, hutokea kupitia sababu za asili za kimaumbile, au kupitia sababu nyengine ambazo zipo nyuma ya pazia la kimaada, au pia mambo hayo yanaweza kutokea kupitia sababu zote mbili; za kimaumbile na zilizo nyuma ya pazia la kimaumbile. Ufafanuzi wa Dhana ya Miujiza na Nafasi Yake Miujiza ni dhana na istilahi maalumu inayotumika katika fani na taaluma ya itikadi (ilmu al-kalamu). Dhana hii inarejelea tukio maalumu la kiajabu lisiloweza kufafanuliwa kupitia kanuni za kawaida za kibinadamu. Kikawaida, tukio hili huambatana na madai ya unabii, ambalo huwa ni changamoto ya kuthibitisha kuwa hakuna mwingine anayeweza kufanya hivyo isipokuwa mwenye kudai madai hayo. [1] Abd al-Razzaq Lahiji, mwanafalsafa na mwanazuoni wa Kishia, anasisitiza akisema kwamba; Muujiza ndio njia pekee ya kuthibitisha ukweli wa wito na madai ya nabii fulani. [2] Hata hivyo, wanazuoni wengine kama vile Jafar Subhani wanaamini kwamba; miujiza ni moja tu ya njia kadhaa zinazoweza kutumiwa katika kuthibitisha uhalali wa madai ya manabii wa Mwenye Ezi Mungu. [3] Tafiti kuhussiana na dhana ya muujiza, kuanisha mipaka yake, sifa zake, pamoja na tafsiri ya matokeo ya kimiujiza, ni miongoni mwa mambo umuhimu na ya msingi katika mijadala ya kiitikadi. Hii ni kwa sababu ya kwamba; dhana ya muujiza ina mahusiano ya moja kwa moja na masuala ya unabii na uthibitisho wa uhalali wa ujumbe wa manabii wa Mwenye Ezi Mungu. [4] Swali la kwamba; je miujiza inafuata au haifuati kanuni ya sababu za kimaumbile (kanuni ya usababishi /causality)? Limekuwa na mjadala wa muda mrefu miongoni mwa wanafalsafa, ambapo wanafalsafa mbali mbali wameamsha maswali kadhaa wakijaribu kuelewa jinsi miujiza inavyohusiana na kanuni za asilia za kimaumbile zilizomo ulimwenguni humu. [5] Na kwa kuwa miujiza inachukuliwa kuwa; ni uingiliaji wa moja kwa moja wa Mwenye Ezi Mungu katika mfumo wa utendekaji wa matendo ya ulimwengu wa kimaumbile, suala la nafasi ya miujiza na uhusiano wake na sheria za kimaumbile limekuwa ni mada kuu katika fani ya theolojia za kisasa (New Theology) . [6] Kwa upande mwingine, katika elimu ya theolojia za kisasa (New Theology), miujiza imekuwa ikiangaliwa kama ni ushahidi wa kuwepo kwa Mwenye Ezi Mungu, kwani matukio haya ya ajabu huonesha na kuakisi nguvu na uwezo wa hali ya juu alionao Mwenye Ezi Mungu. [7] Ingawa neno "muujiza" pamoja na mizizi yake limetajwa mara 26 ndani ya Qur’ani, ila mara nyingi neno hili katika Qur’ani huchukuwa maana ya "udhaifu" au "kuto kuwa na uwezo". [8] Kwa hiyo, maana ya dhana na istilahi ya muujiza iliyomo ndani ya Qur’ani, si kama vile inavyoeleweka katika elimu ya itikadi (theolojia), bali istilahi hii yenye maana ya kiistilahi na lengo la kuwapiku na kutoa changamoto kwa wengine, ilianzishwa na wanazuoni wa fani ya theolojia. [9] Qur’ani hutumia maneno mengine kabisa katika kuelezea dhana ya miujiza kiistilahi. Maneno yaliyotumiwa na Qur’ani kwa maana ya kiistilahi ni pamoja na; "Bayyina" (ushahidi wazi) [10], "Aya" (ishara ya wazi) [11], "Burhani" (ushahidi wa thabiti) [12], "Sultani" (ushahidi wa nguvu) [13], "Basira" (maono ya undani) [14], na "Ajab" (jambo la kushangaza). [15] [16] Maneno haya yanasisitiza kwamba miujiza si tu ile hali ya kupatikana kwa matukio yasio ya kawaida, bali ni ishara za wazi zinazoonesha uwepo wa Mungu na kuimarisha imani ya watu. Tofauti Kati ya Miujiza, Irhas na Karama Irhas ni istilahi ya kikalamu (kitheolojia) inayotumika kwa ajili ya kuelezea matukio ya ajabu yanayotokea kabla ya mtu kuteuliwa rasmi kuwa nabii. [20] Imeelezwa ya kwamba; matukio haya ya Irhas hutokea kwa lengo la kuandaa mazingira kwa ajili ya kuutangaza unabii wa nabii fulani. [21] Ingawa kiasilia matukio ya irhas yanafanana na matukio ya miujiza, ila kuna tofauti kubwa kati ya matukio mawili haya, kwani miujiza hutokea baada ya tangazo la unabii na huambatana na changamoto ya kuthibitisha ujumbe wa Kimungu, wakati irhas hutokea kabla ya hatua hiyo rasmi ya kutangazwa kuwa nabii huyo na bila ya nia ya kutoa changamoto fulani. [22] Pia miujiza inatofautiana na karama, ila karama ni matendo ya ajabu yanayofanywa na watu wema au wacha Mungu, lakini huwa hayahusiani na madai ya unabii ndani yake. Tofauti kuu iliopo kati ya miujiza na karama ni kwamba; miujiza inalenga kuthibitisha nafasi ya Utume au Unabii au Uimamu wa mtu fulani, na mara zote huambatana na changamoto inayothibitisha uwezo huo wa kipekee ila karama, kwa upande mwingine, hutokea bila madai ya Utume. [23]

Tofauti Kati ya Miujiza na Uchawi Makala Asili: Uchawi Kuna tofauti nyingi muhimu zlizotajwa kati ya miujiza na uchawi, kwa ajili ya kupambanua matukio mawili haya ya kiajabu. Tofauti zilizotajwa kati ya matukio mawili haya ya ajabu ni kama ifuatavyo: 1. Chanzo cha Tukio Chanzo cha miujiza kinatokana na nguvu maalumu za Kimungu zisizo na kikomo, ambazo ni zawadi na tunuko kutoka kwa Mwenye Ezi Mungu kwa manabii na wateule wake. Ila matendo na matukio ya kiuchawi hutegemea nguvu za kibinadamu zenye mipaka au msaada kutoka kwa roho za kishetani. [24] 2. Uwezo na Utekelezaji Wake Mchawi anaweza kufanya matendo machache tu, ambayo mtekelezaji wake huwa tayari ameshayafanyia mazoezi na majaribio kwa muda mrefu. Hata hivyo, hawezi kutekeleza kila aina ya matendo ya ajabu ambayo watu wanataka kuyaona kutoka kwake. Kinyume chake, miujiza hufanyika bila mazoezi au maandalizi ya awali, kwa kuwa hutegemea amri na idhini ya ya moja kwa moja kutoka kwa Mwenye Ezi Mungu mwenyewe. [25] 3. Lengo na Madhumuni Miujiza hufanywa kwa lengo la kuthibitisha ujumbe wa manabii na nafasi ya kiroho ya Imamu fulani, huku ikilenga mambo ya kheri na uongofu wa watu. Kwa upande wa pili, mara nyingi uchawi hutumiwa kwa nia mbaya, kama vile udanganyifu au malengo ya kuleta madhara fulani. [26] 4. Asili na Umuhimu Miujiza ni matendo ya ajabu yanayotendeka kupitia njia ya ajabu na isiyozoeleka katika ulimwengu wa matukio ya kimaumbile, yakionyesha wazi uingiliaji wa Mungu katika ulimwengu wa matukio ya ulimwengu wa kimaumbile. Ila kiuhalisia matukio ya kiuchawi, si matukio ya kiajabu; badala yake, ndani yake huwa kunatumika mbinu za kawaida, ambazo sababu zake huwa zimefichwa mbele za watu na kueleweka na wachache tu. [27] 5. Maadili na Usafi wa Nia Ibn Sina, mwanafalsafa maarufu wa Kishia, katika kitabu chake Al-Isharat wa Al-Tanbihat anabainisha akisema kwamba; miujiza na uchawi vinaweza kuonekana na mifanano fulani, kwa sababu yote mawili hutendeka kwa njia za kimaajabu. Hata hivyo, kuna tofauti kubwa kuhusiana na chanzo chake asili, ambacho ni nafsi maalumu zinazotekeleza matendo hayo. Miujiza hutokana na nafsi zilizopa usafi na maalumu kutokana na kumcha Mungu. Na kwamba miujiza hiyo hutumika kwa mambo ya kheri tu, wakati uchawi hutokana na nafsi zilizo mbovu na mara nyingi hutumika kwa ajili ya mambo mabaya. [28]


Namna ya Miujiza Inavyothibitisha Ukweli wa Madai ya Unabii Kwa mujibu wa maoni ya madhehebu ya Shia Imamiyya na Mu'tazila, ni kwamba; imani ya kuamini miujiza imekuja kwa ajili ya kuthibitisha madai ya unabii, inalazimiana na kukubali kimantiki iamni isemayo kwamba; mema na mabaya yanaweza kutambuliwa kupitia kiakili ya mwanadamu, hata bila ya kuwepo sheria maalumu za Kiungu. [29] Hii ina maana ya kwamba; Ingawa Mwenye Ezi Mungu ana uwezo wcha kutokea tukio kama hilo, kuwa kufanya hivyo ni kinyume na maadili ya wenye hekima. Kwa mtazamo wao, hekima ni sifa thabiti kwa Mwenye Ezi Mungu, kwa hiyo, haiwezekani yeye kutenda matendo yakiukayo maadili mema au kwenda kinyuma na akili. Hivyo basi, pale miujiza inapotekea, huwa inathibitisha ukweli wa madai ya unabii yanayodaiwa na mtu huyo. [30] Kwa upande mwingine, Ash'ariyya wanaamini ya wa kwamba miujiza ni sehemu ya desturi ya Mwenye Ezi Mungu anayoitumia katika kuthibitisha ujumbe wa manabii wake. Kwa mtazamo wao, miujiza huwa inaambatana moja kwa moja na madai ya unabii wa nabii fulani, yenye malengo ya kuthibitisha ukweli wa nabii huyo. Wakisistiza itikadi hii wanasema kwamba; Ingawa kiakili inawezekana mtu fulani mwongo akaoyeshe matendo ya kimiujiza, ila jambo hili halilingani na utaratibu wa kawaida wa Mungu katika kuonyesha uthibitisho wa manabii wake. [31] Nini Chanzo na Sababu za Kupatikana kwa Miujiza? Kwa mujibu wa maoni ya wanafalsafa na wanakalam (wanatheolojia), miujiza haivunji kanuni ya sababu na visababishwaji (causality), wala si kwamba ni matukio maalumu yasiokuwa na sababu katika kutokea kwake. [32] Hata hivyo, kuna tofauti za maoni juu ya sababu ya miujiza na chanzo chake, maoni hayo ni kama ifuatavyo: [33] 1. Maoni ya Ash'ariyya: Ash'ariyya wana mtazamo maalum kuhusiana na tawhid katika ngazi ya matendo, wao wanaamini kwamba; Mwenye Ezi Mungu ndiye chanzo pekee, na Yeye ndiye pekee mwenye uwezo juu ya matukio yote ulimwenguni humu. Kwa hiyo, wao wanaamini kwamba; kiasili miujiza ni matendo ya moja kwa moja ya Mwenye Ezi Mungu, [34] nayo ni matokeo yasiyopitia ngazi au au wakala yeyote yule kutoka kwake. [35] 2. Maoni ya Kundi la Kwanza la Wanafalsafa kama Ibn Sina na Mulla Sadra: Wanafalsafa hawa wanaamini kuwa; miujiza inatokana na nafsi au roho ya kinabii walionayo manabii wa Mwenye Ezi Mungu. Mulla Sadra anasema kwamba nafsi za baadhi ya watu ni za kimungu na zina nguvu kubwa mno, kiasi ya kwamba zinaweza kudhibiti mambo yote yaliomo ndani ya ulimwengu wa kimaada. Nguvu za nafsi zao hutawala ulimwengu huu na kuyafanya yote yaliomo ndani yake yawe chini ya amri zake. Kwa hiyo, kadri nafsi inavyokuwa safi na kufanana na misingi ya juu ya uwepo (kuwa karibu na Mungu), ndivyo nguvu zake katika kuutawala ulimwengu wa kimaada zinavyoongezeka. [36] [37] 3. Maoni ya Kundi la Pili la Wanafalsafa Kama Vile Sayyid Mohammad Hossein Tabatabai na Abdullah Jawadi Amuli: Wanafalsafa hawa wanaamini kuwa; Miujiza ni matokeo maalumu yanayofuata kanuni za sababu na visababishwavyo (causality), za ulimwengu wa kimada zisizo za kawaida, ambazo haziwezi kufikiriwa kupitia akili ya mwanadamu, wala kutekelezwa na mtu wa kawaida. [38] Wengine wanasema kwamba; ni manabii tu ndio wanaojua sababu hizi za kimada zisizo za kawaida, jambo ambalo limefichika mbele ya watu wengine. Hii ni kutokana na kule wao kufungamanishwa na ulimwengu wa ghaibu. [39] 4. Chanzo cha Kimalaika: Imani nyengine ni kwamba; miujiza hutokana na matendo ya malaika maalumu, ambao katika Qurani wanajulikana kwa jina la "mudabbirat". [40] Je, Miujiza Inavunja na Kuingilia Kati Kanuni Asilia za Usababishi (causality)? Kuna mitazamo kadhaa juu ya miujiza na uhusiano wake na usababishi (causality), mitazamo hii ni kama ifuatavyo: 1. Mtazamo wa Ufasiri Kinyume na Maana Dhahiri (Ta’awili): Wanaounga mkono mtazamo huu wamekubaliana na uwepo wa miujiza, lakini wanaifasiri kuwa; ni matukio yanayotokea ndani ya sheria za kawaida za usababishi (causality). [41] Kwa mtazamo wao ni kwmaba; Kwa kuwa Quran inautaja fumo wa uumbaji wa Mwenye Ezi Mungu kuwa ni mfumo wenye njia (Sunna) moja tu isiobadilika, kama ilivyoelezwa katika Aya isemayo; وَ لَنْ تَجِدَ لِسُنَّةِ اللَّهِ تَبْدِیلًا "Na katu hutakuta mabadiliko katika Sunna (njia ya uumbaji) ya Mwenyezi Mungu". [42] Kwa kuwa Aya hii inasisitiza kuwa; Sunna za Mwenye Ezi Mungu haziwezi kubadilika, [43] hivyo basi, muujiza hauwezi kuwa tukio la kushangaza liendalo kinyume na mfumo halisi wa maumbile ya Mungu. [44] Mortaza Motahari aliuita mtazamo huu kwa jina la "mtazamo wa Ta’awili” (mtindo wa ufasiri kinyume na dhahiri ilivyo) na kumtaja Syed Ahmad Khan Hindi kama mmoja wa wafuasi wa mtazamo huu. [45] 2. Mtazamo wa Ash'ariyya: Kwa mujibu wa itikadi na imani za Ash'ari, ni kwamb; muujiza ni tendo linalopindua njia na kanuni asilia za kimaumbile, na kuvunja mwenendo wa kawaida wa uumbaji ulimwenguni humu. Kwa mtazamo wao, mapenzi na matakwa ya Mwenye Ezi Mungu ndiyo yaliyojenga na kuweka mfumo huo asilia wa uumbaji na utendekaji wa matendo mbali mbali ulimwenguni. Ila kwa kuwa Mwenye Ezi Mungu ndiye sababu pekee yenye mamlaka kamili na uwezo wa kufanya kila jambo, kulingana na matakwa yake, hivyo basi wakati wowote ule anaweza kuondoa au kusimamisha mfumo huo wa mwanzo, na kisha akatekeleza tendo fulani linalokinzana na desturi za kawaida za maumbile yake. Hivyo basi, Miujiza ni moja wapo ya matendo yake yanayotokea kinyume na mfumo wake wa awali. [46] 3. Mtazamo wa Wanafalsafa: Kwa mujibu wa maoni yanayohusishwa na wanafalsafa kupitia maelezo ya Murtadha Motahhari, ni kwamba; Wanafalsafa waaamini kuwa, ulimwenguni humu kuna kanuni msingi katika mfumo wa maumbile zisizovunjika, ambazo kamwe haziwezi kukiukwa. Kanuni ambazo daima huwa zinafuata msingi wa usababishi (causality) na matokeo, pamoja na kanuni ya uwiano wa kimaumbile kati ya sababu na matokeo yake (visababishwaji). Kwa mtazamo huu, muujiza hauchukuliwi kama ni uvunjaji wa kanuni asilia za mfumo wa maumbile. [47] Motahhari, akikubaliana na mtazamo huu, [48] anafafanua akisema kwamba; muujiza si jambo lilalofuta wala kubatilisha mfumo au kanuni yoyote ile ya kimaumbile. Badala yake, ni utekelezaji wa sheria moja ya maumbile katika kuitawala sheria nyingine kwa namna fulani. [49] Aina za Miujiza Miujiza imegawanywa katika makundi mbalimbali kulingana na vipengele tofauti vilivyomo ndani yake. [50] Khaaje Nasir al-Din Tusi, katika Sharh al-Isharat wa al-Tanbihat, amefafanua miujiza katika aina mbili kuu: miujiza ya kimatamshi (qauli, قولی) na miujiza ya kimatendo (fi'li, فعلی). Kwa mujibu wake, miujiza ya kimatamshi au miujiza ya maneno, unahusika au huwa ni muwafaka zaidi kwa watu wenye elimu ya hali ya juu na maarifa ya kina (khawas ahl al-ma'rifa, خواص اهل معرفت), wakati miujiza ya kimatendo huwalenga zaidi watu wa kawaida ('awam, عوام). [51] Kwa maoni yake; Qur’ani Tukufu ilikuwa muujiza wa maneno aliouja nao Mtume Muhammad (s.a.w.w). [52] Hata hivyo, kuna miujiza kadhaa ya kimatendo imeripotiwa kuhusiana naye. [53] Kwa mujibu wa maelezo ya Abdullah Jawadi Amuli, bana Mtume (s.a.w.w) alikuwa akitumia miujiza ya kimatendo kwa ajili ya kuwaridhisha na kuwathibitishia utume wake watu wa kawaida, huku wasomi na wafuasi wake wakitosheka na Qur’ani Tukufu ambao ni muujiza wake wa kimatamshi, bila ya wao kudai miujiza ya kimatendo kutoka kwake (s.a.w.w). [54]

Mgawanyo Mwengine wa Miujiza: Miujiza ya Kihisia na Kiakili Wanazuoni wengine wameigawanya miujiza katika makundi mawili makuu: miujiza ya kihisia (hissi, حسی) na miujiza ya kiakili (‘aqli, عقلی). [55] 1. Miujiza ya Kihisia Aina hii ya miujiza hutambulika kupitia hisia tano alizonzo binadamu. Mifano ya miujiza hii ni: o Kufufua wafu. o Kuponya magonjwa sugu yasiopenyeka, kama vile upofu. o Kubadilika kwa fimbo kuwa nyoka. Miujiza hii inawalenga zaidi watu wa kawaida ambao hawana kiwango cha juu cha ufahamu na wanaohitaji kuona ishara za kushangaza ili waamini. 2. Miujiza ya Kiakili Aina hii ya miujiza hutambulika kupitia akili na hoja za kimantiki. Mifano wake ni: o Ufasaha na ukomavu wa lugha ya Qur’ani unaopindukia akili za wanadamu. o Kutoa habari za ghaibu. Jalal al-Din Suyuti (aliyefariki 911 Hijria), ambaye ni mfasiri na mwanafiqhi wa Kiash'ari, katika kitabu chake Al-Itqan fi Ulum al-Quran, akielezea mgawanyo huu anasema kwamba; miujiza ya Manabii wa Wana wa Israeli ilikuwa imejikita zaidi kwenye matukio ya kihisia. Hii ni kutokana na kutokamilika kwa ufahamu wa watu wao, kwani watu hao walikuwa ni wachanga mno kifikra, kiasi ya kwamba kila jambo walitaka kulishuhudia kupitia hisia zao za kimwili. Kinyume chake, miujiza ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) ilikuwa ni ya kiakili zaidi, kwani umma wake ulikuwa umefikia ukomavu maalumu wa kiakili unaowezesha kutambua ukweli wa ujumbe wake kwa njia ya tafakuri na uchambuzi wa kiakili. [56] Sheikh Hurru al-Amili, mwanahadhithi na mwanafiqhi wa Kishia, ameigawa miujiza katika aina tatu: [57] 1. Utoaji Habari za Ghaibu, amabo mifano yake ni: o Kutabiri matukio ya baadae. o Kutoa habari za mambo ya zamani ambayo hayakujulikana na mtu yeyote. o Kujua nia na mawazo ya watu. 2. Kujibiwa kwa Dua ambao mifano yake ni: o Dua ya Nabii au Imamu inayojibiwa, na kusababisha utokeaji wa maajabu kama ni matokeo ya dua hizo. 3. Utendaji wa Matendo ya Ajabu Yasiyodirikiwa na Ufahamu wa Binadamu, mfano wake ni: o Matendo ambayo hayawezi kufasirika, kwa kutokana na kwamba matokeo hayo hutokea kinyume na matukio ya kawaida yanayofuata kanuni za kawaida za kimaumbile, kama vile kuponya wagonjwa au kufufua wafu. [58] Ushahidi wa Miujiza Makala Kuu: Ushahidi wa Miujiza Baadhi ya watu wamekuwa wakichukulia matukio maalumu mbali mbali, yakiwemo matukio ya kimiujiza pamoja na kukubaliwa kwa maombi, kuwa ni ushahidi wa kuwepo kwa Mwenye Ezi Mungu. [59] Inadaiwa kwamba; falsafa na theolojia ya Kimagharibi, inayahisabu matokeo kama hayo ya kimiujiza, kuwa ni moja wapo ushahidi wa kuwepo kwa Mungu. Falsafa na theolojia ya Kimagharibi, imeyaweka matukio hayo ya kimiujuza sambamba na hoja nyengine zinazotumika kuthibitisha uwepo wa Mwenye Ezi Mungu. [60] Hata Muhammad Mahdi Naraqi katika kitabu chake kiitwacho Anis al-Muwahhidin, naye pia ametumia ushahidi huu kama ni moja ya hoja za kuthibitisha uwepo wa Mwenye Ezi Mungu. [61] Kulingana na moja ya nukuu, Naraqi anasema kwamba; miujiza na mambo ya ajabu yaliojiri kupitia manabii na waja wema, hayawezi kuwa ni matukio yanayowezekana kutendwa na binadamu. Hivyo basi, ni lazima kuwepo na mtendaji mwenye hekima ambaye utokeaji wa mambo haya unatokana na uwezo na hekima zake kamilifu. [62] Miujiza ya Manabii Katika Qur'an Kulingana na Qur'an, maisha ya baadhi ya manabii yaliambatana na miujiza pamoja na matendo mbali mbali ya ajabu. Baadhi ya miujiza hiyo ni kama ifuatavyo:

Kupoa kwa moto kwa Ajili ya Nabii Ibrahim: Kulingana na Aya ya 69 ya Suratu Al-Anbiya na Aya ya 24 ya Suratu Al-Ankabut, pamoja na kufufua ndege waliokatwa vipande vipande, waliotajwa katika Aya ya 260 ya Suratu Al-Baqara, ni miongoni mwa miujiza na matukio ya ajabu yalioambatana na maisha ya Nabii Ibrahim (a.s). [63] 

Miujiza Tisa ya Nabii Musa (a.s): Kulingana na Aya isemayo;

“وَلَقَدْ آتَیْنَا مُوسَیٰ تِسْعَ آیَاتٍ بَیِّنَاتٍ” "Na hakika tulimpa Musa ishara tisa zilizo wazi", ni kwamba; Mwenye Ezi Mungu alimpa Nabii Musa miujiza tisa ya wazi kabisa. [64] Baadhi ya miujiza hii na miujiza mingine iliyoripotiwa katika Qur'an kuhusu Nabii Musa ni: Fimbo kugeuka nyoka, [65] mkono wake kuwa mweupe, [66] upepo mkali wa dhoruba, mvua ya nzige na damu, njaa na upungufu wa matunda, [67] kupasuka kwa bahari na kuvuka kwa Wana wa Israel kupitia mpasuko huo, [68] kuibuka kwa chemchemi kumi na mbili, [69] kufufuka kwa aliyeuawa miongoni mwa Wana wa Israel, [70] mawingu yaliodhamini kivuli kwa ajili ya Wana wa Israel, [71] na kuinuliwa kwa Mlima Tur kama ni tishio juu ya Wana wa Israel. [72] 

Miujiza ya Nabii Isa: Miongoni mwa miujiza ya Nabii Isa iliyotajwa katika Aya ya 49 ya Suratu Al-Imran, ni pamoja na; kufufua wafu, kuponya vipofu na viziwi na wenye ukoma tangu kuzaliwa kwao, kutoa habari za mambo ya ghaibu pamoja na kuingiza uhai katika vijisanamu vyenye maumbile ya ndege. [73] Qur'ani Kama Muujiza wa Nabii Muhammad (s.a.w.w): Qur'an imekuwa ikichukuliwa kama muujiza muhumi na wa milele wa Nabii Muhammad (s.a.w.w). [74] Baadhi wameichukulia muujiza huu kama ni muujiza pekee wa Nabii Muhammad (s.a.w.w). [75] Hata hivyo, wasomi wengi, [76] wakitegemea Aya ya 1 hadi 5 za Suratu Al-Qamar, wamelihisabu tukio la kupasuliwa kwa mwezi kwa Nabii Muhammad (s.a.w.w), kuwa ni miongoni mwa miujiza yake maalumu (s.a.w.w). [77] Murtadha Mutahhari ameutalija tukio la safari ya mi'raji ya Nabii Muhammada (s.a.w.w) kama muujiza na tendo la ajabu la Nabii Muhammad (s.a.w.w). [78]

Tofauti za Miujiza ya Manabii Mbali Mbali Watafiti wengi wanaamini kwamba tofauti za miujiza ya manabii zinatokana na nyakati, mazingira, na mahitaji ya kijamii na kiutamaduni ya watu waliokuwa wakiishi katika zama hizo. Na kwamba Mwenye Ezi Mungu alichagua muujiza kulingana na ujuzi na mwelekeo wa watu wa wakati husika ili kuthibitisha ukweli wa ujumbe wa Kiungu na kuwahamasisha watu kuamini ya kwamba; miujiza inatokana na uwezo wa Mwenye ezi Mungu mwenyewe. [79] Katika Tarikh al-Ya'qubi (kitabu cha historia cha Ya'qubi), kuna Riwaya fulani iliyonukuliwa kutoka kwa Imamu Sadiq (a.s) inayosema kwamba; Mwenye Ezi Mungu hakutuma nabii yeyote yule, isipokuwa kwa kuzingatia kile kilichokuwa maarufu zaidi ndani ya jamii za watu wa zama hizo. 1. Zama za Uchawi - Nabii Musa (a.s): Wakati wa Nabii Musa, uchawi ulikuwa umeshamiri mno, na ulionekana kuwa ndio njia maalumu ya kuthibitisha mamlaka au uwezo wa kipekee. Kwa hivyo, Mwenye Ezi Mungu naye aliamua kumpa Nabii Musa miujiza yenye uwezo wa kuharibu uchawi wa watu wake, ikiwemo: • Fimbo kugeuka nyoka. • Mkono mweupe wenye nuru. • Kupasua bahari kwa fimbo yake. 2. Uhunzi Katika Zama za Nabii Daudi (a.s): Wakati wa zama za Nabii Daudi, uhunzi na uundaji wa zana mbali mbali, ulikuwa ndiyo kazi maarufu ilioenea ndani ya jamii ya yake. Hivyo Mwenye Ezi Mungu alimjaalia Nabii Daudi uwezo wa kipekee kabisa wa kulainisha vyuma kwa mikono yake bila kutumia moto, akionyesha uwezo wa Kiungu wa hali ya juu aliokuwa nao. 3. Zama za Ujenzi na Talasimu za Nabii Suleiman (a.s): Wakati wa Nabii Suleiman, ujuzi wa ujenzi, na matumizi ya talasimu (uchawi na urogaji), ilikuwa ndiyo mambo ya ajabu yaliokuwa umetawala katika zama hizo. Mwenye Ezi Mungu naye alimua kumpa Nabii Suleiman mamlaka ya kuendesha upepo, kutawala majini, na viumbe wa ajabu, nao ulikuwa ni uwezo wa kipekee uliokuwa ukiashiria uwezo wa Kiungu kutoka kwa Mola wake. 4. Zama za Tiba za Nabii Isa (a.s): Katika zama za Nabii Isa (a.s), kazi ya tiba na masuala yanayohuisana na afya, yalikuwa yameshamiri mno ndani ya jamii ya wakati huo. Ili Mwenye Ezi Mungu kuthibitisha ujumbe wake, alimua kumpa Nabii wake huyu miujiza maalumu inayohusiana na afya, kama vile: • Kufufua wafu. • Kuponya vipofu wenye upofu wa kuzaliwa nao. • Kuponya wenye ukoma na magonjwa mengine yaliyokuwa hayana tiba. 5. Zama za Ushairi na Tungo za Fasaha za Nabii Muhammad (s.a.w.w): Wakati wa zama za Mtume Muhammad, ujuzi wa ufasaha wa lugha, mashairi, na tungo za fasihi, ndiyo mambo maarufu yaliokuwa wakisifika nayo Waarabu wa zama hizo. Hivyo basi Mwenye Ezi Mungu alimpa Mtume wake Qur'an yenye miujiza mikubwa ya kilugha, na yenye ufasaha wa hali ya juu kabisa, ilioshinda uwezo wa washairi na wanafasihi wa wakati huo. [80]

Miujiza ya Maimamu Ma'asumu (a.s) Katika vyanzo vya Hadithi za Kishia, kuna matendo kadhaa ya ajabu yanayo husishwa na Maimamu Ma'asumu (a.s), huku baadhi ya wanazuoni wakizichukulia Hadithi hizo kuwa ni Hadithi mutawatir (zilizopokelewa na idadi kubwa ya wapokezi kupitia njia tofauti). Sheikh Hurr al-Amili, amekusanya baadhi ya miujiza hii ndani kitabu chake Ithbat al-Hudat bi'l-Nusus wa'l-Mu'jizat, na kuichukulia kama ni ushahidi wa kuthibitisha uimamu wa Maimamu (a.s). [82] Seyyed Hashim Bahrami pia naye, amekusanya takriban miujiza 2066 katika kitabu chake kiitwacho Madinat Mu'ajiz al-A'immat al-Ithna Ashar, alizoziorodhesha kwenye malngo aliouita; Babu 12, ambao ni mlango maalumu unaohusiana na Maimamu Ma'asumu (a.s). [83] Hurr al-Amili naye amechukulia ujuzi na taarifa zao za ghaibu, kuwa ni miongoni mwa miujiza na karama zao (a.s). [84] Baadhi ya wanazuoni wa Kishia kuhusiana na miujiza, wamesema kwamba: Miujiza ni jambo la ajabu ambalo hutendeka kwa neema na idhini maalum ya Mwenye Ezi Mungu, kwa lengo la kuthibitisha nafasi maalumu ya Kiungu, ikiwemo unabii na uimamu. [85] Pia, kulingana na moja ya Riwaya iliyonukuliwa kutoka kwa Imamu Sadiq (a.s) katika kitabu Ilal al-Sharai', ni kwamba; Mwenye Ezi Mungu aliwapa manabii na wathibitishaji wa dini yake, muujiza maalumu ili kuthibitisha, ukweli wa nafasi ya Kiungu wanayodai kuwa nayo. [86] Na kwa msingi huo, matendo ya ajabu ambayo yametokea kwa upande wa Maimamu Ma'asumu (a.s), yalikuwa ni kwa ajili ya kuthibitisha uimamu wao, na yanachukuliwa kuwa ni miujiza maalumu kuhusiana nao. [87] Kwa mfano, ushuhuda wa kushuhudia kwa Hajar al-Aswad juu uimamu wa Imam Sajjadu (a.s) unahisabiwa kuwa ni moja ya miujiza yake, na ushahidi wa kuthibitisha uimamu wake (a.s). [88] Kulingana na moja ya Riwaya kutoka katika kitabu kiitwacho Dalail al-Imamah, Muhammad bin Hanafiyyah alizozana na Imamu Sajjad (a.s) kuhusina na suala la uimamu. Hivyo Imamu Sajjad (a.s) alizungumza naye kwa nia ya kumthibitishia uhlali wa nafasi yake ya uimamu; lakini yeye hakukubali. Mwishowe, wote wawili waliamua kulifanya jiwe la Hajar al-Aswad kuwa ni hakimu baina yao. Katika hali hiyo, kwa idhini ya Mungu, Hajar al-Aswad lilishuhudia na kuthibitisha uimamu wa Imamu Sajjad (a.s). [89] Katika baadhi ya kazi za kiteolojia za Kishia, matendo kama vile kung'oa mlango wa Khaibar, kupigana na kundi la majini waliokuwa wakimsumbua Mtume (s.a.w.), kurejea kwa jua ( Radd al-Shams) na kadhalika, yameelezwa kama mifano ya miujiza ya Imam Ali (a.s.) na yanatumiwa kama ushahidi wa kuthibitisha uimamu wake. [90] Bibliografia Mijadala kuhusiana na miujiza inapatikana zaidi katika kazi andishi za kitheolojia na tafsiri; hata hivyo, baadhi ya wanazuoni na watafiti wa Kiislamu wameandika kazi za kipekee na makhususi kwa ajili mada hii. Baadhi ya kazi hizo hizo ni kama ifuatavyo: • Kitabu “Tanaqodh-nama ya Ghayb-nemun; Nigarishi Nu be-Mu'jize”. Amabcho ni kitabu kilichoandikwa kwa Kiajemi kwa maana ya (Kitendawili au Udhihirisho la Ghaibu; Mtazamo Mpya Juu ya Miujiza), kilichoandikwa na Muhammad Amin Ahmadi: Katika kitabu hichi, mwandishi amejadili suala la miujiza kwa kulinganisha falsafa ya Kiislamu na falsafa ya Kimagharibi, akiwasilisha na kuchambua mitazamo ya baadhi ya wanafalsafa wa Kiislamu na wa Kimagharibi. Mada muhimu zilizochambuliwa kitabuni humu ni kama vile; ufafanuzi wa miujiza, uwezekano wa kutokea kwa muujiza, na dhana pamoja na maana ya miujiza. [91] • Kitabu “Mu'jize Dar Qalamro Aql wa Din” (Miujiza Katika Nyanja za Akili na Dini), kilichoandikwa na Muhammad Hassan Qadridan Qaramaliki: Mwandishi wa kitabu hichi, amejadili masuala kadhaa kitabuni humu. Miongoni mwayo ni kama vile; ufafanuzi wa miujiza na aina zake, tofauti kati ya miujiza, uchawi na karama, uhusiano wake na kanuni ya kimaumbile ya usababishi (causality), uchunguzi juu ya tuhuma za wanaoukataa pamoja na majibu kwao, na kadhalika. • Kitabu “Marzha-ye E'jaz” (Mipaka ya Muujiza), ambacho ni tafsiri ya mada kuhusiana na miujiza ya Qur'an zilichopolewa kutoka katika kitabu Al-Bayan Fi Tafsir al-Qur'an, kilichoandikwa na Sayyid Abul Qasim Khui, na kuhaririwa na Ja'far Subhani. [92] • Kitabu “Mu'jize Bozorg” (Muujiza Mkuu), kazi iliyoandikwa na Muhammad Abu Zuhra (aliyefariki mwaka 1395 H), mtafiti wa Qur'ani na mwanahistoria Kimisri. Nacho ni kitabu kuhusiana na miujiza ya Qur'an, kilichoandikwa kwa lugha ya Kiarabu. Kitabu hichi kimetarjumiwa kwenda lugha ya Kiajemi na Mahmoud Zabiihi. [93] Makala Husika: • Irhaas • Karama