Nenda kwa yaliyomo

Bab al-Hawaij

Kutoka wikishia

Bab al-Hawaij (Kiarabu: باب الحوائج) ni mtu ambaye kwa kutawasali kwake (kuomba dua kupitia kwake) hupelekea dua hiyo kukubaliwa na hivyo aliyeomba kutimiziwa haja yake. Bab al-Hawaij ni miongoni mwa lakabu za Imamu Mussa al-Kadhim (a.s), Abbas (a.s) na Ali Asghar (a.s). Hii ni kutokana na kuwa, baadhi ya Waislamu wa madhehebu ya Shia wanaamini kwamba, kufanya tawasuli na kuomba dua kupitia kwa watu hawa watatu hupelekea kutekelezwa maombi na haja.

Bab al-Hawaj ni lakabu ya nani?

Bab al-Hawaij (mlango wa haja) katika utamaduni wa umma wa Mashia hutumiwa kwa Mussa bin Ja'afar (a.s) Imamu wa Saba wa Mashia, [1] Abbas bin Ali (a.s) mmoja wa mashahidi wa Tukio la Karbala [2] na Ali Asghar (mtoto mchanga wa Imamu Hussein (a.s) aliyeuawa shahidi katika tukio la Karbala. [3] Muhammad Ali Urdubadi (aliaga dunia 1380 Hijiria) amebainisha wazi katika kitabu chake cha Hayat Abil Fadhl al-Abbas juu ya kuwa mashuhuri lakabu hii kwa Abul Fadhl (a.s). Mujtaba Tehrani, Mujtahidi wa Kishia anaongezea kuwa, mbali na watu hawa watatu anamtaja Ruqayyah binti ya Imamu Hussein (a.s) kuwa naye ni Bab al-Hawaij (mlango wa haja). [5] Bab al-Hawaij maana yake ni mahali pa haja na mahitaji na anaashiria kiistiara sehemu ambayo hapo dua na haja hutizimizwa. [6]

Kwa nini Imamu Kadhim (a.s) alipewa lakabu ya Bab al-Hawaij

Matumizi ya lakabu ya Bab al-Hawaij kwa Imamu wa saba wa Mashia hakuna chimbuko la hadithi. Kwa mujibu wa Ibn Shahrashub (aliaga dunia 588) katika kitabu chake cha Manaqiq Aal bin Abi Talib, baada ya Imamu Kadhim kuzikwa katika makaburi ya Makureshhi Baghdad, mlango mkuu wa kuingilia ambao ulikuwa na jina la "Bab Tin" jina lake lilibadilishwa na kuwa "Bab al-Hawaij". [7] Kadhalika kwa mujibu wa Ib Hajar Haythami (aliaga duuna 974 Hijria), mmoja wa wanazuoni na Maulamaa wa Kisunni, Imamu Kadhim alikuwa maarufu baina ya Wairaqi kwa lakabu ya Bab Qadhaa al-Hawaij Indallah" (Mlango wa kutimiziwa haja mbele ya Mwenyezi Mungu. [8] Shablanji mmoja wa Maulamaa wa Kishafii pia ametambua sababu ya Imamu Mussa al-Kadhim kupewa lakabu ya "Bab al-Hawaij" kuwa ni kujibiwa maombi na kutekelezewa haja watu waliofanya tawasuli kwake. [9] Dairat al-Marif Tashayui imeandika, Masuni na Mashia wakiwa na lengo la kukubaliwa maombi na haja zao hufanya tawasuli kwake (huomba dua kupitia kwa mtukufu huyo) katika Haram ya Imamu Mussa al-Kadhim (a.s). [10]

Rejea

Vyanzo