Sura za Makka na Madina

Kutoka wikishia

Sura za Makka na Madina (Kiarabu: السور المكية والمدنية): Ni mada inarejelea mgawanyo wa Sura za Qur’ani kulingana na wakati wa kuteremshwa kwao, yaani kabla au baada ya kuhama kwa Mtume (s.a.w.w). Kujua Sura za Makka na Madina ni suala muhimu katika fani ya tafsiri, fiqhi na theolojia; Kwa sababu kwa njia hii tunaweza kujua hatua za wito na ulinganiaji wa bwana Mtume (s.a.w.w) pamoja na nyenendo za masuala ya kisiasa na kijamii yalivyokuwa mwanzoni mwa Uislamu. Kujua Aya zilizofuta na zilizofutwa, kutambua hatua za uwekwaji wa sheria za Kiislamu na namna ya ukamilikaji wake, na pia kujua sababu za kuteremshwa kwa Aya za Qur'ani, ni miongoni mwa faida nyingine za kuzijua Sura za Makka na Madina.

Watafiti wa Qur’ani wanasema kwamba; Katika baadhi ya Sura za Makka, kuna Aya za Madina na pia katika baadhi ya Sura za Madina, kuna Aya za Makka. Aya hizi zinaitwa Aya zilizokiukwa «Ayatu Istithnai» au kuvuliwa kutoka hukumu. Kulingana na maoni yao, ni kwamba; katika Qur'ani, kuna Sura 20 ambazo ni za Madina ambazo ndizo yakinifu kuwa ni za Madina, na Sura 82 ambazo ni yakinifu na zenye uhakika kwamba ni za Makka. Ila kuna khitilafu za maoni kuhusina na Sura zilizobaki katika Qur’ani, ambazo kiuhalisia ni idadi ya Sura 12.

Sura za Makka na Madina zinatafautiana kimtindo na namna ya mtiririko wake, na hii imehesabiwa kuwa ndio njia bora zaidi ya kuzitambua Sura za Makka na Madina. Baadhi ya sifa za Sura za Makka ni: mwito unaolingania juu misingi ya imani, ufupi wa Sura na Aya, na pia kuwa na lugha kali zenye makemeo. Baadhi ya sifa za Sura za Madina ni: kueleza hukumu za kisheria, kujadili masuala ya wanafiki na kuelezea masuala ya jihad na hukumu zake.

Kwa kuzingatia umuhimu uliopo katika kuzitambua Sura za Makka na Madina, jambo hili limekuwa ni lenye kuzingatiwa na kupewa kipau mbele na hata watafiti wa Kimashariki (Wazungu); lakini wao wamefuata njia tofauti na zile za watafiti wa Kiislamu.

Umuhimu wa Kujua Sura za Makka na Madina ya Sayansi na Taaluma za Kiislamu

Kujua Sura za Makka na Madina ni muhimu mno katika taaluma za Kiislamu, nalo ni jambo nyeti kwa; wafasiri katika kufasiri kwao Qur'ani, kwa mafaqihi katika kupata hukumu za kifiqhi [1], na kwa wanatheolojia katika kuthibitisha au kukataa masuala ya kitheolojia. [2] Hii ni kwa sababu kwamba; kubainisha iwapo Sura ni Makka au Madina, hutunawezesha kujua tarehe ya kutokea kwa matukio na wakati wa kupitishwa kwa hukumu fulani. [3] Imenukuliwa kutoka kwa baadhi ya wanafikra wa elimu ya Qur’ani kwamba; si halali wala haruhusiwi kufasiri Qur'ani yule ambaye hana na uwezo kutofautisha kati ya Sura za Makka na Madina, ambaye hajui namna ya kuzibagua kila mmoja kati yake. [4]

Muhammad Hussein Tabatabai, mwandishi wa Tafsir Al-Mizan, anaamini kwamba; Kule kuzijua Sura za Makka na Madina pamoja kujua mpangilio wa kuteremshwa kwa Sura za Qur’ani, kuna taathira muhimu katika tafiti zinayohusiana na wito wa bwana Mtume wa Muhammad (s.a.w.w), pamoja na kuelewa nyenendo au hatua za kiroho, kisiasa na kijamii katika wakati wake, pia ni jambo muhumu katika uchambuzi wa maisha ya kinabii. [5] Kujua iliyobatilishwa na kufutwa, [6] kujua sababu za kuteremshwa kwa Sura na Aya za Qur’ani, [7] kujua jinsi Qur’ani ilivyoteremshwa [8] na kujua madhumuni na makusudio ya Sura, ni miongoni mwa manufaa mengine ya kuijua Makka na za Madina. [9]

Vigezo na Misingi ya Utambuzi

Kuna maoni matatu kuhusiana na vigezo vya kutofautisha kati ya Aya za Makka na Madani ndani Qur'ani Tukufu, nayo ni kama ifuatavyo:

  1. Kigezo cha wakati (zama): Kwa mujibu wa kigezo hichi ni kwamba; Kilichoteremka kabla ya kuhama kwa bwana Mtume (s.a.w.w) kuelekea Madina, kinahisabiwa kuwa ni cha Makka (Makkiyyah), na kilichoteremshwa baada ya bwana Mtume (s.a.w.w) kuwasili Madina ni ni cha Madina (Madaniyyh). Kwa hiyo, ikiwa Sura au Aya iliteremshwa baada ya Hijrah (kuhama), hiyo itakuwa ni Madaniyyah; Hata kama iliteremshwa katika mji wa Makka au katika safari za bwana Mtume (s.a.w.w) katika maeneo mbali mbali, kama vile Aya zilizoteremshwa katika kipindi cha kukombolewa kwa mji Makka au katika Hijja ya kuaga (hijjatu al-Wada’a). [10]
  2. Vigezo vya kimaeneo: Kulingana na kigezo hichi ni kwamba; yale yote yaliyoremshwa Makka na maeneo yake, kama vile Mina, Arafat, na Hudaibia, ni ya Makka au Makkkiyyah, hata kama ilikuwa ni baada ya Hijra, na yaliyoteremshwa kwenye mji wa Madina na maeneo yake, kama vile Badri na Uhudi, ni ya Madana au Madaniyyah. [11]
  3. Kigezo cha hadhira (walengwa): Baadhi wanazuoni wamezingatia kigezo cha "Wahyi" na wakasema kwamba; Kila kilichoteremshwa kwa watu wa Makka ni cha Makka au Makkiyyah, na kilichoteremshwa kwa watu wa Madina ni cha Madina au Madaniyyah. [12] Kipimo cha kuelewa kigezo cha hadhira ni kwamba; kilichoteremshwa kwa usemi usemao:"Yaa ayyuha al-Naas یا ایها الناس" (Enyi watu) ni cha Makka na kilichoteremshwa kwa usemi usemao: "Ya ayyuha Al-lahina Amanu یا ایها الذین آمنو" (Enyi mlioamini), ni cha Madina au Madaniyyah. [13] Maoni haya yamenasibishwa kwa Ibnu Masoud, ambaye ni mmoja wa masahaba wa bwana Mtume (s.a.w.w). [14]

Imeelezwa ya kwamba; ikiwa baadhi ya Aya za Sura fulani ni za Makka na baadhi yake ni Madina, asili ya Makka au Madina ya Sura huamuliwa kwa kuzingatia sehemu kubwa zaidi ya Sura hiyo. Kwa mfano, ijapokuwa sehemu ya baadhi Aya za Surah An'am zinahisabiwa kuwa kuwa ni za Madina, lakini kwa kuzingatia kwamba Aya zake nyingi ziliteremshwa Makka, Sura hii inatambulishwa kuwa ni miongoni mwa Sura za Makka. [15] Kwa upande mwingine, wengine wanaamini kwamba majina ya Sura za Qura’ani yanatokana na Aya za mwanzo za Sura hizo. [16]

Nadharia Mashuhuri

Kigezo cha muda ni maarufu zaidi kuliko vigezo vingine viwili, na ndicho kilicho kubaliwa na watafiti wengi wa sayansi za Qur'ani. [17] Sababu yao ni kwamba; kigezo hichi ni tofauti na vigezo vingine viwili, nacho ni chenye kujumuisha Aya zote za Qur'ani; [18] Hata hivyo, kigezo cha kimahala si cha kina na hakiwezi kutumika kwa Aya zote; Kwa sababu baadhi ya Aya hazikuteremshwa Makka wala Madina; Bali zimeteremshwa katika sehemu za mbali kama kabisa, kama vile Tabuki na Baitul-Maqdis. [19] Kigezo cha hadhira nacho hakiwezi kukubalika, ukiachana na tatizo la kutokuwa na ufahamu wa kina, pia tatizo lake jengine ni kwamba; kuna baadhi ya Aya ambazo kiuyakinifu kabisa ni Aya za Madina, ila nazo pia huanza na usemi usemao "Ya ayyuha al-Naas «یا ایها الناس» na baadhi ya Aya ambazo kiuyakinifu ni Aya za Makka, ila huanza na usemi usemao: «یا ایها الذین آمنو»[20].

Aya Zilizuvuliwa Kutoka Katika Hukumu Kuu

Kuna baadhi ya Sura za Makka ambazo baadhi ya Aya zake ziliteremshwa Madina. Pia, katika baadhi ya Sura za Madani ambazo ndani yake kuna Aya zilizoteremshwa Makka. [21] Aya hizi zinaitwa Aya zilizokiukwa na kukaa nje ya hukumu kuu «Ayaatu Istithnaaiyyah». [22] Bila shaka, kuna baadhi ya wanazuoni wa sayansi za Qur'ani ambao hawakukubali juu ya kuwepo kwa aina kama hii ya kigao cha vigao vya Aya za Qur’ani, na wakasema kwamba hakuna aina kama hii ya Aya katika Sura yoyote ile katika Qur’ni; Hii ina maana kwamba Aya zote za Sura za Qur’ani ima hua ni za Makka (Makkiyyah) au Madina (Madaniyyah). [23]

Idadi ya Sura za Makka na Madina

Idadi ya Sura za Madinai ni 20 na idadi ya Sura za Makka ni Sura 82. Pia kuna tofauti ya maoni kuhusu Sura 12 zilizoko ndani ya Qur’ani. [24] Sura za Madina zinazokubaliwa na wote ni: Baqarah, Aal-Imran, Nisa, Maidah, Anfal, Tawba, Noor, Ahzab, Muhammad, Fat-h, Hujurat, Hadid, Mujadalah, Hashr, Mumtahina, Juma’a, Minafiqina, Talaq, Tahrim na Nasr. [25] Sura zinazobishaniwa au zenye khitilafu ni: Fatiha, Ra’ad, Rahman, Saf, Taghabun, Mutafifin, Qadr, Bayyinah, Zilzaal, Ikhlas, Falaq na Nas. [26] Sura zote zilizo bakia ni Sura za Makka. [27]

Kwa kawada kwenye Qur’ani zinazochapishwa duniani huwa ni jambo la kawada kuainishwa Sura za Makka na za Madina kila mwanzoni mwa Sura hizo. Ukirejea kwenye Qur’ani hizo utakuta kuna idadi ya Sura 28 za Madina na Sura 86 za Makka. [28]

Njia za Tambulishi

Kuna njia tatu zinazotumika katika kuzielewa Sura za Makka na Madina: 1. Kupitia Vielelezo vya Hadithi 2. Kupitia Ushahidi wa Muonekano Dhahiri wa Aya Zake 3. Ishara za Muktadha wa Aya na Wakiroho Zilizomo Ndani Yake. [29] Kuhusiana vielelezo vyaHadith, imeelezwa kwamba, mara nyingi kigezo hichi huwa kinakabiliwa na matatizo kadhaa ndani yake, kama vile; udhaifu wa mlolongo wa wapokezi wa Hadithi, kutosimuliwa Hadithi hizo Maasumina (Watoharifu au Maasumina 14), na kikwazo cha kuwepo kwa Hadith zinazokinzana. Ndio maana utumiaji wa kigezo hichi ukawa unategemea tu zile Hadithi zenye ushahidi sahihi. [30] Kwa mujibu wa baadhi ya wanazuoni wa Qur'ani, muktadha wa Aya, yaliyomo ndani yake na vyanzo vya nje ambavyo ni vielelezo ongozi na saidiza katika kuiarifu Sura fulani, ndiyo njia pekee, [31] au kwa mujibu wa itikadi baadhi yao ndiyo njia bora zaidi, ndiyo njia bora zaidi [32] ya kubainisha kama Sura za Makka au Madina.

Kwa kuwa Makka na Madina zilikuwa na mazingira mawili tofauti kabisa, kama vile makafiri walio wengi huko Makka na kuanzishwa kwa serikali ya kidini huko Madina, [33] hili limepelekea Sura za Makka na Madani kuwa na sifa tofauti za kiibara na kimaudhui yake. [34] Hata hivyo, emeelezwa ya kwamba; sifa hizi si sifa yakinifu, kwani sifa hizi hazijumuishi Aya zote za Sura nzima, bili huptikana kwenye baadha ya Ayat u, kwa hiyo ni sifa zinazo imarisha tu uwezekano wa Sura kupewa sifa ya Makkiyyah au Madaniyyah. [35] Yaweza pia kukawa na Sura ya Makkah au Madina, ila baadhi ya Aya zake zikawa ni Aya za kipekee zisizo na sifa za Makkiyyah wala Madaniyyah. [36]

Sifa za Sura na Aya za Makka (Makkiyyah)

Sifa za Sura na Aya za Makkiyyah zimeelezwa kama ifuatavyo:

  • Kulingania kanuni za imani, kama vile kumwamini Mwenye Ezi Mungu na kuamini Siku ya Kiyama; [37]
  • Ufupi wa Aya na Sura. [38]
  • Kusimulia visa vya Manabii na nyuma zilizopita. [39]
  • Kusimulia visa vya manabii na umma zilizopita. [39]
  • Kuwa na lugha kali. [40]
  • Matumizi ya neno Kallaa (کَلّٰا) katika Sura. [41]
  • Kuwa na Aya za sijda. [42]
  • Kuanzia kwa herufi zilizokatwa kama vile Alif Laam Miim (الم), Alif Laam Raa (الر), Taa Siin Miim (طسم), na Haa Mii (حم) (isipokuwa Surat Al-Baqarah na Al-Imran). [43]
  • Lugha ya mashambulio na makaripio dhidi ya ibada ya sanamu. [44]

Sifa za Sura na Aya za Madina (Madaniyyah)

Sifa zilizotajwa kuhusiana na Sura na Aya za Madina ni kama ifuatavyo:

  • Kueleza faradhi na mipaka ya dini. [45]
  • Urefu wa Aya na Sura zake. [46]
  • Kueleza sheria za kiuchumi na kisiasa. [47]
  • Kutumia lugha laini na ya upole kwa waumini. [48]
  • Kushughulikia masuala yanayohusiana na wanafiki [49]
  • Kueleza hali na matendo ya wanafiki na msimamo wa Waislamu na Mtume (s.a.w.) dhidi yao [50]
  • Kubishana na Watu wa Kitabu [51]
  • Kueleza suala la Jihad na hukumu zake. [52]

Mtazamo wa Wataalamu wa Mashariki (Orientalists)

Kuanzia katikati ya karne ya 13 ya mwandamo, wataalamu wa mambo ya Mashariki (Orientalists) kama vile; Nöldeke na Régis Blachère walianza kujishughulisha na uchunguzi wa tarehe za ufunuo wa Qur’ani. [53] Baadhi yao walizigawanya Surh za Qur'ani kwa mujibu wa wakati wa kuteremshwa kwake, lakini sio katika aina mbili za Makka na Madina tu, bali walizigawa katika aina tatu, nne au tano. [54] Ila watafiti hawa wote kwa pamoja waliziweka Sura za Madina (Madaniyyah) katika kundi moja. [55]

Wanafikra Baadhi ya wataalamu wa Mashariki na wanafikra [56] kama vile; Taha Hussein, wakizingatia tofauti khitilafu za kidhahiri na za kimaudhui kati ya Sura za Makkiyyah na Madaniyyah, wamehitimisha maoni yao na kuibuka na natija ya kwamba; Qur’ani ni kazi ya mwanadamu na si kutoka kwa Mwenye Ezi Mungu; kwani mfumo wa Qur’ani wa Sura za Makka na Madina uliathiriwa na hali ya mazingira ya wakati ya maeneo hayo, ilhali kama ingelikuwa ni kutoka kwa Mwenye Ezi Mungu, isingekuwa ikifuata mazingira hayo. [57]

Muhammad Hadi Ma'rifat, mwandishi wa kitabu cha At-Tamhid, katika kujibu pingamizi hii anasema kwamba; Inapaswa kutofautisha kati ya kufuata mazingira na kwenda sambamba nayo kwa ajili ya kuwa na athari kubwa zaidi. Pingamizi hii inaweza tu kujadiliwa ikiwa tofauti za sifa kati ya Sura za Makka na Madina zinatokana na kufuata mazingira yao. Ila kiuhalisia ni kwamba; Qur’ani iliteremshwa sambamba na mazingira halisi yalio kuwepo kwenye miji ya Makkah na Madina, ili iweze kuwa na athari kubwa zaidi kwa watu wa maeneo hayo. [58]

Rejea

Vyanzo