Wake za Mtume (s.a.w.w)

Kutoka wikishia

Wake za Mtume (s.a.w.w) ni wanawake aliowaoa Mtume na wametajwa ndani ya Qur'an kwa majina ya Umahat al-Muuminina (mama wa waumini) na kuna kanuni na amri maalum juu yao.

Wanachuoni wa Kiislamu wametofautiana kuhusu idadi ya wake za Mtume (s.a.w.w). Wengine wameorodhesha wake zake kuwa ni 13 na wengine wamesema ni 15. Aidha kuna maoni mengine katika suala hili. Asili ya tofauti hii inarejea kwenye kuhesabiwa na kutohesabiwa kwa makanizi (binti au mwanamke asiyekuwa Mwislamu aliyekuwa akikamatwa mateka katika vita vya Waislamu na makafiri) katika idadi ya wake za Mtume. Ndoa za Mtume (s.a.w.w.) ziliwiana na ujumbe wake (kueneza dini ya Kiislamu) na zilifanywa kwa nia kama vile kupata uungaji mkono wa makabila na koo kubwa za Waarabu, kufuta fikra potofu za kijahilia, kuinua na kuimarisha nafasi ya kijamii ya wanawake waliodhuriwa na kuwafariji, pamoja na kuwaachilia huru mateka.

Kuishi maisha ya kawaida kabisa (yasiyo na mambo ya fahari), kujiepusha na majishauwo na kusema mema ni miongoni mwa maamrisho ya Mwenyezi Mungu kwa wake za Mtume. Waislamu pia wameamrishwa kuzungumza na wake za Mtume nyuma ya pazia na wasiwaoe baada ya kufa Mtume (s.a.w.w). Waislamu wanaamini juu ya usafi na utakasifu wa wake za Mtume na hawaoni kama inajuzu kuwatukana. Hata hivyo, wanakosoa utendaji wa Aisha katika matukio ya baada ya kifo cha Mtume (s.a.w.w), kama vile Vita vya Jamal.

Nafasi

Wake za Mtume (s.a.w.w.) ni wanawake walioolewa na Mtume wa Uislamu, na kwa mujibu wa Aya hii:

«وَأَزْوَاجُهُ أُمَّهَاتُهُمْ؛ yaani "na wake zakke ni mama zao" [1] wamepewa lakabu ya Ummu al-Mu'mini (Mama wa Waumini). [2] Ndani ya Qur'an, kuna kanuni na amri maalum juu yao. [3]

Kuharamishwa kuwavunjia heshima wake za Mtume (s.a.w.w)

Waislamu wote wanaamini usafi, staha na heshima kwa wake za Mtume. Hata hivyo, baadhi ya Mawahabi wananawasingizia Mashia kwamba wanawavunjia heshima wake za Mtume. Pamoja na hayo wanachuoni wa Kishia na baadhi ya Masunni wanakosoa mienendo ya baadhi ya wake za Mtume katika matukio ya baada ya kifo cha Mtume (s.a.w.w), kama vile nafasi ya Aisha katika kutokea Vita vya Jamal na uadui wake dhidi ya Imamu Ali (s.a.w.w) [4], lakini hawajamsukumia tuhuma ya uchafu na isiyofaa mke yeyoye yule kati ya wake za Mtume na hawaoni kama inajuzu kuwatukana na kuwavunjia heshima. [5]

Kwa mfano, Seyed Murtadha, mwanateolojia wa Kishia wa karne ya tano Hijria, anachukulia kuingia wake za Manabii katika uchafu kunakinzana na Umaasumu wa Manabii; kwa sababu kwa mujibu wa imani ya Shia Imamiyyah, Mitume wameepukana na kila kitu ambacho kinawafanya watu wawachukie na kujiweka mbali nao. [6] Sheikh Tusi pia amesema katika Tafsir al-Tibyan kwamba hakuna hata mke mmoja wa Mitume ambaye alikuwa mchafu (kimaadili) kwani hilo lingewafanya watu kumkimbia Mtume na pia ni chanzo cha doa, aibu na fedheha kwake, na bila ya shaka yeyote anayesema maneno hayo yasiyo ya kitaalamu na kumkashifu ametenda kosa kubwa. [7] Hii ni katika hali ambayo, baadhi ya wanazuoni wa Kisuni wamezungumzia uwezekano wa kufanya uchafu wa kimaadili (kama kuzini) baadhi ya wake za Mtume na kutokea kwake pia. [8] Ayatullah Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, alitoa fatwa ya kuharamisha kutukana na kuvunjia heshima matukufu ya Masunni na alama za Masunni na wake za Mtume wa Uislamu (s.a.w.w) [9]. Fat'wa ya Ayatullah Khamenei inasema: "Kuzivunjia heshima nembo za ndugu zetu wa Ahlu Sunnah ikiwemo kumzushia tuhuma mke wa Mtume (bibi Aisha) ni haramu. Suala hili linajumuisha wake wa Mitume wote hususan Bwana wa Manabii, Mtume mtukufu Muhammad (saww)."

Idadi ya wake za Mtume (s.a.w.w)

Kuna tofauti ya maoni kuhusu idadi ya wake za Mtume: Kwa mujibu wa Ibn Hisham katika Al-Sirat al-Nabiyyah, idadi ya wake za Mtume ilikuwa kumi na tatu: [10] Khadijah, Saudah, Aisha, Zainab bint Khuzaymah, Hafsa binti ya Omar, Ummu Salama, Zainab binti wa Jahsh, Juwairiyah, Umm Habiba, Safiya, Maimuna, Umrah bin Yazid Kilabi na Asma binti Nu'man al-Kindi. [11] Wakati Mtume alipofariki, ukiwaondoa Khadijah na Zainab binti Khuzayma, wake zake wengine walikuwa hai. [12]

Katika riwaya iliyopokewa kutoka kwa Imamu Sadiq (a.s), idadi ya wake za Mtume imetajwa kuwa ni kumi na tano. [13] Ali bin Hussein Masoudi na Shamsuddin Dhahabi pia wamewachukulia wake za Mtume kuwa ni kumi na watano. Katika baadhi ya riwaya, idadi yao inafikia wake 18. [15] Hata hivyo, Mtume Muhammad (s.a.w.w) alikuwa na mke mmoja tu kwa muda wa miaka 25 katika kipindi ambacho mkewe Bi Khadija alikuwa hai, na baada ya kifo cha Khadija na kuhamia Madina, alioa wake wengine. [16]

Imesemekana kuwa sababu ya kutofautiana kwa idadi ya wake za Mtume (s.a.w.w.) ni kwamba baadhi ya wanahistoria wamejumuisha na wake za Mtume wanawake ambao kimsingi hawakuishi na Mtume (s.a.w.w) na wala hawakuwa makanizi wake. [17] Katika vyanzo vya historia kumetajwa majina ya baadhi ya yao kama, Maria Qibtiyah na Reyhanah, binti ya Zayd [18] Reyhanah, binti ya Zayd bin Amr alitokana na kabila la Bani Nadhir na alikuwa mwanamke wa Kiyahudi ambaye alichukuliwa matekwa na kusilimu katika mwaka wa sita Hijria. Mtume (s.a.w.w) alimkomboa na akamuoa [19].

Watoto

Makala ya asili: Watoto wa Mtume (s.a.w.w)

Katika ya wake za Mtume (s.a.w.w), ni Bibi Khadija na Maria al-Qibtiyah tu ndio waliozaa na Mtume (s.a.w.w). [19] Maria al-Qibtiya alimzaa Ibrahim. [21] Kwa upande wa Bibi Khadija liililo mashuhuri ni kwamba, watoto ambao alizaa na Bwana Mtume (s.a.w.w) ni mabinti wanne ambao ni: Fatima (a.s) Zaynab, Ummu Kulthum na Ruqayyah na watoto wawili wa kiume ambao ni: Abdallah na Qassim. [22} Hata hivyo baadhi ya wahakiki wa Kishia wanaamini kwamba, Zaynab, Ummu Kulthum na Ruqayyah hawakuwa mabinti wa Mtume (s.a.w.w) na Khadija. Bali ni mabinti wa dada yake Khadija waliokulia katika nyumba yake. [23]

Falsafa ya Mtume kuoa wake wengi

Katika zama za Mtume (s.a.w.w) kuoa wake wengi lilikuwa jambo la kawaida na lililokuwa limezieleka na kuenea katika jamii ya wakati huo; [24] pamoja na hayo watu wote wamesema kuwa, Mtume alioa wake wengine kutokana na sababu mbalimbali na katika kutekeleza jukumu la Mwenyezi Mungu la kuhubiri dini ya Uislamu. [25] Baadhi ya hoja na sababu zinazotolewa za Mtume kuoa wake wengi ni:

1. Kuvutia uungaji mkono wa makabila na koo kubwa za Waarabu na kuimarisha ushawishi wao wa kisiasa na kijamii kupitia kiunganishi cha sababu nao; kama kumuoa kwake Aisha.

2. Kutekeleza amri ya Mwenyezi Mungu na kuondoa fikra potofu za kijahili, kama vile kumuoa Zaynab bint Jahsh. Zaynab alikuwa, mke wa Zayd bin Haritha ambaye, alikuwa mtoto wa kupanga (kuasili) wa Mtume, na kwa mujibu wa ada ya zama za kijahilia Waarabu walimchukulia mtoto wa kuasili kama mtoto halisi. Kwa hiyo, baada ya kifo cha mtoto aliyeasiliwa au talaka, hawakuoa mke wake.

3. Kuimarisha nafasi ya kijamii ya wanawake waliodhurika, kama vile wajane na mateka (wengi wa wake za Mtume walikuwa wajane).

4. Kuwafariji wanawake kwa sababu ya madhara waliyoyapata kwa sababu ya kuukubali Uislamu; kama kumuoa Umm Habiba.

5. Kulinda na kudhamini maisha ya wajane masikini (wake wa mashahidi) na mayatima, kama vile kumuoa kwake Umm Salama na Zaynab bint Khuzaymah.

6. Kuonyesha adhama na nguvu ya Uislamu na Waislamu, kama hatua yake ya kumuoa Safiya.

7. Kuwalinda wanawake dhidi ya hatari za uhai, kama ndoa yake na Sauda.

8. Kuwafanya huru mateka na watumwa, kama hatua yake ya kumuoa Juwayriyah bint Harith. [26] Pamoja na hayo baadhi ya waandishi wameichukulia hatua ya Mtume ya kuoa wake wengi kuwa ni matokeo ya hawaa na matamanio ya nafsi. Allama Tabataba'i amewajibu wenye mtazamo huo kwamba: Sira ya Mtume inathibitisha kinyume chake; kwa sababu Mtume aliishi na bibi Khadija tu katika kipindi cha miaka ishirini ya maisha yake (karibu theluthi moja ya umri wake) na mwisho wa maisha yake ndipo alioa wanawake wengine. [27] Pia, kama ndoa za Mtume ziliegemezwa kwenye matakwa na matamanio basi, angeoa wanawake mabinti na wadogo kiumri badala ya wajane na wanawake wazee. [28]

Pia, kwa mujibu wa Allama Tabatabai ni kuwa, tabia na mwenendo pamoja na muamala wa Mtume kwa wanawake ni uthibitisho kwamba hakuwachukulia wanawake kuwa chombo cha matamanio ya wanaume; bali amefanya juhudi za kuwaokoa kutokana na unyonge na utumwa. [29]

Muhammad Hussein Kashif al-Ghita anaamini kwamba Mtume (s.a.w.w) alitaka kuonyesha nafasi yake ya kimalakuti kwa mitala na kuonyesha mfano wa wazi wa kujizuia, ustahimilivu na heshima na kuchunga usawa na uadilifu [30].

Maamrisho ya Qur'ani kwa wake za Mtume

Kuna Aya kadhaa zilizoshuka kuhusiana na wake za Mtume (s.a.w.w) na kutolewa maagizo zikiwahutuubu wao:

Adhabu na thawabu za wake za Mtume ni maradufu

Kwa mujibu wa Aya hizi:
يا نِساءَ النَّبِيِّ مَنْ يَأْتِ مِنْكُنَّ بِفاحِشَةٍ مُبَيِّنَةٍ يُضاعَفْ لَهَا الْعَذابُ ضِعْفَيْنِ وَ كانَ ذلِكَ عَلَى اللَّهِ يَسِيراً (۳۰) وَ مَنْ يَقْنُتْ مِنْكُنَّ لِلَّهِ وَ رَسُولِهِ وَ تَعْمَلْ صالِحاً نُؤْتِها أَجْرَها مَرَّتَيْنِ وَ أَعْتَدْنا لَها رِزْقاً كَرِيماً

Enyi wake wa Nabii! Atakaye fanya uchafu dhaahiri miongoni mwenu, atazidishiwa adhabu mara mbili. Na hayo kwa Mwenyezi Mungu ni mepesi. NA MIONGONI mwenu atakeye mt´ii Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na akatenda mema, tutampa malipo yake mara mbili, na tutamwandalia riziki ya ukarimu. (Surat al-Ahzab 30-31)

Kama wake za Mtume watafanya amali njema ujira wa hilo ni mara mbili na kama wakiletenda uchafu na jambo baya basi adhabu yake ni maradufu; [31] kwa sababu ya kunasibiana kwao na Mtume wapo katika nafasi ambayo wanapaswa kuwa kiigizo na mfano kwa wanawake wengine. [32] Kadhalika wafasiri wa Qur'ani tukufu wakiitumia Aya isemayo: 

يا نِساءَ النَّبِيِّ لَسْتُنَّ كَأَحَدٍ مِنَ النِّساءِ إِنِ اتَّقَيْتُنَّ؛

Enyi wake wa Nabii! Nyinyi si kama yeyote katika wanawake wengine. Kama mnamcha Mungu Wanaamini kwamba, jukumu na taklifu yao ni nzito na kubwa kuliko watu wengine; kwa sababu haiingiliki akilini taklifu iwe sawa lakini ujira uwe tofauti. [33]

Kama mnamtaka Mtume na akhera basi ishini maisha ya kawaida kabisa

Kwa mujibu wa Aya hizi:

يا أَيُّهَا النَّبِيُّ قُلْ لِأَزْواجِكَ إِنْ كُنْتُنَّ تُرِدْنَ الْحَياةَ الدُّنْيا وَ زِينَتَها فَتَعالَيْنَ أُمَتِّعْكُنَّ وَ أُسَرِّحْحْكُنَّ سَراحاً جَمِيلاً (۲۸) وَ إِنْ كُنْتُنَّ تُرِدْنَ اللَّهَ وَ رَسُولَهُ وَ الدَّارَ الْآخِرَةَ فَإِنَّ اللَّهَ أَعَدَّ لِلْمُحْسِناتِ مِنْكُنَّ أَجْراً عَظِيييماً[

Ewe Nabii! Waambie wake zako: Ikiwa mnataka maisha ya dunia na pambo lake, basi njooni, nitakupeni kitoka nyumba, na kukuacheni mwachano mzuri. Na ikiwa mnamtaka Mwenyezi Mungu na Mtume wake na nyumba ya Akhera, basi Mwenyezi Mungu amewaandalia wafanyao mema, miongoni mwenu, malipo makubwa. (Surat al-Ahzab 28-29)

Kama wake za Mtume (s.a.w.w) wanamtaka Mtume na akhera, basi wanapaswa kuishi maiisha ya kawaida kabisa yasiyo ya kifahari na kama wanataka dunia basi anapaswa kuwapa talaka na mahari yao. [34] Imekuja katika tafsiri Nemooneh: Aya hii ilishuka ikitoa jibu na mjibizo kwa kutoridhia na kushtakia baadhi ya wake za Mtume kuhusiana na hali ya maisha yao ya kimaada. Baada ya wake hao kuona ghanima za vita wakigaiwa Waislamu, walitoa maombi ya kimaada kwa Mtume. Mtume alikwepa kutekeleza matakwa yao na akawatenga kwa muda wa mwezi mmoja mpaka Aya iliyotangulia iliposhuka. [35]

Msiregeze sauti zenu

Wake za Mtume wametakiwa kutoregeza sauti zao wanapomzungumza na wanaume ili kuipusha kuathirika watu wenye maradhi. [36]

Aya ya 32 ya Surat al-Ahzab inasema:

فَلا تَخْضَعْنَ بِالْقَوْلِ فَيَطْمَعَ الَّذِي فِي قَلْبِهِ مَرَضٌ

basi msiregeze sauti zenu, akaingia tamaa mwenye maradhi katika moyo wake.

Semeni maneno mema

Kwa mujibu wa Aya ya 32 ya Surat al Ahzab wake za Mtume wanapaswa kuzungumza kwa njia stahikii nay a kumridhjisha Mwenyezi Mungu na Mtume wake huku maneno yao yakiwa yameambatana na haki na uadilifu. [3]. Aya hiyo iinasema:

وَ قُلْنَ قَوْلًا مَعْرُوفاً

Na semeni maneno mema

Na kaeni majumbani kwenu na msijishauwe

Aya ya 33 ya Surat al-Ahzab inasema:

وَ قَرْنَ فِي بُيُوتِكُنَّ وَ لا تَبَرَّجْنَ تَبَرُّجَ الْجاهِلِيَّةِ الْأُولى‏ ...

Na kaeni majumbani kwenu, wala msijishauwe kwa majishauwo ya kijahilia ya kizamani

Katika Aya hii wake za Mtume wametakiwa kubakia majumbani mwao na wasifanye mambo ya kijahili ya kujisahaua na kuonyesha miili na mapambo yao kwa wengine. [38] Kwa mujibu wa wafasiri wa Qur'ani, hukumu hii ni jumla na inajumuisha wanawake wote Waislamu lakini inatilia mkazo mno kwa wake za Mtume (saww). [39]

Shikeni Sala na toeni Zaka

أَقِمْنَ الصَّلاةَ وَ آتِينَ الزَّكاةَ وَ أَطِعْنَ اللَّهَ وَ رَسُولَهُ Na shikeni Sala na toeni Za na mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume wake.

Wake za Mtume wanapaswa kusali, watoe Zaka na wamtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Hata hivyo kwa mujibu wa wafasiri, amri na maagizo haya hayawahusu wake za Mtume tu, balio yanajumuisha watu wote, pamoja na kuwa msisitizo zaidi ni kwa wake za Mtume (saww). [40]

Allama Tabatabai ameandika, sababu ya kuwa katika miongoni mwa hukumu na sheria Aya hii imetaja tu Sala na Zaka ni kwamba, mambo haya mawili ni nguzo za ibada na miamala na hukumu na amri nyingine zimekuja chini ya ibara ya: Mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. [41]

Nufaiikeni na fursa ya kuwa pamoja na Mtume (saww)

Allama Tabatabai anasema kuwa, Aya:

وَاذْكُرْنَ ما يُتْلى‏ فِي بُيُوتِكُنَّ مِنْ آياتِ اللَّهِ وَ الْحِكْمَةِ

Na kumbukeni yasomwayo majumbani mwenu katika Aya za Mwenyezi Mungu na hikima Maana yake ni kwamba, wake za Mtume wanapaswa kuhifadhi zile Aya za Mwenyezi Mungu ambazo wanazisikia katika majumba yao na daima wazikumbuke na wasivuke na kukengeuka njia ambayo Mwenyezi Mungu amewaainishia. [42] Baadhi ya wafasiri wamesema, makusudio ya Aya hii ni kwamba, wake za Mtume wanapaswa kushukuru neema hii kwa kuwa kwao katika nyumba ambayo ndani yake mnasomwa Qur'an na hadithi. [43]

Maagizo ya Qur'an ya namna Waislamu wanavyopaswa kuamialiana na wake za Mtume

Katika Qur'ani kumetajwa hukumu maalumu za namna Waislamu wanavyopaswa kuamiliana na wake za Mtume (saww): Kwa mujibu wa Qur'an Waislamu wametakiwa kwamba, wanapokuwa na haja wawaulize nyuma ya mapazia.

Aya ya 53 ya Surat al-Ahzab inasema:


وَ إِذا سَأَلْتُمُوهُنَّ مَتاعاً فَسْئَلُوهُنَّ مِنْ وَراءِ حِجابٍ ذلِكُمْ أَطْهَرُ لِقُلُوبِكُمْ وَ قُلُوبِهِنَّ

Na mnapo wauliza wakeze haja waulizeni nyuma ya mapazia. Hivyo ndio usafi zaidi kwa nyoyo zenu na nyoyo zao.

Makusudio ya hijab hapa yaani nyuma ya pazia sio vazi la kawaida kama wanawake wengine, hapana bali ni hukumu ya nyongeza juu yake na ambayo imeshuka mahususi kwa wake za Mtume (saww) [44] ambapo lengo loa hilo ni kuzuia watu kuwatoa kasoro wake za Mtume [45] na kulinda hadhi na heshima yao. [46]

Marufuku ya kuoa wake za Mtume (saww)

Kwa mujibu wa mafundisho ya Qura'ni ni marufuku kuoa mke wa Mtume baada ya mbora huyo wa viumbe kufariki dunia; marufuku hiyo sababu yake ni kwamba, wake za Mtume ni mithili ya mama wa kimaanawi wa waumini. [47] Aya ya 53 katika Surat al-Ahzab inasema:

وَ لا أَنْ تَنْكِحُوا أَزْواجَهُ مِنْ بَعْدِهِ أَبَداً؛

wala kuwaoa wake zake baada yake kabisa.

Kuhusiana na marufuku hii kuna mambo kadhaa yaliyotajwa ambayo inawezekana ndio yaliyopelekea hilo:

. Kuzuia kuvunjiwa heshima Mtume: Baadhi ya watu walifikia uamuzi kwamba, baada ya kuaga dunia Mtume (saww) watawaoa wake zake na kwa njia hiyo watoe pigo kwa hadhi na heshima yake.

. Kuzuia kutumia vibaya: Kama ingekuwa inaruhusiiwa kuoa wake za Mtume, kulikuwa na uwezekano huu kwamba, watu wangelitumiai vibaya hilo kwa ajili ya kujipatia cheo na daraja katika jamii, Au kwa kutumia kisingizio kwamba, wana ufahamu maalumu kuhusiana na mambo ya ndani ya nyumba ya Mtuume (saww) na maktaba (njia yake ya kifrikra) wangeupotosha Uislamu. [48] . Haikuruhusiwa kuoa wake za Mtume kwa sababu hii kwamba, wao watakuwa ni wake za Mtume pia huko peponi. [49]


Mahari ya wake za Mtume

Makala kuu: Mahr al-Sunna

Kwa mujibu wa hadithi, mahari ya wake za Mtume (saww) ilikuwa ni dirihamu 500 [50] Mahari ambayo Mtume wa Uislamu (saww) aliwapa wake zake na pia kuainisha kwa ajilii ya mabinti zake, kwa mujibu wa Sheikh Sadouq [51] inaitwa Mahr al-Sunnah (mahari ya Sunna) [52].

Hata hivyo kwa kuzingatia riwaya aliyoisimulia Sheikh Sadouq kutoka kwa Imam Baqir (a.s.), mahari ya Ummu Habiba (mke wa Mtume) ilikuwa ni dirihamu 4000. [53] Inasemekana kwamba katika riwaya hii, Imam Baqir (a.s.) alizingatia mahari hii kwamba, lilikuwa jambo la kipekee ambapo Najjashi, mtawala wa Uhabesh, ambaye alikuwa mwakilishi wa Mtume katika kumchumbia Umm Habiba, alifanya hivyo na alilipa mahari yeye mwenyewe, na Mtume (saww) hakulipinga. [54]

Namna ya kuamiliana na wake za Mtume (saww)

Kwa mujibu wa mwandishi wa Misri Muhammad Hassanin Heikal (aliyefariki 1956), Mtume alikuwa akiwapa hadhi maalumu wake zake ambayo haikujulikana kwa Waarabu. [55] Kwa mujibu wa baadhi ya Aya za Qur'ani, alijiharamishia baadhi ya mambo yanayoruhusiwa ili kuwaridhisha baadhi ya wake zake. Mfano wa wazi ni sababu ya kushuka Aya ya 1 ya Surat al-Tahrim ambayo inasema:

یا أَیهَا النَّبِی لِمَ تُحَرِّ‌مُ مَا أَحَلَّ اللَّهُ لَک تَبْتَغِی مَرْ‌ضَاتَ أَزْوَاجِک ۚ وَاللَّهُ غَفُورٌ رَّ‌حِیمٌ

Ewe Nabii! Kwa nini unaharimisha alicho kuhalilishia Mwenyezi Mungu? Unatafuta kuwaridhi wake zako. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu. [56]

Inaelezwa kuwa, sababu ya kushuka Aya hii ni hatua ya Mtume ya kujiharamisha kula asali kwa ajili ya kumridhisha mkewe Hafsa ambayo aliandaliwa na mkewe mwingine yaani Zaynab bint Jahsh. [57]

Pia, Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akifanya uadilifu miongoni mwa wake zake. Kuna ripoti za kugawa mali kwa usawa kati yao. Miongoni mwa mambo mengine, kwa mujibu wa riwaya ya Muhammad bin Omar Waqidi katika kitabu cha Al-Maghazi (kinachozungumzia maisha ya Mtume), baada ya vita vya Khaybar, Mtume alimlipa kila mmoja wa wake zake wasak (vipimo) 80 vya tende na wasak ishirini za shayiri.[58] Alikuwa akigawa zamu za usiku baina yao na wakati wa vita au safari alikuwa akipiga kura na kumchukua mmoja wao pamoja naye, ingawa kwa mujibu wa Aya ya 51 ya Surat Al-Ahzab, aliruhusiwa kuchelewesha zamu ya yeyote katika wake zake kama angetaka kufanya hivyo.[59]

Bibliografia

Vitabu vingi vimeandikwa kuhusu wake za Mtume kwa Kiarabu na Kiajemi na wanachuoni wa Shia na Sunni. Baadhi yavyo ni:

. Al-Muntakhab Min Kitab Azwaj al-Nabi: Mwandishi, Zubayr bin Bakkar (aliaga dunia 256 H). Kitabu hiki kimefanyiwa uhakiki na Sakina Shihabi na kilichapishwa na kusambazwa na Taasisi ya al-Risalah ya Beirut Lebanon, 1403 H.

. Zaujaat al-Nab: Mwandishi, Saeed Ayub (aliazaliiwa 1363 H), Mmisri ambaye ni Mustabsir (katika utamaduni wa Shia, huitwa mtu ambaye baada ya kufanya utafiti na uhakiki ameamua kubadilisha dini au madhehebu yake kutoka mojawapo ya madhehebu ya Kiislamu au dini za Mwenyezi Mungu na kuingia katika madhehebu ya Shia Ith’naasharia.) [60].

. Sebke Zendegi Rasul Khuda ba Hamsaranesh; Mwandishi Farzaneh Hakimzadeh, kitabu hiki kimeandika kwa mtindo wa kumfanya msomaji amfanye Mtume kuwa kigezo na ruuwaza katika maisha yake. [61]

. Azwaaj al-Nabi, mwandishi Muhammad Yusuf Salehi Dimashqi.

. Zaujaat al-Nabi wa auladih, mwandishi Mahya al-Khiyami.

. Hamsaran Payambar, mwandishi Aqiqi Bakhshayesh.