Mahari ya Sunna

Kutoka wikishia

Mahari ya Sunna (Kiarabu: مَهْر السُّنةِ) ni mahari ambayo bwana Mtume Muhammad (s.a.w.w) aliwaainishia wake zake na binti zake. Kiasi cha mahari ya Sunna ni dirhamu 500 sawa na gramu 1500 ya madini ya fedha safi. Katika Hadithi imeelezwa ya kwamba; mahari ya Fatima Zahra (a.s), ilikuwa na ngao au nguo ya kitani ilio shonwa Yemen, au vitu vingine tofauti na dirhamu vilitajwa ndani ya Hadithi, ambavyo bei yake ilikadiriwa kuwa ni kati ya dirhamu 400 hadi 500. Imamu Jawadi (a.s), pia aliainisha mahari ya mkewe (Umm al-Fadl) ambaye ni binti al-Ma'muni kwa kiasi cha dirhamu 500, sawa na mahari ya bib Fatima Zahra (a.s).

Kwa mujibu wa maoni ya wanazuoni kadhaa; Kuweka mahari zaidi ya mahari ya Sunna ni makruhu (si jambo lililopendekezwa katika Uislamu). Kwa upande mwengine, baadhi ya wanazuoni wametoa rai tofauti katika suala hili. Mtazamo mpaya wa wanazuoni hawa, ni sababu ya kwamba; leo gramu 1500 za fedha hazina thamani ya pesa nyingi kiasi ya kukidhi na kushika nafasi ya mahari, ila wakati wa Mtume (s.a.w.w) na Maimamu (a.s), kiwango hicho kilikuwa na thamani zaidi. Kupitia hoji wao wanaamini kwamba; mahari ya Sunna hayawezi kuwa na thamani ya pesa thabiti, na wamejaribu kuhesabu mahari ya Sunna kulingana na thamani ya zama za leo; hata hivyo wanasema kwamba mahari ya Sunna si mahari kandamizi yenye makalifisho na uzito ndani yake.

Ufafanuzi wa dhana

Mahari ya Sunna (مَهرالسُنَّة): Ni kiwango cha mahari ambayo bwana Mtume Muhammad (s.a.w.w) alikuwa akiwawekea wake zake, na vile vile, kama ilivyoanukuliwa na Sheikh Sadouq, kwamba; pi kiwango hicho hicho ndicho alicho kianisha kwa ajili ya binti zake. (1) (2)

Kiwango na thamani ya mahari

Kulingana na Sunna (Hadithi) ni kwamba, kiasi cha Mahari ya Sunna (مَهرالسُنَّة) kilikuwa ni dirham 500. [3] Hadithi hii inachukuliwa kuwa ni Hadithi yenye mapokezi mutawaatir. [4] Katika baadhi ya Hadithi imeelezwa ya kwamba; bwana Mtume (s.a.w.w) hakuweka mahari kwa ajili wake na binti zake zaidi ya kiwango cha wakia kumi na mbili na nusu (sawa na dirham mia tano). [5]

Hadithi chache tofauti

Kuna Hadithi kadhaa tofauti katika vyanzo vya Hadithi, kuhusiana na Mahari ya Sunna (مَهرالسُنَّة). Miongoni mwa Hadithi hizo ni Hadithi iliyo nukuliwa na Sheikh al-Saduq kutoka kwa Imam Baqir (a.s) isemayo kwamba; mahari Ummu Habiba (mke wa bwana Mtume (s.a.w.w)) yalikuwa ni dirham elfu nne. [6] Katika Hadithi hii Inasemekana kwamba; Imam Baqir (a.s) aliyachukulia mahari haya kuwa ni kesi maalumu na nadra, ambapo uamuzi juu ya mahari hayo ulifanywa na Najashi, gavana wa Abyssinia (Ethiopia), ambaye alimwakilisha bwana Mtume katika kumposa Ummu Habiba, na yeye mwenyewe (Najashi) ndiye aliye lipa mahari hayo na Mtume (s.a.w.w.) hakupingana na maamuzi hayo. [7]

Pia kuna taarifa tofauti kuhusiana na mahari ya bibi Fatima Zahra (a.s). Kwa hiyo kuna maelezo tofauti juu ya kiwango cha mahari yake (a.s). Miongoni mwa kauli hizo ni; dirham 480, mith-qali 400 za fedha na dirham 500. Ibn Shahri Ashub ambaye ni mwanahadithi wa Kishia (aliye zaliwa mwaka 488 na kufariki 588), katika kitabu chake kiitwacho al-Manaqib, alisema kwamba; sababu ya wanazuoni kutofautiana juu ya kiwango cha mahari ya bibi Fatima, inatokana na khitilafu juu vitu na ya vitu alivyopewa kama ni mahari, hii ni kawa sababu kila kimoja kati ya vitu hivyo kina thamani tofauti. Bada ya kutoa maelezo haya, ametaja Hadithi ambazo kwa mujibu wa baadhi yake, mahari ya bibi Fatima (a.s), yalikuwa ni nguo ya pamba yenye mshono wa Yemen na ngozi isiyo chunywa manyoya yake, yalio ambatanishwa na mmea unao nukia, na kulingana na Riwaya nyengine ni kwamba; mahari yake (a.s) ilikuwa ni ngao na ngozi yenye manyoya kamili, ambayo ima ilikuwa ni ya kondoo au ngamia. [9]

Baadhi ya waandishi baada ya tafiti juu ya Hadithi kadhaa, na kwa mujibu wa nyenendo na Sunna za bwana Mtume (s.a.w.w), na pia kwa kuzingatia Hadithi ya Imamu Jawadi (a.s), isemayo kwamba mahari ya mkewe (Ummu Fadhli) yalikuwa ni kiwango cha dirhamu 500, ambayo ni sawa na mahari ya bibi Fatima (a.s), [11] waandishi hawa wameandika wakisema kuwa; Mahari ya bibi Fatima hayakuwa ni zaidi ya dirhamu 500. [11]

Je, ni wajibu kuotoa mahari ya Sunna au ni mustahabu tu

Kulingana na maelezo ya Sahib al-Jawahir, mmoja wa wanazuoni wa karne ya 13 Hijiria ni kwamba; mtazamo maarufu kati ya mafaqihi ni kwamba: mahari ya mwanamke hayana kikomo maalumu na ni halali kuainisha kiwango kinacho pindukia mahari ya Sunna. [12] Kwa mujibu wa fat'wa zao kwamba; kubainisha mahari zaidi ya mahari ya Sunna ni makruhu tu (si jambo lililo pendekezwa). [13]

Kwa mujibu maelezo yake, ni idadi ndogo tu miongoni mwa mafaqihi waliotoa fat'wa za kubatilisha (kuharamisha) mahari yanayo kiuka mahari ya Sunna, ikiwa ni pamoja na Sayyid Murtadha,[14] mmoja wa wanazuoni wa karne ya 4 na 5 Hijiria, ambaye anaamini kuwa; mahari zaidi ya mahari ya Sunna ni batili. Kwa mtazamo wa mafaqihi hawa ni kwamba; ikiwa mahari yatapindukia kiwango cha mahari ya Sunna, basi kiwango kinachomwajibikia mwanamme kulipa, kile kiwango cha Sunna tu. [15]

Mahari ya Sunnah kulingana na zama za leo

Kiasi cha mahari ya Sunna, ambacho ni kiwango cha dirhamu 500, kiendacho sawa na gramu 1,500 za fedha safi, ni kiwango cha chini sana katika zama zetu za leo ukilinganisha na ilivyokuwa wakati huo. Kwa kuwa thamani ya dirhamu 500 wakati wa zama za bwana Mtume (s.a.w.w) na Maimamu (a.s) ilikuwa kubwa zaidi kuliko vipindi vya baadaye, baadhi wanaamini kwamba mahari ya Sunna hayana kiwango cha fedha thabiti kilichoainishwa kisheria, kwa hiyo kiwango cha mahari kinapaswa kuhesabiwa kulingana na thamani ya dirhamu 5000 kulingana na zama zilivyo. Kwa hivyo walijaribu kupata thamani sawa ya dirhamu 500 kulingana na zama zitolewazo mahari hayo. [16]

Kwa mfano, katika siku za nyuma, baadhi ya mafaqihi walikuwa wakipima dirham 500 kwa kulinganisha na thamani ya dinari, na kwa sababu katika zama zao, kila dirhamu 10 zilikuwa ni sawa na thamani ya dinari moja, hivyo wao walichukulia mahari ya Sunna kuwa ni dinari hamsini (yaani mithqali 50 za dhahabu safi). Pia, baadhi ya wanazuoni wamependekeza kwamba; thamani ya leo ya mahari ya Sunna ipatikane kwa kuthamini uwezo mahari hayo katika manunuzi ya bidhaa wakati wa bwana wa Mtume (s.a.w.w). Hii ni kwa sababu, kwa mujibu wa baadhi ya Hadithi, Mtume (s.a.w.w) kupitia mahari ya bibi Fatima, aliweza kununua baadhi ya vifaa na bidhaa ambzo zilitumika kwa ajili ya kuanzisha maisha ya kifamilia baina ya binti yake na Imam Ali (a.s). Hivyo basi njia njema ya kusawazisha suala la mahari na kupata kiwango halali cha mahari ya Sunna ni kupitia mfumo huu. [17]

Kwa kuzingatia thamani ya mithqali hamsini za dhahabu, pia tukitilia maanani kwamba; vitu vilivyonunuliwa kupitia mahari ya bibi Fatima Zahra (a.s), vilikuwa ni rahisi sana na vya kawaida, wanazuoni wamefikia hitimisho lenye natija isemayo kwamba; mahari ya Sunna si mahari mazito yenye makalifisho na uzito ndani yake. [18]

Vyanzo

  • Ḥimyarī, ʿAbd Allāh b. Jaʿfar al-. Qurb al-isnād. Edited by Muʾassisat Āl al-Bayt. Qom: Muʾassisat Āl al-Bayt, 1413 AH.
  • Ḥillī, Jaʿfar b. al-Ḥasan al-. Sharāʾiʿ al-Islām fī masāʾil al-ḥalāl wa l-ḥarām. Edited by Muḥammad ʿAlī Baqqāl. 2nd edition. Qom: Muʾassisa-yi Ismāʿīlīyān, 1408 AH.
  • Ibn Shahrāshūb, Muḥammad b. ʿAlī. Manāqib Āl Abī Ṭālib. 1st edition. Qom: ʿAllāma, 1379 AH.
  • Majlisī, Muḥammad Bāqir al-. Biḥār al-anwār al-jāmiʿa li-durar akhbār al-aʾimmat al-aṭhār. 3rd edition. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1403 AH.
  • Murawwijī Ṭabasī, Muḥammad Jawād. Fāṭima ulgū-yi ḥayāt-i zībā. 1st edition. Qom: Būstān-i Kitāb, 1380 Sh.
  • Masʿūdī, ʿAbd al-Hādī. Pazhūhishī darbāra-yi Mahr al-sunna (Mahr-i Muḥammadī) in Muḥammadī Riyshahrī, Muḥammad. Taḥkīm-i khāniwāda az nigāh-i Qurʾān wa ḥadīth. Translated to Farsi by Shaykhī, Ḥamīd Riḍā. 2nd edition. Qom: Sāzmān-i Chāp wa Nashr-i Dār al-Ḥadīth, 1389 Sh.
  • Mufīd, Muḥammad b. Muḥammad al-. Al-Irshād fī maʿrifat ḥujaj Allāh ʿalā l-ʿibād. Edited by Muʾassisat Āl al-Bayt. 1st edition. Qom: Kungira-yi Shaykh al-Mufīd, 1413 AH.
  • Najafī, Muḥammad al-Ḥasan al-. Jawāhir al-kalām fī sharḥ sharāʾiʿ al-Islām. 7th edition. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1404 AH.
  • Shahīd al-Thānī, Zayn al-Dīn b. ʿAlī. Al-Rawḍa al-bahiyya fī sharḥ al-lumʿat al-Dimashqiyya. Edited by Sayyid Muḥammad Kalāntar. 1st edition. Qom: Kitābfurūshī-yi Dāwarī, 1410 AH.
  • Ṣadūq, Muḥammad b. ʿAlī al-. Al-Muqniʿ fī al-fiqh. 1st edition. Qom: Muʾassisa al-Imām al-Hādī, 1415 AH.
  • Ṣadūq, Muḥammad b. ʿAlī al-. Man lā yaḥḍuruh al-faqīh. Edited by ʿAlī Akbar Ghaffārī. 2nd edition. Qom: Daftar-i Intishārāt-i Islāmī affiliated to Jāmiʿa-yi Mudarrisīn-i Ḥawza-yi ʿIlmīyya-yi Qom, 1413 AH.