Qassim ibn Muhammad (s.a.w.w)

Kutoka wikishia
Kaburi la Khadijah na mwanawe Qasim lililo jengewa katika makaburi ya Moala

Qassim ibn Muhammad (Kiarabu: القاسم بن محمَّد) ni mtoto wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) na ndiye mtoto wa kwanza wa Mtume na Bibi Khadija ambaye alizaliwa Makka kabla ya Mtume kubaathiwa na kupewa Utume. Qassim aliaga dunia akiwa mtoto mdogo,[1] Katika baadhi ya ripoti imeelezwa kuwa, wakati anaaga dunia alikuwa na umri wa miaka miwili.[2] Kuniya ya Mtume (s.a.w.w) ya Abu-Qassim imechukuliwa kutoka katika jina la mwanawe huyo.[3]

Kwa mujibu wa baadhi ya ripoti, baada ya kifo cha Qassim, alAs bin Wail alimuita Mtume kwa jina la Abtar (mtu aliyekatikiwa), na kufuatia hilo, ikashushwa Suratu al-Kawthar.[4] Tukio hili limenukuliwa pia kuhusiana na kifo cha Abdallah, mtoto mwingine wa Mtume (s.a.w.w).[5] Qassim amezikwa Makka.[6]

Rejea

  1. Ibn Ishaq, Sira ibn Ishaq, uk.245; Ibn Hisham, al-Sira al-nabawiyya, juz.1, uk.190.
  2. Diyarbakri, Tarikh al-Khamis, juz.1, uk.273; al-Majlisi, Bihar al-Anwar, juz.2, uk.166.
  3. Ibn Hisham, Sirat al-Nabiyyah, Darul al-Maarifa, juz. 1, uk.190.
  4. Ibn Ishaq, Sira ibn Ishaq, uk.245; Ibn Kathir, Al-Bidaya wa al-nihaya, juz.3, uk.104.
  5. Al-Baladhuri, Ansab al-ashraf, juz. 1, uk. 138-139.
  6. Maliki Makki, Tahswil al-Maram fi Akhbar al-Bayt al-Haram, 1424 AH, juz. 2, uk.650.

Vyanzo

  • Ibn Kathir Damishqi, Isma'il. Al-Bidaya wa al-nihaya. Beirut: Dar al-Fikr.
  • Ibn Hisham, 'Abd al-Malik. al-Sira al-nabawiyya. Beirut: Dar al-Ma'rifa.
  • Ibn Ishaq, Muhammad. Sira ibn Ishaq , (al-musamma bi) Kitab al-siyar wa l-maghazi .Tehran: Daftar-i Mutali'at-i Tarikh Wa Ma'arif Islami, 1410/1989.
  • Al-Baladhuri, Ahmad b. Yahya, Ansab al-Ashraf, 1st edition, Beirut, Dar al-Fikr, 1417/1996.
  • Diyarbakri, Husayn b. Muhammad, Tarikh al-khamis fi ahwal anfus al-nafis, Beirut, Dar al-Sadir.