Abdallah ibn Muhammad (s.a.w.w)

Kutoka wikishia

Abdullah ibn Muhammad (Kiarabu: عبد الله) ni mtoto wa Mtume (s.a.w.w) na Bibi Khadija ambaye aliaga dunia akiwa mtoto mdogo. Kwa mujibu wa ripoti za vyanzo vya historia, baada ya Abdallah kuaga dunia al-A’s bin Wail alimuita Mtume (s.a.w.w) kwa jina la Abtar (aliyekatikiwa) na kufuatia hilo, Mwenyezi Mungu akashusha Surat al-Kawthar.

Akthar ya vyanzo vya historia vimetambua mazazi yake kuwa ni baada ya Muhammad kubaathiwa na kupewa Utume.[1] Hata hivyo nukuu nyingine inaeleza kuwa alizaliwa kabla ya Mab’ath (kupewa Utume Muhammad).[2] Alipewa lakabu ya Tayyib na Tahir;[3] kwa sababu alizaliwa baada ya kushuka Wahyi na katika zama za Uislamu.[4]

Abdalla aliaga dunia katika mji wa Makka akiwa angali mtoto mdogo.[5] Kwa mujibu wa ripoti ya Ahmad bin Yahya Baladhuri katika kitabu chake cha Ansab al-Ashraf ni kuwa, baada ya kifo chake, al-As bin Wail alimuita Mtume kwa jina la Abtar (mwenye mapungufu, asiye na watoto, aliyekatikiwa na kizazi) kwa kuwa hana mtoto wa kiume na hivyo kizazi chake hakitoendelea. Kwa msuingi huo Mwenyezi Mungu akashusha Surat al-Kawthar ambapo Aya ya mwisho ya Sura hii inasema:

((إِنَّ شانِئَکَ هُوَ الْأَبْتَر))
((Hakika mwenye kukubughudhi, yeye ndiye mwenye kukatikiwa)).[6] Aya hiyo ilishuka kujibu maneno hayo ya al-As bin Wail.[7]


Kwa mujibu wa hadithi iliyonukuliwa na Sheikh Kulayni katika kitabu cha al-Kafi ni kuwa, baada ya kuaga dunia Abdallah, Bibi Khalid alikuwa akilia. Mtume (s.a.w.w) akamwambia:

Je huridhika utakapomuona amesimama katika mlango wa pepo na atakapokuona ataushika mkono wako na kukuingiza katika sehemu bora kabisa peponi…? Mwenyezi Mungu ni mbora na mwenye adhama zaidi ambapo hawezi kuchukua tunda la moyo la mja, na mja huyo ashikamane na subira kutokana na hilo na amshukuru Allah, kisha Mwenyezi Mungu aje na kumuadhibu mja huyu.[8]

Rejea

  1. Tazama: Ibn Ḥajar al-ʿAsqalānī, al-Iṣāba, juz. 3, uk. 445; Maqrizī, Imtāʿ al-asmāʾ, juz. 5, uk. 333.
  2. Ibn Isḥāq, Sīrat al-nabawīyy, uk. 82.
  3. Ibn Ḥajar al-ʿAsqalānī, al-Iṣāba, juz. 3, uk. 445; Maqrizī, Imtāʿ al-asmāʾ, juz. 5, uk. 333.
  4. Amīn, Aʿyān al-Shīʿa, juz. 1, uk. 223.
  5. Maqrizī, Imtāʿ al-asmāʾ, juz. 5, uk. 333.
  6. Qurʾān, 108:3.
  7. Balādhurī, Ansāb al-ashrāf, juz. 1, uk. 138-139.
  8. Kulaynī, al-Kāfī, juz. 3, uk. 219.

Vyanzo

  • Amīn, Sayyid Muḥsin al-. Aʿyān al-Shīʿa. Beirut: Dār al-Taʿāruf li-l-Maṭbūʿāt, 1406 AH.
  • Balādhurī, Aḥmad b. Yaḥyā al-. Ansāb al-ashrāf. Beirut: Dār al-Fikr, 1417 AH.
  • Ibn Ḥajar al-ʿAsqalānī, Aḥmad b. ʿAlī. Al-Iṣāba fī tamyīz al-ṣaḥāba. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmīyya, 1415 AH.
  • Ibn Isḥāq, Muḥammad. Sīrat al-nabawīyy. Qom: Daftar-i Muṭāliʿāt-i Tārīkh wa Maʿārif-i Islāmī, 1410 AH.
  • Kulaynī, Muḥammad b. Yaʿqūb al-. Al-Kāfī. Second edition. Tehran: Islāmīyya, 1362 Sh.
  • Maqrizī, Aḥmad b. ʿAlī al-. Imtāʿ al-asmāʾ bi-mā li-l-nabīyy min al-aḥwāl wa l-amwāl wa l-ḥafdat wa l-matāʿ. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmīyya, 1420 AH..
  • Ṭabrisī, Faḍl b. al-Ḥasan al-. Iʿlām al-warā. Qom: Āl al-Bayt, 1417 AH.