Zaynab binti ya Mtume (s.a.w.w)

Kutoka wikishia

Zaynab binti ya Mtume (Kiarabu: زینب بنت محمد) (aliyefariki 8 Hijiria), kwa mujibu wa wanahistoria wengi wa Kiislamu, alikuwa binti mkubwa wa Mtume (s.a.w.w) na Khadija. Kabla ya Mtume kupewa utume rasmi, yeye aliolewa na Abul As bin Rabi’. Baada ya kubaathiwa Mtume Muhammad, tofauti na mumewe, Zaynab alisimu, lakini Abu al-Aas alimzuia kuhajiri na kuhamia Madina.

Zaynab alihamia Madina baada ya Vita vya Badr. Katika mwaka wa saba Hijiria, Abu al-Aas alisilimu na akaenda Madina kwa Zaynab. Kwa mujibu wa vyanzo vingi, Mtume alimtuma Zaynab kwa Abu al-Aas kwa mujibu wa ndoa ya awali, kwani katika zama hizo hakukuwa kumeshuka Aya ya kuwakataza wanawake wa Kiislamu kuolewa na makafiri.

Kwa mujibu wa Sayyid Jafar Murtadha Amili (1441-1364), mwanahistoria wa karne ya 14, Zainab hakuwa mtoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) na Khadija, bali alikuwa binti yao wa kulea. Zainab alifariki mwaka wa 8 Hijiria na akazikwa huko Baqi’.

Uhusiano wake na Mtume

Makala asili: Watoto wa Mtume

Zainab alikuwa binti mkubwa wa Mtume (s.a.w.w) na Khadija [1] Kwa mujibu wa wanahistoria, alizaliwa wakati Mtume (s.a.w.w) alipokuwa na umri wa miaka 30 [2] na ilikuwa ni katika mwaka wa 30, mwaka wa tembo. [3]

Sayyid Jafar Murtadha al-Amili, mmoja wa watafiti wa Kishia, na Abu al-Qasim Kufi, mwanachuoni wa Shia wa karne ya nne, wanaamini kwamba Zainab, Ruqayyah, na Umm Kulthum hawakuwa watoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) na Khadija; bali walikuwa mabinti wao wa kulea. [4] Ja’far Murtadha ameandika kitabu cha “Banat Nabi am Rabaibah”? (Binti za nabii au binti zake wa kulea?) ili kuthibitisha jambo hili. [5]

Kuolewa na Abu al’As

Kwa mujibu wa wanahistoria wa Kiislamu, Zainab aliolewa na Abul As bin Rabi kabla Mtume kubaathiwa na kupewa Utume [6].[7] Abul As alikuwa mtoto wa Hala dada yake Khadija. [8] Baada ya utume wa Mtume, tofauti na Bibi Khadija na mabinti zake Mtume, yeye hakuukubali Uislamu. Kwa hiyo, Maquraishi walimtaka ampe talaka Zainab; lakini Abul As hakukubali. [9] Tofauti na Utba na Otayba, watoto wa Abu laHab, ambao wao waliwataliki Ruqayyah na Umm Kulthum, mabinti wengine wa Mtume, kwa ombi la Maquraishi. [10]

Makaburi ya mabinti wa Mtume (s.a.w.w) karibu na makaburi ya Maimamu katika Baqi kabla ya kubomolewa

Zainab akiwa katika ndoa na Abul-A’as alizaa naye Umamah na Ali. [11] Ali alifariki dunia akiwa mtoto; [12] lakini Umamah akawa mke wa Imam Ali (a.s) baada ya kufa shahidi Fatima (a.s) na baada ya Imamu Ali kuuawa shahidi akaja kuolewa na Mughira bin Nawfal. [13]

Kuhamia Madina

Mutahhar bin Tahir Muqaddasi, mwanahistoria wa zama za ukhalifa wa Bani Abbas ameandika kwamba baada ya Mtume kuhamia Madina, aliwatuma Abu Rafi na Zayd bin Haritha kwenda Makka kuwaleta mabinti zake Madina. Lakini Abul-Aas alimzuia Zainab asiende. [14] Hata hivyo, baada ya Vita vya Badr, alimtuma Zainab kwenda Madina pamoja na masahaba wa Mtume (s.a.w.w) [15] kwa sababu Abul As alitekwa na Waislamu katika Vita vya Badr [16] na akamuahidi Mtume kumuacha Zainab baada ya kuachiliwa huru. [17] Hata hivyo kuna hadithi pia ambayo inaeleza kwamba, Zainab alihamia Madina pamoja na Mtume [18].

Kumpa hifadhi Abul A’as

Kwa mujibu wa wanahistoria, Zainab alimpa hifadhi Abul As mwaka wa 6 Hijiria na Abul As akasilimu. [19] Abul As alikuwa amekwenda Syria na msafara wa Maquraishi kwa ajili ya biashara mwaka wa 6 Hijiria. [20] Wakiwa njiani wakirejea kulitokea mapigano baina yao na Waislamu. Abul-Aas alikimbia na kufika Madina na kuomba hifadhi kwa Zainab. Zainab alileta habari hizo kwa Mtume (s.a.w.w). Mtume alikubali na kuafiki hatua ya Zainab ya kumpa hifadhi Abul As; lakini akamwambia kwamba maadamu Abul As ni mshirikina hatakuwa halali kwake. Abul-Aas alirejea Makka na akatangaza kwamba amesilimu alipokuwa Madina. [21]

Kaburi la Zaynab, binti ya Mtume (s.a.w.w) katika makaburi ya Baqi

Baada ya muda, Abul As alirejea Madina na Mtume (s.a.w.w) akampeleka Zainab kwa Abul As katika Muharram mwaka wa 7 Hijria kwa ndoa ya awali; [22] kwa sababu wakati huo Aya inayokataza wanawake wa Kiislamu kuolewa na makafiri haikuwa imeshuka. [23][24] Hata hivyo wengine wanasema kuwa, akawa mke wa Abul as baada ya kufunga ndoa nyingine. [25]

Kuaga dunia

Mwaka wa kifo cha Zaynab umetajwa kuwa ni 8 AH. [26] Sawdah binti Zam'a bin Qays na Umm Ayman, walikuwa miongoni mwa waliomuosha baada ya kuaga dunia. [27] Kwa mujibu wa ʾAḥmad ibn Yahya ibn Jabir al-Baladhuri mwanahistoria wa Kiislamu wa karne yatatu Hijria, wakati wa kuzzikwa Zaynab, Mtume (s.a.w.w) aliingia kwenye kaburi lake na akamuombea dua. [28]

Katika vyanzo vya kihistoria, imetajwa kuhusu sababu ya kifo cha Zaynab, pale Zaynab alipohamia Madina, Habbar bin Aswad na mshirikina mwingine walimuona njiani. Habbar akamsukuma na kugonga jiwe. Zaynab ambaye alikuwa mjamzito mimba yake ikaharibika na kuanzia hapo hakuwa na furaha hadi alipofariki. [29]

Mazishi ya Zaynab hayajavainishwa na kuwekwa wazi katika vyanzo vya kihistoria; lakini kwa mujibu wa hadithi, baada ya Zaynab kufariki, Mtume alisema: muunganisheni pamoja na mja wetu mwema Uthman bin Madh’un. [30] Kwa msingi huo imefahamika kuwa, mahali alipozikwa ni Baqi’i. [31] Kwa sababu Othman bin Madh’un alikuwa sahaba wa kwanza miongoni mwa Muhajirina ambaye alizikwa Baqi’i. [33] Kadhalika kuna kaburi linalonasibishwa na Zaynab na mabinti wengine wa Mtume katika makaburi ya Baqi’. [33] Kaburi tajwa inasemekana kuwa lilikuwa na dharih huko nyuma [34] pamoja na makaburi mengine ya Baqi’ kabla ya kuvunjwa na kuharibiwa na Mawahabi. [45].

Vyanzo

  • ʿĀmilī, al-Sayyid Jaʿfar al-Murtaḍā al-. Al-Ṣaḥīḥ min sīrat al-nabī al-aʿẓam. Qom: Dār al-Ḥadīth, 1426 AH.
  • ʿĀmilī, al-Sayyid Jaʿfar al-Murtaḍā al-. Banāt al-Nabī am rabāʾibuh. Markaz al-Jawād, 1413 AH.
  • Al-Madanī al-Barzanjī. Nuzhat al-nāzirīn fī masjid sayyid al-awwalīn wa al-ākhirīn. Edited by Aḥmad Saʿīd b. Sālim. [n.p]. 1416 AH.
  • Balādhurī, Aḥmad b. Yaḥyā al-. Ansāb al-ashrāf. Edited by Suhayl Zakār & Rīyāḍ al-Ziriklī. 1st edition. Beirut: Dār al-Fikr, 1417 AH.
  • Ḥākim al-Nayshābūrī. Muḥammad b. ʿAbd Allāh al-. Al-Mustadrak ʿala l-ṣaḥīḥayn. Edited by Musṭafā ʿAbd al-Qādir ʿAṭā. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmīyya, 1411 AH.
  • Ibn al-Athīr al-Jazarī, ʿAlī b. Muḥammad. Usd al-ghāba fī maʿrifat al-ṣaḥāba. Beirut: Dār al-Fikr, 1409 AH.
  • Ibn Ḥajar al-ʿAsqalānī, Aḥmad b. ʿAlī. Al-Iṣāba fī tamyīz al-ṣaḥāba. Edited by ʿĀdil Aḥmad ʿAbd al-Mawjūd and ʿAlī Muḥammad Muʿawwaḍ. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmīyya, 1415 AH.
  • Ibn Saʿd, Muḥammad. Al-Ṭabaqāt al-kabīr. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmīyya, 1410 AH/1990.
  • Ibn ʿAbd al-Barr, Yūsuf b. ʿAbd Allāh. Al-Istīʿāb fī maʿrifat al-aṣḥāb. Edited by ʿAlī Muḥammad al-Bajāwī. Beirut: Dār al-Jail, 1412 AH.
  • Ibn Hishām, ʿAbd al-Malik. Al-Sīra al-nabawīyya. Edited by Muṣṭafā al-Saqā. Beirut: Dār al-Maʿrifa, [n.d].
  • Jaʿfarīyān, Rasūl. Panjāh safarnāma-yi ḥajj Qājārī. Tehran: Nashr-i ʿIlm, 1389 Sh.
  • Jaʿfarīyān, Rasūl. Risāla-yi mufarriḥat al-anām fī taʾsis bayt Allāh al-harām. Mīqāt-i Ḥajj. No 5. 1372 Sh.
  • Kūfī, ʿAlī b. Aḥmad. Al-Istighātha fī bidaʿ al-thalātha. [n.p]. [n.d].
  • Mubārakfūrī, Muḥammad b. ʿAbd al-Raḥmān b. ʿAbd al-Raḥīm. Tuḥfat al-aḥūdhī. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmīyya, 1410 AH/1990.
  • Maqdisī, Muṭahhar b. Ṭāhir. Al-Bidaʾ wa al-tārīkh. Port Said: Maktabat al-Thiqāfat al-Dīnīyya, [n.d].
  • Mūsawī Isfahānī, Ḥasan. Rūznāma safar-i Mashhad, Mecca wa ʿAtabāt 1315-1316 AH. Edited by Rasūl Jaʿfarīyān. Tehran: Nashr-i Mashʿar, 1392 Sh.
  • Ṭabarī, Muḥammad b. Jarīr al-.Tārīkh al-umam wa l-mulūk. Edited by Muḥammad Abu l-faḍl Ibrāhīm. Second edition. Beirut: Dar al-Turāth, 1387 AH.
  • Wāqidī, Muḥammad b. ʿUmar al-. Al-Maghāzī. Edited by Marsden Jones. Beirut: Muʾassisat al-Aʿlamī li-l-Maṭbūʿāt, 1409 AH.