Nenda kwa yaliyomo

Ughulati

Kutoka wikishia

Ughulati (Kiarabu: الغلو) Ni kule muumini kuwa na imani za kupindukia mipaka na kutoka nje ya uwiano wa mizani ya dini, ambapo muumini huwa na imani za zisizo za wastani kuhusiana na haki za Manabii na Maimamu. Kuwa na msimamo wa kupindukia mipaka (Ughulati) ni miongoni mwa nyenendo potovu za dini ambazo pia zlikuwepo mara kwa mara katika historia ya mwanadamu. Baadhi ya mifano ya msimamo kupindukia mipaka (Ughulati) ni pamoja na: kuamini kuwa Nabii au Imamu ni Mungu, kumhisabu mtu fulani kuwa ni mwana wa Mungu, kuamini unabii wa Imamu Ali au mmoja kati ya Maimamu wa Shia, na kuamini katika ujio wa mtu mwingine tofauti na Mahdi aliyetabiriwa pia ni miongoni mwa matendo ya Ughulati.

Miongoni mwa sababu zilizotajwa kuhusiana na chanzo cha Ughulati ni; Motisha Malengo ya kisiasa, udhaifu wa tafakuri, mapenzi ya kupita kiasi na ushabiki pofu usio na misingi pamoja na uwepo wa maadui wa nyuma ya pazia dhidi ya Uislamu. Uwepo wa vishawishi (mashushushu) miongoni mwa Waislamu wenye malengo ya kupotosha fikra za Kiislamu pia ni miongoni mwa sababu zinazotajwa kuhusiana na chanzo kuwepo kwa imani za Ughulati miongoni mwa Waislamu. Maimamu wa Shia (a.s) licha kupingana na imani za Maghulati, pia walisimamisha hoja na vithibitisho kadhaa katika kuwaanika maghulati pamoja na matokeo hatari ya itikadi zao. Wao walizianika njama za Maghulati na wakiwashauri Mashia kujiepusha nao.

Ukirudi katika riwaya, utakuta kwamba Maghulati wametambulishwa kuwa ni makafiri na washirikina. Hadithi hizo wametajwa waja hawa kwa sifa mbaya mno, wao wametambuliwa kama vile viumbe vibaya zaidi vya Mungu ulimwenguni humu. Wanazuoni wa Shia, wakishikamana na riwaya kama hizi, waliamua kujihusisha katika kupambana na Maghulati pamoja na imani zao zilizopitiliza mipaka. Mijadala kuhusiana Ughuhulati imerikodiwa katika vyanzo vya elimu ya Kalam (akida), elimu ya Rijal (elimu ya kutafiti maisha ya wapokezi wa Hadihi), na katika vyanzo vya utambuzi wa madhehebu na makundi ya Kiislamu. Wanafiqhi pia wamejadili kuhusiana na mada ya Ughulati na hatimae kutoa hukumu kuhusiana na watu wenye imani zilizopitiliza mipaka (Maghulati). Kulingana na fat’wa zao, imani yoyote iliyopitiliza mipaka ambayo inasababisha kukataa moja ya msingi ya dini, inachukuliwa kama ukafiri, na wale wanaoamini hivyo wanachukuliwa kama ni makafiri, jambo ambalo hupelekea kuhukumiwa kwa mujibu wa hukumu za ukafiri.

Uchambuzi wa Dhana na Nafasi Yake

Ughulu kiistilahi ni hatua ya mcha Mungu fulani ya kulielezea au kulisifu jambo fulani zaidi ya vile dini yake ilivyo mwagiza. [1] Vile vile katika ufafanuzi wa Ughulati imeelezwa ya kwamba; Ughulati ni kupita kiasi na kutoka nje ya usawa katika kuwasifu Manabii na Maimamu. [2] Neno «غلو» (Ghuluwwu) ni neno la Kiarabu lenye maana ya kupindukia kiwango na kupitiliza mipaka. [3]

Katika Qur'ani, kuna aya mbili zinazozungumzia juu ya Ughulati (kupindukia mipaka), ambapo pia Aya hizo zimekataza suala hilo. [4] Vyanzo vya Hadithi za Shia na Sunni pia vimenukuu Riwaya kadhaa zinazozungumzia imani zilizofurutu ada, ambapo Hadithi hizo pia zimewaonya Waislamu dhidi ya itikadi hizo. [5] Ughulati pia ni mojawapo ya masuala yaliyo jadiliwa na kutafitiwa na wanatheolojia mbali mbali wa Kiislamu, ambao pia wamechunguza asili ya imani hizo na kutoa mifano juu ya matendo ya Ughulati. [6] Kwa kuwa moja ya sehemu ya Ughulati inahusiana na sifa na hadhi za Maimamu watukufu (a.s) na sehemu nyingine inahusiana na dhati yao, ambapo wafuasi wa Ughulati wanajaribu kuwapa Maimamu hao hadhi za kiwango cha Uungu, imekuwa ni jukumu la elimu ya theolojia katika kutoa ushahidi wenye ithibati kamili ili kubainisha mipaka ya sifa stahiki. Ambapo kufanya hivyo ndiko kutakoweza kuelewesha watu katika ni zipi itikadi za Kighulati na waweze kuwasifu waumini wake kwa sifa za Ughulati. [7] Pia elimu ya Rijal ni moja ya sayansi zilizo athiria na gurudumu la Ughulati, na bila shaka wanazuoni wa sayansi hii wamejadili vya kutosha kuhusiana na hilo. [8] Inasemekana kwamba; kwa kuwa moja ya malengo ya elimu hii, ni uchunguzi wa hali za wapokezi walio katika vyanzo na nyaraka za Hadithi, hivyo basi moja ya majukumu ya wataalamu wa elimu Rijal ni kutambua na kugundua, ni wapokezi wepe waliokuwa Maghulati ambao wamejumuishwa katika vyanzo na nyaraka mbali mbali za Hadithi. [9]

Baaada ya sayansi ya tafiti za madhehebu na makundi mbali mbali kutafiti suala la Ughulati na Maghulati, pia sayansi hii imeorodhesha aina mbali mbali za mifano ya matendo ya Ughulati. [10] Wanazuoni wa fiqhi pia wamejadili kuhusu Ughulati na uhusiano wake na ukafiri na kutoa hukumu zinazohusiana na wale wenye imani za Ughulati. [11]

Mifano ya Imani za Ughulati

Wanazuoni wa Kiislamu, kwa kuzingatia Aya za Qur’an, Hadithi, na ripoti za kihistoria, wameainisha mifano kadhaa kuhusiana Ughulati wa kuwakweza kupita kiasi Mitume na Maimamu. [12] Baadhi ya mifano ya imani za Ughulati ni kama ifuatavyo:

Ughulati Katika Imani ya Uungu

Ughulati katika imani ya Uungu ni kama ifuatavyo:

  • Imani ya kuamini kwamba mtu fulani ni Mungu: [13] Kulingana na Aya ya 17 na 72 ya Surat Al-Maa’idah, ni kwamba; imani juu Uungu wa Nabii Isa (Yesu Kristo) ni dai lililopitiliza mipaka (la Kighulati), ambalo Qur’an inalitambua dai hilo kama ni imani ya ukafiri. [14] Vilevile, imani juu ya Uungu wa Imamu Ali (a.s) iliyo buniwa na kikundi cha Sabaa’iyyah (wafuasi wa Abdullah ibn Saba), [15] na imani ya Uungu wa Imamu Swadiq (a.s) ya kikundi cha Khattabiyyah, [16] ni mifano ya imani zilizopitiliza mipaka (za Kighulati), imani ambazo zinachukuliwa kama ni mifano ya ukafiri. [17] Kikundi chanye imani ya «Ithnainiyyah» (uwili au wenza wa Mungu), ni mfano mwingine wa aina hii ya Ughulati. Kulingana na imani za baadhi ya Maghulati, Mtume na Imam Ali wote wawili ni Miungu. Baadhi yao ambao huutanguliza Uungu wa Mtume hujulikana kwa jina la «Mimiyyah» na kundi lili ambalo linautanguliza Uungu wa Imam Ali (a.s) lilijulikana kwa jina la «Ainiyyah». [18]
  • Kuamini kuwa; mtu fulani aina fulani ya anashirika katika Uungu wa Mungu: [19] Imani ya kuyafawisha mamlaka ya Mungu kwa mtu mwengine imetajwa kama ni mfano wa aina hii ya imani ya kupindukia mipaka (Ughulati). [20] Kwa maana moja, imani ya kuyafawidhishwa kwa mamlaka ya Mungu ni kule kuamini kwamba; Mwenye Ezi Mungu alimuumba Mtume Muhammad (s.a.w.w) na Imam Ali (a.s), kisha akawakabidhi wao baadhi ya mamlaka ya mambo fulani kama vile; uumbaji, kifo, maisha, na riziki kwa viumbe wake. [21]
  • Imani ya Mungu kuingia katika mwili wa mtu fulani au kuungana naye (Imani juu ya Hululi «حلول»): [22] [Maelezo 1] Imani za kikundi cha Bayaniyya zinachukuliwa kama aina ya Ughulati. [23] kundi hili kiasilia ni tawi litokanalo na kundi la Kisaniyyah ambalo liamini juu ya imani ya Hululi, isemayo kwamba; roho ya Mwenye Ezi Mungu huingia katika miili ya manabii, pia roho hiyo imemwingia Imamu Ali, pamoja na Muhammad bin Hanafiyyah. [24] Muasisi wa kundi hili alikuwa ni Bayani bin Sam’ani Tamimi. [25] Yeye alikuwa akiamini ya kwamba; roho ya Mwenyezi Mungu ilimuingia ndi ya mwili wa Imamu Ali na uwepo wa roho ya Mungu, ndio uliomfanya yeye kuwa ndio dhihiriko la nguvu za mbinguni ambapo kupitia nguvu hizo yeye aliweza kuung’oa mlango wa ngome ya Khaybar, si kwamba yeye aliweza kufanya hivyo kupitia nguvu za kimwili, bali kwa nguvu ya rehema na mbinguni zilizodhihirika kama nuru ya kiungu ndani yake. [26] Pia, aliamini kwamba; kuna sehemu fulani ya Mungu iliyomuingia Imam Ali (a.s) na sehemu hiyo hiyo ndiyo iliyomuingia Nabii Adam (a.s), hivyo kumfanya yeye (Adamu) astahili kusujudiwa na malaika. [27]
  • Imani ya kuamini kwamba mtu fulani ni mwana wa Mungu: [28] Inasemekana kwamba kuna makundi matatu yanayoamini kwamba Mungu ana mwana: 1. Wakristo ambao kulingana na ripoti ya Qur’ani katika Aya ya 30 ya Surat At-Tawba ni kwamba; Wakristo wanamchukulia Nabii Isa (Yesu) kuwa mwana wa Mungu. [29] 2. Kundi la pili ni Wayahudi ambao kulingana na Aya hiyo hiyo, wanamchukulia Uzairu kuwa ni mwana wa Mungu. [30] 3. Kundi la tatu ni washirikina wa Kiarabu, ambao kulingana na Aya ya 57 ya Surat Al-Nahl na Aya ya 149 ya Surat Al-Saffaat, wao wanawachukulia malaika kuwa ni binti za Mungu. [31]

Ughulati katika Utume na Uimamu

Hapa kuna baadhi ya imani na mawazo ya Ughulati juu ya Utume na Uimamu:

  • Imani ya Utume kwa Maimamu wa Shia: [32] Baadhi ya vyanzo vya itikadi vinasema kwamba madhehebu ya «Ghurabiyya», «Dhubiyya» na «Mukhti-a», ambayo yanachukuliwa kuwa ya madhehebu ya Maghulati, yanaamini kwamba; Kiuhalisia Utume ulikuwa ni haki ya Imamu Ali (a.s). Makundi haya yalidai kwamba; Jibril alikosea wakati wa kushuka kwa Wahyi, jambo lilitokea kwa sababu ya kufanana sana kati ya Imam Ali (a.s) na Mtume (s.a.w.w), na badala ya kumshushia Ali akamshushia bwana Mtume. Na Mtume, ili kumfurahisha Imam Ali, alimpa binti yake na kufunga ndoa naye. [33]
  • Imani ya Ushirikiano na Mtume katika Utume: [34] Al-Maqrizi (aliye ishi baina ya 1364 na 1422 Hijiria), ambaye ni mwanahistoria wa Misri, katika kitabu chake «Al-Mawa'idhu wa al-I'itibar fi Dhikr al-Khitatu wa al-Aathar», anasema kwamba; Madhehebu ya «Sharikiyya», «Shaa'iyya» na «Khuuliyyah» ni miongoni mwa madhehebu ya Shia ya Maghulati. Kwa mujibu wake; Maghulati hawa waliamini kuwa Imamu Ali (a.s), alikuwa ni mshirika wa Mtume katika Utume. [35] Hata hivyo, baadhi ya watu wana shaka kuhusu kuwepo kwa madhehebu yenye majina miongoni mwa madhehebu ya Ushia. [36]
  • Kujitambua kama ni Mtume au Imamu kwa Njia ya Udanganyifu: [37] Hii inahusiana na mtu ambaye si Nabii wala Imamu, lila yeye akajitambulisha mwenyewe mbele za watu kama ni Imamu au Nabii: Kwa mfano, waandishi wa madhehebu wamemtaja mtu anayeitwa «Abu Mansur ‘Ijli» ambaye baada ya kifo cha Imamu Baqir (a.s) alidai kwamba; Imamu Sajjad (a.s) alimtambulisha kama ni wasii na Imamu baada ya Imam Baqir. [38] Kisha akasema kwamba; Imamu Ali, Imamu Hassan, Imamu Hussein, Imamu Sajjad, na Imamu Baqir (a.s), walikuwa ni Mitume na Manabii, kisha akajitambulisha yeye mwenyewe pamoja na watoto wake sita watakaofuata baada yake kama ni Manabii. [39]
  • Kumuitakidi mtu fulani kuwa ndiye Mahdi aliyetabiriwa hali akiwa ni Mahdi bandia: Miongoni mwa watu ambao wamedaiwa kuwa ni Mahdi, ni Muhammad bin Hanafiyya. [40] Kulingana na waandishi wa wanao jihusisha na kazi za rikodi na uchambuzi wa madhehebu mbali mbali, ni kwamba; wafuasi wa madhehebu ya Karbiyya (tawi la Kisaaniyyah) waliamini kwamba; Muhammad bin Hanafiyya ndiye Mahdi aliyetabiriwa, ambaye yupo mafichoni na hatimaye atafichuka kutoka mafichoni mwake na kujaza dunia haki na uadilifu baada ya kuwa imejaa dhuluma na ukandamizaji. [41] Pia, Muhammad bin Abdullah bin Hassan, maarufu kama Nafsu Zakiyya ni miongoni mwa watu wengine ambao waliodaiwa kuwa ni Mahdi mtarajiwa. [42] Kulingana na mawasilisho ya maandishi yalio wasilishwa na waandishi wanaotafiti madhehebu mbali mbali, ni kwamba; wafuasi wa kikundi cha «Mughairiyya» (wafuasi wa Mughaira bin Said al-Bajali) waliamini kwamba; Nafsu Zakiyya ndiye Mahdi aliye tabiriwa katika vyanzo mbali mbali, na baada ya kuuawa kwake, walidai kwamba yeye hajafa bali anaishi mafichoni na atadhihiri tena kutokea mlimani, kwani kwa muda yeye yupo kwenye mjini «Alamiyyah» ulioko mjini Makka. [43]

Ughulati wa Kuzidisha Chumvi Katika Kotoa Wasifu wa Mtu Fulani

Ughulati au kuongeza chumvi katika kumsifu mtu fulani, kwa kiasi kikubwa humaanisha kumhusisha mtu huyo na sifa, matendo, au wasifu ambao hastahili kusifiwa nao. [44] Baadhi ya mifano ya aina hii ya kutia chumvi kupita kiasi, katika kuwasifu viongozi wa dini, Manabii, na Maimamu 12 kama ifuatavyo:

  • Imani ya kukataa uwezekano wa Mtume kusahau: [45] Kulingana na maelezo ya watafiti, ni kwamba; Mzozo mkubwa zaidi upo katika sifa zinazohusishwa na Maimamu (a.s). Malumbano makali zaidi katika uwanja huu yalikuwa kati ya madhehebu ya fani ya kalamu ya chuo cha Qom na madhehebu ya fani ya kalamu ya chuo cha Baghdad katika karne ya tatu na nne. Vyuo viwili hivi vilikuwa vikichuana katika kuafiki imani ya kuwepo kwa uwezekano wa Mtume kusahau au kuto kuwepo kwa uwezekano huo. [46] Sheikh Saduqu anamnukuu mwalimu wake Ibn Walid Qummi akisema kuwa; kiwango cha kwanza cha Ughulati, ni kusema kwamba Mtume hasahau, na yeyote asiyeikubali dhana hiyo kuhusiana na Mtume anahisabiwa kuwa ni mmoja wa Maghulati. [47] Kinyume na mtazamo huu, Sheikh Mufidu ni miongoni mwa wanazuoni wa madhehebu ya Baghdad. [48] Sheikh Mufid anakataa dhana ya kukosea kwa Mtume (s.a.w.w) na ameshutumu wale wanaoamini hivyo kwa kule kuihujumu dini na kuvunja hadhi ya Maimamu (a.s.). [59] Yeye anapingana tu na imani ya kuwapa Maimamu (a.s.) sifa za Uungu na kuwahisabu kuwa ni watangu na tangu, na mambo hayo kwa mtazamo wake ni ndiyo mambo yanayomtumbukiza mtu katika Ughulati. [50]
  • Imani juu elimu ya ghaibu isiyo na mipaka: [51] Baadhi ya wanatheolojia wa Shia wanaamini kuwa Maimamu 12 ni wenye elimu ya ghaibu, kwa mtazamo wa wanatheolojia hao; mbali na wao kuwa na eleimu kuhisiana na hukumu za jumla za Uislamu, pia wanajua matukio yote madogo madogo ya ulimwengu huu, na pia wanajua kila kitu kilichokuwepo katika zama zilizopita na kilochopo katika zama zilizopo. [52] Sheikh Mufid ameihisabu imani kama ni imani ya Kighulati iliyopitiliza mipaka, na kuwahukumu wanaoshikilia mtazamo huu kuwa ni Maghulati. Sheikh Mufid anaamini kwamba; sifa hii ya kuwa na elimu ya ghaibu, ni sifa maalum inayomstahikia Mwenye Ezi Mungu peke yake. [53] Hata hivyo, baadhi yao wamesema kwamba; Ughulati ni kule mtu kuwa na madai ya kuwa Maimamu wala elimu ya ghaibu yenye kujitegemea, bila ya kupata mafunzo ya Kimungu. Wao wanaamini kwamba aina hii ya elimu ya ghaibu ni maalum kwa Mwenyezi Mungu pekee, na elimu na maarifa yote ya manabii na Maimamu ni kwa idhini na kwa kupitia mafunzo ya Kimungu, na haiwezekani mtu kuwa na elimu hiyo bila ya idhini ya Mungu. [54]
  • Imani ya kuamini kuwa Maimamu ni wenye kuishi milele: [55] Nubakhti katika kitabu chake Firaqu al-Shia amerejelea kikundi kiitwachoitwa Bashiriyya ambacho kilidai kwamba Imamu Musa Kadhim (a.s) hakufariki, na badala yake walikuwa wakiaamini kuwa; yeye ndiye Mahdi aliyetabiriwa, ambaye yupo mafichoni na kwamba atadhihiri pale utakapofika wakati wa kudhihiri kwake. Wao walikuwa wakiamini kuwa Imamu Kadhim (a.s) alimteua Muhammad bin Bashir (mwanzilishi wa kikundi hiki) kuwa ni wasii na mrithi wake, na kwamba yeye (Imamu Kadhim (a.s)) amempa pete yake na elimu yake na akamkabidhi kila kitu ambacho watu wanahitajia katika mambo yao ya kidini na kidunia. [56] Pia kulingana na maandishi ya Nubakhti, pia kuna kikundi kiitwacho Kisaaniyya ambacho kiliamini kwamba; Muhammad bin Hanafiyya hakufariki dunia, bali yuko hai na anaishi katika mlima uitwao «Mlima Ridhawi» uliopo kati ya mji wa Makka na Madinah. [57]

Madai Mengine ya Ughulati

Madai mengine ya Kighulati yanayohusiana watu wengine wasio Manabii na Maimamu ni kama ifuatavyo:

Ughulati Katika kuwasifu Makhalifa

Katika baadhi ya vyanzo vya Ahlul-Sunna, kuna Hadithi au madai yalionukuliwa kuhusiana na sifa za makhalifa watatu, ambazo kwa maoni ya baadhi ya wanazuoni, ni za kupindukia mipaka (za Kighulati). [58] Kwa mfano, katika kitabu cha Tarikhu al-Baghdad, kumenukuliwa Hadithi ambayo inanasibishwa na bwana Mtume (s.a.w.w), ambayo kwa mujibu wake ni kwamba; Mbwana Mtume (s.a.w.w) alipokwenda safari ya Mi’iraji, katika usiku huo wa Mi’raj aliiona juu ya Arshi ya Mungu kumeandikwa La ilaha illallah Muhammadur rasulullah, na baada yake kukeandikwa majina ya Abu Bakr, Omar bin Khattab na Othman. [59] Naematullah Salehi Najafabadi ameihukumu sanad ya Hadithi hii kuwa ni dhaifu na maudhui yake kuwa ni maudhui ya Kighulati yenye kupindukia mipaka. [60]

Pia katika kuisifu elimu ya Omar bin Khattab imesemwa ya kwamba; ikiwa elimu ya dunia nzima itawekwa kwenye upande mmoja mizani, na elimu ya Omar iwekwe kwenye upande wa pili wa mizani, basi elimu yake itapiku na kupidukia uzito wa elimu hiyo. [61] Pia imesemwa kwamba; katika mwaka wa ishirini Hijria, yaani wakati wa utawala wa Omar bin Khattab huko Madina kulitokea tetemeko la ardhi na Omar akaipiga ardhi kwa mjeledi wake na kusema: «Ewe ardhi tulia kwa idhini ya Mola». Kisha ardhi ikatulia, na tangu mwaka huo hakukutokea tena tetemeko la ardhi katika mji wa Madina. [62] Baadhi ya wahakiki wanayachukulia maudhui ya madai haya kuwa ni madai ya Kighulati. [63] Pia kuna sifa na madai mbali mbali ya Kighulati yalio nukuliwa kuhusiana na masahaba na makhalifa wengine. Abdul-Hussein Amini katika kitabu cha Al-Ghadir akirejea kwenye vyanzo vya Ahlu-Sunna na ameorodhesha baadhi ya matendo kama haya ya Kighulati na kuyachukulia kuwa ni matendo ya kupitiliza mipaka ambayo hayakubaliki katika dini ya Kiislamu. [65]

Tafsiri Zilizofurutu Ada Katika Kuifasiri Qurani

Inasemekana kuwa moja ya mambo ya Kighulati ni kule kuipotosha tafsiri na kuikiusha maana ya Aya za Qurani ili kuthibitisha uwepo wa maisha mapya ya duniani baada ya kifo (incarnation). [66] Kulingana na maelezo ya Baladhuri, mwanahistoria wa karne ya pili na ya tatu Hijria, katika kitabu chake «Ansaab al-Ashraaf», ni kwamba; wafuasi wa nadharia ya kuwepo kwa maisha mengine ya kidunia baada ya kifo, wametumia sehemu ya Aya ya 8 ya Surat al-Infitar isemayo: «فِي أَيِّ صُورَةٍ ما شاءَ رَكَّبَكَ ; Yeye amekujenga (wewe) katika sura yoyote ile aliyo itaka»;, katika kuthibitisha nadharia yao hiyo. [67] Pia, Fakhur al-Razi katika tafsiri yake ya Qu’rani amesema kwamba; moja ya Aya zinazotegemewa na wafuasi wa nadharia ya wafu kurudi tena katika maisha ya duniani baada ya kufa kwao, ni Aya ya 38 ya Surat al-An’am. [69] Fakru al-Razi ameendelea kwa kusema kwamba; kuwa matumizi haya ya Aya hii si matumizi yenye ithibati halali, na ni matumizi batili yasio na msingi madhubuti katika kuthibitishwa itikadi hiyo. [70]

Katika baadhi ya matukio, kumetumika tafsiri potofu za Qurani ili kuelezea sifa za zilizo pindukia juu ya ya watu fulani. [71] Kulingana na maelezo ya Abdul-Hussein Amini kutoka kitabu cha «Al-Umdah fi Tafsir al-Hurufi al-Muqatta’ah» kilichoandikwa na Ibrahim bin Amir ‘Ubaidi, mwanachuoni wa Kisunni wa karne ya kumi na moja, yeye alipokuwa akielezea tafsiri ya herufi za kiarabu za «Alif Lam Mim» katika Aya ya kwanza ya Surat al-Baqarah, imeelezwa kuwa «Alif» inamaanisha Abu Bakar, «Lam» inamaanisha Allah, na «Mim» inamaanisha Muhammad (s.a.w.w). [72] Amini ameyahisabu madai haya na tafsiri hii kuwa ni za kupindukia mipa na ni moja ya matendo ya Kighulati. [73]

Isma’il Haqqi al-Bursawi, ambaye ni mmoja wa wafasiri wa madhehebu ya Hanafi, aliye fariki mwaka 1137 Hijria, katika tafsiri yake iliyopewa jina la “Ruh al-Bayan,” alinukuu Hadithi kutoka kwa bwana Mtume (s.a.w.w) kuhusu Aya isemayo: (وَيَحْمِلُ عَرْشَ رَبِّكَ فَوْقَهُمْ يَوْمَئِذٍ ثَمَانِيَةٌ ; Na siku hiyo Arshi ya Mola wako itachukuliwa na kubebwa juu ya Malaika wanane). [74] Katika Hadithi hii imeelezwa wa kwamba; Wachukuzi wa ‘Arshi hiyo duniani humu ni wanne, ambao siku ya Kiyama Mwenyezi Mungu atawathibitisha pamoja na wanne wengine. [75] Baadaye, anaendelea kusema; wanne hawo ni: Abu Hanifa, Malik bin Anas, Muhammad bin Idris al-Shafi’i, na Ahmad bin Hanbal, ambao wanachukuliwa kuwa nio wabebaji wa sheria. [76] Watafiti wameona kuwa njia hii ya tafsiri si njia ilio nyooka, bali ni ya kupindukia mipaka na ni tafsiri ya Kighulati. [77]

Imani ya Njama za Kuondoa Sifa za Maimamu Kutoka Kwenye Qur’ani

Muhammad Jawad Mashkur (aliye fariki mwaka 1374 Shamsia), mwanahistoria na profesa wa Chuo Kikuu cha Tehran, katika kitabu cha Historia ya Shia na Madhehebu ya Kiislamu amesema kuwa; baadhi ya wafuasi wa Shia, wanadhani kuwa Qur’ani iliyopo mikononi mwa waislamu hivi sasa, ni Qur’ani iliobadilishwa na wanadai kwamba, ukusanyaji wa Qur’ani ulifanyika wakati wa Utawala wa Othman na umepelekea kuondoa na kubadilishwa sehemu kubwa ya Aya zake, ikiwa ni pamoja na Aya zinazohusiana na sifa na nafsi ya Ali bin Abi Talib (a.s) na familia yake. Pi yeye amesisisitiza juu ya ubatilifu wa mtazamo huu. [79]

Mohammad Hassan Ahmadi, mtafiti wa masomo ya Hadithi na Qur’ani, katika makala yenye jina la «Ghaaliane wa Andishe Tahrife Qur’an», amechunguza wapokezi ambao wanaonekana katika mlolongo wa nyaraka za Hadithi zinazo husiana na dhana ya kupotoshwa kwa Qur’ani katika vyanzo vya Shia. Yeye makalani humo amechunguza iwapo wapokezi hao wanahusika na Ughulati au la, ambapo ameweza kugundua orodha ya watu kumi na tatu ambao anaamini kwamba wanaweza kuwa na athari za Ughulati miongoni mwa wapokezi hao. Mohammad Hassan Ahmadi anaamini kwamba; kutoka kwenye jumla ya Hadithi zilizo nukuliwa kuhusiana na upotoshwaji wa Qur’ani, idadi kubwa ya Hadithi hizo (karibu theluthi mbili), zimepokewa kutoka kwa Maghulati. [81]

Madai ya Kupindikia Mipaka Katika Kusifu Vitabu Fulani

Kitabu maarufu kiitwacho Sahihi Bukhari, ni moja ya vyanzo vya Hadithi vinavyoheshimika miongoni mwa Waislam wa madhehebu ya Sunni, kitabu ambacho ni miongoni mwa vitabu vilivyo sifiwa kwa sifa za kupindukia mipaka. [82] Kitabu hicho kimeelezwa kuwa hadhi yake ni sawa na hadhi ya Qurani, na iwapo kitabu hicho kitasomwa nyumbani wakati wa janga la tauni, basi watu wa nyumba hiyo watakingwa na ugonjwa huo wa tauni, na yeyote atakaye kisoma na kuhitimisha hitima moja ya kitabu hicho, basi bila shaka Mwenye Ezi Mungu atampa matilaba yake. [83] Pia baadhi ya watu wameeleza kuwa; Iwapo kitabu hicho kitakuwepo kwenye nyumba fulani, hiyo itakuwa ndio sababu ya kushuka kwa rehema na kuimarisha baraka nyumbani humo. Pia imedaiwa kuwa Sahihi Bukhari ndio kitabu sahihi zaidi duniani baada ya Qur'ani. [84] Pia kuna kuna aina kadhaa za maneno kama haya ya kupindukia kuhusiana na kitabu cha Muwatta kilichoandikwa na Malik bin Anas, ambapo imesemwa kuwa; kitabu hichi ndio kitabu makini zaidi baada ya Qurani, na kwamba hakuna kitabu sahihi zaidi duniani kuliko hicho. [85]

Pia kuhusu kitabu cha Al-Kafi, kutoka kwa vyanzo vya hadithi vinavyokubalika miongoni mwa wafwasi wa madhehebu ya Washia, kuna madai yasemayo kwamba; Hadithi zote zilizomo ndani yake ni sahihi, na zenye ithibati zinakubalika. [86] Madai haya yamekabiliwa na upinzani kadhaa kutoka kwa baadhi ya wanazoni wa Kishia. Miongoni mwa wanazuoni wanaopinga madai haya na kuyahisabu kuwa ni ya Kighulatin ni Ni’imatullah Salehi Najafabadi. Pia Salehi Najafabadi amepinga kauli zisemazo kwamba; maandishi ya kitabu cha Al-Kafi yalikabidhiwa kwa Imamu Mahdi (a.j.t.f), naye baada ya kuyatupia macho akasema: (الکافی کافٍ لِشیعتُنا ; Kwa kweli kitabu cha al-Kafi ni chanzo tosha kwa Mashia wetu). [87] Najafabadi akirejelea bayana kutoka kwa Allama Majlisi [88] na Muhaddith Nuri, [89] amepinga kauli hii na akasema kwamba; maneno haya ni maneno yasiyo na msingi na ni ya Kighulati yenye kupindukia mipaka. [90]

Madai ya Kighulati Kuhusiana na Wasifu wa Wanazuoni

Pia kuhusu wanazuoni wa dini, mara nyingine kumekuwa na madai ya Kighulati ya kudai kuwepo kamarama na miujiza kutoka kwa baadhi ya wa wanazuoni hao. [91] Kwa mfano, imesemwa kwamba; siku kila asubuhi Nabii Khidr alikuwa akija kwa Abu Hanifa kwa miaka mitano mfululizo na kumfundisha sheria za Kiislamu. [92] Pia wamedai kuwa; Bwana Mtume (s.a.w.w) alisema: ‘Mitume wote wanajifakharisha nami, nami najifakharisha na Abu Hanifa’. [93] Kwa mujibu wa maelezo ya Abu Zahra, mwanahistoria na faqihi wa Misri wa karne ya kumi na nne Hijria, upendeleo au ushabiki pofu kwa Abu Hanifa ulikuwa ni mkubwa mno, kiasi ya kwamba baadhi ya watu walimwona kuwa hadhia yake ni karibu na hadhi ya bwana Mitume (s.a.w.w), na wakadhani kuwa yeye alitabiriwa ndani ya Taurati na kwamba bwana Mtume (s.a.w.w) alimtaja kwa jina na kumtambua kama ni kiongozi atakaye uongoza umma. [94] Kauli kama hizi zimekuwa zikisemwa pia kuhusiana wanazuoni wengine wa madhehebu manne ya Kisunni na baadhi ya mafaqihi wa Kisunni. [95] Abdul-Hussein Amini katika kitabu chake cha Al-Ghadir, [96] ameainisha na kuorodhesha baadhi ya kauli hizi katika kitabu chake hicho, ambapo yeye anaamini kuwa kauli hizo zinaashiria Ughulati katika upendeleo wa kuwapenda watu kama hao, na anaamini kuwa kauli hizo ni kauli za uongo zisizo na mashiko. [97]

Uhusishaji wa Imani ya Kighulati kwa Mashia

Baadhi ya wanazuoni wamehusisha imani za Kighulati za kupindukia mipaka kwa Mashia, baadhi ya waliofanya hivyo kama ifuatavyo: [98]

  • Abu Omar bin Muhammad bin Abd Rabbeh, ambaye ni mwanazuoni wa Kisunni wa karne ya nne Hijria. Mwanazuoni huyu katika kitabu chake ‘Aqdu al-Farid’, amewafananisha Mashia na Wayahudi, akisema kwamba; Shia ni kama Wayahudi, kwani wao wanamchukulia Jibril kama ni adui ambapo wanaamini kwamba; Jibrilu alileta ufunuo kwa Mtume kimakosa, kwani kiasili yeye alitakiwa kuushusha Wahyi huo kwa Imamu Ali (a.s). Katika kujibu madai haya, imeelezwa kwamba; wataalamu wa masuala ya madhehebu wamehusisha imani hii na makundi yaliyoitwa «Dhubaabiyya», «Ghuraabiyya», na «Mukht-ia». [100] Sayyid Muhsin Amin ameona suala la kuyahusisha makundi haya na Shia, ni madai yasiyo na msingi wowote, akidai kwamba yeye hajawahi kuona majina ya makundi kama hayo katika mojawapo ya maandiko ya Shia yaliyotungwa katika kutafiti madhehebu mbali mbali. [101] Yeye pia anaamini kwamba; majina ya makundi haya yalitungwa kwa nia mbaya ya kuipaka matope na kuyaponda madhehebu ya Shia. [102]
  • Abu Muhammad Othman bin Abdullah al-Iraqi, mmoja wa wanazuoni wa madhehebu ya Hanafi wa karne ya tano Hijria, katika kitabu chake kiitwacho «Al-Firaqu Al-Muftaraqah», aliayahisabu madhehebu ya Imamiyyah na Zaidiyyah kuwa mamoja, na akasema kuwa; wao ni kundi la watu ambao mara maoja humfanya Imamu Ali kuwa ni Mungu, na mara nyingine humfanya ni Mtume, na pia mara nyengine humfanya yeye kuwa ni mshirika wa Mtume (s.a.w.w.) katika suala la unabii. 103[] Ibn Taymiyyah pia alipokuwa akiwalaumu Mashia kwa itikadi zao za kupindukia mipaka na Kighulati, alisema kwamba; kuna kundi la Mashia wanaomwamini kuwa Imamu Ali ni Mungu, na wengine humwamini kuwa ni Mtume. [104] Katika jitihada za kaujibu tuhuma hizo, imeelezwa kwamba; kuna idadi ndogo tu ya watu wenye imani kama hizo, ambao hata hivyo walikemewa na kukataliwa na Riwaya mbali mbali za Shia, pia walikanushwa na kutengwa na Imamu wa madhehebu ya Shia. Hivyo basi si sahihi kuhusisha imani ya kundi hilo dogo lililofukuzwa na kutengwa na Mshia wote, hasa Imamiyyah. [105] Katika madhehebu ya Imamiyyah, imani kwamba Imam Ali (a.s) ni Mungu au ni Mtume, itikadi ambazo hupelekea kukataa uwepo wa Mungu na unabii wa bwana Mtume (s.a.w.w), zinachukuliwa kuwa ni miongoni mwa fikra kikafiri, na wale walio na imani hizo nao huhisabiwa kuwa ni makafiri. [106]
  • Abdullahi Ali Qamisi, mwandishi na mtafiti wa Kiwahabi, katika kitabu chake kiitwacho «Al-Sirau Baina al-Islami wa al-Wathaniyya», amesema kwamba; kuna kundi la Mashia wanaoamini kuwa makatazo maamrisho ya kidini kidhahiri huonekana kama ni amri za kisheria tu, bali kuihalisia humaanisha kujenga mapenzi na watu fulani na kuwachukia watu fulani. Hiyo ndio sababu ya wao, kuhalalisha makatazo ya Mungu na kuto telekeza faradhi za Mungu. [107] Waandishi na watafiti wa madhehebu mbali mbali, wamehusisha imani hii na kundi la Maghulat liitwalo Firqat al-Mansuuriyya (wafuasi wa Abu Mansur al-‘Ijli). [108] Abu Mansur anasemekana kuwa alilaaniwa mara tatu na Imamu Sadiq kutokana na mawazo yake na fikra zake za kupindukia mipaka (za Kighulati). [109]
  • Kikundi cha wanazuoni wa Ahlu-Sunnah wameona kuwa; imani kama vile imani ya Badaa (kughairi), Raj’ah (kufufuka kabal ya siku ya Kiama), ‘Ismah na imani ya ‘Ilmu al-Ghaib ya bwana Mtume na Maimamu watoharifu (a.s), -ambaza ni miongoni mwa imani za Shia kuwa- ni miongoni mwa imani za Kighulatia za kupindukia mipaka. [110] Wanazuoni wa Shia hawajaziita imani hizi kuwa ni imani za kupindukia mipaka au za Kighulati, na wametoa ithibati kadhaa kutoka katika Qur’ani, Sunnah pamoja na hoja za akili katika kuthibitisha imani zao hizo. [111]
  • Baadhi ya watu wanaamini kuwa baadhi ya sifa kama vile Umaasumu, elimu ya ghaibu, utendaji wa wa kuleta mabadiliko karika ulimwengu ambao kiuhalisia huwa uko mikononi mwa Mungu, pamoja na baadhi ya sifa zinazokiuka sifa za kawaida za kibinadamu, ambazo zinazohusishwa na Maimamu wa Kishia, ni sifa za Kighulati za kupindukia mipaka. Wao wanashikilia imani kwamba; Maimamu ni watu wakawaida, ambao walikuwa tu ni wasomi wakubwa na wenye kujiepusha na maovu, na ni wajuzi wa sharia za Kiislamu. [112] Mtazamo huu kiumaarufu huitwa ni mtazamo wa «wanachuoni wema». [113] Yaani ni mtazamo onaowahisabu Maimamu kama ni wanazuoni wema tu. Asili ya nadharia hii inaaminika kuwa ni maneno ya Abdullah bin Abi Ya’afur ambaye alitumia ibara ya Kiarabu isemayo «علماءُ اَبرار و اَتقیا اوصیا ; Wanazuoni wema wachamungu na mawasii» [114] kuhusiana na Maimamu watakatifu. [115] Pia, imeelezwa kuwa baadhi ya wanazuoni wa Kishia, hasa wanazuoni wa chuo cha Qom katika karne ya tatu na nne Hijria, walipinga vikali kuhusisha sifa za kupindukia sifa za kibinadamu katika kuwasifu Maimamu, na badala yake waliwahisabu na kuwaona kuwa ni wanazuoni wema na wenye kujiepusha na maovu tu. [116] Nadharia hii imekosolea kwa namna mbali mbali; ikiwa ni pamoja na ukosefu wake wa ushahidi wa kihistoria. [117] Pia baadhi ya wanazuoni wamesema kuwa; katika fasihi ya baadhi ya Masahaba wa Maimamu (a.s), neno «عالِم» (mwanachuoni), linamaanisha elimu ya Ilhamu (ya Kiungu) walio nayo Maimamu (a.s), na maneno «ابرار» (watu wema) na «اتقیا» (wachamungu) yana maana ile ile ya ucha Mungu. [118]

Ughulati wa Kuwasifu Wapokezi wa Hadithi kwa Sifa za Kupindukia Mipaka

Ughulati na kuwa na imani upotofu ni miongoni mwa mambo ambayo katika elimu rijali (elimu ya tafiti juu ya maisha na sifa za wapokezi wa Hadithi), hupelekea mpokezo wa Hadithi kukataliwa Hadithi zake ambapo hupelekea Hadithi za kuhizabiwa kuwa ni Hadithi dhaifu zisizo na ithibati aminifu. [119] Kulingana na maelezo ya Sayyid Hussein Madrasi Tabatabai, mtafiti wa elimu za Kiislamu, ni kwamba; kawaida watu ambao waliwahisabu Maimamu (a.s) kuwa ni Miungu (ambao kiumaarufu walijulikana kama ni Maghulati wa nje ya madhehebu), hutambulika katika vitabu vya rijali vya Shia, kwa majina maalumu kama vile; «Fasidu al-Madhab» au «Fasid al-I’tiqadi». Na wale Maghulat wa ndani ya madhehebu fulani ambao wakati mwengine huitwa Mufawwidha, wao hutambulikana kwa majina kama vile; «Ahl al-Irtifa», «Murtafu’ al-Qawl», na «Fi Hadithihi Irtifa’u». [120]

Inasemekana kwamba; mara nyingi huwa kuna tofauti kati ya wanazuoni wa Hadithi katika kumhusisha mpokezi wa Hadithi fulani na sifa za Kighulati, na ikiwa hali ya wapokezi fulani watakuwa na utata katika kuhusika kwao na sifa za Kighulati, basi Hadithi zilizozisimuliwa na wapokezi hao zinabaki bila ya kuwa na uhakika katika ithibati zake; isipokuwa pale tu ambapo sababu thabiti za kukataa au kuthibitisha uhalali wa Hadithi hizo zitapatikana kutoka mahali pengine. [121] Baadhi ya misingi na asili ya tofauti hizi za maoni katika kumhusisha mpokezi fulani wa Hadithi na upotovu wa Kighulati, huwa inatokana na tofauti za kiufahamu na nadharia katika tafsiri za wanazuoni wa Hadithi kuhusiana dhana ya Ughulati. [122]

Katika mifano ya tofauti za kinadharia katika kumhusisha mpokezi fulani wa Hadithi na Uhgulati zinazo patikana katika vitabu vya rijali, ni kuhusiana na habari za Hussein bin Abdullah Saadi al-Muharrir, ambapo katika kitabu kiitacho “Rijalu al-Kashi’ mpokezi huyo ambaye ni mmoja wa wanapokezi wa Hadithi wa madhehebu ya Shia katika zama za Imam Hadi (a.s), ameelezwa katika kitabu hichi kuwa yeye alifukuzwa kutoka mji wa Qum kwa makosa ya Ughulati. [123] Najashi kuhusiana naye amesema kuwa; mpokezi huyu alipachikwa tuhuma za kuwa na Uhgulati, ila yeye ni mtu mwenye vitabu sahihi na vya kuaminika. [124] Wanazuoni kama vile Abu Ali Ha’iri na Ma’maqani hawakukubaliana na tuhuma hizo dhidi ya mpokezi huyu. Wao wanaamini kuwa tuhuma hizo ziliyotolewa na wanazuoni wa chuo cha Qum katika karne ya tatu na nne Hijria kuhusiana na Ughulati wa mpokezi huyu, au kufukuzwa kwake kutoka Qum, si tuhuma za kuaminika na kutegemeka, na wala hazimaanishi udhaifu wa mpokezi huyu wa Hadithi; kwani imani fulani ambazo zilichukuliwa kuwa ni za kupindukia mipaka (za Kighulati) kuhusiana naye, wanazuoni waliokuja baadae, walizichukulia imani hizo kama ni ndio imani msingi katika madhehebu ya Shia, ambazo miongoni mwake ni; kipanga sulala kusahau kwa Mtume (s.a.w.w). [125]

Kwa mtazamo wa Sayyid Khui ni kwamba; Ughulati ni wenye daraja na viwango tofauti, akielezea viwango hivyo amesema kwamba; yawezekana akapatikana mtu mwenye dara ya chini ya Ughulati ambaye yeye mwenyewe akajidhania kuwa yupo sawa na kumlani yule mwenye daraja ya juu zaidi na kumuona kuwa ni Ghulati mwenye kupindukia mipaka. [126]

Ni’imatullah Safariy Furushani, mtafiti na mwanachama wa bodi ya watafiti wa mambo ya kihistoria za kidini katika chuo cha Qom, kupitia utafiti alio ufanya kuhusiana na kitabu cha Mujamu al-Rijal al-Hadith kilichoandikwa na Sayyid Abu al-Qasim al-Khui, ameeleza kwamba; Kuna takriban idadi ya wapokezi 120 ambao wamekumbwa na tuhuma za Uhgulati katika vitabu vya wapokezi wa Kishia. [127] Ni’imatullah Safariy Furushani anaamini kwamba; kumtuhumu mpokezi fulani kwa tuhuma za upotovu wa Kighulati, hakumaanishi kuthibitika kwa upotovu huo dhidi ya mpokezi huyo wa Hadithi. [128]

Msimamo wa Mashia Dhidi Gurudumu la Ughulati

Maimamu wa Kishia, katika mazingira tofauti, walijitahidi kupigana dhidi ya mafundisho ya Kighulati ya kupindukia mipaka kwa nia ya kutokomeza aina zote za mawazo ya kupindukia. [129] Katika makala yenye jina lisemalo: “Barresi Cheguunegi Taqaabule A-immeh Baa Jarayaanhaaye Ghaaliyaan” “Uchunguzi wa jinsi Maimamu Wanavyokabiliana na Mafundisho ya Kupindukia Mipaka ya Kighulati” imeelezwa ndani yake njia za kukabiliana na mafundisho ya kupindukia mipaka kutoka kwa Maimamu wa Kishia. Hatua ya mwanzo katika kukabilia na Maghulati, ilikuwa ni kuweka wazi na kuanika uhakika wa Maghulati kupiti Hadithi zilizosimuliwa kutoka kwao (Maimamu), [130] Hadithi ambazo zilikusudia kupambana na Ughulati ilikuwa kwa malengo ya kuwaweka watu mbali na Ughulati wao, kupitia hatua tofauti, miongoni mwazo ni; kufafanua na kuuchambua Ughulati, kuwakanusha na kuwakataa, pamoja na kuwaonya wafuasi wao kutokana na mawazo ya kupindukia mipaka ya Maghulati hao. [131] Hatua ya pili iliofuta ili ni tofauti na ile ya kwanza. Wakati wa zama za Imamu Baqir (a.s) na Imamu Sadiq (a.s) na hata baada ya hapo, ambapo mafundisho ya Kighulati yalipoimarika zaidi na madhehebu yao yalionekana kuongezeka zaidi, njia za kukabiliana mkondo wa Maghulati hao kutoka kwa Maimamu ulibadilika. Katika zama hizi kazi ya Maimamu (a.s), haikuwa tu ni kufafanua na kuutambulisha uhalisia wa Maghulati, bali pia waliwatambulisha wahusika wa Maghulati na kuamuru wapigwe marufuku na kutengwa na Mashia. [132]

Miongoni mwa mifano ya Hadithi kuhusiana na mapambano ya Maimamu dhidi ya gurudumu la Maghulati, ni Hadithi kutoka kwa Imamu Sadiq (a.s) ambayo ilionukuliwa kuhusiana na tafsiri ya Aya ya 222 na 223 za Surat Ash-Shu’araa. Katika Hadithi hii imamu ametaja majina ya watu saba ambao ni Ghulat walio kuwa wakiishi katika zama zake, ambao aliwataja akisema kwamba wao ni watu wanaoshukiwa na Mashetani. [133] Pia katika Hadithi nyingine iliyopokewa kutoka kwake, amemlaani wazi wazi Muqhaira bin Said (mwanzilishi wa madhehebu ya Kighulat ya Muqhairiyya), kwa sababu Kuingiza Hadithi za uongo katika vitabu vya wafuasi wa Imamu Baqir. [134] Vile vile katika moja ya Hadithi iliyo nukuliwa kutoka kitabu cha “Rijalu al-Kashi”, ndani yake Imam Ridha (a.s) amewataja jopo la Maghulati ambao walizua uongo dhidi ya Imam Baqir (a.s), Imamu Sadiq (a.s), Imamu Musa Kadhim (a.s), na yeye mwenyewe (a.s). [135]

Mara nyingine katika Hadithi, Maghulati hunatajwa na kusifiwa kama ni viumbe wabaya zaidi wa Mungu, [136] na baadhi ya Hadithi nyengine zinatajwa kama ni makafiri na washirikina. [137] Pia katika Hadithi nyingine imeelezwa kwamba; kukaa na pamoja na Maghulati na kukaa katika mikutano yao hupelekea mtu kutoka katika imani ya Kiislamu. [138]

Kufuatia mafundisho ya Maimamu (a.s), wanazuoni wa Kishia pia walipigana dhidi ya Maghulati na kujibu madai ya imani zao kwa hoja imara kabisa. [139] Kuhusiaana na suala hili, watafiti wanarejelea na kuwataja wasomi na wapokezi wa Hadithi wa chuo cha Qom, ambacho katika karne ya tatu Hijria kilikuwa ndio kitovu kikuu cha elimu ya Kishia. Watafiti wansema kwamba; wanazuoni wa zama walionesha upinzani mkali dhidi ya uenezaji wa fikra za Kighulati. Yeyote yule aliye jaribu kuwapa Imamu sifa za kimungu walimtangaza kuwa ni Mghulati na kumfukuza kutoka mji wao huo. [140] Kwa mfano, Sheikh Saduq kutoka miongoni mwa wanazuoni mashuhuri wa chuo cha Qom, aliwahisabu Maghulati na Mufawwidha kuwa ni makafiri na akawachukulia kuwa ni hatari zaidi kuliko hata wale wasio kuwa Waislamu, kama vile; Wayahudi, Wakristo, na hatari yao ni zaidi wazuao bida’a wote kwa jumla. [141] Pia Sheikh aliwalani na kuwatenga watu hawa. [142]

Kuna kazi kadhaa dhidi ya Maghuati zilizoandikwa katika chuo hicho cha Qum. Miongoni mwa kazi kutoka katika chuo hichi ni pamoja na kitabu kiitwacho “Al-Raddu ‘Ala al-Ghuluwwu” kilichoandikwa na Safar Qummiy, pamoja na athari nyingine zenye jina kama hilo kutoka kwa wanazuoni wengine kama vile; Yunus bin Abdul-Rahman Qummiy, Hussein bin Said Ahwazi na Muhammad bin Urmah Qummiy, ambao ni kati ya wapokezi wa Hadithi wa Kishia na wafuasi wa Imamu Ridha, pamoja na wengine kadhaa. [143]

Mtazamo wa Mafaqihi wa Mdhehebu ya Shia

Wanazuoni hawakujadili kwa kina kuhusu hukumu za Ughulati, bali wameelezea hukumu zake chini ya mjadala unaohusiana na ukafiri na hukumu zake. Ughulati humaanisha kuamini katika Uungu (ألوهیة) wa Imamu Ali (a.s) au Uungu wa mmoja wa ya Maimamu (a.s). Kwa kuwa imani kama hiyo husababisha kukataa uwepo wa Mungu, hivyo basi jambo hili huhisabiwa kuwa ni ukafiri, na kwa mujibu wa makubaliano ya wanazuoni wa Shia na mtu anayeamini imani hiyo ni kafiri na ni najisi. [147]

Wataalamu wa fiqhi kama vile Sayyid Muhammad Baqir Sadr na Sayyid Abdul A'la Sabzewari wanasema kwamba; Maghulati ni makafiri, hii ni kwa kuwa Ughulati unafungamana na imani ya تفویض “tafwidhi” (kuhamishwa kwa mamlaka kutoka kwa Mwenyezi Mungu kuwakilishwa kwa Mtume na Maimamu, na kuwapa wao uwezo wa kufanya chochote kile wakitakacho bila matakwa ya Mwenyezi Mungu). Na kwa kuwa imani hii pia inapingana na imani ya tawhidi (umoja wa Mwenyezi Mungu) na inaashiria imani ya kuwepo kwa Miungu zaidi ya mmoja. Pia kwa upande mwengine; kufuatilia imani ya حلول “huluuli” (Mwenyezi Mungu kuingia ndani ya miili ya viumbe vyake na kuungana nao), jambo ambalo linapingana na imani ya tawhidi na inaashiria imani ya Mwenyezi Mungu kuwa na mwili. [148] Sayyid Muhammad Baqir Sadri anaongeza akisema: Na kwa kuwa Maghulati pia wanaamini unabii mtu mwingine zaidi Mtume Muhammad (s.a.w.w), au kumuona mtu fulani ni bora kuliko Mtume (s.a.w.w), au sawa na bwana Mtume (s.a.w.w). Hilo pia ni miongoni mwa yale yaliopelekea wao kuhukumiwa kwa hukumu ya ukafiri. [149]

Mafaqihi kama vile Sheikh Ansari na Sayyid Muhsin Hakim wanasema kwamba kiwango cha mtu Ughulati kinacho mpelekea yeye kuwa kafiri, ni kukataa mja ya nguzo na misingi ya dini. [150] Kulingana na huo; Imani ya حلول “hululi” (imani ya Mwenyezi Mungu kuingia ndani ya miili ya viumbe vyake na kuungana nao), pamoja na kuwapa Mitume na Maimamu sifa za kupindikia, kama vile; kuamini kuwa wao ni waumbaji au waruzukuji, huwa ni sawa na kukataa nguzo za msingi za dini, na uhalisia wa kufanya hivyo ni kumkufuru Mungu. [151]

Historia ya Ughulati na Nafasi Yake

Ughulati ni mkondo wa mawazo ya upotofu ambao kwa mujibu wa baadhi ya watafiti, imekuwa ni tabia ilipo katika nyakati mbali mbali za historia ndefu ya binadamu. [152] Inasemekana kuwa katika dini zilizopo kabla ya Uislamu, kulingana na ripoti za Qur’ani, kumekuwa na matukio mbali mbali ya Kighulati (غلو). Miongoni mwa matendo ya Kighulati yalioripotiwa ni; Ughulati kuhusisna na viumbe asilia viishivyo ndani ya ulimwengu huu wa kimaada, Ughulati juu ya baadhi ya wanadamu wa kawaida, Manabii, pamoja na malaika. [153] Baadhi ya watafiti wanahusisha uikuibukaji wa mkondo wa Ughulati katika Uislamu wakati na Abdullah ibn Saba. [154] Wengine wanaamini kwamba; vitabu na nyaraka za historia zinaashiria kwa kiasi kidogo mno juu ya ushahidi wa kuwepo kwa mkondo wa Ughulati wakati wa uhai wa Maimamu watatu wa kwanza wa Kishia. Watafiti hawa wanahisi kuwa Ughulati ulianza rasmi baada ya kuuawa kwa Imamu wa tatu wa Kishia na kuibuka kwa kundi la waliojuta kutokana na kuto mhami Imamu Hussein waliojulikana kwa jina la Tawwabina (Waomba Toba), na baada ya kuzidi dhuluma dhidi ya Ahlul-Bayt (a.s) pamoja na uasi wa Mazaidiyyah, Kisaaniyya na Makhawarij, pamoja kuwepo kwa hali kadhaa za kitamaduni na kijamii. Kwa mtazamo wao; mawazo ya Ughulati yalijitokeza kwa kuanzia na imani ya utungu wa Kiungu wa Imam Ali (a.s) au imani katika uwepo wa sehemu ya Kiungu ndani yake. [155]

Ibn Abi al-Hadid katika Sharhu Nahju al-Balaghah alisema kwamba; asili ya fikra za Ughulati katika Uislamu ilianzia katika ardhi ya Iraq na Kufa. Yeye aliendelea kufafanua akisema kwamba; asili ya ardhi ya Iraq ilikuwa ni tofauti na ardhi ya Hijaz. Uwepo wa wanafikra na wataalamu wa mawazo na mijadala katika masuala mbalimbali, kulisababisha kuzaliwa kwa wafuasi wa madhehebu tofauti na ya ajabu, kama Manawi na Mazdaki, na kukapelekea kuzaliwa kwa imani mbalimbali katika ardhi hiyo, na hiyo ndiyo ikawa sababu ya watu wa ardhi hii kuathiriwa na dini na mila mbali mbali. Kuona kwao aina mbali mbali za miujiza na karama kutoka kwa Imamu Ali (a.s), kulipelekea wao kumpa yeye sifa za kupita kiasi na zilizokiuka mipaka ya kibinadamu. Wakati watu wa ardhi ya Hijaz, licha ya wao kuona miujiza na karama za bwana Mtume (s.a.w.w), halikupelekea wao kupindukia mipaka katika kumsifu yeye. [156] Kamal Mustafa Shibi, mwandishi kutoka Iraq na profesa wa falsafa katika Chuo Kikuu cha Baghdad, katika kitabu chake kiitwacho “Al-Silah baina al-Tasawwuf wa al-Tashayyu’u”, ameainisha asili ya upotofu na mwelekeo wa Ughulat katika Shia, akisema kuwa; asili ya Ughuti ni mji wa Kufa ulioko nchini Iraq.[157] Yeye anaamini kwamba; watu wa Kufa, ili kufidia udhaifu na dhulma walizokuwa nazo dhidi ya Imam Ali (a.s), walizidisha na kuimarisha upendo wao kwake yeye kupita kiashi, na kujenga uadui dhidi ya maadui zake, na wakaanza kujenga njia hii ya upotofu wa Kighulati. [158]

Pia, mtafiti wa historia aitwaye Rasul Ja’afarian, akikanusha uwepo wa mawazo ya Kighulati ya kupindukia mipapa katika zama za Imamu Ali (a.s), anasema kwamba; kile kinacho jadiliwa kwa uzito wa mawazo kuhusiana na fikra za Kighulati za kupindukia mipaka, kinahusiana na baada ya nusu ya kwanza ya karne ya kwanza, na ni mawazo yaliokoza rangi zaidi katika miaka ya 66 Hijriya, yaani baada ya uasi wa Mukhtar. [159] Wengine pia wameona kuwa; mawazo ya Kighulati ya kupindukia mipaka, yalitokea kwa mara ya kwanza kabisa wakati wa uhai wa bwana Mtume (s.a.w.w) baada ya kifo cha mwanawe aliyeitwa Ibrahim. [160] Kulingana na ripoti za wanahistoria, tukio la kupatwa kwa jua lilitokea wakati wa kifo cha Ibrahim, na watu wakaamini kuwa; kupatwa huko kwa jua kulitokana na kifo cha mwana wa Mtume (s.a.w.w). [161] Imani hii ilikabiliwa na upinzani mkali na kukemewa na bwana Mtume (s.a.w.w). [162]

Sheikh Mufid, akirejea kwenye riwaya ambazo kulingana nazo Omar bin Khattab alikanusha kifo cha Mtume (s.a.w.w) licha ya kwamba alikuwa amefariki, na alisema kwamba; Mfano wa bwana Mtume (s.a.w.w) ni kama vile Nabii Mussa, na kwamba yeye ameondoka tu machoni mwa watu wake na baada ya siku arobaini atarudi tena. Kwa maoni ya Sheikh Mufid ni kwamba; Tendo hilo la Omar lilikuwa ndio tendo la kwanza ya la Kighulati baada ya kifo cha bwana Mtume (s.a.w.w). Hivyo basi Omar bin Khattab ndiye mwanzilishi wa Ughulati katika jamii ya Kiislamu. [164]

Chanzo cha Kuibuka kwa Ughulati

Watafiti wameorodhesha sababu kadhaa za kuzaliwa kwa itikadi pofu za Kighulati kwa kuchunguza historia na kusoma vyanzo vya kuaminika kuhusiana na itikadi zao, hasa katika ulimwengu wa Kiislamu na Shia. Baadhi ya sababu zilizo orodheshwa na watafiti hao ni pamoja na:

  • Malengo ya kisiasa: Moja ya sababu kuu za itikadi pofu za Kighulati, hasa kuhusiana na Maimamu wa Kishia, zilikuwa na malengo na madhumuni ya kisiasa yanye nia kuwatenga na kuwashutumu ili kupunguza hadhi yao mbele ya watu na kuwafanya watu wawe mbali nao. Watawala pia walikuwa wakiongoza fikra za itikadi Kighulati kwa kuwaruhusu baadhi ya wahubiri na kurahisisha uingiaji wao katika safu za Waislamu ili kuwepesisha ueneneza wa itikadi za Kighulati katika jamii. [167]
  • Udhaifu wa Kuto Komaa kifikra: Mambo kama vile kutokuwa na ufahamu wa kutosha katika kuelewa ukweli wa ibada, kushangazwa na utukufu wa manabii na maimamu, na kutokuwa na uwezo wa kuchunguza na kutambua Hadithi bandia zilizozuliwa na wadanganyifu, ni miongoni mwa sababu za msingi zilizo tajwa katika kuchochea uwepo na ukuwaji wa itikadi za Kighulati. [168] Ahmad bin Ali Tabrasi katika kitabu chake Al-Ihtijaju amenukuu Hadithi kutoka kwa Imamu Ridha (a.s) ambapo kwa mujibu wake, Imamu Ridha (a.s) alilizingatia suala la ujinga kuwa ndio sababu ya Ughulati. [169]
  • Mapenzi yaliozidi kiasi: Kupenda kupita kiasi ni moja ya sababu za kuzalisha mawazo na imani za Kighulati. [170] Katika moja ya Hadithi kutoka kwa Imamu Sajjad (a.s) imeelezwa kuwa; Wayahudi kwa kutokana na mapenzi ya makubwa ya kumpenda Uzairu kupita budi, kulipelekea wao kumtambua yeye kana ni wana wa Mungu, Wakristo nao kutokana na mapenzi yao ya kupindukia mipaka katika kumpenda Nabii Isa (Yesu), iliwapelekea wao kumtambua yeye kama ni mwana wa Mungu. Tabia hii imeendelea kwetu pia na baadhi ya watu wamepelekwa kuelekea katika mienendo ya kupindukia katika suala la sisi. [171]
  • Matakwa ya kidunia: Imenukuliwa kutoka kwa Hassan bin Mussa Nawbakhti katika kitabu Firaqu al-Shia, ya kwamba; Katika zama Imamu Swadiq (a.s), kulikuwa na mtu mmoja aitwaye Muhammad bin Abi Zainab, anayejulikana kama Abul Khatab, mtu alidai kwamba Imamu Sadiq (a.s) ni Mungu na yeye amechaguliwa na Mungu huyo kuwa ni mtume wake, naye aliweza kupata wafuasi kadhaa kupitia imani hii ya Kighulati na ya kupindukia mipaka. [172] Inasemekana kwama Mghulati walijaribu kutafuta njia katika sharia za Kiislamu ili waweze kuzikingiusha kwa nia kutafuta njia ya kuzigeuza dhambi kuwa ni halali na kuacha wajibu wao wa sheria ili waweze kuhalalisha starehe zao za kidunia. [173] Mfano mwingine wa motisha wa aina hii, umeelezwa katika Hadithi ya Imamu Hassan Askari (a.s) ambapo kwa mujibu wa Hadithi hii, kulikuwapo na watu wawili wa udanganyifu katika zama za Imamu Hassan Askari (a.s) walitambulikana kwa majina ya Muhammad bin Nasir Fahri na Hasan bin Muhammad Qummyi. Watu hawa walitambulishwa na Imamu Hasan Askari (a.s) kama na watu wadanganyifu ambao walikuwa wakiwaibia watu mali zao kwa kuwadanganya kupitia imani za Kighulati. [174]
  • Nyezo ya Ushawishi: Kulingana na Salehi Najafabadi, baadhi ya Maghulati wenye itikadi za Kighulati walipenyeza fikra zao potofu kwa mfumo wa kutengezeza Hadithi bandia na kuzihusisha na Maimamu (a.s), wao walitengeneza watu maalumu walio warubuni na kuwaingiza kwenye jamii ili wajikurubishe na wafuasi wa Maimamu (a.s), wao waliwapa jukumu la kujiwasilisha kama ni mawakala wa Maimamu (a.s) ili waweze kuaminiwa na wafuasi wa Maimamu (a.s). Baada ya kuaminiwa na wafuasi hao, waliomba vitabu vya Hadithi vilivyo mikononi mwao kwa madai ya kutaka kukopi Hadithi zilizoko vitabuni humo, kisha wakatengeneza kopi kutoka katika vitabu hvyo, na kubadilishi mafunzo halisi vitabuni homo na kuweka habari za uongo ndani ya kopi za vitabu vyao, kisha kuwarudishia vitabu vyao. Baada ya hapo vitabu hivi vilivyohaririwa vilienezwa na habari za kupotosha ziliweza kusambazwa kila kona. [175] Baadhi pia wanadhani kwamba; ushawishi wa watu kutoka dini za Kiyahudi na Kikristo ambao hata wao wenyewe pia walikuwa wameathiriwa na mawazo ya kupindukia mipaka, ndio moja ya sababu zilizochangia kuenea kwa itikadi za Kighulati miongoni mwa Waislamu kwa lengo la kuleta upotovu. Hii ni pamoja ya nadharia zinazo tajwa kama ni sababu zilizosababisha kuenea kwa mawazo ya kupindukia mipaka katika Uislamu. [176]
  • Hisia za kuunda mashupavu au mashujaa wa kidini: Kuunda mashupavu na kuabudu mashujaa, ni moja ya sababu zilizosababisha kuzuka kwa riwaya za uongo, potofu na za Kighulati kuhusiana na baadhi ya mashujaa wa kidini na kitaifa. [177]
  • Upendeleo wa kichwa mchungwa na mapenzi pofu: Mapezi pofu ni moja ya sababu kuu za kuibuka kwa mawazo ya Kighulati ya kupindukia mipaka katika jamii mbalimbali, hasa miongoni mwa Waislamu. [178]

Bibliografia (Seti ya Orodha ya Vitabu)

Baadhi ya kazi zilizoandikwa kuhusiana na Ughulati wa kidini ni kama ifuatavyo:

  • Ghuluwwu; Dar-amadiy bar Afkare wa ‘Aqaaide Ghaaliyaane na Diin: kilicho andikwa na Ni’imatullah Salehiy Najafabadi: Kitabu hichi kina muktadha wa utangulizi na sura mbili. Mwandishi katika sura ya kwanza anatoa ufafanuzi kuhusiana na Ughulati na kuelezea sababu za kuibuka kwake katika ulimwengu wa Kiislamu, na kutaja mifano ya mawazo na imani zenye sifa ya Ughulati. [179] Sura ya pili ya kitabu hichi inayatambulisha makundi matatu kuhusiana na Ughulati; maadui wa Ahlul Bait (a.s), marafiki wenye itikadi kali kwa nia ya kuwatakasa Ahlul Bait (a.s) na kundi la la tatu ni kundi alililo ingia katika upotovu wa Kighulati kutokana na tamaa za kiduni na kutafuta anasa. Makundi matatu hayo yametajwa kama ndiyo mafiga matatu asilia yaliopika jungu la itikadi za Kighulati. [180]
  • Ghuluwwu Haqiiqat wa Asaame Aan: kilicho andikwa na Sayyid Kamal Haidari, yeye amejadili mambo muhimu kuhusiana na Ughulati ndani ya kitabu hichi. Miongoni mwa yaliomo kitabuni humu ni; Mjadala kuhusu maana ya Ughulati, asili yake na historia yake na maneno ya wafuasi wa Ahlul-Bait (a.s) kuhusiana na Ughulati. [181]
  • Ghaaliyaan; Kaawush dar Jarayanhaye wa Barayand-haaye, kilicho andikwa na Ni’imatullah Safari Furushani: Kitabu hichi kina sura nne. Sura ya kwanza inazingatia mambo ya jumla na masuala yanayo husiana na ufafanuzi wa Ughulati, historia yake na sababu za kuibuka kwake. Sura ya pili inachunguza madhehebu tofauti ya Maghulati katika historia. Sura ya tatu, iitwayo Ghulaat dar Aine Aqiide wa ‘Amal, inachunguza imani maalum za Maghulati na imani wanazoshirikiana na Shia, huku sura ya nne ikijadili athari za Maghulati katika historia ya Shia. [182]

Maudhui Zinazo Husiana

Maelezo

  1. Maana ya Hululi «حلول» ; ni imani ya kwamba roho ya Mwenyezi Mungu au sehemu ya roho yake huingia au imeingia ndani ya mtu fulani kama Nabii au Imamu, kwa njia ambayo Yeye na mtu huyo hukuwa ni kitu kimoja (Safawiy Furushani, Ghalian; Kaawushi dar Jarayanihaye wa Barayandehaye, 1378 Shamsia, uk. 183-184).

Rejea

Vyanzo