Nenda kwa yaliyomo

Abdullah ibn Saba

Kutoka wikishia

Abdullah bin Saba (Kiarabu: عبد الله بن سبأ) ni mojawapo ya watu mashuhuri wenye utata juu yake aliye jadiliwa uwepo wake ndani ya miaka ya 21 hadi 40 Hijiria ya mwanzoni mwa historia ya Uislamu. Vyanzo vya kihistoria na vya Hadithi vimeripoti taarifa tofauti zinye kukinzana kuhusiana naye.

Jina la Ibn Saba lilitajwa kwa mara ya kwanza kabisa na Muhammad bin Jarir al-Tabari, mwanahistoria wa jamii ya Sunni. Katika vyanzo vya Shia, mwanzo kabisa ameanza kutajwa katika kitabu cha Rijal al-Kashi. Kulingana na vyanzo hivyo, yeye alikuwa ni Myahudi ambaye aliye ingia katika Uislamu wakati wa Ukhalifa wa Othman ibn ‘Affan, ambaye ni khalifa wa tatu wa Waislamu baada ya kufariki Mtume (s.a.w.w)

Wanzuoni wa Kisunni wanamchukulia yeye kuwa ndiye sababu ya uasi wa Waislamu dhidi ya Othman na mwanzilishi wa madhehebu ya Shia, ila wanazuoni wa Shia wanadai kwamba; Abdullahi bin Saba alikuwa ni Mwislamu mpya, na haiwezekani Mwislamu huyu mpya kuwa na uwezo kuiathiri jamii ya Waislamu kiasi cha kuasi dhidi ya khalifa wao. Baadhi ya wanazuoni wa Shia wamemtuhumu Abdullah bin Saba kwa kuritadi (ametoka nje ya Uislamu), na wengine wanaamini kwamba; hakukuwa na mtu mwenye jina hilo, bali yeye ni mtu wa kubuniwa.

Kuna maandishi mengi yanayo muhusu Ibnu Saba, na mojawapo ya maelezo yenye ufafanuzi na uchambuzi mpana zaidi juu yake yanapatikana katika kitabu kinachoitwa Abdullah bin Saba wa Asaatiiru Ukhra kilichoandikwa na mwanazuoni wa Shia aitwaye Sayyid Murtada Askari aliye zaliwa mwaka 1293 na kufariki mwaka 1386 Miladia.

Utambuzi Juu ya Uhalisia Wake

Kulingana na maelezo ya Muhammad bin Jarir Tabari mwanahistoria wa Kisunni; Abdullah bin Saba alikuwa ni Myahudi na mkazi wa mji wa Sana'a aliye silimu wakati wa Khalifa wa tatu wa Uislamu (Othman bin ‘Affan).[1]Kulingana na maelezo ya mwandishi huyu, Abdullah bin Saba alimwona Othman bin Affan kama ni mnyang'anyi wa nafasi ya Ukhalifa, na pia kwa maalezo yake, yeye ndiye aliye kuwa mshawishi wa uasi dhidi ya Othman.[2] Lakini mwanahistoria wa Shia, Rasul Ja'fariyan, anaamini kuwa; haiwezekani kuidhania jamii ya Waislamu kuwa ni dhaifu kwa kiasi kwamba, mtu aliyechochea uasi dhidi ya Khalifa wa Waislamu awe ni Myahudi ambaye ndio kwanza ameingia katika Uislamu.[3]

Maoni Tofauti Kuhusu Abdallah bin Saba

Katika vyanzo vya Kiislamu, kuna maoni mbalimbali kuhusiana na mtu aitwaye Abdullah bin Saba. Katika vyanzo vya Ahlus-Sunnah, yeye anahesabiwa kama ndiye mwanzilishi wa madhehebu ya Shia na ni kiongozi au mwanzilishi wa uasi dhidi ya Othman, ambaye ni Khalifa wa tatu wa Waislamu. Mbele ya wengi wa wanazuoni wa Shia, yeye anahisabiwa kuwa ni miongoni mwa Maghulati. Pia baadhi ya watafiti wa kisasa wa Shia, hawamchukulii yeye kuwa ni mtu aliye ishi ulimwenguni humu, bali ni mtu wa kubuniwa.

Tabari, mwanahistoria wa Ahlus-Sunnah, na wengi wanao muunga mkono katika nadharia yake, wanamuhisabu Abdullah bin Saba kuwa ndiye sababu kuu ya matukio muhimu yaliyo tokea katika historia ya Kiislamu, likiwemo tukio la kuuawa kwa Othman, pia wanamuhisabu kuwa ndiye mwanzilishi wa madhehebu ya Shia.[4]

Wanazuoni wa Shia wanamuhisabu Abdullah bin Saba kuwa ni miomgoni mwa Maghulati, aliye songomanisha ukweli na akizidisha chumvi juu wa wasifu wa Imam Ali (a.s), na kumtukuza kiasi cha kumfanya kama ndiye Mungu, na hilo ndila lililo pelekea yeye kulaaniwa na Maimamu wa Shia.[5]

Baadhi ya watafiti wa kisasa kama Ayatullah Tabatabai, Ayatullah Askari, na Dokta Taha Hussein, wanaamini kuwa asili ya mtu aliyeitwa Abdullah bin Saba haijulikani, na utambulisho wake ulibuniwa na baadhi ya watu tu, akiwemo Seif bin Omar.[6]

Ali al-Wardi, mtafiti wa Kiarabu, akisisitiza wazo la kuwa Abdullah bin Saba alikuwa ni mtu wa kubuniwa, na kwamba sifa nyingi zilizotajwa katika kitabu cha historia cha Tabari pamoja na vyanzo vingine vinavyo fanana nacho, ni sifa zinazo patikana katika wasifu Ammar bin Yasir, sahaba wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) pamoja na Imamu Ali (a.s). Amehitimisha akisema kwamba, yawezekana kuwa Ammar bin Yasir amepewa jina hilo la Saba, kutokana na kwamba yeye alikuwa ni kiongozi wa watu wa kabila la Saba'iyyiina, au hata yawezekana kuwa Abdullah bin Saba ni Ammar bin Yasir.[7] Pia moja ya Umaarufu wa Ammar ni Ibn al-Saudaa, ambapo pia Abdullah bin Saba anajulikana kwa umaarufu wa jina hilo katika baadhi ya vyanzo vya historia. Mapenzi makubwa ya Ammar kwa Ali (a.s), kuwalingania watu kumpa kiapo cha utiifu na nafasi muhimu ya Ammar katika vita vya Jamal ni miongoni mwa mifano iliyo tajwa katika kufanana kiutambulisho kati ya Ammar bin Yasir na Abdullah bin Saba.[8]

Tathmini ya Vyanzo

Miongoni mwa vyanzo vilivyotaja jina la Abdullah bin Saba, ni Taarikhu al-Tabari miongoni mwa vitabu vya Sunni na Rijalu al-Kashi katika vitabu vya Shia. Chanzo cha kwanza cha kihistoria ni Tarikhu al-Tabari kilicho andikwa na Ibnu Jariru al-Tabari (aliye zaliwa mwaka 224 na kufariki mwaka 310 Hijiria).  Hati ya Tabari katika kunukuu habari za Abdullahi bin Saba, inatoka kwa mtu ajulikanaye kwa jina la Seif bin Omar. Baadhi ya wanahistoria wengine kama vile, Ibn Athir (aliye fariki mwaka 630 Hijiria)[9] na Ibn Asaakir (aliye fariki mwaka 571 Hijiria)[10] wameelezea tukio hilo kupitia nukuu walio itegemea kutoka kwa Saif.

Mnukuu mkuu wa Tabari katika kuthibitisha uwepo wa Ibn Saba, (yaani Seif bin Omar), ni dhaifu mbele ya wengi miongoni mwa wanazuoni wa madhehebu ya Sunni na wala zi mtu mwenye kukubalika mbele yao. Wanazuoni kama vile Yahya bin Muin (aliye fariki mwaka 233 Hijiria), Nasai (aliye fariki mwaka 303 Hijiria),[11] Abu Dawud (aliye fariki mwaka 275 Hijiria),[12] Ibn Hammam Aqili (aliye fariki mwaka 322 Hijiria),[13] Ibn Abi Hatim (aliyekufa mwaka 327 Hijiria)[14] na Ibn Hibban (aliye fariki mwaka 354 Hijiria)[15] wamemsifu Seif bin Omar kwa sifa kadhaa kama vile: dhaifu wa Hadithi, mwongo wa Hadithi, na asiyeaminika katika nukuu za Hadithi zake.

Pia kuna baadhi ya riwaya ndani ya kitabu Rijalu al-Kashi, kutoka kwa Saif bin Omar zilizozungumzia habari za Ibnu Saba, ila mwandishi wa kitabu hicho hakuzijali wala kuzithamini riwaya hizo. Sayyid Murtadha Askari, mwanahistoria maarufu wa Kishia, ametoa hoja mbili juu ya jambo hili:

  • Riwaya hizi hazipo katika vitabu vinne vikuu vya Shia vijulikanavyo kwa jina la Kutubu al-Arba’a, na hii inaonesha kutokuwa na imani ya wanazuoni wa Shia juu ya riwaya hizi.
  • Wanazuoni kama Najashi, Muaddith Nuri na Muhammad Taqi Shushtari wanamemhisabu Kashi kuwa na hadithi dhaifu, na kwamba kitabu chake ni chenye mkusanyiko wa makossa ndani yake, ambapo ndini yake hupatikana riwaya sahihi pamoja na dhaifu.[16]

Monografia (Seti Makhususi ya Vitabu Juu ya Mada hii)

Maudhui ya Abdullah bin Saba ni miongoni mwa mada maarufu iliyo pewa kipau mbele na maandishi mbali mbali. Vitabu kama Fitnatu al-Kubra cha Taha Hussein (aliye zaliwa mwaka 1889 na kufariki mwaka 1973) na Wia'adhu al-Salatiin cha Ali al-Wardi (aliyezaliwa mwaka 1913), ni miongoni mwa vitabu ambavyo waandishi wake wamemchunguza na na kumjadili Abdullah bin Saba katika mijadala yao. Baadhi ya vitabu makhususi katika mada hii ni pamoja na:

  • Abdullah bin Saba wa Hikaayatun Ukhra: Hichi ni kitabu kilichoandikwa na Sayyid Murtadha Askari (aliye zaliwa mwaka 1293 na kufariki mwaka 1386), ambaye ni mwanahistoria na mtafiti wa Kishia ambacho kilichapishwa mwaka wa 1375 Hijiria sawa na mwaka 1335 Shamsia.[17] Kitabu hiki kimefasiriwa kwa lugha ya Kiingereza, Kifarsi, Kiarabu na Kituruki. Tafsiri yake kwa Kifarsi inaitwa “ Abdullahi Bin Saba wa Diigar Afsanehaye Taarikh”.
  • Nadharia na Maoni juu ya Abdullah bin Saba na Hadithi za Saif katika Magazeti ya Saudi Arabia: Kitabu hiki kimekusanya maoni na ukosoaji wa wasomi wa vyuo vikuu vya Saudi Arabia katika magazeti ya nchi hiyo kuhusu kitabu Abdullah bin Saba wa Hikaayatun Ukhra, na majibu ya Sayyid Murtadha Askari dhidi ya ukosoaji huo.
  • Abdullah bin Saba Min Mandhuri Akhar: kilichoandikwa na Asad Haidar (aliye zaliwa mwaka 1911 na kufariki mwaka 1980 Hijiria). Tafsiri yake kwa Kifarsi inaitwa “Negahi Nou Be Abdullah bin Saba”.
  • Abdullah bin Saba Baina al-Waaqi’i wa al-Khiyal, kilichoandikwa na Sayyid Hadi Khusroshahi (aliye zaliwa mwaka 1317 na kufariki mwaka 1398 Hijiria).
  • Abdullah bin Saba Haqiiwqatun au Khiyal: kilichoandikwa na Ali al-Muhsin. Kitabu hichi kimefasiriwa kwa lugha ya Kifarsi kwa jina la “Abdullah bin Saba Waaqiiyat yaa Khiyale.[18]

Rejea

  1. Tabari, Tarikh al-Umam wal-Muluk, juz. 4, uk. 340
  2. Tabari, Tarikh al-Umam wal-Muluk, juz. 4, uk. 340
  3. Ja'fariyan, Tarikh Khulafa', 1394 HS, uk. 160
  4. Tazama: Tabari, Tarikh al-Umam wal-Muluk, juz. 4, uk. 340; Ibnu Athir, al-Kāmil fi al-Tārikh, juz. 3, uk. 154, Ibnu Asakir, Tārikh Madinah Dimashq, juz. 29, uk. 3-6
  5. Tazama: Tusi, Ikhtiyār Ma'rifat al-Rijāl, juz. 1, uk. 323-224
  6. Tazama: Askari, Abdullah bin Saba wa Asāthir Ukhra, juz. 2, uk. 308; Tabatabai, Abdullah bin Saba, uk. 194; Taha Hussein, al-Fitnah al-Kubra, juz. 2, uk. 134
  7. Al-Wardi, Wi'ādhu al-Salātin, uk. 174
  8. Tabatabai, Abdullah bin Saba, uk. 220-221
  9. Ibnu Athir, al-Kāmil fi al-Tārikh, juz. 3, uk. 154
  10. Ibnu Asakir, Tārikh Madinah Dimashq, juz. 29, uk. 3-4
  11. Nasai, al-Dhu'afa' wa al-Matrukun li al-Nasai, uk. 50
  12. Ibnu Hajar, Tahdhib al-Tahdhib, juz. 4, uk. 295
  13. Ibnu Hammad, al-Dhu'afa' al-Kabir, juz. 2, uk. 175
  14. Ibnu Abi-Hatim, al-Jarh wa al-Ta'adil, juz. 4, uk. 278
  15. Ibnu Hibban, al-Majruhin, juz. 1, uk. 345
  16. Askari, Abdullah bin Saba wa Asāthir Ukhra, juz. 2, uk. 177-180
  17. Askari, Abdullah bin Saba wa Asāthir Ukhra, 1381 H, Utangulizi chapa ya nne, uk. 177-180.
  18. «Abdullah bin Saba haqiqat au khurafah?»

Vyanzo

  • Amīnī, ʿAbd al-Ḥusayn al-. Naẓra fī kitāb al-Sunna wa l-Shīʿa l-Muḥammad Rashīd Riḍā. Edited by Aḥmad al-Kinānī. Tehran: Mashʿar, n.d.
  • ʿAskarī, Murtaḍā. ʿAbd Allāh ibn Sabaʾ wa dīgar afsānihāyi tārīkhī. Translated by Aḥmad Fihrī Zanjānī & ʿAṭāʾ Muḥammad Sardārniā. Qom: Dānishkadi-yi Uṣūl dīn, 1387 Sh.
  • Baghdādī, ʿAbd al-Qāhir b. Ṭāhir al-. Al-Farq bayn al-firaq wa bayān al-firqat al-nājīyya. Beirut: Dār al-Āfāq al-Jadīda, 1977.
  • Balādhurī, Aḥmad b. Yaḥyā al-. Ansāb al-ashrāf. Edited by Muḥammad Bāqir al-Maḥmūdī & et al. Beirut: Muʾassisat al-Aʿlamī , n.d.
  • Dhahabī, Muḥammad b. Aḥmad. Al-Mughnī fī l-ḍuʿafāʾ. Edited by Nūr al-Dīn ʿItir. n,p, n.d. (Version of al-maktaba al- shamela)
  • Guyard, Stanisals. Sāzmānhā-yi tamaddun-i Imprāṭūrī-yi Islām. Translated by Sayyid Fakhr al-Dīn Ṭabāṭabāʾī. Tehran: Kitābkhāni-yi Ibn Sīnā , 1326 Sh.
  • Ḥusayn, Ṭāhā. Al-Fitnat al-kubrā. Cairo: Dār al-Maʿārif, n.d.
  • Ibn Abī Ḥātam, ʿAbd al-Raḥmān b. Muḥammad. Al-Jarḥ wa l-taʿdīl. Hyderabad: Majlis Dāʾirat al-Mʿārif al-ʿUthmānīyya, 1371 AH- 1952.
  • Ibn al-Athīr, ʿAlī b. Muḥammad. Al-Kāmil fī l-tārīkh. Beirut: Dār al-Ṣādir, 1385 AH.
  • Ibn ʿAsākir, ʿAlī b. al-Ḥasan. Tārīkh madīnat Dimashq. Edited by ʿAlī Shīrī. Beirut: Dār al-Fikr, n.d.
  • Ibn Ḥajar ʿAsqalānī, Aḥmad b. ʿAlī. Tahdhīb al-tahdhīb. India: Maṭbaʿat Dāʾirat al-Maʿārif al-Niẓāmīyya, 1326 AH.
  • Ibn Ḥammād al-ʿAqīlī, Muḥammad b. ʿAmr. Kitāb al-ḍuʿafāʾ al-kabīr. Edited by ʿAbd al-Muʿṭī Amīn Qalʿajī. Beirut: Dār al-Maktabt al-ʿIlmīyya, 1404 AH, 1984.
  • Ibn Ḥibbān, Muḥammad. Al-Majrūḥīn min al-muḥaddithīn wa l-ḍuʿafāʾ wa l-matrūkīn. Edited by Maḥmūd Ibrāhīm Zāyid. Aleppo: Dār al-Waʿī, 1396 AH.
  • Ibn Kathīr al-Dimashqī, Ismāʿīl b. ʿUmar. Al-Bidāya wa l-nihāya. Beirut: Dār al-Fikr, 1407AH.
  • Nasāʾī, Aḥmad b. Shuʿayb al-. Al-Ḍuʿafāʾ wa l-matrūkīn. Aleppo: Dār al-Waʿī, 1396 AH.
  • Nashshār, ʿAlī Sāmī al-. Nashʾat al-fikr al-falsafī fī l-Islām. Ninth edition. Cairo: Dār al-Maʿārif, n.d.
  • Ṭabarī, Muḥammad b. Jarīr al-. Tārīkh al-umam wa l-mulūk. Edited by Muḥammad Abu l-Faḍl Ibrāhīm. Beirut: n.p. , n.d. (Version of Noor digital library)
  • Ṭabāṭabāʾī, Sayyid Muḥammad Ḥusayn. " ʿAbd Allāh ibn Sabaʾ" Maktab-i tashayyuʿ. N. 4, 2/1339 Sh.
  • Ṭūsī, Muḥammad b. al-Ḥasan. Ikhtīyār maʿrifat al-rijāl. Edited by Mahdī Rajāyī & Muḥammad Baqir b. Muḥammad Mīrdāmād. Qom: Muʾssisat Āl al-Bayt l-Iḥyāʾ al-Turāth, n.d.
  • Wardī, ʿAlī al-. Wuʿʿāẓ al-salāṭīn. Beirut: Dār Kufān l-l-Nashr, 1955.