Nenda kwa yaliyomo

Mhimili wa Muqawama

Kutoka wikishia

Mhimili wa Muqawama (Upinzani) au Jabhahatu Al-Muqawama: Mhimili wa Muqawama au Jabhahatu Al-Muqawama, ni jina maalumu linalotumiwa kurejelea muungano wa kikanda, unaojumuisha majeshi ya serikali na yasiyo ya kiserikali, hasa ya Kishia, ambayo yanahusika na shughuli mikakati ya kiupinzani dhidi ya ubeberu. Makundi haya ya kijeshi yanajumuisha nchi ya Iran, Syria (wakati wa utawala wa Hafidh na Bashar al-Assad), Iraq, Lebanon, Yemen, na Palestina. Malengo ya Mhimili wa Muqawama yanajumisha mambo kadhaa ndani yake, ikiwa ni pamoja na; kupambana na uvamizi wa Israel na kutetea uhuru wa Palestina, kukabiliana na ushawishi wa nchi za Magharibi (hasa Marekani) katika eneo la Asia Magharibi, kupambana na serikali za kidikteta, pamoja na kuzuia vitendo vya makundi ya kitakfiri (yanayowakufurisha Waislamu) kama vile DAESH (ISIS). Uundwaji wa Mhimili wa Muqawama unachukuliwa kuwa ni moja ya matokeo na mazao ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran. Mapinduzi ya Irani ndiyo msingi wa kuenea kwa hali ya hamasa, jambo liliopelekea uungaji wa mkono wa serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika harakati za kupinga uonevu na ukoloni. Utambulisho wa pamoja wa kikanda unaozingatia maadili na kanuni za kijamii, kidini, na kiutamaduni, pamoja na ushawishi wa itikadi ya Uislamu wa kisiasa, umetajwa kuwa ndio sifa kuu zinazofungamanisha Mhimili wa Muqawama. Jambalo ambalo limesababisha kupatikana kwa mshikamano na umoja wa wanachama wa mhimili huu. Miongoni mwa mikakati mikuu ya Mhimili wa Muqawama, ni kuongeza uwezo wa kijeshi ili kukabiliana na vitisho vinavyohatarisha uwepo wa mhimili huu. Kuimarisha nafasi ya Washia, kuzuia upanuzi wa utawala wa Kizayuni, na kuunda utaratibu mpya katika eneo la Asia Magharibi, ni miongoni mwa mafanikio ya wanachama wa mhimili huu. Miongoni mwa mafanikio muhimu ya Mhimili wa Muqawama ni pamoja na; Kikosi cha Sepahe Qods cha Iran, kikundi cha Hamas na Jihad ya Kiislamu huko Palestina, kikosi cha Hashdu al-Sha’abi cha Iraq, kikosi cha Hizbullahi ya Lebanon, na kikosi cha Ansarullahi huko Yemen. Ili kufikia malengo yao, Majeshi ya Mhimili wa Muqawama, yameanzisha mitandao makhususi ya televisheni na mashirika ya habari, miongoni mwayo ni pamoja na; Shirika la Habari la Al-Manar TV, Al-Mayadeen TV, Al-Masirah TV, na Al-Furat TV. Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB) pia huandaa na kurusha vipindi kadhaa vinavyohusu habari na pamoja na shughuli za mhimili huu. Nafasi Yake Mhimilio wa Upinzani (kwa Kiingereza: Axis of Resistance) ni muungano wa kikanda unaotokana na kuenea kwa mawazo na itikadi za Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran katika ulimwengu wa Kiislamu. Kwa mujibu wa maoni ya wataalamu wa kisiasa, mhimilio huu umebadilisha uwiano wa nguvu zlizokuwa zikitawala katika eneo la Asia Magharibi [1] na kusababisha kupatikana kwa mpangilio mpya wa nguvu tawala katika eneo hili. [2] Serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kwa kuunga mkono vuguvugu la kupinga ukoloni na udikteta, pamoja na kusaidia Uamsho au Mwamko wa Kiislamu, imechangia na kupelekea kuimarika kwa Mhimilio wa Upinzani, jambo amabalo limepelekea kuiwamarisha Mashia, na kukuza usalama wa Iran na eneo hilo kwa jumla. [3] Wachambuzi wa kisiasa wanaona kuwa Mhimilio wa Upinzani umezaliwa kupitia shawishiwa na matokeo ya kihafidhina yanayotokana na Mapinduzi ya Kiislamu ya ndani ya Iran, ambayo yamepelekea kuamka kwa itikadi ziendazo sawa na mawazo ya wanamapinduzi wa Kiirani nje ya mipaka ya nchi hiyo. Kwa hiyo siasa za Iran zenye malengo ya kukosoa utawala wa mataifa makubwa katika siasa za kimataifa ndiyo msingi wa Mhimili wa Upinzani ndani ya baadhi ya nchi duniani. [4] Kwa maoni yao, alama za Mapinduzi za kutafuta mageuzi, Upinzani, na fikra za kuuhami Utambulisho (Nationalism) zilianza wakati wa Vita vya Iraq dhidi ya Iran. Na baada ya kumalizika kwa vita hivyo, kuanzishwa kwa mchakato maalumu wa kueneza fikra za mapinduzi, matunda yake yalijitokeza katika vuguvugu la Uamsho au Mwamko wa Kiislamu na kudhihiri kikanda na kimataifa. [5] Miongoni mwa mafanikio ya Mhimilio wa Upinzani ndani ya maeneo ya Maghribi mwa Asia ni kama ifuatayo: 1. Kuimarika kwa Mashia katika Asia Magharibi. [6] 2. Kutekelezwa kwa haki za Wapalestina. 3. Kupinga ubaguzi wa nguvu fulani za kikanda, 4. Kudumisha heshima ya Serikali ya Iran,[7] 5. Kuanguka kwa baadhi ya serikali za kidikteta katika eneo hilo,[8] 6. Kupungua kwa uenezi wa Marekani katika Mashariki ya Kati, 7. Kupingwa kwa mazungumzo ya kukubaliana na serikali ya Kiyahudi, 8. Kufukuzwa kwa Israel kutoka kusini mwa Lebanon, 9. Kushindwa kwa serikali hiyo katika Vita vya Siku 33 na 22. 10. Upinzani dhidi ya makundi ya kigaidi kama vile ISIS. [9]

Uundaji na Uteuzi wa Jina Jumuiya ya Upinzani au "Safu ya Upinzani" inachukuliwa kuwa ni muungano maalumu wa siasa ya kijiografia na wa kikanda (muungano wa kijeshi na kisiasa), ambao unajumuisha washiriki kadhaa wa wa kiserikali (Iran na Syria chini ya utawala wa Hafez na Bashar al-Assad) na idadi ya washiriki wasio wa kiserikali (Hezbollah wa Lebanon, Hamas, na Harakati ya Jihad ya Kiislamu ya Palestina). [10] Ila imeelezwa kwamba hatamu na uongozi hasa wa umoja huu yako chini ya mamlaka ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. [11] Muungano huu unahisabiwa kuwa ni miongoni mwa matunda ya matukio ya kihistoria yaliotokea mwishoni mwa karne ya 20 na mwanzoni mwa karne ya 21 katika kukabiliana na vitendo vya utawala wa Kizayuni huko Palestina na Lebanon, uvamizi na ueneaji wa ushawishi wa Daesh huko Syria na Iraq, na utawala au ungiliaji kati wa Marekani katika eneo la Mashariki ya Kati. [12]

Watafiti wa kisiasa wanaamini kwamba; wanachama wa Mhimili wa Upinzani wana maslahi ya pamoja ya kitaifa na kiitikadi, hivyo wanajitahidi kupambana na mfumo wa kiutawala unaoongoza kwa kuzingatia maslahi na itikadi za Mmarekani katika eneo la Magharibi mwa Asia, mambambano ambayo huendeshwa kupitia sera zao huru zinazozingatia mambano kwa njia ya upinzani. [13] Pia miongoni mwa sera zao ni kupambana dhidi ya utawala wa Kizayuni na kuitetea Palestina ianayokaliwa kimabavu na utawala huo wa Kizayuni. [14] Mhimili wa Upinzani ulipanua mipaka yake na kuenea katika nchi nyengine, hii ni baada ya kutokea kwa baadhi ya mabadiliko mapya katika eneo la Magharibi mwa Asia, ikijumuisha kuundwa kwa ISIS na mashambulio ya baadhi ya nchi za Kiarabu dhidi ya Yemen katika miaka ya mwanzoni mwa karne ya 21. Matukio haya yalipelekea washiriki wengine kama vile wanamgambo wa Kishia nchini Iraq na Ansar Allah nchini Yemen, kulijiunga na Mhimili huu wa Upinzani. [15] Kwa mara ya kwanza kabisa, Istilahiya kisiasa ya "Mhimili wa Upinzani" ilionekana kutumiwa na gazeti la Libya la “Al-Zahfu Al-Akhdar”, ambayo ni kinyume na istilahiya "Mhimili wa Uovu" ambayo ilitumiwa na Rais wa Marekani wa wakati huo aliyejulikana kwa jina la “George W. Bush na John Bolton”. [Maelezo: John Bolton ni wakili na mchambuzi wa masuala ya kisiasa wa Marekani, anayekuwa akihudumu kama Mshauri wa Usalama wa Kitaifa wa Marekani kuanzia mwaka 2018 hadi 2019 chini ya utawala wa Rais Donald Trump.] George W. Bush na John Bolton walitumia istilahi hii wakirejelea zile nchi ziendazo kinyume na sera za Marekani, ikiwa ni pamoja na; Iran, Syria, Iraq, Libya, Cuba, na Korea Kaskazini. [16] Kabla ya istilahi hii kupata umashuhuri kwa kutumiwa kwana na gazeti hilo la Libya, kwa mara ya kwanza kabisa istilahi hii ilitumiwa na Ayatollah Khamenei, kiongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Yeye alitumia istilahi ya "Safu ya Upinzani wa Kiislamu" mnamo Agosti 1993, wakati wa mkutano wake na Sayyid Hassan Nasrallah, Katibu Mkuu wa wakati huo wa Hezbollah ya Lebanon. Katika matumizi yake ya istilahi hii, alisema kwamba; kuundwa kwa "Safu ya Upinzani wa Kiislamu" ni matunda ya matokeo ya uvamizi wa Israel. [17]

Matawi ya Mhimili wa Muqawama Vikosi na harakati zinazounda Mhimili wa Muqawama vinafanya shughuli zake katika nchi mbalimbali kama ifuatavyo: • Iran: Kikosi cha Quds cha Sepahe Pasdaran (IRGC) na matawi yake, ikiwa ni pamoja na Lashkar Zainabiyoun na Lashkar Fatemiyoun. • Iraq: Hashd al-Shaabi (Vikosi vya Kijeshi vya Wanajamii), Sepahe Badr, Kata'ib Hezbollah, Hizb al-Da'wa al-Islamiyya (Chama cha Da'awa ya Kiislamu), Baraza Kuu la Kiislamu la Iraq, na Harakati ya Sadr. • Syria: Jeshi la Serikali ya Syria na Vikosi vya Ulinzi wa Taifa (National Defence Forces) katika enzi za utawala wa Hafez al-Assad na Bashar al-Asad. • Yemen: Ansarullah (Houthi). • Lebanon: Hizbullah. • Palestina: Harakati ya Jihad ya Kiislamu ya Palestina na Harakati ya Muqawama wa Kiislamu (Hamas). [18]

Mikakati na Sifa za Mhimili wa Muqawama Wanachama wa Mhimili wa Muqawama wanakubaliana na wanaungana pamoja juu ya mikakati na sifa kadhaa, ambazo zimewaletea mshikamano wa pamoja miongoni mwao. Utambulisho wa pamoja wa kieneo na kuathiwa kwao na mtazamo wa Uislamu wa kisiasa, ni miongoni mwa sifa bainifu za muungano huu. Aidha, inasemekana kuwa wanachama wa mhimili huu wanajidhatiti kwa kuimarisha nguvu zao za kijeshi ili kufanikisha malengo yao. Utambulisho wa Kieneo Maadili na mila za kijamii, kidini na kitamaduni zinazoshabihiana, ni miongoni mwa sababu kuu na msingi, ambazo kwa mujibu wa watafiti wa siasa, ndizo zilizochochea kuibuka kwa utambulisho wa pamoja miongoni mwa wanachama wa Mhimili wa Muqawama. [19] Licha ya umbali wa kijiografia na kutokuwe kwa mipaka ya moja kwa moja inayowaunganisha, ila bado wao wanaonekana kushikamana kwa pamoja chini ya utambulisho mmoja wa kieneo ulio imara. Utambulisho wa kieneo unachukuliwa kuwa dhana mpya iliyozuka kati ya utaifa na udugu wa kimataifa, ukiwa na lengo la kuimarisha thamani na desturi zinazofanana za kijamii na kitamaduni miongoni mwa wahusika wa kieneo. [20] Kwa mujibu wa nadharia ya itikadi ya kushikamana na utambulisho wa kieneo, ili kufanikisha malengo yao, wanachama hawa wa Mhimili wa Muqawama hutegemea na kushikamana na mafundisho kadhaa ya kidini, ikiwa ni pamoja na kanuni ya Nafyu al-Sabil (kuondoa udhibiti wa madhalimu juu ya jamii za Kiislamu), mapambano dhidi ya dhulma, pamoja na kauli mbiu kama vile umoja wa ulimwengu wa Kiislamu na kupinga ubeberu. [21] Aidha, inasemekana kuwa; uundwaji wa utambulisho huu wa kieneo umechochewa na kupata nguvu kupitia vipengele maalumu vya kiitikadi, kama vile utamaduni wa kujitolea muhanga (kufa shahadi), [22] kuwatetea wanyonge, kudai haki, kutafuta uhuru, kuunga mkono harakati za ukombozi, imani ya Mahdawiyya (imani ya uwepo kiongozi aitwaye Imamu Mahdi), mafundisho ya Intidhari (kusubiri ujio wa Imam Mahdi), na dhana ya Uislamu wa kidemokrasia, ambayo yote yaliibuka katika mchakato wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran. [23] Baadhi ya watafiti wanaamini kuwa; uundwaji wa utambulisho huu wa kieneo ni kinyume na utambulisho na muungano mwingine ndani ya eneo la Magharibi mwa Asia, ambao umeasisiwa na baadhi ya mataifa ya Kiarabu kwa lengo la kupatana na utawala wa Kizayuni (Israel) na kupunguza ushawishi wa Iran katika eneo hilo. [24] Ushawishi wa Mawazo na Itikati ya Uislamu wa Kisiasa Mawazo ya Uislamu wa Kisiasa [Maelezo 1: Haya ni makundi na harakati za kifikra katika ulimwengu wa Kiislamu ambazo zina mawazo ya kuunda serikali ya Kiislamu na misingi yao muhimu ya mfumo wao huijenga kulingana na mfumo wa sheria za Kiislamu. (Rejea Kitabu: Islam Siasi cha Hosseinzadeh, Iran, 1386 Shamsia, uk. 17)] yanachukuliwa kuwa ndiyo mawazo yenye ushawishi mkubwa zaidi katika mabadiliko ya miongo kadhaa ya hivi karibuni katika eneo la Asia Magharibi. Matumizi ya mawazo haya katika muktadha wa kimadhehebu, yaliofanywa na harakati za Kisalafi na Kitakfiri, yameleta kipindi kilichojaa machafuko, vurugu, na migogoro mbali mbali ya kidini katika eneo hili. [25] Kinyume na harakati hizo za Kisalafi, pia fikra hizi zimeweza kuibua mawazo mapya kabisa ndani ya madhehebu ya Kishia, yaliyojulikana kama Mawazo ya Muqawama wa Kishia. Mawazo haya yaliibuka baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu na kuanzishwa kwa serikali ya Kishia nchini Iran. Mawazo haya yameleta mabadiliko makubwa katika mwelekeo wa matukio katika eneo hili, baada fikra zake kuungwa na Washia wengine wanaishi karibu na Iran, na hatimae kuunwa kwa makundi makundi mengine kama vile Hezbollah, vikiso vya Kishia nchini Iraq, Ansarullah kutoka Yemen, na vilevile uungwaji wake mkono na baadhi ya makundi ya Kisunni kama vile Hamas na Jihad Islamiya ya Palestina. [26]

Kuongezeji wa Nguvu za Kijeshi kwa Ajili ya Kuleta Uwiano wa Nguvu

Kuongezaji wa nguvu za kijeshi kwa nchi wanachama wa Mhimili wa Upinzani, na uboreshaji wa vifaa vya kijeshi vya makundi yanayohusiana nayo, kutokana na suala kuwepo kwa vitisho vinavyoukabili mhimili wao wa upinzani, jitihada zenye malengo kupunguza hatari dhidi ya nguvu hasimu katika eneo hilo, imekuwa ni mojawapo ya mikakati mikuu ya mhimili huu. [27] Kulingana na maelezo ya watafiti wa nyanja za usalama wa kimataifa, ni kwamba; kuongezeka kwa uwezo wa kijeshi wa wanachama wa Mhimili wa Upinzani na kuungwa mko kwao na baadhi ya nchi zenye nguvu duniani, kumesababisha ongezeko la gharama za wale wenye nia ya kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya wanachama wa Mhimili wa Upinzani.  Jambo ambalo limekuwa ni kikwazo kwa nguvu hasimu kuweza kuchukua hatua dhidi yao, au pia kama kama wataamua kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya wanachama wa Mhimili wa Upinzani, basi hilo litapelekea kula hasara kubwa kutokana kuimarika kwa wanachama wa mhimili huo imara. [28]

Hatua na Mafanikio Tangu kuanzishwa kwa Mhimili wa Muqawama, Mhimili umepitia hatua muhimu na kufikia mafanikio kahdaa kupitia harakati zake mbali mbali, jambao ambalo yameufanya kuwa ndiye mhusika mkuu katika masuala ya kikanda, pia kimataifa kwa kiasi fulani. [29] Baadhi ya hatua kuu za Mhimili huu, ni pamoja na mapambano ya makundi ya Kipalestina na Hezbollah ya Lebanon dhidi ya vitendo vya uvamizi wa Israeli, mapambano ya nchi za Iran, Iraq, na Syria pamoja na mapambano ya makundi ya muqawama dhidi ya kuenea kwa ushawishi wa DAESH (ISIS) nchini Iraq na Syria, na hatimaye, kukabiliana na uvamizi wa nchi za Kiarabu dhidi ya Yemen na dhidi ya kundi la Ansarullah ya Yemen.

Kuimarisha Nafasi ya Mashia katika Eneo la Asia Magharibi Ushawishi mkubwa wa mawazo ya Muqawama, unaotokana na mafundisho ya Kishia, umechukuliwa kuwa ni mojawapo ya sababu kuu za kuimarika kwa nafasi ya Mashia katika eneo la Asia Magharibi. [30] Kwa mujibu wa maelezo ya baadhi ya watafiti, nguvu laini au hatua nyororo ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imechangia kikamilifu suala la kuimarika na kuenea kwa ushawishi wa Mashia katika nchi kadhaa za karibu yake, kama vile Iraq, [31] Yemen, [32] na maeneo fulani ya Lebanon. [33] Aidha, watafiti wa kisiasa wamebainisha kwamba; kuboreka kwa nafasi za kisiasa na kijamii za Washia, katika muktadha wa uhusiano ya kimiamala, pia ni moja wapo ya mambo yaliochangia kuongezeka kwa nguvu ya Mhimili wa Muqawama. Hasa nchini Iraq, baada ya kuanguka kwa serikali ya Saddam na kupata nafasi ya kuvuta pumzi kwa jamii ya Mashia waliokuwa wakishii chini humo chini ya vikwazo vya chama cha Ba'ath. Jamabo liliwapa nafasi Mashia wa Iraq, na hatimae Mashia hao kushika nafasi kubwa katika mahusiano ya kisiasa na kijamii ndani ya nchi hiyo. [34]

Kukabiliana na Ukaliaji wa Kimabavu au Ukoloni wa Israeli Kwa mujibu wa mawazo ya watafiti wa kisiasa, utambulisho au uso wa kikoloni wa Israeli, na kukosa kuheshimu mipaka iliyowekwa mwaka 1948, ndiko kulikosababisha Wapalestina kuelekea kwenye uwanja wa mapambano dhidi ya Israeli na kuanzisha makundi ya jihadi kama vile; Harakati za Jihad ya Kiislamu ya Palestina na Kikundi cha Hamas. [35] Makundi haya, yalioanzishwa kwa lengo la ukombozi wa ardhi zilizobaki za Palestina, [36] yamekuwa zikikabiliana moja kwa moja na utawala wa Kizayuni katika zama mbali mbali. [37] Migogoro muhimu iliyotokana na hali hii ya ukaliaji wa kimabavu ni pamoja na; Intifada ya Kwanza na ya Pili ya Palestina, [38] Vita vya Siku 22 vya Gaza, [39] na Operesheni ya Tufani ya Al-Aqsa. [40] Hatua ya kukabiliana na ukaliaji wa Kizayuni haikuhusu makundi ya Wapalestina tu. Mwaka 2000 Miladia, Hezbollah ya Lebanon iliweza kumaliza ukaliaji wa kijeshi wa Israeli wa miaka 18 katika maeneo ya kusini mwa Lebanon. [41] Makabiliano kati ya Hezbollah na Israeli yaliendelea hadi Vita vya Siku 33, ambavyo vilianza mwishoni mwa Julai 2006, na kumalizika mwishoni mwa Agosti mwaka huo huo. [42] Baada ya Operesheni ya Tufani ya Al-Aqsa, Hezbollah iliongoza vitani dhidi ya Israeli ili kuunga mkono wakazi wa Gaza, ambapo kulikuwa na makabiliano makubwa ya risasi kati ya pande hizo mbili. [43] Katika migogoro vita hivyo, Sayyid Hassan Nasrallah, Katibu Mkuu wa tatu wa Hezbollah, pamoja na baadhi ya makamanda wake, waliuawa kama mashahidi wakiwa katika mapambano dhidi ya utawala wa Kizayuni. [44] Aidha, ukaliaji wa maeneo ya Syria, hasa Milima ya Golan, pamoja na utawala wa Kizayuni wakati wa Vita vya Siku Sita kati ya Israeli na nchi za Kiarabu mwaka 1967 (tarehe 5 Juni mwaka 1967), ndiyo uliochochea kuibuka kwa uadu katika mahusiano ya kisiasa kati ya Syria na Israeli. [45] Baada ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, hasa tangu kuanza kwa urais wa Hafedh al-Asad na kuendelea na utawala wa mwanawe Bashar nchini Syria, uhusiano wa kiadui kati ya Syria na Israeli uliimarika zaidi, na hatimae kusababisha kuundwa kwa muungano na kuimarika kwa mahusiano ya karibu kati ya Iran na Syria [46]. Kwa mujibu wa maoni ya watafiti ni kwamba; moja ya sababu kuu za kuimarika kwa muungano huo ni kufanana kwa maoni na itikadi kati ya nchi mbili hizi juu ya kukabiliana na Israeli na kukisaidia kikundi cha Hezbollah ya Lebanon. [47] Kukabiliana na Vitisho vya Daesh Ndani ya Maeneo ya Syria na Iraq Utekwaji kwa maeneo muhimu katika nchi za Syria na Iraq kulikofanya na makundi ya Kisalafi, pamoja na makundi mengine ya kitakfiri hasa Daesh, kulipelekea Mhimili wa Muqawama (Mhimili wa Upinzani) kuimarisha upya muungano wake, kwa lengo la kukabiliana na vitisho vya kijeshi, kisiasa, kiuchumi na kijamii katika eneo hilo. [48] Kutokana na hali hii, serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilianza juhudi maalumu za kuzuia kusambaa kwa Daesh kwa kupeleka wanajeshi na kutoa ushauri wa kiusalama nchini Iraq na Syria. [49] Zaidi ya hayo, miongoni mwa malengo makuu ya kutumwa kwa wanajeshi katika maeneo hayo, ilikuwa ni kulinda maeneo matakatifu, ikiwa ni pamoja na Haram (kaburi) ya Bibi Zainab (a.s). [50] Ulinzi wa Ansarullah ya Yemen Dhidi ya Uvamizi wa Nchi za Kiarabu kwa Yao Kikundi cha Harakati za Ansarallah, kiilichoundwa mwaka 1990, [51] ni mojawapo ya harakati za kisiasa na kidini za Yemen [52] ambazo zinadaiwa kwamba; msukumo wa kuasisiwa kwake unatokana na mafundisho ya Imam Khomeini pamoja na Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran. [53] Harakati hizi zilijiitokeza mnamo mwaka 2011, katika kipindi cha harakati za Mwamko wa Kiislamu dhidi ya serikali ya Yemen, na hatimae wanaharakati hawa walifanikiwa kushikilia maeneo kadhaa ya nchi hiyo. Hatua hiyo ilipelekea kuondoka madarakani kwa Mansour Hadi, Rais wa zamani wa Yemen, ambaye alihama na kuelekea Aden, na hivyo kusababisha kuanzishwa kwa serikali ya muda. [54] Kufuatia hatua za Mansour Hadi, baadhi ya nchi za Kiarabu zilianza mashambulizi makubwa ya kijeshi dhidi ya Ansarallah ili kurejesha serikali ya Mansour Hadi madarakani, [55] ila baada ya upinzani wa miaka kadhaa wa Ansarallah, mashambulizi ya nchi hizo hayakufaulu. [56] Kuimarika kwa Roho ya Upinzani Dhidi ya Marekani katika Eneo la Asia Magharibi Kuibuka kwa roho ya upinzani dhidi ya Marekani na kupungua kwa ushawishi wake katika eneo la Asia Magharibi, ni miongoni mwa mafanikio makubwa ya Mhimili wa Muqawama (Mhimili wa Upinzani) katika eneo hilo. [57] Watafiti wanadai kuwa; baada ya kuanguka kwa Umoja wa Kisovyeti mwaka 1991, Marekani ilijaribu kujidhihirisha kama ni nguvu kuu katika eneo la Asia Magharibi ili kulinda usalama wa Israeli na kuhifadhi maslahi yake katika eneo hilo. [58] Ili kufanikisha maengo yake, Marekani ilitekeleza mikakati mbalimbali, ambayo kwa bahati mbaya ilichangia kuibuka kwa makundi ya Kitakfiri na kuongeza mizozo ya kimadhehebu, hatimae kusababisha kuyumba kwa utulivu wa nchi za eneo hilo. [59] Kinyume na mikakati hii, Mhimili wa Muqawama umeimarisha sera maalumu za kupinga uonevu na kuchukua hatua madhubuti katika safari ya kutimiza malengo hayo. Miongoni mwa hatua zake ni pamoja na kupambana na makundi ya Kitakfiri, kupigania ukombozi wa Palestina dhidi ya Israel, na kuweka shinikizo hasi la kiuchumi dhidi ya Marekani, lililoibebesha hasara kubwa kwa Marekani. Hatua hizi zimewezesha kukwamisha mipango ya Marekani na kuimarisha zaidi hisia za upinzani dhidi yake katika eneo la Asia Magharibi. [60] Shughuli za Vyombo vya Habari vya Mhimili wa Muqawama Vikosi vya Mhimili wa Muqawama (Mhimili wa Upinzani) vimeanzisha mitandao na vyombo vya habari mbalimbali kwa lengo la kuripoti shughuli zao. Miongoni mwa mitandao hiyo ni pamoja na: • Al-Manar (inayohusiana na Hezbollah ya Lebanon) [61] • Al-Mayadeen (mtandao wa habari wenye makao yake makuu Beirut) [62] • Al-Masirah (inayohusiana na Ansarallah ya Yemen) [63] • Al-Furat (mtandao wa Baraza Kuu la Kiislamu la Iraq) [64] • Al-Ghadir (televisheni ya satelaiti ya Kikosi cha Badr cha Iraq) [65] • Al-Ittijah (kituo cha habari cha Kata’ib Hezbollah ya Iraq) [66] • Al-Ahd (kituo cha habari cha Harakati ya Asa’ib Ahl al-Haq ya Iraq) [67] Zaidi ya hayo, Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB), nalo pia hutoa habari na uchambuzi wa kina kuhussiana na shughuli za Mhimili wa Muqawama, hasa baada ya Operesheni ya Tufani al-Aqsa. Miongoni mwa vipindi vya televisheni vinavyorushwa kupitia shirika hli la habari, ni kipindi kijulikanacho kwa jina la “Be Ufuqe Felestiin” (Kuelekea Upeo wa Palestina). [69] Mitandao ya habari kama vile; Al-Alam, Press TV, na IRIB News, inayomilikiwa na Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, imechangia pakubwa katika kuripoti matukio yanayohusiana na mhimili wa muqawama. [70] Makala Zilizohusiana: Walinzi wa Haram/Mudafiane Haram Ukaliwaji Kimabavu wa Palestina Qasem Soleimani Ismail Haniyyah Abdul Malik Al-Huthi