Ismail Haniyeh

Kutoka wikishia
Ismail Abdus-Salam Ahmad Haniyeh

Ismail Haniyeh (Kiarabu: إسماعيل هنية) (1962/1963-2024) alikuwa Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Hamas ambaye aliuawa na Israel huko Tehran.

Haniyeh alikuwa miongoni mwa viongozi wa Muqawama (mapambano) wa Kiislamu dhidi ya ukaliaji wa Palestina na alijitahidi kuikomboa Palestina kutoka kwa ukaliaji wa utawala wa Kizayuni. Aliwekwa gerezani mara kadhaa na Israeli na mwaka 1992 alifukuzwa kwenda kusini mwa Lebanon.

Kuuawa kwa Haniyeh huko Tehran kulizua hisia tofauti. Viongozi na taasisi mbalimbali za kisiasa na kidini zililaani kitendo hicho cha kinyama. Waislamu katika nchi mbalimbali walisimama na kufanya maandamano makubwa ya kupinga mauaji hayo. Mwili wa Haniyeh ulisaliwa mjini Tehran kisha kusafirishwa mnamo tarehe mosi August 2024 kuelekea nchini Qatar. Sala ya maiti ya Haniyeh ilisalishwa na Ayatullahi Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Kiislamu ya Iran. Hatimae mnamo tarehe 2 August, Ismail Haniyeh alizikwa nchini Qatar akibakisha mshangao katika historia ya uwanja wa kugombea uhuru.

Haniyeh hakuwa tu ni mwanaharakati wa kugombea uhuru bali alishika nafasi mbali mbali za kisiasa, miongoni mwa nyadhifa alizowahi kushika ni; Rais wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas kutoka mwaka 2017 hadi 2024, Waziri Mkuu wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina, Rais wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Gaza, na Mkuu wa Ofisi ya Sheikh Ahmed Yassin. Kifo chake kimjengea heshima kubwa kwenye jamii ya Kiislamu, yeye anahisabiwa kama ni nembo ya upinzani wa Palestina, pia amepewa jina la "Shahidi wa Quds" kama ni heshima maalumu kutokana na juhudi zake.

Upambanaji Dhidi ya Ukaliwaji wa Kimabavu wa Israeli

Ismail Haniyeh alikuwa ni kiongozi wa harakati ya Muqawama wa Kiislamu wa Palestina ya Hamas. Naye anajulikana kama nembo.[1] ya Muqawama na mapambano ya Palestina.[2] aliyepewa jina la Shahidi wa Quds. Haniyeh alikamatwa mara kadhaa na kutiwa kizuizini na Israel, ikiwa ni pamoja na tukio la mwaka 1989, ambapo aliwekwa gerezani kwa muda wa miaka mitatu.[3] Mnamo mwaka 1992, yeye pamoja na wanaharakati wengine wa Hamas na wapambanaji wa Kiislamu, alifukuzwa kwa na kutengwa na mji wake kwa muda wa mwaka mmoja, ambapo wote kwa pamoja walilazimika kuishi mji wa Marj al-Zuhoor kusini mwa Lebanon.[4] Watoto wake watatu na wajukuu wake watatu pia waliuawa katika mashambulizi ya Israel dhidi ya Gaza mnamo tarehe 10 Aprili 2024.[5]

Uongozi wa Kisiasa wa Kundi la Hamas

Ismael Haniyeh:
«Kauli Mbiu ya Haniyeh: Katu na Kamwe hatutathubutu kuitambua Israel».[6]

Ismail Haniyeh alikuwa ni kiongozi mashuhuri ndani ya harakati ya kundi la Hamas. Haniyeh alichukua uongozi wa kisiasa wa Hamas mnamo Mei 6, 2017, akimrithi Khaled Meshaal.[7] Kabla ya hapo, baada ya kushinda uchaguzi wa mwaka 2006 nchini Palestina, Ismail Haniyeh aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina. Ushindi huo uliashiria mwanzo mpya katika siasa za Palestina, ambapo Haniyeh alionekana kama kiongozi thabiti na mwenye kujitolea kwa dhati katika harakati za ukombozi wa taifa lake. Pia, kwa muda fulani alihudumu kama Mkuu wa Ofisi ya Sheikh Ahmed Yassin. Katika nafasi hii, Haniyeh alijifunza mengi kutoka kwa Sheikh Yassin, ambaye alikuwa kiongozi na mwanzilishi wa harakati za Hamas. Huduma yake katika ofisi ya Sheikh Yassin ilimsaidia kuimarisha uongozi wake na kupata uelewa wa kina kuhusu harakati za ukombozi wa Palestina. Uzoefu huu ulimsaidia baadaye katika uongozi wa kisiasa na kijamii, na kuimarisha nafasi yake kama kiongozi thabiti na mwenye maono katika harakati za ukombozi wa Palestina. .[8]

Mnamo mwaka wa 2018, serikali ya Marekani alimweka Haniyeh katika orodha ya magaidi.[9] Katika miaka ya mwisho ya maisha yake, aliishi Qatar. Hatua hii iliongeza shinikizo la kimataifa dhidi yake, lakini pia ilionyesha kuendelea kwake na msimamo wake thabiti dhidi ya uonevu wa Israel na washirika wake. Kule Qatar, Haniyeh aliendelea kushiriki katika shughuli za kisiasa na kidiplomasia, akijaribu kuunganisha na kuimarisha harakati za ukombozi wa Palestina.[10]

Uhusiano Wake na Mrengo wa Upinzani

Katika kipindi chake cha mapambano na shughuli za kisiasa, Ismail Haniyeh aliendeleza uhusiano wa karibu na viongozi wa mrengo wa upinzani. Haniyeh alisafiri mara kadhaa kwenda Iran, ambapo alikutana na maafisa wa ngazi za juu, ikiwa ni pamoja na Ayatullah Khamenei, kiongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Kwenye mikutano yake na viongozi hao, alitilia mkazo suala la ushirikiano wa pamoja na kuimarisha mshikamano dhidi ya vitisho vya kigeni na dhuluma mbali mbali.[11] Ismail Haniyeh alikuwa ni miongoni mwa viongozi waliohudhuria katika hafla za mazishi ya Qassim Suleimani, kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH), [12] pia alikuwepo katika hafla ya mazishi ya Sayyid Ibrahim Raisi, ambaye alikuwa ni Rais wa nane wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilizofanyika Tehran.[13]Zaidi ya hayo, pia Haniyeh alifanya mikutano kadhaa na Sayyid Hassan Nasrallah, Katibu Mkuu wa Hizbullah, ambapo walijadiliana naye juu ya masuala muhimu ya ushirikiano na mikakati ya pamoja. Ushirikiano huu ulikuwa na umuhimu mkubwa katika kuimarisha mapambano dhidi ya changamoto zinazokumba eneo hilo na kuendeleza malengo ya pamoja ya mrengo wa upinzani.[14]

Mauaji ya Ismail Haniyeh yaliyo tekelezwa na Israeli katika ardhi ya Iran, yameamsha hisia mbalimbali duniani. Wataalamu wengine wanaona kwamba; mauaji haya yameongeza umoja kati ya vikundi vya upinzani katika kupambana na utawala wa Kizayuni, huku pia yakisababisha kutengwa kwa Israel kwenye medani (nyanja) za kimataifa.[15]

Kuuawa Kwake

Usindikizaji wa Jeneza la Ismael Haniyeh katika mji wa Tehran, mnamo tarehe 1 August 2024.

Ismail Haniyeh aliuawa kishahidi katika hali ya utatanishi mnamo tarehe 10 August mwaka 1403 hijria (25 Muharram 1446 hijria) katika makazi ya hoteli ya wastaafu wa kijeshi waliojeruhiwa vitani, huko mjini Tehran.[16] Yeye alikuwa amesafiri hadi Tehran kwa ajili ya kushiriki katika hafla ya kuapishwa kwa Rais wa tisa wa Iran. Katika hafla hii, ambayo ilikuwa ni tukio muhimu la kitaifa, alikuwepo kama mgeni wa heshima, akishiriki katika kuadhimisha hatua hii muhimu katika historia ya Iran.[17] Kikundi cha Harakati za Hamas.[18] na Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran.[19] walidai kuwa mauaji ya Ismail Haniyeh yanahusiana moja kwa moja na utawala wa Kiyahudi wa Israel. Kwa upande mwingine, ofisi ya habari ya utawala wa Kiyahudi ilitoa taarifa rasmi ikikiri kuhusika kwake katika tukio hilo la kikatili.[20] Hii ilizua majadiliano ya kimataifa kuhusu usalama na uhusiano wa kimataifa, na kuongeza mvutano kati ya pande zinazohusika na mzozo wa Kiyahudi na Kipalestina. Katika zama tofaoti za mwaka 2003 na 2006, utawala wa Kiyahudi wa Israel ulifanya majaribio ya kumuua Ismail Haniyeh kwa kupitia mashambulizi ya anga. Hata hivyo, Haniyeh aliweza kupona kutokana na mashambulizi hayo, na kuendelea na shughuli zake za mapambano dhidi ya udhibiti wa Kiyahudi wa eneo la Palestina.[21] Haya yalionyesha uthabiti na ujasiri wake katika kukabiliana na changamoto za hali ngumu katika vita vya kisiasa na kijeshi dhidi ya dhulma.

Mazishi Yake Nchini Qatar

Ayatullah Khamenei akiongoza Sala ya maiti katika mji wa Tehran.

Mnamo tarehe 11 Murdad Shamsia (tarehe mosi August 2024), Ayatullah Khamenei, Kiongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, alikuwa ndiye aliye salisha sala ya maiti katika kuusalia mwili wa Ismail Haniyeh. Baada ya sala hiyo, mwili wa Haniyeh ulisindikizwa kwa heshima kubwa na wananchi wa Iran, wakimpa heshima zao za mwisho kiongozi huyo shujaa na mzalendo wa Palestina.[22] Mnamo tarehe 2 August 2024, mwili wa Ismail Haniyeh ulisafirishwa hadi Doha, mji mkuu wa Qatar, ambako mazishi yake yalihudhuriwa na halaiki ya watu, wakiwemo viongozi mbali mbali wa kisiasa na kidini, akiwemo mfalme wa Qatar. Hatimae mwili wa Haniyeh ulizikwa katika mji wa Lusail, karibu na Doha nchini Qatar.[23] Swala ya maiti iliyosalishwa na Ayatollah Khamenei, Kiongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na faqihi wa Kiislamu wa Kihia, katika kuusalia mwili wa Ismail Haniyeh, mpiganaji wa Kisunni, ibada ambayo ilifanyika katika mji mkuu wa Kishia na kuhudhuriwa na Waislamu wengi kutoka madhehebu ya Kishia, kulivutia vyombo vya habari na watumiaji wa mitandao mbamlbali ya kijamii.[24] Tukio hili lilipata umaarufu mkubwa katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, likionesha mshikamano na umoja kati ya Waislamu wa madhehebu mbalimbali duniani.[25]

Sayyid Ali Khamenei, kiongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran:

Kiongozi shupavu na mpigania jihad wa Palestina Bw. Ismail Haniyeh alfajiri ya leo ameaga dunia na wanaharakati wa upinzani kwa masikitoko makubwa wameomboleza... Shahidi Haniyeh alijitolea maisha yake ya thamani kwa miaka mingi katika uwanja wa mapambano na alikuwa tayari kuuawa shahidi yeye na wafuasi wake, na aliwatoa watoto na watu wake kipaumbele katika kupigania njia ya hii. Hakuogopa kuwa shahidi katika njia ya Mungu na kuwaokoa watumishi wa Mungu.[26]

Muitikio ya Tukio la Mauaji

Kuuawa kwa Haniyeh kuliamsha hisia za watu mbali mbali na kusababisha msururu wa makombora ya majibu kutoka kwa viongozi wa kisiasa na kidini. Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.[27] pamoja na mafaqihi maarufu wa Kishia kama vile; Nuri Hamedani,[28] Nassir Makarim Shirazi.[29] na Abdullah Jawadi Amuli.[30] ni miongoni wa watu wa kwanza waliotoa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Haniyeh. Rais wa Uturuki.[31] vikundi vya upinzani dhidi ya dhulma kama Hizbullah ya Lebanon, Kikundi cha Harakati cha Ansarullah cha Yemen, Kikundi cha Harakati za Jihad ya Kiislamu cha Palestina, Waziri Mkuu wa Lebanon, mawaziri wa mambo ya nje wa nchi mbali mbali kama vile; China, Uturuki, Urusi, Syria, Qatar, Jordan, Misri, Iraq, Pakistan, na Oman, vikundi huru ya Palestina, Kikundi cha Harakati cha Fatah, Kikundi Harakati cha Hikma Milli Iraq, na Ikhwanul Muslimin wa Jordan wote walilaani mauaji ya kinyama ya Haniyeh.[32] Mawaziri wa Mambo ya Nje wa baadhi ya nchi kama vile Iraq, Oman.[33] na Jordan walilaani vikali mauaji ya Haniyeh wakilihisabu jambo hili kuwa ni ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa, na kusema kwamba jambo hili ni tishio kwa usalama na utulivu wa kanda mzima ulioko karibu na tukio hilo.[34] Walisisitiza kwamba kitendo hicho kinavuruga amani na kuongeza mvutano katika eneo hilo lenye migogoro.

Viongozi hawa walionyesha mshikamano wao na kuendelea kulaani vitendo vya kigaidi dhidi ya wapiganiaji wa uhuru wa Palestina, huku wakiutaka kimataifa kuchukua hatua madhubuti dhidi ya ukiukaji wa haki za binadamu. Mwitikio huu wa pamoja ulionesha umoja na mshikamano wa kiitikadi na kisiasa kati ya nchi na harakati mbalimbali katika kanda hiyo, na zaidi, kuthibitisha azma yao ya kuunga mkono mapambano ya Wapalestina dhidi ya uvamizi na ukoloni. Mauaji ya Haniyeh yalizua hasira za maandamano katika nchi mbalimbali duniani. Miongoni mwa nchi zilizoandama kufuatia tukio hili ni; Yemen.[35] Jordan.[36] Uturuki, Morocco, Tunisia, na Lebanon.[37] ambapo watu waliandamana kulaani kitendo hicho. Nchi ya Iran na Yemen.[38] zilitangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa, huku Palestina ikitangaza siku moja ya maombolezo kufuatia tukio hilo.[39] Aidha, bendera nyekundu yenye kauli mbiu isemayo Ya Latharat Al-Hussein, yenye ishara ya matakwa ya kulipiza kisasi, ilipepea juu ya Msikiti wa Jamkaran, moja ya vituo vya kidini vya Kishia huko Qom. [40]

Katika mwitiko wa haraka, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilifanya kikao cha dharura ambapo baadhi ya wanachama wake walilaani vikali mauaji ya Haniyeh.[41] Maandamano na maombolezo ya yaliyo fanyika ndani ya nchi mbali mbali, yalionyesha mshikamano wa kimataifa dhidi ya mauaji hayo na kuonesha hasira na huzuni ya jamii ya kimataifa kuhusu kupotea kwa kiongozi muhimu wa harakati za ukombozi wa Palestina.[42]

Ahadi ya Kulipiza Kisasi

Picha ya mwisho kabisa kati ya Ayatullah Khamenei na Ismael Haniyeh siku moja kabla ya umauti kumkuta.

Katika ujumbe wake wa rambirambi, Ayatollah Khamenei alisisitiza kwamba mauaji haya yametokea ndani ya Iran, na hivyo kulipiza kisasi kwa ajili ya damu ya Haniyeh ni jukumu la Iran. Alitangaza kuwa adhabu kali itatolewa kwa wale waliohusika na mauaji hayo.[42] Sayyid Hassan Nasrallah,[43] na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (Sepah Pasdaaraan)[44] pia nao walilaani vikali mauaji ya Haniyeh yaliyofanywa na utawala wa Kizayuni na kuahidi majibu makali ya kulipiza kisasi katika kuamiliana na tukio hilo. Hamas pia nayo ililaani vikali kitendo hichi, ikikielezea kama ni kitendo cha kihuni na cha kinyama. Walisisitiza kwa nguvu kwamba mauaji haya ya Esmail Haniyeh hayataachwa bila jibu.[45] Katika taarifa yao rasmi, viongozi wa Hamas walionyesha hasira zao kali na walitangaza kuwa watachukua hatua kali ili kulipiza kisasi kwa ajili ya kiongozi wao, na katu hawataachana na harakati zao za kiukombozi. Mnamo tarehe 7 August, ili kuhakikisha uongozi thabiti na unaoendelea nchini Palestina, Hamas ilifanya uchaguzi wa kiongozi mpya na kumchagua Yahya Sinwar kuwa kiongozi wa juu wa harakati hiyo. Chaguo hili lilikuwa ni ishara ya kujitolea kwa nguvu katika kuendeleza malengo yao ya ukombozi, huku wakionesha dhamira yao ya kuimarisha msimamo wao dhidi ya utawala wa Kizayuni. Yahya Sinwar, ambaye alikuwa na uzoefu mkubwa katika harakati za mapambano, alikubali jukumu hilo na aliahidi kuendeleza juhudi za Hamas kwa lengo la kudumisha umoja na kupinga ukandamizaji wa Israel.

Elimu na Utendaji Wake

Ismail Haniyeh na kundi la maafisa wa Hamas, akiwa amesimama karibu na Sayyid Hassan Nasrallah

Ismail Abdus Salam Ahmed Haniyeh, anayejulikana kiumaarufu kwa jina la Ismail Haniyeh au Abul Abd, ima alizaliwa mnamo tarehe 23.[46]au tarehe 29 Januari.[47] mwaka 1962.[48] au pia yawezekana kuwa mnamo mwaka 1963.[49] katika kambi ya al-Shati ilioko huko Gaza. Alipata elimu yake ya msingi katika kambi hiyo hiyo na baadaye akaendelea na masomo yake ya ngazi za juu katika Chuo Kikuu cha Gaza.[50] ambapo alihitimu katika taaluma ya Fasihi ya Kiarabu mwaka mnamo 1987.[51] Haniyeh alishika nyadhifa kadhaa za uongozi katika sekta mbali mbali za kielimu. Aliwahi kuwa Katibu wa Bodi ya Wadhamini wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Gaza, Mkurugenzi wa Kisayansi wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Gaza, na mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Chuo Kikuu cha Gaza. Alihudumu kama Rais wa Kamati ya Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Gaza kwa zaidi ya miaka kumi.[52] baadaye Haniyeh alikuja kuchaguliwa kuwa Rais wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Gaza.[53] Kwa pamoja, majukumu haya yalithibitisha mchango mkubwa wa Haniyeh katika kukuza na kuimarisha elimu na utamaduni katika nyanja hizo, huku akichangia kwa kina katika maendeleo ya kitaaluma na kiroho katika jamii ya watu wa Gaza.

Rejea

  1. Lihat: Faidan: Haniye Nemad Muqawemat Falestin Bud, Tovuti Anadolu; Ismail Haniye; Rahbari Ke Nemad Muqawemat Siyasi Wa Nedhami Falestin, Tovuti Mehr News.
  2. Lihat: Maraseme Gerami Dasht Shahid al-Quds Ismail Haniye, Tovuti IRNA; Peyman Jebhe Muqawemat Az Tehran Ta Gaza; Enteqam Khun Shahid al-Quds Qat'i Ast, Tovuti Mehr News; Peikar Shahid al-Quds Dar Khane Abadi Aram Gereft, Tovuti Mashregh News.
  3. Guzaresh ha Az Teror Ismail Haniye Rahbar Siyasi Hamas Dar Tehran, Tovuti BBC Persian; Ismā'īl Haniyyah.. Lāji' Min Mukhayyam as-Shāthi' Qāda Harakat Hamās, Tovuti Aljazeera Net.
  4. Ismail Haniye Mulaqqab Be Abul Abd Ke Bud? Tovuti Mehr News; Ismail Haniye Ke Bud? Tovuti ISNA.
  5. Ismail Haniye Ke Bud? Tovuti ISNA.
  6. Ismail Haniye Ke Bud? Tovuti Alalam Persian.
  7. Ismail Haniye Mulaqqab Be Abul Abd Ke Bud? Tovuti Mehr News; Guruh Islamgiray Hamas Chist? Tovuti BBC Persian; Ismā'īl Haniyyah.. Lāji' Min Mukhayyam as-Shāthi' Qāda Harakat Hamās, Tovuti Aljazeera Net.
  8. Ismā'īl Haniyyah.. Lāji' Min Mukhayyam as-Syāthi' Qāda Harakah Hamās, Tovuti Aljazeera Net. Negahi Be Zendegi Wa Eqdamat Shahid Ismail Haniye, Tovuti Tasnim News.
  9. Ismail Haniye Mulaqqab Be Abul Abd Ke Bud? Tovuti Mehr News.
  10. Guzaresh ha Az Teror Ismail Haniye Rahbar Siyasi Hamas Dar Tehran, Tovuti BBC Persian; Ismā'īl Haniyyah.. Lāji' Min Mukhayyam as-Shāthi' Qāda Harakat Hamās, Tovuti Aljazeera Net.
  11. Guzaresh ha Az Teror Ismail Haniye Rahbar Seyasi Hamas Dar Tehran, Tovuti BBC Persian.
  12. Lihat: Didar Ismail Haniye Ra'is Daftar Seyasi Hamas Ba Rahbar Enqelab, Tovuti Khamenei; Didar Nukhust Wazir Falestin Wa Hei'at Hamrah Ba Rahbar Enqelab, Tovuti Khamenei.
  13. Ismā'īl Haniyyah: Qasim Sulaimani Shahid al-Quds Tovuti Aljazeera Mubasher Net.
  14. Huzur Ismail Haniye Dar Marasem Tasyi' Peikar Ra'is Jumhur, Tovuti Tasnim News.
  15. Lihat: Sayid Hasan Nasrullah Ba Haniye Dar Beirut Didar Kard, Tovuti Mehr News.
  16. Pas Az Teror Shahid Haniye, Jebhe Muqawemat Wared Marhale Ta'yin Kunande'i Shud, Tovuti Mehr News.
  17. Ismail Haniye Dar Tehran Kushte Shud, Tovuti Anadolu.
  18. Ismail Haniye Dar Tehran Kushte Shud, Tovuti Anadolu.
  19. Bayaniye Hamas Dar Pei Shahadat Ismail Haniye, Tovuti Alalam Perisan.
  20. Bayaniye Wezarat Umur Khareje Jumhuri Eslami Iran Dar Khusus Shahadat Rais Daftar Seyasi Junbesh Muqawemat Falestin, Tovuti MFA GOV Ir.
  21. Dar Pei Shahadat Ismail Haniye, Se Ruz Azae Umumi Dar Keshwar E'lam Shud, Tovuti Mehr News.
  22. Ismā'īl Haniyyah.. Lāji' Min Mukhayyam as-Shathi' Qada Harakat Hamas, Tovuti Aljazeera Net; Isma'il Haniye Ke Bud? Tovuti ISNA.
  23. Marasem Tashi'i Jenaze Ismail Haniye Rais Daftar Seyasi Hamas Dar Tehran Barguzar Shud, Tovuti Anadolu; Guzaresh ISNA Az Tashi'i Peikar Ismail Haniye Shahid Dar Tehran, Tovuti ISNA.
  24. Ismail Haniye Dar Qatar Be Khak Sepurde Shud, Tovuti Euro News.
  25. Lihat: Badraqe Irani Haniye, Tovuti Javan Online.
  26. Wakunesh Karbaran Majazi Be Tashi'i Peikar Shahid Ismail Haniye Dar Iran, Tovuti YCJ.
  27. Payam Rahbar Enqelab Eslami Dar Pei Shahadat Mujahed Buzurg Agha Ismail Haniye, Tovuti Khamenei.
  28. Ayatullah Nuri Hamedani: Shahadat Haniye Rah Mehwar Rezim Sahyunisti Ra Hamware Khahad Kard, Tovuti IRNA.
  29. Wakunesh Ayatullah Makarem Shirazi Be Teror Haniye; Dushman Kinetuz Ra Be Ashad Mujazat Beresonid, Tovuti IRNA.
  30. Payam Yek Marja' Taqlid Dar Wakunesh Be Teror- Shahid Dar Tehran, Tovuti Hamshahri Online.
  31. Erdogan Teror Ismail Haniye Dar Tehran Be Syeddat Mahkum Kard, Tovuti Anadolu.
  32. Wakunesh ha Be Shahadat Ismail Haniye, Tovuti ISNA; Dar Pei Shahadat Ismail Haniye 3 Ruz Aza Umumi Dar Keshwar E'lam Shud, Tovuti Mehr News.
  33. Al-'Irāq: Ightiyal Haniyyah Fi Iran 'Amaliyah 'Udwaniyah Wa Tahdid Li Istiqrar al-Mantiqat, Tovuti Alforat News.
  34. Wakunesh ha Beinul Melali Be Teror Shahid Haniye Dar Tehran, Tovuti Fars News.
  35. Ejtema' Mardum Yaman Dar Mahkumiyat Tror Haniye, Tovuti Alalam Persian.
  36. Tazahurat Gustarde Dar Urdun Dar Mahkumiyat Teror Haniye, Tovuti Alalam Perisan.
  37. Ightiyal Haniyah.. Ghadhab Wa Muzaharat Bi'Iddat Duwal Wa Da'wat Li Tard as-Safir al-Amriki, Tovuti Aljazeera Net.
  38. Dar Pei Shahadat Ismail Haniye, 3 Ruz Aza Umumi Dar Keshwar E'lam Shud, Tovuti Mehr News.
  39. Mahmud Abbas Yek Ruz Aza Umumi E'lam Kard, Tovuti Tasnim News.
  40. Ehtezaz Parcham Surkh Enteqam Barafraz Gunbad Firuzei Jamkaran, Tovuti Mehr News.
  41. Barkhi Az A'za Shura Amniyat Teror Haniye Ra Mahkum Kardand, Tovuti Anadolu.
  42. Payam Rahbar Enqelab Eslami Dar Pei Shahadat Mujahed Buzurg Agha Ismail Haniye, Tovuti Khamenei.
  43. Sayid Hasan Nasrullah: Iran Teror Haniye Ra Khudesh Be Amniyat Wa Hakimiyat Khud Mi Danad, Tovuti Alalam Persian.
  44. Ettela'iye Jadid Sepah: Pasukh Sakht Wa Dardnak Muqawemat Dar Rah Ast, Tovuti Fars News.
  45. Wakunesh ha Be Shahadat Ismail Haniye, Tovuti ISNA.
  46. As-Sinwar Ra'isan Li Hamas Khalfan Li Haniyah, Tovuti Aljazeera.
  47. As-Sinwār Ra'isan Li Hamas Khalfan Li Haniyah, Tovuti Aljazeera.
  48. Ismā'īl Haniyah.. Lāji' Min Mukhayyam as-Shathi' Qada Harakat Hamas, Tovuti Aljazeera Net.
  49. Ismail Haniye Mulaqqab Be Abu al-Abd Ke Bud? Tovuti Mehr News; Ismail Haniye Ke Bud, Tovuti Alalam.
  50. Ismail Haniye Ke Bud? Tovuti ISNA.
  51. Ismail Haniye Mulaqqab Be Abu al-Abd Ke Bud? Tovuti Mehr News; Ismail Haniye Ke Bud, Tovuti Alalam.
  52. Ismail Haniye Ke Bud? Tovuti Alalam.
  53. Ismail Haniye Ke Bud?, Tovuti ISNA.

Vyanzo