Nenda kwa yaliyomo

Kikundi cha Kiislamu cha Harakati za Jihadi cha Palestina

Kutoka wikishia
Harakati ya Jihadul Islami ya Palestina

Harakati ya Jihadul Islami ya Palestina (Kiarabu: حركة الجهاد الإسلامي في فلسطين) Ni kikundi cha muqawama na upinzani kinachojulikana kwa msimamo wake dhidi ya uvamizi wa Israel katika ardhi za Palestina. Harakati hii ilianzishwa na Fat-hi Shiqaqi mnamo mwaka 1981 huko Gaza. Nia na imani ya kuanzishwa kwake, ni kutumia mbinu maalumu za kivita ili kupinga utawala wa Israel na kuipatia uhuru kamili ardhi hiyo ya Palestina. Mbinu fikra za uanzilishi wake zinatokana na mawazo ya Imam Khomeini, ambaye alisisitiza kwamba njia pekee ya kuondoa ukoloni wa Kiyahudi, ni kupingana na utawala huo kwa kutumia nguvu.

Misingi hasa ya harakati hizi, ni imani thabiti juu ya mafundisho ya Kiislamu na kukataa rasmi kuitambua Israel kama taifa halali. Harakati hizi imekuwa na matawi ya kijeshi ambayo yameendesha mashambulizi kadhaa dhidi ya Israel, wakati Israel nayo imejibu kwa kuua baadhi ya viongozi wa kijeshi wa kukundi cha harakati hizi, kwa nia ya kuendelea kuikalia ardhi hiyo kimabavu. Katibu Mkuu wa harakati hii ni Ziyad al-Nakhalah ambaye anahusika na usimamizi wa shughuli na sera za harakati hizi kwa sasa. Kabla ya Ziyad al-Nakhalah kuchukua jukumu hili, Ramadhani Abdullah ndiye aliye kuwa akiongoza harakati hizi, akichangia katika kupanga mikakati na kuhakikisha utekelezaji wa malengo ya harakati mbali mbali. Kabla ya Ramadhani Abdullah, Fathi Shiqaqi ndiye aliyekuwa akisimamia harakati hizi, akiwa na jukumu la kutoa mwongozo wa kuongoza hatua za maendeleo na maamuzi muhimu ndani yake. Nchi kadhaa, ikiwa ni pamoja na Marekani na Uingereza, pamoja na Umoja wa Ulaya, zimejumuisha kikundi cha harakati hizi katika orodha yao ya makundi ya kigaidi. Hii ina maana kwamba; kikundi hichi kinahidabiwa kuwa ni tishio la usalama wa kimataifa na linakubalika rasmi kama ni kundi linaloshiriki katika vitendo vya kigaidi. Katika muktadha huu, Marekani na Uingereza, kwa kutumia mifumo yao ya sheria na ulinzi, wameweka vikwazo vya kiuchumi na kijamii dhidi ya kikundi hicho, huku wakizuia ushirikiano wa kimataifa na kutoa mwongozo kuhusiana na hatua zinazopaswa kuchukuliwa dhidi yake. Umoja wa Ulaya, kwa upande wake, umeongeza hatua za usalama na ufuatiliaji ili kuhakikisha kwamba kikundi cha harakati hizi hakipati rasilimali au aina yoyote ile ya msaada wa kimataifa.

Utambulisho Pamoja na Uanzishwaji Wake

Harakati ya Jihadul Islami ni moja wapo wa makundi yenye mwamko wa kijihadi, kundi ambalo linaamini kwamba; hakuna njia ya kupata uhuru zaidi ya kupambana na serikali ya Kizayuni. [2] Mwamko huu umepata umaarufu mkubwa kutokana na msimamo wake mkali na thabiti wa kutafuta uhuru na kukataa kata kata mahusiano na Israel. [2] Harakati hizi zinasisitiza kwamba; upinzani wa silaha ndio njia pekee ya kuhakikisha ukombozi wa Jerusalem, jambo ambalo ni kinyume kabisa na makubaliano ya amani au ushirikiano wa kisiasa na Israel. Ingawa Kikundi cha Kiislamu cha Harakati za Jihadi cha Palestina, ni moja ya vikundi muhimu vya upinzani dhidi ya uvamizi wa Israel, ila kinaungwa mkono kwa kiwango kidogo zaidi kijamii ikilinganishwa na vikundi vikubwa vya harakati za jihadi, kama vile Hamas na Fat-hu. [3] Hamas, ambacho pia ni kikundi cha harakati za Kiislamu, kinaungwa mkono kwa kiwango kikubwa kutokana na huduma zake za kijamii pamoja na uwezo wake wa kijeshi kilichokuwa nao, wakati kikundi cha Fat-hu, kikiwa ni chama cha kisiasa kinacho tambulika kiduniani, kinaungwa mkono kwa kiasi kikubwa na Wapalestina kutokana na historia yake refu ya kupambana na utawala wa Israel na kushiriki katika michakato mbali mbali ya kisiasa ya Palestina. Kikundi cha Kiislamu cha Harakati za Jihadi cha Palestina, kinajulikana kwa nguvu zake za kijeshi, hasa katika eneo la Ukingo wa Magharibi. Uwepo wake wa kijeshi katika eneo hili unachukuliwa kuwa ni moja ya alama kuu za nguvu na ushawishi wake. Uwepo huu unaiwezesha harakati hii kujihusisha moja kwa moja katika upinzani wa kijeshi dhidi ya Israel, na kuimarisha nafasi yake katika harakati za ukombozi wa Palestina. [4] Kwa mujibu wa ripoti za baadhi ya vyombo vya habari vya Ulaya, Kikundi cha Kiislamu cha Harakati za Jihadi cha Palestina, ni maarufu kwa mbini zake za kuwa na muundo na mfumo wa siri ulioratibiwa kwa ufanisi mkubwa. Muundo huu wa siri unaiwezesha harakati za kikundi hichi kufanya shughuli zake kwa urahisi na bila kugunduliwa. Sifa hii imekiwezesha kikundi hicho kuongeza uwezo wake wa kujihusisha na kuboresh operesheni zake za kijeshi dhidi ya Israel na kuendeleza malengo yake ya ukombozi wa Palestina. [5]

Upinzani dhidi ya Makubaliano ya Oslo mwaka 2003, kususia uchaguzi wa Bunge la Palestina mwaka 2006, kupinga mkataba wa amani uliosainiwa na Misri mwaka 2014, pamoja na hatua za kutatua mvutano kati ya Hamas na serikali ya Misri mwaka huo huo, ni miongoni mwa hatua muhimu za kisiasa zilizochukuliwa na Harakati ya Jihad ya Kiislamu. Hatua hizi zinaonyesha msimamo thabiti wa harakati hii katika kupinga juhudi zozote za kidiplomasia ambazo zinaonekana kudhoofisha lengo lao la kupinga Israel na kuhakikisha uhuru kamili wa Palestina. [6]

Harakati za Kiislamu za Jihad, zilianzishwa katika Jiji la Gaza mnamo mwaka 1981, na mwanzilishi wake ni Fat-hi Shaqaqi, ambaye ni daktari wa Kipalestina. [7] Shaqaqi alishirikiana na watu kama Abdulaziz Awdeh, Ramadan Abdullah, na Nafeez Azzam katika kuunda na kuimarisha harakati hizi. Waanzilishi hawa walikuwa na lengo la kuleta mabadiliko ya kisiasa na kijamii kupitia upinzani wa silaha dhidi ya utawala wa Israel, wakijikita katika itikadi ya Kiislamu na harakati za kitaifa za Kipalestina. [8] Wanachama na waanzilshi wa vuguvugu hili walihamishwa hadi Lebanon mnamo mwaka 1987, jambo ambalo liliwawezesha kuwa na uhusiano wa karibu na Hizbullah ya Lebanon. Wakiwa nchini humo, waliweza kupata mafunzo mbali mbali kutoka kwa Walinzi wa Mapinduzi kutoka Iran. [9] Mafunzo haya yalilenga kuwaimarisha kijeshi na kimkakati katika mapambano yao dhidi ya Israel. Mnamo mwaka 1989, makao makuu rasmi ya vuguvugu hili yalihamishiwa Damascus mji mkuu wa Syria, ambako waliendelea na harakati zao za kisiasa na kijeshi wakishirikiana na washirika wao katika kanda hizo. Damascus ilitoa mazingira salama na yenye ushawishi kwa harakati hizo kuendelea na shughuli zake za upinzani. [10]

Fat-hi Shiqaqi, mwanzilishi na katibu mkuu wa kwanza wa harakati ya Jihad ya Kiislamu ya Palestina.

Fat-hi Shiqaqi, Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihad ya Kiislamu, aliuawa kupitia shirika la kijasusi la Israeli la Mossad mnamo mwaka 1995, na nafasi yake ilichukuliwa na Ramadhani Abdullah Shalah (aliyefariki mwaka 2020). Ramadhani Abdullah alichukua na athari kubwa katika nyenendo za kisiasa za harakati za Jihadi, akiongoza kwa ufanisi na kuhakikisha maendeleo ya malengo ya harakati hizo. Hata hivyo, kufuatia kuugua kwa Ramadhani Abdullah, Ziad Nakhla aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa kundi hili la harakati za Jihadi mnamo mwaka 2018, akiendeleza uongozi na msimamo thabiti wa harakati hizo katika malengo yake ya kisiasa na kijeshi. [11]

Misingi na Malengo

Kikundi cha Harakati za Kiislamu za Jihad kimejijenga kupitia kanuni maalumu ambazo ndio msingi wa fikra zao. Kanuni hizi msingi, ndizo zinazo wapambanua na makundi mengine mbali mbali. Mingi ya kanuni inanazosisitiza ya kwamba; dini ya Kiislamu ndiyo msingi mkuu fikra unaojenga imani na matendo ya harakati zao mbali mbali. Kwa mujibu wa kanuni hizo, ardhi yote ya Palestina inachukuliwa kuwa ardhi ya Kiislamu na Kiarabu. Utambuzi wa utawala wa Kizayuni katika ardhi hii unachukuliwa kuwa ni haramu, na uwepo wa Israel katika Palestina unaonekana kuwa ni kitendo cha kutawaliwa na kugawanyika kwa ardhi hiyo ya Kiislamu. [12] Pia, ni makossa kuchukua hatua yoyote inayolenga kutoa maamuzi ya utambuzi rasmi kwa utawala wa Kizayuni, na tendo hilo halikubaliki mbele ya kikundi hicho cha Harakati za Kiislamu za Jihad. Kwa mujibu wa msimamo wao, kurasimisha utawala wa Kizayuni ni sawa na kukubali uvamizi na udhibiti wa ardhi ya Palestina, jambo ambalo linapingana na kanuni na imani zao msingi. Harakati hii inaamini kuwa; hatua kama hizo ni miongoni mwa hatua zinazo halalisha ukoloni na kudumaza juhudi za ukombozi wa Palestina. [13]

Kikundi cha Harakati za Kiislamu za Jihad cha Palestina kimetangaza kuwa; lengo lake kuu ni kukomboa kikamilifu ardhi yote ya Palestina, kuangamiza utawala wa Kizayuni na kuanzisha serikali ya Kiislamu. Malengo mengine ya harakati hii ni pamoja na:

  • Kuwajenga na kuwatayarisha wananchi wa Palestina kwa ajili ya jihadi ya kijeshi na kisiasa.
  • Kuwapanga Waislamu duniani na kuwahimiza kutekeleza wajibu wao kwa Palestina.
  • Kujaribu kuunganisha fikra na vitendo vya Waislamu kuhusiana na Palestina.
  • Kuimarisha uhusiano na harakati za Kiislamu na ukombozi wa Palestina.
  • Kutoa wito kwa Waislamu na kueneza fikra na mafundisho yake.

Kikundi cha Harakati za Kiislamu za Jihad cha Palestina kinaamini kwamba malengo haya yatafikiwa kupitia juhudi za pamoja za Waislamu wote na kwa kuendeleza upinzani mkali dhidi ya Israel. Kwao, jihadi ni jukumu muhimu ambalo linahitaji maandalizi ya kina ya kijeshi na kisiasa ili kuhakikisha ushindi na ukombozi wa Palestina. [14]

Mkutano wa Katibu Mkuu wa Kikundi cha Harakati za Kiislamu za Jihad cha Palestina, Ziyad Nakhale na Shahidi Ismail Haniyeh, mkuu wa zamani wa ofisi ya kisiasa ya Hamas.

Kikundi cha Harakati za Kiislamu za Jihad cha Palestina kina ushirikiano wa kisiasa na kijeshi na kikundi cha harakati cha Hamas, [15] ila uhusiano wake na Jumuiya ya Ukombozi wa Palestina (PLO) haufai na yapaswa kuto endeleza uhusiano huo. Hii ni kutokana na tofauti za kimtazamo baina yake na PLO, kwa sababu mtazamo PLO ni wa kufurutu ada, ambapo PLO inaoyesha hamu ya kuafikiana na kuitambua rasmi Israeli, jambo ambalo linapingwa vikali na Kikundi cha Harakati za Kiislamu za Jihad cha Palestina. Kwa upande wa ushirikiano wake na Hamas, harakati hizi mbili zinaungana katika malengo yao ya kukomboa Palestina kupitia upinzani wa silaha na kushiriki katika mapambano dhidi ya Israel. Ushirikiano huu unajumuisha kuratibu operesheni za kijeshi na kushirikiana katika mikakati ya kisiasa ambayo inalenga kuimarisha nafasi ya upinzani wa Palestina. Kwa mtazamo wa Kikundi cha Harakati za Kiislamu za Jihad cha Palestina; msimamo wa PLO wa kutafuta suluhu ya amani na Israeli, ni usaliti dhidi lengo la ukombozi wa Palestina. Wao wanaamini kwamba; kuitambua Israel ni sawa na kukubalina na ukoloni wa Kizayuni katika unyakuzi wa ardhi ya Palestina. [16]

Upinzani Dhidi ya Ukoloni wa Kizayuni

Vikosi vya Al-Quds (Kiarabu: Saraya Al-Quds), tawi la kijeshi na kiusalama la Kundi la Harakati za Kiislamu za Jihad cha Palestina, lilianzishwa katika nusu ya pili ya miaka ya themanini ya karne ya ishirini. Kabla ya kipindi hicho, kikosi hichi kilijulikana kama Kikosi cha Wanajahid wa Kiislamu, na hapo awali kiliitwa Kataib Saif al-Islam. [17] Kikosi cha Al-Quds ndio kikosi kikubwa zaidi cha kijeshi huko Gaza kinachofuatia baada ya tawi la kijeshi la Hamas. [18]

Vikosi vya Al-Quds vimekuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya Israel, vikiendesha operesheni zake za kijeshi na mashambulizi ya kujitolea mhanga. Kikosi hichi kimejikita zaidi katika kuimarisha uwezo wake wa kijeshi kupitia mafunzo na ushirikiano na makundi mengine ya upinzani. Vikosi hivi vimechukua jukumu muhimu kwenye mikakati ya kijeshi ya Harakati za Kiislamu za Jihad za Palestina, wakilenga kupinga suala la kukabiliana na uwepo wa Israel katika ardhi ya Palestina. Israel imewaua makamanda kadhaa waandamizi wa Harakati za Kiislamu za Jihad za Palestina, wakiwemo: Fat-hi Shiqaqi (1995), Essam Barahamah (1992), Hani Aabid (1994), Mahmoud Al-Khawaja (1995), Mahmoud Tawaliba (2002), Mahmoud al-Zamtah (2003), Bashir Al-Dabesh (2004), Khalid Al-Dahduuh (2006), Danial Mansour (2014), [19] na Hisam Abu Harbid (2021), aliyekuwa kamanda wa tawi la vikosi vya kijeshi vya Quds. [20]

Operesheni

Mauaji haya ni moja ya juhudi za Israel za kudhoofisha uongozi wa Kundi la Harakati za Kiislamu za Jihad la Palestina, ili kupunguza uwezo wake wa kijeshi. Makamanda hawa walikuwa na nafasi muhimu katika kupanga na kuendesha operesheni za kijeshi dhidi ya Israel, na kuondolewa kwao kumeleta athari kubwa kwa harakati hizo. Hata hivyo, licha ya mauaji haya, Jihad za Kiislamu zimeendelea kuimarisha safu zake na kuendeleza mapambano yake dhidi ya Israel. Tawi la kijeshi la Harakati za Kiislamu za Jihad za Palestina limefanya operesheni nyingi mno dhidi ya uvamizi wa Israel. Baadhi ya operesheni hizi maarufu ni pamoja na mashambulizi yaliyofanyika Beit Lied, Dizengof, Kafar Darum, Netsaariim, Jabalia Mashariki, Muraaj, na Bashaer al-Intisar. [22]

Intifadha ya Palestina 1987

Operesheni hizi ni miongoni mwa mikakati ya Tawi la Kijeshi la Harakati za Kiislamu za Jihad la Palestina, katika kupinga na kudhoofisha uwepo wa Israel katika maeneo ya Palestina Intifadha (Wimbi la Maandamano ya Ghasia) ya Palestina ya Mwaka 1987, Kundi la Harakati za Kiislamu za Jihad za Palestina lilikua athari muhimu katika Intifadha ya Kwanza ya Wapalestina ya mwaka 1987. Hotuba za Abd al-Aziz Audah, kiongozi wa kidini wa harakati hizo, katika Msikiti wa Izzuddin Qassam zilikuwa ni juu ya mambo muhimu yaliyoamisha na kuchochea Intifadha hiyo. [23] Hotuba zake ziliwahamasisha Wapalestina kupinga uvamizi wa Israel na kuimarisha upinzani wao dhidi ya ukaliwaji wa ardhi zao. Katika Intifadha ya Pili (2000), Israeli ilimtambua Ramadhani Abdullah, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Harakati za Kiislamu za Jihad za Palestina wa wakati huo, kama ndiye mhusika mkuu wa mtiririko wa mashambulizi na mwenezaji wa itikadi zilizolenga kupinzani dhidi ya Israel. [24] Uongozi wake uliongeza msukumo kwa harakati hizo na ulisababisha ushirikiano mkubwa wa vikosi vya kijeshi vya Jihad katika mapambano hayo. Kushiriki kwa vikosi vya kijeshi vya Jihad katika Intifadha ya Pili kulisababisha operesheni nyingi za kijeshi dhidi ya Israel, na kwa sababu hiyo, makamanda kadhaa wa tawi la kijeshi la harakati hizo walilengwa na kuuawa na Israel. Mauaji haya yalilenga kudhoofisha harakati hizo hatari dhidi ya Wazayuni, lakini pia yalionyesha jinsi ujasiri wa Jihad ya Kiislamu ulivyokuwa ni tishio kubwa kwa Israel wakati wa Intifadha hizo. [25]

Kushiriki Katika Operesheni ya Dhoruba ya Al-Aqsa

Makala kuu: Kimbunga cha al-Aqswa

Kwa mujibu wa ripoti kutoka baadhi ya vyombo vya habari vya Ulaya, Kundi la Harakati za Kiislamu za Jihad la Palestina lilihusika katika Operesheni ya Kimbunga cha al-Aqswa cha mwaka 2023. [26] Operesheni hii ilisababisha vifo vya Waisraeli wapatao 1,400 na kukamatwa kwa mamia ya Waisraeli wengine. [27] Imeripotiwa kuwa; wale waliokamatwa walichukuliwa mateka na kundi la harakati hizo, na Kundi la Jihad za Kiislamu liliweka wazi kwamba wapo tayari kuwaachilia huru mateka hao kwa masharti ya kubadilishana wafungwa na Israel. Kundi hilo la wanajihadi wa Kiislamu ilitangaza kwamba linawashikilia zaidi ya wafungwa 30 wa Israeli, na likasisitiza litawaachilia huru tu kwa masharti ya kubadilishana na wafungwa wa Kipalestina walioko mikononi mwa Israel. Taarifa ambayo ilisisitiza msimamo wa harakati zao za kutumia mbinu ya kubadilishana wafungwa kama ni moja ya njia ya kuendeleza lengo lao la kukomboa ardhi za Palestina na kulinda maslahi ya Wapalestina. [28]

Baadhi ya nchi, zikiwemo Marekani, Uingereza, Canada na Japani, zikiambatana na pamoja na Umoja wa Ulaya, zimejumuisha Kundi la Harakati za Kiislamu za Jihad la Palestina katika orodha ya makundi ya kigaidi duniani. Hatua hii inatokana na msimamo wa vuguvugu hili katika kutumia mbinu za kijeshi na mashambulizi dhidi ya Israel, ambazo zinaonekana kuwa ni tishio kwa usalama wa kimataifa. Kuwekwa kwao kwenye orodha hii kunamaanisha kwamba; Kundi la Harakati za Kiislamu za Jihad la Palestina linakabiliwa na vikwazo vikali vya kiuchumi na kisiasa, huku nchi hizo zikijitahidi kudhibiti na kuzuia shughuli zake katika maeneo ya nchi zao. [29]

Athari ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran

Tangu kuanzishwa kwake, Kundi la Harakati za Kiislamu za Jihad la Palestina limeathiriwa kwa kiasi kikubwa na fikra za Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yaliyokuwa yakiongozwa na Imam Khomeini. [30] Kwa mujibu wa fikra hizo, Uislamu na mafundisho yake maridadi yamekuwa ndiyo msingi pekee wa Kundi la Harakati za Kiislamu za Jihad la Palestina, ambapo mapambano yao yamekuwa yakithamini mno umoja wa umma wa Kiislamu katika shughuli zake mbali mbali. [31] Kabla ya kuanzishwa kundi hilo la Jihadi, Fat-hi Shiqaqi, ambaye alikuwa ni kiongozi wa harakati hizi, aliandika kitabu kiitwacho "Al-Khomeini al-Hal al-Islami wa al-Badail" (Khomeini, Suluhisho la Kiislamu na Mbadala). Kitabu hichi kkikawa ndiyo kisingizio kilichosababisha kukamatwa kwake na serikali ya Misri kwa kutangaza malengo yake kwa ulimwengu wa Kiislamu, hasa mawazo yake juu ya njia za ukombozi wa Palestina. [33] Kundi la Harakati za Kiislamu za Jihad la Palestina limekuwa likilaumiwa kwa tuhuma kuwa na mwelekeo wa Kishia kutokana na uungaji wake mkono kwa Imam Khomeini na kwa kutokana na msisitizo wake wa kujenga umoja kati ya Mashia na Masunni. [34] Dukuduku hili linatokana na jinsi kundi hilo kupokea na kutilia maanani fikra za Imam Khomeini, ambazo zinaonekana kuhamasisha umoja wa Waislamu wa madhehebu yote katika mapambano yao dhidi ya utawala wa Kizayuni. Licha ya lawama hizi, Kundi la Harakati za Kiislamu za Jihad la Palestina limekuwa likisisitiza kuwa bado linafuata na kushikamana na kanuni za madhehebu ya Kisunni, liikilenga kudhihirisha kuwa lengo lake kuu ni kuleta umoja wa Waislamu wote bila kujali tofauti za kimadhehebu zilizoko baina yao. [35]

Kwa mujibu wa kauli ya Khalid al-Batash, mjumbe wa ofisi ya kisiasa ya Kundi la Harakati za Kiislamu za Jihad la Palestina, ni kwamba; Iran imekuwa ni muungaji mkono mkubwa wa harakati za kundi hilo pamoja na wagombea uhuru wengine wateteao ardhi ya Palestina. [36] Iran imekuwa ikiisaidia vikundi vya Jihad kwa nyanja mbalimbali, ikiwemo misaada ya kijeshi, kifedha, na kiitikadi, hali inayochangia kuimarisha mapambano dhidi ya utawala wa Kizayuni. [37] Uhusiano huu wa karibu umeitia nguvu mikakati ya harakati za Jihad na kuleta ushawishi mkubwa katika harakati za ukombozi wa Palestina, huku ikisalia kuwa ndiye mshirika mkuu na muhimu katika kanda hiyo. Kulingana na Kituo cha Tafiti za Kisiasa cha Kiarabu, Kundi la Harakati za Kiislamu za Jihad la Palestina lichukua msimamo wa kutoegemea upande wowote katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Syria vilivyoanza mnamo mwaka 2011, pia lilishikamana na msimamo wake huo huo katika shambulio la muungano wa Waarabu dhidi ya vuguvugu la Ansarullah la Yemen lililoanza mnamo mwaka 2015. Msimamo huu wa kutokuegemea upande wowote ulisababisha kudhoofika kwa kiasi fulani uhusiano mwema kati ya Kundi la Harakati za Kiislamu za Jihad la Palestina na Iran. [38]

Kituo cha TV cha Palestina

Mtandao wa televisheni wa satelaiti wa Palestina, Alyoum, ambacho makao makuu yake yapo mjini Gaza, kina unashirikiano wa karibu mno na Kundi la Harakati za Kiislamu za Jihad la Palestina. Hata hivyo, kutoka na matatizo ya kifedha yaliyoukumba mtandao huo mnamo mwaka 2015, ilipelekea kufungwa kwa ofisi za mtandao huo zilizopo mjini Quds, pamoja na kupunguzwa kwa wafanyakazi katika ofisi nyingine za mtandao huo.[39] Changamoto hizi za kifedha zimeathiri kwa kiasi uwezo wa mtandao huo katika kuendelea na shughuli zake kiufanisi kama ilivyokuwa hapo awali, ila bado mtandao huu unajulikana kwa shughuli zake maridadi za kushirikiana na Kundi la Harakati za Kiislamu za Jihad katika kuikomboa ardhi ya Palestina. Ofisi ya mtandao huo ilioko katika Ukingo wa Magharibi, ilifungwa na kusimamishwa kazi zake na utawala wa Israel mnamo mwaka wa 2016.[40]

Maudhui Zinazo Husiana

Rejea

Vyanzo