Kukufurisha Waislamu

Kutoka wikishia

Ukufurishaji au Kukufurisha Waislamu (Kiarabu: التكفير (تكفير أهل القبلة)) maana yake ni kumnasibisha mtu au kundi miongoni mwa makundi ya Waislamu na ukafiri, kitendo ambacho hufanywa na Waislamu wengine. Hatua hii imekuwa na matokeo mabaya kama kuidhinisha mauaji na mali za wanaokufurishwa. Kundi la mawahabi ambalo limekuwa na ufahamu wake na maalumu kuhusiana na mafundisho ya Uislamu kama tawhidi (kumpwekesha Mwenyezi Mungu), kufanya ziara katika makaburi na maeneo matakatifu na Waislamu kufanya tawasuli, hivyo limekuwa likimkufurisha kila anayepinga fikra zake hususan Waislamu wa madhehebu ya Shia.

Akthari ya Maulamaa na wanazuoni wa Kiislamu wanaamini kwamba, mpaka wa Uislamu na kufuru (kukufuru) ni kutamka shahada mbili na wanasema kuwa, haijuzu kuwakufurisha wafuasi wa madhehebu za Kiislamu. Pamoja na hayo, katika kipindi chote hiki cha historia ya Uislamu, daima baadhi ya Waislamu wamekuwa wakiwakurisha wafuasi wa madhehebu nyingine ambao wanapinga itikadi zao. Kukufurishwa Imamu Ali bin Abi Twalib (a.s) na Makhawariji katika tukio la hukumu ya Qur'ani na kukufurishwa Ahlu-Ridda katika zama za ukhalifa wa Khalifa wa Kwanza Abubakar bin Abi Quhafa ni mifano ya matukio ya mwanzo ya kukufurishwa Waislamu. Baada ya hapo, matukio ya utakfiri na kukufurishwa Waislamu yalikuwa yakitokea baina ya wafuasi wa madhehebu za Kiislamu, na kuna watuu wengi waliuawa kwa sababu hii. Hata hivyo utakfiri haujaishia katika mduara wa madhehebu tu, bali baadhi ya wakati baadhi ya mafakihi, wanafalsafa na maurafaa (wasomi wa elimu ya irfani) wa madhehebu moja walikuwa wakikufurishana wao kwa wao. Kadhalika katika fitina ya kuumbwa Qur'ani, wafuasi wa kila mtazamo ambao wote walikuwa wafuasi wa madhehebu ya Kisuni walikuwa wakiwakufurisha wafuasi wa nadharia ya upande wa pili.

Lililo dhahir shahir ni kwamba, baada ya kuibuka na kuundwa kundi na Uwahabi, kadhia ya utakfiri na kukufurisha wengine ikachukua wigo mpana zaidi. Aidha kupitia kuathirika na fikra za Kiwahabi na himaya na uungaji mkono wa Mawahabi wakufurishaji kukaibuka makundi ya kitakfiri na kigaidi kama Daesh ambalo linawakufurisha Waislamu hususan wafuasi wa madhehebu ya Ahlul-Beiti (a.s).

Kuhusiana na utakfiri kuna athari na maandiko mengi ambapo akthari yake yameandikwa kukosoa fikra za kundi hili. Kadhalika kumefanyika warsha na makongamano ya kukosoa utakfiri na harakati ya utakfiri.

Umuhimu na nafasi

Utakfiri ni maudhui ya kifikihi na kiteolojia (kiitikadi) ambayo katika historia ya Uislamu kutokana na kunasibishwa nayo mtu au kundi miongoni mwa makundi ya Kiislamu, damu na mali zao zimehalalishwa na matokeo yake yalipelekea kuibuka vita na watu wengi kuuawa na wengine kubakia bila makazi. [1] Vilevile ikiwa ni natija ya kunasibishwa baadhi ya wafuasi wa madhehebu za Kiislamu kwamba wamekufuru, baadhi ya maeneo na majengo yao yenye kuheshimiwa na kutukuzwa yamebomolewa. [2] Katika karne za hivi karibuni kuenea fikra za kitakfiri na kukufurishwa Waislamu na wafuasi wa fikra hizi, mjadala kuhusu utakfiri umepamba moto zaidi na kumeandikwa vitabu katika uwanja huu [3] sambamba na kufanyika makongamano mbalimbali kwa minajili ya kuweka wazi fikra na mitazamo ya harakati ya utakfiri.

Utambuzi wa maana na vigawanyo

Kukufurisha maana yake ni kumuita Mwislamu kafiri [4] au kunasibisha ukafiri na Waislamu. [5] Hata hivyo kufuru inagawanyika mara mbili. Ukafiri wa kifikihi na kiitikadi ambapo kunasibishwa na Mwislamu kila moja kati ya hayo lina matokeo maalumu kwake yeye:

  • Kukufuru kifikihi au kidhahiri maana yake ni kutoka katika dini ya Uislamu. Kwa muktadha huo, Mwislamu ambaye amekuwa kafiri wa kifikihi watu huamiliana naye kama kafiri.
  • Ukafiri wa kiitikadi au kibatini, maana yake ni kutoka katika imani na siyo katika Uislamu. Kwa msingi huo, kwa Mwislamu ambaye amekuwa kafiri wa kiitikadi watu huamiliana naye kwa muamala wa Waislamu na sio kafiri kama mnafiki ambaye kidhahiri ni Mwislamu lakini hana imani. [6] Imamu Ruhullah Khomeinii anasema: Hadithi ambazo zimekuja katika vitabu vya Mashia na zina ishara ya kukufurisha wapinzani wa madhehebu, kama tukijaalia kwamba, tunazikubali, basi zinahusiana na ukafiri wa kiitikadi. [7]

Marufuku ya kukufurisha Waislamu

Kwa mujibu wa fat'wa za wanazuoni wa fikihi wa madhehebu za Kiislamu, haijuzu kuwakufurisha Waislamu bali kuwakufurisha bila sababu Waislamu kuna adhabu kwa kitendo hicho. [8] Mafuqahaa wanaamini kwamba, mpaka wa kafiri na Mwislamu ni kutamka shahada mbili na kuamini ufufuo (kufufuliwa Siku ya Kiyama). [9] Ni kwa kuzingatia ukweli huo, ndio maana katika baadhi ya matukio licha ya itikadi za baadhi ya makundi kutokuwa sahihi, lakini walijizuia kuwakufurisha wafuasi wake. [10]

Historia ya ukufurushaji

Historia ya utakfiri na kukufurisha Waislamu wengine inarejea nyuma katika karne ya kwanza Hijiria na baada ya kuaga dunia Bwana Mtume (s.a.w.w). Katika zama za Ukhalifa wa Abu Bakr bin Abi Quhafa, kundi la Waislamu liililokuwa likipinga Ukhalifa lilikufurishwa na kuelezwa kwamba, limeritadi na kutoka katika Uislamu na vikaanzishwa vita dhidi yao ambapo vita hivi ni mashuhuri kama vita vya ridda. [11 Rasul Jaafariyan, mtafiti wa historia ya Uislamu anasema: Miongoni mwa Ahl ridda walikuwemo watu kama Malik bin Nuwayrah ambao walikuwa Waislamu na walikuwa wakiswali. Lakini hawakuwa wakiutambua na kukubali ukhalifa na uongozi wa Abu Bakr na badala yake walikuwa wakitaka ukhalifa na uongozi wa Ahlul-Beiti (a.s). [12] Hivyo basi walikuwa wakikataa kutoa Zaka na kumkabidhi Khalifa wa zama hizo na maana kutokana na sababu hiyo wakatajwa kuwa makafiri na walioritadi na kutoka na Uislamu na hivyo wakauawa. [13]

Katika zama za utawala wa Ali bin Abi Twalib (a.s) makhawarij walimkufurisha Imamu Ali (a.s) kutokana na kukubali kwake kuhukumiwa kwa Qur'ani. [14] Ni kutokana na sababu hiyo ndio maana wakakataa kuendelea kuwa pamoja naye katika vita na Muawiyah bin Abi Sufiyan. [15] na kisha wakaja kuanzisha vita vya Nahrawan dhidi yake. [16]

Ayatullah Ja'afar Sobhani anasema katika kitabu chake cha Buhuth Fil-Milal na Wanihal kuhusiana na fitina ya kuumbwa Qur'ani: Kila mmoja miongoni mwa waliokuwa wakiamini nadhari ya kuumbwa Qur'ani na kwamba, ni ya kale ambapo makundi yote mawili yalikuwa ya Masuni, waliwakufurisha waliokuwa wakiaamini nadharia nyingine. [17] Baada ya hapo, makundi miongoni mwa makundi ya Kiislamu walikufurishwa na watu wa kundi fulani au watu miongoni mwao. Katika karne za hivi karibuni kwa kuenea fikra za kisalafi na za Kiwahabi, Waislamu hususan Mashia, wamekuwa wakiandamwa na fikra hizi za kitakfiri.

Sababu na msukumo

Kukufurisha Waislamu kumekuwa kukifanyika kwa sababu na misukumo mbalimbali kama vile:

  • Kuwa na ufahamu mbaya na usio sahihi kuhusu mafundisho ya dini: Kundi la Khawarij likiwa na ufahamu wake maalumu kuhusiana na Aya isemayo: Hapana hukumu ila ya Mwenyezi Mungu lilisimama na kulalamikia tukio la kuhukumiwa na Qur'ani katika vita vya Siffin na wakamtambua Imamu Ali (a.s) kuwa ni kafiri. [18] Kadhalika Mawahabi wakiwa na ufahamu wao wa kipekee na maalumuu kuhusiana na mafundisho ya Tawhidi, kumshiirikisha Mwenyezi Mungu, kufanya ziara, kutabaruku, kufanya tawasuli na kadhalika, wamekuwa wakiwakufurisha akthari ya Waislamu hususan Mashia. [19] Muhammad ibn Abdul-Wahhab muasisi na mwanzilishi wa Uwahabi (aliaga dunia 1206 Hijiria) anaamini kuwa, damu yao na kuwaua ni halali kutokana na wao kufanya tawasuli kwa Mitume na waja wema na kulifanya hilo kama wenzo wa kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu. [20]
  • Mambo ya kiitikadi: Kila Mwislamu alipokuwa akifanya dhambi kubwa kundi la makhawarij lilikuwa likimkufurisha. [21] Makhawarij walikuwa wakitumia Aya isemayo: ((وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْكَافِرُونَ ; Na wasio hukumu kwa aliyoteremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio makafiri)) [22], ili kuthibitisha kwamba, wahusika wametenda dhambi. [23] Hata hivyo kwa mujibu wa Waislamu kutenda dhambi kubwa kunapelekea mhusika kutoka katika imani na sio kutoka katika Uislamu na natija yake ni kuwa, mhusika anakuwa fasiki na sio kafiri. [24] Vilevile katika fitina ya kuumbwa Qur'ani Abul-Hassan Ash'ari [25] na Ahmad bin Hanbal [26] walikuwa wakiwakufurisha waliokuwa wakisema kwamba, Qur'ani imeumbwa, na Muutazilah walikuwa wakiwakufurisha waliokuwa wakiamini kwamba, Qur'ani haijaumbwa yaani ni ya tangu na tangu. [27] Katika hadithi za Mashia pia maghulati (watu ambao walichupa mipaka kuhusiana na shakhsia ya Maimamu maasumina) na waliokuwa wakiamini taf-widh (uhuru usio na mipaka) wametajwa kuwa ni makafiri. [28]
  • Taasubi za Kimadhehebu: Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali za kihistoria katika zama za baadhi ya wafuasi wa madhehebu za Kiislamu walikuwa wakikufurishana wao kwa wao. Kwa mfano katika karne ya 8 Hijiria, wafuasi wa Madhehebu ya Ahlu-Sunna walikuwa wakiwakufurisha wafuasi wa madhehebu ya Kihanbali kutokana na miaka ya Ibn Taymiyah na mkabala wa hilo, Ibn Hatim aliyekuwa Mhanbali alikuwa akiwakufurisha Waislamu wote isipokuwa Mahanbali. [29] Kadhalika hali ya kukufurishana baina ya wafuasi wa Kisuni na Kishia ilikuweko. Ibn Jibreen Mufti wa Kiwahabi amewanasibisha Mashia na itikadii kama Qur'ani kupotoshwa, akthari ya masabaha ni makafiri, kuamini kwamba, Masuni ni makafiri na kuchupa mipaka katika shakhsia ya Imamu Ali (a.s) na watoto wake, na kuwatambua Mashia kuwa ni makafiri. [30] Hata hivyo Mashia hawana itikadi kama hizi. Karibu wanazuoni wote wa Kishia na Kisuni wanaamini kuwa, wafuasi wa madhehebu zingine sio makafiri [31] na kama hilo limekuja katika vitabu, basi linafasiriwa kwa maana ya ukafiri wa kiitikadi. [32]
  • Maudhui za Kiirfani na Kifalsafa: Baadhi ya Maulamaa wa Kiislamu wamekufurisha falsafa na irfani. Kwa mfano, Ghazali amekufurisha falsafa katika kitabu cha Tahafut al-Falasifah. [33] Kadhalika kama alivyosema Sayyid Muhammad Baqir Khonsari (aliaga dunia 1313 Hijiria) ni kwamba, kundi la mafaqihi lililimkufurisha Mulla Sadra kutokana na matamshi yake ambayo kidhahiri hayakuwa yakienda sambamba na sheria. [34]

Vilevile fitina zilizoanzisha na tawala mbalimbali zilizokuwa na lengo la kufanya juhudi za kubakia madarakani na njama za maadui wa Uislamu ni sababu nyingine ambazo zinaweza kutambuliwa kama chimbuko la kuenea fikra ya utakfiri na ukufurishaji. [35]

Matokeo yake

Kuna matokeo ambayo yametajwa kama sababu ya ukufurishaji. Baadhi yake ni:

  • Kuuawa Waislamu: Katika historia ya Uislamu daima Waislamu wengi wameuawa kutokana na jinai za utakfiri na ukufurishaji.
  • Kubomolewa turathi za kihistoria na majengo ya kidini: Mawahabi wamebomoa turathi za kihistoria zilizokuwa zikiheshimiwa na kuthaminiwa na Waislamu kama haram za Maimamu kwa kisingizio eti cha kupambana na shirki.
  • Kuonyesha sura ya Uislamu ulimwenguni kwamba, ni ya kikatili: Utendaji wa makundi ya kitakfiri kwa jina la Uislamu ni jambo ambalo limewafanya wapinzani wa Uislamu waione dini hii kwamba, ni ya kikatili na utumiaji mabavu. [36]

Kadhalika kuanzisha harakati za utumiaji silaha dhidi ya tawala za Kiislamu na kuzidhoofidha, kuzusha mifarakano baina ya nchi za Kiislamu na kuhalalisha wanawake wa Kiislamu wanaokamatwa mateka na matakfiri na kufanywa kuwa mali ya matakfiri hao, ni matokeo mengine ya harakati ya utakfiri na ukufurishaji. [37]

Kuibuka Makundi ya Kitakfiri

Katika karne za hivi karibuni Uwahabi na makundi kama Daesh ambalo limeibuka na kujitokeza likiwa limeathirika na fikra za Kiwahabi na likiwa linapata himaya na uungjai mkono wao, limekuwa likiwakufurisha Waislamu na kufanya mauaji sambamba na kupora mali zao likiamini kwamba, ni halali kufanya hivyo [38]. Linafanya haya likitegemea Aya zilizoshuka kuhusiana na washirikina na makafiri na hivyo kuzitabikisha Aya hizo kwa Waislamu. [39] Hii ni katiika hali ambayo, Maulamaa na wasomii wa Kiislamu wanapinga kitu kama hicho na kama wanavyosema ni kwamba, kukana dharura miongoni mwa dharura za dini tu yaani kukana Tawhidi, Utume na kadhalika ndiko kunakomtoa mtu katika Uislamu na hivyo kuhesabiwa kuwa ni kafiri. [40], tena hilo lifanyike katika hali ya ufahamu kamili. [41]

Kongamano la kimataifa

Mwaka 1393 Hijiria Shamsia kulifanyika kongamano chini ya anuani ya "Kongamano la Kimataifa la Harakati za Kufurutu Ada na Utakfiri Kwa Mtazamo wa Maulamaa wa Kiislamu" chini ya kwa usimamizi wa Ayatullah Makarem Shirazi mmoja wa Marjaa Taqlidi wa Iran. Kongamano hilo lilifanyika katika mji wa Qom, Iran. Maulamaa wa Kisuni na Kishia kutoka nchi 80 duniani walishiriki katika kongamano hilo. [42] Jumla ya makala 830 zilitumwa katika kongamano hilo na kuchapishwa katika kitabu cha juzuu 10 chini ya anuani ya " Mjumuiko wa Makala za Kongamano la Kimataifa la Harakati za Kufurutu Ada na Utakfiri". Kadhalika sekretarieti ya kudumu ya kongamano hilo ilichapisha na kusambaza vitabu 40 kwa lugha mbalimbali na kuanzisha jarida la Umma Mmoja wa Kiislamu kwa lugha za Kifarsi na Kiarabu. [43]

Bibliografia

Kuhusiana na utakfiri na ukosoaji dhidi yake kuna athari nyingi zimeandikwa. Katika bibliografia ya utakfiri kuna takribani athari 528 kwa lugha za Kiarabu na Kifarsi ambapo 235 kati ya athari hizo ni vitabu, makala 240, tasnifu 49 na athari nne ambazo ni barua maalumu. [44]

  • Kitabu Araa Ulamaa al-Muslimin Wafatawahum Fi Tahrim Takfiri atibaa Madh'hab al-Islamiya kimeandikwa na Sheikh Fuad Kadhim Miqdadi, muasisi wa Dar al-Taqrib Iraq. Katika kitabu hii kumefanyiwa utafiti fatuwa na nadhari za Maulamaa wa Kishia na Kisuni kuhusiana na kukataza kuwakufurisha wafuasi wa madhehebu za Kiislamu. Majmaa al-Thaqalain al-Ilmi Tehran ilichapisha kitabu hiki 1428 Hijiria. [45]
  • Al-Islam Wal-unf Fii Dhahirah al-Takfiri kimeandikwa na Hussein Ahmad al-Khashn, al-Khashan, kitabu hiki kinachungza na kkutafiti suala la utumiaji mabavu na utakfiri katika Uislamu sambamba na kuangazia misingi na vigezo vya utakfiri, kama ambavyo kitabu hiki kibainisha mambo mbalimbali na sifa maalumu za matakfiri. Kitabu hiki kilichapishwa mwaka 1390 Hijiria Shamsia chiini ya anuani ya Islam va Khushunat: Pitio Jipya Katika Kadhia ya Utakfiri kikiwa na kurasa 344 baada ya kutarjumiwa kwa lugha ya Kifarsi.

Masuala yanayo fungamana