Nenda kwa yaliyomo

Kikosi cha Quds

Kutoka wikishia

Kikosi cha Quds (Kiarabu: فيلق القدس أو قوة القدس) ni kitengo maalum kilioko ndani ya Jeshi la Walinzi wa Serikali ya Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), nacho ndicho kikosi pakee chenye mamlaka ya kuratibu na kutekeleza shughuli za kijeshi na kimkakati za taasisi hiyo nje ya mipaka ya Iran. Kuanzishwa kwa Kikosi cha Quds kulifanyika mano mwaka 1990 (sawa na 1369 Hijria Shamsia kwa kalenda ya Kifarsi). Uanzishwaji huo ulikamilika kufuatia agizo la Kiongozi Mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, mheshimiwa Ayatollah Sayyid Ali Khamenei.

Amiri jeshi wa kwanza wa aliyeongoza Kikosi cha Quds, alikuwa ni Ahmad Wahidi, aliyeshikilia wadhifa huo kwa kipindi cha miaka saba mfululizo. Mnamo mwaka 1997 Miladia (1376 H.S), nafasi hiyo ilishikwa na kamanda Qassim Suleimani, baada kupokea uteuzi wa nafasi hiyo kutoka kwa Kiongozi Mkuu, na tokea wakati huo yeye ndiye aliyekuwa kamanda mkuu wa kikosi hicho. Katika mwaka wa 2020 (1398 H.S), Qassim Suleimani alilengwa na kuuawa kupitia shambulio la anga lililoidhinishwa na Rais wa Marekani wa wakati huo Donald Trump, shambulio hilo lilifanyika karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad. Baada ya tukio nafasi yake ilichukuliwa na Ismail Qaani aliyeteuliwa kuwa ndiye kamanda mpya wa kikosi hicho.

Miongoni mwa shughuli kuu za Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (Sepah) ni; kushiriki katika kazi za kiushauri na kijeshi katika mataifa ya kigeni, kuhifadhi maeneo tukufu na turathi (nembo) za madhehebu ya Shia, hususan Haram za Maimamu (a.s), katika nchi za kikanda. Aidha, kazi nyengine muhimu za kikosi hichi ni kujenga Mhimili wa Ngome ya Muqawama (Mhimili wa Mapambano) ndani na nje ya maeneo yanayotawaliwa kimabavu. Miongoni mwa vikundi muhimu vya muqawama, kama vile; Hizbullah nchini Lebanon na Hash’d al-Shaabi nchini Iraq. Baadhi ya shughuli za kiushauri na kijeshi za kikosi hiki zinajidhihirisha katika ushiriki wake nchini Iraq na Syria katika mapambano ya nchi hizo dhidi ya Daesh na makundi yenye itikadi kali za Kitakfiri.

Pia tusisahau kwamba, kikosi cha Quds ndicho kikosi hasa chenye jukumu la kuungamkono vuguvugu la ukombozi wa Palestina, na ndischo kilichoviwezesha vitengo vya muqawama wa Wapalestina kwa kuvipatia silaha imara kwa ajili kujihami na kukabiliana na utawala dhalimu wa Israel.

Tarehe na Namna ya Kuanziswha Kwake

Kikosi cha Quds kinachofungamana na Jeshi la Ulinzi la Serikali ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (Sepahe Quds), ambacho hufahamika rasmi kama Gadi ya Quds, ni mojawapo ya matawi matano makuu yanayounda Jeshi la Ulinzi la Serikali ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (Sepahe Pasdaran). [1] [Melezo 1: Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi limeundwa na vikosi vikuu vitano vya kijeshi, kila kimoja kikiwa na dhamana tofauti za kiutendaji katika kazi zake. Vikosi hivi ni; Jeshi la Nchi Kavu, Jeshi la Majini, Jeshi la Anga, Jeshi la Wananchi la Uhamasishaji (Basij), na Kikosi au Jeshi Maalumu la Quds." (Rejea: “Nadharia Tatu Kuhusu Uasisi wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi,” Wakala wa Habari wa ISNA.)] Kitengo hichi kiliasisiwa na kuingizwa katika muundo wa gadi ya serikali hiyo ya mapinduzi mnamo mwaka 1369 kwa kalenda ya Jua (sawa na takriban 1990 Miladia), jambo lililotekelezwa kufuatia agizo la Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Mkuu wa pili wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. [2]

Inaripotiwa kwamba; historia hasa ya kuanzishwa kwa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), inarejea kwenye Kikosi cha Kambi ya Ramadhani na Brigedi ya Badr. [3] Kikosi cha Kambi ya Ramadhani, kilikuwa ndiyo kikosi cha kwanza cha IRGC kilichoanzishwa mwaka 1983 kwa ajili ya kufanya operesheni za kijeshi nje ya mipaka ya Iran, chini ya uongozi wa Murtadha Ridhai. [4] Hata hivyo, baadhi ya vyanzo vinasema kwamba; chimbuko la Kikosi cha Quds ni linarejea kwenye Vikosi vya Harakati za Ukombozi. [5] [Maelezo 1]

Katika moja ya khutba zake za Sala ya Ijumaa aliyoitoa mnamo tarehe 27 mwezi wa Dey 1398 H.Sh. (sawa na 17 Januari 2020 M), Ayatullahi Sayyid Ali Khamenei alikielezea Kikosi cha Ulinzi wa Mapinduzi cha Quds, kuwa ni kikosi cha mashujaa kisichokuwa na mipaka maalumu, ambacho huwepo na kuhudhuria popote pale kinapohitajika. Aliendelea kufafanua zaidi akisema kuwa; wahusika wake hukimbilia kusaidia mataifa yenye kuhitajia msaada, huku wakifidia mali pamoja maisha yao katika juhusi za kusaidia mataifa hayo dhaifu yaliyoko katika maeneo mbali mbali. Jitihada zao hizi ndizo zilizowawezesha kuweka kando makundi ya Wailamu wenye siasa kali zisizojali sheria, na hatimae kuikinga Iran na hatari ya makundi kama hayo. [6]

Ukamanda au Uongozi wa Kijeshi wa Kikosi cha Quds

Pia Rejea: Qasim Suleimani

Ukamanda wa mwanzo wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) ulishikiliwa na Ahmad Wahidi, aliyeshika nafasi hiyo kuanzia mwaka 1369 hadi 1376 kwa mujibu wa kalenda ya Shamsi (sawa na 1990-1997 Miladia), yeye alikama wadhifa huo kwa kipindi cha miaka saba mfululizo. [7] Aliyemfuatilia baada yake, alikuwa ni Qassim Suleimani, aliyeteuliwa kushika wadhifa wa ukamanda wa kikosi, hicho mnamo mwaka 1376 Shamsia (sawa na mwaka1997 Miladia), pale alikabidhiwa funguo za wadhifa huo na Kiongozi Mkuu wa Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu, Ayatullah Ali Khamenei. [8] Mnamo tarehe 13 mwezi wa Dey mwaka 1398 Shamsia (sawa na tarehe 22 December 2019), Suleimani alipoteza maisha kufuatia shambulio la anga lililotekelezwa na ndege isiyo na rubani ya Marekani. Tukio hilo lililotokea karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad, lilitekelezwa chini ya agizo la rais wa Marekani Donald Trump, na kusababisha kifo Suleiman pamoja na wenzake wengine kadhaa, miongoni mwao akiwa ni Abu Mahdi al-Muhandis (kamanda wa kikosi cha Hashdu Al-Sha’abi cha nchini Iraq). [9] Baada ya tukio hilo, Kiongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kupitia amri rasmi, alimuidhinisha Ismail Qaani kuwa Kamanda ndiye kamanda mkuu mpya wa Kikosi cha Quds. [10]

Harakati na Majukumu

Uchambuzi wa baadhi ya shughuli za kiutendaji za Kikosi cha Quds:

Uendeshaji wa Misingi ya Harakati za Ukinzani za Kikanda

Miongoni mwa harakati muhimu kabisa za Kikosi cha Quds cha Walinzi wa Mapinduzi katika kusimamia matatizo ya eneo la mipakani ni; kuanzisha, kuongoza, na kutia nguvu na kuimarisha makundi ya Muqawama (harakati za ukinzani). Mifano ya makundi ya harakati hizi ni pamoja na; Hizbullah ya Lebanon, Hashd al-Sha'abi nchini Iraq, Kikosi cha Fatemiyyun cha Afghanistan, pamoja na makundi ya kijeshi ya Ansarullah ya Yemen. [11] Dira ya pamoja ya makundi haya ni kukabiliana na Marekani na Israel dhidi ya ajenda zao za kikanda za maeneo yao. [12] Kiongozi Mkuu, Ayatollah Khamenei, analichukulia suala la uanzishwaji wa harakati za umma za Hizbullah dunianai kote, kuwa ni moja ya utimilifu wa za njozi za kimkakati za Imam Khomeini, jambo ambalo kwa hivi sasa limeainishwa kuwa ndiyo dhamira na wajibu mkuu wa kiutendaji wa Kikosi cha Quds. [13]

Ushiriki Wake wa Kiushauri na Kijeshi Katika Mataifa Mbali Mbali

Miongoni mwa majukumu makuu ya Kikosi cha Quds cha Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi ya Iran, ni pamoja na ushiriki wake wa kiushauri na kijeshi katika mizozo ya kimaeneo (kikanda). [14] Baadhi ya ithibati za uwepo na utendaji kazi wa Kikosi cha Quds katika mataifa ya eneo hilo ni kama ifuatavyo:

  • Utendaji Wake Kazi Nchini Bosnia

Uwepo rasmi wa awali wa Kikosi cha Quds kwa ajili ya kuwasaidia Waislamu wa Ulaya unahusishwa na wakati wakati wa Vita vya Bosnia. [15] Katika kipindi cha vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya Bosnia na Herzegovina, vilivyohusisha Waserbia, Wabosnia, na Wakroatia, [16] Kikosi cha Quds ndicho kilichobeba dhima ya kutoa msaada kwa Waislamu wa Bosnia waliokosa nguvu za kijeshi zenye uwezo wa kujihami dhidi ya maadui zao. [17]

  • Shughuli Zake nchini Afghanistan
Uwepo wa Qassim Suleimani pamoja na Ahmad Shah Massoud

Uwepo wa Kikosi cha Quds nchini Afghanistan ulijikita zaidi katika kuyasaidia makundi ya Mujahidina yaliyokuwa yakipambana dhidi ya mashambulizi ya Taliban. Baada ya Taliban kuchukua udhibiti wa Afghanistan na kuundwa kwa kundi la upinzani katika Bonde la Panjshir chini ya uongozi wa Ahmad Shah Massoud, Kikosi cha Quds kiwatuma washauri kadhaa wa kijeshi, akiwemo Qasim Suleimani, kwa lengo la kulisaidia kundi hilo katika mikakati yake. [18]

  • Vita vya Siku 33

Mgogoro wa Siku 33, uliotokea mwaka 2006, ulikuwa ni makabiliano ya kijeshi baina ya Israel na kundi la Hizbullah ya Lebanon. [19] Vyanzo vinavyohusiana na na mgogoro huo, vinaeleza kuwa; Qassim Suleimani, aliyekuwa kamanda mkuu wa Kikosi cha Quds wakati huo, alishiriki kikamilifu katika kitovu cha operesheni za kijeshi kwa kipindi chote cha siku 33, akiwa bega kwa bega na safu ya uongozi wa kijeshi wa Hizbullah. [20] Aidha, katika muktadha wa moja ya mahojiano yake aliyoyafanya, alibainisha akisema kuwa; utoaji wa himaya kwa Hizbullah katika mgogoro huo -himaya iliyojumuisha nyanja za kimorali, kimali, kisilaha, kilojistiki na kimawasiliano- ulikuwa ni agizo la kimkakati kutoka kwa Kiongozi Mkuu pamoja na viongozi wengine wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. [21]

  • Kukabiliana na Daesh nchini Iraq na Syria
Qassim Suleimani, kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu kutoka 1997 hadi 2019.

Harakati za kukabiliana na Daesh na makundi ya Kitakfiri nchini Iraq na Syria zinahisabiwa kuwa ni moja ya majukumu makuu ya Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi. [22] Shughuli hizi zilijumuisha usaidizi wa kiushauri, usanifu na uelekezaji wa operesheni, na utekelezaji wa operesheni za kijeshi dhidi vikosi vya Daesh. [23]

  • Uwepo wa Kikosi cha Quds Nchi Yemen

Kuna mkinzano wa masimulizi kuhusiana na kiwango cha uhusikaji wa Kikosi cha Quds katika harakati za upinzani nchini Yemen. Vyanzo vya habari vinavyohusishwa na muungano wa kijeshi wa Saudia vinatoa madai ya uwepo wa maajenti na makamanda wa Kikosi cha Quds tokea mwanzoni mwa vuguvugu la mapinduzi ya Yemen la mwaka 2014. [24] Kwa mujibu wa vyanzo hivyo tokea wakati huo, baadhi ya maafisa wa Kikosi cha Quds walichukuwa majukumu kadhaa ya kimkakati ikiwemo; usaidizi wa kilojistiki, utengenezaji au usafirishaji wa ya makombora kutoka Iran kwenda Yemen, kutoa msaada wa ndege zisizo na rubani (droni), pamaoja na zana za kijeshi kutoka Iran kwa ajili ya kundi la Ansarullah lilipo nchini Humo. [25] Kinyume chake, Rustam Qasimi, aliyekuwa Naibu Kamanda wa Uchumi wa Kikosi cha Quds, alikanusha madai hayo yake mahojiano yake ya mwaka 1399 Shamsia (mwishoni mwa mwaka 2020 Miladia), akisema kwamba; kikosi hicho hakina aina yoyote ile ya uwepo nchini Yemen. [26]

Uimarishaji na Utoaji Himaya kwa Harakati za Ukinzani za Palestina

Daima Kikosi cha Quds kimeonekana kutoa himaya na uwezeshaji kwa harakati za ukinzani za Palestina. Kulingana na maelezo ya mmoja kati ya viongozi wa Hamas, ni kwamba; Qassim Suleimani, katika kipindi chake cha ukamanda wa Kikosi cha Quds, alijitahidi kuipatia Hamas zana za kijeshi za kisasa ili kukabiliana na Israel. [27] Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatullah Khamenei, naye amebainisha akisema kwamba; Qassim Suleimani, alisimama dhidi ya Wamarekani waliotaka kuwadumisha Wapalestina na kwaweka katika hali ya udhaifu ili wasiweze kupambana dhidi ya Wazayuni, Kinyume chake, yeye aliwatia nguvu na kuwapa uwezo. Qassim Suleimani alifanya Wapalestina waweze kusimama na kuonyesha upinzani wao shupavu, jambo ambalo lilisababisha eneo dogo tu kama Ukanda wa Gaza, kusimama kidete mbele ya utawala wa Kizayuni pamoja na majigambo yao yote waliyokuwa nayo. [28] Mnamo Juni mwaka 2023, Ziyad al-Nakhalah, Katibu Mkuu wa Harakati za Jihad ya Kiislamu ya Palestina, alisimama na kutoa shukrani zake kwa maandishi za kumshukuru Ayatullahi Khamenei, akitambua msaada wa Jamhuri ya Kiislamu na jukumu la Kikosi cha Quds na kamanda wake wshupavu, Esmail Qaani, aliyesimama kidete katika mzozo wa siku kumi na mbili kati ya Wapalestina na Israel. [29] Aidha, kufuatia Operesheni ya Tufan al-Aqsa, kamanda wa sasa wa Kikosi cha Quds, Ismail Qaani, alithibitisha na kutangaza wazi himaya ya kikosi hicho katika kuunga mkono harakati hizo za Jihad ya Kiislamu ya Palestina. [30]

Ulinzi wa Maeneo Matakatifu ya Maimamu

Imeelezwa kwamba; mojawapo ya hatua za kiutendaji za Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi, hususan nchini Iraq na Syria, ilikuwa ni kuhakikisha usalama wa turathi na maeneo matakatifu ya Maimamu wa Kishia (a.s) mbele ya vitisho na mashambulizi ya Daesh na makundi ya Kitakfiri. [31] Katika mawanda haya, kutengua shambulio la Daesh dhidi ya Samarra kumebainishwa kama ni kielelezo cha hatua hizi muhimu. Mnamo tarehe 15 Khordad 1393 kwa kalenda ya Kiajemi (sawa na tarehe 5 June 2014 Miladia), Daesh ilianzisha uvamizi mkubwa katika mji wa Samarra. Madhumuni ya uvamizi huo ilikuwa ni kutwaa na kuharibu turathi za Maimamu pamoja na Haramu ya Imamu Hadi na Imamu Hassan al-Askari (a.s). Hii iliweza kuwapa nguvu fulani na sababisha udhibiti wao wa baadhi ya vitongoji vya mji huo, [32] hata hivyo, Kikosi cha Quds, chini ya amri ya Qassim Suleimani na kwa uratibu na ushirikiano na vikundi vya muqawama (ukinzani) na jeshi la Iraq, kilifanikiwa kuyapinga na kuyapiku mashambulizi hayo haraka iwezekanavyo. [33]

Maelezo

  1. Idara ya Mienendo (Harakati) za Ukombozi ndani ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi, iliasisiwa katika hatua za awali za mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran, ikiwa na dhamira ya kutambulisha na kusambaza itikadi za kimapinduzi ng'ambo ya mipaka ya Iran. Idara hii ilisimama na kuendesha kazi zake chini ya dhamana ya Muhammad Muntadhari. Baada ya kipindi cha Mohammad Muntadhari (Mwana wa Ayatullahi Hussein Ali Mintadhari), usukani wa idara hiyo ulikabidhiwa kwa Sayyid Mehdi Hashimi (ambaye ni kaka wa mkwe wa Ayatullahi Hussein Ali Montazeri). Katika kipindi cha utawala wa Muhammad-Ali Rajai (Aliyekuwa Raisi wa Iran wa zama hizo), Idara ya Harakati (Mienendo) za Ukombozi ilijumuishwa rasmi ndani ya Jeshi la Walinzi wa Serikali ya Mapinduzi ya Iran. Katika kipindi hicho, idara hiii ilionekana kuwa na ushirikiano wa karibu mno na harakati nyengine za ukombozi katika medani za kimataifa. (Baarsiqian, Serge, Shahrwand, Toleo la 47, Ordibehesht 1387 S.H.)

Rejea

Vyanzo