Hamas

Kutoka wikishia
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu (Hamas)

Hamas (Kiarabu: حماس) Kwa jina kamili ni Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ( حركة المقاومة الإسلامية), ni mojawapo ya makundi ya harakati za Kiislamu na vikosi vya muqawama (mapambano) vilivyoko Palestina. Kikundi hichi kilianzishwa mnamo mwaka 1987 Miladia/1366 Hijria Shamsiya, baada ya uvamizi wa kimabavu uliofanya na Wazayuni huko Palestina, kwa malengo ya makuu ni kupambana na uvamizi wa Kizayuni, hadi kukomboa ardhi zote za Palestina zinazokaliwa kimabavu. Hamas ni moja ya matawi ya vuguvugu la Ikhwan al-Muslimin, na wanachama wake ni wafwasi wa madhehebu ya Kisunni.

Kupitia harakati zake, Hamas inaendelea kuwa mstari wa mbele katika juhudi za kisiasa na kijeshi kwa ajili ya kuleta uhuru na kurejesha haki za Wapalestina. Msingi wa katiba ya Hamas umejikita katika kusisitiza na kuhakikisha kuwa ardhi hiyo ni ardhi ya Kiislamu na ni ya Kipalestina (siyo ya Kiyahudi). Katiba yake inajali zaidi umuhimu wa uhuru wa ardhi zinazokaliwa kwa mabavu. Hamas pia inaamini kwamba; Palestina ni mali ya kila Muislamu kokote aliko ulimwenguni hadi Siku ya Hukumu. Kwa hiyo, moja ya malengo yake makuu ya kistratijia; ni kupambana dhidi ya utawala wa Kizayuni, ambao Hamas unaona kuwa unakalia ardhi zao za Wapalestina kwa mabavu. Katika katiba yake hiyo, Hamas inatilia mkazo mno umuhimu wa kupinga ukoloni na kupigania uhuru wa ardhi za Palestina kwa misingi ya kidini na kitaifa, ikiwa ni sehemu muhimu ya harakati zake.

Vuguvugu hili la Hamas lilijitokeza rasmi katika ulingo wa kisiasa mnamo mwaka 2005, na kufanikiwa kujiimarisha zaidi baada ya uchaguzi wa mwaka 2007, ambapo liliweza kushinda kundi la Fatah na kutwaa udhibiti wa Ukanda wa Gaza. Katika kipindi kilichofuata, Hamas iliendelea na juhudi zake za kukomboa Palestina huku ikipambana na mashambulizi ya utawala wa Kizayuni. Kwa nyakati tofauti, imekuwa ikiendesha operesheni za kijeshi dhidi ya Israel kwa lengo la kuwalinda wananchi wa Gaza na kuhakikisha kuwa wanapata haki zao za msingi. Hamas imekuwa ikichukua hatua hizi kama ni moja ya mikakati yake wa muda mrefu wa kutetea uhuru wa Wapalestina na kusimamia usalama wa watu wake.

Hamas mara zote imeonekana na wafuasi wake kama nguvu halali ya upinzani, ikiwakilisha harakati za kupinga uvamizi na ukandamizaji. Hata hivyo, kwa upande wa wapinzani wake kama vile utawala wa Kizayuni, Marekani na Uingereza, Hamas inachukuliwa kama kundi la kigaidi na kuwekewa vikwazo vikali nan chi hizo. Mtazamo huu tofauti umeibua mjadala mkubwa kimataifa kuhusiana na uhalali na nafasi ya Hamas katika harakati za ukombozi wa Palestina, huku wafuasi wake wakiendelea kuiona kama ni ngome muhimu ya kupigania haki na uhuru wa Wapalestina, wakati wapinzani wake wakisisitiza hatari inayotokana na shughuli zake.

Shambulio kubwa zaidi lililofanywa na Hamas kwa lengo la kukabiliana na uhalifu wa utawala wa Kizayuni, ikiwa ni pamoja na mauaji ya Wapalestina na kuvunjia heshima Msikiti wa Al-Aqsa, linajulikana kama Tufani ya Al-Aqsa. Shambulio hili lilitekelezwa mnamo tarehe 15 Mehr 1402 Hijria Shamsiya sawa na Jumatatu tarehe 7 October 2023. Tukio hili limekuwa ni tukio muhimu katika historia ya harakati za Hamas dhidi ya ukandamizaji wa Kizayuni. Tukio hili linaashiria juhudi za Hamas za kulinda maeneo matakatifu ya Kiislamu na kulipiza kisasi kwa vitendo vya kinyama dhidi ya raia wa Palestina.

Hamas ni Kiungo Kilicho Mbele Dhidi ya Ukoloni wa Kizayuni

Makala Kuu: Mhimili wa Upinzani

Hamas, ikiwa ndio kiungo muhimu katika mhimili wa upinzani, kinacho tambuliwa kupitia harakati za kidini, kikundi kinachofungamana na madhehebu ya Kisunni kinayojulikana rasmi kama kikundi cha Harakati ya Mapambano ya Kiislamu (Kiarabu: حركة المقاومة الاسلامية). Hamas ni moja ya matawi ya kundi la “Ikhwanu Al-Muslimina” huko Palestina. [1] Hamas ndio kundi kubwa zaidi la wanamgambo wa Kiislamu nchini Palestina. [2] Kundi hili Ilianzishwa kwa lengo kuu la kukomboa maeneo ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu na kujenga upinzani wa kijeshi na kisiasa dhidi ya utawala wa Kizayuni. [3] Ingawa Hamas inajikita katika mapambano yake dhidi ya ukandamizaji wa Palestina, ila harakati za hao zinasisitiza kwamba; haipaswi kuwepo uadui wa moja kwa moja na Wayahudi kama jamii, bali upinzani wao unalenga kuondoa ukaliaji kimabavu wa ardhi za Wapalestina. [4]

Kikundi cha harakati cha Hamas kimejikita zaidi katika kuwaelimsha watu binafsi, familia na jamii kwa ujumla ili kuandaa msingi thabiti wa kuundwa kwa dola ya Kiislamu nchini Palestina. Mwanzoni mwa kuanzishwa kwake, Hamas haikuwa na mkakati wa moja kwa moja wa kukabiliana na ukaliaji wa mabavu wa Palestina. Badala yake, ililenga zaidi katika kujenga na kuimarisha jamii kupitia elimu na mwamko wa kidini. Hata hivyo, baada ya muda, kikundi hichi kilibadilisha mwelekeo wake na kuanza kushiriki katika mapambano ya silaha, hatua ambayo iliashiria kuingia kwake katika vita vya kijeshi dhidi ya utawala wa Kizayuni kwa lengo la kukomboa ardhi za Palestina. [5]

Wafuasi wa Hamas wanaliona kundi hili kama ni harakati halali za upinzani, zinazotenda kazi zake kulingana na sheria na kanuni madhubuti katika eneo wanaloendesha shughuli zao. Kwao, Hamas inachukuliwa kama ngome ya kupinga ukandamizaji na kulinda haki za Wapalestina, wakizingatia misingi ya kidini na kijamii inayowaongoza. [6] Hamas, yaani vikosi vya Ezzeddin Qassam, vinachukuliwa kama vikundi vya kigaidi na wapinzani wao. Hata hivyo, Umoja wa Mataifa haujaorodhesha tawi lolote lile la Hamas kama ni kundi la kigaidi katika orodha yake rasmi ya makundi ya kigaidi duniani. Hali hii inaashiria tofauti ya mtazamo kati ya jamii ya Umoja wa Mataifa na wale wanaokosoa harakati za Hamas, ambapo Umoja wa Mataifa haujaidhinisha hadharani ya kwamba kundi hili ni kundi la kigaidi, jambo linaloendelea kuwa na athari katika uhusiano wa kimataifa na mikakati ya usalama kuhusiana na eneo hilo. [7]

Himaya ya Jamhuri ya Kiislamu Kwa Hamas

Sheikh Ahmed Yassin, kiongozi wa Hamas, alipokutana na Ayatullah Khamenei, kiongozi wa Iran mnamo Mei 12, 1377 S.

Katika himaya na uungaji mkono wake kwa Hamas, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inachukuliwa kuwa ndiye mdhamini mkuu zaidi inayosaidia kundi hilo kifedha, vifaa na silaha. Vyanzo muhimu vya taarifa vinathibitisha kwamba; Iran ndiye msaidizi mkubwa wa Hamas, inayohami kikundi hicho kwa kudhamini kwa njia ya kifedha, vifaa vya kijeshi na silaha, hali ambayo inaongeza nguvu za harakati hizo katika mapambano yake. Msaada huu umeimarisha uwezo wa Hamas katika kutekeleza malengo yake ya kisiasa na kijeshi, na kuunda ushirikiano wa karibu kati ya kundi hilo na Iran. [8] Mnamo mwaka 1991, Iran ilianza kutoa misaada kwa Hamas kutokana na malengo ya pamoja yaliyowakutanisha. Himaya na udhamini huu ulimea zaidi baada ya kuanzishwa kwa ofisi ya kisiasa ya Hamas huko Tehran, na ukawa na umuhimu mkubwa kwa ushirikiano kati ya pande mbili hizi. Ziara za viongozi wa Hamas nchini Iran zilichangia katika kuimarisha uhusiano wao, ambapo Iran imezidi kukuza dhamira yake ya kuunga mkono harakati za Hamas kwa njia ya kifedha, vifaa, na ushauri wa kisiasa. Hali hii inachangia kwa kiasi kikubwa katika kuimarisha nguvu za Hamas na kufanikisha malengo yao ya kitaifa na kidini. Hata hivyo, katikati ya migogoro iliyokuwa ikitokea nchini Syria kati ya serikali na waasi wenye silaha pamoja na kundi la kigaidi la ISIS, uhusiano kati ya Hamas na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ulikumbwa na changamoto na mawimbi ya khitilafu za kimtazamo kati yao. Hitilafu zilizojitokeza kati ya baadhi ya wanachama wa Hamas na serikali ya Iran kuhusu msimamo wa makundi yenye silaha nchini Syria zilisababisha kupoza kwa mahusiano yao kwa muda fulani. Migogoro hii ilihusisha tofauti za kisiasa na kistratijia kuhusiana na jinsi ya kukabiliana na hali ya kiusalama ya katika kanda hizo, na kusababisha mapitio ya kutalii upya ushirikiano wao wa awali. [9] Kikundi cha Upinzani wa Kiislamu cha Hamas kinajitahidi kudumisha mahusiano yake na vikundi mbali mbali vya Kishia, kama vile Hizbullah nchini Lebanon na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Kikundi cha harakati hizo pia kinajitahidi kutafutia mahusiano mazuri na nchi nyingine za Kiislamu, ikiwa ni pamoja na Uturuki na Saudi Arabia. Kwa kufanya hivyo, Hamas inalenga kuimarisha ushirikiano wake wa kistratijia na kiusalama na washirika wake, huku ikiimarisha nafasi yake katika mataifa mbali mbali ili kuhakikisha msaada na ushirikiano katika harakati zake za kisiasa na kijeshi. [10]

Msimamo wa Upinzani Dhidi ya Ukoloni wa Kizayuni

Hamas mara kwa mara imekuwa ikijibu kwa mashambulizi ya Israel kwa kuingia vitani dhidi yake na kulenga miji ya Israel kwa kutumia makombora. Katika juhudi zake za kupinga ukaliaji wa kimabavu unaofanywa na utawala wa Kizayuni, Hamas imeanzisha operesheni kadhaa za kijeshi ili kulinda na kudai haki za Wapalestina. Harakati hizi zinaashiria kuwepo mapambano ya kila mara kati ya Hamas na Israel, huku Hamas ikiendelea kutumia mbinu za kijeshi kama sehemu ya mikakati yake wa kupinga utawala wa Kizayuni na kuhakikisha usalama na haki za watu wa Gaza. Hadi sasa, kumeshuhudiwa vita vikubwa kati ya Israel na Hamas, ambapo mara nyingi vita hivi vilihitaji usitishaji kupitia upatanishi wa nchi za Kiislamu kama vile Qatar au kupitia juhudi za Umoja wa Mataifa. Kundi la Hamas lina rasilimali chache za kifedha, likitegemea hasa fedha za zakat na rasilimali nyengine zilizoruhusiwa na Sharia ya Kiislamu kutoka kwa Wapalestina. Aidha, linapata msaada wa kifedha kutoka kwa nchi za Kiislamu na washirika wake, ikiwa ni pamoja na Saudi Arabia, Misri, Jordan, Iran na Sudan. Misaada hii imewezesha Hamas kuendeleza shughuli zake na kukabiliana na changamoto za kiuchumi zinazozikabili kukindi hicho. [11]

Operesheni ya Kimbunga cha al-Aqswa

Makala Kuu: Kimbunga cha al-Aqswa
Maandamano ya kupinga Uzayuni mjini London baada ya operesheni ya Kimbunga cha al-Aqswa, yenye kauli mbiu «Uhuru wa Palestina».

Mnamo tarehe 15 Mehr 1402 S sawa na 7 Oktoba 2023, Hamas ilifanya operesheni ya “Kimbunga cha al-Aqswa” kwa lengo la kujibu jinai za utawala wa Kizayuni, ikiwa ni pamoja na kulipiza kisasi mauaji ya Wapalestina na uvunjaji wa heshima wa Msikiti wa Al-Aqsa. [12] Katika shambulio hili la kushtukiza dhidi ya ardhi zinazokaliwa kwa mabavu, Hamas ilitekeleza operesheni yenye jina kubwa na la kutisha la "Dhoruba ya Al-Aqsa". Operesheni hii ilihusisha mashambulizi ya roketi dhidi ya makazi ya Wazayuni, huku vikosi vya Hamas vikijipenyeza katika maeneo mbalimbali ya Israel kupitia nchi kavu, angani na baharini. [13] Katika hatua hii, Hamas ilikamata walowezi kadhaa wa Kiisrael na kuwachukua hadi Gaza. Pia, Hamas ilifanikiwa kuchukua udhibiti wa maeneo kadhaa ya Wazayuni huko Gaza kwa kipindi cha muda fulani. [14]

Aina hii ya operesheni ya kijeshi imetathminiwa kuwa ni ya kipekee kwa Hamas katika muktadha wa mapambano yake dhidi ya Israel. [15] Kwa mujibu wa taarifa kutoka mtandao wa Al-Alam na vyombo vya habari vya Israel, operesheni hii imeonekana kuwa na athari kubwa zaidi kuliko mapigano yoyote ya hapo awali, na utawala wa Kizayuni haujawahi kuona kiwango kama hichi cha kushindwa na kudhalilika katika historia yake yote. [16] Kulingana na takwimu zilizotolewa, hadi siku ya kumi baada ya kuanza kwa mashambulizi ya Hamas kwenye maeneo yanayokaliwa kimabavu, [17] Waisraeli 1,400 waliuawa na zaidi ya wengine 3,000 kujeruhiwa. Hali hii ilipelekea furaha na sherehe kubwa miongoni mwa Waislamu katika nchi za Kiislamu, kama vile Iran. [18] Katika nchi hizi, mikutano ya hadhara ilifanyika ili kuonyesha mshikamano na kuunga mkono harakati za Hamas. Matukio haya yalithibitisha msaada wa kistratijia na kihemko kwa Hamas kutoka kwa mataifa mbali mbali ya Kiislamu. [19]

Wachambuzi wengi wanaona kwamba operesheni hii ni matokeo ya moja kwa moja ya miongo kadhaa ya ukandamizwaji na ukaliwaji kwa mabavu uliofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya watu wa Palestina. Kwa maoni yao, hali hii ilijenga msingi wa malalamiko na hasira miongoni mwa Wapalestina, ambayo hatimaye ilichochea operesheni hii. Uchambuzi huu unaonyesha jinsi hali mbaya ya maisha na uvunjaji wa haki za kibinadamu ulivyochangia katika kuongezeka kwa mapambano na mzozo wa muda mrefu katika eneo hilo. [20]

Historia ya Kuundwa kwa Hamas

Historia ya kuundwa kwa Hamas inaonesha kwamba harakati hizi zilianzishwa rasmi tarehe 9 Desemba mwaka, 1987. Kipindi hicho kilikuwa ni samabamba na maandamano makubwa ya wananchi wa Palestina dhidi ya utawala wa Israel, ambayo yanajulikana kwa jina la “Intifadha ya Kwanza”. Kuanzishwa kwa Hamas kulikua ndiyo mwanzo wa kutoa majibu ya kijeshi dhidi ya ukandamizaji wa Kizayuni, ambalo lilikuwa ni tukio muhimu katika muktadha wa mapambano ya kitaifa na kidini ya Wapalestina. [21] Kwa mujibu wa tovuti ya Al Jazeera, Hamas ilianzishwa mnamo mwezi Desemba mwaka 1986 na Sheikh Ahmed Yassin akiwa pamoja na baadhi ya wanachama wa Muslim Brotherhood (Ikhwanu Al-Muslimina), wakiwemo Abdul Aziz Rantisi na Mahmoud Zahar. Hata hivyo, kuanzishwa kwa harakati hizi kulitangazwa rasmi mnamo mwaka 1987. Hii inaonesha kwamba; ingawa maandalizi na mipango ya kuanzishwa kwa Hamas yalifanyika mapema, ila kutangazwa kwake rasmi kulifanyika mwaka mmoja baadae, katika kipindi ambacho maandamano ya intifadha ya kwanza yalikuwa yanaendelea nchini Palestina. [22]

Uongozi wa awali wa Hamas uliongozwa na kundi la watu saba, likiwa chini ya uongozi wa Sheikh Ahmed Yassin, [23] ambaye alikuwa kiongozi wa harakati hizo kwa kipindi kirefu. Sheikh Ahmed Yassin, ambaye alikumbwa na ajali akiwa na umri wa miaka kumi na miwili na hivyo kubaki na ulemavu wa kudumu, alilazimika kutumia kiti cha magurudumu kwa muda wote wa maisha yake. [24] Licha ya changamoto hizi za kiafya, alijitolea kwa moyo wote katika kuongoza Hamas kwa miaka mingi. Uongozi wake ulikuwa na athari kubwa katika kuimarisha na kukuza harakati za muqawama (Kusimama dhidi ya dhulma) nchini Palestina. Hata baada ya kifo chake, mchango wake katika historia ya Hamas unakumbukwa kwa taadhima na heshima. Sheikh Ahmed Yassin aliuawa na wanajeshi wa Israel mwaka 2004, na kifo chake kilikuwa pigo kubwa kwa harakati ya Hamas. Mwaka huo huo, Abdulaziz Rantisi alichukua uongozi wa Hamas, ila naye mwaka huo huo akakumbwa na hatima sawa na ya Sheikh Ahmad Yassin, na kuuawa na vikosi vya Israel. Baada ya kifo cha Rantisi, Khalid Meshaal alichukua uongozi wa Hamas, akiimarisha nafasi yake katika kipindi hicho cha mabadiliko na changamoto mbali mbali. Mnamo mwaka 2017, Ismail Haniyeh alichaguliwa kuwa kiongozi wa Hamas, akiongoza harakati hizo katika nyakati za mabadiliko na mzozo. Haniyeh alifanya kazi kwa karibu na viongozi na mashirika ya kimataifa, akilenga kuimarisha ushirikiano na kuboresha hali ya kiusalama na kisiasa kwa Wapalestina. [25] Baada ya kuuawa kwa Ismail Haniyeh mnamo tarehe 31 Julai 2024, Yahya Sinwar alichaguliwa kuwa mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Hamas. Sinwar ameshika nafasi hii muhimu katika kipindi cha mabadiliko makubwa, akiongoza harakati za kikundi cha Hamas kwa mikakati na mbinu mpya za kisasa. [26]

Mnamo mwaka 2005, kundi la Hamas lilipata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa Palestina, na kwa ushindi huo, likawa ndio kundi la kwanza la Kiislamu katika ulimwengu wa Kiarabu kushinda uchaguzi na kuingia rasmi katika ulingo wa kisiasa. Ushindi huu ulikuwa na athari kubwa katika siasa za Palestina na ulimwengu wa Kiarabu kwa jumla, kwani ulionesha uwezo wa harakati za Kiislamu kushiriki na kushinda katika mchakato wa kidemokrasia. Hata hivyo, mwaka 2007, baada ya kipindi cha mvutano na mapigano kati ya Hamas na vikosi vya Fat-hu vilivyoongozwa na Mahmoud Abbas, Hamas iliweza kulishinda kundi hilo na kuchukua udhibiti wa Ukanda wa Gaza. Hatua hii ilifanya Ukanda wa Gaza kuwa chini ya udhibiti wa kisiasa wa Hamas, na kwa hivyo eneo hilo likawa ni ardhi iliyotengwa kutoka katika ardhi za Palestina inayosimamiwa na kundi hilo. [27]

Yasemekana kwamba; Hamas, kama yalivyo matawi mengine ya “Ikhwanu Al-Muslimina”, imechota sehemu kubwa ya itikadi yake kutoka kwa Hassan al-Banna, ambaye ni mwanzilishi na mwananadharia maarufu wa kundi la “Ikhwanu Al-Muslimina” kutoka Misri. [28] Hassan al-Banna alitoa mchango mkubwa katika kuunda misingi ya kiitikadi na kimaadili inayotumiwa na makundi ya waharakati wa Kiislamu, ikiwemo Hamas. Muundo mfumo wa Hamas unaakisi muundo na misingi mikuu ya “Ikhwanu Al-Muslimina”, ambapo umeengwa juu ya misingi na kanuni za Kiislamu, ambapo kamati na uongozi wake unaotokana na “Bai’a” (muafaka wa utiifu) wa wanachama wake. [29] Hamas inaongozwa kupitia taasisi tatu umuhimu; Ofisi ya Kisiasa, Ofisi ya Enezi (inayohusika na uenezaji ujumbe wa harakati mbali mbali), pamoja na Ofisi ya Kijeshi (inayosimamia shughuli za kijeshi). Tawi la kijeshi la vuguvugu hili, linalojulikana kama Batalioni (vikosi) za Ezzeddin Qassam, lilianzishwa rasmi mnamo mwaka 1991 Miladia, likiwa na jukumu la kutekeleza mikakati ya kijeshi na kulinda maslahi ya Hamas katika eneo la Palestina. Tawi hili limekuwa ndio nguzo muhimu katika harakati za Hamas dhidi ya wapinzani wake, hasa utawala wa Kizayuni wa Israel. [30]

Waraka wa Ahadi

Mnamo tarehe 18 Agosti 1988, kundi la Hamas lilitoa waraka wa ahadi uliojumuisha vifungu 36, ambapo walieleza kwa kina malengo na mikakati yao huku wakisisitiza waziwazi msimamo wao dhidi ya utawala wa Kizayuni. [31] Waraka huu, unaojulikana rasmi kama Katiba ya Hamas, ulitolewa kwa nia ya kidhihirisha dhamira ya harakati zao katika kusimamia mapambano ya ukombozi wa Palestina. Katiba yao hii haikuonekana kuwa na tofauti na ile misingi asli ya kundi la “Ikhwanu Al-Muslimina”. [32] Katiba ya Hamas inatilia mkazo zaidi juu ya umuhimu wa kuitambua Palestina kama ni ardhi asili ya Kiislamu, na kwamba kusimama dhidi ya utawala dhalimu wa Kizayuni, ndio mhimili mkuu wa kimkakati wa harakati kundo hilo. [33] Katiba hii inasisitiza umuhimu wa kuendeleza Jihad kwa jina la Kadhia ya Kiislamu, ambapo Palestina inaonekana kuwa ni sehemu muhimu isiyoweza kutenganishwa na umma mzima wa Kiislamu hadi Siku ya Kiyama, na kwamba ardhi ya Palestina haiwezi kugawanywa au kupunguzwa kwa namna yoyote ile. Aidha, katiba hiyo inasisitiza juu ya haja ya kuanzishwa kwa dola ya Kiislamu inayotawaliwa kwa mujibu wa sheria za Kiislamu (Sharia), ikibainisha kuwa lengo kuu ni uhuru wa ardhi yote ya Palestina kutoka mikononi mwa utawala wa Kizayuni. [34] Kifungu cha nane cha ibara katiba hiyo, kinatangaza kauli mbiu ya Hamas, ambayo inaendana na ile ya “Ikhwanu Al-Muslimina”, ikidhihirisha kwamba; harakati hizi zimejengwa juu ya misingi thabiti ya itikadi za Kiislamu na mshikamano wa kidini, na inalenga kuimarisha msimamo wa Kiislamu kwa njia za kidini na kijamii ili kufikia malengo yake ya kimapinduzi na uhuru wa Palestina.

Mnamo Mei 1, 2017, waraka wa pili wa kisiasa wa Hamas ulizinduliwa na kuchapishwa huko Doha, ambao una tofauti na ule wa kwanza. Waraka huu mpya, ambao ulitarajiwa kwa muda mrefu, ulilenga kuboresha na kurekebisha baadhi ya misimamo ya awali ya harakati hii, ili kujibu changamoto mpya za kisiasa na kimkakati zinazokabili eneo la Mashariki ya Kati. Waraka huu uliakisi mabadiliko katika mtazamo wa Hamas kuelekea masuala ya kimataifa, huku ukijaribu kuleta uwiano kati ya misingi ya itikadi ya Kiislamu na mahitaji ya kisasa ya kisiasa. Pia, waraka huu ulisisitiza zaidi juu ya juhudi za kidiplomasia, wakati ukibakisha msimamo wake thabiti kuhusu ukombozi wa Palestina na upinzani dhidi ya utawala wa Kizayuni. Katika hali hii, waraka wa pili ulikuwa na lengo la kuonyesha ulimwengu kuwa Hamas ina uwezo wa kujibadilisha kulingana na mazingira ya kisiasa, huku ikibaki kushikilia malengo yake ya msingi. [35]

Monografia

  • Hamas harakatu al-Islamiyyah: Judhuruha, nashatiha wa fikruha al-Siyasi, mwandishi: Khalid Abu Omaraini, Chapa ya Misri ya Markazu Al-Muhadharati Al-Arabiyyah.
  • Tajrube hukumati Hamas: Arziyabi wa chashm-Andoz, waandishi: Salman Radhawi na Ali Pashaqasmiy, chapa ya Taasisi ya Mafunzo ya Noor Thinkers Tehran, Toleo la kwanza, 1391 (Kulingana na kalenda ya Kiirani).

Rejea

  • Makala hii imetafsiriwa kutoka katika makala ya kifarsi, wikishia. [1]