Sayyid Hassan Nasrallah
Sayyid Hassan Nasrallah (Kiarabu: السيد حسن نصر الله) (1960 - 2024): alikuwa ni Katibu Mkuu wa tatu wa Hizbullah, chama cha kisiasa na kijeshi cha Lebanon ambacho kiliasisiwa mano mwaka 1982. Chini ya uongozi wake, Hizbullah iliimarika na kuwa ni nguvu muhimu ya kikanda iliyofanikiwa kuilazimisha Israel kuondoka kusini mwa Lebanon mwaka 2000, baada ya operesheni za kijeshi zilizojumuisha kurudisha huru wafungwa wa Kilebanoni. Sayyid Hassan Nasrallah aliaga dunia kwa kuuawa shahidi mnamo tarehe 28/9/2024 Miladia kupitia mashambulizi ya anga yaliyofanywa na vikosi vya Israel.
Nasrallah alihitimu masomo yake ya kidini katika chuo maarufu cha Najaf kilicho nchini Iraq, ambapo aliendeleza uhusiano wake wa karibu na viongozi mbali mbali wa kidini, kama vile Sayyid Muhammad Baqir al-Sadr na Sayyid Abbas al-Mousawi, ambao walimhamasisha kushiriki katika harakati za kupinga uvamizi wa Israel.
Kwa muda mrefu, Sayyid Nasrallah alijiepusha na kudhihiri ndani ya hadhara mbali mbali kutokana na hali ya hatari na vitisho vya usalama. Mwanawe, Sayyid Hadi Nasrallah, aliuawa shahidi mwaka 1997 Miladia katika mapambano dhidi ya vikosi vya Israel.
Wasifu na Elimu Yake
Sayyid Hassan Nasrallah, kiongozi mashuhuri na mwenye ushawishi mkubwa nchini Lebanon,[1] alizaliwa mnamo tarehe 31 Agosti 1960 Miladia (sawa na tarehe 9 Shahrivar 1339, kwa kalenda ya Kiajemi) katika kitongoji cha Karantina, kilichoko mashariki mwa Beirut, eneo linalokaliwa na watu wenye kipato cha chini wa nchi hiyo. Baba yake akiitwa Sayyid Abdulkarim, huku mama yake akiitwa Nahdiyya Safi al-Din, wakazi wa kijiji cha al-Bazuriyya kusini mwa mji wa Sur, kusini mwa Lebanon. Familia hiyo ilihamia Beirut,[2] ingawa baadhi ya vyanzo vinadokeza kwamba Sayyid Hassan Nasrallah alizaliwa katika kijiji cha al-Bazuriyya.[3] Nasrallah alikuwa na ndugu watatu wa kiume na dada watano.[4] Wakati wa ujana wake, alifanya kazi katika duka la kuuza matunda la baba yake akishirikiana na ndugu zake katika kazi hiyo[5]
Sayyid Hassan Nasrallah alianza elimu yake ya msingi katika shule binafsi ya al-Najah iliyoko katika eneo la al-Tarbawiyya nchini Lebanon. Hata hivyo, baada ya kuzuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Lebanon mnamo mwezi wa Aprili mwaka 1975, Sayyid Hassan alilazimika kuhama pamoja na familia yake kwenda kijiji cha al-Bazuriyya, makazi ya asili ya baba yake. Akiwa huko aliendelea na masomo ya sekondari katika mji wa Sur.[6]
Mnamo mwaka 1976 Miladia, akiwa na umri wa miaka 16, alihamasishwa na Sayyid Muhammad Ghurawi, Imam wa Mji wa Sur aliyekuwa rafiki wa karibu wa Sayyid Muhammad Baqir al-Sadr, kwenda Najaf, Iraq, kuendeleza masomo ya dini. Sayyid Ghurawi aliandika barua ya utambulisho kwa al-Sadr, ambaye alimkabidhi Sayyid Abbas Mousavi jukumu la kumsaidia Sayyid Hassan katika safari yake ya elimu ya kidini.[7] Mwaka 1978, Sayyid Hassan Nasrallah alihitimisha masomo yake ya awali ya kidini huko Najaf nchini Iraq. Hata hivyo, baada ya miaka miwili, alilazimika kurejea Lebanon kutokana na shinikizo za kisiasa kutoka kwa utawala wa Ba’ath “Baathist” nchini Iraq.[8] Mwaka 1979, aliporejea Lebanon, alianzisha chuo cha Imamu al-Mundhazar (Imamu Mahdi) huko Baalbak, ambapo aliendelea na masomo yake ya kidini huku pia akiwa ni mwalimu wa chuoni humo.[9] Mnamo mwaka 1989, Nasrallah alielekea mji wa Qom, Iran, akiwa na nia ya kubaki huko kwa muda wa mwaka mmoja kwa ajili ya kujiendeleza katika masomo yake ya kidini.[10] Hata hivyo, alirejea Lebanon baada ya muda mfupi kutokana na shinikizo la kisiasa, ikisemekana kuwa kulikuwa na mvutano kati yake na chama cha Hizbullah, pamoja na kuongezeka kwa tofauti kati ya Hizbullah na harakati za kikundi cha Amal, hali iliyopelekea Baraza la Uongozi kumtaka arudi nyumbani.[11]
Mke na Watoto Wake
Mnamo mwaka 1978, Sayyid Hassan Nasrallah akiwa na umri wa miaka 18, alifunga ndoa na bibi Fatimah Yassin. Matunda ya ndoa hii, ilikuwa ni kujaaliwa watoto watatu wa kiume, waliotwa; Muhammad Hadi, Muhammad Jawad, na Muhammad Ali, pamoja na binti mmoja aliye itwa Zaynab.[12] Sayyid Muhammad Hadi, mtoto wao mkubwa, aliuawa shahidi mnamo tarehe 12 Septemba mwaka 1997 Miladia, katika mapambano dhidi ya vikosi vya ulinzi vya Israel kusini mwa Lebanon. Mwili wake uliangukia mikononi mwa Wazayuni, lakini baada ya mwaka mmoja baadae, ulirejeshwa nchini Lebanon kupitia operesheni ya kubadilishana wafungwa kati ya Israel na Hizbullah.[13]
Shughuli Zake za Kijamii na Kisiasa
Sayyid Hassan Nasrallah alianza kushiriki katika shughuli za kisiasa tangu akiwa na umri mdogo.
- Baada ya yeye kumaliza masomo yake ya sekondari mwaka 1975 Miladia, aliteuliwa kuwa kiongozi wa kikundi cha harakati za Amal katika kijiji chake cha al-Bazuriyya.
- Baada ya yeye kurejea kutoka Najaf mwaka 1979, alijiunga na ofisi ya kisiasa ya harakati za Amal na kuwa mwakilishi wa harakati hizo katika bonde la Biqaa. [19]
- Mnamo mwaka 1982, akiwa pamoja na kundi la wanazuoni na wanafunzi wa kidini waliohamasishwa na mapambano, alijitenga na kundi la harakati za Amal na kuanzisha kundi la Hizbullah ya Lebanon.
- Kuanzia mwaka 1982 hadi 1992 Miladia, Sayyid Hassan alitumia muda wake wote katika Hizbullah. Mbali na kuwa mjumbe wa Baraza Kuu la Hizbullah, pia alishiriki katika kuandaa vikosi vya upinzani na kuanzisha vikundi mbali mbali vya kijeshi. Pia alihudumu kama naibu wa Ibrahim Amin al-Sayyid, kiongozi wa Hizbullah mjini Beirut, na kwa kipindi fulani alikuwa ni naibu mtendaji wa Hizbullah ya Lebanon. [20]
Ukatibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon na Sayyid Baba wa Upinzani
Sayyid Hassan Nasrallah alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon kwa makubaliano ya wanachama wa chama hicho baada ya kuuawa kwa Sayyid Abbas Mousawi, tukio lilotokea mnamo tarehe 16 Februari mwaka 1992 Miladia. Wakati wa kuchukua wadhifa huo, Sayyid Hassan Nasrallah alikuwa na umri wa miaka 32.
Katika kipindi cha uongozi wake, Sayyid Hassan aliiongoza Hizbullah katika ushindi kadhaa dhidi ya utawala wa Kizayuni, ikiwa ni pamoja na kukombolewa kwa kusini mwa Lebanon mwaka 2000, ushindi katika vita vya siku 33 vya mwaka 2006, pamoja na ushindi dhidi ya vikundi vya kigaidi mwaka 2017.
Kupia mchango wake binafsi pamoja na jitihada za Hizbullah katika kukombolea kusini mwa Lebanon mwaka 2000, baada ya miaka 22 ya uvamizi wa Israel, pamoja na ushindi katika vita vya siku 33, Sayyid Hassan alikiriwa na kupatiwa jina la "Sayyid wa Upinzani (Baba wa Upinzani)".
Rejea
- ↑ Nuri, Shiiyan Lebanon, 1389 S, uk. 172.
- ↑ «Sayyid Hassan Nasralla», Webgah Farhkhatgan Tamadun Shia; «Sayyid Hassan Nasralla Rahbar wa Ulgu Jahan Arab», Khabargozari Jamhuri Islami.
- ↑ «Sayyid Hassan Nasrallah.. Kharij al-Hawzat Alladhi Yaqud Hizbullah al-Lubnani», Shabakat al-Jazeera «Sayyid Hassan Nasrallah: Sambul Muqawamat», Webgah Diplomasi Iran.
- ↑ «Sayyid Hassan Nasrallah.. Kharij al-Hawzat Alladhi Yaqud Hizbullah al-Lubnani», Shabakat al-Jazeer.
- ↑ «Zindeginame: Sayyid Hassan Nasrallah», Webgah Hamshahri Online.
- ↑ Khameyar, «Hizbullah wa Sayyid Hassan Az Jangehaye Dakhili Ta Jange 33 Ruze», Muasase Farhange Tahqiqi Imamu Mussa Sadir.
- ↑ Khameyar, «Hizbullah wa Sayyid Hassan Az Jangehaye Dakhili Ta Jange 33 Ruze», Muasase Farhange Tahqiqi Imamu Mussa Sadir.
- ↑ Khameyar, «Hizbullah wa Sayyid Hassan Az Jangehaye Dakhili Ta Jange 33 Ruze», Muasase Farhange Tahqiqi Imamu Mussa Sadir.
- ↑ «Zindeginame: Sayyid Hassan Nasrallah», Webgah Hamshahri Online.
- ↑ Nuri, Shiiyan Lebanon, 1389 S, uk. 144.
- ↑ Khameyar, «Hizbullah wa Sayyid Hassan Az Jangehaye Dakhili Ta Jange 33 Ruze», Muasase Farhange Tahqiqi Imamu Mussa Sadir.
- ↑ «Zindeginame: Sayyid Hassan Nasrallah», Webgah Hamshahri Online.
- ↑ «Sayyid Hassan Nasrallah Ke Bud?», Khabarigozari Baina al-Milali Quds.
Vyanzo
- «Infijarehaye Mehib Dar Bairut; Israel: Maqar Farmandahi Markazi Hezbollah Ra hadaf Gereftim», Tovuti Euro News, Tarikh Darj Matolib: 27 Sep 2024 M, Tarikh Bazdid: 7 Mehr 1403 S.
- «Al'amin al-amu Li Hezbollah al-sayid Hassan Nasrallah», Tovuti khanadiq, Tarikh Darj Matolib: 21 Feb 2021 M, Tarikh Bazdid: 7 Mehr 1403 S.
- «Bambaran Shadid va Payapi Bairut/Artesh Israel: Hadaf, Markaz farmandahi Asli Hezbollah bud»، Tovuti ISNA, Tarikh Darj Matolib: 7 Mehr 1403 S, Tarikh Bazdid: 7 Mehr 1403 S.
- «Payom Doktor Pezeshkian dar pei shahadat sayyid Hassan Nasrallah», Tovuti ISNA, Tarikh Darj Matolib: 7 Mehr 1403 S, Tarikh Bazdid: 7 Mehr 1403 S.
- «Al-harb Alaa Gaza Mubashar.. al-jaysh al'israel Ya'lan Maqtal Nasrallah waqadat Bi Hezbollah», Tovuti Al jazeera. Tarikh Darj Matolib: 28 Sep 2024 M, Tarikh Bazdid: 7 Mehr 1403 S.
- «Zindeginameh: Sayyid Hassan Nasrallah», Online news, Tarikh Darj Matolib: 25 Murdad 1387 S, Tarikh Bazdid: 7 Mehr 1403 S.
- «Sayyid Hadi Nasrallah ke bud?», Tovuti Bainulmilali Quds, Tarikh Darj Matolib: 26 Shahrivar 1402 S, Tarikh Bazdid: 7 Mehr 1403 S.
- «Sayyid Hassan Nasrallah: Sambul muqawemat», Tovuti Irdiplomacy, Tarikh Darj Matolib: 20 Farvaldin 1386 S, Tarikh Bazdid: 7 Mehr 1403 S.
- «Shahadat dabir kar Hezbollah sayyid Hassan Nasrallah», Tovuti Al Manar, Tarikh Darj Matolib: 28 Sep 2024 M, Tarikh Bazdid: 7 Mehr 1403 S.
- Sahyfat al-wahdah: al-sayid Hassan Nasrallah siyrat dhatiyat.. Quwat Shakhsiyat wa A'bqaryat.
- Biografi va Wasiat nameh sayyid Hadi Nasrallah, Tovuti Al Manar.
- Al-Shahid al-sayyid Muhammad Hadi Hassan Nasrallah, Tovuti Muqawemat Islami lubnon.
- Sahyfat ma'arif Tanshur Taqrir An mukhabaratiaan mufasilaan A'n hayaat Hassan Nasrallah wa amnih.
- Yatar'as al-hirasat 'abu Ali jawadi... ma'arif: wahdat <<mukhtara
- Haqayiq Takshaf al-awal mraatan an Abu Aly marafiq al-sayid Nasrallah
- Shabakeh Al-a'lam, Nasrallah mudir Shabakeh al-Arabia ra Ikhraj kard, Tovuti Al-a'lam.
- Guftegu ba «joolia petres» khanandeh masihi lubnani, Tovuti fars.
- Safar Shahid Amad moghnieh va Sayid Hassan Nasrallah be shumal iran
- Guzarsh tasviri huzur Sayid Hassan Nasrallah dar manzel sardar shahid Ahmad kadhemi, Tovuti muqawemat.
- Sayid Hassan Nasrallah: Pehpad Sakhte iran bud va ma an ra farestadim, Tovuti Tabnak.
- Sayid Hassan Nasrallah: man sokhangoye iran nistam, Tovuti entekhab.
- https://kayhan.ir/fa/news/143040/Sayid-Hassan-Nasrallah-az-negah-resane-ha-siyasatmadaran-va-sahyunist-ha
- «Vakonash muqawemat be shahadat sayid Hasan Nasrallah», Tovuti Javan. Tarikh Darj Matolib: 7 Mehr 1403 S, Tarikh Bazdid: 7 Mehr 1403 S.
Kategoria:Viongozi wa Kishia na wanasiasa Kategoria:Viongozi wa Kishia kutoka Lebanon Kategoria:Viongozi wa Hezbollah Lebanon Kategoria:Aliuwawa na Utawala wakizayuni Kategoria:Mashahidi wa Hezbollah Lebanon Kategoria:Mashahidi wa Upinzani wa Kiislamu