Abdul-Malik al-Houthi

Kutoka wikishia
Abdul-Malik al-Houthi

Abdul-Malik al-Houthi ni kiongozi wa tatu wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen. Yeye ni muungaji mkono na mfuasi wa umoja wa Kiislamu na mtetezi wa Palestina. Katika kipindi cha uongozi wake wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen ilikabiliana na uvamizi wa kijeshi wa muungano wa Kiarabu unaojumuisha nchi kadhaa za Kiarabu, ikiwemo Saudi Arabia. Harakati ya Ansarullah ya Yemen kwa uongozi wa Abdul-Malik al-Houth imeweza kulenga shabaha ndani ya ardhi ya Saudi Arabia.

Miongoni mwa hatua za Harakati ya Ansarullah wakati wa uongozi wa Abdul-Malik, ni shambulio la makombora dhidi ya Israel na kulenga meli zinazohusiana na utawala huo katika Bahari Nyekundu na Bab al-Mandab, kwa ajili ya kuwaunga mkono watu wa Ukanda wa Gaza.

Hatua za kijeshi za Abdul-Malik al-Houthi zilipelekea kuwekewa vikwazo na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na serikali ya Marekani.

Wasifu Wake

Abdul-Malik Houthi ni kiongozi wa tatu wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen, baada ya kaka yake Hussein ambaye naye alichukua uongozi baba yake Badruddin.[1] Kulingana na ripoti, aliteuliwa kwenye nafasi hii na baba yake Badruddin.[2] Baadhi wanasema kuwa, uongozi wake kwa Harakati ya Ansarullah ulianza mwaka 2010 (mwaka wa kifo cha Badruddin al-Houthi)[3] huku wengine wakisema kuwa, ni mwaka 2004 (mwaka aliouawa Hussein Houthi)[4] na wengine wanasema ni mwaka 2006.[5]

Abdul-Malik amechukuliwa kuwa mmoja wa watu muhimu sana wa kisiasa duniani[6] kwa akili na nguvu zake.[7] Miongoni mwa sifa zake zilizoelezwa ni kutoa hotuba ndefu zisizoandikwa (bila ya kusoma katika karatasi) na kujihusisha na suala la Palestina.[8]

Abdul-Malik alizaliwa katika mkoa wa Sa’dah. Baba yake, Badruddin, alikuwa mmoja wa Marajii (kiongozi wa juu kabisa wa kidini) wa madhehebu ya Zaydiya na babu yake, Amir al-Din, alikuwa mmoja wa wanazuoni mashuhuri wa eneo hilo.[9] Tarehe zake za kuzaliwa zimetajwa kuwa ni mwaka 1979 na 1982.[10] Alipewa kuniya ya Abu Jibril.[11] Kutokana na nasaba yake kuishia kwa Mtume (s.a.w.w) amepewa lakabu ya Sayyid.[12] Abdul-Malik alisoma sayansi ya kidini[13] na fasihi ya Kiarabu kutoka kwa baba yake. Hana shahada ya elimu ya akademia.[14]

Sifa Maalumu na Mitazamo Yake

Kulingana na wataalamu, baada ya kifo cha kaka yake Hussein, Abdul-Malik al-Houthi, akiwa kama kamanda, aliweza kuzuia kusonga mbele kwa vikosi vya kijeshi vya serikali ya Yemeni.[15] Uongozi wa Abdul-Malik unahesabiwa kuwa sababu muhimu kabisa ya mafanikio ya Ansarullah ya Yemen dhidi ya Saudi Arabia.[16] Nguvu ya Abdul-Malik imetokana na kukubalika kwake na wananchi.[17] Inaelezwa kuwa, akifuata nyendo za Sayyid Hassan Nasrullah kiongozi wa Hizbullah ya Lebanon ameweza kuwavutia mamia ya maelfu ya wananchi wa Yemen.[18]

Baada ya Ansarullah ya Yemen kuushambulia mji mkuu wa Saudi Arabia Riyadh kujibu mashambulizi ya muungano wa Kiarabu mwaka 2017, nchi hiyo ilitenga kiasi cha dola milioni 30 kama zawadi kwa atakayetoa taarifa zitakazopelekea kutiwa mbaroni Abdul Malik Houthi.[19]

Abdul-Malik Houthi anachukuliwa kuwa mfuasi wa umoja wa Kiislamu na dhidi ya migogoro ya kidini.[20] Yeye ni mtetezi wa haki za Palestina na waungaji mkono wa vikosi vya wanamapambano wa Palestina dhidi ya Israel. Anaamini kuwa, operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa ni ushindi wa kihistoria na mkubwa kwa Palestina na Umma wa Kiislamu.[21]

Uhusiano Wake na Iran

Mwanzo wa uhusiano wa Abdul Malik al-Houthi na Iran umezingatiwa kuwa mwanzoni mwa miaka ya themanini, ambao ulianzishwa na babake, Badruddin al-Houthi.[22] Baadhi wanaamini kuwa, shakhsia yake ya kifikra na kiitikadi iliibukia nchini Iran.[23] Wataalamu wa mambo wanaamini kuwa, hatua ya Ansarullah ya kudhibiti sehemu ya ardhi ya pwani ya magharibi mwa Yemen katika Bahari Nyekundu ni mafanikio ya kistratijia kwa ajili ya Iran.[24]

Hatua na Harakati Zake

Abdul Malik al-Houthi alikuwa na jukumu la kumlinda kaka yake Hussein alipokuwa Sana'a akiwa mwakilishi katika bunge la Yemen.[25] Abdul-Malik anahesabiwa kuwa ameathirika mno na kaka yake Hussein kwa kiwango ambacho Hussein anahesabiwa kuwa baba wa kiroho na kiigizo cha Abdul Malik.[26]. Baadhi ya mambo aliyoyafanya akiwa kiongozi wa Ansarullah:

  • Kuitambulisha Ansarullah kupitia kuanzisha mtandao wa al-Mimbar (2007) na kuanzisha Kanali ya Televisheni ya al-Masira (2012) hatua ambazo zilipelekea kuongezreka idadi ya waungaji mkono harakati hii.[27]
  • Kuanzisha vuguvugu na harakati iliyokuwa na lengo la kuuondoa madarakani utawala fisadi, kuleta marekebisho ya kiuchumi na kutekeleza maamuzi ya mazungumzo ya kitaifa (2012).[28]
  • Kusimama kidete mbele ya muungano wa kijeshi wa Saudi Arabia dhidi ya Harakati ya Ansarullah ya Yemen.[29]
  • Kupambana na ufisadi wa kiuchumi.[30]
  • Mashambulio dhidi ya Israel na meli zinazomilikiwa na utawala huo ikiwa ni katika kuunga mkono Gaza katika operesheni ya Kimbunga cha al-Aqswa (2023-2024).[31]

Vikwazo

Mnamo mwaka wa 2015, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilimuwekea vikwazo Abdul Malik Houthi kwa kile kilichoelezwa kufanya uasi dhidi ya serikali halali.[32] Serikali ya Marekani mwishoni mwa 2020 sambamba na kuliweka jina la Ansarullah katika orodha yake ya makundi ya kigaidi, ilimuwekea vikwazo Abdul-Malik al-Houthi. Serikali mpya ya nchi hiyo mwaka 2021 ilifutilia mbali uamuzi huo.[33]

Matukio Yaliyotokea Wakati Abdul-Malik akiwa kiongozi wa Ansarullah

Kuna matukio yaliyotokea wakati Abdul-Malik al-Houthi akiwa kiongozi wa Harakati ya Ansarullah. Baadhi ya matukio hayo ni:

  • Kutokea vita mbalimbali kati ya Ansarullah na serikali ya Yemen mwanzoni mwa uongozi wake mpaka 2010.
  • Kupigana vita na jeshi la Saudi Arabia katika ardhi ya nchi hiyo. (2010)
  • Kuanza Intifadha na mapinduzi ya Februari 2011 dhidi ya serikali ya Ali Abdullah Saleh.
  • Kuendesha mazungumzo ya kitaifa na kulaani mashambulio ya serikali dhidi ya Wahouthi (2013).[34]
  • Kudhibiti mji wa Sana’a na kuiangusha serikali ya Ali Abdullah Saleh (2014). [35]
  • Hujuma na mashambulio ya muungano wa Kiarabu dhidi ya Yemen kwa uongozi wa Saudi Arabia (2015).[36]
  • Kuuawa Ali Abdullah Saleh na vikosi vya Ansarullah (2017).[37]
  • Mashambulio ya Marekani na Uingereza dhidi ya ngome za kijeshi za Ansarullah Yemen katika kujibu mashambulio ya harakati hiyo dhidi ya meli za Israel. (2024).[38]

Rejea

  1. Abdul-Malik al-Houthi Min Mutamarid Min al Akalim Ila Zaim Watani, Tovuti Ruitarz.
  2. Abdul-Malik al-Hoūthī, Tovuti Aljazeera.
  3. Abdul-Malik al-Hoūthī, Webgah Nashr.
  4. Abdul-Malik al-Hoūthī.. Al-Murshid al-A'lā Fī al-Yemen, Webgah Bawabat Al-Harakat al-Islamiyah.
  5. Haqā'iq Lā Ta'rifuhā 'An 'Abdul-Malik al-Hoūthī, Webgah Majaleh Wasii Sadrak.
  6. Sheikh Husseini, Janbash Ansarullah Yemen, uk. 194.
  7. Haqā'iq Lā Ta'rifuhā 'An 'Abdul-Malik al-Hoūthī, Webgah Majaleh Wasii Sadrak.
  8. Al-Yemen: Man Huwa Qā'id Ansārullah 'Abdul-Malik al-Hoūthī, Webgah Shabake Khabari France 24.
  9. Qā'id Ansārullah as-Sayyid 'Abdul-Malik al-Hoūthī, Webgah Khanadiq.
  10. Abdul-Malik al-Hoūthī, Tovuti Aljazeera.
  11. Qā'id Ansārullah as-Sayyid 'Abdul-Malik al-Hoūthī, Webgah Khanadiq.
  12. Abdul-Malik al-Hoūthī.. Al-Imām at-Thālith, Webgah Ruzname al-Sharq al-Awsat.
  13. Qā'id Ansārullah as-Sayyid 'Abdul-Malik al-Hoūthī Webgah Khanadiq.
  14. Sheikh Husseini, Janbash Ansarulah Yemen, uk. 105.
  15. Abdul-Malik al-Hoūthī Min Za'īm al-Mutamarridīn Ilā Sāni' al-Mulūk, webgah Noon Post.
  16. Raz-e Muqawemat Wa Shekast Na Paziri- Rahbar- Ansarullah Yemen Chist? webgah khabari Fars.
  17. Min Ain Yastamid Abdul-Malik al-Hoūthī Quwwatah,webgah khabari dochevele.
  18. Abdul-Malik al-Hoūthī.. Al-Murshid al-A'lā Fī al-Yemen, webgah bawabah Harakat Islamiya.
  19. Ahmadi, Abdul-Malik al-Hoūthī.. Za'īm Khufiya Talahuquh Qā'imah Irhāb Trump, webgah khabari anadolu Ajansi.
  20. As-Sayyid 'Abdul-Malik al-Hoūthī Yad'ū Ilā Wahdah al-Ummah Wa Nabz al-Khilāfāt, khabargazari Taqhrib.
  21. An-Nas al-Kāmil Li Kalimah 'Abdul-Malik al-Hoūthī Haul Tūfān al-Aqsā Wa ar-Radd al-Isrā'īlī, webgah shabake khabari CNN.
  22. Hādhā 'Abdul-Malik al-Hoūthī Dhirā' Īrān Fī al-Yemen, webgah shabake khabari Alarabiya.
  23. Lihat: Abdul-Malik al-Hoūthī.. Al-Imām al-Thalatha,webgah ruznome sharq Awsat; Abdul-Malik al-Hoūthī.. Al-Murshid al-A'lā Fī al-Ymen, Webgah Bawabah Harakat Islamiya.
  24. Man Huwa Za'īm al-Hūthiyyīn 'Abdul-Malik al-Hoūthī, Webgah Masrawy.
  25. Qā'id Ansārullah as-Sayyid 'Abdul-Malik al-Hoūthī, Webgah Alkhanadiq.
  26. Qā'id Ansārullah as-Sayyid Abdul-Malik al-Hoūthī, Webgah Alkhanadiq.
  27. Haqā'iq Lā Ta'rifuhā 'An 'Abdul-Malik al-Hoūthī, webgah majaleh Wasii Sadrak.
  28. Sheikh Husseini, Janbash Ansarullah Yemen, uk. 252-253.
  29. Haqā'iq Lā Ta'rifuhā 'An 'Abdul-Malik al-Hoūthī, webgah majaleh wasii Sadrak.
  30. Haqā'iq Lā Ta'rifuhā 'An 'Abdul Malik al-Hoūthī, webgah majaleh wasii Sadrak.
  31. As-Sayyid al-Hoūthī: Narsud as-Sufun al-Isrā'īliyyah Fī al-Bahr al-Ahmar...Sanadhfar Bihā Wa Sa Nastahdifuhā, webgah shabake al-Mayadeen; Raz-e Muqawemat Wa Shekast Na Paziri Rahbar Ansarullah Yemen Chist? Site Fars.
  32. Jamā'ah al-Hūthiyyīn.. Harakah Yamaniyyah Jama'at Baina Zaidiyyah Wa Nahj al-Īrānī Wa al-Hukm al-'Ā'ilī, Webgah shabake khabar Aljazeera.
  33. Jamā'ah al-Hūthiyyīn.. Harakah Yamaniyyah Jama'at Baina Zaidiyyah Wa Nahj al-Īrānī Wa al-Hukm al-'Ā'ilī, webgah shabake khabari Aljazeera.
  34. Abdul-Malik al-Hoūthī.. Al-Murshid al-A'lā Fī al-Yemen, webgah bawabah Harakat Islamiya.
  35. Abdul-Malik al-Hoūthī, webgah shabake khabari Aljazeera.
  36. Al-Khurūj Min Harb al-Yemen Yu'azziz Amn as-Su'ūdiyyah Wa Ru'yatuhā al-Istithmāriyyah, webgah Ruznome Alarab.
  37. Maqtal 'Alī 'Abdullāh Sālih Bi Rasās al-Hūthiyyīn, webgah shabake khabari Aljazeera.
  38. Dharbāt Amrīkiyyah Wa Brītaniyyah 'Alā Ahdāf Fī San'ā' Wa al-hadīdah Wa al-Hoūthī Yatawa'aduhū Bi ar-Radd,webgah shabake khabari Aljazeera.

Vyanzo