Mateka wa Karbala

Kutoka wikishia

Mateka wa Karbala ni manusura wa tukio la Karbala na baadhi yao ni kama Imam Sajjad (as) ambaye ni Imamu wa Nne wa Waislamu wa madhehebu ya Shia na Bibi Zaynab (as) ambao walichukuliwa mateka na jeshi la Umar bin Saad. Mateka hao walibakishwa Karbala usiku ya tarehe 11 Muharram kwa amri ya Umar bin Saad na kisha adhuhuri ya tarehe 11 Muharram walipelekwa katika mji wa Kufa mbele ya Ubaydullah ibn Ziyad. Mateka hao walisafirishwa kwa madhila kuelekea Sham (Damascus) kwa Yazid ibn Muawiya. Baadhi ya mateka hao walifungwa minyororo wakati wa kuondoka kuelekea Sham na walitaabika mno wakiwa njiani. Hotuba na maneno yaliyotolewa na Imam Sajjad (as) na Bibi Zaynab (as) wakati wakiwa katika hali ya umateka, yalikuwa sababu ya kutokea mabadiliko ya kiroho na majuto kwa baadhi ya watu. Baadhi ya nukuuu zinaonyesha kuwa, hata Yazid mwenyewe alionyesha kujuta (hata kama ni kidhahiri) kwa kile alichowafanyia watu wa nyumba ya Mtume (saww) pamoja na jinai zake dhidi yao. Wanazuoni kama Sheikh Mufid, Sheikh Tusi na Sheikh Nouri Tabarsi ambaye ni mpokezi wa hadithi wanaamini kuwa, baada ya mateka wa Karbala kuachiliwa huru walirejea Madina na sio Karbala; hata hivyo kwa mujibu wa nukuu ya Sayyid ibn Tawus katika kitabu chake cha Luhuf fi Qatla al-Tufuf ni kwamba, msafara wa mateka ulirejea Karbala mara tu baada ya kuachiliwa huru.

Kuanza umateka

Baada ya tukio la Karbala, manusura wa jeshi la Umar bin Saad, tarehe 11 Muharram walizika watu wao waliuoawa na manusura wa mashahidi wa Karbala walipelekewa Kufa. [1] Maafisa wa Umar bin Saada, waliwapitisha wanawake wa Ahlul-Bayt kando ya miili ya mashahidi. Wanawake wa familia ya Imam Hussein (as) walikuwa wakilia na kuomboleza kwa huzuni kubwa huku wakijipiga nyuso zao. Qurrah bin Qais amenukuu ya kwamba, wakati Zaynab alipokuwa akipita kando ya mwili wa kaka yake Imam Hussein (as) kutokana na ghamu na huzuni kubwa aliyokuwa nayo, alisema maneno ambayo yalimliza rafiki na hata adui.

Maneno ya mtukufu Bibi Zaynab (as) aliyoyasema wakati alipokuwa akipita kando ya mwili wa Imam Hussein (as) ni: Ewe Muhammad! Ewe Muhammad! Malaika wa mbinguni wakuswalie, huyu ni Hussein ameadondoka jangwani, ametapakaa damu huku akiwa amekatwa viungo! Ewe Muhammad! Mabinti zako ni mateka, dhuria wako wameuawa ambapo upepo unawapuliza. Msimulizi anasema: Wallahi rafiki na adui walikuwa wakilia kwa uchungu baada ya kusikia maneno haya. [2]

Idadi na majina ya mateka

Angalia pia: Tukio la Ashura (kwa mujibu wa takwimu)

Nukuu za wanahistoria kuhusiana na idadi na majina ya mateka wa Karbala pamoja na manusura wa masahaba wa Imam Hussein (as) zinatofautiana. Idadi ya mateka wanaume imeelezwa kuwa ni watu 4, 5, 10 na 12. Idadi ya mateka wanawake imetajwa pia kuwa ni watu 4, 6 na 20. [4] Baadhi wametaja idadi ya mateka wa Karbala kuwa inafikia 25. [5] Kwa msingi huo imeelezwa kuwa, haiwezekani kueleza idadi ya mateka wa Karbala kwa kauli moja na kudai kwamba, hii ndio sahihi mia kwa mia. [6] Baadhi ya majina ya mateka wa Karbala waliotajwa katika vyanzo vya historia ni: • Wanaume: Imam Sajjad (as), Imam Muhammad Baqir (as), Omar bin Hussein bin Ali (as), ni mtoto wa Imam Hussein (as), Muhammad bin Hussein bin Ali (as), mtoto wa Imam Hussein (as). Zayd mtoto wa Imam Hassan Mujtaba (as) na Muhammad mjukuu wa Imam Hassan Mujtaba (as), [7], Hassan Muthanna ambaye kutokana na majeraha aliyokuwa ameyapata katika vita alikuwa amezimia, [8] Qassim bin Abdallah bin Ja’far, Qassim bin Muhammad bin Ja’far, Muhammad bin Aqil. [9] Katika katika kitabu cha Tarikh Qiyam na Maqtal Jami’ Shuhadaa, kumetajwa majina 17 ya wanaume kama ndio mateka na manusura wa tukio la Karbala. [10] • Wanawake: Mtukufu Bibi Zaynab, Fatma na Ummu Kulthum [11], Ruqayyah [12] ambao ni mabinti wa Imam Ali bin Abi Twalib (as), Rubab mke wa Imam Hussein, [13] na Fatma binti wa Imam Husseein (as), [14] mabinti wanne wa Imam Hussein (as) kwa majina ya: Sukayna, Fatma, Ruqayyah na Zaynab. [15]

Kuelekea Kufa Kwa mujibu wa kile kilichonukuliwa na kuandikwa na Ibn Abil Hadid katika Sherh ya Nahaj al-Balagha ni kwamba: Mateka wa Karbala walipandishwa katika vipango ambavyo havikuwa na suhula kwa ajili ya kupelekwa Kufa na watu walikuwa wakiwatazama. Katika hali hiyo hiyo, wanawake wa Kufa walikuwa wakiangukia kilio kutokana na kuona watu wa nyumba ya Mtume wakiwa katika hali hiyo. [16] Inaelezwa kuwa, hakuna nukuu ya wazi kabisa katika vyanzo vya kale kuhusiana na siku waliyowasili mateka hao katika mji wa Kufa. [17]; lakini kwa mujibu wa ibara ya Sheikh Mufid, [18] inawezekana kutambua kwamba, mateka wa Karbala waliingia Kufa 12 Mfunguo Nne Muharram. [19] Maafisa wa Omar bin Saad baada ya kuwatembeza mateka hao katika mitaa na vichochoro vya Kufa, waliwaingiza katika kasri la Ubyadullah bin Ziyad. Kumenukuliwa mazungumzo makali mno yaliyojiri baina ya mtukufu bibi Zaynab (as) na Ubaydullah bin Ziyad. [20] Sentensi mashuhuri ya Bibi Zaynab (as) ya:

«ما رَأیْتُ اِلّا جَمیلاً

Sijaona isipokuwa uzuri, inahusiana na kikao hiki. Kadjalika Ubaydullah alitoa amri ya kuuawa Imam Sajjad (as), lakini alibadilisha uamuzi wake baada ya Bibi Zaynab kumjia juu na kuonyesha upinzani wa hilo na vilevile maneno makali aliyoyatoa Imam Sajjad (as). [21]

Njiani Sham

Ubaydullah bin Ziyad alilituma kundi la watu fulani akiwemo Shimr bin Dhil Jawshan na Tariq bin Muhaffar kwa ajili ya kuongozana na mateka hao kuelekea Sham. [22] Kwa mujibu wa baadhi ya ripoti na nukuu zinaonyesha kuwa, Zahr bin Qays alikuwa pamoja nao pia. [23] Njia hasa waliopita mateka hao kutokana Kufa mpaka Sham haifahamiki wazi; baadhi wanaamini kwamba, kwa kuzingatia maeneo ambayo yananasibishwa na Imam Hussein (as), inawezekana kuainisha njia waliopita mateka wa Karbala kuanzia Kufa mpaka Sham; miongoni mwa hayo ni Maqam Raas al-Hussein na Imam Zaynul Abidin huko Damascus, [24] Maqama Homs, [25] Hamaa, [26] Baalabek, [27] Hajar, [28] na Turh. [29] Imekuja katika ensaiklopidia ya Imam Hussein (as) kwamba, katika zama hizo, baina ya Kufa na Sham kulikuwa na njia tatu kuu (Njia ya jangwani, Njia ya kando ya Furat na njia ya kando ya Dijlah) ambapo kila moja kati ya hizo ilikuwa na njia ya mkato. [30] Waandishi wa ensaiklopidia hii wanaamini kwamba, kutokana na kutokuweko hoja za wazi na zisizo na shaka, haiwezekani kutoa mtazamo wa miaa kwa mia kuhusiana na hili; hata hivyo kwa mujibu wa utafiti na dalili kuna uwezekano mkubwa njia waliopita mateka wa Karbala kutoka Kufa kwenda Sham ilikuwa ni ya jangwani. [31] Kwa mujibu wa baadhi ya ripoti kama ya Tarikh Tabari, Sheikh Mufid na Tarikh Dimashq, awali kichwa cha Imam Hussein (as) na vichwa vya mashahidi wengine wa Karbala vilitumwa Sham na kisha baada ya hapo, mateka wa Karbala wakapelekwa Sham; hata hivyo kwa mujibu wa ripoti na nukuu nyingine ni kwamba, vichwa vya mashahidi vilitumwa Sham pamoja na mateka wa Karbala. [32]

Muamala wa maaskari Kwa mujibu wa nukuu ya Ibn A’tham na Khwarazmi, maaskari wa Ubaydullah bin Ziyad waliwachukua mateka wa Karbala kutoka Kufa mpaka Sham hali ya kuwa wamewaweka katika vipango visivyo na mapazia wala vizuri, waliwachukua mji hadi mji na nyumba hadi nyumba kama vile mateka makafiri wa Kituruki na Daylam walivyokuwa wakichukuliwa. [33] Sheikh Mufid amenukuu akisema kwamba, kwa msingi huo, Imam Sajjad (as) alionekana baina ya mateka akiwa amefungwa minyonyoro ya chuma miguuni na shingoni. [34] Katika hadithi inayonasibishwa na Imam Sajjad (as) inaelezwa mbinu ya maaskari wa Ibn Ziyad ya kwamba, Ali bin Hussein alipandishwa katika ngamia mkondefu na mlemavu na hakukuwa na kiti na kikalio; katika hali ambayo, kichwa cha Imam Hussein (s) kilikuwa kimechomekwa katika mshale na wanawake walikuwa nyumba yake huku mishale ikiwa karibu yao. Kama ikitokea mmoja machozi yamemtiririka, basi alikuwa akipigwa kwa mishale kichwani mpaka wakati wa kuingia Sham. [35]

Kuwepo Sham

Kuna nukuu na ripoti mbalimbali katika vyanzo vya historia kuhusiana na matukio ya mateka wa Karbala kuingia Sham na namna walivyoamiliwa, sehemu walipokaa na hotuba ziliztolewa na baadhi ya mateka. Ripoti zinaeleza kuwa, vichwa vya mashahidi wa Karbala viliwasili Sham tarehe Mosi Mfunguo Tano Safar. [36] Kwa mujibu wa nukuu mji huo ulikuwa umepambwa na kuwa na mandhari isiyo ya kawaida siku hiyo kutokana na amri iliyokuwa imetolewa na Yazid. Ukawa kwa namna ambayo haukuonekana mfano wake. [37] Watu 15,000 katika hali ambayo walikuwa wamevaa nguo mpya na wakipiga madufu, ngoma na honi walikuwa wamejitokeza kuwaangalia mateka hao wakiwasili. [38] Baadhi ya vitabu vinaeleza kuwa, mateka hao walibakishwa nje ya mji na katika mlango wa kuingilia jiji kwa muda wa siku tatu. [39] Baada ya mateka hao kuingia katika mji wa Sham, waliwekwa juu katika sehemu ya kuingia katika Msikiti wa Jamia wa umawi. [40] Hii leo msikiti huu upo mkabala na mihrabu na mimbari kuu ya msikiti. Kuna sehemu ya mawe yenye ngazi za mbao ambayo ni maarufu kwamba, ndio sehemu ambayo mateka wa Karbala waliwekwa hapo. [41]

Hotuba za mateka

Baada ya mateka wa Karbala kuingia Kufa, Imam Sajjad (as) [42] na Bibi Zaynab (as) walizungumza na watu na kwa mujibu wa nukuu za baadhi ya vyanzo vya historia, waliwalaumu watu wa Kufa kutokana na kuzembea kwao katika kumuunga mkono Imam Hussein (as) katika tukio la Ashura. [43] Kuna hotuba pia ambazo zinanasibishwa na Fatma Sughra binti wa Imam Hussein (as), [44] na Ummu Kulthum binti wa Imam Ali (as). [45] Imam Sajjad (as) na Bibi Zaynab (as) walitoa hotuba pia wakiwa Sham. Maudhui ya hotuba hizo zilikuwa ni kumlaumu Yazid kutokana na dhulma yake kwa Ahlul-Bayt wa Imam Hussein (as) na kuwazungusha kwao katika miji [46] na kadhalika kubainisha fadhila za Ahlul Bayt wa Mtume na Ali (as). [47] Maneno haya ni mashuhuri kwa hotuba ya Imam Sajjad (as) na hotuba ya Bibi Zaynab (as) katika mji wa Sham. [48] Historia inaonyesha kuwa, Bibi Zainab alitoa hotuba iliyowafanya watu hao wajute mno na kuona aibu kubwa mpaka wakakaribia kufanya uasi dhidi ya utawala, ambapo utawala huo wa kifasiki ulimzuia mtukufu huyo asiendelee kuwahutubia watu. Alipofikishwa kwenye kasri la Liwali wa Kufa Ubaydullah Ibn Ziyad, Bibi Zaynab (as) alitolewa maneno ya vijembe na ya kutaka kumdunisha. Lakini mtukufu huyo alielezea kwa ufasaha mkubwa kuuawa shahidi Imam Hussein (as) na wafuasi wake kwa kusema: "Mimi sijaona lolote zaidi ya uzuri tu. Mashahidi wa Karbala walikuwa watu ambao Mwenyezi Mungu alikuwa amewachagulia kufa shahidi". Binti huyo wa Ali bin Abi Talib, alizungumza kwa ushujaa mkubwa pia katika kasri la Yazid, na katika sehemu moja ya hotuba yake alimuelekea mtawala huyo fasiki na kumwambia: "Ewe Yazid fanya hila na vitimbi vyovyote vile utakavyo, lakini kadiri utavyofanya hila, hutoweza katu kuuondoa utajo wetu kwenye kumbukumbu na wala hutoweza kamwe kuufuta wahyi wetu".

Kurejea kutoka Sham

Ili kupata taarifa zaidi, angalia hapa pia: Arobaini ya Imam Husseini Kuhusiana na kurejea mateka wa karbala kutoka Sham na kuelekea Madina na tujaalie kwamba, walirejea Karbala, kuna tofauti za kimitazamo kuhusiana na wakati na kipindi hasa walichorejea kutoka Sham. Kuna tofauti kwamba, ilikuwa ni Arobaini ya kwanza au ya pili ya tangu kuuawa shahidi Imam Hussein (as). Sheikh Mufid [49], Sheikh Tusi,[50] na Kaf’ami, [51] wamebainisha wazi kwamba, msafara wa Ahul-Bayt (as0 baada ya kuondoka Sham ulirejea madina na sio Karbala. Nouri Tabarsi, [52] Sheikh Abbas Qomi, [53] na Murtadha Mutahhari, [54] nao wamepinga suala la kurejea Karbala mateka wa Karbala katika Arobaini ya kwanza. Sayyid ibn Tawus amezitaja kauli zote mbili katika kitabu chake cha Iqbal yaani kurejea Madina na Karbala msafara wa mateka wa Karbala katika siku ya arobaini kwamba, ni jambo lililo mbali, kwani kurejea kwao Karbala au Madina kulichukua zaidi ya siku 40. Licha ya kuwa yeye anaamini huenda mateka wa Karbala walirejea Karbala, lakini hakubali kwamba, ilikuwa katika siku ya Arobaini. [55]

Monografia

• Asiran wajambazan Karbala, ni jina la kitabu kilichoandikwa na Muhammad Mudhaffari na Said Shamshidi.