Nenda kwa yaliyomo

Maqtal

Kutoka wikishia
Maqtal

Maqtal au Uandishi wa maqtal (Kiarabu: المقتل أو كتابة المقتل) ni aina ya uandishi wa historia ambao unaeleza na kusimulia jinsi mauaji yalivyotokea au namna shakhsia muhimu walivyouawa shahidi. Uandishi wa kusimulia mauaji umedhihirika zaidi baina ya Waislamu wa madhehebu ya Kishia wakibainisha na kutoa ufafanuzi na simulizi kuhusiana na kuuawa shahidi Maimamu Maasumina (a.s) na shakhsia muhimu wa Kishia; hata hivyo kutokana na kuenea uandishi wa maqtal (uandishi wa simulizi ya mauaji) kuhusiana na tukio la Karbala, utumiaji wa istilahi hii umekuwa ni maalumu tu katika kunukuu matukio yanayohusiana na kuuawa shahidi Imamu Hussein (a.s) na masahaba zake.

Simulizi ya mauaji ya Imamu Hussein (a.s) kikawaida inajumuisha hadithi zilizonukuliwa kutoka kwa Bwana Mtume (s.a.w.w) na Imamu Ali (a.s) kuhusiana na utabiri wa tukio la Karbala, barua, hotuba na maneno ya Imamu Hussein (a.s), mambo yanayohusiana na walioandamana na Imamu Hussein (a.s) katika tukio la Karbala ambao hawakuuawa, hotuba za Imamu Sajjad (a.s) na Bibi Zaynab (a.s) baada ya tukio la Ashura, hadithi za Maimamu wa Waislamu wa Kishia kuhusiana na kuuawa shahidi Imam Hussein (a.s) na nukta za maadui wa Imamu Hussein (a.s) kuhusiana na tukio la Karbala.

Asbagh bin Nubata Mujashi’i ametambuliwa kuwa mtu wa kwanza aliyeandika simulizi zinazohusiana na mauaji za tukio la Karbala. Kitabu cha Maqtal al-Hussein kilichoandikwa na Abi Mikhnaf kinahesabiwa kuwa moja ya vitabu vikongwe na vya kale vilivyoandikwa kuhusiana na maudhui hii.

Uandishi wa simulizi za mauaji ulishika kasi katika karne ya tatu na ya nne lakini baada ya hapo mpaka kuingia madarakani utawala wa ukoo wa Safavi kilikuwa kipindi cha kudorora uandishi wa maqtal (uandishi wa simulizi za mauaji hususan tukio la Karbala) na athari za kipindi hiki hazina itibari na hazina nyaraka ambapo kulikuwa na mchango mkubwa wa upotoshaji wa tukio la Ashura kama kitabu cha Rawdhat al-Shuhadaa kilichoandikwa na Mulla Hussein Kashifi.

Kuwa rasmi marasimu na hafla za Ashura sambamba na kushika hatamu za uongozi utawala wa Safavi kulipelekea kuandikwa simulizi mpya za mauaji (maqtal) ambazo hazikuwa na vyanzo makini na tukio la Ashura zaidi likiwa ni kwa ajili ya kutumika katika vikao vya kusimulia msiba na maombolezo na kuandaa uwanja na mazingira ya kuhuzunika na kulia. Athari kama Ibtilaa al-Auliya, Aksir al-Ibadah Fi Asrar al-Shahadah na Muhriq al-Qulub ni miongoni mwa kundi la vitabu hivi.

Nafs al-Mahmum na Maqtal Jami’ Sayyid al-Shuhadaa ni katika vitabu muhimu vya Maqtal vya zama hizi.

Utambuzi wa Maana

Ripoti ya maandiko ambayo inajumuisha mambo kuhusiana na mauaji au kuuawa shahidi shakhsia muhimu wa kihistoria kunajulikana kawa jina la usomaji wa maqtal. [1] Maqtal ni matokeo ya aina ya uandishi wa historia kwa mujibu wa monografia. Monografia ni aina ya uandishi wa kihistoria ambao unatumika katika kusajili matukio muhimu. Uandishi wa namna hii aghlabu huundika katika uwanja na uga wa matukio yenye matukio mengi na yenye kuainisha hatima na hunukuliwa kila kitu chake hata mambo madogo madogo. [2] Maqtal katika lugha ina maana ya sehemu ilipotokea mauaji. [3]

Historia ya Uandishi wa Maqtal

Maqtal ya Imamu Hussein (a.s) kilichoandikwa na Ibn Abi Dunia

Maqtal (simulizi za mauaji) za kwanza zilizoandikwa na Mashia kawaida zinahusu kuuawa shahidi Imam Ali (a.s) [4] Baadhi ya vyanzo, vimetaja maqtal kumi na nne zenye anuani zinazoshirikiana: "Maqtal Amir al-Mu'minin" (a.s) kutoka kwa wanazuoni kama vile Abi al-Hasan Bakri, Jabir Ju’fi, Yahya Bahrani Yazdi na Ibn Abi Dunia. [5]

Baada ya kuuawa shahidi Imam Hassan (a.s) na Imam Hussein (a.s), uandishi wa simulizi za mauaji miongoni mwa Mashia ulishamiri na kushika kasi. Hata hivyo hii leo, kati ya kazi zilizotangulia kwa anuani ya "Maqtal al-Hussein", au zimebakia tu katika orodha ya uandishi au sehemu yake imenukuliwa katika maandiko yaliyokuja baadaye. [6]

Kuna maqtal pia ambazo zimeandikwa ambazo zinabainisha na kutoa ufafanuzi kuhusiana na shakhsia wengine wasio wa Ahlul-Bayt (a.s). Maqtal Omar bin al-Khattab kutoka kwa Muhammad bin Abdallah bihn Mehran, [7] Maqtal Abdallah bin Zubeir na Maqtal Hujr bin Adi kutoka kwa Abi Mikhnaf (aliaga dunia 157 Hijiria), maqtal zingine mbili ambazo zimeandikwa katika miaka ya hivi karibuni kutoka kwa Nasr bin Muzahim Kufi (aliaga dunia 212 Hijiria) na Hisham Kalbi (aliaga dunia 204 au 206 Hijiria), Maqtal Rashid, Maytham na Juwairiyah bin Musahhir kutoka kwa Hisham Kalbi na Maqtal Muhammad bin Abi Bakr kutoka kwa Abdul Aziz Jaludi (aliaga dunia 330 au 332) ni miongoni mwa athari hizo. [8]

Maqtal za Imamu Hussein (a.s)

Kwa mujibu wa rai na mtazamo mashuhuri ni kuwa, Maqtal ya Abi Abdallah al-Hussein, iliyoandikwa na Asbagh bin Nubata Mujashi’ ndio maqtal na simulizi kongwe zaidi ya mauaji katika uga wa matukio ya kuuawa shahidi Imamu Hussein (a.s). [9] Hata hivyo kwa mujibu wa hadithi iliyonukuliwa katika kitabu cha Thawab al-A’ma cha Sheikh Saduq, Asbagh bin Nubata alidiriki kuuawa shahidi Imamu Hussein [10], lakini hakujanukuliwa kutoka kwake mambo ya ndani yanayohusiana na tukio la Ashura. Pamoja na hayo yote, baadhi ya wahakiki wanaamini kwamba, mwanawe Qassim, ameandika maqtal kuhusiana na tukio la Ashura. [11]

Uandishi wa simulizi za mauaji ulishika kasi na kufikilia kilele katika karne ya tatu na ya nne Hijiria na inaelezwa kuwa, baada ya karne ya nne ukachukua mkondo wa kupungua. [12] Baadhi ya maqtal hizi zimechapishwa na baadhi yake zinapatikana na maktaba za dunia huku zingine zikiwa zimetoweka. [13] Baadhi ya wahakiki wanaamini kwamba, kuna simulizi nyingi za mauaji (maqtal) ambazo zilitoweka baada ya kupita zama na kumetajwa majina 14 ya maqtal. [14]

Karne tatu za 8, 9 na 10 kimetajwa kuwa kipindi cha kudorora uandishi wa simulizi za mauaji (maqtal). [15] Hata athari ambazo ziliandikwa katika kipindi hiki zilichukuliwa kutoka katika ripoti za awali za tukio la Karbala au kwa kutumia ripoti zisizo na itibari na bila ya kuwa na nyaraka. [16] Baadhi ya athari hizi zilikuwa na mchango muhimu katika kupotosha tukio la Ashura; [17] kama kitabu cha Rawdhat al-Shuhadaa kilichoandikwa na Mulla Hussein Kashi (820-910) ambacho kiliandikwa mwanzoni mwa karne ya 10 Hijiria. [18]

Kuingia madarakani utawala wa ukoo wa Safavi marasimu na hafla za Ashura zilichukua nafasi na sura rasmi zaidi na kuandikwa maqtal mpya ambazo hazikuwa na vyanzo makini na tukio la Ashura liliandikwa zaidi katika upande wa huzuni, msiba, belua na balaa. Athari hizi zaidi zilikuwa na lengo la kutumika katika vikao vya kusimulia msiba na maombolezo na kuandaa uwanja na mazingira ya simanzi na kulia. Athari kama Ibtilaa al-Awliya, Izalat al-Awham fil Bukaa, Askir al-Ibadah fi Asrar al-Shahadah na Muhriq al-Qulub ni miongoni mwa vitabu hivyo. [19]

Itibari ya Maqtal za Imamu Hussein (a.s)

Rasul Ja’afariyan anaamini kuwa, miongoni mwa vitabu vya simulizi za mauaji vilivyoandikwa katika karne ya pili hadi ya nne Hijria ni athari tano tu ndio zenye itibari: [22]

  • Maqtal al-Hussein (a.s) kilichoandikwa na Abu Mikhnaf Lut bin Yahya al-Azdi (aliaga dunia 157 Hijiria).
  • Tarjumat al-Husein (a.s) wa maqtaluh kutoka katika kitabu cha al-Tabaqat al-Kubra cha Ibn Sa’d (168-230).
  • Tarjuma wa maqtal al-Husayn (a.s) kutoka katika kitabu cha Ansab al-Ashraf cha Ahmad bin Yahya Baladhuri (karne ya pili na ya tatu Hijria)
  • Gozaresh Qiyam Karbala katika kitabu cha al-Akhbar al-tiwal cha Dinawari (222-282 hijria).
  • Kitabu cha Futuh cha Ibn Ibn A'tham (aliaga dunia: baada ya 320 Hijiria). [23]

Maudhui Zilizopo Katika Maqtal ya Imamu Hussein

Baadhi ya madhui zilizopo katika simulizi za mauaji (maqtal) ya Imam Hussein (a.s):

  • Hadithi kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) na Imamu Ali (a.s) kuhusiana na utabiri wa tukio la Ashura
  • Barua na maneno ya Imamu Hussein (a.s) kuanzia mwanzo wa harakati mpaka kuuawa kwake shahidi.
  • Mambo yaliyonukuliwa na watu walioandamana na Imamu Hussein katika tukio la Karbala lakini walibakia hai. [26]
  • Hotuba za Imamu Sajjad (a.s) na Bibi Zaynab (a.s) katika kipindi chote cha safari Kufa, Sham na Madina.
  • Hadithi zinazonasibishwa kwa Maimamu wa Kishia kuhusiana na kuuawa shahidi Imamu Hussein (a.s)
  • Nukta zilizonukuliwa kutoka kwa maadui wa Imamu Hussein (a.s) kuhusiana na tukio la Karbala. [27]

Simulizi Muhimu za Mauaji (Maqtal) za Zama Hizi

Kitabu Maqtal Jami'i Sayyid Shuhada

Baadhi ya simulizi muhimu za mauaji katika zama hizi (karne za 14 na 15 Hijiria) ni:

Vyanzo

  • Āqā Buzurg al-Tihrānī, Muḥammad Muḥsin. Al-Dharīʿa ilā taṣānīf al-Shīʿa. Beirut: Dār al-Aḍwāʾ, [n.d].
  • Jaʿfarīyān, Rasūl. 1380 Sh. "Darbāra-yi manābiʿ-i tārīkh-i ʿĀshūrā." Majalla-yi Āyina-yi Pazhūhish 71, 72:41-52.
  • Group of authors. Maqtal-i jāmiʿ-i sayyid al-shuhadāʾ. Qom: Intishārāt-i Muʾassisa-yi Imām Khomeini, 1389 Sh.
  • Nūrī, Mīrzā Ḥusayn al-. Al-Luʾluʾ wa l-marjān. Tehran: Nashr-i Āfāq, 1388 Sh.
  • Group of authors. Pazhūhishī dar maqtalhā-yi Farsi. Qom: Zamzam-i Hidāyat, 1386 Sh.
  • Ṣadūq, Muḥammad b. ʿAlī al-. Thawāb al-aʿmāl. Beirut: Muʾassisat al-Aʿlamī li-l-Maṭbūʿāt, 1403 AH.
  • Ṣāḥibī, Muḥammad Jawād. 1373 Sh. "Maqtal wa maqtal nigārān." Kiyhān-i Farhangī 111:31-33.
  • Yāwarī, Muḥammad Jawād. 1386 Sh. "Maqtal nigari-yi shīʿayān." Tārīkh-i Islām 32:7-40.