Sura (Kiarabu: السورة) ni istilahi ya Qur'ani, imaanishayo mkusanyiko wa Aya za Qur'ani zenye mwanzo na mwisho ulio wazi na maalumu, mara nyingi Sura za Qur’ani huanza na Bismillahi al-Rahmani al-Rahim. Baadhi ya wafasiri wanaamini kwamba; Aya zote zilizoko katika Sura moja, zina uhusiano na zote kwa pamoja zinafuata au zinahusiana na mada kuu moja ya Sura hiyo. Kwa kuwa baadhi ya Sura za Qur'ani zina aina fulani ya kufanana, hilo limepelekea Sura hizo kugawanywa katika makundi mbalimbali kutokana na kufanana kwake huko. Kugawanya kwa Sura za Qur’ani wakati mwengine huwa ni kulingana na zama za kushuka kwake (Makka au Madina), [Maelezo 1] na wakati mwengine ni kulingana na idadi ya Aya, ambapo Sura hizo za Qur’ani zimegawanywa na kupewa majina tofauti, kama vile (Sab’u Tiwal, Mi-un, Mathani na Mufassal).

Kwa mujibu wa maoni maarufu ya watafiti wa Qur'an ni kwamba; Qur'an ina sura 114. Hata hivyo, waandishi wengine, bila kupunguza Aya zilizoko ndani ya Qur'an, wamedai kuwa idadi ya Sura za Qur'an ni 112 au 113. Hii ni kwa sababu baadhi yao wanaamini kuwa Surat al-Tawba ni mwendelezo wa Surat al-Anfal na si miongoni mwa Sura zinazojitegemea. Wengine pia hawakuizingatia Surat al-Fil na Quraish, wala Surat al-Dhuha na Inshirah kuwa ni Sura zinazojitegemea. Kila moja ya Sura za Qur'an imepewa jina maalum, na mara nyingi jina hilo huchukuliwa kutoka ndani ya maneno ya mwanzo ya Sura au kutoka kwenye maudhui yake. Watafiti wa Qur'ani wanaamini kuwa, majina ya Sura za Qur’ani yalichaguliwa na bwana Mtume (s.a.w.w) mwenyewe, na hairuhusiwi kuitwa kwa jina jingine. Lakini watafiti wengine wanapinga mtazamo huu, wakidai kuwa, majina ya Sura yalikuja baada ya muda fulani, kutokana na matumizi ya mara kwa mara ya watu katika kuziita Sura hizo kwa majina hayo maalumu.

Ni Sura ipi ya kwanza kabisa na ya mwisho kabisa iliyoteremshwa kwa Bwana Mtume (s.a.w.w), ni miongoni mwa masuala yanayojadiliwa katika fani ya elimu za Qur'an (‘Ulumu al-Qur’ani). Kwa mujibu wa maoni ya baadhi watafiti wa Qur’ani, ni kwamba, Surat Fatihatu al-Kitab (Sura al-Fatiha), ndiyo ya kwanza kuteremshwa, na Surat al-Nasri ndiyo ya mwisho iliyoteremshwa kwa ukamilifu kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w). Kuna Hadithi nyingi zinazohusiana na faida za Sura za Qur'ani ndani ya vyanzo vya Hadithi vya Shia pamoja na Sunni. Hata hivyo, watafiti wamezitila shaka Hadithi nyingi kati ya hizo, na wakazijadili kwa upande wa kimapokezi (sanad) na pia kwa upande wa kimatini.

Maana ya Sura na Umuhimu Wake katika Tafiti za Kiislamu

Sura ni istilahi inayotumika katika Qur'ani, inayomaanisha mkusanyiko wa Aya za Qur'ani ambazo ni zenye mwanzo na mwisho maalum. Mara nyingi Sura za Qur’ani huanza kwa Bismillahi al-Rahmani al-Rahim (isipokuwa Surat al-Tawba ambayo haina Bismillahir Rahmanir Rahim).[1] Katika baadhi ya maandiko, Sura za Qur'an zimefananishwa na Sura za kitabu,[2] lakini baadhi ya watafiti wameona kuwa mlinganisho huu si sahihi, kwa sababu Sura za Qur'ani hazina sifa za sura za kitabu.[3] Miongoni mwa migawanyo mbalimbali ya Qur'ani, mgawanyo wake kupitia mfumo wa juzuu na hizb, na mgawanyo wake kupitia mfumo wa Aya na Sura, ndio migawanyo pekee iliyokubalika kuwa ndiyo migawanyiko ya kweli ya Qur'ani yenye asili ya kiqur’ani.[4]

Sura ndogo ndogo na katika baadhi ya matukio Sura refu za Qur'ani (kama vile surat An'aam) ziliteremshwa kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) kwa mpigo mmoja (kwa mfumo wa Sura nzima).[5] Pia baadhi ya Sura zilteremshwa kwa bwana Mtume Muhammad (s.a.w.w) kwa awamu mbali mbali, na mpangilio wa Aya zake uliwekwa kwa amri ya Mtume mwenyewe (s.a.w.w).[6] Inasemekana kwamba; Kugawanywa Qur’an’ kwa mfumo Sura ni suala lenye faida kadhaa, zikiwemo: kurahisisha kujifunza na kuhifadhi Qur'ani, kuleta hisia tofauti na shauku kwa msomaji wa Quran, kuweka pamoja Aya zinazohusiana, na kutofautisha Sura moja na nyingine ambazo zina mada tofauti.[7]

Kuna maoni tofauti yaliyotolewa kuhusiana na suala la jinsi gani Aya za sura moja zinavyohusiana.[8] Wafasiri kama vile Sayyid Muhammad Hussein Tabatabai, Sayyid Qutub, na Muhammad Izzat Darwaza, wanaamini kwamba; kila Sura ina aina fulani ya mshikamano na umoja fulani ambao unatofautiana na Sura nyingine.[9] Kwa mujibu wa maoni ya Tabatabai, mwandishi wa kitabu cha Al-Mizan, ni kwamba; Sura za Qur’ani zina malengo tofauti, na kila moja inafuata maana na lengo maalum ambalo ndio kusudio maalumu linalo elezwa na Aya zote za Sura hiyo.[10] Imeelezwa ya kwamba; Katika karne ya ishirini, mtazamo huu ulikuwa ndio ulienea na ulio chukua nafasi katika zama hizo.[11] Kinyume chake, ni kwamba; Baadhi ya wafasiri wengine kama vile: Nasir Makarim Shirazi, mwandishi wa kitabu cha tafsiri kiitwacho Tafsiri Nemune, hawatilii maanani suala la kuwepo kwa mshikamano wa Aya zote za Sura moja, ila wao wanaamini kwamba, Sura moja inaweza kuelezea ndani mada tofauti.[12]

Pia imeelezwa kuwa; Mwanzoni mwa utume wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), neno Sura lilikuwa likirejelea sehemu tu ya Aya za Qur'ani zinazo fungamana kimaana. Kwa maana hii, Surat al-Baqara yenyewe itakuwa na idadi ya karibu ya Sura thelathini.[13] Hata hivyo, katika miaka ya mwishoni mwa maisha ya bwana Mtume (s.a.w.w), neno Sura lilianza kutumika kama tunavyolifahamu leo hii.[14] Majiid Ma'arif, mtafiti wa Kiislamu, anaamini kwamba; Jambo hili limeleta tofauti kati ya madhehebu ya Shia na Sunni, kwani kwa mujibu wa fiqhi ya Kishia, baada ya Surat al-Hamdu katika swala, ni lazima kusoma Sura moja kamili ya Qur'ani (isipokuwa haifai kusoma Sura zenye sajda), lakini katika fiqhi ya Kisunni, ni kwamba, baada ya kusoma Surat al-Hamdu katika swala, basi unaweza kusoma sehemu yoyote ile ya Qur'ani.[15]

Mgawanyo wa Sura

Nambari Jina la Sura Jina la Sura kwa Kingereza Aya Mpangilio wa
Kuteremka[16]
Mahali
1 Surat al-Fatiha (the Opening) 7 5 Makki
2 Surat al-Baqara (the Cow) 286 87 Madani
3 Surat Al 'Imran (the Family of 'Imran) 200 89 Madani
4 Surat al-Nisa' (Women) 176 92 Madani
5 Surat al-Ma'ida (the Table) 120 112 Madani
6 Surat al-An'am (Cattle) 165 55 Makki
7 Surat al-A'raf (the Elevations) 206 39 Makki
8 Surat al-Anfal (the Spoils) 75 88 Madani
9 Surat al-Tawba (Repentance) 129 113 Madani
10 Surat Yunus (Jonah) 109 51 Makki
11 Surat Hud 123 52 Makki
12 Surat Yusuf (Joseph) 111 53 Makki
13 Surat al-Ra'd (Thunder) 43 96 Madani
14 Surat Ibrahim (Abraham) 52 72 Makki
15 Surat al-Hijr 99 54 Makki
16 Surat al-Nahl (the Bee) 128 70 Makki
17 Surat al-Isra' (the Night Journey) 111 50 Makki
18 Surat al-Kahf (the Cave) 110 69 Makki
19 Surat Maryam (Mary) 98 44 Makki
20 Surat TaHa 135 45 Makki
21 surat al-Anbiya (the Prophets) 112 73 Makki
22 Surat al-Hajj (the Pilgrimage) 78 103 Madani
23 Surat al-Mu'minun (the Faithful) 118 74 Makki
24 Surat al-Nur (the Light) 64 102 Madani
25 Surat al-Furqan (the Criterion) 77 42 Makki
26 Surat al-Shu'ara (the Poets) 227 47 Makki
27 Surat al-Naml (the Ants) 93 48 Makki
28 surat al-Qasas (the Story) 88 49 Makki
29 Surat al-'Ankabut (the Spider) 69 85 Makki
30 Surat al-Rum (the Byzantines) 60 84 Makki
31 Surat Luqman 34 57 Makki
32 Surat al-Sajda 30 75 Makki
33 Surat al-Ahzab (the Confederates) 73 90 Madani
34 Surat Saba' (Sheba) 54 58 Makki
35 Surat Fatir (the Originator) 45 43 Makki
36 Surat Yasin 83 41 Makki
37 Surat al-Saffat (the Ranged Ones) 182 56 Makki
38 Surat Sad 88 38 Makki
39 Surat al-Zumar (the Throngs) 75 59 Makki
40 Surat al-Ghafir (the Forgiver) 85 60 Makki
41 Surat Fussilat (Elaborated) 54 61 Makki
42 Surat al-Shura (Consultation) 53 62 Makki
43 Surat al-Zukhruf (Ornaments) 89 63 Makki
44 Surat al-Dukhan (Smoke) 59 64 Makki
45 Surat al-Jathiya (Crowling) 37 65 Makki
46 Surat al-Ahqaf 35 66 Makki
47 Surat Muhammad 38 95 Madani
48 Surat al-Fath (Victroy) 29 111 Madani
49 Surat al-Hujurat (Apartments) 18 106 Madani
50 Surat Qaf 45 34 Makki
51 Surat al-Dhariyat (the Scatterers) 60 67 Makki
52 Surat al-Tur (the Mount) 49 76 Makki
53 Surat al-Najm (the Star) 62 23 Makki
54 Surat al-Qamar (the Moon) 55 37 Makki
55 Surat al-Rahman (the All-beneficent) 78 97 Madani
56 Surat al-Waqi'a (Imminent) 96 46 Makki
57 surat al-Hadid (Iron) 29 94 Madani
58 Surat al-Mujadila (the Pleader) 22 105 Madani
59 Surat al-Hashr (the Banishment) 24 101 Madani
60 Surat al-Mumtahana (the Tested Woman) 13 91 Madani
61 Surat al-Saff (Ranks) 14 109 Madani
62 Surat al-Jumu'a (Friday) 11 110 Madani
63 Surat al-Munafiqun (the Hypocrites) 11 104 Madani
64 Surat al-Taghabun (Disposession) 18 108 Madani
65 Surat al-Talaq (Divorce) 12 99 Madani
66 Surat al-Tahrim (the Forbidding) 12 107 Madani
67 Surat al-Mulk (Sovereignty) 30 77 Makki
68 surat al-Qalam (the Pen) 52 2 Makki
69 Surat al-Haqqa (the Inevitable) 52 78 Makki
70 Surat al-Ma'arij (Lofty Stations) 44 79 Makki
71 Surat Nuh (Noah) 28 71 Makki
72 Surat al-Jinn (the Jinn) 28 40 Makki
73 Surat al-Muzzammil (Enwrapped) 20 3 Makki
74 Surat al-Muddaththir (Shrouded) 56 4 Makki
75 Surat al-Qiyama (Resurrection) 40 31 Makki
76 Surat al-Insan (Man) 31 98 Madani
77 Surat al-Mursalat (the Emissaries) 50 33 Makki
78 Surat al-Naba' (the Tiding) 40 80 Makki
79 Surat al-Nazi'at (the Wrestlers) 46 81 Makki
80 Surat 'Abasa (He Frowned) 42 24 Makki
81 Surat al-Takwir (the Winding Up) 29 7 Makki
82 Surat al-Infitar (the Rending) 19 82 Makki
83 Surat al-Mutaffifin (the Defrauding) 36 86 Makki
84 Surat al-Inshiqaq (the Splitting) 25 83 Makki
85 Surat al-Buruj (the Houses) 22 27 Makki
86 Surat al-Tariq (the Nightly Visitor) 17 36 Makki
87 Surat al-A'la (the Most Exalted) 19 8 Makki
88 surat al-Ghashiya (the Enveloper) 26 68 Makki
89 Surat al-Fajr (the Dawn) 30 10 Makki
90 Surat al-Balad (the City) 20 35 Makki
91 Surat al-Shams (the Sun) 15 26 Makki
92 Surat al-Layl (the Night) 21 9 Makki
93 Surat al-Duha (the Morning Brightness) 11 11 Makki
94 Surat al-Sharh (Expanding) 8 12 Makki
95 Surat al-Tin (the Fig) 8 28 Makki
96 Surat al-'Alaq (Clinging Mass) 19 1 Makki
97 Surat al-Qadr (the Ordainment) 5 25 Makki
98 Surat al-Bayyina (the Proof) 8 100 Madani
99 Surat al-Zalzala (the Quake) 8 93 Madani
100 Surat al-'Adiyat (the Chargers) 11 14 Makki
101 Surat al-Qari'a (the Catastrophe) 11 30 Makki
102 Surat al-Takathur (Rivalry) 8 16 Makki
103 Surat al-'Asr (Time) 3 13 Makki
104 Surat al-Humaza (the Scandal-monger) 9 32 Makki
105 Surat al-Fil (the Elephant) 5 19 Makki
106 Surat Quraysh 4 29 Makki
107 Surat al-Ma'un (Aid) 7 17 Makki
108 Surat al-Kawthar (Abundance) 3 15 Makki
109 Surat al-Kafirun (the Faithless) 6 18 Makki
110 Surat al-Nasr (the Help) 3 114 Madani
111 Surat al-Masad (Palm Fibre) 5 6 Makki
112 Surat al-Ikhlas (Monotheism) 4 22 Makki
113 Surat al-Falaq (Daybreak) 5 20 Makki
114 Surat al-Nas (Humans) 6 21 Makki

Baadhi ya Sura za Qur’ani, kwa sababu ya kufanana kwao, zimegawanywa katika makundi tofauti.[17]

Mwanyo wa Sura kulingana na Nyakazi za Kuteremshwa Kwao

Makala Asili: Makkiyyah na Madaniyyah

Kulingana na mtazamo maarufu wa wataalamu na watafiti wa Qurani, Sura za Qur’ani zinagawanywa katika makundi makuu mawili kulingana na wakati wa kuteremka kwao, nayo ni; Makkiyyah (za Makka) na Madaniyyah (za Madian).[18] Kwa msingi huu, kile kilichoteremshwa kabla ya Hijra ya bwana Mtume (s.a.w.w) kwenda Madina kinaitwa "Makkiyyah", na kile kilichoteremshwa baada ya kufika kwake Madina kinaitwa "Madaniyyah". Kwa hiyo, ikiwa Sura au Aya fulani imeteremka baada ya Hijra, hiyo itakuwa Madaniyyah, hata kama iliteremshwa kwenye mji au maeneo ya mji wa Makkah au katika hali ambayo Mtume (s.a.w.w) alikuwa yumo safarini, kama vile Aya zilizoteremshwa wakati wa Fat-hu Makka au Hijjatul Wida’a.[19]

Baadhi ya wataalamu na watafiti wa Qur'ani, hawakuzigawa Sura za Makkiyyah na Madaniyyah kulingana na wakati wa kuteremka kwake, bali ni kulingana na mahali au walengwa wa Sura hizo. Kulingana na kipimo cha mahali, ni kwamba; Yale yote yaliyoteremshwa Makkah na vitongoji vyake kama vile Mina, Arafat, na Hudaybiyyah huitwa Makkiyyah, hata kama yaliteremshwa baada ya Hijra, na yale yote yaliyoteremshwa Madina na vitongoji vyake kama vile Badr na Uhud huitwa Madani.[20] Lakini kulingana na kipimo cha walengwa wa Sura hizo, ni kwamba; Yale yote yaliyolengwa kwa watu wa Makkah huitwa Makkiyyah na yale yote yaliyolengwa kwa ajili ya watu wa Madina huitwa Madaniyyah.[21] Kigezo cha kuwatambua walengwa kwa kile kilichoteremshwa, ni kamba; Aya yenye ibara isemayo: Enyi watu huhisabiwa kuwa ni Makkiyyaha, na zile zenye ibara isemayo: Enyi mlioamini hushisabiwa kuwa ni Madaniyyah.[22]

Mgawanyo wa Sura kwa Kigezo cha Urefu na Ufupi wa Sara

Sura za Qurani zimegawanywa katika makundi kadhaa kulingana na urefu au ufupi wake. Kulingana na kigezo hicho, Sura za Qur’ani zimegawika katika makundi yafuatayo; Sura za Sab'un Tiwaal, Mi-un, Mathani, na Al-Mufassalaat.[23]

Aina Nyengine za Mgawanyo wa Sura za Qur’ani

Miongoni mwa aina nyingine za vigao vilitajwa kwa ajili ya Sura za Qurani ni:

‘Aza-im «عَزائِم», Musabbihaat «مُسَبِّحات», Hawamiim «حَوامیم» , Mumtahinaat «مُمتَحِنات», Haamidaat «حامدات», Sura zinazoanzia na Qul «قُل», Tawaasiin «طَواسین», Mu’awwidhataini «مُعَوَّذَتیْن», na Zahraawaan «زَهراوان».[30]

  • ‘Aza-im «عَزائِم»: Sura zenye Sajda ambazo ni; Surat al-Sajda, Fussilat, Najm, na Alaq, ambazo ikiwa mtu atakuwa katika hali ya kuzisoma au kusikiliza, papo hapo hupaswa kusudu Sajda mara moja pale isomwapo Aya yenye sijda ndani ya Sura hizo.[31]
  • Hawamiim «حَوامیم»: Hii ni kuanzia Sura ya arobaini (Surat Ghafir) hadi arobaini na sita (Surat Ahqaf) za Qur'ani ambazo zinaanza na herufi mbili zilizogawanywa; Ha-Mim «حم»[32] Katika Sura zote hizi, mara tu baada ya kutajwa kwa herufi hizo zilizogawanywa, Mwenye Ezi Mungu amelezea suala la kushushwa kwa Qur'ani.[33]
  • Mumtahinaat «مُمتَحِنات»: Sura hizi ni kama vile: Al-Hadid, Al-Hashr, As-Saff, Al-Jumu'ah, na At-Taghabun ambazo zinaanza na tasbihi ya Mwenye Ezi Mungu.[34]

Idadi ya Sura za Qur’ani

Watafiti wengi wanaamini kuwa idadi ya Sura za Qur’ani ni 114.[35] Hata hivyo, baadhi ya waandishi bila kupunguza idadi ya Aya za Qurani, wanaamini kuwa idadi ya Sura za Qurani ni 112, na wanauhisabu mtazamo huu kuwa ndio mtazamo maarufu wa Shia.[36] Kwa mtazamo wao, ni kwamba; Surat al-Fil na Quraysh ni Sura moja, pia surat al-Dhuha na Inshirah kiasilia zilikuwa ni Sura moja, na siyo sura mbili tofauti.[37] Nadharia hii imetokana na juhudi za kuchanganya aina mbili za kanganyifu za Riwaya.[38] Kwa mujibu wa baadhi ya riwaya, mwenye kusali ni lazima asome Sura moja tu ya Qur'ani baada ya kumaliza kusoma Surat al-Hamd.[39] Ila kwa mujibu wa kundi jingine la Hadithi, ni kwamba; ikiwa mwenye kusali atasoma Suratu a-Fil baada ya kumaliza kusoma Suratu al-Hamd, basi ni lazima asome pia Surat Quraish, au kama baada ya Suratu al-Hamd ataamua kusoma Surat al-Duha, basi ni lazima aunganishe na Surat a-l Inshirah.[40] Baadhi ya watafiti wamekataa nadharia hii na wamependekeza njia nyingine ya kutatua riwaya hizi mbili kanganyifu. Kwa mujibu wao, ingawa katika sala ni lazima mtu kusoma Sura moja tu baada ya kumaliza Surat Al-Fatiha, ila huku hii imeondolewa juu ya surat al-Fil na Quraish, pamoja na Surat al-Duha na Inshirah.[41] Baadhi ya wafasiri wa Shia na Sunni pia wanaamini kuwa Surat al-Anfal na Tawba ni Sura moja, na bila kupunguza idadi ya Aya za Qur'ani, wanazihisabu idadi ya Sura za Qur'ani kuwa ni 113.[42]

Idadi ya Sura za Qur'ani katika Hadithi za Sunni

Katika baadhi ya Hadithi za Sunni, tofauti na khitilafu za kuhesabu idadi ya Sura za Qur'ani zimepelekea kupunguza au kuongeza Aya katika Qur'ani.[43] Kwa mujibu wa alivyosema Suyuti, mwandishi wa kitabu cha Al-Itqan, ni kwamba; Mus'haf wa Abdullah bin Masud ulikuwa na sura 112, kwa sababu yeye aliiona kuwa Mu'awadhataini (Surat Al-Falaq na An-Nasi) kama ni dua tu, na si sehemu ya Qur'ani.[44] Pia, Suyuti anasema kuwa; Mus'haf wa Ubayya bin Ka'ab ulikuwa na sura 116, kwa sababu Ubayya bin Ka'ab alikuwa ameongeza Sura mbili ambazo zinaitwa Khal-‘u na Hafdu kwenye Qur'ani.[45] Baadhi ya wanazuoni wa Mashariki pia wameongeza idadi ya Sura za Qur'ani na kuzihesabu kuwa 116, jambo ambalo limetimia kwa njia ya kuzigawa nusu kwa nusu Surat al-Alaq na Muddathir, na kuzifanya kila moja kuwa ni Sura mbili tofauti.[46]

Uwekaji wa Majina ya Sura za Qurani

Kila moja ya Sura za Qur’ani ina jina lake maalum, ambalo mara nyingi linatokana na maneno ya mwanzo ya Sura hiyo au kutoka kwenye maudhui na ujumbe uliomo ndani yake. Kwa mfano, surat Al-Baqara imepewa jina hili kutokana na kutajwa kwa ng'ombe wa Wana wa Israeli ndani ya Sura hiyo, na Surat An-Nisa imepewa jina hili kutokana na kutajwa kwa sheria zinazohusiana na wanawake ndani yake.[47] Baadhi ya Sura za Qurani zina majina zaidi ya moja. Kwa mfano, Suyuti ameelezea idadi ya majina 25 tofauti kwa ajili ya surat Al-Fatiha.[48]

Kuna tofauti ya maoni; iwapo uwekaji majina haya ulifanywa kwa maagizo ya bwana Mtume (s.a.w.w) kupitia ufunuo au ulifanywa na Masahaba baada yake.[49] Baadhi ya watafiti wa Qurani kama vile Al-Zarkashi na Al-Suyuti wanaamini kwamba; Uwekaji majina wa Sura za Qur’ani ulifanywa na bwana Mtume mwenyewe, na ni suala la tawqifiyyun,[50] yaani haupaswi kubadilishwa majina hayo.[51] Kwa kutegemea hoja hii ya kwamba; Majina ya Sura za Qur’ani yamewekwa na bwamna Mtume (s.a.w.w) kwa mwongozo wa wahyi, na kuwepo umarufuku wa kuleta mabadiliko ndani yake, baadhi ya waandishi wameuelezea uwekaji wa majina ya Sura za Qur’ani kama ni sehemu ya miujiza ya kifasihi ya Qurani, wakidai kwamba; kusudio kuu na muhtasari wa Sura unaweza kueleweka kutoka kwa majina hayo.[52]

Kinyume na mtazamo wa Sayyid Muhammad Hussein Tabataba'i na Abdullah Jawadi Amuli, baadhi ya wafasiri wa Shia wa karne ya kumi na nne, hawaamini kuwa majina ya Sura yaliteuliwa na bwana Mtume (s.a.w.w), na kwamba suala hili ni lenye umarufu mbele ya Mwenye Ezi Mungu.[53] Kwa mtazamo wao ni kwamba; hata katika zama za Mtume (s.a.w.w), majina ya Sura nyingi yaliibuka kutokana na Masahaba kutumia majina hayo mara kwa mara.[54] Kwa mujibu wa maoni ya Jawadi Amuli, haiwezekani Sura yenye maarifa ya kiwango cha juu na hekima za kupindukia, ipewe jina la mnyama, au kwa mfano; Surat al-An'am ambayo ina majadiliano na tafiti kahdaa kuhusiana na tauhidi, iitwe kwa jina la al-An'am leneye maana ya wanyama, au Surat al-Namli yenye visa kadhaa vya mitume ije kuitwa kwa jina la al-Namlu kwa maana ya mdudu chungu (sisimizi).[55]

Mpangilio wa Sura za Qur’ani

Watafiti wengi wanaamini kwamba mpangilio wa Sura za Qurani katika Mus'haf (Msahafu), haukufanywa kwa amri ya bwana Mtume (s.a.w.w), bali ulifanywa na Masahaba.[56] Moja ya sababu zinazothibitisha mtazamo huu, ni tofauti ya mpangilio wa Sura katika misahafu tofauti ya Masahaba;[57] kama vile Mus'haf wa Imamu Ali uliopangwa kulingana na mpangilio wa kushuka kwa Sura ulivyokuwa.[58] Toleo la sasa la Qur’ani lililopo miongoni mwa Waislamu ni toleo lililokusanywa kwa amri ya Khalifa wa tatu, ambaye ni Othman ibn Affan,[59] na kuidhinishwa na Imam Ali na Maimamu wengine wa Ahlul-Bayt (a.s).[60]

Hata hivyo, baadhi ya watafiti wa Qur’ani wanaamini kuwa mpangilio wa sasa wa sura za Qur’ani ulifanywa kwa amri ya bwana Mtume (s.a.w.w).[61] Baadhi ya watafiti hawa wanaamini kuwa; Sura za Qur’ani zimewekwa kwa namna maalumu iliyounda fungamano lenye mlingano na uhusiano maalumu kati yao.[62] Kikundi kingine kinadai kuwa; Mpangilio wa Sura za Qur’ani ni mchanganyiko wa amri kutoka kwa bwana Mtume (s.a.w.w) pamoj na ijtihadi (uamuzi wa kibinafsi) wa Masahaba waliokabidhiwa jukumu la kukusanya Qur’ani na Othman.[63]

Sura ya Kwanza na ya Mwisho Kushuka

Kuna mitazamo mitatu kuhusu Sura ya kwanza kushuka kwa bwana Mtume (s.a.w.w). Kundi moja  linasema kwamba; Sehemu ya mwanzo kushuka ilikuwa ni Aya za mwanzo za surat al-Alaq, huku wengine wakiamini kwamba; Cha mwanzo kushuka kilikuwa ni Aya za mwanzo za Surat al-Muddathir, pia kuna wengine wanaosema kwaba; Cha mwanzo kushuka kilikuwa ni surat al-Fatiha.[64] Muhammad Hadi Ma'arifati, mwandishi wa kitabu Al-Tamhid, anaamini kuwa; Ingawa Aya za mwanzo za Surat al-‘Alaq ndizo Aya za kwanza kushuka, na kwamba Aya za mwanzo kushuka baada ya kipindi cha ulinganiaji wa chini kwa chini ni baadhi ya Aya za Surat al-Muddathir, Ila Sura ya kwanza kabisa iliyoshuka kikamilifu, ilikuwa ni Surat al-Hamd (Fatihatul Kitab).[65]

Pia kuna mitazamo tofauti kuhusiana na Sura ya mwisho kushuka kwa Mtume Muhammad (s.w.w.w); Baadhi ya watafiti wanasema kuwa, Sura ya mwisho ilikuwa ni Surat Baraa-a, huku wengine wakidai kuwa ni Surat al-Nasri, na wengine wanasema kuwa ni Surat al-Maida.[66] Katika moja ya Hadithi kutoka kwa Imamu Sadiq ni kwamba; Sura ya mwisho kushuka ilikuwa ni Surat al-Nasri.[67] Kwa kuwa Sura al-Nasr ilishuka kabla ya ufunguzi (ukombozi) wa mji wa Makka, na Surat al-Tawba ni baada ya ukombozi wa Makka, hii imemfanya Muhammad Hadi Ma'arifati kuamini kwamba; ingawa Aya za kwanza za Surat Baraa-a zilishuka baada ya Surat al-Nasri, ila Sura ya mwisho iliyoshuka kikamilifu ilikuwa ni Surat al-Nasri.[68]

Faida za Sura

Makala Asili: Faida za Sura

Katika vyanzo vikuu vya mwanzo vya Hadithi za Shia, kuna Hadithi kadhaa kuhusiana na faida za Sura za Qur’ani, na milango kadhaa katika vitabu kama vile; Al-Kafi[69] na Thawab al-A'mal,[70]imekusanya na kutafiti ndani yake aina hii ya Hadithi. Katika nyakati zilizofuata baadae, pia wanazuoni kadhaa waliandika kuhusiana na Hadithi hizi vitabuni mwao.[71] Katika vyanzo vya Hadithi za Sunni pia, kuna Hadithi nyingi kuhusiana na faida za Sura na Aya fulani za Qurani.[72] Hata hivyo, Hadithi hizi zimekabiliwa na tatizo la udhaifu wa ithibati katika asili mapokezi na matini yake na nyingi kati yake zimeelezwa kuwa ni Hadithi za kughushi (bandia).[73]

Maelezo

  1. Kuhusiana na suala la kuteremshwa kwa Qur’ani, ni kwamba; Kuna Sura zilizoteremshwa katika zama ambazo Mtume Muhammad (s.a.w.w) alikuwa akiishi Makka, nazo ndizo Sura ziitwazo Makkiyyah, na kuna Sura zilizoteremshwa wakati ambo Mtume Muhammad (s.a.w.w) alikuwa akiishi Madina, nazo ndizo ziitwazo Madaniyyah

Rejea

  1. Ma'arif, Mabahith Dar Ulumi Qur'ani, 1383, uk. 52.
  2. Rukni, Ashnayi Ba Ulumi Qur'an, 1379 S, uk. 104.
  3. Ma'arif, Mabahith Dar Ulumi Qur'ani, 1383, uk. 52.
  4. Tabatabai, Al-Mizan, 1417 AH, juz. 13, uk. 230-231
  5. Ma'arif, Dar Omad Bar Tarikh Qur'an, 1383 S, uk. 137
  6. Ma'arif, Dar Omad Bar Tarikh Qur'an, 1383 S, uk. 137
  7. Zarqani, Manahel al-Irfan, Dar Ihya al-Trath al-Arabi, Juz. 1, uk.
  8. Khamegar,Sakhtar Handasi Surehaye Qur'an, 1386 S, uk. 19-14.
  9. Mir, «Peyvastegi Sure, Tahwili Dar Tafsir Qur'an Dar Qur'an Bistom», Tarjume Muhammad Hassan, Muhammadi Mudhafar, uk. 443.
  10. Tabatabai, Al-Mizan, 1417 AH, juz. 1, uk. 16.
  11. Mir, «Peyvastegi Sure, Tahwili Dar Tafsir Qur'an Dar Qur'an Bistom», Tarjume Muhammad Hassan, Muhammadi Mudhafar, uk. 443.
  12. Makarim Shirazi, Qur'an wa Akhirin Payambar, 1385 S, uk.307.
  13. Ma'arif, Mabahith Dar Ulumi Qur'ani, 1383 S, uk. 137.
  14. Ma'arif, Mabahith Dar Ulumi Qur'ani, 1383 S, uk. 137.
  15. Ma'arif, Mabahith Dar Ulumi Qur'ani, 1383 S, uk. 137.
  16. Maarifat, At-Tamhid, 1386 S, juz. 1, uku. 135-138.
  17. Ramiyar, Tarikh Qur'an, 1369 S, uk.
  18. Maarifat, At-Tamhid, 1386 S, juz. 1, uku. 131.
  19. Maarifat, At-Tamhid, 1386 S, juz. 1, uku. 130.
  20. Suyuti, al-Itqan, 1421 AH, juz. 1, uk. 55.
  21. Suyuti, al-Itqan, 1421 AH, juz. 1, uk. 56.
  22. Suyuti, al-Itqan, 1421 AH, juz. 1, uk. 81.
  23. Ahmadian, Qur'an Shenasi, 1382 S, uk. 56-57.
  24. Radmanesh, Ashnayi Ba Ulumi Qur'an, 1374 S, uk. 150.
  25. Radmanesh, Ashnayi Ba Ulumi Qur'an, 1374 S, uk. 150.
  26. Maarifat, At-Tamhidi, 1386 S, juz. 1, uk. 282.
  27. Javan Arasteh, Darsiname Ulumi Qur'ani, 1380 S, uk. 192-193.
  28. Ramiyar, Tarikh Qur'an, 1369 S, uk. 595
  29. Ramiyar, Tarikh Qur'an, 1369 S, uk. 595
  30. Ramiyar, Tarikh Qur'an, 1369 S, uk. 595
  31. Bani Hashimi, Tawdhih al-Masail Marajii, 1381 S, juz. 1, uk. 592-593.
  32. Ramiyar, Tarikh Qur'an, 1369 S, uk. 596
  33. Suyuti, Tanasuq Ad-durar Fi Tanasub As-suwar, 1406 AH, uk.
  34. Tabatabai, Al-Mizan, 1417 AH, juz. 19, uk. 144.
  35. Muhammadi, Soroush Asimani, 1381 S, uk. 99.
  36. Guruhe Az Mualifan, Ulumi Al-Qur'an Inda Al-Mufasiriin, 1375 S, uk. 273.
  37. Guruhe Az Mualifan, Ulumi Al-Qur'an Inda Al-Mufasiriin, 1375 S, uk. 273.
  38. Doshti, «Barresi Wahadat Dhuhs wa Inshirah wa Fil Quraysh», uk. 77-78.
  39. Kuleini, Al-Kafi, 1407 AH, juz. 3, uk. 314
  40. Tazama: Sheikh Tusi, Tahdhib al-Ahkam, 1407 AH, juz. 2, uk. 72; Tabrasi, Majmau al-Bayan, 1372 S, juz. 10, uk. 827.
  41. Tabatabai, Al-Mizan, 1417 AH, juz. 20, uk. 365; Dashti, «Barresi Wahdat Dhuha wa Inshrah wa Fil wa Quraysh», uk. 87.
  42. Tazama: Tabatabai, Al-Mizan, 1417 AH, juz. 9, uk. 146; Suyuti, al-Itqan, 1421 AH, juz. 1, uk. 228.
  43. Suyuti, al-Itqan, 1421 AH, juz. 1, uk. 229.
  44. Suyuti, al-Itqan, 1421 AH, juz. 1, uk. 229.
  45. Suyuti, al-Itqan, 1421 AH, juz. 1, uk. 229.
  46. Badawi na Sayyidi, Difaa Az Qur'an Dar Barabar Araye Khavarshenasan, 1383 S, uk. 175.
  47. Suyuti, al-Itqan, 1421 AH, juz. 1, uk. 203.
  48. Suyuti, al-Itqan, 1421 AH, juz. 1, uk. 193-196.
  49. Abu Shahbeh, Al-Madkhal Lidirasat Al-Qur'an Al-Karim, 1423 AH, uk. 1423 AH, uk. 321.
  50. Tazama: Zarakashi, Al-Burhan, 1410 AH, juz. 1, uk. 367; Suyuti, Al-Itqan, 1421 AH, juz. 1, uk. 192.
  51. Abu Shahbeh, Al-Madkhal Lidirasat Al-Qur'an Al-Karim, 1423 AH, uk. 1423 AH, uk. 321.
  52. Khamegar, Sakhtar Handasi Surehaye Qur'an, 1386 S, uk. 132.
  53. Tabatabai, Qur'an Dar Islam, 1353 S, uk. 219 ; Jawadi Amuli, Tafsir Tasnim, 1389 S, juz. 2, uk. 27.
  54. Tabatabai, Qur'an Dar Islam, 1353 S, uk. 219 ; Jawadi Amuli, Tafsir Tasnim, 1389 S, juz. 2, uk. 27.
  55. Jawadi Amuli, Tafsir Tasnim, 1389 S, juz. 2, uk. 27.
  56. Faqhizadeh, Pezuhesh Dar Nadhm Qur'an, 1374 S, uk. 72.
  57. Ramiyar, Tarkh Dar Qur'an, 1369 S, uk. 598.
  58. Sheikh Mufid, Al-Masal al-Sarawiyah, 1413 AH, uk. 79.
  59. Faqhizadeh, Pezuhesh Dar Nadhm Qur'an, 1374 S, uk. 73.
  60. Maarifat, Tamhid, 1386 S, juz. 1, uk. 341-342.
  61. Suyuti, Al-Itqan, 1421 AH, juz. 1, uk. 223; Subhi Saleh, Mabahith Fi Ulumi al-Qur'an, 1372 S, uk. 71.
  62. Suyuti, Tartib Suwari al-Qur'an, 2000 AD, uk. 32.
  63. Ibn Atiyyeh, Al-Muhariru al-Awajiz, 1422 AH, juz. 1, uk. 50.
  64. Suyuti, Al-Itqan, 1421 AH, juz. 1, uk. 106-108; Maarifat, Tamhid, 1386 S, juz. 1, uk. 124-126.
  65. Maarifat, Tamhid, 1386 S, juz. 1, uk. 127.
  66. Maarifat, Tamhid, 1386 S, juz. 1, uk. 127.
  67. Sheikh Saduq, Uyun Akhbar al-Ridha (a.s), 1378 AH, juz. 2, uk. 6.
  68. Maarifat, Tamhid, 1386 S, juz. 1, uk. 128.
  69. Kuleini, Al-Kafi, 1407 AH, juz. 2, uk. 596.
  70. Sheikh Saduq, Thawab al-Amal, 1406 AH, uk. 103.
  71. Tazama: Hurr Amili, Wasail al-Shia, 1409 AH, ju. 6, uk. 37; Majlisi, Bihar al-Anwar, 1403 AH, juz. 89, uk. 223, juz. 110, uk. 263; Burujurdi, Jamiu Ahadith al-Shia, 1386 S, juz. 23, uk. 790.
  72. Malik bin Anas, Al-Mautwa, 1425 AH, juz. 1, uk. 202; Bukhari, Sahih Bukhari, 1422 AH, juz. 6, uk. 187-189; Tirmidhi, Sunan al-Tirmidhi, 1419 AH, juz. 4, uk. 231.
  73. Nasiri, «Chegunegi Taamul Ba Riwayat Fadhail wa Khawas Ayat wa Suwari», uk. 67

Vyanzo

  • Majlisī, Muḥammad Bāqir al-. Biḥār al-anwār.Chapa ya pili. Beirut: Muʾassisat al-Wafāʾ, 1403 AH.
  • Maʿrifat, Muḥammad Hādī. Al-Tamhīd fī ʿulūm al-Qurʾān. Qom: Daftar-i Nashr-i Islāmī, 1412 AH.
  • Muṣṭafawī, Ḥassan al-. Al-Taḥqīq fī kalimāt al-Qurʾān. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmīyya, 1430 AH
  • Rāghib al-Iṣfahānī, Ḥusayn b. Muḥammad al-. Mufradāt alfāẓ al-Qurʾān. Beirut: Dār al-Qalam, 1412 AH.
  • Suyūṭī, Jalāl al-Dīn al-. Al-Itqān fī ʿulūm al-Qurʾān. Chapa ya pili. Qom: Manshūrāt-i Raḍī, 1363 Sh.
  • Ṭabāṭabāī, Sayyid Muḥammad Ḥussein al-. Al-Mīzān fī tafsīr al-Qurʾān. Beirut: Muʾassisat al-Aʿlamī li-l-Maṭbūʿāt, 1417 AH.
  • Ṭabrasī, Faḍhl b. al-Ḥassan al-. Majmaʿ al-bayān. Beirut: Muʾassisat al-Aʿlamī li-l-Maṭbūʿāt, 1415 AH.
  • Zamakhsharī, Maḥmūd al-. Al-Kashshāf ʿan ḥaqāʾiq ghawāmiḍ al-tanzīl wa ʿuyūn al-aqāwīl fī wujūh al-taʾwīl. Chapa ya tatu. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿArabī, 1407 AH.
  • Zarkashī, Muḥammad b. ʿAbd Allāh. Al-Burhān fī ʿulūm al-Qurʾān. Beirut: Dār al-Fikr, 1408 AH.