Nenda kwa yaliyomo

Qul Nne

Kutoka wikishia

Qul nne (Kiarabu: القلاقل) ni jina la sura zinazoanza na neno Qul ambazo ni: Surat al-Kafirun, Surat al-Ikhlas, Surat al-Falaq na Surat al-Nas. Sura hizo hizi nne zote zinaanza na neno Qul (sema) Sura hizi zinafahamika kwa jina la Qul nne au Dhat al-Qalaqil. Kwa mujibu wa hadithi iliyonukuliwa kutoka kwa Bwana Mtume (s.a.w.w) na ambayo imeondokea kuwa mashuhuri kwa jina la hadithi ya Dhat al-Qalaqil ni kwamba, imekokotezwa na kutiliwa mkazo wa kusoma sura hizo tajwa kwa ajili ya kusalimika na balaa.

Utambulisho

Qul nne ni anuani na jina la Sura nne za Qur'an Tukufu ambazo zinaanza na neno Qul yaani sema. [1] Sura hizo ni: Surat al-Kafirun, ambayo inaanza na: قل یا ایها الکافرون, Surat al-Ikhlas, ambayo Aya yake ya kwanza ni: «قل هو الله احد», Surat al-Falaq, ambayo inaanza na: «قل اعوذ برب الفلق», Surat al-Nas ambayo inaanza na: «قل اعوذ برب الناس». []

Majina mengine ya sura hizi ni: "Suwar Qul", [3] na "Dhat al-Qalaqil". [4] Surat al-Jinn pia imeanza na Qul [5], lakini pamoja na hayo haitambuliwi kuwa miongoni mwa sura nne mashuhuri kwa jina la Qul nne. [6]

Fadhila na sifa maalumu

Katika riwaya na hadithi mbalimbali katika Uislamu, hakujanukuliwa fadhila maalumu za kusoma Sura na Qul nne; pamoja na hayo katika baadhi yya hadithi kumeusiwa na kutiliwa mkazo juu ya kusoma Suratu al-Ikhlas, Falaq, Nas pamoja na Fatiha (Alhamdu) [7] au Ayat al-Kursiyy [8] kwa ajili yya kusalimika na hatari mbalimbali; kama ambavyo imeelezwa kuwa, ili kusalimika na hatari mbalimbali mtu anaweza kusoma Sura za Qul nne pamoja na Suratu al-Nasr. [9]

Imesisitizwa juu ya kusoma sura nne zinazoanza na Qul katika Sala ya usiku na Sala za mustahabu katika nyusiku za mwezi Rajab. [10] Katika hadithi iliyopokewa kutoka kwa Bwana Mtume (s.a.w.w) ambayo ni mashuhuri kwa jina la hadithi ya "Dhat al-Qalaqil" imeusiwa na kutiwa mkazo juu ya kusoma sura hizi ili kusalimika mtu yeye mwenyewe, watoto na mali yake. [11]

Katika duru mbalimbali Qul nne zilikuwa viini vya utamaduni wa wananchi wa Iran na sura hizi zilikuwa zikisomwa kwa ajili ya kusalimika na hatari; kiasi kwamba, Sanai Ghaznavi, mshairi Mfursi wa karne ya 5 Hijiria amezitaja katika moja ya mashairi yake Sura za Qul kwamba, ni hirizi. [12] Kadhalika pia imekuja katika moja ya visa vya Jalal Aal Ahmad, mwandishi wa visa wa zama hizi kwamba: Wakati wa asubuhi alipokuwa akifungua duka lake, alikuwa akisoma Sura hizi nne zinazoanza na Qul (Qul nne). [13]

Tafsir al-Qalaqil

Ibn Sina amejihusisha na kufasiri sura tatu kati ya Qul nne (yaani Suratu al-Ikhlas, al-Falaq na al-Nas) katika kitabu kinachojulikana kwa jina la "Tafsir al-Qalaqil. Athari hii imechapishwa kwa hima ya Ihsan Yarshater kwa anuani ya Tafsiri ya Surat Tawhid, Tafsiri ya Surat al-Falaq na Tafsiri ya Surat al-Nas. Kitabu hiki kimechapishwa katika risala tano, [14] na Mahmoud bin Muhammad Hassani Waidhi, mmoja wa wafasiri wa Qur'an wa karne ya 7 Hijiria pia, ana tafsiri inayojulikkana kwa la Balabil al-Qalaqil ambamo ndani yake amejihusisha na kusafiri Aya za Qur'an ambazo zinaanda na kitendo cha kuamrisha cha Qul (sema). [15]