Arafaat

Kutoka wikishia
Muonekano wa viwanja vya Arafa

Arafaat au Arafa (Kiarabu: عرفات أو عرفة) ardhi yenye eneo la kilomita za mraba kumi na nane mashariki mwa Makka. Kusimama Arafa ni moja ya nguzo za Haji na mahujaji lazima wasimame katika jangwa la Arafat siku ya 9 ya Dhu al-Hijjah. Kwa mujibu wa riwaya kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kuna dhambi zinazoweza kusamehewa tu kwa kuhudhuria Arafa. Imamu Hussein(a.s) aliomba dua katika ardhi hii ya Arafat, na dua hiyo ni maarufu kwa dua ya Arafa.


Taarifa za jumla

Njia ya Arafa kuelekea Masjid al-Haram

Arafa ni ardhi pana na tambarare mashariki mwa Makka, yenye eneo la kilomita za mraba kumi na nane, ambayo leo hii ni sawa umbali wa kilomita 21 kutoka mji wa Makka.[1]

Jabalur-rahmah (mlima wa rahmah), mlima huu upo kaskazini mwa viwanja vya Arafa[2] na kutokana na sababu hii pia huitwa kwa jina la (mlima wa arafaat).[3]

Ardhi ya Arafa, kwa mtizamo wa kifiqhi haihesabiki kuwa ni sehemu ya Haramu ya Makkah,[4] na kutokana na hali hii mipaka yake imekuwa ni yenye kufahamika katika zama fotauti za historia na zimekuwa zikitumika alama na mabango au vibao vya kuainisha mita, na imekuwa ikiainishwa na kutofautishwa kwa umakini wa hali ya juu.[5]

Kwa Mujibu wa riwaya na simulizi za historia ya maeneo hayo, katika zama za Nabii Ibrahim(a.s) na tukio au kisa cha kuhamia mkewe Hajir kwenye ardhi ya Makkah, Watu wa Jurhum walikuwa wakiishi katika ardhi ya Arafa.[6] Baadhi ya wataalamu wa mambo ya jografia wa zamani wameitambulisha arafa kuwa ilikuwa ni kijiji kidogo sana.[7]

Dalili za kuitwa ardhi hii kwa jina la arafaat

Kwa mujibu wa uandishi wa Muhammad bin Abdur-rahman Sakhawiy, muandishi wa hisroria wa karne ya kumi Qamariah. Anasema neno Arafaat ni sawa na neno Qaswabaat (ni wingi wa neno Qaswaba lenye maana ya kumi) kiasi kwamba kwa msingi huu, kila sehemu ya ardhi ya Arafaat, huitwa kwa jina la Arafa na Arafaat ni jina la eneo lote hili.[8]

Kwa mujibu wa baadhi ya riwaya na baadhi ya simulizi ni kuwa, wakati Jibril alipomfundisha Nabii Ibrahiim Ibada ya hija katika ardhi ya Arafaat alimwambia nabii Ibrahim: (je, umefahamu vyema ibada yako?) kwa maana ( je, umeshika vema na kufahamu vema taratibu za ibada yako?) na Ibrahimu akajibu kwa kusema (ndio, bila shaka). Kutokana na majibizano hayo na kutokana na matumizi ya neno la kiarabu (أعرفت) lenye maana ya kwamba (je umefahamu neno lililotumika kwenye swali, eneo hilo likaitwa na kujilikana kwa jina la Arafaat au Arafa.[9] Vyanzo vingine, vinasema kuwa Arafaat ni sehemu na mahali walipo kutana na kutambuana Adamu na Hawaa.[10] Vivyo hivyo Arafaat imetambulishwa kuwa ni mahala au sehemu ambayo waislaamu hukiri dhambi zao mahala hapo na kutokea sehemu hiyo wakamuomba na kumtaka Mwenyezi Mungu msamaha.[11]

Ndani ya Qur'an tukufu limetajwa jina la Arafaat katika aya ya 198 ya surat al-baqarah, katika kutaja hukumu na adabu za hija:

{{لَیسَ عَلَیکمْ جُناحٌ أَنْ تَبْتَغُوا فَضْلاً مِنْ رَبِّکمْ فَإِذا أَفَضْتُمْ مِنْ عَرَفاتٍ فَاذْکرُوا اللَّهَ عِنْدَ الْمَشْعَرِ الْحَرامِ وَ اذْکرُوهُ کما هَداکمْ وَ إِنْ کنْتُمْ مِنْ قَبْلِهِ لَمِنَ الضَّالِّین}}.[12]

Umuhimu wa arafa

Arafaat inamafungamano na faradhi ya Ibada ya Hija[13] na ni miongoni mwa sehemu takatifu za kiislaam.[14] kusimama Arafaat, ni miongoni mwa nguzo za ibada ya hija ya Tamatui na ibada ya hija haitekelezwi bila ya kisimamo cha Arafah, kwa msingi huu, mahujaji ni lazima kuhudhuria na kuwepo kwenye eneo hilo siku ya tarehe 9 ya dhul-hijjah, kuanzia Adhuhuri ya kisheria hadi magharibi ya kisheria na wanatakiwa kubakia kwenye jangwa la Arafaat kwa muda wote huo.[15]

Kabla ya uislamu, watu wa Makka hawakufanya vitendo fulani, ikiwa ni pamoja na kusimama Arafa, kwa sababu walijiona kuwa ni watu wa mahala patakatifu na wateule.[16] Kwa msingi huu baadhi ya simulizi na riwaya zingine katika vitabu vya hadithi vya ahli-sunna zinasema ya kuwa Mtume(s.a.w.w) pia alisimama katika viwanja vya Arafaat katika kuweka misingi ya ibada ya hija kabla ya uislam.[17]

Na kwa mujibu wa riwaya na simulizi zigine ambazo zimenukuliwa kutoka kwa Mtume wa uislamu ni kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu katika magharibi ya siku ya Arafa muda wa kuzama kwa jua hujifaharisha mbele ya Malaika kutokana na watu wasimamao kwenye viwanja vya Arafaa, hujifaharisha kwa visimamo hivyo na huwasamehe na kuwafutia madhimbi yao yote.[18] Kubakia na kusimama kwa mahujaji katika viwanja vya Arafaat, ni sababu ya kusamehewa kwa madhambi ya waja na imefahamika kuwa ni sababu ya kusamehewa kwa madhambi ya wenye kusimama kwenye jangwa hilo, na kwa mujibu wa simulizi na riwaya kutoka kwa Mtume Mtukufu (s.a.w.w) ni kuwa kuna madhambi ambayo hayasemehewi isipokuwa tu siku ya Arafa na kwa kusimama katika viwanja vya Arafa.[19] na kwa msingi wa simulizi zingine au riwaya nyingine kutoka kwa Imamu Swadiq(a.s) ni kuwa mtu mwenye madhambi zaidi ni yule ambae atasimama katika viwanja vya Arafa na kuamini kuwa hakusamehewa madhambi yake katika viwanja hivyo.[20]

Vivyo hivyo Arafaat katika riwaya mbalimbali imeelezwa kuwa inamafungamano na Duhuwil-ardhi (kubadilishwa au kutawanywa na kuumbwa kwa ardhi), ikiwa pembezoni mwa al-Kaaba na ardhi ya Mina, ni sehemu ambazo au ni mahali ambapo ardhi itokae eneo hili ilitawanywa na kusambaa.[21] Imamu Husein(a.s) katika dua ya Arafah aliomba dua hiyo akiwa nje ya hema lake katika ardhi ya Arafaat na kusimama upande na kwenye ukingo wa kushoto wa mlima wa Arafaat, yaani kwenye mlima au Jabalur-rahmah na kusimama eneo hilo akiomba dua hiyo.[22]

Rejea

  1. Pur'aminiy, (Negareshii bar Aarafaat, uk. 164.
  2. Borusawiy, Awdhahul-masaalik, 1427 h, uk. 468; Jaafariyaan, Aathaar islaami Makkeh wa Madineh, 1382 S, uk.131.
  3. Kurdiy, At-taarikhul-qawiim limakata wabaitil-laahil-kariim, 1420 H, juz. 1, uk. 492.
  4. Shekhe Swadouq, Manlaa yahdhuruhul-faqihi, 1413 H, juz. 2, uk. 464; Harawiy, al-ishaaraat ilaa ma'arifatiz-ziyaraat, 1423 H, uk. 74.
  5. Ja'afariyaan, Aathaar islaami Makkeh wa Madineh, 1382 S, uk. 129-130; Ibnul-faqiihi, Al-buldaan, 1416 H, uk. 78, Borusawiy, Awdhahul-masaalik, 1427 H; Shekhe Swadouq, Manlaa yahdhuruhul-faqihi, 1413 H , juz. 2, uk. 463.
  6. Twabatwabai, Al-miizaan, 1393 H, juz. 1, uk. 288-289-294.
  7. Al-istibswaar fii Ajaaibil-amswaar, 1986 A.D, uk. 35.
  8. Sakhaawiy, Al-buldaaniyaat, 1422 H, uk. 225.
  9. Azraqiy, Akhbaru Makkah, 1416 H, juz. 1, uk. 67; Faakihiy, Akhbaru Makkah, 1424 H, juz. 5, uk. 9.
  10. Sakhawiy, Al-buldaniyaat, 1422 H, uk.225; Bii Aazaar Shiraziy, Bostan shanaasii wa joghrafiyaye taarikh qiswase qur'an, 1380 S, uk. 240.
  11. Sakhawiy, Al-buldaniyaat, 1422 H, uk. 225.
  12. Surat al-baqarah, aya ya 198
  13. Farhang Fiqhi, 1392 S, juz. 5 uk. 376.
  14. Farhang Fiqhi, 1392 S, juz. 5 uk. 375.
  15. Muusawiy Shahroudiy, Jaamiul-fataawa manaasikil-hajji, 1428 H, uk. 173-174.
  16. Twabatwabai, Al-miizaan, 1393 H, juz. 2, uk. 80.
  17. Mudiir shaanechiy, (Hajji peyambar s.a.w.w), uk. 83.
  18. Nuuriy, Mustadrakul-wasaail, 1408 H, juz. 8, uk. 36.
  19. Nuuriy, Mustadrakul-wasaaili, 1408 H, juz. 10, uk. 30.
  20. Shekhe Swadouq, Manlaa yahdhuruhul-faqihi, 1413 H, juz. 2, uk. 211; Nuuriy, Mustadrakul-wasaaili, 1408 H, juz. 10, uk. 30.
  21. Shekhe Swadouq, Manlaa yahdhuruhul-faqihi, 1413 H, juz. 2, uk. 241.
  22. Umraaniy, (Bar'rasiy sanade wa dhaile duaye arafeh Imamu Husein(a.s), uk. 65.

Vyanzo

  • Qur'an Tukufu.
  • Ibnul-faqiih, Ahmad bin Muhammad, Al-buldaan, kilicho sahihiswha na Al-haadiy, Bairut, Aalamul-kutub, cha mwaka 1416 H.
  • Azraqiy, Abul-waliid, Akhbaru Makkah wamaa jaa'a fiiha minal-aathaar, kilicho sahihishwa na Mulhas na Rushdi Swaaleh, Bairut, mwaka 1416 H.
  • Al-istibswaar fii ajaaibil-amswaar, mtunzi hajulikani, kilicho sahihshwa na Saad Zaghluul Abdul-hamiid, Baghdaad, Darus-shu'uunit-thaqafiyah, mwaka 1986 A.D.
  • Borusawiy, Muhammad bin Aliy, Awdhahul-masaalik ilaa ma'arifatil-buldaan wal-mamaalik, Bairut, Darul-gharbiil-islaamiy, chapa ya kwanza, mwaka 1427 H.
  • Bii Aazaar Shiraziy, Abdul-kariim, Bostan shanasi wa joghrafiyaye taarikh qiswas qur'an, Daftar farhangiye islaamiy, mwaka 1380 S.
  • Poor Aminiy, Muhammad Amin, (Negaaresh bar Arafaat), katika jarida la Miiqaatu Hajj, namba 11 na 12, Taabestaan mwaka 1374 S.
  • Jaafariyaan, Rasoul, Aathaar islaamiy Makkeh wa Madineh, Tehran, Mash'ar, mwaka 1382 S.
  • Sakhawiy, Muhammad bin bdur-rahman, Al-buldaaniyaat, kilicho sahihshwa na Husaam bin Muhammd Qatwan, Riyaadh, Darul-atwaa, mwaka 1422 H.
  • Shekhe Swadouq, Muhammad bin Aliy, Manlaa yahdhuruhul-faqihi, Qom, Intishaaraat Jaamieye Mudarrisiin, mwaka 1413 H.
  • Twabatwabai, Sayyid Muhammad Husein, Al-miizaan fii tafsiril-qur'an, Bairut, Muassasatul-aalami lil-mat'buuaat, mwaka 1393q/ 1973 A.D.
  • Umraaniy, Mas'oud, (Bar'rasiy sanade wa dhaile duaye arafeh imam Husein (a.s), katika jarida la Mishkaat, namba 110, Bahaar mwaka 1390 S.
  • Faakihiy, Muhammad bin Is'haaq, Akhbaru Makkah fii qadiimid-dahri wahadiithihi, Makkah, Maktabatul-asadiy, chapa ya nne, mwaka 1424 H.
  • Farhange fiqhi mutwaabiq madh'hab Ahlul-bait, kilicho hakikiwa na kutungwa na Taasisi ya Dairatul-ma'aarif fiqhi islaamiy bar madhhabe Ahlul-baiti chini ya usimamizi wa Mahmoud Haashimiy Shaharoudiy, j5, Qom, Muassasatu darul-ma'aarif fiqhi islaamiy bar madhhabe ahlul-baiti, mwaka 1392 S.
  • Kurdiy, Muhammad Twaahir, At-taarikhul-qawiim limakta wa baitil-llahil-kariim, Bairut, Daru Khudhri, mwaka 1420 H.
  • Mudiir shaakhchiy Kaadhim, (Hajje peyambar (a.s.w.w), katika jarida la Miqaat hajj. Namba 25 na 26, Zemestan mwaka 1377 S.
  • Muusawiy Shaaharoudiy, Sayyid Murtadhaa, Jaamiul-fataawa manaasikil-hajj: Kwa njia mpya inayo endana na fatawa za marajiu watano kati ya marajiu watukufu na wakubwa wa taqliid, Tehran, Nashru Mash'ar, mwaka 1428 H.
  • Nooriy, Husein bin Muhammad Taqiy, Mustadrakul-wasaaili wa mustanbatul-masaaili, Bairut, Muassasatu Aalul-baiti li'ihyaait-turaath, mwaka 1408 H / 1987 A.D.
  • Harawiy, Aliy bin Abu Bakar, Al-ishaaraat ilaa Ma'arifatiz-ziyaaraat, kilicho sahihishwa na Omar Ali, Kairo, Maktabatut-thaqaafatid-diniyah, mwaka 1423 H.