Suratu al-Maa'uun

Kutoka wikishia

Surat Al-Ma'wun (Kiarabu: سورة الماعون) au Surat Al-Araayta ladhii ni surah ya 107 na ni moja ya sura za Makka za Qur-ani, ambayo iko katika juzuu ya thelathini. Jina la Ma'wun limechukuliwa katika neno la mwisho la sura hii na linamaanisha Zaka. Katika surah hii zimetajwa sifa za wale wanaoikadhibisha siku ya Kiyama. Qur'an inasema kuwa watu hawa hawahimizi kulisha maskini, wanapuuza swala na ni wanafiki wanaojionesha na wakazuilia watu manufaa.

Imesemekana kwamba Suratul Al- Ma'un iliteremshwa kuhusu Abu Sufyan. Kuna fadhila za kusoma sura hii, ikiwa ni pamoja na kwamba mwenye kusoma Suratul Al- Ma'uun baada ya swala ya I’sha, Mwenyezi Mungu atamsamehe na atamlinda mpaka wakati wa adhana ya sala ya asubuhi.

Utangulizi

Imenukuliwa kuhusu maana ya Ma'uun ya kwamba, katika zama za ujahilia, manufaa yoyote (au kitu chochote kile chenye thamani na faida) kiliitwa Ma'uun, na baada ya Uislamu, iliitwa zakat. Majina mengine ya sura hii ni Dini na Kukadhibisha au kusema uwongo. Kwa hiyo, maudhui mawili haya ni miongoni mwa mada za sura hii.[3]

Mahali na Mpangilio wa Uteremshwaji

Surah Ma'uun ni mojawapo ya sura za Makkah na ni sura ya kumi na saba iliyoteremshwa kwa Mtume (s.a.w.w). Sura hii ni sura ya 107 katika mpangilio wa sasa wa mas-haf [4] na imejumuishwa katika juzuu ya 30 ya Qur’ani.

Idadi ya Aya na Vipengele Vyake

Surah Ma'un ina aya 7, maneno 25 na herufi 114. Kwa upande wa juzuu, imejumuishwa katika juzuu ya 30, surah hii ni mojawapo ya surah (yenye aya fupi).[5]

Maudhui

Ishara na dalili za watu wasio na Imani thabiti Katika sura hii, sifa na matendo ya wale wanaoikadhibisha Siku ya Kiyama yameelezwa katika hatua tano, kwamba kwa sababu ya kukanusha siku ya Kiama, wanakataa kutumia njia ya Mwenyezi Mungu ya kuhimiza na kuwasaidia mayatima na masikini, na wanapuuza Sala na ni wanaafiki, hujionyesha na kuzuia watu manufaa. [6]

Dalili na Sababu ya Kuteremshwa

Imenukuliwa kuhusu sababu ya kuteremshwa kwa Suratul Al- Ma'uun ya kwamba, Sura hii iliteremshwa baada ya Abu Sufiyan kukataa kumsaidia maskini aliyekwenda kwake kumuomba msaada, Abu Sufiyani alikuwa na ngamia wawili wakubwa aliwokuwa akiwatumia kila siku kwa ajili ya chakula chake yaye na masahaba zake Lakini siku moja alipokuja yatima na kumuomba msaada alikataa na akampiga kwa fimbo na kumfukuza.[8]

Fadhila na Sifa za Kusoma Suratul-Al-Maa’un

Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kwamba mwenye kusoma Suratul Al- Ma’un baada ya Swala ya I’shaa, Mwenyezi Mungu atamsamehe na atamlinda mpaka wakati wa asubuhi wa kusali. Na Imenukuliwa kutoka kwa Imamu Swadiq (a.s) ya kwamba yoyote atakayeisoma sura hii baada ya sala ya Alasiri atakuwa katika ulinzi na usalama wa Mwenyezi Mungu mpaka jioni ya siku inayofuata, [10] Imeelezwa katika Hadithi nyingine kwamba kusoma Sura Al-Ma'un katika sala za faradhi na sunna Mwenyezi Mungu atazikubali sala za mtu huyo bila ya kuangalia amali zake (nyingine zisizokuwa njema). [11]

Matini na Tafsiri (Tarjuma) ya Surat Al-Maa’un

Kwa jina la Mwenyeezi Mungu mwingi wa Rehema Mwenye kurehemu بِسْمِ اللَّـهِ الرَّ‌حْمَـٰنِ الرَّ‌حِيمِ
Jee unamjua ambaye anakadhibisha dini? (1) أَرَأَيْتَ الَّذِي يُكَذِّبُ بِالدِّينِ ﴿١﴾
Huyo ndiye anayemsukuma yatima (2) فَذٰلِكَ الَّذِي يَدُعُّ الْيَتِيمَ ﴿٢﴾
Wala hahimizi kumlisha masikini, (3) وَلاَ يَحُضُّ عَلَى طَعَامِ الْمِسْكِينِ ﴿٣﴾
Basi ole wao wanaosali, (4) فَوَيْلٌ لِلْمُصَلِّينَ ﴿۴﴾
Ambao wanapuuza swala zao! (5) الَّذِينَ هُمْ عَنْ صَلاَتِهِمْ سَاهُونَ ﴿۵﴾
Ambao wao hujionyesha, (6) الَّذِينَ هُمْ يُرَاءُونَ ﴿۶﴾
Wakazuia watu manufaa. (7) وَيَمْنَعُونَ الْمَاعُونَ ﴿۷﴾

Rejea

Vyanzo