Kifo cha Mtume (s.a.w.w)
Kifo cha Mtume (s.a.w.w) ( رحلة النبي (ص)) ni miongoni mwa matukio makubwa ya mwaka wa 11 Hijria tukio lililopelekea Waislamu kukumbwa na mgawanyiko mkubwa baina yao, suala ambalo kwa hakika lilikuwa na athari ya moja kwa moja na ya kudumu juu ya mustakabali wao. Mjadala juu ya kifo au kuuawa kishahidi kwa Mtume (s.a.w.w) ni mojawapo ya matokeo machungu ya tukio hili. Kwa mujibu wa masimulizi yanayo patikana katika vyanzo mbali mbali vya Waislamu wa Kishia na Kisunni, inasemekana kwamba; Bwana Mtume (s.a.w.w) alilishwa sumu na mwanamke wa Kiyahudi, na hatimae kufa shahidi. Hata hivyo, kuna wengine wanaoamini kuwa; Bwana Mtume (s.a.w.w) alikufa kifo cha kawaida, bila kuhusisha tukio lolote lile la kutendewa uovu.
Kwa mujibu wa maoni ya Jafar Murtadha Amoli, mwanazuoni mashuhuri na mtafiti wa historia ya Kiislamu, ni kwamba; Mtume wa Mwenye Ezi Mungu (s.a.w.w) alijaribiwa mara kadhaa kudhuriwa, na hatimae majaribio hayo yalifanikiwa kumuondoa Bwana Mtume (s.a.w.w) duniani. Akiendelea na maelezo yake, amesisitiza kuwa Mtume (s.a.w.w) alikufa kutokana na kupewa sumu mara kwa mara. Mjadala huu umeacha alama isiyofutika katika fikra za Waislamu na unaendelea kuwa ni moja ya sehemu muhimu inayojadiliwa katika historia ya Uislamu, ikiwakilisha mgawanyiko wa mitazamo juu ya tukio hilo kubwa.
Matokeo muhimu ya siku za mwisho za uhai wa Bwana Mtume (s.a.w.w) yameelezwa kwa kina katika vyanzo vya kihistoria. Miongoni mwa matokeo haya, ni pamoja na kuandaliwa kwa Jeshi la Usama, ambalo bwana Mtume (s.a.w.w) aliliagiza kuelekea vitani ili kudumisha amani na kulinda Uislamu. Tokeo jingine ni la Dawaat na Kalamu (kalamu na chupa ya wino), ambapo bwana Mtume (s.a.w.w) aliagiza kwa ajili ya kuandika maandiko muhimu kabla ya kifo chake, ila baadhi ya Masahaba walipingana na suala hilo, na kuibua mjadala ulioacha athari kubwa katika historia ya Uislamu. Aidha, bwana Mtume (s.a.w.w) alisimulia Hadithi ya “Thaqalaini”, akiwataka Waislamu kushikamana na Qur'ani na Ahlul-Bait (kizazi chake kitakatifu), kama ndio urithi wake wa thamani. Hadithi hii inachukuliwa kuwa na umuhimu mkubwa mno katika kuelewa mafundisho ya Uislamu na urithi wa bwana Mtume (s.a.w.w). Hatimae, suala la kumteua mrithi wa bwana Mtume (s.a.w.w) limekuwa ni moja ya mijadala mikubwa zaidi katika historia ya Kiislamu, likiwa na athari kubwa juu ya mgawanyiko wa Waislamu katika madhehebu tofauti.
Kwa mujibu wa vyanzo vya kihistoria, baada ya kifo cha Mtume (s.a.w.w), watu wa Madina, hususan binti yake Fatima (s.a.w.w), walikumbwa na huzuni kubwa mno. Omar bin Khattab alisisitiza kuwa Mtume hakuwa amekufa, na akawatishia kuwaua wale waliokuwa wakiamini kuwa Mtume amefariki kwa akiwakaripia kwa makelele, hali ambayo ilimfanya Abu Bakar kuja kumtuliza kwa kusoma Aya ya 144 ya Surat Al-Imran. Wengine wanaamini kuwa hatua ya Omar ilikuwa ni sehemu ya mpango ulioandaliwa kabla ya kumweka Abu Bakar katika nafasi ya uongozi.
Kwa mujibu wa maelezo ya wanahistoria, Imam Ali (a.s), akisaidiwa na baadhi ya watu kama vile Fadhlu bin Abbas na Usama bin Zaid, ndiye aliychukua jukumu la kuutayarisha mwili wa bwana Mtume (s.a.w.w) kwa ajili ya mazishi na hatimae kumzika katika nyumba yake. Wakati harakati za mazishi zikiendelea, baadhi ya viongozi wa Ansari (watu wa Madina) na Wahajirina (waliohamia Madina kutokea Makka) walikusanyika katika banda la Saqifa ya Bani Sa’edah, na hatimae wakachagua Abu Bakar kuwa mrithi wa Bwana Mtume (s.a.w.w), kinyume na maagizo ya Mtume mwenyewe (s.a.w.w).
Kulingana na Hadithi mashuhuri za Shia, kifo au kuuawa kishahidi kwa bwana Mtume (s.a.w.w) kulitokea mnamo tarehe 28 ya mwezi wa Safar, wakati Hadithi za Sunni zinaeleza kuwa tokeo hilo lilitokea mnamo tarehe 12 ya mwezi wa Rabi'ul Awal. Suala hili limezua mijadala mikubwa miongoni mwa wafuasi wa madhehebu haya mawili, kwani linahusisha moja kwa moja masuala ya uongozi na urithi wa uongozi baada ya kifo cha bwa Mtume (s.a.w.w).
Nafasi
Bwana Mtume (s.a.w.w) alifariki mwaka wa 11[1] Hijiria katika mji wa Madina.[2] Waislamu wote wanakubaliana ya kwamba, kifo cha Bwana Mtume (s.a.w.w), kilichotokea mnamo siku ya Jumatatu.[3] Miongoni mwa wanazuoni na wasomi wa Kishia, Sheikh Mufidu na Sheikh Tusi wameshikilia mtazamo usemao kwamba; tukio hili lilitokea tarehe 28 ya mwezi wa Safar.[4] Maoni ambayo kwa maelezo ya Sheikh Abbas Qomi, ni maoni yaungwayo mkono na wanazuoni wengi wa madhehebu ya Shia.[5] Kulingana na mwanahistoria wa Kishia, ajulikanaye kwa jina la Rasul, ni kwamba; hakuna simulizi zozote zile zilizo sahihi zinazo thibitisha tarehe hii,[6] lakini Mashia wameikubali kutokana kwa kuwamfua wanazuoni wao wawili ambao ni Sheikh Mofid na Sheikh Tusi. [7]
Kuna Riwaya tofauti zinazohusiana na tarehe ya kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w) zilizo nukuliwa na Wanazuoni mbali mbali wa Kisunni. Wanazuoni hawa wamesimulia ya kwamba; tukio hili lilitokea ndani ya masiku ya mwanzo mwezi wa Rabi-ul-Awwal, ambapo baadhi yao wakisema kuwa lilitokea mwezi mosi,[9] wengine wakasema mwezi pili,[10] na kundi jengine likasema kuwa alifariki mnamo tarehe 12 ya mwezi mwezi huo huo.[11] Baadhi ya wanazuoni wa Kisunni wameizingatia siku hii ya mwezi 12, kuwa ndiyo rai maarufu zaidi miongoni mwa wafuasi wa madhehebu ya Kisunni.[12] Katika kitabu cha Kashfu al-Ghumma, Imam Baqir (a.s) amenukuliwa akisema kwamba; Bwana Mtume (s.a.w.w) alifariki mnamo tarehe pili mwezi wa Rabi-ul-Awwal.[13] Hata hivyo, Sheikh Abbas Qummi ameeleza ya kwamba; Riwaya hii imetaja tarehe hiyo kutokana na khofu (taqiyyah).[14] Ila, wanazuoni wengine wawili wa Kishia, ambao ni Kulaini na Muhammad bin Jarir al-Tabari, pia nao wanaamini kwamba tukio hili lilitokea mnamo tarehe 12 Rabi-ul-Awwal.[15]
Vyanzo kama vile Al-Sira al-Nabawiyyah kilichoandikwa na Ibnu Hisham (aliyefariki mnamo mwaka 218 Hijria), [16] Tabaqatu al-Kubra kilichoandikwa na Muhammad bin Sa’ad (aliyefariki mwaka 230 Hijria),[17] Tarikh Yaqoubi kilichoandikwa na Ahmad bin Abi Yaqub (aliyefariki mwaka 284 Hijria),[18] Al-Irshad kilichoandikwa na Sheikh Mufidu (aliyefariki mwaka 413 Hijria),[19]. na Sahih Min Sirati al-Nabiyyi al-Adhami kilichoandikwa na Jafar Murtaza Amili (aliyefariki mwaka 1441 Hijria), vyote kwa vimebeba ndani yake maudhui muhimu zinazohusiana na maisha ya bwana Mtume Muhammad (s.a.w.w) hadi kufikia kifo chake. Vyanzo hivi vyenye hadhi na umuhimu mkubwa katika historia ya Kiislamu vimekusanya taarifa na matokeo muhimu ambayo yamekuwa yakirejelewa na wanazuoni wa Kiislamu kwa karne tofauti zilizopita. Kila kimoja kina mchango wake wa kipekee katika kufafanua maisha ya bwana Mtume (s.a.w.w) na kujenga uelewa wa kina kuhusiana na matokeo muhimu yaliojiri wakati wa mwisho wa uhai wake (s.a.w.w).[20]
Yaliyojiri Baada ya Kifo cha Mtume
Kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w) ilikuwa ni tokeo kubwa na lenye athari za kudumu kwa hatima ya Uislamu na Waislamu kwa jumla.[21] Tukio hili liliishtusha jamii ya Kiislamu, na mara tu baada ya kifo chake, kundi la wazee kutoka kwa Muhajirina na Ansari walikusanyika kwenye banda la Saqifah Bani Sa'idah na kumchagua Abu Bakar kama khalifa wa kwanza wa Uislamu baada ya bwana Mtume (s.a.w.w).[22] Wakati huu, nyumba ya bibi Fatima, binti wa bwaba Mtume (s.a.w.w), ilikabiliwa na uvamizi wa wafuasi wa waunga mkono ukhalifa wa Abu Bakar, ulioivamia nyumba yake kwa lengo la kuchukua kiapo cha utiifu kutoka Ali bin Abi Talib kwa ajili ya kumtambua Abu Bakar kama ni khalifa halali.[23]kwa mujibu wa masimulizi ya Mashia, shambulio la uvamizi huo lilipelekea kujeruhiwa kwa bibi Fatima,[24] [Maelezo 1] na hatimae kusababisha kifo chake cha kishahidi.[25] Tukio hili limeacha athari kubwa katika historia ya Uislamu, kwani amri za Mtume kuhusu urithi wa Imam Ali (a.s) hazikutekelezwa kama alivyo usia,[26] na badala yake, mzozo wa urithi huo ulisababisha mgawanyiko mkubwa ndani ya jamii ya Kiislamu. Mgawanyiko huu ulikuwa ndio msingi wa kuundwa kwa madhehebu makuu mawili ya Kiislamu, Shia na Sunni, ambayo yamebaki hadi leo.[27]
Katika sehemu mbalimbali duniani, Waislamu wanaadhimisha kumbukumbu ya kifo cha bwana Mtume (s.a.w.w) kwa kufanya maadhimisho mbali mbali yanayo ashiria maombolezo ya tokeo hilo.[28] Tarehe 28 Safar Nchini Iran, inatambulika rasmi kama ndiyo siku ya kifo cha bwana Mtume (s.a.w.w), na Mashia huadhimisha tokeo hili kwa maombolezo na dua maalum.[29]
Tokeo la Kupewa Sumu Bwana Mtume (s.a.w.w)
Hadithi ya kupewa sumu kwa Mtume (s.a.w.w), ni mojawapo ya masimulizi yanayozungumzia sababu ya kifo chake (s.a.w.w). Kuna aina mbili za Riwaya zinazojadili iwapo Mtume alifariki kutokana na kifo cha kawaida au kutokana na kupewa sumu.[30] Baadhi ya watafiti wanaamini kwamba; kifo cha Mtume wa Mwenye Ezi Mungu (s.a.w.w) kilijiri kupitia hali na sababu za kawaida na za kimaumbile, kama vile kuumwa magonjwa ya kawaida. [31]
Hata hivyo, katika vyanzo mbalimbali vya Kiislamu, khususan katika vitabu vya Hadithi vya Kishia,vinavyotoa ushahidi unaoeleza kwamba; kifo cha bwana Mtume (s.a.w.w) kinatokana na kupewa sumu. Katika kitabu cha al-Kafi, ambacho ni mojawapo ya vitabu vikubwa vya Hadithi kwa mujibu wa madhehebu ya Kishia, kuna Riwaya iliyosimuliwa na Imamu Swadiq (a.s) isemayo kwamba; bwana Mtume ugonjwa wa mwishoni mwa maisha ya bwana Mtume (s.a.w.w), yanatokana na kupewa sumu.[32]
Hadithi hii pia inapatikana katika kitabu cha Basair al-Darajat, ambacho ni kitabu chengine cha Hadithi cha Kishia.[33] Aidha, Hadithi inapatikana katika cha “Tabaqatu” cha Ibnu Sa’ad, ambacho ni kitabu cha kihistoria cha karne ya tatu Hijria, kuna ripoti inayoeleza kwamba; Mtume Muhammad (s.a.w.w) alipatwa na magonjwa kutokana na kula nyama ya kondoo iliyokuwa imetiwa sumu ndani yake. Nyama hii ililetwa na mwanamke wa Kiyahudi baada ya kutekwa kwa Khaybar, kwa ajili ya bwana Mtume (s.a.w.w) pamoja na Masahaba zake. Masimulizi haya yanaonyesha kuwa ugonjwa uliomsumbua bwana Mtume (s.a.w.w) mwishoni mwa maisha yake ulisababishwa na sumu hiyo, na hatimae kifo chake kikahusishwa na tukio hilo. [34]
Sheikh Mufidu,[35] Sheikh Tusi,[36] Allama Hilli[37] na waandishi wengine wa baadhi ya vyanzo vya Kisunni kama vile Sahihi Bukhari,[38] Sunan Daarmi,[39] na Al-Mustadrak ‘Alaa Al-Sahihaini,[40] wote wamelihusiha suala la kifo cha bwana Mtume Muhammad (s.a.w.w) na sumu. Jafar Murtaza Amili, mwanahistoria maarufu wa Kishia, alifanya juhudi kubwa za kukusanya taarifa kutoka kwenye vyanzo vya Kishia pamoja na Kisunni kuhusiana na jaribio la kumuua Mtume (s.a.w.w) lililo fanywa na watu fulani. [41] Yeye aliunga mkono imani isemayo kwamba; bwana Mtume alipewa sumu na hatimae kufariki kishahidi[42] kutokana na kitendo hicho cha kuhujumiwa kupitia sumu hiyo kilicho fanywa na watu wa karibu yake.[43]
Tafsiri ya Ayyashi, ambayo ni moja ya tafsiri mashuhuri za Qur'ani za Kishia, kuna Riwaya iliyo pokewa kutoka kwa Imamu Swadiq (a.s) ambayo inabainisha ya kwamba; wake wawili wa Mtume ndio walio kuwa na jukumu kubwa katika kitendo hicho cha kumpa sumu bwana Mtume (s.a.w.w). Riwaya hii imesababisha mijadala na khitilafu nyingi miongoni mwa wanazuoni wa Kiislamu kuhusu mazingira halisi ya kifo cha bwana Mtume (s.a.w.w).[44]
Kisa cha Dawa Iitwayo Ladud
- Makala Asili: Hadithi ya Ladud
Kisa cha Ladud, ambacho baadhi ya watu wamekihisabu kuwa ni kisa cha kutunga,[45] huku wengine wakikiona kama ni ngano za kutunga,[46] ni mojawapo ya matukio yaliyotokea katika siku za mwishoni mwa ugonjwa wa bwana Mtume (s.aw.w). Katika Sahihi al-Bukhari na Tabaqatu Ibnu Sa’ad, kuna Riwaya iliyo pokewa kutoka kwa bibi Aisha isemayo kwamba; katika siku za mwisho za uhai wa bwana Mtume (s.aw.w), alipokuwa akiugua maradhi makali, walimmimina Ladud (dawa chungu inayotumika kwa wagonjwa wa nimonia) kwenye kinywa chake, ingawa bwana Mtume (s.a.w.w) alikuwa ameashiria wasifanye hivyo.
Mtume alipopata nafuu kidogo, aliamuru kwamba dawa hiyo imiminwe kwenye midomo ya kila mmoja mwa waliokuwepo hapo, isipokuwa ami yake Abbas.[47] Najmi, mtafiti wa Kishia, anatilia shaka ya kwamba; wale waliofanya ughushi wa hadithi hii walikuwa wakitafuta uhalali wa kitendo cha Omar bin Khattab katika suala la Duwat na Qalam, ambapo yeye aliamua kumtuhumu bwana Mtume (s.a.w.w) kwa tuhuma za kuwewezeka kutokana na uchungu wa mauti.[48]
Mazishi ya Bwana Mtume (s.a.w.w)
Ibnu Sa’ad amesimulia akisema kwamba; baada ya kifo cha Mtume wa Mwenye Ezi Mungu (s.a.w.w), watu walijawa na huzuni kubwa.[49] Binti yake (Fatima (a.s)), aliendelea kulia kwa huzuni na akisema, "Ya Abtaah!" Bibi Fatima alikuwa mtu mchangamfu wakati wa uhai wa bwana Mtume (s.a.w.w), ila baada ya kifo cha baba yake, katu hakuna aliyewahi kumuona akitabasamu. [50] Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) katika Nahj al-Balagha, ya kwamba, Imamu Ali anasema kuwa; “Baada ya kufariki Mtume wa Mwenye Ezi Mungu (s.a.w.w), nikukuwa nikiutayarisha mwili wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w) huku kuta na milango ya nyumba ikiangusha kilio, huku Malaika nao wakuwa pamoja nami katika shughuli hiyo.[51]
Kwa mujibu wa vyanzo vya kihistoria, bwana Mtume (s.a.w.w) alifariki akiwa mikononi mwa Imamu Ali (a.s.),[52] na Imam Ali (a.s) ndiye aliye muosha bwana Mtume (s.a.w.w) akisaidiwa na watu wachche ambao baadhi yao ni; Fadhlu bin Abbas, Usama bin Zaid na wengineo. Alimkosha kwa nje ya kanzu yake yake kisha akampamba kama kawaida ya maiti wa Kiislamu apambwavyo, kumvisha sanda tayari kwa mazishi.[53] Kwa mapendekezo ya Imamu Ali (a.s),[54] watu waliruhusiwa kuingia nyumbani kwa bwana Mtume (s.a.w.w) kwa njia ya makundi, wakimsalia bila ya kumfuata imamu maalum katika sala hiyo, utaratibu huo uliendelea hadi siku iliyofuata. [55] Hata hivyo, kwa msisitizo wa Imam Ali (a.s), aliyekuwa na imani kuwa Mwenye Ezi Mungu huchukua roho za Mitume wake katika mahali bora patatifu, wote walikubaliana kuwa mwili wa Mtume uzikwa palepale alipoaga dunia, ambapo ni ndani ya nyumba yake mwenyewe, aliyo kuwa akiishi ndani yake yeye pamona na Aisha.[56] Kaburi la bwana Mtume (s.a.w.w) lilichimbwa na Abu Ubaida Jarraah akishirikiana na Zaidu bin Sahli.[57] Mazishi hayo yalikamilika kupitia mkono wa Imamu Ali (a.s) akisaidiwa na Fadhlu pamoja na Usama.[58]
Suala la Ukhalifa
Suala la mfululizo wa haki ya kumrithi Mtume na kuiongoza serikali ya Kiislamu baada ya kifo chake limekuwa mojawapo ya masuala nyeti na chanzo kikuu cha mgawanyiko miongoni mwa Waislamu.[59] Hivyo basi, matukio yaliyojiri kabla ya kifo cha bwana Mtume (s.a.w.w), na yale yaliotokea muda mfupi baada ya tokeo la kifo chake, yanachukuliwa kuwa ni miongoni mwa matokeo yenye umuhimu mkubwa na yaliyojaa siasa zilizo kifichoni na nyuma ya pazia, yamezungukwa na usiri na utata mwingi ndani yake.[60]
Kulingana na uchambuzi wa vyanzo vya Kishia, bwana Mtume alijitahidi kuwaweka mbali na mji wa Madina wale wote walikuwa na uchu wa ukhalifa. Alifanya hivyo ili kuthibitisha urithi wa Imamu Ali (a.s) unachukua nafasi yake kama alivyo wausia Wasilamu katika bayana za Ghadir.[61] Pia, bwana Mtume (s.a.w.w) alisisitiza umuhimu wa kuandika wasia wake,[62]akakumbusha mara kadhaa Hadithi ya Thaqalaini,[63] huku akimtambulisha wazi mrithi wake baada yake.[64]
Aidha, bwana Mtume (s.a.w.w) alimzuia Abu Bakar kusimamisha sala akiwa ni Imamu, ili isije kutumika baada ya kifo chake kama ni hoja ya kumtambua Abu Bakar kama ni khalifa baada ya Mtume (s.a.w.w). Hatua hizi mbali mbali zilibeba uzito wa kisiasa na kidini ndani yake, ili kuhakikisha mwendelezo wa uongozi wa Kiislamu baada ya kifo chake.[65] [Maelezo 2]
Kwa msingi wa ushahidi wa kihistoria, Masahaba wa bwana Mtume (s.a.w.w) waliamiliana na suala la urithi wa kushika nafasi ya ukhalifa kwa njia tafauti; Kundi moja lilidai kwamba bwana Mtume (s.a.w.w) hakuchagua mrithi wa kushika nafasi yake, kwa hiyo walijikusanya kwenye banda la Bani Sa’idah. Baada ya mzozo mkubwa baina yao, mwishowe wakamteua Abu Bakar kama ni khalifa wao.[66] Kundi jingine, ambalo wengi wao walikuwa ni kutoka ukoo wa Bani Hashim, walikuwa na imani thabiti ya kwamba; bwana Mtume (s.a.w.w) alimteua Ali (a.s) kuwa ni mrithi wa kushika nafasi yake baada ya kifo chake. Kwa msingi wa maneno ya bwana Mtume (s.a.w.w), walihisi kuwa ilikuwa ni haki yao kufuata uongozi wa Ali (a.s).
Hivyo kundi hili lilikataa kumkubali Abu Bakr kama kiongozi halali wa Kiislamu, na kwa muda fulani wakakataa kutoa kiapo cha utiifu juu yake. Wao waliamini kuwa maamuzi ya urithi wa uongozi wa Kiislamu ulikuwa tayari umeshatolewa na bwana Mtume mwenyewe, na kwamba Ali (a.s) ndiye mtu pekee wa kushika nafasi hiyo. Hivyo wao hawakutaka kuvunja ahadi hiyo ya urithi kwa kumpa mtu mwingine uongozi ambaye kwa mtazamo wao, hakuwa na haki ya kushika mamlaka hayo. Hii ilileta mgawanyiko mkubwa ndani ya jamii ya Kiislamu baada ya kifo cha Mtume (s.a.w.w), huku kundi la Bani Hashim likisalia na msimamo wao kwa muda fulani, hadi hali ya kisiasa na kijamii ilipowalazimu kufanya maamuzi mapya. [67]
Tofauti kati ya mawili makundi haya zilisababisha machafuko makubwa ndani ya mji wa Madina, na kupelekea kuvamiwa kwa nyumba ya Imamu Ali (a.s).[68] Kulingana na baadhi ya ripoti, Imamu Ali (a.s) hakukubali kutoa kiapo cha utiifu kwa ajili ya kumtambua Abu Bakar, na aliendelea na msimamo huo hadi baada ya kufariki kwa Fatima (a.s).[69] Kulingana na kitabu cha Salim bin Qais na vyanzo vengine, inasemekana kwamba; tokea zama za wa uhai wa bwana Mtume (s.a.w.w), kuna baadhi ya watu walio fanya makubaliano ya siri kuhusiana na suala la urithi wa uongozi baada ya Mtume (s.a.w.w), tukio ambalo katika vyanzo hivyo linajulikana kwa jina la Sahīfatu al-Mal’ūnati.[70]
Monografia
Kuna kazi kadhaa andishi zilizoandikwa makhususi juu ya suala la kifo cha bwana Mtume (s.a.w.w). Miongoni mwa kali hizo maalumu ni kama ifuatavyo:
- Wafaat al-Nabi (s.a.w.w), kitabu kilicho andikwa na Abdulwahid al-Mudhafar. Kitabu hichi kinajadili sababu za kifo, maradhi ya bwana Mtume (s.a.w.w), muda wa maradhi hayo, matokeo ya wakati wa kifo chake, maandalizi ya mazishi, na maombolezo baada ya kifo chake (s.a.w.w). [71]
- Wafaat al-Nabi Muhammad (s.a.w.w) kitabu kilichoandikwa na Sheikh Hussein al-Darazi al-Bahrani, kilichochapishwa na Taasisi ya Balagh huko Beirut.[72]
- Wafaat Rasulullah (s.a.w.w) wa Mawdhi’i' Qabrihi, kitabu kilichoandikwa na Nabil al-Hassani. Kitabu hichi kinazungumzia jinsi Mtume alivyofariki, mahali pa maziko yake, na tofauti zilizozuka miongoni mwa masahaba kuhusiana na suala hilo. [73]
- Wa Athlamat al-Madina: Wafaat al-Nabi (s.a.w.w), kitabu kilichoandikwa na Nizar al-Na'lawani al-Asqalani, kilicho chapishwa mano mwaka 1424 Hijiria na Dar al-Minhaj huko Beirut.[74]
- Salwatu al-Ka-īb bi-Wafaat al-Habib (s.a.w.w), kilichoandikwa na Ibn Nasir al-Din na kuchunguzwa na Saleh Yusuf Ma’atuq. Kitabu hichi kinazungumzia matokeo ya baada ya kifo cha bwana Mtume (s.a.w.w), maombolezo ya malaika, jinsi mwili wa wake (s.a.w.w) ulivyooshwa na Ali bin Abi Talib, na pia ndani yake kuna maelezo juu ya watoto na wake zake Mtume (s.a.w.w).[75]
Maelezo
- ↑ فوجهوا الى منزله فهجموا عليه، و أحرقوا بابه، و استخرجوه منه كرها، و ضغطوا سيّدة النساء بالباب حتى اسقطت (محسنا) ; Watu hao wakelekea kwenye nyumba yake, wakaivamia na kuchoma mlango wake, kisha wakamtoa kwa nguvu, wakamkandamiza mbora wa wanawake kupitia mlango wa nyumba yake hadi akaharibu mimba ya mwanawe aliyekuwa tumbomi mwake (Muhsin)
- ↑ Aliingia msikitini akiwa katika hali hii akiwa ni mgonjwa mno, wakaithamini hali hiyo, Mtume wa Mwenye Ezi Mungu (s.a.w.w) naye akajitokeza na kumvuta Abu Bakar na kumweka nyuma yake kutoka katika mihrabu yake, Abu Bakar naye akasimama yeye pamoja na kundi lake nyuma ya Mtume (s.a.w.w), watu nao wakakaribia na kusali nyuma ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w).
Rejea
- ↑ Sheikh Mufid, al-Irshad, juz. 1, uk. 182, 1410 H, Tabari, Tarikh al-Tabari, juz. 3, uk. 200, 1387 H.
- ↑ Sheikh Mufid, al-Irshad, juz. 1, uk. 182, 1413 H, Tabari, Tarikh al-Tabari, juz. 3, uk. 195, 1387 H.
- ↑ Ja'fariyan, Sire Rasul Khuda, uk. 682, 1383 S.
- ↑ Sheikh Mufid, al-Irshad, juz. 1, uk. 189, 1413 H, Sheikh Tusi, Tahzib al-Ahkam, juz. 6, uk. 2, 1407 H.
- ↑ Qummi, Muntaha al-Amal, juz. 1, uk. 249, 1379 S.
- ↑ Ja'fariyan, Sire Rasul Khuda, uk. 682, 1383 S.
- ↑ Ja'fariyan, Sire Rasul Khuda, uk. 682, 1383 S.
- ↑ «Maombolezo ya watumishi wa kaburi la Imam Ali (a.s) katika mnasaba wa tarehe 28 Safar.",
- ↑ Ibnu Kathir, al-Bidayah wa al-Nihayah, juz. 5, uk. 254, 1407 H, Suhaili, al-raudh al-Unuf, juz. 7, uk. 579,1412 H.
- ↑ Tabari, Tarikh al-Tabari, juz. 3, uk. 200, 1387 H, Suhaili, al-raudh al-Unuf, juz. 7, uk. 579,1412 H.
- ↑ Ibnu Kathir, al-Bidayah wa al-Nihayah, juz. 5, uk. 276, 1407 H, Waqidi, al-Maghazi li al-Waqidi, juz. 3, uk. 1089, 1409 H, Khalifah bin Khayat, Tarikh Khalifah bin Khayat, uk. 46, 1415 Mas'udi, Muruj al-zahab, juz. 2, UK. 280, 1409 H.
- ↑ Tari Jalil, Taammuli dar Tarikh Wafat Peyambar, uk. 12.
- ↑ Qummi, Muntaha al-Amal, juz. 1, uk. 249, 1379 S.
- ↑ Qummi, Muntaha al-Amal, juz. 1, uk. 249, 1379 S.
- ↑ Kulaini, al-Kafi, juz. 4, uk. 439, 1362 H, Tabari, al-Mustarshid, uk. 115, 1415 H.
- ↑ Ibnu Hisham, al-Sirat al-Nabawiyah, Dar al-Maarifat, juz. 2, uk. 649-666.
- ↑ Ibnu Sa'ad, al-Tabaqat al-Kubra, juz. 2, uk. 129-253, 1410 H.
- ↑ Ya'qubi, Tarikh Ya'qubi, Dar Sadir, juz. 2, uk. 113-115.
- ↑ Sheikh Mufid, al-Irshad, juz. 1, uk. 179-192, 1413 H.
- ↑ 'Amali, al-Sahih min Sirat al-Nabi al-A'dham, juz. 33, uk. 125-355 va 5-230, 1375 S.
- ↑ Shahidi, Tarikh Tahlili Eslam, uk. 106-107, 1390 S.
- ↑ Tabari, Tarikh Umam wa al-Muluk, juz. 3, uk. 201-203, 1387 S.
- ↑ Ibnu Qutaibah, al-Imamah wa al-Siyasah, juz. 1, uk. 30-31, 1410 H.
- ↑ Mas'udi, Ithbat al-Wasiyah, uk. 146, 1384 S.
- ↑ Mahdi, al-Hujum, uk. 221-356, 1425 H.
- ↑ Shahidi, Tarikh Tahlili Eslam, uk. 106-107, 1390.
- ↑ Tazama: Tabatabai, Shieh dar Eslam, uk. 28, 1378 S.
- ↑ Marasim Salruz Rehlat Peyambar Akram dar Kharij az Keshwar, Tovuti mehernews.com.
- ↑ Tazama: Harakat va Tajammu Dastejat Azadari dar Salruz Rehlat Peyambar Akram dar Bushhar, Tovuti tasnimnews.com.
- ↑ 'Amali, al-Sahih min Sirat al-Nabi al-A'dham, juz. 33, uk. 141-158, 1385 S.
- ↑ Ibnu Abi al-Hadid, Sharh Nahj al-Balaghah, juz. 10, uk. 266, 1404 H.
- ↑ Kuleini, al-Kafi, juz. 6, uk. 315, hadith no 3, 1407 H.
- ↑ Safar, Basair al-Darajat, uk. 503, 1404 H.
- ↑ Ibnu Sa'ad, al-Tabaqat al-Kubra, juz. 2, uk. 156-155, 1410 H.
- ↑ Sheikh Mufid, al-Muqni'ah, uk. 456, 1413 H.
- ↑ Tusi, Tahdhib al-Ahkam, juz. 6, uk. 2, 1407 H.
- ↑ Hilli, Muntaha al-Matlab, juz. 13, uk. 259, 1412 H.
- ↑ Bukhari, Sahih al-Bukhari, juz. 6, uk. 9, hadith no. 4428, 1422 H.
- ↑ Al-darami, Sunan al-Darami, juz. 1, uk. 207, hadith no. 68, 1412 H.
- ↑ Hakim Neishaburi, al-Mustadrak, juz. 3, uk. 61, hadith no. 4395, 1411 H.
- ↑ 'Amali, al-Sahih min Sirat al-Nabi al-A'dham, juz. 33, uk. 141-158, 1385 S.
- ↑ 'Amali, al-Sahih min Sirat al-Nabi al-A'dham, juz. 33, uk. 159, 1385 S.
- ↑ 'Amali, al-Sahih min Sirat al-Nabi al-A'dham, juz. 33, uk. 159-193, 1385 S.
- ↑ 'Ayashi, Kitab al-Tafsir, juz. 1, uk. 200, 1380 S.
- ↑ Ibnu Abi al-Hadid, Sharh Nahj al-Balaghah, juz. 13, uk. 32, 1404 H, Najmi, Dastan Durugin Darbare Peyambar A'dham, uk. 120.
- ↑ 'Amali, al-Sahih min Sirat al-Nabi al-A'dham, juz. 32, uk. 130, 1385 S.
- ↑ Bukhari, Sahih al-Bukhari, juz. 6, uk. 14,1422 H, hadith no. 4458, & juz. 7, uk. 127, hadith no. 5712, Ibnu Sa'ad, al-Tabaqat al-Kubra, juz. 2, uk. 181, 1410 H.
- ↑ Najmi, Dastan Durugin Darbare Peyambar Akram, uk. 120; Najmi, Adhwa ala al-Sahihain, Muasese al-Maarif al-Eslamiya S uk. 264.
- ↑ Ibnu Sa'ad, al-Tabaqat al-Kubra, juz. 2, uk, 238, 1410 H.
- ↑ Ibnu Sa'ad, al-Tabaqat al-Kubra, juz. 2, uk, 237-238, 1410 H.
- ↑ Sayid Radhi, Nahj al-Balaghah, uk. 311, 1414 H khotbah no. 197; Makarim Shirazi, Nahj al-Balaghah ba Tarjumeh Farsi Ravan, uk. 485, 1384 S.
- ↑ Ibnu Sa'ad, al-Tabaqat al-Kubra, juz. 2, uk, 201, 1410 H.
- ↑ Ibnu Sa'ad, al-Tabaqat al-Kubra, juz. 2, uk, 212 va 214, 1410 H; Ibnu Hisham, al-Sirat al-Nabawiyah, Daru al-Maarifah, juz. 2, uk. 263-662.
- ↑ Sheikh Mufid, al-Irshad, juz. 1, uk. 188, 1413 H.
- ↑ Ibnu Sa'ad, al-Tabaqat al-Kubra, juz. 2, uk. 220, 1410 H; Ya'qubi, Tarikh Ya'qubi, juz. 2, uk. 114.
- ↑ Irbili, Kashf al-Ghummah, juz. 1, uk. 19, 1381 H.
- ↑ Ibnu Hisham, al-Sirat al-Nabawiyah, Daru al-Maarifah, juz. 2, uk. 263.
- ↑ Ibnu Sa'ad, al-Tabaqat al-Kubra, juz. 2, uk. 229, 1410 H
- ↑ Madelung, Janeshini Hazrat Muhammad, uk. 13, 1377 S.
- ↑ Ghulami, Pas az Ghurub, uk. 21, 1388 S.
- ↑ Sheikh Mufid, al-Irshad, juz. 1, uk. 180, 1413 H.
- ↑ Bukhari, Sahih al-Bukhari, juz. 6, uk. 9, 1422 H, hadith no. 4432.
- ↑ Sheikh Mufid, al-Amali, uk. 135, 1413 H; Ibnu Hajar Haithami, al-Sawaiq al-Muhriqah, juz. 2, uk. 438 & 440, 1417 H.
- ↑ Sheikh Mufid, al-Irshad, juz. 1, uk. 185,1413 H; Dhahabi, Tarikh al-Islam, juz. 11, uk. 224, 1413 H; Ibnu Kathir, al-Bidayah wa al-Nihayah, juz. 7, uk. 359, 1407 H.
- ↑ Ja'fariyan, Sire Rasul Khuda, UK. 679, 1383 S; Kitab Sulaim bin Qais, uk. 420, 1378 S.
- ↑ Ibnu Qutaibah, al-Imamah wa al-Siyasah, juz. 1, uk. 22, 1410 H; Ibnu Athir, al-Kamil fi al-Tarikh, juz. 2, uk. 327.
- ↑ Ya'qubi, Tarikh al-Ya'qubi, juz. 2, uk. 124; Askari, Saqifah, Barresi Nahve Shikr giri hukumat pas az peyombar, uk. 99, 1387 S.
- ↑ Ya'qubi, Tarikh al-Ya'qubi, juz. 2, uk. 124; Askari, Saqifah, Barresi Nahve Shikr giri hukumat pas az peyombar, uk. 99, 1387 S.
- ↑ Ibnu Qutaibah, al-Imamah wa al-Siyasah, juz. 1, uk. 30-31, 1413 H.
- ↑ Sulaim bin Qais, Asrar Ali Muhammad, uk. 269, 1378 S, Qummi, Safinah al-Bihar, juz. 5, uk. 56, 1414 H, Sayid Ibnu Tawus, Tarf min al-Anba wa al-Manaqib, uk. 564; Sheikh Mufid, al-Fushul al-Mukhtarah, juz. 1, uk. 232, 1413 H.
- ↑ Al-Mudhaffar, A'bdulwahid, uk. 3, 1386 S.
- ↑ Al-Darazi, Wafat an-Nabi, uk. 2, 1428 H.
- ↑ [Wafat Rasulullah (S.a.w.w) Wa Maudhi’u Qabrihi».Tovuti Ghbook.ir.
- ↑ Al-Na'lawani, Wafat an-Nabi, uk. 2, 1424 H.
- ↑ Ibnu Nasir ad-Din, Salwat Al-Kaib, Daru al-Buhuth Li Darasati al-Islamiyah, uk. 211, 200 M.
Vyanzo
- Ibnu Abi al-Hadid, Abdul Hadmid bin Hibatullah. Sharh Nahj al-Balaghah. Mhakiki na Mhariri: Ibrahim, Muhammad Abu al-Fadhl. Qom: Maktaba Ayatullah Mar'ashi Najafi, juz. 1, 1404 H.
- Ibnu Athir, Ali bin Muhammad. al-Kamil fi al-Tarikh. Beirut: Dar Sadir, Bita.
- Ibnu Hajar Haitami, Ahmad bin Muhammad. al-Sawaiq al-Muhriqah ala Ahli al-Rafdh wa al-Dhalal wa al-Zinndiqah. Beirut: Muasese al-Risalah, juz. 1, 1417 H.
- Ibnu Sa'ad, Muhammad. al-Tabaqat al-Kubra. Tahkiki: Ata, Muhammad Abdul Qadir. Beirut: Dar al-Kutub al-Ilmiah, juz. 1, 1410 H.
- Ibnu Qutaibah, Abdullah bin Muslim. al-Imamah wa al-Siyasah. Mhakiki: Ali Shiri. Beirut: Dar al-Adhwa, 1410 H.
- Ibnu Kathir Dimashqi, Ismail bin Umar. al-Bidayah wa al-Nihayah. Beirut: Dar al-Fikr, 1407 H.
- Ibnu Hisham, Abdul Malik. al-Sirah al-Nabawiyah. Tahkiki: Musthafa al-Saqa, Ibrahim al-Abyar, Abdul Hafidh Shalbi. Beirut: Dar al-Ma'rifah, juz. 1, Bita.
- Ibnu Nasir ad-Din. Silwah al-Kaib bi Wafat al-Habib. Emirat: Dar al-Buhuth li al-Dirasat al-Islamiah, Bita.
- Irbili, Ali bin Isa. Kashf al-Ghummah. Tahkiki: Sayid Hashim Rasuli Mahalati. Tabriz: Nashir Bani Hashim, juz. 1, 1381 H.
- Bukhari, Muhammad bin Ismail. Sahih al-Bukhari. Tahkiki: An-Nasir, Muhammad Zuhair. Damaskus: Dar Tuq al-Najah, juz. 1, 1422 H.
- Tari Jalil. Ta'ammuli dar Tarikh Wafat Peyambar. Dalam majalah Tarikh Islam, juz. 5, Bahar, 1380 S.
- Ja'fariyan, Rasul. Sire Rasul Khuda. Dalil Ma, Qom: 1383 S.
- Hakim Neishaburi. Muhammad bin Abdullah. al-Mustadrak ala al-Sahihain. Tahkik: Abdul Qadir Musthafa. Beirut: Dar al-Kutub al-Ilmiaya, juz. 1, 1411 H.
- Harakat va Tajammu' Dastejat Azadari dar Salruz Rehlat Peyambar Akram dar Bushahr. Tovuti Tasnim News, Tarikh Darj Matalib: 5 Aban 1398 S, Tarikh Bazdid 1 Murdad 1403 S.
- Hilli, Hasan bin Yusuf. Muntaha al-Matlab fi Tahqiq al-Mazhab. Mashhad: Majma' al-Buhuth al-Islamiaya, 1412 H.
- Khalifah bin Khayat. Tarikh Khalifah bin Khayat. Tahqiq: Najib Fawaz. Beirut: dar al-Kutub al-Ilmiaya, 1415 H.
- Darami, Abdullah bin Abdul Rahman. Sunan al-Darami. Tahqiq: Husain Salim al-Darani. Saudi Arabia: Dar al-Mughni lilnashir wa al-Tauzi', juz. 1, 1412 H.
- Darazi al-Bahrani, Sheikh Husain. Wafat an-Nabi saw. Beirut: Muasese Balagh, juz. 1, 1428 H.
- Dhahabi, Muhammad bin Ahmad, Tarikh al-Islam. Tahqiq: Umar bin Abdu al-Salam. Beirut: Dar al-Kitab al-Arabi, juz. 2, 1413 H.
- Salim Ibn Qays, Kitab Salim ibn Qays, Tahqiq: Muhammad Baqir Ansari Zanjani, Qom, Nashar al-Hadi, al-Tab'at al-Awali: 1420 H/ 1378 S.
- Suhaili, Abdul Rahman. al-Raudh al-Unuf fi Sharh al-Sirat al-Nabawiyah. Beirut: Dar al-Turath al-Arabi, juz. 1, 1412 H.
- Sayid Ridha Muhammad Ibn Hussein, Nahju al-balagha, Tahqiq: Sabahi Saleh, Qom, juz 1, 1414 H.
- Shahidi, Sayid Ja'far. Tarikh Tahlili Islam. Tehran: Markaz Nashr Daneshgahi, 1390 S.
- Sheikh Tusi, Muhammad bin Hasan. Tahdhib al-Ahkam. Mhariri: Muhammad Akhundi. Tehran: Dar al-Kutub al-Islamiya, juz. 4, 1407 H.
- Sheikh Mufid, muhammad bin Muhammad. al-Amali. Tahqiq: Hussein Ustad Vali, Ali Akbar Ghafari, Qom, Kongres Sheikh Mufid, juz. 1, 1413 H.
- Sheikh Mufid, muhammad bin Muhammad. al-Muqni'ah. Qom: Kongres Jahani Hezar Sheikh Mufid, juz. 1, 1413 H.
- Safar, Muhammad bin Hasan. Basair al-Darajat. Qom: kitabkhane Ayatullah Mar'ashi Najafi, juz. 2, 1404 H.
- Tabari, Muhammad bin Jarir. Tarikh Tabari (tarikh al-Umam wa al-Muluk). Tahqiq: Ibrahim, Muhammad Abul Fadhl. Beirut: Dar al-Turath, juz. 2 1387 H.
- Tabatabai, Sayid Muhammad Hussein. Shieh dar Islam. Qom: Jamiah Mudarrisin hauzah Ilmiah Qom, Daftar Intisharat Islami, 1378 S.
- Tabari, Muhammad bin Jarir bin Rustam.al-Mustarshid fi Imamat Amir al-Mu'minin Ali bin Abi Thalib. Tahqiq: Ahmad Mahmudi. Tehran: Muasese al-Thaqafah al-Islamiah Lakushanpur, 1415 H.
- 'Amili, Sayid Ja'far Murtadha. al-Sahih min Sirat al-Nabi al-A'zham. Qom: Dar al-Hadith, juz. 1, 1385 S.
- Askari, Sayid Murtadha. Saqifah. -Barresi nahwey Shiklgiri Hukumat pas az Rehlat Peyambar, Mahdi Dashti. Qom: Daneshgah Usuluddin, 1387 HS.
- 'Ayashi, Muhammad bin Mas'ud. Tafsir al-'Ayashi. Tehran: al-Matba't Ilmiaya, juz. 1, 1380 H.
- Qummi, Sheikh Abbas. Muntaha al-Amal. Qom: Dalil Ma, juz. 1, 1379 HS.
- Kulaini, Muhammad bin Ya'qub. al-Kafi. Mhakiki na Mhariri: Ghafari, Ali Akbar Akhundi, Muhammad. Tehran: Dar al-Kutub al-Islamiaya, juz. 4, 1407 H.
- Marasim Salruz Rehlat Peyambar Akram dar Kharij az Keshwar. Tovuti Mehr News, Tarikh Nashr: 22 Azar 1394 S, Tarikh Bazdid: 6 Dey 1402 HS.
- Madelung, Wilferd. Janeshini Hazrat Muhammad. Pajuhesh Piramune khilafah Nakhstain, Tarjume: Ahmad namai, Jawad Qasimi, Muhammad Jawad Mahdi Va Haidar Ridha Dhabit. Masyad: Buniyad Pajuheshha Islami Astan Quds,Mashhad, 1377 S.
- Mas'udi, Ali bin Husain. Muruj al-Dhahab wa Ma'adin al-Jauhar. Tahqiq: As'ad Daghir Yusuf. Qom: Muasese Dar al-Hijrah, 1409 H.
- Al-Muzhaffar, Abdul Wahid. Wafat an-Nabi. Qom: Intesharat al-Maktaba al-Haidariyah, juz. 1, 1386 S.
- Mahdi, Abdu al-Zahra. al-Hujum ala bait Fatimah. Tehran: Intesharat Barg Rezvan, 1425 H.
- Najmi, Muhammad Sadiq. Dastani Durugin Darbare Peyambar A'zham. Faslname Miqat Haj, juz. 58, Zemestan 1385 S.
- Al-Na'lawi al-Asqalani, Nezar. Wafat an-Nabi wa Adhlamat al-Madinah. Beirut: Dar al-Minhaj, 1443 H.
- Waqidi, Muhammad bin Umar. al-Magazi li al-Waqidi. Marzeden Jones. Beirut: Muasese al-A'lami li al-Mathbu'at, 1409 H.
- [Wafat Rasulullah (S.a.w.w) Wa Maudhi’u Qabrihi» Bazar Kitab Qaimiye, Tarikh Bazdid: 17 Dei 1402 S.
- Ya'qubi, Ahmad bin Abi Ya'qub. Tarikh al-Ya'qubi. Beirut: Dar Sadir, juz. 1, Bita.
- «Maombolezo ya watumishi wa kaburi la Imam Ali (a.s) katika mnasaba wa tarehe 28 Safar.". Tovuti Shafaqna, Tarikh Darj Matalib: 14 Sep 2023 M, Tarikh Bazdid: 22 Jun 2024 M.