Nyumba ya Fatima (a.s)

Kutoka wikishia
Mlango wa kuingilia Masjid al-Nabii ambapo kaburi la Mtume (s.a.w.w.) na nyumba ya Fatima (a.s) ilipo kuwepo.

Nyumba ya Bibi Fatima (a.s) (Kiarabu: دار السيدة فاطمة (ع)) ilikuwa imeungana na Masjid al-Nabi (Msikiti wa Mtume) na palikuwa mahali walipokuwa wakiishi Imam Ali (a.s) na Fatima (a.s). Fadhila zilizoorodheshwa kuhusiana na nyumba ya Fatima ni kwamba, Mwenyezi Mungu aliamuru milango yote ya nyumba zilizounganishwa na Msikiti wa Mtume ifungwe katika tukio la Saddu-al-Abab, (kufungwa milango) na akaruhusu tu mlango wa nyumba hii ya msikiti kubaki wazi.

Imekuja katika hadithi iliyonukuliwa kutoka kwa Imam Sadiq (a.s) ya kwamba amesema, kuswali katika nyumba hii kuna fadhila zaidi kuliko kuswali katika Rawdhat al-Nabi (eneo ambalo ni baina ya mimbari na kaburi la Mtume). Nyumba hii iliharibiwa wakati wa utawala wa Bani Umayya kwa ajili ya kupanua Masjid al-Nabi na sasa iko pamoja kwenye chumba ambacho amezikwa Mtume (s.a.w.w). Wanachuoni wengi wa Shia wanaamini kwamba kaburi la Fatima liko katika nyumba yake.

Baadhi wameichukulia nyumba ya Fatima (a.s) ambayo ilishambuliwa katika tukio la hujuma dhidi ya nyumba ya Fatima na kumjeruhi binti huyo wa Mtume kuwa ni nyumba ya Imam Ali (a.s) iliyoko katika mtaa wa Bani Hashim. Watafiti hawa wametaja sababu na ushahidi wa kuwepo kwa nyumba hii na kutokea tukio hili katika mtaa wa Bani Hashm katika nyumba hii.

Nafasi ya nyumba ya Fatima kwa Waislamu na fadhila zake

Nyumba ya Fatima ni ashirio la makazi ya Fatima huko Madina, ambapo katika hadithi zilizonukuliwa na Waislamu wa madhehebu ya Shia na Sunni na vyanzo vya kihistoria kumenukuliwa fadhila yake [1] na tukio la kushambuliwa kwake [2]. Pia, baadhi ya wanazuoni wa Kishia wanaona kuwa ni Mahali alipozikwa Bibi Fatima (a.s). [3]

Nyumba ya Fatima palikuwa mahali walipozaliwa watoto wake [4] na kwa mujibu wa hadithi, ni mahali alipozaliwa Imam Sajjad (a.s) [5]. Kwa mujibu wa riwaya iliyotajwa katika kitabu cha Al-Kafi, Imamu Swadiq (a.s) aliona kuswali katika nyumba ya Fatima (a.s) ni bora kuliko kuswali katika Rawdhat al-Nabi. [6] Pia, Imamu Jawadi (a.s) alikuwa akiswali kila siku katika nyumba hiyo ya Fatima (sa). [7]

Kadhalika sambamba na siku za Fatimiyya katika baadhi ya miji ya Iran hususan Qom, hufanyika maonyesho yanayojulikana kwa jina la mitaa ya Bani Hashim ambapo watu wote huruhusiwa kutembelea na kuona maonyesho hayo ambamo ndani yake hujengwa nyumba ya Fatima kwa jina la mitaa ya Madari. [8]

Takwa la Mtume na kuhamishwa makazi ya Fatima (a.s)

Mwanahistoria wa Kisunni Ibn Sa'ad (aliyefariki dunia: 230 AH) ameandika katika kitabu chake cha Tabaqat al-Kubra akinukuu kutoka kwa Imam Baqir (a.s) kwamba, Imam Ali (a.s) baada ya kumuoa Fatima (a.s), alitayarisha nyumba ambayo ilikuwa mbali kidogo na nyumba ya Mtume. Mtume (s.a.w.w) alisema kwamba anataka binti yake aishi karibu na nyumba yake. Fatima (a.s) alimuomba Mtume (s.a.w.w) aongee na Haritha bin Nu'man ili waweze kuishi katika nyumba yake. [9] Mtume (s.a.w.w) alisema kwamba aliona haya kumwambia Haritha kuhusu hili; kwa sababu tayari Haritha alimpa baadhi ya nyumba zake, na kwa sababu yake, alilazimika kuhama kutoka chumba kimoja hadi kingine ili wakeze Mtume waishi humo. [10] Haritha alipata habari ya jambo hilo na akatoa nyumba yake na kumpa zawadi Mtume (s.a.w.w) na kusema, kukubaliwa na kuchukuliwa mali yake na Mtume kunapendeza zaidi kuliko kutokubaliwa. [11]

Kwa mujibu wa baadhi ya vyanzo vya Kishia, Mtume (s.a.w.w) alimtaka Imam Ali (a.s.) kuandaa nyumba ya kwenda kuishi baada ya kufunga ndoa. Ali (a.s) alisema kwamba hakuna nyumba iliyo karibu na nyumba ya Mtume isipokuwa nyumba ya Haritha bin Nu'man. Mtume akasema, Haritha amempa baadhi ya nyumba zake na anaona haya kumwambia. Haritha akapata habari hiyo na akaja kwa Mtume na kumpa nyumba yake. Kwa muktadha huo, Ali (a.s) na Fatima (a.s) walikwenda na kuishi katika nyumba ya Haritha ambayo alimpatia zawadi Mtume (s.a.w.w). [12]

Nyumba pekee iliyokuwa na mlango wa kuingilia msikitini

Makala asili: Saddu al-Abwab

Nyumba ya Fatima ilikuwa upande wa mashariki mwa Masjid al-Nabi na katikati ya vyumba vingine vya Mtume (s.a.w.w). [13] Nyumba hii ilikuwa na milango miwili: Mlango mmoja ulifunguliwa kwa ndani ya msikiti na mlango mwingine kwa nje. [14] Kimsingi ni kuwa, katika kuutekelezwa amri ya Mwenyezi Mungu ya kufungwa milango yote iliyokuwa ikifungukia katika msikiti wa Mtume, Mtume aliamriisha kufungwa milango yote isipokuwa mlango wa nyumba hii ya Fatima (a.s). [15] Tukio hili la Saddu al-Abwab linahesabiwa kuwa moja ya fadhila za kipekee za Imamu Ali bin Abi Twalib (a.s). [16]

Mahali ilipo kwepo nyumba ya Bibi Fatima (a.s) katika Masjid al-Nabii

Nyumba ya Fatima (a.s) ilikuwa nyuma ya nyumba ya Mtume (chumba cha Aisha). [17] Kulikuwa na upenyo baina ya nyumba hizi mbili [18] ambapo Mtume alikuwa akiutumia kumjulia hali binti yake. [19] Usiku mmoja kulitokea mabishano baina ya Fatima na Aisha, mke wa Mtume (s.a.w.w) ambayo yalipelekea Fatima kuudhika na kwa takwa la Fatima (a.s), Mtume akaufunga upenyo huo. [20]

Tukio la Kushambuliwa nyumba ya Fatima

Makala asili: Tukio la kushambuliwa nyumba ya Fatima (a.s)

Kwa mujibu wa vyanzo vya Shia na Sunni, baada ya kifo cha Mtume (s.a.w.w) na tukio la Saqifa, baadhi ya Masahaba walivamia nyumbani kwa Fatima ili kuchukua baia na kiapo cha utii kutoka kwa Imam Ali (a.s) na watu wengine waliokataa kutoa kiapo cha utii kwa Abu Bakr na kuketi na kukusanyika katika nyumba hiyo. [21] Kulingana na vyanzo vya Shia, mlango wa nyumba hiyo ulichomwa moto katika tukio hili. Katika tukio la kushambuliwa nyumba ya Fatima, mlango wa nyumba ya Fatma ulichomwa moto, Fatma alijeruhiwa na kupelekea pia ujauzito wake wa mimba ya Muhsin kuharibika, [23] na baada ya muda usiokuwa mrefu, Bibi Fatima akafa shahidi. [24]

Ni nyumba ipi iliyoshambuliwa?

Baadhi ya watafiti wanaamini kwamba, kushambuliwa na kuvamiwa nyumba ya Fatima hakukufanyika karibu na msikiti, bali nyumba iliyoshambuliwa ilikuwa mbali na msikiti. [25] Kulingana na Muhammad Sadiq Najmi (aliyefariki dunia: 1390) katika kitabu cha Tarikh Haram Aimeh Baqi, (Historia ya Haram ya Maimamu Baqi'i) baadhi ya ripoti za kihistoria zinathibitisha nadharia hii. Miongoni mwao ni riwaya kwamba Ali (a.s.) alipopelekwa msikitini kutoa kiapo cha utii kwa Abu Bakr, watu walikuwa wakitazama matukio haya katika mitaa ya Madina. [26] Riwaya hii imo katika kitabu cha Al-Saqifah wa Fadak cha Ahmad bin Abdulaziz Jowhari Basri (aliaga dunia: 323 Hijiria). [27] Pia wanasema kwamba, nyumba hii ilikuwa upande wa mashariki ya Masjid al-Nabi, nyuma ya Baqi na kando ya nyumba ya Abu Ayyub Ansari, na ilijumuisha ua, ghala, vyumba kadhaa na mlango mkubwa wa mbao. [28]

Je Fatima amezikwa katika nyumba yake?

Makala asili: Mahali alipozikwa Bibi Fatima (a.s)

Kulingana na wanazuoni wa Kishia ni kwamba, haiwezekani kubainisha kwa uhakika eneo lilipo kaburi la Fatima. [33] Hata hivyo, wanazuoni wa Kishia wamezungumzia maeneo kadhaa ambayo wanasema kuna uwezekano Fatima akawa amezikwa katika moja ya maeneo hayo. Kwa mujibu wa Ismail Ansari Zanjani katika al-Masua'a al-Kubra An Fatima al-Zahra (Ensaiklopidia Kubwa Kuhusu Fatima) ni kwamba, wanazuoni wengi wa Kishia wamechukulia kwamba kuna uwezekano Fatima akwa amezikwa nyumbani kwake [34]. Ayatulla Makarim Shirazi anasema kuwa maneno ya ((النَّازِلَةِ فِي جِوَارِكَ)) yaani anayeshuka jirani yako (karibu na wewe) yaliyosemwa na Imamu Ali (a.s) wakati akimzika Fatima]] yanayotumiwa kama hoja ya kuonyesha kuwa kaburi la Bibi Fatima (a.s) liko jirani na kaburi la Mtume (s.a.w.w) yanaipa nguvu dhana na nadharia ya watu wanaosema kuwa, Fatima amezikwa katika nyumba yake. [35]

Nyumba ya Fatima yawa ndani ya dharih ya Mtume wakati wa upanuzi wa Masjid al-Nabi

Nyumba ya Fatima iliharibiwa wakati wa utawala wa Abdul Malik bin Marwan (utawala: 65-86 AH) [36] au Walid bin Abdul Malik (utawala: 86 AH-96 AH) [37] ili kupanua msikiti. Chumba hicho kikawa pamoja na chumba alichokuwa amezikiwa Mtume katika dharih. [38] Dharih hii ilifunguliwa mwaka 1397 Hijiria Shamsia kwa ajili ya kutembelea Rais wa Jamhuri ya Chechnya. [39]