Tukio la kushambuliwa nyumba ya Bibi Fatma (a.s)

Kutoka wikishia
Makala hii inahusiana na tukio la kihistoria la kushambuliwa nyumba ya Bibi Fatma (a.s). Ili kufahamu matukio yanayohusiana na tukio hili, rejea maudhui ya kufa shahidi Bibi Fatma (a.s).

Tukio la kuvamiwa na kushambuliwa nyumba ya Bibi Fatma Zahra (a.s) (Kiarabu: واقعة الهجوم على بيت الزهراء (ع)) linaashiria kwenda Omar bin al-Khattab na watu aliombatana nao mbele ya nyumba ya Fatma binti ya Mtume (s.a.w.w) kwa ajili ya kumtaka Ali ibn Abi Twalib (a.s) na watu wengine waliokuwa katika nyumba hiyo watoe baia na kiapo cha utii kwa Abu Bakr. Kwa mujibu wa nukuu kutoka katika vyanzo vya Kishia na Kisuni, tukio hili lilitokea baada ya kuaga dunia Bwana Mtume (s.a.w.w) (28 Mfunguo Tano Safar). Omar ibn al-Khattab alitishia kwamba, kama watu walioko ndani ya nyumba hiyo hawatatoka nje, basi ataichoma moto nyumba hiyo.

Imekuja katika kitabu cha Sulaym ibn Qays, Ithbat al-Wasiyah na Tafsir Ayyashi miongoni mwa vitabu na vyanzo vya Mashia ya kwamba, katika tukio hilo la uvamizi na shambulio, mlango wa nyumba ya Bibi Fatma ulivunjwa na kuchomwa moto. Ujauzito wa Bibi Fatma (wa kichanga Muhsin) ukaharibika na baada ya muda bibi Fatma akafa shahidi. Vitabu na vyanzo vya Waislamu wa madhehebu ya Kisuni vinakana tukio la kuvunjwa mlango na kuchomwa moto nyumba ya Bibi Fatma (a.s) na kujeruhiwa binti ya Mtume na vinawatuhumu wapokezi wake kuwa ni marafidha. (Mashia huitwa kwa jina hili na maadui wa Ushia)

Kuhusiana na sababu zilizopelekea kutokea tukio hilo inaelezwa kuwa, Abu Bakr alikuwa akihitajia baia na kiapo cha utiifu cha Imam Ali (a.s) ili kwa njia hiyo aweze kuimarisha nafasi na Ukhalifa wake, kwani angeweza kujigamba kwamba, hata Ali amempa kiapo cha utii, hivyo utawala wake una uungaji mkono hata wa mtu kama Ali. Muhammad-Hadi Yusuf Gharawi msomi na mtaalamu wa historia ya Kiislamu anasema: Tukio hili lilitokea takribani siku 50 baada ya kufariki dunia Bwana Mtume (s.a.w.w).

Kwa mujibu wa nukuu ya kitabu cha Sulaym na al-Imama wa al-Siyasa ni kwamba, Bibi Fatma wakati alipokutana na Abu Bakr na Omar sambamba na kuwakumbusha Hadithi ya Bidh-'ah (pande la nyama) aliwashuhudishia Mwenyezi Mungu wawili hao kwamba, wamemuudhi. Imekuja katika vitabu vya Ahlu-sunna kwamba, Abu Bakr alionyesha majuto mwishoni mwa uhai wake kuhusiana na baadhi ya mambo aliyoyafanya ambapo alinukuliwa akisema: Laiti asingetoa amri ya kuvamiwa nyumba ya Bibi Fatma.

Umuhimu

Maombolezo ya wafuasi wa Ahlul-bayt (a.s) katika masiku ya Fatimiyyah

Tukio la kushambuliwa na kuvamiwa nyumba ya Bibi Fatma lilitokea baada ya tukio la Saqifa na lengo lilikuwa ni kuchukua kiapo cha utii kutoka kwa Imam Ali (a.s) kwa ajili ya ukhalifa na uongozi wa Abu Bakr, [1] na kupelekea Kufariki kishahidi kwa bibi Fatima (s.a). [2] Hili ni moja ya matukio ambayo yana taathira mno katika uhusino wa Mashia na Masuni. Baadhi ya vyanzo vya mwanzo vya Kishia kama kitabu cha Sulaym ibn Qays, Ithbat al-Wasiyah, Tafsir Ayyashi na Dalail al-Aimah vimeelezea tukio hilo la uvamizi na shambulio dhidi ya nyumba ya Bibi Fatma. [3] Mkabala na mtazamo huo, vitabu na vyanzo vya Waislamu wa madhehebu ya Kisuni vinakana tukio la kuvunjwa na kuchomwa moto mlango wa nyumba ya Bibi Fatma (a.s) na kuharibika mimba na ujauzito aliokuwa nao wa Muhsin na vinawataja wapokezi wake kuwa ni marafidha na watu wasioaminika.

Katika kumbukumbu ya kufa shahidi Bibi Fatma, Mashia wamekitaja kipindi hiki hiki kuwa ni Ayyam Fatimiyyah ambapo Mashia huandaa vikao vya maombolezo. [5]

Nafasi ya Nyumba ya Fatma na Watu Wake

Halikadhalika, tazama: Ahlul-Bayt (a.s) na Nyumba ya Fatima (a.s)
Eneo la sasa la nyumba ya Fatima karibu na safuya kaburi (namba 7 pichani)

Katika hadithi zilizopokewa na Waislamu wa madhehebu ya Shia na Suni ni kwamba, Mtume (s.a.w.w) aliitambulisha nyumba ya Fatma na Ali kwamba, ni misdaqi na mfano bora kabisa wa nyumba ambapo imekuja katika Qur'ani ya kwamba: ((فِی بُیوتٍ أَذِنَ اللهُ أَن تُرْ‌فَعَ وَیذْکرَ فِیهَا اسْمُهُ یسَبِّحُ لَهُ فِیهَا بِالْغُدُوِّ وَالْآصَالِ ; Katika Nyumba ambazo Mwenyezi Mungu ameamrisha zitukuzwe, na humo litajwe jina lake, wanamtakasa humo asubuhi na jioni)). [6]

Katika vyanzo vya Shia na Ahlu-Sunna, kuna Aya za Qur'ani zilizoshuka ambazo zinahusishwa sababu zake na watu wa nyumba ya Fatma (Imam Ali, Fatma, Imam Hassan, na Imam Hussein). Miongoni mwa Aya hizo ni Aya ya It'am [7] na Aya ya Tat'hir. [8]

Sababu na Msukumo

Makala asili: Tukio la Ghadir na Tukio la Saqifa Bani Sai'da

Baada ya kuaga dunia Bwana Mtume (s.a.w.w) kundi la watu miongoni mwa muhajirina na Ansari lilikusanyika katika ukumbi wa Saqifa Bani Sai'da na kutoa kiapo cha utii kwa Ukhalifa wa Abu Bakr. [9] Kwa mujibu wa Ibn Kathir ni kwamba, Abu Bakr alipewa baia na kiapo cha utii kabla hata ya mwili wa Mtume kuzikwa; [10] ilikuwa ni katika masaa na wakati ambao Imam Ali (a.s) alikuwa ameshughulishwa na maandalizi ya kumzika Mtume. [11]

Tarehe 18 Mfunguo Tatu Dhul-Hija mwaka wa 10 Hijiria, wakati Mtume (s.a.w.w) anarejea kutoka katika Hija ya kuaga (Hijjat al-Wada') na iliyokuwa Hija yake ya mwisho, alimtambulisha Imam Ali ibn Abi Twalib (a.s) kuwa kiongozi wa Waislamu baada yake. Siku hiyo Mtume (s.a.w.w) alitoa hotuba mbele ya hadhara kubwa ya Waislamu kisha akaushika mkono wa Ali bin Abi Twalib na kusema: "Kila mtu ambaye mimi ni kiongozi wake basi huyu Ali pia ni kiongozi wake, Mwenyezi Mungu ampende atakayempenda, na amfanyie uadui atakayemfanyia uadui." Mtume (s.a.w.w) pia aliwausia Waislamu kushikamana na Qur'ani na Ahlul-bayt wake na akasema viwili hivyo havitatengana hadi vitakapomkuta yeye katika Hodhi ya Kauthar, Siku ya Kiyama. Omar ibn al-Khattab alikuwa miongoni mwa watu waliokuweko katika tukio na alijitkeza siku hiyo na kumpongeza Imam Ali kwa kuchaguliwa huko. [13]

Muhammad Hussein Ja'fari mwandishi wa kitabu cha Tashayyu' dar Masir-e Tarikh anasema: Abu Bakr na Omar walikuwa wakihofia radiamali kali ya Imam Ali au wafuasi wake na ndio maana wakawataka watoe baia na wakati walipokataa wakaamua kutumia nguvu. [14]

Ufafanuzi wa Tukio

Kwa mujibu wa nukuu ya Ya'qubi mwanahistoria wa karne ya tatu Hijria ni kwamba, katika tukio la Saqifa Bani Sa'ida baadhi ya masahaba kama Abbas ibn Abdul-Muttalib, Fadhl ibn Abbas, Salman Farsi, Abu Dharr al-Ghiffari, Ammar ibn Yassir na Bura' ibn Azib walikataa kumpa baina na kiapo cha utii Abu Bakr. [15]. Sayyid Murtadha Askary mhakiki wa historia wa karne ya 15 Hijiria anasema: Wale wale watu ambao hawakumpa baia na kiapo cha utiifu Abu Bakr wakiwa pamoja na Ali ibn Twalib (a.s) walifanya mgomo wa kuketi katika nyumba ya Fatma. [16] Tabari amewataja Talha na Zubeir pia kwamba, walikuwa miongoni mwa watu waliokuwa wamekusanyika na kuketi katika nyumba ya Fatma baada ya kukataa kumpa baia Abuu Bakr. [17]

Amri ya Abu Bakr ya Kuchukuliwa Baia Kutoka kwa Ali na Masahaba Zake

Baada ya kukamilika zoezi la kupewa baia na kiapo cha utii, Abu Bakr alianza kuwafuata baadhi ya masahaba ambao walikataa kumpa baia. [18] Kwa mujibu wa nukuu ya kitabu cha al-Imama wa al-Siyasa inayonasibishwa na Ibn Qutaibah ni kwamba, Abu Bakr alimtuma Omar na Qunfudh mara nne katika nyumba ya Fatma ili akamwambie Ali na waliokuwa pamoja naye katika nyumba hiyo watoe baia na kiapo cha kumkubali yeye kuwa Khalifa na kiongozi baada ya Mtume (s.a.w.w). [19] Kwa mujibu wa nukuu hiyo ni kuwa, katika mara ya kwanza, wanaume waliokuwa ndani ya nyumba walitoka na kutoa baia kwa Abu Bakr baada ya tishio la Omar la kuuvunja mlango na kuchoma moto nyumba, isipokuwa Ali yeye alikataa na kusema kuwa, ameapa asitoke ndani ya nyumba hiyo mpaka atakapomaliza kukusanya Qur'ani. Katika mara ya pili na ya tatu Abu Bakr alimtuma Qunfudh katika nyumba ya Fatma, yeye pia alipokea jibu hasi. Mara ya nne Omar akiwa na baadhi ya watu walikwenda katika nyumba ya Fatma, wakamtoa Ali na kumpeleka kwa Abu Bakr. [20] Muhammad Hadi Yusuph Gharawi mtafiti wa masuala ya kihistoria na Kishia anasema: Abu Bakr aliwatuma watu mara tatu katika nyumba ya Imam Ali na kutaka wampe baina na kiapo cha utii; mara ya kwanza na ya pili, Imam aliwarejesha na mara ya tatu Khalifa na watu wake walichukua hatua ya kutumia nguvu. [21]

Imekuja katika kitabu cha Ikhtisas kinachonasibishwa na Sheikh Mufid ya kwamba: Wakati walipokuwa wakimpeleka Ali upande wa msikiti, Zubeir ambaye alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa wamekusanyika nyumbani kwa Fatma baada ya kukataa kumpa baia Abu Bakr alitoa upanga na kusema: Enyi watoto wa Abdul-Muttalib! Hivi nyinyi mko hai na mnaona Ali anafanyiwa hivi?! Alielekea upande wa Omar ili amshambulie, lakini Khalid ibn al-Walid alimrushia jiwe na upanga wake ukadondoka. Omar alichukua upanga na kuubamiza katika jiwe na ukavunjika. [22] Kwa mujibu wa nukuu ya Tabari mwanahistoria wa karne ya tatu Hijria: Zubair wakati alipokuwa akitoka katika nyumba ya Fatma, mguu wake uliteleza na upanga ukamdondoka. [23]

Baada ya hapo, wakampeleka Ali kwa Abu Bakr na kumtisha kwamba, kama hatatoa baia na kiapo cha utii watamkata shingo yake. [24] Imekuja katika kitabu cha Sulaym kwamba, Ali akiwa katika mkusanyiko huo aliwahoji wahusika na kukumbushia maneno ya Bwana Mtume (s.a.w.w) siku ya Ghadir na matukio mengi yaliyokuwa yakithibitisha kwamba, yeye ndiye kiongozi na Khalifa wa Waislamu baada ya Mtume (s.a.w.w). Hata hivyo Abu Bakr alisema, alisikia kutoka kwa Bwana Mtume akisema ya kwamba'; Utume na Ukhalifa havikusanyiki kwa Ahlu-Bayt wake. [25]

Sheikh Mufid anasema, Imam Ali (a.s) hakumpa baia Abu Bakr katika siku ya Saqifa lakini kuhusiana na kwamba, baadaye alimpa baia au, kuna nukuuu tofauti; moja ya nukuu hiyo ni kwamba, Ali alimpa baia Abubakr baada ya siku arobaini au miezi sita au baada ya kufa shahidi Bibi Fatma (a.s). Sheikh Mufid anaamini kwamba, Imam Ali hakumpa katu baia Abu Bakr. [26]

Kwa mujibu wa hadithi, wakati Ali alipotishiwa kwamba, kama hatotoa baia na kiapo cha utii kwa Abu Bakr atakatwa shingo, Abbas bin Abdul-Mutalib ami yake Bwana Mtume akiwa na lengo la kumuokoa Ali alichukua mkono wake na kupangusha juu ya mkono wa Abu Bakr na kisha wao wakamuachilia huru, [27] hata hivyo kwa mujibu wa nukuu ya kitabu cha al-Imama wa al-Siyasa ni kwamba: Abu Bakr alisema, hatomlazimisha Ali kumpa baia madhali Fatma angali pamoja naye. [28]

Radiamali ya Fatma (a.s)

Baada ya watu waliotumwa na Abu Bakr mara ya kwanza kwenda katika nyumba ya Fatma kwa ajili ya kumchukua Ali (a.s), Bibi Fatma alienda kando ya mlango na kusema: Sijaona kaumu ambayo uwepo wao ni mbaya kuliko nyinyi; nyinyi muliacha jeneza la Mtume wa Mwenyezi Mungu mikononi mwetu na mkachukua uamuzi wenu (kuhusiana na Ukhalifa) na hamkutuuliza mtazamo na rai yetu na hamkutuoa haki zetu. [29]

Mara ya nne wakati Omar alipokwenda katika nyumba ya Fatma kwa ajili ya kumchukua Ali, Fatma alipaza sauti na kusema: " Ewe baba! Ewe Mtume wa Allah! Sisi baada yako tumetaabika kiasi gani na mwana wa Khattab na mwana wa Abu Quhafa!", baadhi ya watu waliokuwa wameafuatana na Omar baada ya kusikia maneno hayo ya Fatma waliathirika na hivyo waliamua kurejea. [30]

Mwanahistoria mashuhuri Ya'qubi anasema: Fatma aliwahutubu watu waliovamia na kuingia kwa nguvu nyumbani kwake kwa kuwaambia: Naapa kwa Mwenyezi Mungu, kama hamtatoka hapa ndani, nitapaza sauti kwa Mwenyezui Mungu kulilia uadilifu na haki" (nitakushtakini kwa Mwenyezi Mungu). Baada ya kusikia maneno haya, watu wote waliokuwa wameingia kwa nguvu katika nyumba yake wakatoka. [31] Abu Bakr Jawhari (aliaga dunia 323 Hijria) ameandika katika kitabu chake cha al-Saqifah Wafadak ya kwamba: Wakati Omar alipomchukua kwa nguvu Ali kumtoa nje ya nyumba, Fatma alikwenda kando ya mlango na akamhutubu Abu Bakr kwa kusema: "Ni kiasi gani, umewashambulia watu wa nyumba ya Mtume haraka namna hii! Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu, sitazungumza na Omar mpaka nitakapokutana na Mwenyezi Mungu." Kwa mujibu wa hadithi hii, baadaye Abu Bakr alikwenda kwa Fatma (a.s) na kumuombea Omar na Fatma akawa radhi naye. [33] Pamoja na hayo kwa mujibu wa hadithi sahihi iliyokuja katika Sahih Bukhari: Fatma alikuwa na hasira na ghadhabu na Abu Bakr kutokana na kupora shamba la fadak na hakuwa radhi naye katika kipindi chote cha uhai wake na mpaka anaaga dunia hakuwahi kuzungumza naye. [34]

Imekuja katika tafsiri ya Ayyashi: Wakati walipomtoa Ali nje, Fatma alikwenda kwa Abu Bakr na kumwambia: Kama hamtoamuachilia Ali nitakwenda katika kaburi la Mtume na kumshtakia Mwenyezi Mungu nikiwa na nywele zilizovurugika. Imam Ali amtuma Salman Farsi kwa Fatma ili akamzuie kufanya kitendo hicho. Baada ya kusikia ujumbe wa Ali aliondoka na kurejea nyumbani. [35]

Tishio la kuchoma moto nyuma

Kwa mujibu wa kile kilichoelezwa na kutajwa na baadhi ya vitabu na vyanzo vya Ahlu-Sunna kama al-Aqd al-Farid, [36] Tarikh Tabari, [37] Ansab al-Ashraf, [38] al-Musannaf, [39] na al-Imama wa al-Siyasa [39] ni kwamba, Omar ibn al-Khattab alikwenda nyumbani kwa Fatma kwa amri ya Abu Bakr ili akamchukue Ali na waliokuwa pamoja naye na kuwapeleka kwa Abu Bakr kwa ajili ya kutoa bai na wakati alipokutana na upinzani wa waliokuwa ndani ya nyumba, aliamrisha zikusanywe kuni na kutishia kwamba, ataichoma moto nyumba na walioko ndani yake. Kwa mujibu wa kauli ya Abd Rabbuh, mwanafasihi na mwanahistoria wa karne ya tatu na nne Hijria ni kwamba, Abu Bakr alimwambia Omar kama walioko katika nyumba ya Fatma watakaa kutoka basi apigane nao vita. Omar akiwa ameshikilia mwenge wa moto alitishia kwamba, kama walioko ndani hawatatoa baia ataichoma moto nyumba hiyo. [41] Kwa mujibu wa kile kilichonukuliwa katika kitabu cha al-Imama wa al-Siyasa ni kuwa, wakati Omar alipotoa kitisho hicho aliambiwa, Fatma yumo ndani ya hii nyumba. Omar akajibu kwa kusema: "Hata kama Fatma yupo ndani". [42] Hii inaonyesha ni kwa kiasi gani, Omar hakuwa hata akijali uwepo wa Fatma ambaye ni binti ya Bwana Mtume (s.a.w.w).

Katika vyanzo na vitabu vya historia kumetajwa majina ya baadhi ya watu ambao waliandamana na Omar katika tukio la kuvamia na kushambulia nyumba ya Fatma. Miongoni mwao ni: Usayd ibn Hudhayr, Salama ibn Salaamah ibn Waqsh, Thabit ibn Qays ibn Shammas Khazraji [43], Abd al-Rahman ibn 'Awf, Muhammad ibn Muslima [44] na Zayd ibn Aslam. [45]

Sayyid Ja'far Shahidi anaamini kuwa, tishio la Omar la kuchoma moto nyumba ya Fatma ambalo limenukuliwa katika vitabu vya Ansab al-Ashraf [46] na al-Aqd al-Farid miongoni mwa vyanzo vya Ahlu Sunna, haliwezi kuwa ni jambo na tukio bandia na la kutunga la Mashia au kundi la kisiasa la watu wenye kukubaliana na Mashia; hii ni kutokana na kuwa, wao (Mashia) hawakuwa na nguvu katika karne za mwanzo na walikuwa ni katika jamii ya walio wachache. Fauka ya hayo, kumesajiliwa ripoti katika vyanzo vya eneo la Magharibi ya Kiislamu (ardhi za pwani ya Magharibi ya Bahari ya Atlantic ambayo yalikombolewa na Waislamu ambapo mojawapo ni Andalusia) ambalo Mashia hawakuweko huko. [48] Shahidi anaamini kwamba, waliohudhuria katika ukumbi wa Saqifa walikuwa na daghadagha na wasiwasi juu ya utawala na madaraka kuliko kuwa na wasiwasi na dini. [49] Kwa maaana kwamba, walichokuwa wanakizingatia na kukipa kipaumbele ni uongozi na madaraka na sio dini.

Kuchoma Moto Mlango, Kujeruhiwa Fatima (a.s) na Kuharibika Mimba ya Muhsin

Katika baadhi ya vyanzo vya kale vya Kishia imenukuliwa kwamba, katika tukio la kushambuliwa nyumba ya Fatma, mlango wa nyumba ya Fatma ulichomwa moto, Fatma alijeruhiwa na kupelekea pia ujauzito wake wa mimba ya Muhsin kuharibika. Imekuja katika kitabu cha Sulaym ibn Qays kwamba, Omr ibn al-Khattab ambaye alitekeleza kivitendo tishio lake na kuchoma moto mlango wa nyumba ya Fatma, aliingia ndani ya nyumba na alipokutana na kusimama kidete Fatma alimpiga binti huyo wa Mtume kwa ala ya kuhifadhia upanga katika mbavu zake. [50] Aidha imekuja katika kitabu cha Ithbat al-Wasiyyya kinachonasibishwa na Ali ibn Hussein Mas'udi mwanahistoria wa karne ya nne ya kwamba: Walivamia na kushambulia na kuuchoma moto mlango na kumchukua kwa nguvu Ali na kumkandamiza Fatma nyuma ya mlango kiasi kwamba, ujauzito aliokuwa wa Muhsin ukaharibika."[51. Vilevile imekuja katika nukuu ya kitabu cha Dalail al-Aimah ya kwamba, Omar alimuamrisha Qunfudh ampige Fatma. [52]

Ayyashi ambaye ni mpokezi wa hadithi wa Kishia katika zama za Ghaibat Sughra (Ghaiba ndogo) anaye amesema, Omar aliupiga mlango wa nyumba ya Fatma uliokuwa umetengenezwa kwa matawi ya mtende na kuuvunja na kisha akaingia ndani na kumtoa Ali (a.s) akiwa amemfunga mabega. [53]

Zama za Kutokea Tukio

Vilevile angalia: Ayyam Muhsiniya

Muhammad-Hadi Yusufi Gharawi mhakiki na mtaalamu wa historia ya Uislamu na Ushia kutokana na ushahidi uliopo anaamini kuwa, zama za kutokea hujuma na shambulio dhidi ya nyumba ya Fatma (a.s) sio mara tu baada ya tukio la Saqifa na kupewa kiapo cha utii kwa Abu Bakr, bali tukio hili lilitokea takribani siku 50 au zaidi baada ya kifo cha Bwana Mtume (s.a.w.w). [54] Moja ya ushahidi wake ni kuwa, mtu anayejulikana kwa jina la Buraydah ibn Khusayb Aslami ambaye aliambatana na jeshi la Usama kuelekea Mu’tah baada ya kurejea Madina na kupata habari ya tukio la Saqfa akiwa pamoja na baadhi ya watu wa kabila lake aliamua kuwa upande wa Imam Ali (a.s) na kusema kuwa, madhali Ali hajatoa baia sisi pia hatutatoa bai na kiapo cha utii. Ni baada ya tukio hili ambapo Khalifa na watu wake wa karibu walifikia natija ya kuchukua baia na kiapo cha utiifu kutoka kwa Imam Ali. Kwa mujibu wa Yusufi Gharawi kwa kuzingatia kipindi cha kwenda na kurejea jeshi la Usama na matukio yaliyotokea kabla na baada yake, tukio la kuvamiwa na kushambuliwa nyumba ya Bibi Fatma litakuwa limetokea takribani siku 50 baada ya kufariki dunia Bwana Mtume (s.a.w.w). [55]

Matokeo ya Kushambuliwa Nyumba ya Bibi Fatma (a.s.)

Kuna matokeo yaliyotajwa na wanahistoria yaliyotokea baada ya tukio la kushambuliwa nyumba ya Bibi Fatma (a.s). Miongoni mwayo ni:

Fatma Aghadhibika na Omar na Abu Bakr

Kadhalika angalia: Hadithi ya Bidh-'ah

Imekuja katika kitabu cha Sulaym bin Qays, al-Imama wa al-Siyasa na Dalail al-Aimah ya kwamba, baada ya tukio la kushambuliwa na kuvamiwa nyumba ya Bibi Fatma (a.s), Abu Bakr na Omar walikuwa na nia ya kuomba msamaha na kuhakikisha kwamba, wanamfanya Fatma awaridhie. Hivyo wakafunga safari na kwenda kwake. Hata hivyo Fatma alikataa kuonana nao. Pamoja na hayo waliamua kumfanya Imam Ali (a.s) awe muombezi wao wa kumfanya Fatma akubali kukutana nao. Hatimaye wakafanikiwa kukutana na Fatma. Hata hivyo, katika kikao hicho, Fatma aliwapa mgongo na akawakumbusha maneno ya Mtume (a.s) aliposema: “Fatma ni pande la nyama yangu, mwenye kumuudhi ameniudhi mimi”. Kisha Fatma akawaambia Abu Bakr na Omar: Ninamshuhudisha Mwenyezi Mungu ya kwamba, nyinyi wawili mumeniudhi na kunighadhibisha. [56]

Kuharibika Mimba ya Muhsin na Kufa Shahidi Fatma (a.s)

Makala asili: Muhsin ibn Ali (a.s), kufa shahidi Fatma (a.s) na Ayyam Muhsiniya

Chanzo cha kale kabisa kilichonukuu mkasa wa kuharibika mimba ya Muhsin (a.s) katika tukio la kuvamiwa nyumba ya Bibi Fatma ambaye alikuwa mjamzito wa mimba ya Muhsin ni kitabu cha Sulaym ibn Qays miongoni mwa vyanzo na vitabu vya karne ya kwanza Hijiria na akthari ya vyanzo na vitabu vya baadaye vya Mashia kama al-Ihtijaj kilichoandikwa na Ahmad ibn Ali Tabarsi, Ghayatul Maram cha Sayyid Hashim Bahrani na Bihar al-Awar cha Allama Muhammad Baqir Majlisi vilinukuu mkasa huo kutoka katika kitabu hicho. [57]

Kujuta Abubakr

Katika baadhi ya vyanzo vya Ahlu-Sunna kama kitabu cha Tarikh Madinat Dimashq [58] kilichoandikwa na Ibn Asakir, al-Mu’jam al-Kabir [59] kilichoalifiwa na Tabarani na Tarikh al-Islam [60] kilichoandikwa na Dhahabi imekuja ya kwamba, katika masaa ya mwisho ya umri wake Abu Bakr alijuta na kuonyesha kusikitishwa kwake kwa kufanya mambo matatu ambapo mojawapo ni pale aliposema: Laitani nisingetoa amri ya (watu) kuingia kwa nguvu katika nyumba ya Fatma.

Mtazamo wa Masuni

Ripoti na nukuu zinazohusiana na tishio la Omar ibn Khattab la kuchoma moto nyumba ya Bibi Fatma (a.s) zimekuja katika vitabu vya Masuni kama cha Ansab al-Ashraf, [61] Tarikh Tabari, [62] al-Aqd al-Farid, [63] al-Musannaf, [64] na al-Imamah wa al-Siyasa [65], lakini tukio la kuchomwa moto mlango wa nyumba ya Fatma na kujeruihiwa binti huyo wa Mtume kutokana na mkandamizo wa mlango na kuharibika ujauzito aliokuwa nao wa Muhsin ni mambo ambayo yamekanwa na Masuni na wamesema kuwa, wapokezi wa kisa na mkasa huu ni marafidha.

Muhammad ibn Abdul-Karim Shahrestani, mtambuzi wa makundi ya Kiislamu ambaye ni mfuasi wa madhehebu ya Ash’ari (aliaga dunia 548 H) akitambulisha nadharia za Abu Hudheil (mwasisi wa kundi la Hudheiliya ambalo ni moja ya makundi ya Mu’tazila) anasema: Wao wanaamini kuwa, siku ya Omar kuchukua baia alimdhuru Bibi Fatma na kupelekea kuharibika ujauzito wa Muhsin. Shahrestani anaitaja ripoti hii kwamba, ni ya uongo. [66]

Khalil Aybak Safadi (aliaga dunia 746) katika kitabu chake cha al-Wafi Bi al-Wafiyat akimtambulisha Ibrahim ibn Sayar mashuhuri kwa jina la Nadhaam mmoja wa shakhsia wakubwa wa kundi la Mu’tazilah anamtaja kuwa mtu mwenye mielekeo ya urafidha na ananukuu kauli kutoka kwake kwamba, Omar alimdhuru na kumjeruhi Fatma na kupelekea kuharibika mimba ya Muhsin. [67]

Monografia

Kumeandikwa vitabu vyenye maudhui hii ya kujitegemea kuhusiana na hujuma na shambulio dhidi ya nyumba ya Bibi Fatma (a.s) ambapo baadhi ya vitabu hivyo ni:

  • Al-Hujum Ala Beit Fatma (a.s), mwandishi: Abdul-Zahra. Lugha: Kiarabu. Lengo la kitabu hiki ni kutoa taswira wadhiha na ya wazi kuhusiana na tukio la kuvamiwa na kuhujumiwa nyumba ya Fatma (a.s) kutoka katika vyanzo vyenye itibari vya Kishia na Kisuni. [68]
  • Haqiqat Hujum Be Khaneh Fateme Zahra (a.s) Az Manabe’ Ameh, mwandishi Ja’far Tabrizi. Kitabu hiki kimeandikwa kwa lugha ya Kifarsi. Mwandishi wa kitabu hiki, ndani yake amekusanya matukio na dhulma alizofanyiwa Fatma (a.s) baada ya kuaga dunia baba yake. Kitabu hiki kimetoa na kunukuu tukio la kushambuliwa nyumba ya Fatma kutoka katika vyanzo vya Kisuni na kinajibu maswali yanayoulizwa kuhusiana na tukio hili. [69] Kitabu hiki kimetajumiwa kwa lugha ya Kiarabu kwa anuani ya:
  • Al-Hujum Alaa Beit al-Sayyidad Fatma al-Zahra (a.s) Minal I’tidaa Ilal I’tiraf (Bilisan Masadir Ahl al-Sunnat Wal-Jamaa). [70].

Masuala yanayo fungamana

Vyanzo

  • Abū Ḥayyān Tawhīdī, ʿAlī b. Muḥammad. Al-Baṣāʾir wa al-Dhakhāʾir. Beirut: Dār al-Ṣādir, Beirut: Dār al-Ṣādir, 1408 AH.
  • Abū Nuʿaym al-Iṣfahānī, Aḥmad b. ʿAbd Allāh. Maʿrifat al-sahāba. Edited by ʿAzāzī ʿĀdil bin Yusuf. 1st edition. Riyadh: Dār al-Waṭan, 1419 AH.
  • ʿAbd al-Zahrāʾ, Mahdī. Nigarishī bi asnād wa madārik-i hujūm bi khana-yi Ṣiddīqa-yi Ṭāhira (a) az qarn-i awwal-i Hijrī tā kunūn. 5th edition. Tehran: Nashr-i Tak, 1391 Sh.
  • Allāh Akbarī, Muḥammad. Muḥsin b. ʿAlī (a). Majalla-yi Ṭulūʾ 29 (1388 Sh).
  • Amīn, Sayyid Muḥsin al-. Naqḍ al-washīʿa. Beirut: Muʾassisat al-Aʿlamī, 1403 AH.
  • ʿAskarī, Murtaḍā. Saqīfa; barrasī-yi nahwa-yi shiklgīrī-yi ḥukūmat pas az riḥlat-i Payāmbar. Edited by Mahdī Dashtī. Qom: Intishārāt-i Dānishkada-yi Uṣūl al-Dīn, 1387 Sh.
  • ʿAyyāshī, Muḥammad b. Masʿūd al-. Tafsīr al-ʿAyyāshī. Edited by Rasūlī Maḥallātī. Tehran: al-Maktaba al-ʿIlmiyya al-Islāmiyya, 1380 Sh.
  • Baḥrānī, Hāshim b. Sulaymān al-. Al-Burhān fī tafsīr al-Qurʾān. Qom: Muʾassisa Biʿthat, [nd].
  • Bukhārī, Muḥammad b. Ismāʿīl al-. Ṣaḥīḥ al-Bukhārī. Edited by Muḥammad Zuhayr. Beirut: Dār Ṭawq al-Nijāh, 1422 AH.
  • Balādhurī, Aḥmad b. Yaḥyā al-. Ansāb al-ashrāf. Beirut: Dār al-Fikr, 1417 AH.
  • Dīyārbakrī, Ḥusayn b. Muḥammad. Tārīkh al-khamīs fī aḥwāl ʾanfas al-nafīs. Beirut: Dār Ṣādir, [n.d].
  • Dhahabī, Muḥammad b. al-Aḥmad al-. Tārīkh al-Islām wa wafayāt al-mashāhīr wa l-aʿlām. Beirut: Dār al-Kitāb al-ʿArabī, 1413 AH.
  • Dhahabī, Muḥammad b. al-Aḥmad al-. Siyar aʿlām al-nubalāʾ. Beirut: Muʾassisat al-Risāla, 1405 AH.
  • Fakhr al-Rāzī, Muḥammad b. al-ʿUmar al-. Al-Tafsīr al-Kabīr. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth, 1420 AH.
  • Ganjī al-Shāfiʿī, Muḥammad b. Yūsuf al-. Kifāyat al-ṭālib fī manāqib ʿAlī b. Abī Ṭālib. 2nd edition. Tehran: Dār Iḥyāʾ al-Turāth Ahl al-Bayt, 1404 AH.
  • Hilālī, Sulaym b. Qays. Kitāb Sulaym b. Qays al-Hilālī. Qom: Al-Ḥadī, 1420 AH.
  • Ḥillī, al-Ḥasan b. Yūsuf al-. Nahj al-ḥaq wa Kashf al-ṣidq. Qom: Dār al-Kitāb al-Lubnānī, 1982 CE.
  • Haythamī, ʿAlī b. Abūbakr. Majmaʿ al-zawāʾid wa manbaʿ al-fawāʾid. Cairo: Maktabat al-Qudsī, 1414 AH.
  • Ibn Abī l-Ḥātam, ʿAbd al-Raḥmān b. Muḥammad. Tafsīr al-Qurʾān al-ʿaẓīm. Edited by Asʿad Muḥammad al-Ṭayyib. Mecca: Maktabat Nazār Muṣṭafā al-Bāz, [nd].
  • Ibn Abī l-Ḥadīd, ʿAbd al-Ḥamīd b. Hibat Allāh. Sharḥ Nahj al-balāgha. Qom: Maktabat Āyat Allāh al-Marʿashī, 1404 AH.
  • Ibn Ḥajar al-ʿAsqalānī, Aḥmad b. ʿAlī. Lisān al-mīzān. Beirut: Dār al-Bashāʾir, 2002.
  • Ibn Saʿd, Muḥammad b. Manīʿ al-Ḥāshimī al-Baṣrī. Al-Ṭabaqāt al-kubrā. Edited by Muḥammad ʿAbd al-Qādir ʿAṭā. Beirut: Dar al-Kutub al-ʿIlmiyya,1410AH-1990.
  • Ibn Shahrāshūb, Muḥammad b. ʿAlī. Manāqib Āl Abī Ṭālib. Qom: Nashr-i ʿAllāma, 1379 Sh.
  • Ibn ʿAbd Rabbih, Aḥmad Muḥammad. Al-ʿIqd al-farīd. 1st edition. Beirut: 1404 AH.
  • Ibn Athīr al-Jazarī, ʿAlī b. Abī l-Karam. Al-Kāmil fī l-tārīkh. Beirut: Dār Ṣādir, 1385 AH-1965.
  • Ibn ʿAsākir, ʿAlī b. al-Ḥasan. Tārīkh madīnat Dimashq. Beirut: Dār al-Fikr, 1415 AH.
  • Ibn Qutayba al-Dīnawarī, ʿAbd Allāh b. Muslim . Al-Imāma wa l-sīyāsa al-mʿrūf bi-tārīkh al-khulafāʾ. Qom: Sayyid Raḍī, 1413 AH.
  • Ibn Kathīr, Ismāʿīl b. ʿUmar. Al-Bidāya wa l-nihāya. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1408 AH.
  • Ibn Hishām, ʿAbd al-Malik. Al-Sīra al-nabawīyya. Egypt: Shirkat Maktabat wa Maṭbaʿat Muṣṭafā al-Bābī al-Ḥalabī, 1375 AH.
  • Irbilī, ʿAlī b. ʿĪsā al-. Kashf al-ghumma fī maʿrifat al-aʾimma. Qom: Raḍī, 1421 AH.
  • Jaʿfarī, Ḥusayn Muḥammad. Tashayyuʿ dar masīr-i tārīkh. Translated by Muḥammad Taqī Āyatullāhī. 14th edition. Tehran: Daftar-i Nashr-i Farhang-i Islāmī, 1386 Sh.
  • Jawharī Baṣrī, Aḥmad b. ʿAbd al-ʿAzīz. Al-Saqīfa wa Fadak. 2nd edition. Beirut: Shirka al-kutubī li-ṭibaʿat wa al-Nashr, 1401.
  • Kūfī, Ibn Abī Shayba al-. Al-Muṣannaf. Edited by: Muḥammad Laḥīdān. Riyadh: Maktaba al-Rushd, 1425 AH.
  • Khaṭīb Baghdādī, Aḥmad b. ʿAlī. Tārīkh-i Baghdād. Edited by Musṭafā ʿAbd al-Qādir ʿAṭā. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmīyya, 1417 AH.
  • Masʿūdī, ʿAlī b. al-Ḥusayn al-. Ithbāt al-waṣiyya. Qom: Muʾassisat Anṣārīyān, 1384 Sh.
  • Masʿūdī, ʿAlī b. al-Ḥusayn al-. Murūj al-dhahab wa maʿadin al-jawhar. 2nd edition. Edited by Asʿad Dāghir. Qom: Dār al-Hijra, 1409 AH.
  • Mufīd, Muḥammad b. Muḥammad al-. Al-Fuṣūl al-mukhtara. 1st edition. Edited by: ʿAlī Mīrsharīfī. Qom: Kungira-yi Shaykh Mufīd, 1413 AH.
  • Mufīd, Muḥammad b. Muḥammad al-. Al-Ikhtiṣāṣ. Edited by ʿAlī Akbar Ghaffārī and Maḥmūd Muḥarramī Zarandī. Qom: al-Muʾtamar al-ʿĀlamī li-Alfīyat al-Shaykh al-Mufīd, 1413 AH.
  • Mufīd, Muḥammad b. Muḥammad al-. Al-Irshād fī maʿrifat ḥujaj Allāh ʿalā l-ʿibād. [np], 1413 AH.
  • Muntaẓirī Muqaddam, Ḥamīd. Rashk bar Amīr-i Muʾminān (a): Darāmadī bar rawānshināsi-yi munāsibāt dar Tārīkh-i Islām. Majalla-yi Tārīkh dar āyīna-yi pajūhish 3 (1383 Sh).
  • Samhudī, ʿAlī b. ʿAbd Allāh. Wafāʾ al-wafā bi akhbār dar al-Muṣṭafā. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmiyya, 2006.
  • Suyūṭī, ʿAbd al-Raḥmān b. Abī Bakr al-. Al-Durr al-manthūr fī tafsīr al-maʾthūr. Beirut: Dār al-Fikr, [nd].
  • Shahristānī, Muḥammad b. ʿAbd al-Karīm. Al-Milal wa al-niḥal. Beirut: Dār al-Maʿrifa, [nd].
  • Shahīdī, Sayyid Jaʿfar. Zindigānī-i ʿAlī b. Ḥusayn (a). Tehran: Daftar-i Nashr-i Farhang, 1363 Sh.
  • Shūshtarī, Nūr Allāh al-Ḥusaynī al-. Iḥqāq al-ḥaqq wa izhāq al-bāṭil. Edited by Marʿashī al-Najafī. Qom: Kitābkhāna-yi Āyatollāh Marʿashī al-Najafī, 1409 AH.
  • Shaybānī Baghdādī, ʿAbd Allāh b. Aḥmad. Al-Sunna. Saudi Arabia: Dār Ibn al-Qayyim, 1406 AH.
  • Ṣadūq, Muḥammad b. ʿAlī al-. ʿUyūn akhbār al-Riḍā. Tehran: Nashr-i Jahān, 1378 AH.
  • Ṣadūq, Muḥammad b. ʿAlī al-. Maʿānī al-akhbār. Edited by ʿAlī Akbar Ghaffārī. Qom: Intishārāt-i Islāmī, 1403 AH.
  • Ṣafadī, Khalīl b. ʾAybak al-. Al-Wāfī bi l-wafayāt. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth, 1420 AH.
  • Tabrīzī, Jaʿfar. Ḥaqīqat-i Hujūm bi Khāna-yi Hadrat-i Fāṭima-yi Zahrā (a) az manābiʿ-i ʿĀmma. Qom: Dār al-Ṣiddīqa al-Shahīda, 1397 Sh.
  • Tirmidhī, Muḥammad ibn ʿĪsā al-. Sunan al-tirmidhī. 2nd edition. Edited by: ʿAbd al-Wahhāb ʿAbd al-Laṭīf. Beirut: Dār al-Fikr, 1403 AH.
  • Ṭabarānī, Sulaymān b. Aḥmad. Al-Muʿjam al-kabīr. Cairo: Maktaba Ibn Taymīyya, 1415 AH.
  • Ṭabrisī, Faḍl b. al-Ḥasan al-. Majmaʿ al-bayān fī tafsīr al-Qurʾān. Beirut: Dār al-Maʿrifa, [nd].
  • Ṭabarī, Muḥammad b. Jarīr al-. Al-Mustarshid fī al-Imāma. Qom: Kūshanpūr, 1415 AH.
  • Ṭabarī, Muḥammad b. Jarīr al-. Dalāʾil al-imāma. Qom: Biʾthat, 1413 AH.
  • Ṭabarī, Muḥammad b. Jarīr al-.Tārīkh al-umam wa l-mulūk. 4th edition. Beirut: Muʾassisat al-Aʿlamī, 1413 AH.
  • Ṭabarī, Muḥammad b. Jarīr al-. Jāmiʾ al-bayān ʿan taʾwīl āyāt al-Qurʾān. Beirut: Muʾassisat al-Risāla, 1420 AH.
  • Ṭūsī, Muḥammad b. al-Ḥasan al-. Al-Tibyān fī tafsīr al-Qurʾān. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, [n.d].
  • Yaʿqūbī, Aḥmad b. Abī Yaʿqūb al-. Tārīkh al-Yaʿqūbī. Beirut: Dār Ṣādir, [nd].
  • Yūsufī Gharawī, Muḥammad Hādī. Tārīkh-i hujūm bi khana-yi Ḥaḍrat-i Zahrā (a). Āyīna-yi pajūhish 27 (1379 Sh).
  • ایام شھادت حضرت فاطمه الزھرا سلام اللہ علیھا در پاکستان‎ ( The days of martyrdom of Lady Fatima al-Zahra (a) in Pakistan (Persian)). Accessed: 2023/11/29.
  • مراسم سوگواری ایام فاطمیه در مرکز اسلامی هامبورگ (Mourning Ceremony of the Fatimiyya in the Islamic Center of Hamburg (Persian)). Accessed: 2023/11/29.
  • مراسم سوگواری شهادت حضرت فاطمه(س) در جمهوری آذربایجان و تاجیکستان (The mourning ceremony of the martyrdom of Lady Fatima (a) in the Republic of Azerbaijan and Tajikistan (Tajik: not accessed)).