Kuelekea kibla

Kutoka wikishia
Makala ya kuelekea kibla ina uhusiano na makala za: Kibla, Kukengeuka kibla, kubadilisha kibla na kibla cha Waislamu.

Kuelekea kibla (Kiarabu: استقبال القبلة) ni kuielekea Kaaba wakati wa kufanya baadhi ya hukumu za wajibu. Kufanya matendo mengi ya kiibada na yasiyo ya kiibada ya Waislamu, kama vile kuswali, amali na matendo ya Hija, adabu za mazishi na kuchinja kisheria kunahusiana na kuna mfungamano na kibla.

Kusihi na kukubaliwa kwa matendo ya ibada, kama vile kuswali kunashurutishwa na suala la kuelekea kibla. Kadhalika kuchinja mnyama, ni wajibu kwa mnyama kuelekezwa kibla, kinyume na hivyo ni haramu kula nyama yake.

Kwa upande mwingine, ni haramu kufanya mambo kama vile kujisaidia hali ya kuwa mtu ameelekea kibla. Pia, kuelekea kibla wakati wa kusoma Qur’an, kutawadha na kula kunapendekezwa na kufanya baadhi ya mambo kama vile kujamiiana huku ukiwa umeelekea kunachukuliwa kuwa ni makuruhu.

Umuhimu na Nafasi

Mafakihi wamezungumzia kwa mapana na marefu suala la kuelekea kibla wakati wa kufanya amali na matendo mengi ya dini ya Uislamu, kama vile kuswali, kuhiji, kuwinda na kuchinja, hukumu za kujisadia na hukumu za wafu. Kuelekea kibla kunajumuishwa chini ya kanuni nne za wajibu, haramu, makuruhu na mustahabu. [1] Katika mafundisho mengi ya kidini, kuelekea kibla kumetambuliwa kuwa sababu ya kupata thawabu kwa ajili ya kutekeleza baadhi ya mambo. Imekuja katika sira ya Mtume wa Uislamu (s.a.w.w) kwamba kila mara alikuwa akiketi akiwa ameelekea kibla [2] na alitambua malipo ya kukaa kuelekea kibla kwa muda wa saa moja kuwa ni sawa na malipo ya Mahujaji na wanaofanya ibada ya Umra. [3]

Makusudio ya Kuelekea Kibla

Kwa mujibu wa mafaqihi wa Kishia, maana ya kuelekea kibla kwa wale waliomo ndani ya Masjid al-Haram ni kusimama hali ya kuwa wameielekea Kaaba. Yaani Kaaba iko mbele ya macho yao. [4] Kuhusu wale ambao hawako ndani ya Masjid al-Haram na hawaioni Al-Kaaba maana yake ni kuwa, kiada [5] wanapaaswa kuwa wameelekea upande wa Kaaba [6] na sio kwa usahihi wa kimantiki na wa kihalisia; kwa sababu hilo haliwezekani. [7]

Njia za Kuainisha Kibla

Kwa mujibu wa mafaqihi wa Kishia, kibla kinaweza kuainishwa kwa msingi wa elimu (maarifa) na dhana yenye nguvu, na ikiwa kwa njia hizi haiwezekani, kama mtu ana muda wa kutosha anapaswa kuswali akiwa ameelekea pande zote nne (kwa maana kwamba, aswali Sala ya kwanza akiwa ameelekea mbele, Sala ya pili, akiwa ameelea nyuma, na kisha kulia na kushoto kwake) na ikiwa muda ni mdogo na hautoshi, basi mtu anaweza kuswali akiwa ameelekea upande wowote kadiri anavyoweza. [8]

Ili kupata maarifa zaidi, aangalia makala hii: Qibla

Hekima ya Kuelekea Kibla

Wanazuoni wa Kiislamu wanaamini kwamba, kuelekea kibla wakati wa kufanya ibada, sambamba na kuwa ni kutenda kulingana na amri ya Mwenyezi Mungu, lakini kuna faida kama vile kujenga umoja baina ya Waislamu. [9] Kwa mujibu wa Allama Tabatabai, Waislamu licha ya tofauti zilizopo katika imani zao (za kimadhehebu) lakini wote wanaswali na kufanya ibada zao wakiwa wameelekea kibla (kibla chao ni kimoja) na hivyo roho ya upole zaidi inawezekana kupulizwa ndani ya mwili wa mwanadamu na kuleta mshikamano baina yao. [10] Kulingana naye, umakini wa moyo kwa mahali fulani umepelekea kupatikana umoja wa kiakili na kiroho wa Waislamu. [11]

Imekuja katika hadithi kwamba, falsafa ya kumuelekeza kibla mtu anayekata roho ni Malaika kumzingatia mtu huyo na ni ishara ya mtu anayekata roho kumzingatia Mungu hadi wakati wa kifo. [12]

Wajibu wa Kuelekea Kibla

Kuelekea kibla kumetambuliwa kuwa ni wajibu katika baadhi ya taklifu za kisheria kama vile Sala, hukumu za anayekata roho na kuchinja:

Sala

  • Sala za wajibu: Kwa mujibu wa fatwa ya mafaqihi wa Kishia, usahihi wa Sala za faradhi (swala za kila siku, Sala ya Majanga na Sala ya maiti) na baadhi ya yanayoifuata Sala, kama vile Sala ya tahadhari na kutetekeza vipengee vya Sala vilivyosahaulika ili hayo yasihi ni lazima kuelekea kibla. [13] Hoja ya hukumu hii imetambuliwa kuwa ipo katika Aya za Qur'an, [14] hadith [15] na makubaliano (ijmaa). [16] Iwapo haiwezekani kwa mwenye kuswali kuelekea kibla kwa mfano, ikiwa mtu huyo ni mgonjwa, sharti hili linapaswa kutekelezwa kwa kadiri inavyowezekana. [17]
  • Sala za mustahabu: Katika Sala za mustahabu kama anayesali yupo katika sehemu tulivu, inapaswa kusali hali ya kuwa mtu ameelekea kibla. [18] Baadhi ya wanazuoni wa fikihi wakitegemea Aya ya 115 ya Surat al-Baqara na hadithi kadhaa [19] wanasema, sio lazima kuelekea kibla katika Sala ya mustahabu inayosaliwa hali ya kuwa mtu yupo katika hali ya harakati (kwa mfano anayesali katika chombo cha usafiri kama meli au ndege). [20]
  • Namna ya kuchunga kuelekea kibla katika Sala: Kwa mujibu wa fat’wa za mafakihi, mtu anayesali hali ya kuwa amesimama, sehemu ya mbele ya mwili wake inapaswa kuwa imeelekea kibla, [21] mtu anayesali hali ya kuwa amekaa, uso wake, kifua, kichwa na magoti mawili vinapaswa kuwa vimeelekea upande wa kibla na mtu anayesali hali ya kuwa amelalala anapaswa kulala kwa ubavu wa kulia au kushoto kwa namna ambayo sehemu ya mbele ya mwili wake iwe imeelekea kibla na kama hawezi alalie mgongo na nyayo zake za miguu zielekee kibla. [22]

Kuchinja

Kwa mujibu wa fat’wa ya mafakihi wa Kishia, [23] wakati wa kumchinja mnyama, ni lazima sehemu anapochinjwa (koo) na sehemu ya mbele ya mnyama viwe vimeelekea kibla. Tegemeo la hukumu hii ni hadithi, [24] na ijmaa (maafikiano) ya Maulamaa. [25] Hata hivyo ikiwa atachinjwa na mchinjaji kusahau, kuwa jahili au hajui kibla (upande wa kibla ulipo) uchinjaji huo ni sahihi na nyama ni halali kuliwa. [26]

Muhtadhar (Anayekata Roho)

Akhthari ya wanazuoni wa fikihi wa Kishia wanaona kuwa ni wajibu kumuelekeza kibla Muislamu ambaye yupo katika hali ya kukata roho [27]. Mkabala na nadharia hiyo, kuna wanazuoni wanaoona kuwa kufanya hivyo ni mustahabu. [28]

  • Namna ya kumuelekeza kibla mtu anayekata roho: Imekuja katika vitabu vya fikihi kwamba, muhtadhar (anayekata roho) anapaswa kulazwa chali huku nyayo zake zikiwa zimeelekezwa kibla; kwa namna ambayo kama ataamka na kukaa basi atakuwa ameelekea kibla. [29]
  • Kumuelekeza kibla maiti wakati wa kumuosha na kumzika: Kuna mitazamo miwili kuhusiana na kumuelekeza kibla maiti wakati wa kumuosha: Wanazuoni wengi wa fikihi wametoa fat’wa ya kuwa mustahabu kufanya hivyo, [30] huku kundi jingine la wanazuoni likiamini kwamba, kufanya hivyo ni wajibu. [31] Kwa mujibu wa fat’wa ya mafakihi ni wajibu kumuelekeza kibla maiti wakati wa kumzika; kwa sura hii kwamba, alazwe kwa ubavu wa kulia kwa namna ambayo sehemu ya mbele ya mwili wake iwe imeelekea kibla. [32]

Haramu na Makuruhu Kuelekea Kibla

Kwa mujibu wa fat’wa ya mafakihi wa Kishia, ni haramu kukielekea au kukipa mgongo kibla wakati wa kujisaidia. [33] Kwa mtazamo wa Maraji Taqlidi walio wengi ni kwamba, haipaswi kumkalisha mtoto akiwa ameelekea kibla au amekipa mgongo kibla wakati wa kujisaidia; lakini kama mtoto amekaa mwenyewe wakati anajisaidia, sio wajibu kumzuia. [34]

Mafakihi wa Kishia wanaona kuwa ni makuruhu kuchunga suala la kuelekea kibla wakati wa kufanya jambo lolote ambalo linapingana na heshima na adhama ya kibla; [35] kama vile kujamiiana (kufanya tendo la ndoa). [36]

Mustahabu Kuelekea Kibla

Kwa mujibu wa kile kilichokuja katika vitabu vya fikihi ni kwamba, ni mustahabu kuelekea kibla wakati wa kufanya jambo lolote lile na katika hali yoyote isipokuwa katika mambo ambayo yametajwa kuwa ni haramu au ni makuruhu kuyafanya hali ya kuwa mtu ameelekea kibla. [37] Pamoja na hayo, katika maandiko ya fikihi, kumebainisha wazi kwamba, ni mustahabu kufanya baadhi ya amali na matendo hali ya kuwa mtu ameelekea kibla. Baadhi ya mambo hayo ni:

Rejea

Vyanzo