Kukengeuka na kuwa mbali na upande wa Qibla
Kukengeuka upande wa Qibla (Kiarabu: الانحراف عن القبلة) Ni istilahi ya fiqhi ambayo inamaanisha ile hali ya mtu kuukingiusha uso wake kutoka kwenye makadirio ya kawaida ya mwelekeo wa Kaaba. Suala la kuelekea Qibla ni miongoni mwa masuala yanayo tafitiwa kwenye vyanzo vya fiqhi. Suala hili hupatikana katika milango inayozungumzia matendo ya ibada maalumu kama vile; sala, hijja, dhabihu (vichinjwa) pamoja na hukumu za kujisaidia (kwenda msalani).
Mafaqihi wanalihisabu suala la kuelekea Kaaba kuwa ni miongoni mwa mambo muhimu katika baadhi ya ibada. Miongoni mwa ibada zinazolazimiana na uelekeaji Qibla ni sala, ambapo kuto fanya hivyo hupelekea kubatilika kwa ibada hiyo. Pia, kwa mujibu wa fat’wa zao, ni wajibu mtu kujikingiusha na upande wa Qibla wakati wa kujisaidia kwake, yaani ni haramu mtu kujisaidia huku akiwa ameelekea Qibla.
Dhala na Nafasi Yake
Waislamu Kaaba au mwelekeo wa upande wa Kaaba huita Qibla. Maana ya mtu kujikingiusha au kukaa mbali na Qibla, ni kule mtu kuukingiusha uso wake na kuwa mbali na upande wa kawaida wa Kaaba. [1] Ila lililo muhimu ni kule mtu kuwa mbali na mwelekeo wa Qibla kama inavyofahamika na watu wa kawaida katika jamii, [2] na wala hakuna haja ya mtu kutumia vipimo vya kisayansi au upeo wa juu wa kiakili [3] katika jambo hilo. [4]
Suala la kuelekea Qibla na kuto kengeuka mwelekeo wa Kaaba, ni miongoni mwa mada zinazotafitiwa na mafaqihi pale wanapozungumzia wajibu mbali mbali wa kidini wa, ikiwemo; sala, hijja, dhabihu (uchinjaji), hukumu za kujisaidia pamoja na hukumu zinazo husiana na wafu. Wao wametafiti na kujadili vya kutosha katika kuonesha umuhimu wa kuelekea Qibla na kuto kingiusha uso na kuto kuwa mbali na mwelekeo wa upande wa Qibla wakati wa kutenda ibada hizo. Kwa mujibu wao kuto fanya hivyo kunaweza kubatilisha baadhi ya ibada hizo. [5]
Kwa imani ya baadhi ya wanazuoni, kuelekea Qibla wakati wa sala, na kuto kingiusha uso na Kibala hicho, si alama tu kutii amri ya Mungu, bali pia moja ya mamabo yaletayo umoja kati ya Waislamu. [6]
- Kwa taarifa zaidi, angalia: Qibla na Kuelekea Qibla.
Hukumu za Fiqhi Kuhusu Kuelekeza Mbali na Qibla
Mafaqihi wanaona kwamba; kuelekea mbali na Qibla kunaweza kubatilisha baadhi ya matendo ya ibada. Kuna mambao kadhaa katika hukuku zinazohusiana na mambo ya Qiblaza, ambayo baadhi yake ni wajibu na mengine ni haramu. Miongoni mwao ni kama ifuatavyo:
- Wakati wa kusali: Ikiwa msimamisha sala ataelekeza uso mbali na Qibla kwa makusudi kiasi kwamba amuonaye hawezi kusema kuwa ameelekea Qibla, ama akageuza kichwa chake kushoto au kulia, hayo yatapelekea sala yake kubatilika. [8] Lakini ikiwa kuelekea kwake huko mbali na Qibla ni kwa bahati mbaya, na ni chini ya digrii 90, hapo sala yake itakuwa ni sahihi. [9] Pia si tatizo kuelekeza kichawa chake kiasi kidogo mbali na Qibla. [10]
- Wakati wa kuchinja mnyama fulani: Ni lazima wakati wa kumchinja mnayama fulani, kuuelekeza Qibla mwili wa mnyama huyo, [11] vinginevyo kichinjwa hicho kitakuwa ni najisi na nyama yake ni haramu. [12] Hata hivyo, kama amefanya kwa kusahau au kwa kutojua upande wa Qibla, haitoharamika wala kunajisika nyama ya mnyama huyo. [13] Hoja ya hukumu hii ni baadhi ya Hadithi [14] na Ijmaa (mwafaka wa wanazuoni). [15]
- Wakati wa kujisaidia: Ni wajibu kuelekea mbali na Qibla wakati wa kujisaidia, [16] na ni haramu kwa mwenye kujisaidia kuelekea Qibla au kukipa mgongo Qibla hicho. [17]
- Wakati wa ibada ya kutufu (kuzunguka Kaaba): Ni wajibu bega la kushoto la mwenye kutufu kuelekezwe kwenye Kaaba na lisiwe limeelekea mbali na Kaaba, [18] kiasi ya kwamba amuonaye aweze kusema kwamba bega hilo liko mbali na Kaaba hiyo. [19]