Qibla
Qibla Qibla ni mwelekeo unaotakiwa kuchungwa na kuelekewa wakati wa kufanya baadhi ya matendo ya kidini na hata baadhi ya matendo ya kawaida. Qibla kimejadiliwa katika sura na milango mbalimbali ya fiqh, kama vile mlango sala, dhabihu (vichinjwa), mazishi na hija. Kila dini ina qibla chake. Kwa Waislamu, qibla chao ni Kaaba ilioko Makka. Kwa Wayahudi ni Mwamba wa Hekalu la Mlima Moria (Beitul Muqaddas). Kwa Wakristo ni upande wa mashariki. Kwa mujibu wa fiqh ya Shia, baadhi ya matendo yanapaswa kufanywa kwa kuelekea qibla, kama vile sala, huku matendo mengine yakiwa ni haramu kufanywa kwa kuelekea qibla, kama vile kujisaidia. Hekima ya kuwa na qibla kimoja, ni kuleta umoja na mshikamano miongoni mwa Waislamu. Ufafanuzi na Umuhimu wa Qibla Qibla ni nini? Qibla ni mwelekeo unaoelekewa kimwili na kiroho na Waislamu wakati wa kufanya baadhi ya matendo yao ya kidini, hasa sala. [2]Waislamu katika kutekeleza baadhi ya ibada zao hulazimika kuelekea mwelekeo huo ambao ndio upande wa Kaaba ilioko huko Makka. [3] Kwa mujibu wa maelezo ya mwanazuoni al-Tusi (aliyefariki mwaka 1360 Shamsia) katika tafsiri ya Al-Mizan, ni kwamba; wafuasi wa dini zote kikawaida hua wana vibla vyao maalumu. [4] Qibla cha Waislamu ni Kaaba ilioko Makka. Qibla cha Wayahudi ni Jiwe maalumu lililoko huko Beit-ul-Muqaddas [5] na qibla cha Wakristo, -popote pale walipo- ni upande wa Mashariki. [6] Hata hivyo, baadhi ya Wakristo Bethlehem (mahali alipozaliwa Yesu) wameifanya kuwa ndio qibla chao. [7]
Qibla cha Waislamu
Hapo awali ambapo ni mwanzoni mwa utume wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), Qibla cha Waislamu kilikuwa ni Msikiti wa Al-Aqsa. Lakini baada ya kuteremshwa kwa Aya ya Qibla, Qibla hicho cha Waislamu kilibadilishwa kutoka Msikiti wa Al-Aqsa na kuwa ni Kaaba ilioko Makka. [8] Kisheria, wanazuoni wa Kiislamu hawaruhusu kumtuhumu mtu anaye sali kwa kuelekea Qibla, kuwa si Mwislamu. [9] Kuelekea Qibla ni Moja ya Masharti ya Kukubalika kwa Baadhi ya Matendo ya Waislamu Kwa mujibu wa maoni ya mafaqihi wa Shia ni kwama; baadhi ya matendo ya ibada na sheria za Kiislamu kuhusiana na mwelekeo kuelekea wa Qibla, zibidi kujadiliwa chini ya sheria nne; za wajibu, za haramu, za makruh na za mustahab. [10] Kulingana na hili, suala la kuelekea Qibla wakati mwingine huwa ni miongoni mwa sharti ya usahihi wa tendo la ibada fulani kama vile sala, na kutofuata sheria hii kutasababisha tendo kubatilika kwa tendo hilo. [11] Pia, ni wajibu kumwelekeza mnyama Qibla wakati wa kumchinja, na ikiwa mnyama huyo -kwa makusudi- atachinjwa kinyume na Qibla, basi itakuwa ni haramu kula nyama ya myama huyo. [12] Katika baadhi ya matukio, kama vile kujisaidia haja kubwa, kuelekea Qibla ni haramu. [13] Katika baadhi ya misikiti, maeneo ya kidini na sehemu nyengine za umma wa Waislamu, huwekwa alama ya mshale ili kuonesha upande sahihi wa Qibla. [14]
Falsafa ya Kuainishwa Qibla Maalumu Kitabu cha Tafsiri Nemune, kikielezea falsafa ya kuteuliwa na kuanishwa Qibla maalumu kwa Waislamu, ni kuunda umoja na uratibu katika safu za Waislamu na kuzuia machafuko na mgawanyiko ndani ya jamii za Waislamu. Pia kuielekea Kaaba, kama ni Qibla cha Waislamu, ni kichocheo cha kumbukumbu za Tawhidi. Hii kwa sababu kwamba; Kaaba ni moja ya vituo vya kale zaidi vya tauhidi katika historia ya Wanadamu. [15] Njia za Kisheria za Kuainitisha Upande wa Qibla Kwa mujibu wa nadharia za wanazuoni wa Shia ni kwamba; kuainisha upande sahihi wa Qibla kunaweza kutegemea elimu, makisio ya dhana, na uhakika na yakini. Baadhi ya njia za kutambua upande wa Qibla ni kama ifuatavyo: 1- Jitihada binafsi za kutafuta Qibla kwa kutumia njia mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kutumia vifaa vya kisayansi kama vile ramani ya na dira. [16] 2- Kauli ya mashahidi wawili waadilifu ambao wamegundua wenyewe mwelekeo wa Qibla kupitia ishara za hisia maalumu. [17] 3- Kauli ya mtambuzi anatambua upande wa Qibla kwa misingi ya kanuni ya kisayansi ambaye kauli yake ni yenye kuaminika. [18] 4- Kutumia dhana yenye uhakika kama vile kuangalia mwelekeo wa makaburi ya Waislamu, mihrabu za misikiti (vibla vya misikiti), na hali ya jua, mwezi, na nyota iwapo elimu ya Qibla haiwezekani kupatikana. [19] Ikiwa njia hizi haziwezekani, hali hiyo italapelekea watu kusali kwa kuelekea pande zote nne, na ikiwa hana muda wa kusali sala zote nne, basi itambidi asali kadri ya muda anavyomruhusu, yaani ikiwa wake utakuwa ni mfupi wa kiasi cha kusali kwa pande tatu, basi itabidi asali kwa kuelekea pande tatu, na ikiwa wakati wake ni wa kiasi cha kusali sala mbili tu basi atasali kwa kuelekea pande mbili. [20]
Jinsi ya Kutafuta Qibla Kielimu • Kutumia Dira: Dira (compass) ni kifaa cha kisayansi cha kutambua upande wa Qibla. Kwa mujibu wa maoni ya wanazuoni wa Shia, matumizi yake hutoa uhakika wa Qibla na kuabudu kulingana na kifaa hiki ni halali. [21] Baadhi ya Marjaa, licha ya uwepo wa dira za kuaminika, ila bado wanaona kuwa ni vigumu kutegemea mihrabu za misikiti na makaburi ya Waislamu yaliojengwa kulingana dira hizo katika kutafuta upande wa Qibla. [22] • Kutumia Kiashiria cha Kivuli: Kutumia kiashiria cha kivuli (fimbo au kifaa chengine kilicho simama wima) wakati wa adhana ya Dhuhuri huko Makka, ambayo huwa ni sawa na saa 12: 48 ya siku ya tarehe saba mwezi wa Khordad na saa 12: 57 ya tarehe 25 ya mwezi Tir. Tarehe mbili hizi zilizo tajwa hapo ni tarehe za kalenda ya Kifarsi au Shamsia. Katika siku hizi mbili, jua huwa linaangaza Kaaba moja kwa moja na halina kivuli, na mtu aliyepo mahali popote alipo, iwapo atasimama na kuelekea upande wa kinyume na kivuli chake (yaani kulielekea jua), yeye atakuwa amesibu upande halisi wa Qibla. [23] • Kutumia Nyota ya Kaskazini: Nyota ya Kaskazini, inapatikana katika upande kaskazini wa nusu ya umbo la mpira wa ramani ya dunia, na tukisimama kuielekea nyota hiyo, tunakuwa tumeelekea kaskazini. Ili kutumia njia hii katika kutafuta Qibla, simama kuelekea kusini na kuzingatie kiasi cha mkingiuko wa Qibla kutoka kusini, bila sha tutaweza kubaini mwelekeo halisi wa Qibla. [25]