Harakati za al-Yamani

Kutoka wikishia

Harakati ya al-Yamani (Kiarabu: قيام اليماني) au Harakati ya Qahtani (Kiarabu: قيام القحطاني) ni katika ishara na alama za kudhihiri Imamu Mahdi (a.t.f.s) ambayo inaashiria harakati itakayoanzishwa na Bwana mmoja kutoka katika kizazi cha Imamu Hussein (a.s). Bwana huyu asili yake ni Yemen na harakati yake itatokea kabla ya kudhihiri Imamu Mahdi. Kwa mujibu wa Hadithi mbalimbali, harakati yake itatokea sambamba na kutoka Sufyani (kuibuka harakati ya Sufyani) na harakati ya Sayyid Khorasani.

Kuwalingania na kuwaita watu upande wa Imamu Mahdi (a.t.f.s), kupigana na Sufyani, kuikomboa Roma na Constantinople ni miongoni mwa hatua zilizotajwa kwamba, zitafanywa na kuchukuliwa na Yamani na harakati yake imetambuliwa kuwa itaanzia Yemen.

Kuanzia karne ya kwanza ya Hijria kuna watu waliojitokeza na kudai kuwa wao ni al-Yamani. Miongoni mwao ni Abdul-Rahman bin Muhammad bin Ash’ath Kindi ambaye alianzisha uasi dhidi ya Hajjaj bin Yusuf al-Thaqafi na Ahmad Ismail Basri maarufu kama Ahmad al-Hassan.

Utambuzi wa Shakhsia ya Al-Yamani

Yamani ni lakabu ya mtu ambaye kwa mujibu wa riwaya na hadithi ataanzisha harakati yake kabla ya kudhihiri Imamu Mahdi (a.t.f.s) [1] na atawaita na kuwalingania watu wamfuate. [2]

Katika hadithi hakujatajwa jina asili la Yamani; lakini yeye anatokana na kizazi cha Imamu Hussein (a.s) [3] au ametambuliwa kuwa anatokana na wajukuu wa Zayd bin Ali [4]. Imeelezwa kwamba, katika baadhi ya vyanzo vya Ahlu-Sunna jina lake limetajwa kuwa ni Jahjah, Hassan au Hussein. [5] Mwandishi wa kitabu cha «Rayaat al-Huda wal-Dhalal fi Asr al-Dhuhur» anasema: Hata kama nasaba ya Yamani haijatajwa katika hadithi, lakini hoja za wazi zinathibitisha kwamba, yeye anatokana na Ahlul-Bayt (a.s) na kutoka katika kizazi cha Imamu Hussein (a.s). [6]

Katika hadithi iliyonukuliwa kutoka kwa Bwana Mtume (s.a.w.w) Yamani ametajwa kwa jina la Mansur ambaye atajitokeza kumsaidia na kumnusuru Imamu Mahdi (a.t.f.s). [7] Kadhalika katika vyanzo vya Ahlu-Sunna ametajwa kwa jina la Qahtani [8] na Mansur Yamani. [9] Qahtani ananasibishwa na mtu anayejulikana kwa jina la Qahtan [10] ambaye nasaba yake inafikia kwa Waarabu wanaoishi Yemen. [11]

Kutoka al-Yamani ni Katika Ishara za Kudhihiri Imamu Mahdi (a.t.f.s)

Katika hadithi, harakati ya al-Yamani imetajwa kuwa miongoni mwa alama na ishara za kudhihiri Imamu Mahdi (a.t.f.s). Kwa mujibu wa hadithi iliyoko katika kitabu cha Kamal al-Din cha Sheikh Saduq na ambayo imenukuliwa kutoka kwa Imamu Swadiq (a.s), Harakati ya al-Yamani pamoja na Harakati ya Khorasani sambamba na ngurumo au sauti kali kutoka mbinguni, kuuawa nafsi takasifu (nafs Zakiyyah), kujitokeza Sufiyani na Khasf al-Bayda' (kumezwa eneo la Bayda') ni katika alama za kudhihiri Imam Mahdi mtarajiwa (a.t.f.s). [12] Kwa mujibu wa wahakiki, kuna hadithi 36 kuhusiana na Harakati ya Yamani katika vyanzo vya Kishia na Kisuni [13] na akthari ya hadithi hizi hazijaashiria kwamba, Harakati ya Yamani ni katika alama zisizo na shaka za kudhihiri Imamu Mahdi (a.t.f.s) [14] na katika hadithi zilizonukuliwa kutoka kwa Waislamu wa Kishia, kuna hadithi mbili tu ambazo zinaeleza kuwa, hiyo ni alama isiyo na shaka. [15] Kwa msingi huo baadhi ya wahakiki wametilia shaka kuhusiana na Harakati ya Yamani kuwa ni katika ishara na alama zisizo na shaka za kudhihiri Imamu Mahdi (a.t.f.s) [16] na wametumia hoja hii kwamba, katika baadhi ya nakala hadithi hizi mbili hakujawekwa nukta ya kuonyesha kwamba, kutokea kwake hakuna shaka [17] na wamejaalia kwamba, qayyid (sharti) hiyo imeongezwa na wapokezi. [18]

Wakati na Mahali

Kwa mujibu wa riwaya na hadithi mbalimbali, harakati ya al-Yamani itatokea pamoja na kutoka Sufyani. [19] Kwa mujibu wa hadithi iliiyonukuliwa kutoka kwa Imamu Baqir (a.s) ni kuwa, kutoka Sufyani, Yamani na Khorasani kutatokea katika mwaka mmoja, mwezi mmoja na katika siku moja. [20] Imamu Sadiq (a.s) katika hadithi moja amenukulia akieleza kwamba, harakati Sufyani itatokea katika mwezi Rajab. [21] Baadhi kwa kuweka pamoja hadithi hizi mbili, wametambua pia kwamba, harakati ya Yamanii pia itatokea katika mwezi wa Rajab. [22] Baadhi ya waandishi wanaona kuwa, kutokea matukio haya katika siku moja, ni kinaya ya mfungamano mkubwa uliopo baina ya Harakati ya Yamani na kutoka Sufyani na wanaamini kwamba, jambo hilo halina mgongano na suala la kuweko tofauti ndogo baina ya matukio haya mawili. [23]

Kadhalika katika vyanzo vya Waislamu wa madhehebu ya Sunni, kuna hadithi zinazoeleza juu ya kushuka Nabii Issa na kutokea Dajjal katika zama zake, [24] na kutokea yeye ni baada ya kuja Mahdi (atfs). [25] Kwa uoni wa waandishi wa Kishia ni kwamba, hadithi hizi hazina itibari kwani hazijatoka kwa Maasumu [26] na vilevile kutokana na kuwa, hadithi zinazoeleza kwamba Harakati ya Yamani itatokea baada ya kuja Imamu Mahdi zinakinzana na hadithi zinazoeleza kwamba, Harakati ya al-Yamani ni katika ishara na alama za kudhihiri Imamu Mahdi. [27]

Harakati ya al-Yamani kwa mujibu wa hadithi itatokea Yemen. [28] Katika hadithi zinazohusiana na Harakati ya al-Yamani miji ya Sana'a, Aden, Kinda na eneo la Abyan yameashiriwa. [29] Baadhi wanaamini kwamba, hadithi zinazohusiana na Sana'a ni mustafidh (yaani mpokezi wake ni zaidi ya mtu mmoja lakini haijafikia kiwango cha kuwa mutawatir yaani mapokezi mengi) na zimenukuliwa kutoka upande wa Shia na Sunni na zinaashiria makao makuu yake. [30]

Hatua za Al-Yamani

Katika hadithi hakujashiriwa kwa undani kuhusiana na Harakati ya al-Yamani lakini kumetajwa baadhi ya hatua zake atakazochukua na baadhi ya mambo atakayoyafanya; miongoni mwayo ni kulingania haki, kupigana vita na Sufyani na kuikomboa Roma na Constantinople.

  • Kulingania haki: Kwa mujibu wa hadithi kutoka kwa Imamu Muhammad Baqir (a.s), Harakati ya Yamani imetambuliwa kuwa ni ya haki na kumetiliwa mkazo juu ya udharura wa kujiunga na harakati hiyo. [31] Baadhi ya waandishi wanasema, makusudio ya kuanzisha harakati kwa ajili ya haki wamefasiri kuwa ni kulingania Uimamu. [32] Katika hadithi kumetajwa jina la mtu anayejulikana kama Mansur ambaye ni msaidizi wa Imamu Mahdi na ambaye ana waungaji mkono 70,000. [33] Kwa mujibu wa hadithi, wakati Yamani atakapoanzisha harakati uuzaji silaha utakuwa haramu. [34]
  • Kupigana vita na Sufyani: Baadhi ya hadithi zinaelezea juu ya kutokea vita na mapigano baina ya Yamani na Sufyani; kwa mfano mtu ambaye atatoa jicho la Sufyani atatokea Sana'a, [35] au mtu kwanza ambaye atapigana na Sufyani atakuwa na asili ya ukoo wa Qahtan. [36] Hadithi zimetofautiana kuhusiana na matokeo ya vita baina ya Yamani na Sufyani; baadhi zinazungumzia kuibuka na ushindi Yamani [37] na zinasimulia kushindwa kwake. [38] Baadhi ya waandishi wakiwa na lengo la kuhalalisha hitilafu za hadithi hizi wamesema, kila moja kati ya hadithi hizi, zinatoa habari juu ya kupigana pande mbili katika sehemu maalumu. [39] Kuna shaka kuhusiana na kuwa sahihi mapokezi ya hadithi hizi. [40] Kwa mujibu wa hadithi iliyopokewa na Ibn Hammad, msomi na mwanazuoni wa Kisunni katika kitabu cha al-Fitan, Yamani ataungana na Imamu Mahdi mjini Madina. Sufyani atapeleka jeshi Madina lakini wawili hao watatoka Madina kuelekea Makka. [41] Jeshi la Sufyani litawafuata na jeshi la Sufyani litamezwa katika eneo la Bayda. [42]
  • Ukombozi: Imekuja katika baadhii ya vyanzo vya Ahlu-Sunna ya kwamba, Yamani atayakomboa maeneo ya Roma na Constantinople. [43] Bendera yake na za wafuasi wake zina rangi nyeupe. [44] Katika vyanzo vya Kishia, kukombolewa maeneo hayo kumenasibishwa na Imamu wa Zama. [45]

Waliodai Kwamba ni Yamani

Kwa mujibu wa hadithi, Mashia kuanzia katika zama za Imamu Sadiq (a.s) walikuwa wakimsubiri Yamani. Imamu Sadiq alikanusha kwamba mtu anayeitwa "Talib Haq" ni Yamani kwa sababu Yamani ni rafiki wa Ali (a.s), lakini Talib Haq hampendi Ali (a.s). [46] Kuanzia karne ya kwanza, kuna watu waliojitokeza na kujitambulisha kwamba, wao ni Yamani. Miongoni mwao ni:

  • Abdul Rahman bin Muhammad bin Ash’ath (aliyefariki mwaka wa 85 Hijiria), katika zama za Abdul Malik bin Marwan, alimuasi Hajjaj bin Yusuf Thaqafi, mtawala wa Iraq, na akajiita Qahtani ambaye watu wa Yemen walikuwa wakimngojea. [47] Ibn Ash'ath baada ya kushindwa na Bani Umayya alikwenda Sistan na akaaga dunia akiwa huko. [48]
  • Ibn Faras: Kwa mujibu wa ripoti ya Ibn Khaldun ni kuwa, Abdul Rahim bin Abdur Rahman bin Fars alikuwa mmoja wa wanazuoni wa karne ya 6 na 7 huko Andalusia. Siku moja Mansour alitoa hotuba kali katika kikao kimoja. Baada ya hapo, aliishi kwa siri kwa muda na Mansour alipoaga dunia, akatokea na kudai kuwa ni Qahtani yule yule ambaye Mtume alieleza habari za ujio wake. Hatimaye, Nasir bin Mansour alimpelekea jeshi na Ibn Zayd akauawa katika vita hivi. [49]
  • Ahmad bin Ismail Basri, anayejulikana kama Ahmad al-Hassan, alijitambulisha kama Yamani. Alidai kuwa yeye ndiye mwenye dhamana ya kuweka misingi ya kudhihiri Imamu Mahdi (as) na ataichukua serikali baada ya Imam wa Zama. [50] Kitabu «Dawa Ahmad al-Hasan Baina al-Haq wa al-Batil» kiliandikwa kukanusha madai hayo na kukosoa imani yake. [51]

Pia, Yazid bin Mulhib [52] na Abd al-Rahman bin Mansour (wakati wa Hisham bin Hakam al-Mu’yyad Billah) [53] ametajwa kuwa mtu aliyedai kwamba, yeye ni Yamani.

Monografia

Kitabu cha «al-Yamani Rayat Huda» kinahusiana na Harakati ya Yamani na kimeandikwa kwa lugha ya Kiarabu. Mwandishi wa kitabu hiki ni Sayyid Mohammad Ali Al-Hulw (aliyezaliwa mwaka 1376 Hijiria), mwanachuoni wa Kishia kutoka Iraq. Katika kitabu hiki, mada kama vile jina na nasaba ya Yamani, mahali na wakati wa uasi wake zimejadiliwa. Mwandishi amezingatia harakati ya Yamani kama mojawapo ya dalili na alama za uhakika na zisizo na shaka za kudhihiri Imamu Mahdi (a.t.f.s). [54]

Vyanzo

  • Ibn Ḥammad, Naʿīm b. Ḥammād. Al-Fitan. Edited by Majdi b. Mansur. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmiyya, [n.d.]
  • [https://www.noormags.ir/view/fa/articlepage/1002896/بررسی-برخی-ادله-روایی-احمد-بصری-یمانی-دروغین Yusufiyan, Mahdi and Shahbaziyan, Muhammad. Barrasī-yi barkhī adilla-yi riwayī Aḥmad Baṣrī yamānī-yi durūghīn. Published in Mashriq-i Maw'ud journal, no. 27, 1392 Sh.
  • [https://www.noormags.ir/view/fa/articlepage/1077103/بررسی-تطبیقی-روایات-یمانی-از-منظر-فریقین Mahdawi Rad, Muhammad Ali, et al. Barrasī-yi taṭbīqī-yi riwāyat-i Yamānī az manzar-i farīqayn. Published in Hadith Pazhuhi journal, 1393 Sh.
  • Āyatī, Nuṣrat Allāh. Yamānī dirafsh-i hidayat. Published in Mashriq-i Maw'ud, no. 1, 1385 Sh.
  • Azdī al-Nayshābūrī, Faḍl b. Shādhān al-. Mukhtaṣar ithbāt al-rijʿa. Translated by Mir Lawhi. Edited by Basim al-Hashimi. Beirut: Dār al-Karam, 1413 AH.
  • Fakhr al-Rāzī, Muḥammad b. al-ʿUmar al-. Al-Maḥṣūl. Edited by Taha Jabir Fayda al-'Alwani. Muʾassisa al-Risāla, 1418 AH.
  • Fatlāwī, Mahdī al. Rayat al-hudā wa l-ḍilāl fī ʿaṣr al-zuhūr. Beirut: Dār al-Mahja al-Bayḍā ʾ, 1420 AH.
  • Ḥulw, al-Sayyid Muḥammad ʿAlī al-. Al-Yamānī rāyat hudā. Najad: Markaz al-Dirāsāt al-Takhaṣṣusīyya fī l-Imām al-Mahdī, 1425 AH.
  • Ibn Kathīr, Ismāʿīl b. ʿUmar. Al-Bidāya wa l-nihāya. Beirut: Dār al-Fikr, 1407 AH.
  • Ibn Khaldūn, ʿAbd al-Raḥmān b. Muḥammad. Diwān al-mubtadaʾ wa l-khabar fī tārīkh al-ʿarab wa l-barbar wa man ʿaṣarahum min dhawi l-shaʾn al-akbar. Edited by Khalil Shahata. Beirut: Dār al-Fikr, 1408 AH.
  • Ibn Manẓūr, Muḥammad b. Mukarram. Lisān al-ʿArab. Beirut: Dār al-Fikr, 1414 AH.
  • Ibn Ṭāwūs, ʿAlī b. Mūsā. Falah al-sa'il wa najah al-masa'il. Qom: Būstān-i Kitāb, 1406 AH.
  • Khalīfa b. Khayyāṭ. Tārīkh-i Khalīfa b. Khayyāṭ. Edited by Muṣṭafā Najīb Fawwāz and Ḥikmat Kashlī Fawwāz. Beirut: Dar al-Kutub al-ʿIlmiyya, 1415 AH.
  • Kulaynī, Muḥammad b. Yaʿqūb al-. Al-Kāfī. Edited by ʿAlī Akbar Ghaffārī & Muḥammad Ākhūndī. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmīyya, 1407 AH.
  • Laythī al-Wasīṭī, ʿAlī b. Muḥammad al-. ʿUyūn al-ḥikam wa l-mawāʿiz. Edited by Husayn Hasani Birjandi. Qom: Dār al-Ḥadīth, 1376 Sh.
  • Majlisī, Muḥammad Bāqir al-. Biḥār al-anwār. Second edition. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1403 AH.
  • Masʿūdī, ʿAlī b. al-Ḥusayn al-. Al-Tanbīh wa al-ishrāf. Edited by ʿAbd Allāh Ismāʿīl al-Ṣāwī. Cairo: Dār al-Ṣāwī, [n.d].
  • Muqaddasī, Muṭahhar b. Ṭāhir al-. Al-Bidaʾ wa al-tārīkh. Edited by Pur Sa'id. Cairo: Maktaba al-Thiqāfīyya al-Diniyya, [n.d.].
  • Nuʿmanī, Muḥammad b. Ibāḥīm al-. Kitāb al-ghayba. Edited by Ali Akbar Ghaffari. Tehran, Maktaba al-Saduq, [n.d].
  • Ṣadūq, Muḥammad b. ʿAlī al-. Kamāl al-dīn wa itmām al-niʿma. Edited by ʿAlī Akbar Ghaffārī. Tehran: Islāmiyya, 1395 AH.
  • Ṭūsī, Muḥammad b. al-Ḥasan al-. Al-Amālī. Edited by Muʾassisat al-Biʿtha. Qom: Dār al-Thiqāfa li-ṭibaʿat wa al-Nashr wa al-Tawzīʿ, 1414 AH.
  • Ṭūsī, Muḥammad b. al-Ḥasan al-. Kitab al-ghayba li-l-hujja. Edited by Ibad Allah Tihrani and Ali Ahmad Nasih. Qom: Dar al-Ma'arif al-Islamiyya, 1411 AH.