Kuuawa Kwa Nafsu Zakiyya

Kutoka wikishia

Kifo cha Nafsu Zakiyyah (Kiarabu: قتل النفس الزكية) ni moja ya ishara za kudhihiri kwa Imamu Mahdi (a.s), tukio hili linaashiria kuuliwa kwa mtu mmoja kutoka upande wa wafuasi wa Imamu Mahdi (a.s) karibu na Kaaba. Kulingana na Riwaya, Nafs Zakiyyah ni mtu kutoka upande wa kizazi cha Imamu Hussein (a.s) na atauawa kabla ya kudhihiri kwa Imamu Mahdi (a.s) katika Masjid al-Haram.

Kulingana na baadhi ya riwaya, kifo cha Nafsu Zakiyyah kimeorodheshwa miongoni mwa dalili za wazi za kudhihiri kwa Imamu Mahdi (a.s). Mulla Sadiq Mazandarani katika kitabu chake Sharhu al-Kafi ameelezea uwezekano kwamba Sayyid Husayni na Nafsu Zakiyyah wanaweza kuwa ni mtu mmoja, mwenye majina tofauti."

Utambulisho na wasifu wake

Nafsu Zakiyyah (mtu mtoharifu) anatambulishwa kama ni mtu mwema na mchamungu katika riwaya, [1] na kifo chake kinachukuliwa kama ishara ya kudhihiri kwa Imamu Mahdi (a.s). [2] Kulingana na Hadithi, yeye ni mtu atokaye katika kizazi cha Imamu Hussein (a.s) [3] na jina lake ni Muhammad bin Hassan. [4] Nafsu Zakiyyah ni mmoja wa wafuasi wa Imamu Mahdi (a.s), atakaye tumwa na Imamu Mahdi (a.s) kwa ajili ya kuwalingania watu wa Makkah. Imamu Mahdi (a.s) atawaambia wafuasi wake "Watu wa Makkah hawanitaki, lakini nitawatumia mtu ili kutimiza hoja juu yao." Lakini, pale Nafsu Zakiyyah atakapojitambulisha kwao kwamba yeye ni mjumbe wa Imamu Mahdi (a.s), watu watamvamia na kumkata kichwa akiwa katika eneo la Ruknu na Maqamu Ibrahim. [5]

Ishara hakika za kudhihiri kwa Imamu Mahdi (a.s)

Kulingana na hadithi kutoka Imamu Swadiq (a.s), mauaji ya Nafsu Zakiyya sambamba na sauti ya ukelele wa kimbingu, kuzuka kwa Sufiani, kudhihirika kwa Yamani, na tukio la Khasfu al-Baidaa (kudidimia kwa ardhi ya al-Baidaa ya kuhiliki kwa jeshi la Sufiani), miongoni mwa ishara hakika za kudhihirika kwa Imamu Mahdi (a.s). [6] Kulingana na riwaya kutoka kwa Imam Sadiq (a.s) iliyo nukuliwa katika kitabu “Kamalu al-Ddiin” ni kwamba; baina ya tukio la kuuliwa kwa Nafsu Zakiyya hadi tukio la kudhihiri kwa Imamu Mahdi (a.s) ni mausiku kumi na tano. [7] Kwenye moja ya hadithi kutoka kwa Imamu Baqir (a.s), imeelezwa kuwa; eneo la mauaji yake litakuwa ni Masjidi al-Haramu kati ya Maqamu Ibrahim na Ruknu (kona ya Mashariki ya Hajaru al-Aswad). [8] Hata hivyo, katika kitabu cha "Al-Kafi (kitabu)", Mulla Saleh Mazandarani mchambuzi wa kitabu “al-Kafi” alipokuwa akichambua moja ya Hatidhi kuhusiana na suala la kudhihiri kwa Imamu Mahdi (a.s), amekadiria uwezekano wa kwamba; Nafsu Zakiyya ni Sayyid Husseini, ambaye anatambuliwa kama ni alama ya kudhihiri kwa Imamu Mahdi (a.s). [9] Sababu ya kushikamana na msimamo huu, ni Hadithi inayoelezea mauaji ya Sayyid Husseini kupitia mikono ya watu wa Makkah na kutuma kichwa chake kwa Sufiani karibu ya tukio la kudhihiri kwa Imamu Mahdi (a.s). [10]

Tabaka za wanahistoria

Kwa mujibu wa vyanzo vya kihistoria, baadhi ya wafuasi wa Muhammad bin Abdallah al-Mahdhi (aliye fariki mwaka wa 145 Hijria) waliamini kwamba yeye (Muhammad bin Abdallah al-Mahdhi), ndiye Nafsu Zakiyya. [11] Baada ya kuuawa kwa Yahya bin Zaid, baadhi ya watu walimpa yeye kiapo cha kumtambua kama ni khalifa wao, ambaye kwa mtazamo wao yeye ndiye Imamu Mahdi. [12] Ulipofika mwaka wa 145 Hijria, Muhammad bin Abdallah al-Mahdhi aliasi dhidi ya utawala wa Mansur Abbasi na kuuawa katika eneo la Aahjaar al-Zait karibu na mji wa Madina. [13]

Katika baadhi ya Hadithi, pia kuna marejeleo ya kuuawa kwa watu wawili waliojulikana kama ni Nafsi Zakiyya, mmoja ni yule anaye tarajiwa kuuawa huko Makka, na mwingine ni yule aliyetarajiwa kuuawa yeye pamoja na watu sabini huko nyuma ya mji wa Kufa (Najaf). [14] Bwana Korani katika kitabu chake Asaaru al-Dhuhuur ameeleza uwezekano kwamba Sheikh Muhammad Baqir al-Sadri (aliyafariki mwaka wa 1980 Mialadia) ndiye Nafsi Zakiyya aliyetajwa katika Hadithi kuwa atauawa nyuma ya Kufa. [15] Mada zinazohusiana: Kuzuka kwa Sufiani, Ukelele wa Mbinguni, Kusimama kwa Yamani. Kudidimia kwa Ardhi ya Baidaa.

Rejea

Vyanzo

  • Abū l-Faraj al-Iṣfahānī, ʿAlī b. al-Ḥusayn. Maqātil al-ṭālibīyyīn. Edited by Sayyid Aḥmad al-Ṣaqar. Beirut: Dār al-Maʿrifa, [n.d].
  • Kūrānī al-Amilī, ʿAlī al-. Muʿjam al-aḥādīth al-Imām al-Mahdī. Qom: Maʿārif al-Islāmīya inistitute, 1411 AH.
  • Kūrānī, ʿAli. ʿAṣr-i ẓuhūr. Translated by Mahdi Haqqi. Fourth edition. Tehran: International Publishing Co., 1385 Sh.
  • Majlisī, Muḥammad Bāqir al-. Biḥār al-anwār. Beirut: Muʾassisa al-Wafaʾ, 1403 AH.
  • Nuʿmanī, Muḥammad b. Ibāḥīm al-. Kitāb al-ghayba. Tehran, Maktaba al-Saduq, [n.d].
  • Riḍwānī, ʿAlī Aṣghar. Mawʿud shināsī. First edition. Qom: Publication of Masjid-i Jamkran, 1384 Sh.
  • Ṣadūq, Muḥammad b. ʿAli al-. Kamāl al-dīn wa tamām al-niʿma. First edition. Beirut: al-A'lami inistitute, 1412 AH.
  • ʿAyyāshī, Muḥammad b. Masʿūd al-. Tafsīr al-ʿAyyāshī. Edited by Rasūlī Maḥallātī. Tehran: al-Maktaba al-ʿIlmīyya al-Islāmīyya, 1380 Sh.