Dajjal

Kutoka wikishia

Dajjal (Kiarabu: الدجال) ni mtu au kiumbe ambaye ni miongoni mwa maadui wa Imam Mahdi (a.t.f.s). Kutoka au ujio wa Dajjal kwa mujibu wa hadithi zilizopokewa na Waislamu wa Kishia ni katika alama za kudhihiri Imam Mahdi, Imam wa 12 wa Waislamu wa madhehebu ya Shia. Inaelezwa kuwa, Dajjal atadhihiri wakati wa njaa, taabu na mashaka (wakati mambo yakiwa magumu mno) ambapo atawavuta upande wake baadhi ya watu waliohadaika. Hata hivyo, hatimaye Dajjal ataangamizwa na Imam Mahdi (a.t.f.s).

Kwa mujibu wa baadhi ya hadithi na riwaya za Kiislamu ni kwamba, Dajjal atadai uungu na kupelekea umwagaji damu na kuibuka fitina kubwa. Sifa maalumu za kidhahiri za Dajjal zimenukuliwa katika hadithi zilizonukuliwa tu na wapokezi wa hadithi wa Ahlu-Sunna; alama kama jicho lake la kushoto lipo katikati ya paji la uso na kwamba, ni mahiri katika uchawi. Sayyied Muhammad Sadr na Makarem Shirazi miongoni mwa Marajii wa Kishia wanaamini kwamba, Dajjal sio mtu bali ni harakati ya upotofu.

Kujitokeza Dajjal

Katika athari za Waislamu wa madhehebu ya Kishia, kumenukuliwa hadithi kadhaa tu ambazo kwa mujibu wake, ujio wa Dajjal sambamba na Ukelele wa mbinguni, ujio wa Sufyani na harakati ya al-Yamani kwamba, ni moja ya alama za kudhihiri Imamu Mahdi (a.t.f.s).[1] Hata hivyo hadithi hizi hazijatambuliwa kuwa zenye itibari na za kuamika.[2] Katika hadithi zilizopokewa na Waislamu wa Kisuni, kuja Dajjal kumetambuliwa kuwa ni katika ishara na alama za Kiyama.[3]

Vitabu vya hadithi vya Kishia, havijaashiria ujio wa Dajjal na fitina za kabla ya kudhiri Imam Mahdi (a.t.f.s) bali vimzunguumzia tuu suala la kuuawa Dajjal na Imam Mahdi (a.t.f.s) au Nabii Issa (a.s).[4] Hadithi hizi hazizungumzii kabisa maudhui zilizozungumziwa katika hadith za Waislamu wa Kisuni, yakiwemo masuala kama fitina za Dajjal, sura yake na vilevile wafuasi wake. Sheikh Swaduq amenukuu hadithi kutoka kwa Bwana Mtume (s.a.w.w) ambayo kwa mujibu wake, utajo wa Dajjal upo katika watu waliotangulia na uwepo wake upo katika mustakabali.[5]

Kwa mujibu wa hadithi, Dajjal atadhihiri wakati wa njaa, taabu na mashaka ambapo atawavuta upande wake baadhi ya watu waliohadaika.[6] Katika baadhi ya hadithi, pamepatajwa sehemuu ambayo Dajjal atajitokeza na kuibuka ingawa sio kwa uhakika wa mia kwa mia. Maeneo ya kutokeza Dajjal yaliyotajwa katika baadhi ya hadithi ni Isfahan[7] au Khorasan[8].

Wasifu

Kwa mujibu wa hadithi na riwaya za Kiislamu ambazo nyingi kati yazo zimenukuliwa na Waislamu wa Ahlu-Sunna, Dajjal atadai uungu na hilo litapelekea kutokea umwagaji damu na fitina ulimwenguni. Jicho lake la kushoto lipo katikati ya paji la uso na linang'ara kama nyota na kuna kipande cha damu katika jicho lake. Ni mkubwa na mwenye nguvu na ana umbo la ajabu na la kushangaza, na ni mahiri katika uchawi. Mbele yake kuna mlima mweusi ambapo watu wataona mlima huo kuwa ni mkate na nyuma yake kuna mlima mweupe ambapo kutokana na uchawi alioufanya watu wataona kuwa ni maji yenye kutiririka. Atapiga mayowe akisema: Waja wangu! Mimi ni Mungu wenu mkubwa.[9]

Kwa mujibu wa hadithi, Dajjal atauawa na Imam Mahdi huko Kufa au katika eneo moja jirani na Baytul-Muqaddas.[10] Kwa mujibu wa nukuu nyingine Dajjal ataangamia huko Sham.[11]

Neno Dajjal katika lugha ya Kiebrania na katika mafundisho ya Kiyahudi lina maana ya adui wa MNwenyezi Mungu na limeundika kwa maneno mawili ya daj yaani adui na al yaani Mungu.[12]

Dajjal ni Harakati

Sayyied Muhammad Sadr (alikufa shahidi 1377 Hijri) mmoja wa Marjaa Taqlidi na mwandishi wa Kishia ameandika katika kitabu chake cha Tarikh al-Ghaibat al-Kubra kwamba, Dajjal ni neno la siri na nembo inayoasiria harakati ya kikafiri na harakati ya upotofu wa kisiasa, kifikra na kiuchumi. Anasema, umri wa Dajjal ulioashiriwa katika hadithi ni ushahidi wa kuwa sahihi mtazamo huu.[13] Kadhalika Ayatullah Makarem Shirazi, mmoja wa Marjaa wa Taqlidi anaamini kwamba, suala la Dajjal sio kitu kinachohusika na mtu mmoja bali ni anuani jumla kwa ajili ya watu ambao ni wajanja na wenye hila ambao wanatumia kila wenzo kwa ajili ya kuwavuta watu upande wao.[14]

Rejea

  1. Tazama: Hur al-Amili, Ithbat al-Hudat, juz. 5, uk. 354, hadithi no. 46
  2. Allamah Majlisi, Bihar al-Anwar, juz. 52, uk. 193
  3. Tazama: Tirmidzi, Sunan al-Tirmidzi, juz. 4, uk. 507-519
  4. Allamah Majlisi, Bihar al-Anwar, juz. 52, uk. 194 na 308
  5. لدَّجَّالَ اسْمُهُ فِی الْأَوَّلِینَ وَ یخْرُجُ فِی الْآخِرِینَ (Sheikh Saduq, al-Khisal, juz. 2, uk. 457-458, hadith no. 2).
  6. Allamah Majlisi, Bihar al-Anwar, juz. 52, uk. 194 na 308.
  7. Allamah Majllisi, Bihar al-Anwar, juz. 52, uk. 194.
  8. Ibnu Thawus, al-Malahim wa al-Futn, uk. 126
  9. Qummi, Muntaha al-Amal, Babu. 14, Fasli 7, uk. 873-874
  10. Hairi, al-Zam al-Nashab, juz. 2, uk. 172
  11. Nuwri, Al-Najm al-Tsaqib, uk. 185
  12. Tazama: Muhammad Pur, Barresi Tathbiqi Dajjal dar Adyan Iran-e Bastan wa Adyan-e Ibrahimi, uk. 84-85; Khazali, A'lam Qur'an, uk. 478-479
  13. Sadr, Mausuah al-Imam al-Mahdi ajs, juz. 2 uk. 484
  14. Makarim Shirazi, Hukumate Jahani Mahdi ajs uk. 171-172

Vyanzo

  • Hairi, Ali, Ilzām an-Nāshib, Beirut: Muassasah al-A'lami li al-Mathbu'at, 1422 H.
  • Hurr Amili, Muhammad bin Hussein, Ithbāt al-Hudā: Bi an-Nushūsh wa al-Mu'jizah, Pengantar Sayyied Shihabuddin Mar'ashi an-Najafi, Penyunting Ala'uddin A'lami, Beirut: Muassasat al-A'lami li al-Mathbu'at, 1425 H.
  • Ibn Tawus, Ali bin Musa, al-Malāhim wa al-Fitan: At-Tashrīf bi al-Minan wa al-Fitan. Qom: Muassese Shahib al-Amr, 1416 H.
  • Majlisi, Muhammad Baqir, Bihār al-Anwār. Beirut: Dar Ihya' at-Turath al-'Arabi, 1403 H.
  • Makarim Shirazi, Nashir. Hukumat-e Jahani-e Mahdi (a.t.f.s). Qom: Nasl-e Jawan, 1386 HS/2007.
  • Muhammad Pur, Khair an-Nisā' wa Ma'shume Zendiye, Barresi-e Tathbiqi-e Dajjal dar Adabiyat-e Adyan-e Iran-e Bastan wa Adyan-e Ebrahimi, Jurnal Muthale'at-e Qurani, juz: 7, 1390 HS/2011.
  • Nuri, Hussein, Najm Thāqib: Mushtamel Bar Ahwal Imam-e Gha'ib Hazrat Baqiyyatullah Shāhib al-'Ashr wa Az-Zamān, Pengantar Mirza Shirazi. Qom: Entesharat Masjid Jamkaran, 1383 HS/2004.
  • Qummi, Abbas, Muntahā al-Amāl, Qom: Muassese Entesharat-e Hejrat, 1378 HS/1999.
  • Sadr, Sayyied Muhammad. Mausū'ah al-Imām Mahdī (a.t.f.s), Beirut: Dar at-Ta'aruf li al-Mathbu'at, 1412 H.
  • Saduq, Muhammad bin Ali, Al-Khisāl, Penyunting Ali Akbar Ghaffari, Qom: Jami'i Mudarrisin, 1362 HS/1983.
  • Tirmidhi, Muhammad bin Isa, Sunan at-Tirdmidzī. Mhakiki Ahmad Muhammad Shakir, Muhammad Fu'ad Abdul Baqi, Ibrahim Athwah Iwadh. Misry: Sharikat Maktabat wa Mat-ba'at Mustafa al-Babi al-Halabi, 1395 H.