Bayda'

Kutoka wikishia

Makala hii inazungumzia eneo linalojulikana kwa jina la Bayda'. Ili kujua kuhusiana na kuangamia jeshi la Sufiyani katika eneo hili, unaweza kuangalia makala ya Khasf al-Bayda'.

Al-Bayda' au Dhat al-Jaysh ni eneo ambalo kijiografia lipo baina ya Makka na Madina (nchini Saudi Arabia) ambapo jeshi la Sufiyani litaangamia katika eneo hilo mwisho wa zama (Akher Zaman). Kwa mujibu wa riwaya na hadithi mbalimbali ni kwamba, jeshi la Sufiyani litafunga safari na kuelekea huko Makka kwa ajili ya kwenda kupigana vita na Imam Mahdi (atfs) na litakapofika katika eneo hilo kutatokea muujiza ambapo litamezwa na ardhi hiyo ya eneo hilo. Wanazuoni wa Fiqhi wa Kishia wanasema kuwa, ni makuruhu kuswali katika eneo hilo. Kadhalika kwa mtazamo wa wanazuoni hao ni kuwa, ni bora kwa Mahujaji wanaotoka Madina wakielekea Makka wakiwa katika kipando, wacheleweshe kutamka talbiya (kusema Labbaika Allahumma na Labbaika...) mpaka watakapopita katika eneo la al-Bayda'.

Lilipo Eneo la Bayda' na Umuhimu wa Kadhia

Bayda' katika hadithi linaashiriwa eneo ambalo lipo baina ya miji mitakatifu ya Makka na Madina. [1] Ibn Idris Hilli anasema: Umbali wake mpaka Dhul-Hulayfa (Miqati ya watu wa Madina) ni farsakh tatu. [2] Bayda' kilugha ina maana ya jangwa ambalo ndani yake hakuna maji wala majani. [3] Istilahi hii imezungumziwa katika mlango wa alama za kudhihiri Imam Mahdi (atfs) wa vitabu vya hadithi [4] na katika milango ya Swala [5] na Hija [6] katika vitabu vya Fiq'h.

Khasf Bayda', Alama ya Kudhihiri Imam Mahdi (atfs)

Kwa mujibu wa hadithi, Khasf Bayda' ni katika ishara na alama za kudhihiri Imam Mahdi (atfs) [7]. Makusudio ya Khasf Bayda' ni kumezwa na kuangamia jeshi la Sufiyani katika ardhi ya Bayda', jeshi ambalo lilikuwa likielekea Makka kwa ajili ya kupigana vita na Imam Mahdi (atfs). [8] Ni kwa kuzingatia hilo ndio maana katika baadhi ya hadithi, ardhi ya Bayda' imetajwa pia kama Dhat al-Jaysh (mwenye jeshi). [9] Imam Muhammad Baqir (as) amenukuliwa katika hadithi moja akisema: Mwisho wa zama wakati jeshi la Sufiyani litakapoingia katika eneo la Bayda', mwenye kunadi atanadi kutoka mbinguni na kusema: Ewe ardhi, iangamize kaumu hii! kisha ardhi italimeza jeshi la Sufiyani na kisha wote wataangamia isipokuwa watu watatu." [10]

Hukumu za Fiq'h

Katika vitabu vya fiq'h kumezungumziwa hukumu za kisheria kuhusiana na Bayda'. • Kuwa makuruhu kuswali Swala katika eneo hilo: Kwa mujibu wa hadithi zilizonukuliwa katika vyanzo vya fikihi, inaelezwa kuwa, ni makuruhu kuswali Swala katika eneo la Bayda'. • Kuchhelewwesha talibiya (kutamka Labbayka Alahumma Labbayka). Fatuwa ya baadhi ya wanazuoni wa fikihi inasema, ni vyema kwa hujaji anaelekea katika ibada ya Hija akitokea Madina asitamke talbiya mpaka atakapopita katika eneo la Bayda' ndio aanze kufanya hivyo. [13] Talbiya ni kutamka:

(لَبَّیكَ الّلهُمَّ لَبَّیكَ، لَبَّیكَ لاشَریكَ لَكَ لَبَّیكَ، إنَّ الْحَمْدَ وَ النِّعْمَةَ لَكَ وَالْمُلكَ، لاشَریكَ لَكَ لَبَّیكَ)

Hata hivyo baadhi yao wanasema kuwa, hukumu hii ni maalumu kwa hujaji ambaye anaenda Makka akiwa amepanda kipando. [14] Mwandishi wa kitabu cha Swahib al-Jawahir anasema: Wakati Hujaji aliyeko katika kipando anapofika katika eneo la Bayda' ni mustahabu atamke talibiya kwa sauti ya juu. [15]