Nenda kwa yaliyomo

Khasf al-Bayda'

Kutoka wikishia

Makala hii inahusiana na tukio la Khasf Bayda'. Kama unataka kufahamu kuhusiana na sehemu inayojulikana kwa jina hili basi angalia makala ya Bayda'.

Al-Khasf bil-Bayda' au Khasf al-Bayda' (Kiarabu: خسف البيداء) (kumezwa eneo la Bayda') ni katika alama za kudhihiri Imam Mahdi (a.t.f.s) ambapo katika tukio hili, jeshi la Sufiyani litaangamizwa katika eneo la Bayda' (eneo ambalo kijiografia linapatikana baina ya Makka na Madina). Kwa mujibu wa hadithi mbalimbali, jeshi hili litafunga safari kuelekea Makka kwa ajili ya kupigana vita na Imam Mahdi. Katika baadhi ya hadithi tukio hili sambamba na matukio mengine ya ngurumo au sauti kali kutoka mbinguni, kuuawa nafsi takasifu (nafs Zakiya) na kujitokeza Sufiyani ni mambo ambayo yametajwa kuwa ni katika alama za wazi kabisa na zisizo na shaka za kudhihiri Imam Mahdi Mtarajiwa (a.t.f.s).

Khasf Bayda' ni Katika Alama za Kudhihiri Imam Mahdi (a.t.f.s)

Khasf Bayda ni ashirio la kuangamizwa na kumezwa na ardhi jeshi la Sufiyani katika sehemu inayojulikana kwa jina la Bayda' (eneo lililopo baina ya Makka na Madina nchini Saudi Arabia), ambapo jeshi hilo litafunga safari na kuelekea Makka kwa ajili ya kwenda kupigana vita na Imam Mahdi (a.t.f.s). [1] Tukio hili limeelezwa katika hadithi zilizopokewa na Waislamu wa madhehebu ya Shia kwamba, ni miongoni mwa alama za kudhihiri Imam Mahdi (a.t.f.s). [2] Kwa mujibu wa hadithi iliyonukuliwa kutoka kwa Imam Swadiq (a.s) ni kwamba, Khasf Bayda' (kumezwa eneo la Bayda') sambamba na ngurumo au sauti kali kutoka mbinguni, kuuawa nafsi takasifu (nafs Zakiya) na kujitokeza Sufiyan ni mambo ambayo yametajwa kuwa ni katika alama za wazi kabisa na zisizo na shaka za kudhihiri Imam Mahdi mtarajiwa (a.t.f.s). [3]

Tofauti za Hadithi za Ahlu Sunna Kuhusiana na Khasf al-Bayda

Hadithi zilizopokewa na Waislamu wa madhehebu ya Suni kuhusiana na maudhui hii ya Khasf al-Bayda' zimetofautiana: Katika baadhi ya hadithi tukio la Khasf al-Bayda' limetajwa kuwa moja ya ishara za kudhihiri Imam Mahdi (a.t.f.s), [4] huku zingine zikilitaja tukio hilo kuwa moja ya ishara za Kiyama (Ashrat al-Sa'ah) [5]. Katika hadithi kumeashiriwa tu tukio la kumezwa na kuangamia jeshi katika eneo la Bayda' ambalo lilikuwa likilifuatilia kundi lililokuwa limejificha na kuomba hifadhi katika Kaaba. Katika hadithi hizi hakujaashiriwa kabisa suala la kwamba, Khasf al-Bayda' ni katika ishara na alama za kudhihiri Imam Mahdi (a.t.f.s) au kwamba, ni ishara za Kiyama. [6]

Kuafikiana Baadhi ya Aya za Qur'ani na Tukio la Khasf Bayda'

Kwa mujibu wa hadith zilizonukuliwa kutoka kwa Maimamu wa Waislamu wa madhehebu ya Shia ni kuwa, Aya ya 51-52 za Surat Saba'i zinaashiria tukio la kuangamia jeshi la Sufiyani huko Bayda'. Aya hizo zinasema: Na lau ungeliona watapobabaika, basi hapana pa kukimbilia! Na watakamatwa mahala pa karibu. Na watasema: Tunaiamini! Lakini wataipata wapi kutoka huko mahala mbali? Na hapo kabla yake waliikataa, na wakiyatupilia mbali maneno ya ghaibu kutoka mahali mbali.

Tukio Lenyewe

Kwa mujibu wa hadithi iliyopokewa kutoka kwa Imam Muhammad Baqir (a.s) ni kuwa, Sufiyani atatuma kundi la watu huko Madina na Mahdi (a.t.f.s) atatoka pale kuelekea Makka. Kamanda wa jeshi la Sufiyani atafahamishwa kwamba, Mahdi ameondoka na kuelekea Makka. Hivyo atatuma askari wake kumfuatilia. Wakati jeshi la Sufiyani litakapoingia katika ardhi ya Bayda', itasikika sauti kutoka mbinguni ikinadi: Ewe ardhi, iangamize kaumu hii! kisha ardhi italimeza jeshi la Sufiyani na kisha wote wataangamia isipokuwa watu watatu." [8]

Baadhi ya hadithi zinasema kuwa baada ya tukio hilo ni watu wawili tu ndio waliobakia hai. Mmoja alielekea upande wa Imam Mahdi (a.t.f.s) na kwenda kumpa habari ya kuangamia jeshi la Sufiyani. Kuna hitilafu kuhusiana na idadi ya askari wa jeshi la Sufiyani katika tukio hili. Baadhi ya vyanzo vimetaja idadi ya askari hao kuwa ni 12,000 [10] huku vingine vikisema kuwa, walikuwa askari 170,000. [11.

Rejea

Vyanzo

  • Aḥmad b. Ḥanbal. Musnad. Cairo: Muʾassisat Qurṭuba, [n.d].
  • Ḥamawī, Yāqūt ʿAbd Allāh al-. Muʿjam al-buldān. Beirut: Dār al-Ṣādir, 1995.
  • Hāshimī Shahrūdī, Sayyid Maḥmūd. Faqhang-i fiqh muṭābiq bā madhhab-i Ahl al-Bayt. Qom: Muʾassisat Dāʾirat al-Maʿārif al-Islāmī, 1392 Sh.
  • Ibn Abī Shayba al-Kūfī. Al-Musannaf. Edited by Saʿīd al-Liḥām. Beirut: Dār al-Fikr, 1409 AH.
  • Ibn Manẓūr, Muḥammad b. Mukarram. Lisān al-ʿarab. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1408 AH.
  • Ibn Ṭāwūs, ʿAlī b. Mūsā. Al-Malāḥim wa l-fitan. Fifth edition. Qom: Nashr al-Raḍī, 1978.
  • Kulaynī, Muḥammad b. Yaʿqūb al-. Al-Kāfī. Edited by ʿAlī Akbar Ghaffārī. Third edition. Beirut: Dār al-Taʿāruf, 1401 AH.
  • Nahāwandī, ʿAlī Akbar. al-ʿAqbarī l-ḥisān fī aḥwāl mawlānā ṣāḥib al-zamān. Tehran: Intishārāt-i Dabistānī, [n.d].
  • Nuʿmānī, Muḥammad b. Ibrāhīm al-. Al-Ghayba. Edited by ʿAlī Akbar Ghaffārī. Tehran: Maktabat al-Ṣadūq, [n.d].
  • Ṣadūq, Muḥammad b. ʿAlī al-. Al-Khiṣāl. Edited by ʿAlī Akbar Ghaffārī. Fifth edition. Qom: Daftar-i Intishārāt-i Islāmī, 1416 AH.
  • Ṣadūq, Muḥammad b. ʿAlī al-. Kamāl al-dīn. Beirut: Aʿlamī, 1412 AH.
  • Ṣanʿānī, ʿAbd al-Razzāq al-. Al-Muṣannaf. Beirut: al-Majlis al-ʿIlmī
  • Sulaymān, Kāmil. Rūzigār-i rahāyī. Translated by Laṭīf Rāshidī. Tehran: Armaghān-i Ṭūbā, 1386 Sh.