Ukelele wa mbinguni

Kutoka wikishia

Ngurumo, ukelele au sauti kali kutoka mbinguni ni katika ishara na alama zisizo na shaka za kudhihiri Imam Mahdi (atfs). Sauti hii kali itasikika kutoka mbinguni. Kwa mujibu wa hadithi mbalimbali, muhtawa wa sauti hii kali ni kutoa bishara ya kudhihiri Imam Mahdi (atfs), kubainishwa jina la mtukufu Imam Mahdi (atfs) na kwamba, Ushia ni madhehebu ya haki. Mwishoni mwa siku hiyo hiyo, kutasikika pia sauti kutoka kwa shetani ambayo itampa haki Othman bin Affan na wafuasi wake na hilo kupelekea baadhi ya watu kuingiwa na shaka. Katika hadithi kumenukuliwa sifa maalumu za ukelele na sauti ya mbinguni au wito kutoka mbinguni: Mojawapo ni kwamba, watu wote watasikia na kila mmoja atasikia kwa lugha yake na baada ya hapo jina la mtukufu Imam Mahdi litatawala katika ndimi za watu. Kuhusiana na namna ya kutokea tukio hili kuna mitazamno miwili:

• Kundi moja linaamini kwamba, hii ni ishara na alama ambayo itatokea kwa sura ya muujiza.

• Hata hivyo baadhi ya wengine wanasema, yumkini hilo likatokea kwa msaada wa nyenzo za kimaada na hivyo kutokea katika hali ya kawaida.

Ukelele, ishara isiyo na shaka ya kudhihiri Imam Mahdi

Ukelele wa mbinguni, ngurumo na sauti kubwa kutoka mbinguni inaashiria suala la kutokea sauti kutoka mbinguni ambayo itakuwa ni alama ya kukaribia kudhihiri Imam Mahdi. [1] Kwa mujibu wa riwaya na hadithi mbalimbali sauti na kelele hiyo italetwa na Jibril [2] na imetajwa kuwa ni miongoni mwa alama za kudhihiri Mahdi mtarajiwa Imam Mahdi (atfs). [3] Baadhi wanaamini kwamba, hadithi zinazohusiana na hili zimefikia kiwango cha kuwa ni mutawatir kimaanawi. [4] Imeelezwa kuwa, kati ya hadithi 68 zilizotajwa katika kitabu cha al-Ghaibah cha Abu Abdallah Muhammad bin Ibrahim Nu’mani 30 kati ya hizo zinaelezea ishara na alama hii. [5] Katika vitabu vya hadithi Saihat Samaa (ukelele wa mbinguni) imetumika pia kwa neno la al-Nidaa (wito). [6] Katika katika baadhi ya hadithi Aya isemayo:

إِنْ نَشَأْ نُنَزِّلْ عَلَيْهِمْ مِنَ السَّماءِ آيَةً فَظَلَّتْ أَعْناقُهُمْ لَها خاضِعِينَ Tunge penda tungeli wateremshia kutoka mbinguni Ishara zikanyenyekea shingo zao”. [7][8] na Aya isemayo:

“فَإِذا نُقِرَ فِي النَّاقُور”

“Basi litapopulizwa barugumu”[9][10] zimetolewa taawili ya ukelele wa mbinguni.

Kutokuwa na shaka

Kwa mujibu wa hadithi ambayo Sheikh Swaduq ameinuikuu kutoka kwa Imam Swadiq (as) ni kuwa, tukio la ngurumo au sauti kali kutoka mbinguni sambamba na Khasf Bayda' (kumezwa eneo la Bayda') sambamba na ngurumo au sauti kali kutoka mbinguni, kuuawa nafsi takasifu (nafs Zakiya) na kujitokeza Sufiyani na Yamani ni mambo ambayo yametajwa kuwa ni katika alama za wazi kabisa na zisizo na shaka za kudhihiri Imam Mahdi mtarajiwa (atfs). [11] Katika hadithi nyingine, ishara na alama ya kwanza kabisa kati ya hizi imetajwa kuwa ni wito wa mbinguni katika mwezi wa Ramadhani. [12]

Muhtawa na sifa maalumu

Kwa mujibu wa hadithi muhtawa wa mwito wa mbinguni ni kumtambulisha Imam Mahdi (atfs) kwa jina na sifa zake maalumu. [13] Kwa mujibu wa baadhi ya hadithi hizi ni kuwa, katika mwito wa mbinguni na ukele huo kutatambulishwa pia kwamba, haki ipo pamoja na Ali (as) pamoja na Mashia na wafuasi wake. [14] Kadhalika inasimuliwa kwamba, ukelele wa mbinguni utatoa habari pia ya kufikia mwisho wa utawala wa utumiaji mabavu na kuja mtu bora kutoka katika Umma wa Mtume (sawww) na watu huko Makka wataitwa kwa ajili ya kujiunga na Imam Mahdi (atfs). [15]

Sifa maalumu

Katika hadithi kumetajwa sifa maalumu kuhusiana na ukelele wa mbinguni:

• Watu wote kila mmoja atasikia kwa lugha yake. [16]

• Wito na sauti itasikika kutoka mbinguni. [17]

• Itasikika kwa pamoja kwa mtu wa karibu na wa mbali. [18]

• Watu waliokuwa wamelala wataamshwa na wote wataingiwa na woga. [19]

• Hilo litakuwa kwa waumini ni rehema na kwa makafiri ni adhabu. [20]

• Baada ya wito huo, jina la Imam Mahdi (atfs) litatawala katika vinywa na ndimi za watu. [21]

Wakati wa kutokea kwake

Kuhusiana na wakati wa kutokea ukelele wa mbinguni kuna hadithi tofauti: Kwa mujibu wa baadhi ya hadithi sauti na wito huu utatokea kabla ya kudhihiri Imam Mahdi (atfs) [22] na kwa mujibu wa baadhi ya hadithi nyingine ni kuwa, hilo litatokea baada ya kudhihiri Imam Mahdi na kabla ya harakati ya mwokozi huyo mtarajiwa. [24] Kadhalika kwa mujibu wa baadhi ya hadithi, tukio hili litatokea katika mwezi wa Ramadhani, [25] na kwa mujibu wa baadhi ya hadithi nyingine tukio hili litatokea katika mwezi wa Rajab [26] na kwa mujibu wa hadithi nyingine ni kuwa, litatokea katika siku ya Ashura. [27]

Wito wa shetani

Imekuja katika baadhi ya hadithi ya kwamba, mwishoni mwa siku hiyo hiyo, shetani atatoa sauti kwa minajili ya kutia shaka watu katika kumfuata Imam Mahdi (atfs). [29] Shetani ataita akisema: Tambueni kwamba, haki iko pamoja na Othman bin Affan na wafuasi wake. Yeye aliuawa kidhulma. Hivyo simameni na anzisheni harakati kwa ajili ya kulipiza kisasi cha damu yake.” [30] Kundi la watu litaingiwa na shaka kufuatia wito huo. [31] Katika hadithi nyingine inaelezwa kuwa, wito wa shetani utakuwa ni kuwalingania watu Ukristo. [32] Baadhi wanaamini kwamba, hakuna mgongano baina ya makundi mawili ya hadithi zilizotajwa; kwa sababu yumkini kukatokea miito tofauti na harakati mbalimbali kutoka kwa watu na makundi dhidi ya Imam Mahdi (atfs), [33] na inawezekana kunasibishwa miito hiyo na shetani kutokana na kuwa, wito huo utafanyika kwa uchochezi wa iblisi. [34] Kuhusiana na tofauti baina ya mwito wa mbinguni na mwito wa shetani imeelezwa kuwa, ukelele na sauti ya mbinguni itatokea mbinguni na kwa njia zisizo za kawaida na kwa sura na namna ya muujiza kinyume na mwito wa shetani ambao utatokea kwa msaada wa nyenzo za kimaada. [35]

Namna linakavyotokea

Sayyid Muhammad Sadr amesema katika kitabu chake cha Tarikh al-Ghaibat al-Kubra kwamba, baadhi ya alama za kudhihiri Imam Mahdi (atfs) ni kama vile ukelele kutoka mbinguni ambao utatokea kwa sura ya muujiza. [36] Kwa mujibu wa Khodamurad Suleimani mtafiti wa masuala ya itikadi ya Mahdi ni kwamba, kinachofahamika katika hadithi ni kwamba, kutokea sauti na ukelele wa mbinguni kutakuwa kwa sura isiyo ya kawaida. [37] Mkabala na na mtazamo huo, kuna watu waliosema kwamba, ukelele wa mbinguni utatokea kwa kutumia nyenzo na kwa kutumia teknolojia ya kisasa kama satalaiti, jambo ambalo linawezekana kwa sura ya kawaida. Kwa msingi huo, hakuna haja ya kuamini kwamba, kuna ulazima matukio haya yakatokea kwa sura ya muujiza.