Ahlu al-Qibla

Kutoka wikishia

Ahlu al-Qibla (Kiarabu: أهل القبلة) ni kila Muislamu anaye itambua Kaaba kama ndio qibla chake. Matumizi ya msemo huu ni kwa jili ya kuzuia kuwatuhumu Waislamu. Nafsi au roho, Mali na Heshima ya Ahlu al-Qibla, mbele ya wanazuoni wa pande zote mbili za Sunni na Shia ni mambo yanayo stahiki kulindwa na kuheshimiwa na kila mmoja miongoni mwa Waislamu. Kwa msinguu basi, katu haisihi (si halali) kuwatuhumu kwa ukafiri na kuua wateka wao, na ni wajibu kusalia maiti zao bila ya kujali madhehebu yao.

Ufafanuzi na Utambulisho

Ahlu al-Qibla ni mtu aliyejiunga au anaye jinasibisha na dini ya Kiislamu. [1] Kwa hivyo, madhehebu yote ya Kiislamu ambayo yanaizingatia Kaaba kawa ndio qibla chao ni, wote hutambuliwa kama ni Ahlu al-Qibla. [2] Kulingana na kauli ya Muhammad Jawad Maghniyyah, mfasiri wa upande wa madhehebu ya Shia wa karne ya kumi na nne, ni kwamba: istilahi ya Ahlu al-Qibla, ni sawa na istilahi nyengine zote zinazotumika kumaanisha Waislamu kama vile; Ahlu al-Qur'an, Ahlu Shahadataini. Hii imaanisha kwamba istilahi zote hizo zinawalenga Waislamu wote, ambapo humaanisha wale wote ambao wanao muamini Mwenye Ezi Mungu, Mtume wake (s.a.w.w) pamoja na Sunna zake, ambao husali hali wakiwa wameelekea qibla (Kaaba). [3] Vilevile, Mulla Ali Qari kutoka upande wa maulamaa wa madhehebu ya Kihanafi, yeye anamtambua Ahlu al-Qibla kama mtu ambaye hajakataa mojawapo ya misingi muhimu ya dini; kwa hivyo, kulingana naye, ni kwamba; kwa mujibu wa mawazo ya wanazuoni: mtu yeyote yule atayekanusha mojawapo ya misingi mikuu ya dini, kama vile utangu wa milele wa ulimwengu na ufufuo, huyo hahesabiwi kuwa miongoni mwa Ahlu al-Qibla, hata kama atakuwa amejishughulisha maishani mwake mwote katika kazi ya kufanya ibada. [4]

Sheria za Kifiqhi

Maisha (roho), mali, na heshima ya Ahlu al-Qibla inachukuliwa kuwa miko ya Kiislamu mbele ya wanazuoni wengi wa Shia na Sunni. [5] Vilevile, si halali kuwatuhumu kwa sifa ya ukafiri [6] na kuua mateka wao, [7] bali pia ni wajibu na kusalia maiti zao bila kujali madhehebu yao. [8] Kulingana maoni ya Mulla Ali Qari ni kwamba; Abu Hanifa, na Muhammad bin Idris al-Shafi'i, hawakuwa na tabia ya kuwatuhumu Ahlu al-Qibla. [9] Vilevile, amesema kuwa; idadi kubwa ya wanazuoni wa Kisunni hawakuwa wakiwatuhumu Ahlu al-Qibla. [10]

Hata hivyo, katika baadhi matukio fulani ya Kiislamu, wanafuata wa madhehebu mengine wameonekana kuwatuhumu kwa ukafiri na kuhalalisha kuwaua wafuasi wa madhehebu fulani. [11] Muhammad bin Abdul Wahhab, mwanzilishi wa Uwahabi, amehalalisha kuwaua wale wanaomtambua Mitume, Malaika, na mawalii wa Mungu kuwa ni waombezi mbele ya Mungu. Pia kwa mtazamo wake ni halali kuwakufurisha na kuwaua waonafuta ukaribu wa Mwenyezi Mungu kupitia kwa Mtume au walii fulani, hata kama wafanyao hayo watakuwa wamekiri Tauhid ya Rububiyya ya Mwenye Ezi Mungu. [12]

KuhusIana na Nawasib, Khawarij, na Waislamu ambao wamekanusha mambo misingi ya dini, licha ya kutambua kwao Kaaba kama qibla chao, ila Waislamu wametoa hukumu za kuwahisabu kuwa ni miongoni mwa wenye kukufuru [13] na kuwahukumu kuwa ni najisi. [14]

Matumizi ya istilahi ya Ahlu al-Qibla masuala ya kifiqhi

Kuhusiana na matumizi ya Kifiqhi juu ya istilahi ya Ahlu al-Qibla, ni kwamba; istilahi hii imetumika katika hukumu za wafu [15] na hukumu za jihadi [16]. Imeelezwa kwamba Waislamu kabla ya Vita vya Jamal hawakuwa wakijua hukumu za vita na dhidi ya Ahlu al-Qibla, walijifunza hukumu hizo katika vita hivyo kutoka kwa Imam Ali (a.s). [17]

Vyanzo

  • Group of authors. Jahād dar āʾīna-yi riwāyāt. Qom: Zamzam-i Hidāyat, 1428 AH.
  • Mughnīya, Muḥammad Jawād al-. Tafsīr al-Kāshif, Qom: Dār al-Kutub al-Islāmiyya, 1424 AH.
  • Muḥammad b. ʿAbd al-Wahhāb. Kashf al-shubahāt. Saudi Arabia: Wizārat al-Shuʾūn al-Islamīyya, 1418 AH.
  • Muḥaqqiq al-Karakī, ʿAlī b. al-Ḥusayn al-. Jāmiʿ al-maqāṣid fī sharh al-qawāʿid. Qom: Muʾassisat Āl al-Bayt, 1414 AH.
  • Muntaẓirī, Ḥusayn Alī. Dirāsāt fī wilayat al-faqīh wa fiqh al-dawla l-Islāmīyya. Qom: Nashr-i Tafakkur, 1409 AH.
  • Narāqī, Aḥmad b. Muḥammad Mahdī. Rasāʾil wa masāʾil. Qom: Kungira-yi Buzurgdāsht-i Mullā Mahdī Wa Mullā Aḥmad Narāqī, 1422 AH.
  • Qārī, Mullā ʿAlī b. Sulṭān al-. Sharḥ kitāb al-fiqh al-akbar. Beirut: Dār al-Kutub al-Ilmiyya, 1428/2007.
  • Taftāzānī, Masʿūd b. ʿUmar al-. Sharḥ al-maqāṣid. Edited by ʿAbd al-Raḥmān ʿUmayra. Qom: al-Sharīf al-Raḍī, 1409 AH.
  • Ṭūsī, Muḥammad b. al-Ḥasan al-. Al-Istibṣār fīmā ikhtalafa min al-akhbār. Edited by Sayyid Ḥasan al-Khirsān. 1st edition. Tehran: Dar al-Kutub al-Islāmiyya, 1390 AH.
  • Ṭūsī, Muḥammad b. al-Ḥasan al-. Tahdhīb al-aḥkām. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmīyya, 1407 AH.
  • Rustamī, ʿAbbās ʿAlī. Mamnūʿīyyat-i takfīr-i ahl-i qibla az nigāh-i faqīhān wa mutakallimān-i Tashayyuʿ wa Tasannun. In Pazhūhish-hā-yi iʿtiqādāī kalāmī 30 (1397 Sh).