Shahada mbili
![]() | Makala hii inahusiana na wasifu kuhusu mafuhumu na maana ya kifikihi na hivyo haiwezi kuwa kigezo cha amali na matendo ya kidini. Kwa ajili ya amali za kidini, rejea katika vyanzo vingine. |

Shahada Mbili (Kiarabu: الشهادتان) ni kushuhudia na kukiri umoja na upweke wa Mwenyezi Mungu na utume wa Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w) na kukiri pia kukubali tawhidi na upweke wa Mwenyezi Mungu na utume na kwamba vitu viwili hivyo ni miongoni mwa misingi ya dini ya kiislamu. Shahada mbili zinatambulika kuwa ndio mpaka kati ya uislamu na ukafiri. Hivyo basi mtu ambae atatamka shahada mbili, huzingatiwa na kuhesabiwa kuwa ni mwislamu na sharia na hukumu za kiislamu zitatumika kwake au juu yake. Waislamu katika tashahudi ya kila sala na katika adhana na Iqamah hutamka na kusoma shahada mbili.
Mafaqihi na wanazuoni wa kisheria wa kishia wamezungumzia shahada mbili katika milango mbali mbali ya kifiqhi. Kwa mujibu wa fat'wa zao ni kuwa ni wajibu kutamka na kusoma shahada mbili katika sala ya maiti baada ya takbira ya kwanza na kumtamkisha shahada mbili mtu ambae yuko karibu kukata roho na kuziandika juu ya kafan na sanda ya maiti ni jambo la mustahabu.
Shahada mbili katika ujenzi wa kiislamu, fani ya uandishi na utengenezaji wa pesa pia ni sehemu ambazo shahada mbili zimetumika na kuzingatiwa na kutiliwa umuhimu katika maeneo hayo.
Utambulisho
Shahada mbili: Ni kushuhudia juu ya Upweke na umoja wa Mwenyezi Mungu na kukiri na kushudia ujumbe wa Mtume Muhammad (s.a.w.w).[1] kwa mujibu wa maneno ya wanazuwoni wa kifiqhi wa kishia, shahada mbili ni kutamka jumla au sentensi hizi mbili au kuthibiti kwa madhumuni ya sentensi hizi: «أشْهَدُ أنْ لا الهَ الاّ الله وأشْهَدُ أنَّ مُحَمَّداً رَسُولُ اللّه» Nashuhudia ya kwamba hakuna Mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu mmoja na nashuhdia ya kwamba Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Lazima madhumuni ya sentensi mbili hizi yathibiti.[2] Kwa mujibu wa maneno ya sheikh Swadouq ni kuwa shahada mbili ni kukiri na kukubali Tawhidi (Upweke wa Mwenyezi Mungu) na Utume na hii ni misingi miwili kati ya misingi ya dini ya kiislamu.[3]
Thamani ya Kifiqhi na Kisheria
Kwa mtazamo wa waislaam shahada mbili ni mpaka kati ya Uislamu na Ukafiri, kwa maana kwamba mtu ambae atatamka shahada mbili kwa ulimi wake, basi hukumu za kiislamu zitatumika kwake[4] na miongoni mwa hukumu hizo ni kwamba mwili wake utahukumiwa kuwa ni twahara na msafi na nafsi yake na mali yake ni vyenye kuheshimika na kuhifadhika na kulindwa kwa mujibu wa sharia za kiislaam.[5]
Kwa mujibu wa maelezo ya sheikh Swadouq ni kuwa, katika baadhi ya riwaya Imani imefasieiwa kwa maana ya shahada mbili.[6] kwa msingi wa mtazamo na nadharia ya Allamah Twabatwabai (1281-1360 SH) ni kwamba Imani ina daraja kadhaa kiasi kwamba daraja ya kwanza ya Imani, ni kuitakidi na kuamini kwa moyo na kuamini madhumuni ya shahada mbili Imani ambayo itamfanya mtu kutekeleza hukumu mbali mbali za kiislaam (furu'uid-dini).[7]
Katika vitabu vya kifiqhi na kisheria imezungumziwa shahada mbili katika maeneo na sehemu tofauti kama vile hukumu za maiti (Wafu) katika mlango wa Tohara.[8] Tijara na miamala.[9] mlango wa sala.[10] na jihadi.[11]
Desturi na Sheria
- Adabu na hukumu kwa mujibu wa mtizamo na maono ya wanazuwoni wengi wa kisheria wa kishia, kutamka shahada mbili katika sala ya maiti baada ya takbira ya kwanza ni jambo la wajibu. Wanazuwoni wengine wamesema kuwa kufanya hivyo ni sunna.[12]
- Kumtamkisha shahada mbili na uimamu wa maimamu kumi na mbili (a.s) mtu ambae yuko katika hali ya kukata roho ni jambo la mustahabu.[13]
- Na ni mustahabu kuandika shahada mbili juu ya kafan na sanda ya maiti na iandikwe kwamba yeye anashuhudia shahada mbili na ana kiri shahada mbili.[14]
- Wanazuoni wa fiqhi walio wengi, wanasema kuwa kutamka na kusoma shahada mbili katika hotuba za Sala ya Ijumaa kupitia imamu wa jamaa ni jambo la mustahabu.[15]
- Kwa mujibu wa maneno ya Swahibu Jawahiir ni kuwa miongoni mwa adabu za biashara, ni kutamka shahada mbili wakati unapokaa mahala pa biashara.[16]
Matumizi ya Shahada Mbili katika Tamaduni za Kiislamu

Matumizi ya shahada mbili katika mambo yaujenzi na fani za kiislamu. Katika dua na ibada mbali mbali za waislaam ibara za shahada mbili zinamatumizi mengi sana[17] kwa mfano, waislamu huitamka katika tashahudi ya kila sala[18] na pia katika Adhana na Iqamah[19] hutamkwa shahada mbili katika maeneo hayo.
Shahada mbili katika Ujenzi (miimar) ya kiislaam, katika fani ya uandishi na utengenezaji wa sarafu pia ni maeneo ambayo shahada mbili zimetumika.[20]
Rejea
- ↑ Najafiy, Jawaahirul-kalaam, cha mwaka 1404 H, juz. 41, uk. 630.
- ↑ Kama mfano angalia kitabu cha Najafy, Jawaahirul-kalaam, cha mwaka 1404q, j41, ukurasa 630.
- ↑ Angalia kitabu cha Sheikh Swadouq, Manlaa yahdhuruhul-faqiih, cha mwaka 1413 H, juz. 1, uk. 299.
- ↑ Najafiy, Jawaahirul-kalaam, cha mwaka 1404 H, juz. 41, uk. 630, Twabatwabai, Al-mizan, cha mwaka 1417 H, juz. 1, uk. 301-303.
- ↑ Najafiy, Jawaahirul-kalaam, cha mwaka 1404 H, juz. 21, uk. 143.
- ↑ Angalia kitabu cha sheikh Swadouq, Manlaa yahdhuruhul-faqiih, cha mwaka 1413 H, juz. 1, uk. 299-300.
- ↑ Twabatwabai, Al-mizan, cha mwaka 1417 H, juz. 1, uk. 301-303.
- ↑ Najafiy, Jawaahirul-kalaam, cha mwaka 1404q, j12, ukurasa 40, Yazdiy twabatwabai, Al-ur'watul-wuthqaa miizaan, cha mwaka 1409q, j1, ukurasa 417.
- ↑ Kama mfano angalia kitabu cha :Najafiy, Jawaahirul-kalaam, cha mwaka 1404q, j22, ukurasa 452.
- ↑ Kama mfano angalia kitabu cha :Najafiy, Jawaahirul-kalaam, cha mwaka 1404 H, juz. 10, uk. 245,246,264.
- ↑ Najafiy, Jawaahirul-kalaam, cha mwaka 1404 H, juz. 41, uk. 630.
- ↑ Najafiy, Jawaahirul-kalaam, cha mwaka 1404 H, juz. 12, uk. 40.
- ↑ Najafiy, Jawaahirul-kalaam, cha mwaka 1404 H, juz. 4, uk. 14.
- ↑ Najafiy, Jawaahirul-kalaam, cha mwaka 1404 H, juz. 9, uk. 224.
- ↑ Najafiy, Jawaahirul-kalaam, cha mwaka 1404 H, juz. 11, uk. 216, Najafiy, Kashful-ghitwa, cha mwaka 1422 H, juz. 3, uk. 255.
- ↑ Najafiy, Jawaahirul-kalaam, cha mwaka 1404 H, juz. 22, uk. 452.
- ↑ Kama mfano angalia kitabu cha sheikh Tuusiy, Misbahul-mutahajjidi, cha mwaka 1411 H, juz. 1, uk. 15,16,49.
- ↑ Najafiy, Jawaahirul-kalaam, cha mwaka 1404q, j10, ukurasa 245,246.
- ↑ Sheikh Tuusiy, Misbahul-mutahajjid, cha mwaka 1411 H, juz. 1, uk. 29, Najafiy, Jawaahirul-kalaam, cha mwaka 1404 H, juz., uk. 81-82.
- ↑ «مضامین و عناصر شیعی در هنر عصر صفوی با نگاهی به هنر قالی بافی، نگارگری و فلزکاری».
Vyanzo
- Afruugh, Muhammad, (Madhaamiin wa anaasir shii'i dar Honar asri swafawiy boo negaahi be honar qaali boofi), negaargariy wa felezkaarii), Mutwala aati Iraaniy, namba 20, Paaiiz 1390sh.
- Shekhe Swadouq, Muhammad bin Ali, Manlaa yahdhuruhul-faqihi, Qom, Daftar Intishaarat waabaste be Jaamiatul-mudarrisiin Hawzeye ilmiye qom, cha mwaka 1413q.
- Shekhe Tousiy, Muhammad bin Hasan, Misbahul-mutahajjid wa silaahul-muta'abbid, Bairut, Muassase fiqhi shiie, cha mwaka 1411q.
- Shekhe Tousiy, Muhammad bin Hasan, Misbahul-mutahajjid wa silaahul-muta'abbid, Bairut, Muassasatul- fiqhi shiie, cha mwaka 1411q.
- Twabatwabai, Sayyid Muhammad Husein, Al-miizaan fii tafsiril-qur'an, Qom, Daftare intishaaraat islaamiy waabaste be Jaamiatul-mudarrisiin Hawzeye ilmiye qom, cha mwaka 1417q.
- Abbas Zaadeh wa diigaraan, (Bar'rasi naqshe madh'habe shiie bar honar wa miimaari imam zaadegaan iran), Intishare 2 mehri 1395sh, mushaahadeh 30 day mwaka 1398sh.
- Najafiy, Jaafar bin Khudhri, Kashful-ghitwaa an mubhamaatis-shariatil-ghar-raa, qom, Daftar Tablighaat islaamiy Hawzeye ilmiye qom, mwaka 1422q.
- Najafiy, Muhammad Hasan, Jawaahirul-kalaam fii sharhi sharaai'il-islaam, Bairut, Darul-ihyaait-turaathil-arabiy, cha mwaka 1404q.
- Yazdiy Twabatwabaiy, Sayyid Muhammd Kaadhim, Al-urwatul-wuthqaa fiima taummu bihil-bal'waa, Bairut, Muassasatul-aalamiy lilmatbuuaat, cha mwaka 1409q.