Nenda kwa yaliyomo

Kutoharisha

Kutoka wikishia
Isifahamike kimakosa na tohara

Kutoharisha (Kifarsi: تطهیر) maana yake ni kusafisha na kuondoa najisi. Mafakihi wanasema kuwa, endapo baadhi ya vitu vitanajisika kama msikiti, Haram za Maimamu (a.s), nguo na mwili wa mwenye kusali ni wajibu kutoharisha na kusafisha hayo. Maji ni njia iliyoenea zaidi ya vitoharishi na yanasafisha na kuondoa kila najisi. Baadhi ya mutahhirat ni: Jua, ardhi na istihala.

Kwa mujibu wa Fat’wa ya mafakihi kitu ambacho kimenajisika kinatoharika kwa kusafishwa mara moja; lakini katika kusafisha na maji machache, najisi ya mkojo husafika na kutoharika mara mbili na chombo husafika na kutoharika mara tatu. Kadhalika mafakihi wanaamini kuwa, maji yanatoharisha kwa sharti kwamba, yawe halisi, tohara na wakati wa kusafisha najisi yasiwe mudhafu (yawe maji halisi) na baada ya kusafisha kiini cha najisi kiondoke na kisibakie. Hata hivyo, hakuna tatizo kama harufu na rangi itabakia.

Mafuhumu na Nafasi

Kutotahirisha katika lugha maana yake ni kusafisha. [1] Katika mijadala ya fikihi na katika mlango wa najisi, makusudio yake ni kuondoa najisi. [2] Kutoharisha kila kitu ambacho kimenajisika na ambacho kinatumiwa ni jambo linalofaa. [3] Katika baadhi ya mambo na maeneo, mafakihi wanaamini kuwa, ni wajibu kutoharisha na kuondoa najisi; miongoni mwayo ni: Misikiti, [4] Haram za Maimamu (a.s) [5], Qur’an, [6] nguo na mwili katika Sala [7] na tawafu, [8] mahali pa kuweka paji la uso katika sijida wakati wa kusali, [9] viungo vya udhu na ghusli, [10] mwili na sanda. [11]

Katika vitabu vya fikihi, maudhui ya tat’hir (kutoharisha) na kuondoa najisi inajadiliwa sana katika milango ya tohara na Sala. [12]

Tazama pia: Kuondoa Najisi

Mutahhirat (Vinavyotoharisha)

Makala Asili: Mutahhirat

Mutahhirat ni vitu ambavyo kupitia kwavyo najisi huondolewa. [13] Vitu hivi ambavyo vinajulikana kwa jina la vitoharishi au vitu vinavyotoharisha vimegawanyika katika mafungu kadhaa na wanazuoni wa fikihi wamebainisha idadi yake ambayo inafikia mpaka 21. [14]

Baadhi ya vitu vinavyotoharisha ni: Maji, ardhi, jua, istihala (kubadilika utambulisho wa najisi na kisha kuwa chenye kutoharisha kama mbwa akifa na kisha akabadilika na kuwa udongo), kupinduka hali ya kitu (kwa mfano kubadilika pombe na kuwa siki), kuhama, Uislamu (kusilimu kafiri), kumtoharisha mnyama anayekula vinyesi (kumzuia mnyama huyo asile najisi kwa muda fulani) na kutoweka Muislamu. [15] Kila moja kati ya haya ina hukumu maalumu ambayo imebainishwa na kufanunuliwa katika vitabu vya fikihi. [16]

Njia ya Kutoharisha kwa Maji

Maji kwa Waislamu wote ndio njia iliyoenea zaidi ya kusafisha na kutoharisha. [18] Mafakihi wanasema kuwa, kama kitu (kisichokuwa chombo) kitanajisika kwa najisi, (ghairi ya mkojo) baada ya kuondoa kiini cha najisi, kinasafika na kutoharika kwa kuosha mara moja (kwa maji machache au yasiyokuwa machache); [19] lakini kitu ambacho kimenajisika kwa mkojo ili kukisafisha na kukitoharisha ni lazima kioshwe mara mbili. [20] Kwa mujibu wa baadhi ya mafakihi, katika vitu mfano wa nguo na busati ni lazima kukamua ili maji yaliyobakia humo yatoke. [21]

Kwa mujibu wa fat’wa ya mafakihi, ili kusafisha chombo kilichonajisika kwa kutumia maji kidogo ni lazima kukiosha mara tatu; [22] lakini maji ya kuru au maji yanayotiririka na kutembea inatosha kuosha mara moja tu; isipokuwa kama chombo hicho kitakuwa kimenajisika kwa kileo, mbwa au nguruwe. [23]

Hukumu za Kutoharisha

Katika vitabu vya fikihi kumebainisha hukumu na masuala mbalimbali kuhusiana na kutoharisha na kusafisha kitu kilichonajisika. Miongoni mwazo:

  • Katika kutoharisha ni sharti kufanya hivyo kwa nia ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu. [24]
  • Kuwa wajibu kutoharisha katika mambo mengi kama vile kutoharisha nguo kwa ajili ya kusalia, kutoharisha sehemu ya kusujudia na wajibu wa utangulizi; [25] kwa maana ya kuwa wajibu kutoharisha kwa ajili ya kusali; na sio kwamba, ni wajibu kutoharisha nguo yenyewe kama nguo tu.
  • Maji ya kutoharisha na kuondoa najisi yanapaswa kuwa mutlaki na tohara. Kadhalika wakati wa kuosha yasiwe mudhafu na baada ya kuosha kiini cha najisi kiondoke na kusibakie najisi katika kitu kilichokuwa kimenajisika. [26]
  • Kitu kilichonajisika, hakiwezi kusafika na kutoharika mpaka kwanza kiini cha najisi kitakapotolewa; lakini hakuna tatizo kama rangi na harufu vitabakia. Hivyo basi kama damu itaondolewa na kusafishwa kutoka katika nguo, na nguo ikamwagiwa maji lakini rangi yake ikabakia, inakuwa imesafika. [27]
  • Sehemu ya kutokea mkojo (haja ndogo) haitohariki na kusafiki isipokuwa kwa maji tu na kama baada ya kukojoa (sehemu hiyo ikaoshwa mara mbili (hata kama ni kwa maji machache), inasafika. Kundi la baadhi ya mafakihi linaamini kwamba, inatosha kuosha hata mara moja tu. [28]
  • Sehemu ya kutokea kinyesi (haja kubwa) ni bora ikaoshwa na kusafishwa kwa maji; lakini inawezekana pia kuitoharisha kwa kutumia vipande vitatu vya karatasi, jiwe, kitambaa na mfano wa hivyo. [29]
  • Vitu kama nyayo na viatu vinavyogusana na ardhi iliyonajisika, vitatoharika kwa kutembea juu ya ardhi; kwa sharti kwamba, ardhi iwe tohara na kavu na kiini cha najisi kiondoke. Kadhalika ardhi inapaswa kuwa ya udongo, mawe, michoro ya mawe, tofali na mfano wa hayo. [30]
  • Jua linatoharisha ardhi, majengo na mfano wake kama vile milango, madirisha ya majengo yakinajisika vivyo hivyo hutoharisha misumari iliyopigiliwa ukutani na hiyo ni kwa masharti. [31]
  • Kitu ambacho hapo kabla kilinajisika, kama mtu mwenyewe atakuwa na uhakika kwamba, kimetoharika, watu wawili wakatoa ushahidi wa kutoharika kwake au mmiliki wake akatoa habari kwamba, ni tohara, kinahesabiwa kuwa ni tohara na kisafi. [32]
Angalia pia: Kujisaidia

Monografia

  • Mutahhirat Dar Eslam: Mwandishi, Mahdi Bazargan. Kitabu hiki kimechunguza na kufanya utafiti wa hukumu za tohara na usafi katika Uislamu kupitia biokemia na kwa msaada wa kanuni za fizikia na kemia na mifumo ya hisabati.
  • Ahkam Mutahhirat, Najasat va takhali mutabik nazaraat davazdahatan maraajii (Hukumu za vinavyotoharisha, najisi, na kujisaidia, kwa mujibu nadharia za Marajii 12). Kitabu hiki kimeandikwa na jopo la watafiti.
  • Ahkam Mutahhirat, kimeandikwa na Sayyid Ridha Musawi Baigi na Ali Tabatabai. Kitabu hiki hiki ni majimui ya nyaraka kwa mujibu wa vyanzo vya fiq’h kama al-Ur’wah al-Uth’qa, Tahrir al-Wasilah, minhaj al-Salihin, vitabu vya Tawdhih al-Masail (ufafanuzi wa sheria za Kiislamu) na vya fat’wa na tovuti zenye itibari za Marajaii ambacho kimechapishwa na taasisi ya uchapishaji ya Zair Razavi.

Rejea

Vyanzo

  • Imam Khomeini. Tahrir al-Wasilah. Qom: Muasasah Matbu'at Dar al-Ilm, juz. 1, Bita






  • Bahrani, Yusuf bin Ahmad. al-Hadaiq al-Nadhirah fi Ahkam al-Itrah al-Tahirah. Qom: Muasasah al-Nashr al-Islami al-Tab'at al-Jamiah al-Mudarrisin, Bita
  • Bani Hashimi Khomeini, Sayid Muhammad Hussein. Taudhih al-Masail Maraji'. Qom: Daftar Intesharat Islami, juz. 8, 1424 H.
  • Dehkhoda, Ali Akbar. Lugat Nameh Dehkhoda. Teheran: Penerbit Universitas Teheran, 1377 S
  • Hamedani, Agha Ridha. Misbah al-Faqih. Qom: Yayasan al-Ja'fariah li Ihya al-Turats, cet. 1, 1416 HS
  • Imam Khomeini. Tahrir al-Wasilah. Qom: Yayasan Mathbu'at Dar al-Ilm, cet. 1, tanpa tahun
  • Khu'i, Sayid Abu al-Qasim. al-Tanqih fi Syarh al-'Urwah al-Wutsqa. Catatan Mirza Ali Ghurawi. Qom: Cet. 1, 1418 HS
  • Misykini Ardabili, Ali. Musthalahat al-Fiqh. Qom: Dar al-Hadits, 1392 S
  • Yayasan Dairah al-Ma'arif Fiqh Islami. Farhangg-e Fiqh. Qom: Yayasan Dairah al-Ma'arif Fiqh Islami, 1387 S
  • Yayasan Dairah al-Ma'arif Fiqh Islami. Mausu'ah al-Fiqh al-Islami. Qom: Yayasan Dairah al-Ma'arif Fiqh al-Islami, 1387 S
  • Mughniyah, Muhammad Jawad. al-Fiqh ala al-Madzahib al-Khamsah. Beirut: Dar al-Tayar al-Jadid wa Dar al-Jawad, cet. 10, 1421 HS
  • Muhaqqiq Ardabili, Ahmad bin Muhammad. Majma' al-Faidah wa al-Bayan. Qom: Yayasan al-Nashr al-Islami, cet. 1, 1403 HS
  • Najafi, Muhammad Husain. Jawahir al-Kalam. Beirut: Dar al-Ihya al-Turats al-'Arabi, cet. 7, 1362 S
  • Najafi, Muhammad Husain. Majma' al-Rasail (Muhassya), Masyhad: Yayasan Shahib al-Zaman as. cet. 1, 1415 HS
  • Syahid Awal, Muhammad bin Makki. Dzikra al-Syiah fi Ahkam al-Syari'ah. Qom: Yayasan Ali al-Bait, cet. 1, 1377 S
  • Thabathabai Yazdi, Sayid Muhammad Kadhim. al-'Urwah al-Wutsqa. Beirut: Yayasan al-A'lami li al-Mathbu'at, cet. 2, 1409 HS