Ainu Al-Najas

Kutoka wikishia

Ainu Al-Najas (Kiarabu: عین النجس) au Dutu ya najisi; Ni kitu ambacho kiasili na kidhati ni najisi, na hakiwezi kusafika kwa mfumo wowote ule miongoni mwa mifumo ya utoharishaji wa Kiislamu. Kwa mujibu wa nadharia za mafaqihi wa Kishia, ikiwa kitu kichafu kitagusa kitu kilicho safi, huku kimojawapo kikiwa na unyevunyevu, kitu kisafi hicho nacho pia kitanajisika. Kwa mujibu sheria za madhehebu ya Kishia, damu, mkojo, kinyesi, shahawa, nyamafu, mbwa, nguruwe, makafiri, Mvinyo na bia ni najisi.

Welewa wa Dhana

Kwa mujibu wa maoni ya mafaqihi mashuhuri, dhati ya najisi (عین النجس) ni uchafu asili, na kwa mujibu wa Uislamu, haiwezi kusafishwa wala kutakasika. [1] Katika fiqhi ya Shia, kuna vitu kumi ambavyo ni najisi asili, ambavyo huitwa dhati ya najisi au najisi asilia (عین النجس), navyo ni: damu, mkojo, kinyesi, shahawa, nyamafu, mbwa, nguruwe, kafiri, mvinyo na bia. [2] Hata hivyo, Sayyid Murtadha, mmoja wapo wa Mafaqihi wakubwa wa Kishia wa karne ya tano ya Hijiria, anaamini ya kwamba sehemu zisizo na uhai za mbwa na nguruwe ni safi, na sababu usafi wake ni kwa sehemu hizo hazina uhai na zina manufaa fulani. [3] Baadhi ya mafaqihi wategemewa kifatwa, wametowa fatwa ya unajisi wa jasho la ngamia aliyekula najisi. [4]

Hukumu

Katika fiqhi ya Shia, kuna hukumu maalumu zinazojadili masuala ya najisi; Kati yake ni kama ifuatavyo:

  • Najisi asilia ikigusa kitu kilicho safi, kitu hicho safi pia nacho kinakuwa ni najisi, [5] na kitu hicho hitwa Mutanajis مُتَنَجِّس (kitu kililichonajisika). Bila shaka, uambukizaji wa najisi hutimia iwapo moja ya vitu viwili hivyo, kiwe na unyevunyevu, au pia iwapo vyote viwili (najisi asilia na kilicho safi) vitakuwa na hali unyevunyevu. [6] Imenasibishwa kwa Faidh Kashani ya kwamba; baada ya kuondoa najisi asilia kutoka kwenye kitu kilichonajisika (bila kutumia maji, bali hata kupangusa kwa kutumia tishu ), kitu hicho hakituwa na uwezo tena wa najisi kwenye vitu vingine vyenye unyevu. [7]
  • Ni haramu kubeba najisi asilia msikitini ikiwa kitendo hicho kitapelekea kuvunjia heshima msikiti. [8]
  • Ni haramu kula najisi asilia. [9]
  • Iwapo maji yatakutana na najisi asilia, yakabadilika harufu yake, rangi au ladha yake, hata yakiwa na kiwango cha kurru au yanatiririka, maji hayo yatakuwa ni najisi. [10]
  • Ni wajibu kuondoa na kusafisha najisi asilia kutoka katika viungo vyote vya udhu na viungo vyote vinavyokoshwa katika josho la wajibu, kama vile janaba. [11] Katika udhu, inawezekana kuondolewa najisi asilia kabla ya udhu, au wakati wa kuosha au kupangusa viungo vya udhu. [12] Lakini katika josho, ni lazima iondolewe kabla ya josho hilo. [13]
  • Ikiwa mwili au nguo imechafuliwa na damu ambayo ni najisi asilia, ambayo itakuwa ni chini ya ukubwa wa dirham (ukubwa wa kifundo cha kidole cha shahada), hakutakuwa na tatizo kusali na kiwango hicho cha damu. [14]

Masuala yanayo fungamana