Nenda kwa yaliyomo

Kugusa maiti

Kutoka wikishia
Makala hii inahusiana na kugusa maiti. Ili kufahamu kuhusiana na ghusl (josho) angalia makala ya josho la kugusa maiti.

Mass al-Mayyit (Kiarabu: مَسّ المَیِّت) ina maana ya kugusa maiti (mtu aliyefariki) [1] Maudhui ya kugusa maiti huzungumziwa katika mlango wa hukumu za tohara katika vitabu vya Fiq’h.[2]

Hukumu za Kugusa Maiti

  • Fat'wa ya wanazuoni wa fikihi wa Kishia inasema: kugusa maiti (mwili wa mtu aliyekufa) hupelekea ghusl ya wajibu endapo mwili wa maiti huyo utakuwa umeshapoa. Katika hali hii mtu atalazimika kuoga josho linajulikana kama ghusl ya kugusa maiti.[3]
  • Kugusa mwili wa Maasumu, shahidi katika vita na mtu ambaye kabla ya kutekelezwa adhabu dhidi yake (kutokana na kufanya dhambi fulani) au kufanyiwa kisasi alifanya ghusli ya maiti, haipelekei kuoga josho la kugusa maiti.[4] Hata hivyo baadhi ya wanazuoni wa fikihi wamesema kuwa, huenda kugusa maiti ya shahidi kukapelekea kuwa wajibu ghusl ya kugusa maiti.[5]
  • Kwa mujibu wa mtazamo mashuhuri miongoni mwa wanazuoni wa fikihi ni kwamba, kugusa maiti hakubatilishi udhu. [6] Ingawa baadhi ya mafakihi wanaamini kwamba, kugusa maiti kunabatilisha udhu. [7]
  • Fat'wa ya Marajii taqlidi wengi ni kwamba, kugusa kiungo kilichotengana na mwili wa mwanadamu kama kitakuwa na mfupa hupelekea kuwa wajibu ghusli. [8] Mkabala na wanazuoni hao, Ayatullah Ali Sistani anaamini kwamba, kugusa kiungo kilichotengana na mwili hata kama kitakuwa na mfupa na nyama, hilo halipelekea mtu kutakiwa aoge ghusli ya kugusa maiti.[9]
  • Kwa mujibu wa baadhi ya mafakihi ni kwamba, kuoga josho la kugusa maiti kunahitajika tu kwa ajili ya kufanya mambo ya wajibu ambayo kimsingi yanahitajia kuwa na udhu; kama Swala na kugusa maandishi ya Qur'ani. Baadhi wanatambua kitendo cha kugusa maiti kuwa ni hadathi kubwa. Kwa muktadha huo, wanaamini kwamba, ni lazima kuoga ghusl ya kugusa maiti ili kuweza kufanya amali ambazo zinahitajia kuwa na tohara kama Swala, kufanya tawafu na kadhalika.[10]

Rejea

  1. Fadhil al-nakaranii, Risale taudhihul-masail, 1426 Qamarii, uk. 541
  2. Tazama: Tabatabai Yazdi, Al-uruwatul-uthqaa, 1419 Qamarii, juz. 2, uk. 12
  3. Tabatabai Yazdi, Al-uruwatul-uthqaa, 1419 Qamarii, juz. 2, uk. 3; Isfahanii, wasilatu al-najat, 1422 Qamarii, uk. 60
  4. Najafii, Jawahirul-kalam, 1362 Shamsii, juz. 5, uk. 307
  5. Tabrizii Uruwii, Al-tankihu, 1411 Qamarii, juz. 8, uk. 294-298
  6. Tabatabai Yazdi, Al-Uruwat al-Uthqa, 1419 Qamarii, juz. 2, uk. 9
  7. Tabatabai Yazdi, Al-uruwatul-uthqaa, 1419 Qamarii, juz. 2, uk. 9
  8. Tabatabai Yazdi,Al-Uruwat al-Uthqa, 1419 Qamarii, juz. 2, uk. 5
  9. Sistani, Manahij-swalihiin, 1417 Qamarii, juz. 1, uk. 116
  10. Tazama: Tabatabai Yazdi, Al-Uruwat al-Uthqa, 1419 Qamarii, juz. 2, uk. 11; Husseini Amulii, Mafatihul-karama, muasasatu nashri al-islam, juz. 4, uk. 314-317

Vyanzo

  • Fadhil Lankaroni, Muhamamd, Risalah Taudhih al-Masail, Qom, 1426 H.
  • Husseini Amili, Sayyid Muhammad Jawad, Miftah al-Karamah Fi Sharhi Qawaid al-Allamah, Mhariri: Muhammad Baqir Khalishi, Qom, Muassase al-Nashr al-Islami.
  • Isfahani, Sayyid Abu al-Hassan, Wasilah al-Najah, Qom, Sharh, Sayyid Ruhullah Musawi Khomaini, Muasase Tandhim wa Nashr Athar Imam Khomaini, 1422 H.
  • Najafi, Muhammad Hassan, Jawahir al-Kalam Fi Sharhi Shara'i al-Islam, Mhariri: Abbas Qauchani, Beirut, Dar Ihya' al-Turath al-Arabi, 1362 S.
  • Sistani, Sayyid Ali, Minhaj al-Salihin, Qom, Daftar Maktabat Ayatullah Sistani, 1417 H.
  • Tabrizi Ghuruwa, Mirza Ali, Al-Tanqih Fi Sharhi al-Urwat al-Wuthqa taqriran li Bahthi Ayatillah al-Udhma al-Sayyid Abu al-Qasim al-Khui, 1411 H.
  • Tabatabai Yazdi, Sayyid Muhammad Kadhim, Al-Urwat al-Wuthqa, Qom, Muassase al-Nashr al-Islami, 1419 H.