Nenda kwa yaliyomo

Mkopo:Ukimya wa miaka 25 wa Imamu Ali (A.S)

Kutoka wikishia

Ukimya wa Miaka 25 wa Imamu Ali (a.s) (Kiarabu:عزلة الإمام علي (ع) عن السياسة لمدة 25 سنة) Kipindi kijulikanacho kihistoria kama ukimya wa miaka 25 wa Imamu Ali (a.s) kinaelezea wakati wa maisha yake ya tangu kufariki kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) -tukio lililotokea mnamo mwaka 11 Hijria- hadi alipokubali kukamata nafasi ya khalifa mwano mwaka 35 Hijria. Katika kipindi hichi chote, Imamu Ali (a.s) alifanya uamuzi wa kukaa kando na kuepuka kudai haki yake ya uongozi kwa njia ya moja kwa moja. Alifanya hivyo kwa nia ya kulinda maslahi ya dini ya Kiislamu, na kuhakikisha kuwa umoja wa umma wa Kiislamu hauvunjiki. Hivyo basi, aliendelea kushirikiana na kuwapa usaidizi makhalifa watatu waliomtangulia bila pingamizi yoyote.

Baada ya kufariki Mtume Muhammad (s.a.w.w), tukio la mkutano wa Saqifa Bani Sa'ida ulipelekea kuchaguliwa Abu Bakar kuwa Khalifa wa kwanza. Ali bin Abi Talib (a.s) na baadhi ya sahaba walipinga na hawakukubaliana na uamuzi huo. Hata hivyo, Ali (a.s) alikaa kimya kwa miaka 25 kutokana na hofu juu ya usalama Ahlul Bait (a.s) pamoja na Waislamu wengine, na pia kwa lengo la kuzuia mgawanyiko katika jamii ya Kiislamu.

Ni muhimu kutambua kwamba, licha ya hatua yake ya kunyamaza kimya, ila unafunuliwa na uchambuzi wa kihistoria na wa taaluma ya Hadithi unasema kwamba: Imamu Ali (a.s.) alikuwa na msimamo wa kiutendaji wenye uzito wa pekee ndani ya uwanja wa siasa na jamii. Katika kipindi hicho, Imamu Ali (a.s) alionekana kuisadia jamii ya Kiislamu katika mambo mbali mbali. Miongoni michango yake muhimu ndani ya jamii ya Kiislami ni pamoja na; mchango wake katika ukusanyaji wa Qur'ani, kutoa mapendekezo ya kimkakati katika vita vya Waislamu, kuhudumu kama mshauri mkuu kwa makhalifa watatu wa kisiasa, na kujitolea kwake katika shughuli za kijamii za kuwasaidia maskini.

Hadhi na Nafasi ya Kipindi cha Miaka 25 ya Ukimya

Kipindi maarufu cha miaka 25 cha maisha ya Imamu Ali (a.s) alichokaa kimya ndani yake, ni sehemu muhimu ya maisha yake wakati wa utawala wa makhalifa watatu. Akiwa katika kipindi hicho, Imamu Ali (a.s) aliachana na suala la kukidai haki yake ya urithi wa nafasi ya uongozi baada ya bwana Mtume (s.a.w.w). Kipindi hichi kilianza wakati wa Kifo cha Mtume (s.a.w.w) hadi alipokubali kushika nafasi ya ukhalifa, tukio lililojiri mnamo mwaka wa 35 baada ya Hijra.[1] Waandishi wengine wameufasiri ukimya huu wa miaka 25 kama ni mmoja wa mifano hai ya Taqiyyah (kutofichua imani kwa sababu za kiusalama), ambayo ni miongoni mwa tabia ya Maimamu,[2] na hivyo waliifasiri aina hii ya Taqiyyah kuwa ni Taqiyyah inayolenga kuepusha migogoro.[3] Ingawa Imamu Ali (a.s.) katika kipindi hichi hakuruhusiwa kushika nafasi ya ukhalifa, ila kulingana na hadithi kutoka kwa Imamu Ridha (a.s), yeye alikuwa ni Uimamu katika kipindi chote cha maisha yake.[4]

Kwa mujibu wa baadhi ya wachambuzi wa kihistoria, inaonekana kuwepo khitilafu juu ya ukimya huu. Kwa mfano Jawad Muhaddithi, katika kazi yake iitwayo Farhange Ghadeer, anaonekana kupinga vikali dhana ya dhana ya ukimya wa Imamu Ali (a.s) kwa muda wa miaka ishirini na mitano. Akirejelea ushahidi wa kihistoria unathibitisha akisema kwamba; mara kadhaa Imamu Ali (a.s) alionekana kujitokeza na kusimama mbele ya mijadala ya kisiasa ili kuthibitisha haki yake, huku akiwaonya na kuwakosoa viongozi walionyakua utawala (viongozi wa kisiasa) wa wakati ule.[5] Aidha mwanahistoria mwengine mwenye mtazamo kama huo ni bwana Rasul Jafarian, ambaye ameandika akisema kwamba; siku baada ya siku msuguano na mfarakano kati ya Imamu Ali (a.s) na wapinzani wake wa kiutawala ulionekana kuongezeka, hali hiyo lizidi kupamba moto hadi kusababisha matukio makubwa mbali mbali, ikiwemo tukio la uvamizi wa nyumba yake, makasiriko ya Bibi Fatima (a.s) dhidi ya Makhalifa wawili (Omar na Abu Bakar), na hatimaye kifo mapema cha  bibi Fatima kilichojiri ndani ya mzozo huo.[6] Hivyo basi, kwa kuwa suala la kudai haki yake kwa mabavu kungeliathiri malengo yake makuu ya kulinda maslahi ya Uislamu, pamoja na kuhifadhi matunda ya juhudi za bwana Mtume (s.a.w.w), hii ilimpelekea yeye kustahamili na kutoinuka dhidi ya wapinzani wake.[7]

Katika Hotuba yake mashuhuri ya Shaqshaqiyyah, Imamu Ali (a.s) hakuoinekana kujibana na kuto weka wazi ukiritimba uliandaliwa katika tukio la Saqifa, bali alizungumza kwa uwazi wa hali ya juu kabisa kuhusiana na suala la urithi wa uongozi baada ya Mtume (s.a.w.w)[8] huku alilalamika jinsi makhalifa waliomtanguli walivyochukua nafasi hiyo kabla yake.[9] Hotuba hii inatoa mtazamo wake wa kina juu ya historia yote ya utawala wa makhalifa watatu wa kwanza. Pia inaelezea sababu ya kustahamili kwake kwa muda wa miaka 25, na ni nini kilichomfanya hatimaye akubali kushika nafasi ya uongozi.[10] Waandishi wengine wanasema kwamba; pale watu walipoona mapungufu na makosa ya utawala wa makhalifa waliopita kabla yake, ndipo walipogundua thamani ya Ali (a.s) na hekima zake. Hivyo basi, mara tu ya Othman kuuawa, walichukuwa hatua za kumlazimisha Ali (a.s) avunje ukimya wake na akubali kuwa kiongozi wao.[11]

Kuna Somo muhimu mno tunaloweza kujifunza katika kipindi hichi hatari cha miaka ishirini na tano, kipindi ambacho Imamu Ali (a.s) alihiari kustahamili na kujizuia kwa ajili ya udumishaji wa umoja wa Waislamu. Tukio hili ni tukio lenye uzito mkubwa mno kwa Waislamu wa sasa. Kwa kuiga mfano huu wa hali ya juu wa kiuvumilivu, na kujali umoja wa kidini kuliko maslahi ya kibinafsi, Waislamu wanaweza kupata uwezo mkubwa zaidi katika kukabiliana na changamoto mbali mbali za kisasa, pamoja na kuhakikisha kuwa maadui hawakuwa na mwanya wa kuusambaratisha Uislamu[12]

Sababu ya Ukimya wa Imamu Ali (a.s)

Uchunguzi wa kitheolojia wa madhehebu ya Kishia unaonyesha kwamba, ijapokuwa kuna ushahidi wa kutosha wa kihistoria pamoja na maandiko halali yenye kuthibitisha haki ya Imamu Ali (a.s) ya kurithi nafasi ya uongozi baada ya bwana Mtume (s.a.w.w),[13] ila aliamua kukaa kimya bila ya kuchukuwa hatua yoyote ile ya kimkakati katika kudai haki yake. Badala yake alionekana kukaa kimya na hata kutoa ushauri unaohitajika kwa makahlifa waliomtangulia, jambo ambalo lililenga kulinda umoja wa kidini na kuzuia mgawanyiko ndani ya jamii ya Waislamu.[14] Mwanafalsafa Muhammad Taqi Misbah Yazdi anaeleze akisema kwa kwamba; Kulingana na sheria ya mbinguni, Imamu Ali (a.s) alikuwa na haki kamili ya kutawala kwa muda wote wa miaka yote 25 aliokaa kimya ndani. Lakini, kwa kuwa watu hawakushikamana naye wala hawakumnyosha mkono wa kiapo cha kumtii (bai’a), aliamua kukataa kimya bila kutumia mkono wa chuma (nguvu) kuwalazimisha watu waukubali uongozi wake.[15]

Kwa upande mwingine, watafiti wengine wa Kishia kama vile Mehdi Bazargan na Mehdi Hairi Yazdi wanaamini kwamba; njia pekee na yenye kutoa haki na kuhalalisha uongoza wa kiongoni fulani, inapatikana kupitia chaguo na ridha za watu wenyewe. Wao wanasema kwamba; hata Mwenye Ezi Mungu, manabii na Maimamu, hawana haki ya kiasili ya kuwatawala watu bila ridhaa zao.[16] Kupitia mtazamo huu, wanafafanua wakisema kwamba; sababu ya kukaa kimya kwa Imamu Ali (a.s) ilikuwa inatokana na hisia ya kuona kuwa yeye hana haki ya kujitwalisha mwenyewe kwa mwenyewe na kushika uongozi bila kuchaguliwa na umma.[17] Waislamu wa upande wa madhehebu ya Kisunni pia nao wanaamini kwamba; suala la kumrithi bwana Mtume (s.a.w.w) liliachwa mikononi mwa watu wenyewe.[18] Wao wanaamini kwamba; hata Ali (a.s) hakuwa akijiona kuwa ni meteuliwa aliyeteuliwa na bwana Mtume (s.a.w.w) wa kuja kumrithi na kushika nafasi yake. Ndio maana baada ya kifo cha Othman, -mwanzo kabisa- pale watu walipomuomba kushika nafasi ya ukhalifa, alionekana kukataa katakata, ila baada masisitiza lao juu ya kutaka kuwa khalifa, mwishowe akaamua kukubaliana nao.[19]

Kutowepo kwa Waungaji Mkono

Kulingana na chambuzi mbali mbali za kihistoria, sababu kuu iliyomfanya Imamu Ali (a.s) ajizuie (sukut) na aendelee kustahamili bila ya kuchukuwa hatua dhidi ya makhalifa waliotangulia kabla yake, ni kukosekana kwa wafuasi (ansar) wa kumuunga mkono katika hatua za kutafuta haki yake. Jambo ambalo pia linaonekana kuthibitisha na yeye mwenyewe katika Hotuba ya 26 ya Nahj al-Balagha.[20] Aidha dhana hii ni yenye kuungwa mkono moja kwa moja na mkondo wa Hadithi zilizopo katika kitabu cha Al-Amali cha Al-Sheikh al-Tusi, ambapo Imamu Hassan (a.s) analitaja suala la kukosekana kwa ridhaa ya umma (muwafaqat al-nas) kama ndio kipimo muhimu katika maamuzi mbali mbali, ikiwemo  hijra bwana Mtume (s.a.w.w) ya kuhama na kuelekea Madina, kunyamaza na kukaa kimya (sukut), pamoja na maamuzi ya kufanya sulhu na Muawiya (mapatano) katika historia ya Kiislamu.[21]

Wasiwasi wa Ali Juu ya Usalama wa Ahlul-Bait na Umma wa Kiislamu

Ripoti lilizomo ndani ya Nahj al-Balagha, hususan Hotuba namba 26[22] na 217,[23] zinabainisha kwamba hofu ya kuhatarika kwa maisha ya familia ya Imamu Ali (a.s) ndiyo sababu kuu ya ukimya wa Imamu Ali (a.s).[24] Zaidi ya hayo, kulingana na moja ya Hadithi iliyonukuliwa na Ibnu Abi al-Hadid, ambaye ni mmoja wa wachambuzi wenye asili ya Kisunni wa kazi ya Nahj al-Balagha, yaonekana kwamba; pia Ali (a.s) alihofia hatari itakayowakabili Waislamu kwa ujumla na hivyo kuamua kendelea na hali ya kustahamili na kuto chukua hatua maalumu itakayoweza kuhatarisha maisha ya Waislamu hao.[25]

Imamu Ali:
أَفْلَحَ مَنْ نَهَضَ بِجَنَاحٍ أَوِ اسْتَسْلَمَ فَأَرَاحَ هَذَا مَاءٌ آجِنٌ‏ وَ لُقْمَةٌ يَغَصُّ بِهَا آكِلُهَا وَ مُجْتَنِي الثَّمَرَةِ لِغَيْرِ وَقْتِ إِينَاعِهَا كَالزَّارِعِ بِغَيْرِ أَرْضِهِ.‏


Amefaulu yule anayesimama (kuinuka) kwa kuwa na bawa (nguvu au msaidizi), au akasalimu amri akapumzika. Haya ni maji yaliyoharibika (yaliyobadilika ladha), na ni tonge ambalo mlaji wake hukabwa nalo; na anayechuma tunda kabla ya wakati wa kuiva kwake ni kama mkulima anayepanda katika ardhi isiyo yake.

Rejea: Nahj al-Balagha, tahqiq ya Subhi Saleh, 1414 H, Hotuba ya 5, uk. 52.

Ukosefu wa Utayari wa Umma kama Sababu ya Ukimya wa Ali (a.s)

Ibn Maitham al-Bahrani, ambaye ni mwandishi wa kitabu ijulikanayo kwa jina la Misbahu al-Salikin, anajenga hoja zake juu ya msingi wa Hotuba ya 5 ya Nahj al-Balagha, akisema kwamba; Ali bin Abi Talib (a.s) alitambua ukosefu wa masharti yanayofaa ya kurejesha utawala wa Ukhalifa, baada ya tukio la Saqifa lililopora nafasi nafasi yake na kusimamisha misingi mipya kabisa ndani ya Uislamu. Kwa mantiki hiyo, mwandishi huyu anasema kwamba; kudai haki hiyo kungekuwa ni sawa na kuchuma matunda kabla ya msimu wake.[26] Muhammad Taqi Ja'afari, ambaye pia ni msomi, mhakiki na mchambuzi wa Nahj al-Balagha, ana madai yasemayo kwamba; imani iliyokuwepo miongoni mwa watu wa zama hizo, pamoja na uvumi ulikuwa umeenezwa kwamba Ali (a.s) ameridhika na matokeo ya Saqifa, uliuweka umma katika hali ya kutokuwa tayari kuyakaribisha na kuyapokea mamlaka ya Imam Ali (a.s).[27]

Kuulinda Umoja wa Kiislamu na Hatari ya Usambaratikaji

Katika kitabu Al-Fusul al-Mukhtarah, Sheikh Mufidu akitoa tafsiri ya kitheolojia juu ya sababu ya ukimya wa Imamu Ali (a.s), anabainisha kwa kusema; kulinda umoja wa Kiislamu na hofu ya kurudi kwa ukafiri ndiyo sababu za msingi zlilomfanya Imamu Ali (a.s) kunyamaza na kutochukuwa hatua za kudai haki yake kimabavu.[28] Miongoni mwa dalili zilizotumiwa na Sheikh Mufid katika kuthibitishamsimamo huu ni ile Riwaya iliyomo katika kitabu cha Amali.[29] Pia maudhui hii ndiyo kiini cha ibara zilizomo ndani ya barua 62 ya Nahj al-Balagha.[30] Aidaha tukirudi kwenye mazungumzo yaliojiri kati ya Ali na bibi Fatima (a.s) tutakuta kwamba "istimrar al-Islam" (kuendelea kuwepo kwa Uislamu) ndio jambo lililopewa kipaumbele zaidi kuliko haki ya ukhalifa. Kulingana mazungumzo hayo, pale mazungumzo yalipokuwa yakiendelea kujadili haki ya ukhalifa, mara sauti ya adhana ya kuwaita Wailamu waelekee msikini ilipaa angani, baada Imamu kusikia sauti hiyo, aliitumia kama ndiyo hoja msingi iliyomfanya abaki kimya bila kudai madara yake yaliporwa na wale waliotangulia kabla yake. Kwani kusikika kwa adhana hiyo kulionesha uhai wa Uislamu na umoja wa Waislamu wenyewe, na endapo Ali (a.s) angeliamua kutumia nguvu, bala shaka jambo hilo lingilipelekea mgawanyiko kati yao.[31]

Hatari ya Mashambulizi ya Warumi

Mahdi Pishwai, ambaye ni mtafiti wa kihistoria wa kutoka madhehebu ya Kishia, anataja uwezekano wa mashambulizi ya Warumi dhidi ya Waislamu, kama ni sababu nyingine ya ukimya wa Ali (a.s) kwa miaka ishirini na tano.[32] Warumi walikuwa wakiuchukulia Uislamu kuwa ni tishio kubwa kwa usalama wao. Hivyo basi, walikuwa wakitafuta fursa nzuri ya kuwashambulia Waislamu wa wakati huo, na migawanyiko ya ndani miongoni mwa Waislamu ingeweza kuwapa fursa nono ya kuuangamiza Uislamu.[33] Ikumbukwe kwamba, wakati wa zama za bwana Mtukufu (s.a.w.w), Warumi walikabiliana na Waislamu mara tatu.[34]

Kufuata Nyayo za Mitume

Kulingana na iliyonukuliwa kutoka kwa Imamu Ali (a.s),[35] akijibu na kutoa ufafanuzi juu ya maamuzi yake wa katika vipindi mbali mbali, alieleza akisema kwamba; tofauti katika za kimikakati zilizopo kati kukaa kimya wakati wa Makhalifa watatu, na baadaye kusimama na kupigania haki hiyo, ambapo alionekana kusimama na kupambana na Aisha, Talha na Zuberi, ilikuwa ikifuata mifano ya Mitume waliopita. Katika kufafanua suala hilo, alirejelea manabii sita ambao ni; (Ibrahim, Lut, Yusuf, Musa, Harun na Muhammad) walivyochagua kukaa kimya katika hali fulani. Hivyo basi kukaa kwake kulikuwa kukifuata nyayo za Mitume hao. Ufafanuzi huu wake huu unathibitisha kwamba; kuendelea kwa ukimya katika nyakati ngumu si ishara ya udhaifu, bali ni mojawapo ya njia na hekima za Manabii.[36]

Uchambuzi wa Msimamo Tendaji wa Ali Katika Kipindi cha Miaka 25

Mustafa Dilshad Tehrani, mwanahistoria wa Kishia, haukuchukulia ukimya wa miaka 25 wa Imam Ali (a.s) kama ni dalili ya kujitenga au kutowajibika katika kipindi hicho. Badala yake, yeye anaamini kwamba; Imamu Ali (a.s) alitumia kipindi hicho katika kupanga na kuendesha mipango maalum ya kukabiliana na matukio na mabadiliko muhimu yaliyokuwa yakitokea ndani ya jamii ya Kiislamu ya wakati huo.[37]

Ukusanyaji wa Qur'ani

Makala asili: Ukusanyaji wa Misahafu

Mara tu baada ya Mtume (s.a.w.w) kufariki, Ali (a.s) alifanya juhudi za kuzikusanya Aya na Sura zote za Qur'ani na kuziweka katika kitabu kimoja (Msahafu).[38] Hata hivyo, kutokana na kutokubalika kwa Msahafu huo miongoni mwa baadhi ya Masahaba, Imamu Ali (a.s) alilazimika kuuficha na kuuondoa katika matumizi ya hadhara ya Wailamu.[39] Licha ya msimamo wake huo, ila Imamu Ali (a.s) alitambua na kuunga mkono hatua ya Khalifa Othman ya kusanifisha Msahafa mmoja, ambao utakaotambuliwa na Wailamu wote ulimwenguni. Hatua hiyo ya kimsingi ya khalifa wa tatu wa Waislamu, ndiyo sababu ya kuundwa kwa Msahafu wa Othman. Zaidi ya hayo, imethibitika kwamba; Ali (a.s) hakuwa ni mpinzani wa kupingana na Msahafu wa Othamani, bali alizingatia matumizi ya Msahafu huo kuwa ni matumizi halali kabisa, na hata baada ya yeye kushika wadhifa wa Ukhalifa aliendea kuhukumu na kuendesha mambo yake kwa kutumia Msahafu huo huo.[40]

Msimamo wa Ali (a.s) Kuhusu Upanuzi wa Dola (Futuhat)

Makala asili: Upanuzi wa Dola ya Kiislamu

Kulingana na uchambuzi wa Mas’udi, uliomo katika kazi yake mashuhuri iitwayo Muruj al-Dhahab, Imam Ali (a.s) alikataa katakata ombi la Khalifa wa pili (Omar bin Al-Khattab) la kushiriki katika vita dhidi ya Uajemi kwa lengo la upanuzi wa himaya (Dola) ya Kiislamu.[41] Hata hivyo, katika vipindi vya utawala wa Ababakr na Omar, Ali (A.S.) hakikukataa kutoa ushauri wa kimkakati kuhusiana na masuala ya vita na upanuzi wa ardhi ya Kiislamu.[42]

Msimamo wa Ali (A.S) Katika Machafuko Yaliopelekea Kuuliwa kwa Othman

Machafuko na ghasia zilizojitokeza wakati wa utawala wa Othman bin Affan yanatajwa kama matukio yenye athari kubwa zaidi ya kisiasa katika kipindi chote cha miaka 25 ya utawala wa Makhalifa watatu walitawala kabla ya Ali bin Abi Talib (a.s).[43] Mwanahistoria Rasoul Ja'afarian akifafanua machafuko hayo anasema kwamba; Imam Ali (a.s) alikubaliana na sehemu kubwa ya shutuma zilizokuwa zikielekezwa kwa Othman. Hata hivyo, kulingana na na hali ya kisiasa ya wakati huo, aliwajibika kupingana mauaji hayo, akihisi kuwa mauaju hayo yangeliweza kumweka Mu'awiah katika nafasi bora zaidi ya kisiasa.[44] Kutokana na hali hiyo, Ali (a.s) alikuwa na wajibu wa kuwanasihi waasi walioinuka dhidi ya Othamn na kuchukuwa hatua ya kurekebisha kasoro za kiutendaji.[45]

Shughuli za Imamu Ali (a.s) Katika Kipindi cha Ukimya Wake

Ja'far Subhani, mmoja wa wanazuoni wa Kishia wenye mamlaka ya kutoa fatwa za kidini (Marja' at-Taqlid), ameorodhesha baadhi ya shughuli za Imam Ali (a.s) katika kipindi cha ukimya wake kama ifuatavyo:

  1. Kufasiri Qur'ani na kulea wanafunzi maalumu katika faniu hiyo kama vile Ibn Abbas.
  2. Kujibu maswali kutoka kwa wasomi wa pande mbali mbali za ulimwengu, hasa wasomi wa Kiyahudi na Kikristo.
  3. Kutoa hukumu za matukio mapya.
  4. Kuwapa ushauri Makhalifa watatu kuhussiana na matatizo na masuala ya kisiasa.
  5. Kujena waumini safi wenye haisia za kibinadamu.
  6. Kutoa misaada ya kibinadamu kwa ajli ya kusahilisha maisha ya wanyonge.[46]

Mada Zinazo Fungamana

  1. Uongozi wa Imam Ali (a.s)
  2. Hadithi ya Manzila

Rejea

  1. ↑ Rafi'i, Zindegii Aime (a.s), Taasisi ya Utafiti wa Kiislamu, uk. 34-35.
  2. ↑ Ridhwanfar, Farhange Akhlaq Maasumiin (a.s), 1387 S, uk. 400.
  3. ↑ Mousavi, Mabani Fiqhi Taqiye Mudarat, 1392 S, uk. 120; Kamali Ardakani, Pezhuhesh Piramuni Iqtidaa Be Ame, Shirika la Hijja na Ziyarat, uk. 43.
  4. ↑ Sheikh Sadouq, Uyun Akhbar al-Ridha (a.s), 1378 H, juz. 2, uk.a 81-82.
  5. ↑ Muhadisi, Farhange Ghadir, 13, uk. 313-314.
  6. ↑ Ja'farian, Hayat Fikri Siyasa Imaman Shia, 1390 S, uk. 58.
  7. ↑ Pishva'i, Sire Pishvayan, 1397 S, uk. 71.
  8. ↑ Makarim Shirazi, Payam Imam (a.s), 1386 S, juz. 1, uk. 318.
  9. ↑ Bahrani, Sherh Nahjul-Balagha, 1404 H, juz. 1, uk. 251.
  10. ↑ Tazama: Nahjul-Balagha, Tas-hih Subhi Saleh, 1414 AH, Hotuba ya 3, uk. 48-50.
  11. ↑ Zamani, Nahjul-Balagha, 1369 S, juz. 1, uk. 134.
  12. ↑ Jabbari, «Ittihad wa Insijam, Dharurat Tarikh», uk. 4.
  13. ↑ Kwa baadhi ya mifano ya hoja, tazama: Sayyid Murtaza, Al-Dhakhira, 1411 AH, uk. 437-483; Ibn Nawbakht, Al-Yaqut, 1413 AH, uk. 80-86; Homsi Razi, Al-Munqidh Min al-Taqlid, 1412 AH, juz. 2, uk. 299-365; Muhaqiq Lahiji, Gohar Murad, 1383 S, uk. 485-538.
  14. ↑ Danesh, Taamul Imam Ali (a.s) Ba Khulafai Dar Jihat Wahdat Islami», uk. 110.
  15. ↑ Misbah Yazdi, Pasukh Be Purseshha, 1391 S, juz. 1, uk. 29.
  16. ↑ Bazargan, Biisat (2), 1387 S, uk. 298; Ha’iri, Hikmat wa Hukumat, 1388 S, uk. 209-212.
  17. ↑ Bazargan, Biisat (2), 1387 S, uk. 299.
  18. ↑ Taftazani, Sherh al-Maqassid, 1412 H, juz. 5, uk. 262.
  19. ↑ Ibn Abi al-Hadid, ShErh al-Nahjul-Balagha, 1404 H, juz. 7, uk. 34.
  20. ↑ Nahjul-Balagha, Tas-hih Subhi Saleh, 1414 H, Hotuba ya 26, uk. 68.
  21. ↑ Sheikh Tusi, Al-Amaali, 1414 H, uk. 560.
  22. ↑ Nahjul-Balagha, Tas-hih Subhi Saleh, 1414 H, hotuba ya 26, uk. 68.
  23. ↑ Nahjul-Balagha, Tas-hih Sobhi Salih, 1414 AH, hotuba ya 217, uk. 336.
  24. ↑ Pishvai, Sire Pishvayan, 1397 S, uk. 72.
  25. ↑ Ibn Abi al-Hadid, Sherh Nahjul-Balagha, 1404 H, juz. 1, uk. 308.
  26. ↑ Bahrani, Sherh Nahjul-Balagha, 1404 H, juz. 1, uk. 278.
  27. ↑ Ja'fari, Sherh Nahjul-Balagha, 1376 S, hotuba ya 5.
  28. ↑ Sheikh Mufid, Al-Fusul Al-Mukhtara, 1413 H, uk. 258.
  29. ↑ Sheikh Mufid, Al-Amaali, 1413 H, uk. 155.
  30. ↑ Nahjul-Balagha, Tas-hih Subhi Saleh, 1414 H, barua ya 62, uk. 451.
  31. ↑ Ibn Abi al-Hadid, Sherh Nahjul-Balagha, 1404 H, juz. 11, uk. 113.
  32. ↑ Pishvai, Sire Pishvayan, 1397 S, uk. 77.
  33. ↑ Pishvai, Sire Pishvayan, 1397 S, uk. 77.
  34. ↑ Pishvai, Sire Pishvayan, 1397 S, uk. 77.
  35. ↑ Sheikh Saduq, Ilal al-Shara’i, 1385 S, juz. 1, uk. 149.
  36. ↑ Al-Qutit, Waqfah Ma Dk. al-Buti fI Mas’aile, 1417 H, uk. 112-114.
  37. ↑ Dilshad Tehrani, «Kuhusisha ukimya wa miaka 25 kwa Imam Ali (AS) ni makosa», Shirika la Habari la Tasnim.
  38. ↑ Ibn Nadim, Al-Fehrest, 1417 H, uk. 45; Sijistani, Kitab al-Musahif, 1423 H, uk. 59.
  39. ↑ Ma’rifat, Ulum al-Qur’an, 1381 S, uk. 122.
  40. ↑ Ma’rifat, Ulum al-Qur’an, 1381 S, uk. 122.
  41. ↑ Masoudi, Muruj al-Dhahab, 1409 H, juz. 2, uk. 310.
  42. ↑ Ranjbar, «Misimamo ya Imam Ali Dhidi ya Ushindi wa Makhalifa», uk. 62.
  43. ↑ Jafarian, Tarikh Khulafai, 1394 S, uk. 185.
  44. ↑ Jafarian, Tarikh Khulafai, 1394 S, uk. 185.
  45. ↑ Tazama: Ibn Athir, Al-Kamil, 1385 H, juz. 3, uk. 173.
  46. ↑ Subhani, «Vifungu Nyeti kutoka kwa Maisha ya Amiri wa Waumini (a.s): Kwa Nini Miaka Ishirini na Mitano ya Ukimya?», uk. 52-53.

Vyanzo

  • Qur’an
  • Al-Qutayt, Hashim, Waqfah ma‘a al-Duktur al-Buti fi Masa’ilih, Beirut, Dar al-Mahajjah al-Bayda’, 1417H.
  • Ibn Abi al-Hadid, Abdulhamid bin Hibatullah, Sharh Nahj al-Balaghah, Qum, Kitabkhanah Ayatullah Mar‘ashi Najafi, 1404S.
  • Ibn al-Athir, Ali bin Abi al-Karam, Al-Kamil fi al-Tarikh, Beirut, Dar Sadir, 1385H.
  • Ibn Maytham Bahrani, Maytham bin Ali, Sharh Nahj al-Balaghah, Tehran, Daftar Nashr Kitab, chap do, 1404H.
  • Ibn Nawbakht, Ibrahim, Al-Yaqut fi ‘Ilm al-Kalam, Qum, Kitabkhanah Ayatullah Mar‘ashi Najafi, 1413H.
  • Ibn Nadim, Muhammad bin Ishaq, Al-Fihrist, Beirut, Dar al-Ma‘rifah, 1417H.
  • Bazargan, Mahdi, “Akhirat wa Khuda, Hadaf Bi‘that”, Faslnameh Kiyan, shomareh 28, zemestan 1374S.
  • Pishva’i, Mahdi, Sirah Pishvayan, Qum, Mu’assasah Imam Sadiq (a), 1397S.
  • Taftazani, Mas‘ud bin Umar, Sharh al-Maqasid, Qum, Al-Sharif al-Radi, 1412H.
  • Jabbari, Muhammadridha, “Ittihad wa Insijam, Darurati Tarikhi”, dar Majalleh Ma‘rifat, shomareh 114, 1386S.
  • Ja‘fari, Muhammad Taqi, Sharh Nahj al-Balaghah, Tehran, Daftar Nashr Farhang Islami, 1376S.
  • Ja‘farian, Rasul, Tarikh Khulafa az Rihlat Payambar (s) ta Zawal Umaviyan, Qum, Dalil Ma, 1394S.
  • Ja‘farian, Rasul, Hayat Fikri-Siyasi Imaman Shi‘ah, Tehran, Nashr ‘Ilm, 1390S.
  • Ha’iri Yazdi, Mahdi, Hikmat wa Hukumat, London, Nashr Mawj Azadi, 1388S.
  • Himmasi Razi, Sadid al-Din, Al-Munqidh min al-Taqlid, Qum, Daftar Intisharat Islami, 1412H.
  • Danesh, Isma‘il, “Ta‘amul Imam Ali (a) ba Khulafa dar Jahat Wahdat Islami”, dar Majalleh Andisheh Taqrib, shomareh 4, 1384S.
  • Delshad Tehrani, Mustafa, “Intisab 25 sal Sukut, be Imam Ali (a) Ishtibah ast”, Khabargozari Tasnim, 16 Bahman 1392, 1398S.
  • Ridwanfar, Ahmad, Farhang Akhlaqi Ma‘sumin (a), Qum, Markaz Pazhuhesh-haye Islami Seda wa Sima, 1387S.
  • Rafi‘i, Ali, Zendegi A’immeh (a), Tehran, Pazhuheshkadeh Tahqiqat Islami, bi-ta.
  • Ranjbar, Muhsin, “Mawadi‘ Imam Ali dar Barabar Futuhat Khulafa”, dar Majalleh Tarikh Islam wa Ayeneh Pazhuhesh, shomareh 2, 1382S.
  • Zamani, Mustafa, Nahj al-Balaghah, Qum, Al-Zahra’, 1369S.
  • Subhani, Ja‘far, “Farazhayee Hassas az Zendegani Amir al-Mu’minin (a): Bist wa Panj Sal Sukut Chira?”, Mahnameh Dars-hayi az Maktab Islam, sal shanzdahom, shomareh 8, 1354S.
  • Sijistani, Abdullah bin Sulayman, Kitab al-Masahif, Qahirah, Al-Faruq al-Hadithah, 1423H.
  • Sayyid Radi, Muhammad bin Husayn, Nahj al-Balaghah, tashih Subhi Salih, Qum, Hijrat, 1414H.
  • Sayyid Murtadha, Ali bin Husayn, Al-Dhakhirah fi ‘Ilm al-Kalam, Qum, Daftar Nashr Islami, 1411H.
  • Sheikh Saduq, Muhammad bin Ali, ‘Ilal al-Shara’i‘, Qum, Kitabforushi Dawari, 1385S.
  • Sheikh Saduq, Muhammad bin Ali, ‘Uyun Akhbar al-Rida (a), Tehran, Nashr Jahan, 1378H.
  • Sheikh Tusi, Muhammad bin Hasan, Al-Amali, Qum, Dar al-Thaqafah, 1414H.
  • Sheikh Mufid, Muhammad bin Muhammad, Al-Amali, Qum, Kongreh Sheikh Mufid, 1413H.
  • Sheikh Mufid, Muhammad bin Muhammad, Al-Fusul al-Mukhtarah, Kongreh Sheikh Mufid, 1413H.
  • Kamali Ardakani, Hamid, Pazhuheshi Piramun Iqtida’ be ‘Ammeh, Tehran, Sazman Hajj wa Ziyarat, bi-ta.
  • Muhaddithi, Jawad, Farhang Ghadir, Qum, Nashr Ma‘ruf, 1386S.
  • Muhaqqiq Lahiji, Abdulrazzaq bin Ali, Gawhar Murad, Tehran, Nashr Sayeh, 1383S.
  • Mas‘udi, Ali bin Husayn, Muruj al-Dhahab wa Ma‘adin al-Jawhar, Qum, Dar al-Hijrah, 1409H.
  • Misbah Yazdi, Muhammad Taqi, Pasokh be Porsesh-ha, Qum, Mu’assasah Amuzeshi wa Pazhuheshi Imam Khomeini (rh), 1391S.
  • Ma‘rifat, Muhammad Hadi, ‘Ulum Qur’ani, Qum, Al-Tamhid, chap chaharom, 1381S.
  • Ma‘rifat, Muhammad Hadi, ‘Ulum Qur’ani, Qum, Mu’assasah Farhangi Intisharati Al-Tamhid, 1381S.
  • Makarim Shirazi, Nasir, Payam Imam Amir al-Mu’minin (a), Tehran, Dar al-Kutub al-Islamiyyah, 1386S.
  • Musawi, Sayyid Muhammad Ya‘qub, Mabani Fiqhi Taqiyyah Madarati, Qum, Markaz Fiqhi A’immeh Athar (a), 1392S.