Uandishi wa Qur’ani

Kutoka wikishia

Uandishi wa Qur’ani (Kiarabu: كتابة القرآن أو تدوين القرآن) Mada ya Uandishi wa Qur’ani unarejelea harakati za kukusanya na kuiandika Qur’ani katika mfumo ‎mmoja. Uandishi wa Qur’ani ambao unahakikisha Qur’ani inahifadhiwa kutokana na upotoshaji, ni ‎moja ya mambo yalosisitizwa na bwana Mtume (s.a.w.w). Aliwaagiza baadhi ya Masahaba, kama vile ‎Imam Ali (a.s) na Zaid bin Thabit, waandike na kuihifadhi Qur’ani hiyo tukufu. Misahafu ya kwanza ‎kabisa ulimwenguni humu, ni ile iliyo andikwa katika zama za Mahaba. Misahafu maarufu kati yake ni: ‎Msahafu wa Ali bin Abi Talib, Zaid bin Thabit, Abdullah bin Masoud na Ubay bin Ka'b. Ila kuwepo kwa ‎wingi wa Misahafu pamoja na tofauti za nakala za Qur’ani za wakati huo, kulisababisha tofauti miongoni ‎mwa watu. Hiyo ndiyo sababu iliyomfanya Othman bin Affan kuanzisha baraza la kuoanisha Qur’ani na ‎kutoa nakala moja ya Qur’ani tukufu badala ya nakala tofauti. Ni muhimu kutambua kuwa, Qur’ani ‎iliyokusanywa katika mfumo mmoja kupitia barza hizo haikupata upinzani kutoka kwa Maimamu wa ‎Shia, bali nao pia walikubaliana walikubalana nayo bila pingamizi.‎

Qur’ani iliyo andikwa mwanzoni mwa Uslamu iliandikwa kwa mfumo wa kale na kizamani, ambapo ‎iliandikwa bila kuwa na alama za kiuandishi zinazoeleweka hivi sasa, nayo haikuwa na vokali wala nukta ‎ndani yake. Hili lilisababisha watu mbali mbali kufanya makosa katika usomaji wa Qur’ani hiyo. Kwa ‎hiyo, Abu al-Aswad al-Du'ali, Nasr bin Asim na Khalil bin Ahmad al-Farahidi waliongeza nukta na alama ‎za vokali kwenye Qur’ani, walitumia alama hizi ili kurahisisha usomaji wa Qur’ani kwa watu mbali mbali.‎

Uandishi wa Qur’ani umeonekana kuthaminiwa kupitia sanaa mbalimbali kama vile uandishi kupitia ‎nakshi za kuvutia (kaligrafia), uchoraji wa kimapambo, uchora wa kurasa za Msahamu kwa nakshi ‎maalumu, kusanifu majala Misahafu kwa njia tofauti. Kazi hizo zifanywazo na Waislamu mbali mbali ni ‎jitahida ya kutumia kila kitu kiwezekanacho katika kuakisi uzuri wa maandishi ya Qur’anii. Hiyo ndiyo ‎sababu ya wao kubuni hati (font) za aina mbalimbali, ikiwa ni pamoja na hati za Thuluth, Naskh, ‎Rayhan na Nasta'liq. Uandishi wa kutumia hati za Naskh ulipata umuhimu mkubwa kwa sababu ya ‎uwazi wake unaorahisisha kusoma Qur’ani, kumeipa hadhi ya kutambulika kama ndiyo hati zifaazo zaidi ‎katika uandishi wa Qur’ani.‎

Nafasi ya Uandishi wa Qur’ani

Uandishi wa Qur’ani ni miongoni mwa mada za sayansi ya Qur’ani (ulumu al-Qur’ani), [1] inayotafiti ‎ndani yake historia na jinsi kukusanywa na kuandikwa kwa Qur’ani tukufu. [2] Uandishi wa Qur’ani ni ‎miongoni mwa sababu za kuzuia upotoshaji wa Qur’ani, na hiyo ndiyo sababu hasa iliyo mfanya bwana ‎Mtume (s.a.w.w) kusisitiza utekelezaji wa kazi hiyo. [3] Jinsi Qur’ani ilivyoandikwa ina athari ya moja ‎kwa moja katika welewa wa maana ya Aya za Qur’ani tkufu; kama ilivyosemwa, moja ya sababu za ‎uwepo wa maana nyingi na tofauti za Aya za Qur’ani, kunatokana na athari ya kuto andikwa kwa ‎Qur’anii katika zama za mwanzoni mwa Uislamu. [4]‎

Kwa mujibu wa maoni ya watafiti ni kwamba, uandishi au fasihi andishi katika ulimwengu wa Kiislamu ‎ilianza na uandishi wa Qur’ani, na kutokana na uhusiano wa moja kwa moja kati ya hati (fon) na ‎maandiko au uandishi wa Qur’ani, hii ilipelekea suala la hati kulipata umuhimu mkubwa katika ‎ulimwengu wa Kiislamu. [5] Kwa kuibuka kwa Uislamu na kushushwa kwa Qur'ani, hati na uandishi ‎vilianza kupewa umuhimu ndani ya jamii. Lililokoleza rangi katika kazi hii, ni kule Qur’ani kuwa ni ‎muujiza wa bwana Mtume (s.a.w.w), na kwamba usomaji na uandishi wake ni wajibu mtakatifu. [6] ‎

Historia ya Uandishi wa Qur’ani

Wakati wa kuibuka kwa Uislamu, masuala ya hati na uandishi haykuwa ni maarufu miongoni mwa ‎Waarabu wa Hijazi, na ni chini ya watu ishirini miongoni mwa ndiwo waliokuwa wakijua kusoma na ‎kuandika. Hivyo basi ilibidi bwana Mtume (s.a.w.w) kuawaajiri wale waliokuwa na ujuzi wa kusoma na ‎kuandika miongoni mwa Masahaba wake wafanye kazi ya kuandika wahyi, huku akiwahimiza Waislamu ‎kujifunza kusoma na kuandika. [7] Mtume (s.a.w.w) kando na kuhifadhi Qur’ani, pia aliipa umuhimu ‎kazi ya kuandika Qur’ani, na aliwaagiza watu maalumu kama Ali bin Abi Talib na Zaid bin Thabit ‎kuiandika Qur’ani hiyo. [8] Wakati wa za mwanzo za Uislamu, Masahaba walikuwa wakiandika Qur’ani ‎kwenye ngozi za wanyama, makozi ya mitende, mifupa mipana, na kwenye karatasi. [9]‎

Misahafu ya Kale Zaidi

Qur'ani yenye hati ya mkono inayohusishwa na Imam Ali (a.s.)

Ibn Nadim, mwanazuoni wa karne ya nne Hijria, katika kitabu chake cha Al-Fahrist, alimtaja Imam Ali ‎‎(a.s) kuwa ndiye aliye andaa msahafu wa kwanza kabisa katika uislamu. [10] Baada ya kufariki kwa ‎bwana Mtume (s.a.w.w), Imam Ali (a.s) alikusanya Qur’ani katika msahafu mmoja kwa mpangilio wa ‎kushushwa kwake na kuwaonyesha Masahaba na watu mbali mbali. [11] Baadhi ya Masahaba ‎hawakuukubali musahaf huu, na kwa sababu hiyo, Imam Ali (a.s) aliuficha na kuuondoa mwa watu. ‎‎[12]‎

Baada ya Mtume (s.a.w.w) kufariki na kutokubaliwa kwa msahafu wa Imam Ali (a.s), Masahaba kadhaa ‎walijishughulisha na kazi ya kukusanya Qur’anii kwenye Msahafu mmoja. Miongoni mwa Masahaba ‎waliofanya kazi hiyo ni pamoja na Zaid bin Thabit, Abdullah bin Masoud, Ubayya bin Ka'ab, Miqdad bin ‎Aswad, Salim Mawla Abi Hudhayfa, Ma'adh bin Jabal na Abu Musa Ash'ari. [13]‎

Kotoa Toleo la Msahafu Mmoja

Makalah kuu: Mus'haf wa Othman
Picha ya nakala ya Qur'ani huko Misri, ambayo inadaiwa kutoka katika misahafu ya Othman.

Masahaba walikuwa na misahafu mbalimbali waliyoiandika kwa ajili ya matumizi yao wenyewe, ‎ambayo kila mmoja ulikuwa ni tofauti na mwingine. Tofauti hizi katika misahafu hiyo pamoja na ‎khitilafu za kiusomaji zilizopo baina yao, zilisababisha migogoro mikubwa miongoni mwa watu. [14] Hii ‎ndiyo sababu iliyo mfanya Othman (Khalifa wa tatu), kuoanisha misahafu hiyo ili kupata muwafaka wa ‎toleo moja tu. [15] Kwa ajili ya kazi hii, Masahaba kumi na mbiili, wakiwemo Zaid bin Thabit, Abdullah ‎bin Zubair na Abdullah bin Abbas, chini ya uongozi wa Ubayya bin Ka'ab walikusanya Qur’ani zilizopo ‎mikononi mwa watu mbali mbali na kutengeneza toleo moja tu. [16]‎ Hata Imamu Ali (a.s) pia alikubaliana na Qur’ani iliyokusanywa katika toleo moja hilo, na pia aliposhika ‎nafasi ya Khalifa, alijitolea kufuata na kushikamana na Qur’ani hiyo. [17] Hata Maimamu wa waliofuata ‎Baada ya kufariki kwa Imamu Ali (a.s), pia nao waliiunga mkona Qur’ani ya Othman huku wakisisitiza ‎umuhimu wa kuhifadhi Qur’ani. [18]‎

Kuenea kwa Uandishi wa Qur’ani

Katika enzi za utawala wa Safawi huko Iran na Othmaniyya huko Uturuki, Suala la uandishi wa Qur’ani ‎lilipewa kipau mbele mno ndani ya twala mbili hizo. [19] Qur’ani zilionekena kuandikwa kwa mitindo ‎tofauti; ikiwemo mtindo kuandika Qur’ani kiukamilifu, katika mfumo wa mijalada mine, mijalada kumi ‎na tano, na mijalada thelathini na wakati mwengine mijalada sitini. Ila mtindo huo ulififia polepole, na ‎hatimae Qur’ani zote zikaanza kuandikwa kwa ukamilifu kwenye mjalada mmoja. [20] Katika zama za ‎kuenea sanaa na kazi za uchapishaji wa vitabu, Qur’ani zilizochapishwa kupitia viwandani nazo zilianza ‎kutumika na kuenea dunianai, mwishowe desturi ya kuandika Qur’ani kwa mkono ikaanza kufifia na ‎kupungua kasi. [21] ‎

Mfumo wa Hati za Uandishi wa Qur’ani

Neno «Rasmu al-Mus'haf» linarejelea mwandiko maalum wa Masahafu wa Othman. Maneno ya Qur’ani ‎Katika msahafu huu, yameandikwa kinyume na kanuni za uandishi wa kawaida wa hivi sasa, kuwahiyo ‎utakuta kuna tofauti za kiuandishi zilizomo ndani yake; [22] kama vile kuandikwa kwa neno «‎الصلوٰة» ‎‎[23] badala ya «‎الصلاة‎» na «‎‎ابرٰهــٖم» [24] badala ya «‎ابراهیم‎». [25] Kuna kanuni sita zilizotumika katika Rasmu ‎al-Mus'haf, ambazo ni; kanuni ya kufuta (kupunguza), ya kuongeza, kanuni inayohusiana na hamza, ‎kubadilisha, kuunganisha, na kutenganisha, ambazo zote hazifuati kanuni za uandishi wa kawaida au ‎uandishi mashuhuri. [26] Kwa mtazamo wa baadhi ya watafiti wa Qur’ani, mwandiko au uandishi wa Othman umepewa ‎umuhimu mkubwa, kiasi ya kwamba ikiwa msomaji atasoma tofauti na mwandiko huo, hupaswa ‎kurekebishwa. [27] Kwa mujibu wa watafiti, ni kwamba; makosa ya waandishi wa wahyi, mwandiko ‎wa usio wa kitaalamu (mchanga) wa mwanzo wa Uislamu, na athari za tofauti za usomaji wa Qur’ani, ni ‎miongoni mwa sababu za kutokubaliana kwa Rasmu al-Mus'haf na kanuni za uandishi wa kawaida. [28] ‎Kinyume chake, baadhi ya Masunni wanaamini kuwa; mwandiko wa Qur’ani ni «tawqifi au marufuku isiyoruhusu mabadiliko», yaani wanaamini kuwa; bwana Mtume (s.a.w) ndiye aliye wafundisha ‎Masahaba jinsi ya kuandika maneno yaliyomo kwenye Qur’ani, amfundisho ambayo asili yake ilikuwa ‎ni wahyi utokao kwa Mwenye Ezi Mungu mwenyewe. [29]‎

Kuna maoni tofauti kuhusuiana na uhalali wa kubadilisha maandishi ya Rasmu al-Mus'haf, maoni ya ‎yaliyowasilishwa kuhusiana na tofauti hizo ni kama ifuatavyo:‎

  • Si halali kuleta aina yoyote ile ya mabadiliko kwenye Msahafu huu, Hii ni kwa kuzingatia kuwa; Rasmu ‎al-Mus'haf ni "tawqifi marufuku isiyoruhusiwa kutiwa mkono», kwa sababu ya kwamba mfumo huo ‎unatokana na mafunzo ya bwana Mtume (s.aw.w.) kupitia wahyi. [30]‎
  • Ingawa Rasmu al-Mus'haf sio «tawqifi", ila Msahafu huu unapaswa kubaki kama ulivyo, hii ni kwa ajili ‎ya kujenga umarufuku wa kuzuia mabadiliko mengine yasiweze kutokea katika Qur’ani hii. [31]‎
  • Hakuna ulazima na wajibu wowote ule wa kushikamana au kuwa ni wahafidhina wa Rasmu al-‎Mus'haf, bali Qur’ani yaweza kuandikwa kwa mwandiko mwingine usiokuwa huo. [32] ‎
  • Kwa sababu ya kutoelewa kwa watu wa wakati huu kuhusu Rasmu al-Mus'haf na ili kuzuia kusomwa ‎vibaya kwa Qur’ani, Qur’ani inapaswa kuandikwa kwa njia ambayo inaweza kusomwa kwa usahihi; ‎hivyo, haipaswi kuandikwa kwa kufuata Rasmu al-Mus'haf. [33]‎

Nasir Makarim Shirazi, mwandishi wa tafsiri ya Tafsir Nemooneh, yeye anaona kuwa; ni muhimu ‎kubadilisha Rasmu al-Mus'haf na kuandika kwa mwandiko wa kileo zaidi. [34]‎

Mabadiliko ya Uandishi wa Qur’ani

Katika kipindi cha uhai wa Mtume (s.a.w.w), Qur’ani iliandikwa kwa mwandiko wa hati (font) za Kihijazi ‎‎(ambao unafanana na mwandiko wa Naskh wa karne ya tano Hijiria). [35] Baada ya kuanzishwa kwa mji ‎wa Kufa mnamo mwaka 17 Hijri na kuenea kwa mwandiko wa Kufi, Qur’ani iliandikwa kwa mwandiko ‎wa Kufi. Katika kipindi hicho Misahafu yote ya zama hizo, (ikiwemo misahafu ya awali iliyoandikwa ‎wakati wa Othman amabayo ilikuwa ndiyo Misahafu mama irejewayo na waandishi wa Qur’ani mbali ‎mbali) iliandikwa kwa hati za Kufi. [36] Qur’ani zilizoandikwa awali hazikuwa na alama za nukta wala ‎vokali, jambo ambalo lilisababisha makosa katika usomaji wa Qur’ani hiyo. [37]‎

Abu al-Aswad al-Du'ali na Harakati za Qur’ani

Nakala ya Qur'ani yenye hati ya mkono, yenye mafungamano na Karne ya Kwanza Hijria, unaweza kuiona Aya ya 43 na 56 ya Surat Nisaa.

Abu al-Aswad al-Du'ali (aliyefariki mwaka 69 Hijria) ndiye mtu kwanza kabisa kuweka alama za fatha, ‎kasra na dhumma katika Qur’ani, aliifanya kazi hiyo kupitia mwongozo na amri ya Imam Ali (a.s), ila ‎yeye hakutumia alama za kawaida za vokali zilizo zoeleka hivi sasa, bali alitumia alama za nukta. [38] ‎Alama ya fathah ilikuwa ni nukta juu ya herufi, alama ya kasrah ilikuwa ni nukta chini ya herufi, na alama ‎ya dhammah ilikuwa ni nukta mbele ya herufi, na hizi nukta ziliwekwa kwa rangi tofauti na maandiko ya ‎asili ya Qur’ani. [39]‎ Baada ya Abu al-Aswad, mwanafunzi wake Nasir bin Asim (aliyefariki mwaka 89 Hijri) alikuja na fikraa ‎mpya katika kuendeleza kazi hii. Yeye aliamua kutumia tena nukta ili kutofautisha herufi zenye nukta ‎zile zisito na nukta. Ili kuepuka kuchanganya nukta hizi na zile zilizowekwa na mwalimu wake ambazo ‎zilikuwa zikiwakilisha vokali za herufi za Qur’an, yeye aliziandika nukta zake kwa rangi ya maandiko asilia ‎ya herufi za Qur’ani. [40]‎ Baada ya muda, Khalil bin Ahmad al-Farahidi (aliyefariki mwaka 175 Hijria) alikuja na mfumo ‎mwenngine mpya, ambapo alizibadilisha nukta zilizotumiwa na Abu al-Aswad kwa ajili ya vokali na ‎kutumia alama nyengine za vokali. Yeye alitumia ‎ــَـ‎ kwa jili ya fathaha, alama ya ‎ــِـ‎ kwa ajili ya (kasrah), ‎na alama ya ‎ــُـ‎ kwa ajili ya (dhammah). Pia aliongeza alama za shadda, hamza, na nyenginezo ili ‎kurahisisha usomaji wa Qur’ani. [41]‎

Waislamu katika karne ya kwanza Hijria waliweka kipaumbele mno suala la uandishi wa Qur’ani na ‎walijitahidi kurekebisha njia za uandishi. [42] Katika karne ya nne, mbinu za uandishi wa Qur’ani ‎zilikuwa nyingi na zenye mifumo mbalimbali. Kulijitokeza na zaidi ya mitindo ishirini ya uandishi katika ‎ulimwengu wa Kiislamu. [43] Utofauti huu wa mitindo ulisababisha matatizo kwa waandishi na ‎wasomaji wa Qur’anii. [44] Kwa sababu hii, Ibn Muqla (aliyefariki mwaka 328 Hijria) alijitahidi ‎kurekebisha mitindo hii, [45] na hatimae kuwe kanuni maalumu za kiuandishi kuhusiana na aina sita ya ‎hati ambazo zilizokuwa zikitumika kuandikia Qur’ani, ambayo ni (1. Thuluth, 2. Muhaqqaq, 3. Rayhan, 4. ‎Naskh, 5. Tawqi, 6. na Ruq'ah) . [46]‎

Sanaa na Uandishi wa Qur’ani

Ukiachilia mbali juhudi za uandishi wa Qur’ani katika zama mbali mbali za Uislamu, pia uandishi wa ‎Qur’anii uliweza kuakisiwa katika sanaa mbali mbali, kama vile; kaligrafia, upambaji wa hati kwa rangi za ‎kupendeza, usanifu wa kurasa za Qur’ani na ufumaji wa majalada ya Qu’ran. [47] Waislamu walitumia ‎kila kitu kinacholeta uzuri katika uandishi wa matini ya Qur’ani, miongoni mwa mbinu hizo ni kutia rangi ‎na kuisanifu Qur’anii kwenye karatasi kwa mfumo wa kupendeza). [48] Kwa mujibu wa watafiti, ni ‎kwamba; Sanaa ya uandishi wa Qur’ani ni sanaa yenye umuhimu mkubwa kuliko sanaa nyingine, hii ni ‎kwa sababu sanaa hii ni sanaa inayoakisi maneno ya ufunuo kwa wasomaji na kujumuisha dhana za ‎kidini ndani yake. [49] Uandishi wa Qur’ani ulifikia kilele chake katika kipindi cha Ilkhani (Ilkhanate) ‎‎(karne ya saba Hijria), na Qur’ani zilizoandikwa katika kipindi hicho zina thamani kubwa mno katika ‎hifadhi za nyaraka, kwani zilikuwa ni Qur’anii zenye ukamilifu zaidi kwenye upande wa mapambo ya ‎rangi pamoja na hati. [50]‎

Uandishi kwa Mfumo wa Kaligrafia

Surat al-Fatiha iliyoandikwa kwa maandishi ya aina yake na mwandishi Mir Imad Hassani Qazvini.

Uandishi wa kaligrafia ni sanaa ya kuandika maandiko kwa njia ya kuvutia na yenye umbo maalum. ‎Ibn Muqla (aliyefariki mnamo 328 Hijria) alibuni aina (hati) sita za maandishi kaligrafia ambazo ni: ‎Thuluth, Muhaqqaq, Rayhan, Naskh, Tawaqi, na Ruq'ah. [51] Ibn Muqla alibuni herufi kulingana na ‎kanuni za jiometri na akabuni alama za herufi kulingana na kanuni za "sat-hu" (alama za herufi ‎zilizorefuka kama Alif na Ba) na "daur" (alama za herufi za mduara kama Jim na Nun). [52] Baada ya Ibn ‎Muqla, Ibn Bawwab katika karne ya tano kisha Yaqut Musta'simi katika karne ya saba, walikamilisha na ‎kuboresha maandishi hati (font) ya Naskh, na kuiarifisha fonti hii kuwa ndio fonti inayofaa zaidi kwa ‎katika uandishi wa Qur’ani. [53]‎ Maandishi ya Naskh yaliibuka na kudhihiri kwa mitindo tofauti, muhimu zaidi ya mitindo hiyo ni; mtindo ‎wa Kiarabu, Kituruki, na Kiajemi. [54] Katika enzi za utawala Timurid (Taimurian) nchini Iran, sanaa ya ‎kaligrafia ilipitia mabadiliko makubwa ya uborefu ndani. [55] Katika kipindi hichi, kwa kuchanganya hati ‎za Riq'ah na Tawqi ilizaliwa hati (font) mpya iitwayo Taliq, kisha kwa kuchanganya maandishi (hati) za ‎Naskh na Taliq ilizaliwa hati (font) ya Nastaliq. [56] Waislamu nchini India nao hawakuwa nyuma katika ‎usanifu wa maandishi ya Qur’ani, bali nao pia walitumia sanaa yao ya uandishi katika kazi ya uandishi wa ‎Qur’anii. Wao waliandika Qur’ani kwa maandishi (font) ya Bihari (Bihari script font), na nchini China ‎ikaandikwa kwa maandishi ya Sini (ambayo ni aina maalum ya Naskh). [57]‎

Hati (font) za Naskh zimekuwa na umuhimu mkubwa katika uandishi wa Qur’ani, hii ni kutokana na ‎uwazi pamoja na urahisi wa usomekaji wake. [58] Qur’ani iliyoandikwa na Musta'simi mnamo mwaka ‎‎669 Hijria, ni Qu’ran iliyo andikwa kwa maandishi ya Thuluth, Naskh, na Rayhan. [59] Qur’ani ‎iliyoandikwa na Ahmad Nayrizi ndiyo maarufu zaidi miongoni mwa Qur’anii zilizo andikwa kwa uandishi ‎wa hati (font) ya Naskh ya Kiajemi. [60] Hati (font) ya Nastaliq hutumika sana katika maandishi ya ‎kifasihi, lakini kutokana na ugumu wake katika uwekaji wa alama za irabu, siyo mara nyingi Qur’ani ‎kamili kuandikwa kwa hati hizi. [61] Mir Imad Hassani Qazvini aliandika Sura ya Al-Fatiha kwa maandishi ‎ya Nastaliq, kazi ambayo ilipata umaarufu mkubwa katika nchi za Kiajemi. [62] Katika enzi ya Safavid ‎‎(Safawiyyuna), tafsiri za Kifarsi za Qur’ani ziliandikwa kwa maandishi (font) ya Nastaliq katika ‎mwonekano mwembamba kabisa chini ya kila Aya miongoni mwa Aya za Qur’ani. [63]‎

‎=== Sanaa ya Tadh-hib (Upambaji wa Rangi ya Dhahabu)‎ ===

Tadhhib inahusisha kupamba kurasa za kitabu au jalada lake kwa dhahabu na rangi nyinginezo. [64] ‎Mara nyingi sanaa hii hutumika kawa ajili ya kuashiria mwanzo wa sura na mwanzo wa juzuu ndani ya ‎Qur’ani. [65] Kazi ya tadh-hib ilishikamana sambamba na kazi uandishi kaligrafia katika uandishi wa ‎Qur’ani, hadi ikawa waandishi wa Qur’ani pia ni watendaji wa kazi hiyo ya tadh-hib. [66] Kazi za zamani ‎kabisa za uchoraji na tadhhib za Qur’ani zilizobaki hasi sasa, ni kutokea karne ya tatu Hijria na ‎kuendelea. [67] Mara nyingi Qur’ani hizi ziliandikwa kupitia maagiza ya watawala wa wakati huo. [68]‎ Mwishoni mwa karne ya sita na mwanzoni mwa karne ya saba, mji wa Tabriz ulikuwa ni kituo muhimu ‎cha sanaa ya tadhhib, na mtindo wa Kitabriz katika tadhhib ulianzishwa katika kipindi hichi. [69] Sanaa ‎ya tadhhib ilistawi sana katika kipindi cha utawala Timurid (Taimiriyyun), hii ni kutokana na watawala ‎wao kuipenda sana sanaa hii. [70] ‎

Uandishi wa Kiuchongaji

Uandishi wa Ayat Noor katika hati ya Thuluth, katika Kibla, iliyoandikwa na Sayyid Muhammad Husseini Muwahid, katika Haram ya la Imam Ridha (a.s).

Kuna Aya na Sura Kadhaa zilizochongwa na kunakishiwa kwa nakshi zipendezazo ambazo ‎hutayarishwa kwa ajili ya kupambia vibla (mihrabu), minara ya misikiti, kuta za makaburi pamoja na majengo ‎matakatifu. [71] Michoro ya kiuchongaji iliandikwa kiumaridadi kabisa juu vitu kadhaa kama vile; vigae ‎vya kauri, matofali, au juu ya plasta, kupitia hati (font) zivutiazo kama vile; Kufi, Thuluth, Naskh, ‎Nastaliq, na Mualla. [72] Uandishi wa kiuchongaji ulikuwa ni maarufu katika kipindi cha utawala wa ‎Timurid na hatimae ulifikia kilele chake katika kipindi cha Safavid. [73]‎

Usanifu wa Majalada

Waislamu walitumia sanaa ya usanifu wa majalada ili kuinda Qur’ani isiharibike. [74] Sanaa ya usanifu ‎wa majalada kama vile uandishi wa kikaligrafia, ulishika kasi kutokana na utakatifu wa Qur’ani mbele ya ‎Waislamu. [75] Majalada ya kwanza yalikuwa ni ya kawaida tu, lakini kuanzia karne ya nne Hijria, nakshi ‎za kijiometri kama vile nakshi za duara na mviringo zilijitokeza katikati fani ya usanifu wa majalada. [76] ‎Baada ya muda, majalada yalianza kupambwa kwa kutumia dhahabu na rangi za kuvutia. [77] Upambaji ‎wa majalada ya ngozi ulikuwa na umuhimu maalum katika kipindi cha utawala wa Timurid nchini Iran na ‎kipindi cha Mamluk nchini Misri, [78] ambapo sanaa hii ya usanifu wa majalada ilifikia kilele chake katika ‎kipindi cha utawala waTimurid. [79]‎

Chapisho la Kwanza la Qur’ani

Kwa mara ya kwanza kabisa Qur’ani ilichapishwa mnamo mwaka 950 Hijria katika mji wa Venice ‎‎(Venezia) nchini Italy, lakini baadae ilikuja kuharibiwa kwa amri ya viongozi wa kanisa. [80] Baada ya ‎hapo, mnamo mwaka wa 1104 Hijria, mtaalamu wa mambo ya Kiislamu wa Kijerumani, Abraham ‎Hinckelmann, alichapisha Qur’ani huko Hamburg, Ujerumani. [81] Chapa ya kwanza ya Kiislamu ya ‎Qur’ani ilichapwa mnamo mwaka 1200 Hijria na mtu aitwaye Mulla Osman huko St. Petersburg, Urusi. ‎‎[82] Iran ilikuwa serikali ya kwanza ya Kiislamu kuchapisha Qur’ani kwa kutumia uchapaji wa mawe, ‎moja ilichapwa mwaka wa 1243 Hijria huko Tehran na nyingine mwaka wa 1248 Hijria huko Tabriz. [83] ‎Baada ya Iran, mnamo mwaka 1294 Hijria, serikali ya Uthmaniyya ya Uturuki ilichapisha Qur’ani katika ‎machapisho mbalimbali. [84] Baada ya hapo, serikali ya Misri mwaka wa 1342 Hijria na serikali ya Iraq ‎mwaka wa 1370 Hijria ndizo zilikuja kuchapisha Qur’ani na kutoa nakala za madhubuti na zenye ‎thamani. [85]‎

Masuala Yanayo Fungamana

Maktaba ya Picha

Rejea

Vyanzo